Jiji la Dar limenishinda kuishi. Wengine mnawezaje au mnajikaza?

Jiji la Dar limenishinda kuishi. Wengine mnawezaje au mnajikaza?

MFALME WETU

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2021
Posts
5,824
Reaction score
14,757
Ugonile,

Ni muda kidogo (kwa zaidi ya miaka miwili) sikuwa Tanzania, ila nilirudi mwaka huu mwezi wa pili nikakaa Dar kidogo maisha yakanishinda, nikaamua kutimkia mkoani. Kabla ya kutimkia nchi za wenzetu riziki yangu nilikuwa naitaftia Kariakoo kwa zaidi ya miaka mitano, niseme tu ukweli nilikua najikaza sana kuishi kwenye hilo jiji.

Kero yenyewe ni makelele na hali ya hewa, aisee Dar kuna purukushani za kufa mtu, uswahili mwingi, miundombinu mibovu, ukienda maeneo ya soko kama Kariakoo, Mbagala, Tandika kuna makelele mpaka unatamani uzibe masikio!

Bodaboda wanaendesha hovyo kama wapo kwenye mashindano ya vichaa muda wowote usipokua makini wanakukwatua, maofisini hakuendeki sababu ya queues zisizoisha, hospitali ndio usiseme, foleni barabarani mpaka unajuta kuwa road.

Kwa sasa Dar naichukulia kama sehemu ya kuja kulia Bata tu, nimekua nikijikaza kuja mara mojamoja ila huwa nikifikia Hotelini sitoki au nikiboeka navuka zangu maji kwenda Zenji ila sio kukaa Dar, imagine tangu niondoke Kariakoo nakaribia mwaka wa tatu sasa sijawahi kurudi. Kila nikifikiria yale makelele naishiwa pawa!

Nyie mnaoishi Dar miaka yote iyo mnawezaje au ndio mnajikaza? Mmewahi kufikiria kuishi mikoani muone maisha yalivokua matamu?😁

Chukulia mfano watu wa ukanda wa Gaza, Mbagala, Chanika, Kigamboni aisee Mungu awasaidie.

Sasa hivi napanga kujenga kwa Mama Abduli, wale mnaoshadadia Muungano uvunjike acheni izo 🫵
 
Kwahyo huko kabwe na mwanjelwa ndo kuna miundombinu mizur?

Madereva wazuri?

Na hakuna makelele? Maana huko kila baada ya nyumba 3 kanisa la mabat na makelele kila muda

Uko nje ya nchi ndo malawi hapo?

Ungekua na hela ungeishi masak

Toka kwa shemeji, katafute kibarua
 
Kwahyo huko kabwe na mwanjelwa ndo kuna miundombinu mizur?

Madereva wazuri?

Na hakuna makelele? Maana huko kila baada ya nyumba 3 kanisa la mabat na makelele kila muda

Uko nje ya nchi ndo malawi hapo?

Ungekua na hela ungeishi masak

Toka kwa shemeji, katafute kibarua
Punguza stress mdogo wetu
 
Dsm ndio Tanzania 🇹🇿 ...
Pamoja na kero zote kuanzia foleni, joto, uchafu , population n.k lakini ndio sehemu pekee Tanzania hii penye rizk hasa kwa wafanya biashara!!!! Ishi/jenga pembezoni mwa mji, mishe zako pigia town......

Chukua kauusafiri kako .... hutojuta
 
Dsm ndio Tanzania 🇹🇿 ...
Pamoja na kero zote kuanzia foleni, joto, uchafu , population n.k lakini ndio sehemu pekee Tanzania hii penye rizk hasa kwa wafanya biashara!!!! Ishi/jenga pembezoni mwa mji, mishe zako pigia town......

Chukua kauusafiri kako .... hutojuta
we itakuwa bado mgeni wa jiji au vinginevyo ushazoea kero za jiji.!! Dar ni sehemu ya Tz sio Tz na wala hakufai kwa makazi ya binadamu acheni ulimbukeni
 
Ugonile,

Ni muda kidogo sikuwa Tanzania kwa zaidi ya miaka miwili ila nilirudi mwaka huu mwezi wa pili nikakaa Dar kidogo maisha yakanishinda nikaamua kutimkia mkoani.

Kabla ya kutimkia nchi za wenzetu riziki yangu nilikua naitaftia kariakoo kwa zaidi ya miaka mitano, niseme tu ukweli nilkua najikaza sana kuishi kwenye ilo jiji.

Kero yenyewe ni makelele na hali ya hewa, aisee Dar kuna purukushani za kufa mtu, uswahili mwingi, miundombinu mibovu, ukienda maeneo ya soko kama Kariakoo, mbagala, tandika kuna makelele mpaka unatamani uzibe masikio, Bodaboda wanaendesha hovyo kama wapo kwenye mashindano ya vichaa muda wowote usipokua makini wanakukwatua, maofisini hakuendeki sababu ya queues zisizoisha, hospitali ndo usiseme, foleni barabarani mpaka unajuta kuwa road.

kwa sasa Dar naichukulia kama sehemu ya kuja kulia Bata tu, nmekua nikijikaza kuja mara mojamoja ila huwa nikifikia Hotelini sitoki au nikiboeka navuka zangu maji kwenda kwa Bi Ushungi ila sio kukaa Dar, imagine tangu niondoke Kariakoo nakaribia mwaka wa tatu sasa sijawahi kurudi. Kila nikifikiria yale makelele naishiwa pawa

Nyie mnaoishi Dar miaka yote iyo mnawezaje au ndo mnajikaza? mmewahi kufikiria kuishi mikoani muone maisha yalivokua matamu? 😁

Chukulia mfano watu wa ukanda wa Gaza, Mbagala, Chanika, Kigamboni aisee Mungu awasaidie.

Saiv napanga kujenga kwa Mama Abduli, wale mnaoshadadia Muungano uvunjike acheni izo 🫵
Mimi tangu nihamishie makazi yangu mkoani morogoro wilaya ya malinyi kijiji cha kilosa kwa mpepo sijawahi kutamani kurudi dsm. japo hapo kariakoo nimewekeza mamilioni ya pesa. Hakika dsm hapafai ndio maana serikali imepakimbia ikahamia kijijini Dodoma
 
Back
Top Bottom