Jiji la Arusha limekosa vituo vya daladala, pembeni ya barabara kuu ndio mwisho wa kituo

Jiji la Arusha limekosa vituo vya daladala, pembeni ya barabara kuu ndio mwisho wa kituo

Sister achana na stand ya daladala kuna mambo mengi hayapo sawa, Arusha haina stand kuu ya mabus yaani ni kila kampuni ya mabus ina stand yake na kushusha abiria na kuwapakiza kila kampuni inaamua sehemu yake kwa mfano BM coach, Dar Express na Kilimanjaro express ushusha abiria pale kwenye jengo la NHC pembeni ya Golden crest sehemu ambayo abiria akishuka inamlazimu kutembea hadi kilombero au klokoni kupata daladala ya route yake vivyo ivyo wanaoshushiwa stand ndogo, pia Arusha municipal wanafeli kwenye management ya masoko yao kwa mfano soko la kilombero mvua ikinyesha ni hapatoshi ni kuna tope balaa😂, kitu kingine Arusha waondoe vipanya bhana waweke coasters , waache ushamba coasters sio kwa ajili ya tourists tu.
Kitu nacho ipendea Arusha ina hali ya hewa nzuri , sema udongo wake sasa ni vumbi na tope😂ndo maana boots zinahusika sana,
Kama wakifanyia kazi ivyo vitu na hakika Arusha ni mkoa poa sana sema ndo ivyo imesaulika
well said
 
Natamani wenye mamlaka husika waone haya malalamiko, huku hali ni mbaya yani mavi matupu
 
Arusha inayosifiwa mitandaoni ni tofauti na Arusha yenyewe ilivyo kiukweli huo mji Bado upoupo tu, kuanzia mpangilio Hadi watu wake wako rafurafu tu, wajifunze Kwa majirani zao Moshi mji unavutia na kupendeza
Dah siku nilipoenda Arusha mara ya kwanza nilichoka Yani Arusha inasifiwa mtandaoni ila ukifika uhalisia hamna mji hauna miundombinu mizuri kabisa
 
Halafu nilimshangaa jiji kuwa na nyumba za tope na makazi holela yasiyokuwa na barabara za mtaani.
Hao wenye nyumba za tope ni Waarusha, na ni za miaka mingi
 
Mitaa mingi Giza..hakuna taa za barabarani
Ni karibu mji mzima tu. Taa za barabarani zipo sehemu chache sana kama vile barabara ya sakina,Uswahilini.
Lakini sehemu kubwa ni giza
 
Arusha inayosifiwa mitandaoni ni tofauti na Arusha yenyewe ilivyo kiukweli huo mji Bado upoupo tu, kuanzia mpangilio Hadi watu wake wako rafurafu tu, wajifunze Kwa majirani zao Moshi mji unavutia na kupendeza
Ukweli
 
Dah siku nilipoenda Arusha mara ya kwanza nilichoka Yani Arusha inasifiwa mtandaoni ila ukifika uhalisia hamna mji hauna miundombinu mizuri kabisa
Nilichoona ni kuwa baadhi ya watu wanatoa maoni kwa lengo la kujenga na wengine wanatoa maoni binafsi ya chuki juu ya Arusha.
Ni kweli kama miji yote Tanzania hasa uliokua chini ya upinzani kwa mda mrefu serikali kuna namna iliusisia huu mji lakini bado haiondoi ukweli ndio jiji la pili kwa maendeleo nyuma ya dar.
 
Hao wenye nyumba za tope ni Waarusha, na ni za miaka mingi
uyo ameuliza kwa chuki binafsi ndio nilikua na sema pamoja na changamoto tulizonazo Arusha bado kwenye nyanja zingine tupo bora sana mfano halmashauri ya Arusha jiji ndio inayoongoza kwa kuwa na makazi bora nchi nzima sasa uyo anayesema aliona nyumba ya udongo Arusha basi ujue huko alipotoka kuna utitiri wa hizo nyumba na ndio maana hapa watu wenye constructive arguments ni wachache mtoa mada kasema Arusha hamna vituo mtu anachangia eti Arusha aliona nyumba ya udongo seriously 🤣 ni kweli Arusha inachangamoto na kubwa ni taa za barabarani ambazo mwezi huu wa 12 wanaanza kufunga mpya manake sio kwamba zilikua hazipo zilikuwepo ila zilikua haziwaki na kuhusu stendi ya kilombero it's just a temporary thing japo kama halmashauri kuna uzembe stendi haiwezi kuachwa kuwa vile lakini hilo haliondoi uzuri wa mengi ambao Arusha inao na bado ndio halmashauri iliyoendelea zaidi nje ya dar. Naomba kuwasilisha

download (1).jpeg


IMG_20211121_170157.jpg
 
"Ina dar mi na hot slama gyal 2 times mi jus float,dats y Mi luv a city weda si don wi mi bway stackin togeda ina consat mi gi ve dem fleva"...Yokoi
 
Bidii zao Wakazi wa huko za kupenda Kuvuta na Kulima sana Sigara Bwege ( Bangi ) bila kusahau Kutafuna Mirungi na Kuvimba hovyo Macho yao wakizihamishia tu katika Kuujenga zaidi huu ( huo ) Mkoa wao hizi Changamoto ulizozitaja hapa zitakuwa ni Historia.
wewe bila shaka ni zwaza mmoja hujawahi kufika hata Arusha tunaposema changamoto zetu haimaanishi mikoa mingine hamna mfano ukiangalia taarifa ya habari kila siku utakuta wakazi wa dar wanalalamika mara barabara nk haimaanishi dar haina sehemu nzuri ila ni watu wao wanataka huduma bora zaidi. ningependa kufahamu ndugu wewe unatoka wapi??? lazima tu utakua kanda ya ziwa wewe kule kwenye ufukara wakutupwa🤣🤣 tafuta hela uje kutembea Arusha wewe 😎
 
Back
Top Bottom