Ugonile,
Ni muda kidogo (kwa zaidi ya miaka miwili) sikuwa Tanzania, ila nilirudi mwaka huu mwezi wa pili nikakaa Dar kidogo maisha yakanishinda, nikaamua kutimkia mkoani. Kabla ya kutimkia nchi za wenzetu riziki yangu nilikuwa naitaftia Kariakoo kwa zaidi ya miaka mitano, niseme tu ukweli nilikua najikaza sana kuishi kwenye hilo jiji.
Kero yenyewe ni makelele na hali ya hewa, aisee Dar kuna purukushani za kufa mtu, uswahili mwingi, miundombinu mibovu, ukienda maeneo ya soko kama Kariakoo, Mbagala, Tandika kuna makelele mpaka unatamani uzibe masikio!
Bodaboda wanaendesha hovyo kama wapo kwenye mashindano ya vichaa muda wowote usipokua makini wanakukwatua, maofisini hakuendeki sababu ya queues zisizoisha, hospitali ndio usiseme, foleni barabarani mpaka unajuta kuwa road.
Kwa sasa Dar naichukulia kama sehemu ya kuja kulia Bata tu, nimekua nikijikaza kuja mara mojamoja ila huwa nikifikia Hotelini sitoki au nikiboeka navuka zangu maji kwenda Zenji ila sio kukaa Dar, imagine tangu niondoke Kariakoo nakaribia mwaka wa tatu sasa sijawahi kurudi. Kila nikifikiria yale makelele naishiwa pawa!
Nyie mnaoishi Dar miaka yote iyo mnawezaje au ndio mnajikaza? Mmewahi kufikiria kuishi mikoani muone maisha yalivokua matamu?😁
Chukulia mfano watu wa ukanda wa Gaza, Mbagala, Chanika, Kigamboni aisee Mungu awasaidie.
Sasa hivi napanga kujenga kwa Mama Abduli, wale mnaoshadadia Muungano uvunjike acheni izo 🫵