Jihadhari, utakufa mapema bure kwa sababu ya uchungu ulio nao!

Duh, kwanza pole sana kwa uchungu huo unaokusibu.

Pili, naamini umeisoma vizuri mada yangu, mwanzo hadi mwisho na kuanza kuufanyia kazi ushauri nilioutoa katika mada hiyo.

Tatu, napenda kukushauri kibiblia maana Biblia ndio mwongozo wetu sisi tunaomwamini Mungu. Ukiuzingatia ushauri huu, utavuka salama katika hilo tatizo linalokuandama.

Umesema unampenda sana mpenzi wako. Sasa kama kweli unampenda sana, hupaswi kuhesabu mabaya yake. Nimeona umeorodhesha mabaya yake mengi: kukawia kupokea simu, unafiki, kukimbilia kwa ma-x wake, kutokujua kupika...
Hapo hujataja hata moja zuri alilo nalo.

Sasa sikiliza: Katika kitabu cha 1 Wakorintho 13:4-8, Biblia inatutajia sifa za mtu mwenye upendo: ni mvumilivu, ni mwenye fadhili, haoni wivu, hana majivuno, hana kiburi. Hakosi kuwa na adabu, hatafuti mambo yake mwenyewe, hakasiriki upesi, hahesabu mabaya (yaani haweki kumbukumbu ya mambo mabaya aliyo/anayotendewa)...

Hilo la kuhesabu mabaya ndilo linalokuhusu sana hapo. Na yamkini sababu kubwa ya yeye kukukimbia ni tabia yako ya kumhesabia mabaya kila mara.

Hivyo nakushauri, badala ya kutaja tu mabaya yake kila unapoongea naye, msifie/mtajie mazuri aliyo nayo utaona jinsi atakavyobadilika na kuvutwa kuwa karibu na wewe.

Katika Mt 18:21-22, Biblia inatuambia pia kwamba: ndugu yako akikukosea hata saba mara sabini unapaswa kumsamehe. Hiyo maana yake ni kwamba, msamaha haupaswi kuwa na kikomo. Ukisamehe leo, achilia. Akirudia kosa lile lile kesho, usimuulize kwanini amerudia kosa lile lile. Kosa la kesho, hesabu kuwa hilo ni la kwanza, maana jana uliishasamehe na kuachilia au kusahau.

Halafu, Maandiko yanatuambia katika Luka 6:41-45 hivi: "Mbona unatazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, wala huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako?"

Hiyo ina maana kwamba kabla ya kumuona mwenzako kuwa ana tatizo, ujichunguze mwenyewe; uhakikishe kwanza wewe ni safi. Kwa mantiki hiyo, nikuulize: je wewe huna udhaifu hata mmoja? Jaribu umuombe huyo mpenzi wako akuambie bila kuficha, anakuonaje wewe, au umuulize akutajie bila kuficha, makosa anayoyaona kwako; utashangaa na wewe unayo makosa au udhaifu mwingi. Kwa sababu hiyo ukijua na wewe unao udhaifu, utajirekebisha kwanza kabla ya kumkosoa mwenzako.

Huo ndio ushauri wangu kwa kifupi.

Naomba nikuulize: huyo mpenzi wako, mmeoana au mko tu kwenye mahusiano yatakayowapelekea kufunga ndoa? Na je, hao ma-x wake ni Ex-boyfriends au ni Ex-husbands?
 
Tupo kwenye mahusiano hao x boyfriend wake ni wanaume wake ambao aliwahi kudate kabla yangu
 
Ni uchungu sana.
My friend, great to meet you!
Kweli, dunia hii ni chungu, lakini kila chenye mwanzo kina mwisho.
Sisi tunaoisoma na kuitafakari Biblia kila mara, tunajua mwisho wa dunia hii (na mambo yote yanayotia uchungu), umekaribia. Kwa sababu hiyo tunakesha katika sala (1 Pet 4:7), ili tusiikose ahadi aliyotuahidi Yesu ya kuja kutuchukua na kutupeleka kwenye makao yenye raha ya milele.

Ahadi hizi zitatimia in the near future:
"Behold, I am coming soon! Blessed is the one who keeps the words of the prophecy written in this book." (Revelation 22:7)
“Do not let your heart be troubled; believe in God, believe also in Me. In My Father’s house are many dwelling places; if it were not so, I would have told you; for I go to prepare a place for you. If I go and prepare a place for you, I will come again and receive you to Myself, that where I am, there you may be also. And you know the way where I am going.”(John 14:1-4).

By the way, bado unaamini atheism? Kama kuna watu ninaowaombea sana ni wewe. Maombi yangu Mungu anayasikia, hivyo naamini siku moja utaokoka na kujiunga na familia ya waendao mbinguni. Amen.
 
Tupo kwenye mahusiano hao x boyfriend wake ni wanaume wake ambao aliwahi kudate kabla yangu
Asante sana. Hebu ufanyie kazi ushauri niliokupa, then unipe mrejesho.
Ushauri mwingine ninaokupa ni huu: Piga magoti umuombe Mungu akudhihirishie kuwa huyo ndiye anayepaswa kuwa mke wako. Kama Mungu amekuandalia huyo, hata akikupiga chenga namna gani atakuja tu kuwa wako.

Mithali 19:14
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.

Nikuulize tena: Je, umeokoka? Kama hujaokoka, je, unajua kuwa mahusiano ya kimwili kabla ya kufunga ndoa ni dhambi?
 
Tupo kwenye mahusiano hao x boyfriend wake ni wanaume wake ambao aliwahi kudate kabla yangu
Dogo mapenzi ni ya pande zote ,ukiona hana ushirikiano kwenye mawasiliano usilazimishe kaa kimya. Ukiona umekaa kimya na yeye amekaa kimya na akaja kukutafuta baada ya mwaka au miaka usimpe ushirikiano maana alikuchukulia ni chaguo la pili au tatu hivyo amerudi baada ya kushindwa kwake kupata chaguo lake la kwanza.

Mpende akupandae ni msemo wa maana sana na uchukuliea
userious.
 
Welcome back, servant of God
 
Ni kweli uchungu unaua. Mara nyingi wanandoa wakiachana yule aliyeachwa hufariki mapema sijui kwa Nini ila sababu kuu itakua uchungu.
Ni vema tukawa na uchungu kwa kiasi kidogo ili utupush kwenye maendeleo.
 
Hivyo huu ni muda mwafaka wa kutubu na kuomba Mungu atusamehe
Kweli mtumishi. Tuongoze sala ya toba.
Am contemplating mafuriko yaliyowaua maelfu ya watu Nepal, I dont think wote walikuwa wametubu kabla
 

Kumbe Kijakazi una ID nyingi humu
 
I presume hujaelewa Andiko hili: "...jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka.”
Waefeso 4:26
Tafadhali litafakari tena
Wameandikiwa waefeso na sio wagogo, wachaga, wazaramo au wasukuma. Kwanini mambo ya waefeso unataka kuya apply kwetu huku? Tupe reference ya kwetu huku kama ipo.
 
Wameandikiwa waefeso na sio wagogo, wachaga, wazaramo au wasukuma. Kwanini mambo ya waefeso unataka kuya apply kwetu huku? Tupe reference ya kwetu huku kama ipo.
Kama hukubaliani na kitabu cha Waefeso, je hata ushauri wa kisayansi hukubaliani nao?Nilianza mada yangu kwa kutaja hasara za kisayansi za kubeba uchungu. Na hizo ndizo zitakazokuua mapema kama utaendelea kuhifadhi uchungu moyoni mwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…