Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Hili jiji kwa miundombinu bado kabisa, ni zaidi ya miaka kumi (10) sasa tangu litangazwe jiji, lakini cha kushangaza na kusikitisha hakuna vituo maalumu vya kushusha na kupakia abiria.
Vile vituo vya njiani hakuna alama yoyote inayoonyesha kuwa hapa ni sehemu ya kushusha na kupakia abiria, kwa maana kuwa hakuna kibao wala sehemu ya abiria kumkinga na Mvua wala jua, mteja anasimama popote na anashushwa popote.
La pili kituo /stand ya daladala, hakuna kituo maalumu cha daladala kuingia bali zote hugeuzia barabarani au mwisho wa barabara ambapo hushusha na kupakia abiria hapo hapo, kwa jinsi inavyoonekana sehemu nyingi au mwisho wa vituo vilivyo vingi madereva na Makonda ndio waliopanga uwe mwisho wa kituo na si serikali.
Mfano mzuri daladala za kutoka mjini kwenda Lemara hazina kituo maalumu kilichotengenezwa huko Lemara mwisho bali hugeuzia barabarani.
Daladala za Kwenda Morombo kutoka mjini hadi Morombo pale hawajajengewa kituo maalumu cha kuingilia bali pembeni ya barabara ndo mwisho wao na hugeuzia hapo hapo.
Daladala za kwenda Usa nalo vile vile hawana kituo maalumu huko mwisho.
Daladala za kwenda Engosengiu nao mwisho wao ni barabarani ndipo hugeuzia gari zao hawajajengewa kituo maalumu cha kugeuzia ambapo abiria anaweza kukaa na kusubiri usafiri.
Na sehemu nyingine nyingi tu.
Ni wakati sasa wa jiji kuamka na kuandaa Ramani nzima ya jiji pamoja na kuandaa miundombinu /vituo maalumu vya kujengewa ili kuweka jiji katika hadhi yenye ramani nzuri.