Jiji la Dar limenishinda kuishi. Wengine mnawezaje au mnajikaza?

Nafikiri wengi hawakumuelewa mleta mada,au labda mimi ndio sijamuelewa mleta mada,
Atakuja mwenyewe MFALME WETU ili kutoa ufafanuzi zaidi,

Mleta mada ameongelea issue ya infrastructure and Noise pollution na matatizo mengine ya kijamii kwa ujumla,
Issue sio kumwambia mleta mada tafuta hela au huna hela,

Tuseme unazo hizo hela na una Gari kali,ila ukitoka tu nje kwa safari zako za ndani unakutana na hayo matatizo anayo yaongelea mleta mada,kuanzia foleni,noise pollution,barabara mbovu,huduma pale inapotokea ajali au ikitokea ajali ya moto,

Kuna watu hua wanahama nchi sio tu kwenda kutafuta hela peke yake bali kufuata huduma za kijamii pia pamoja na usalama wa maisha yao na mali zao,

Mfano jiji la Tokyo Japan lina popullation ya zaidi ya wakaazi 37 milioni ila hakuna noise pollution kama Dar,Dubai au China wana masoko makubwa ya bidhaa kwa jumla na reja reja ili huwezi kukuta wana piga kelele kwa vispika ili kuuza bidhaa zao,

Mimi kama mbeba box mzoefu toka kitambo nimekuelewa vizuri sana mleta mada,

Haya ni maoni yangu tu wala simchallenge mtu hapa.
 
We umenielewa sana mkuu, mfano mzuri ni jana baada ya kufika Dar nilikuja vizuri tu na Private yangu nikafikia Golden Tulip Oysterbay kuzuga kidogo huku nikitafuta Hotel ya kukaa yenye beachfront inayoeleweka nikapata wazo la kwenda Bahari Beach ila kila nilpokua nafikiria Foleni na zile barabara maana sehemu nyingi nilzokuwa napita kulikua na matengenezo nikaamua kuwasha mkweche wangu mpaka Ubungo kwa mshikaji wangu nikapaki, akanisindikiza na gari yake mpaka Ferry nikavuka zangu maji kiroho safi.
 
Kwa utafiti wangu, ukishindwa maisha Dar, rudi tu kijijini. Dar ukiwa mzima wa afya unafanya kazi yoyote ili mradi mkono uende kinywani.
 
kupanga ni kuchagua, na maisha hayana extra time,

songa mbele na maisha yako kadiri uwezavyo na upendavyo bila kubabaika na ya wengine na itapendeza zaidi gentleman 🐒
 
kupanga ni kuchagua, na maisha hayana extra time,

songa mbele na maisha yako kadiri uwezavyo na upendavyo bila kubabaika na ya wengine na itapendeza zaidi gentleman 🐒
gentleman upo sahihi kabisa,
Life is not a matter of chance but a matter of choice.
 
MImi nazani inategemeana mtu na mtu.

Kwngu mimi licha ya changamoto za jiji la Dar kam foleni, Joto.
Bado ni sehemu bora kwangu kuishi.
 
Ha ha ha dah. Sasa Golden Tulip si iko pembezoni mwa bahari? Au Sea Clff? Best Western au Double Tree kwanini uache hizo uhangaike na foleni mpaka Bahari beach?
 
Ha ha ha dah. Sasa Golden Tulip si iko pembezoni mwa bahari? Au Sea Clff? Best Western au Double Tree kwanini uache hizo uhangaike na foleni mpaka Bahari beach?
Machaguo mkuu, huwezi linganisha beachfront ya izo hotel ulizotaja na bahari beach. apo Golden Tulip hata spot ya kuogelea hamna kabisa/sio rafiki zaidi ya pool ilhali mimi swimming ndo starehe yangu namba 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…