Jihadhari, utakufa mapema bure kwa sababu ya uchungu ulio nao!

Nini kifanyike ili tusiwe na machungu?
Kwa ufupi, ili uwe mbali na uchungu fanya hivi:
Kwanza, mkabidhi Mungu (kwa njia ya maombi) kila jambo linalokuletea uchungu (Zab 55:22). Yesu anasema kama unalemewa na mizigo uje kwake; ataitua mizigo yako na kukupa raha nafsini mwako (Mt 11:28-30; Yn 14:27).

Pili, usiruhusu hasira ikae moyoni. Mtu akikukosea, msamehe. Usitafute kulipiza kisasi (Rum 12:19). Kisasi atalipa Mungu.

Tatu, jifunze kushukuru kwa kila jambo (1 Thes 5:18) na kufurahi katika Bwana hata wakati ambapo mambo hayaendi kama unavyotaka (Flp 4:4)

Na mwisho, kumbuka kwamba dhiki za dunia hii ni za kitambo tu; Yesu Kristo karibu atakuja kutuchukua na kutupeleka mbinguni kwenye raha ya milele. Mbinguni hakutakuwa na kulia wala kuomboleza. Yesu atatufuta machozi kabisa (Ufu 21:4). Uchungu na mauti havitakuwepo tena.
 
Well said mafundisho mazuri,ndiyo maana itabaki kuwa uchungu ni mlango wa adui kuingia katika maisha yako uwahi kuufunga maana una lengo la kukudimiza
 
Good
 
Endelea kuumia sababu ya Ke maana ndiyo uvulana huo kuelekea uanaume.

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
"Usijifanyie sanamu ya kuchonga wala kuiabudu" Zingatia amri hii hakika hutateseka tena mkuu.

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
Focus on what really matters.
Absolutely. And what really matters is learning to live according to the Word of God. When we follow His commands, choosing forgiveness, love, peace, and letting go of bitterness, we protect our hearts from carrying unnecessary pain.
 
Kama hukubaliani na kitabu cha Waefeso, je hata ushauri wa kisayansi hukubaliani nao?Nilianza mada yangu kwa kutaja hasara za kisayansi za kubeba uchungu. Na hizo ndizo zitakazokuua mapema kama utaendelea kuhifadhi uchungu moyoni mwako.
Kwanza elewa kiumbe hai chochote lazima kife na sababu za vifo vipo vingi sana, kwa hiyo kwa sababu yako hiyo naona unaiamini sana kuwa ndio inaua mapema, mwili wa binadamu uko adaptive sana kukabiliana na mazingira yanayokuja ukiona una uchungu ujue kuna automatic adjustment zitafanyika ku counter balance changamoto hiyo nawewe by consious huwezi kuitawala hali hiyo na ukijaribu ndio utajiumiza. Ndio maana ikibidi kulia lia na ikibidi kulipa kisasi lipa maana ndio maamuzi yaliyokuja ili upate hali ya kawaida na sio kulazimisha eti ufute maumivu kwa kutumia reference za waefeso
 
Naona kitabu cha Waefeso kinakukereketa. Na maneno ya Yesu je, unayakubali? Labda tuanzie hapo kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…