Jihadhari, utakufa mapema bure kwa sababu ya uchungu ulio nao!

Jihadhari, utakufa mapema bure kwa sababu ya uchungu ulio nao!

Sina ubaya nae sema shida ni kutumia reference za wakorintho, walawi na waefeso, wakati mimi msukuma sijaona reference yangu.
Kwa maana hiyo nikikupa direct references za Yesu utazikubali?
 
Eeh kama nilivyojaribu kusamehe na kuachilia, ila ni safari ndefu kweli.
 
Wala sitopinga kabisa kama zitataja walaka wa yesu kwa wasukuma
Tunaenda vizuri. Hebu turudi nyuma kidogo, kabla hatujaendelea, uniambie: Wasukuma wana genealogy gani? Wametoka wapi, na asili yao inaanzia kwa nani?
 
Tunaenda vizuri. Hebu turudi nyuma kidogo, kabla hatujaendelea, uniambie: Wasukuma wana genealogy gani? Wametoka wapi, na asili yao inaanzia kwa nani?
Hizo story zifanye wewe sasa mimi siwezi kujua
 
Nambie basi nahusiana vipi na wakolosai?
Okay, asili yetu sisi sote ni Adam. Huyo ndiye mtu wa kwanza kuumbwa duniani.
Kitabu cha Matendo ya Mitume(hiki hakijalengwa kwa taifa au kabila lolote), kinasema katika sura ya 17:26 kwamba: "Kutoka kwa mtu mmoja, Yeye (Mungu) aliumba mataifa yote ya wanadamu ili waikalie dunia yote..."
Kwa maneno mengine, yaliyoandikwa kwa Waefeso yanawahusu pia Wasukuma kwa sababu sisi sote tumetokana na mtu mmoja. Na kuna mtu mmoja maarufu alisema: "Binadamu wote ni ndugu zangu..." If so, tuweke pembeni ubaguzi.
 
Nini maana ya waefeso?
 
Nini maana ya waefeso?
Waefeso ni wenyeji au wakazi wa mji wa kale wa Efeso, uliokuwa katika jimbo la Asia ndani ya Dola ya Rumi (kwa sasa nchi ya Uturuki)
 
Waefeso ni wenyeji au wakazi wa mji wa kale wa Efeso, uliokuwa katika jimbo la Asia ndani ya Dola ya Rumi (kwa sasa nchi ya Uturuki)
Wakati huo wasukuma hatuwepo?
 
Wakati huo wasukuma hatuwepo?
Ndiyo, wakati huo kabila la Wasukuma lilikuwa halijazaliwa. Mtume Paulo aliongea na kuwaandikia Waefeso karibu mwaka 52 hadi 62 BK. Na utambulisho thabiti wa Kabila la Wasukuma unaanzia mnamo karne ya 16 hadi ya 18 BK.

Halafu usisahau nilivyokuambia: Sisi sote tumetokana na mtu mmoja - Adam. Adam baada ya kupewa mke (Eva au Hawa), Mungu aliwaambia wazae, waongezeke waijaze dunia. Hivyo nyakati zile za mwanzo mwanzo, sehemu kubwa ya dunia ilikuwa bado haina watu (na makabila mengi yalikuwa bado hayajaundwa).

Kwahiyo ndugu yangu, naamini umeona wazi sasa kwamba maneno ambayo Paulo aliwaambia Waefeso yanawahusu pia Wasukuma. Kwa maneno mengine tunaweza kusema Paulo aliongea na mababu na mababu wa Wasukuma!
Efe 4:26-27
"...jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka..."
 
Back
Top Bottom