Jiji la Kampala linaweza kufananishwa na mji gani wa Tanzania kwa uzuri na maendeleo?

Nimefika Kampala na pia nimeishi Nairobi. Tofauti ya huko na hapa bongo bana ni kuwa ikifika weekend ni weekend kweli. Yani watu wanakula bata haswa. Utaona magari ambayo weekdays huyaoni utaona pisi ambazo hazionekani weekdays.

Yani wao siku za bata ni bata kweli na siku za kazi ni kazi kazi.
 
Kwa siku chache ambazo nimekuwepo hapa Kampala, nimeweza kujionea, japo ni kwa sehemu ndogo tu, jinsi lilivyo.

Ni jiji kwenye hadhi ya kuitwa jiji. Lina mandhari nzuri na pia hali ya hewa nzuri.

Pamoja na kwamba ni jiji, lakini ukililinganisha na jiji la Dar Es Salaam ni kulionea, na ukisema ulilinganishe na jiji la Tanga au Mbeya ni sawa na kulitukuna.

Ikiwa halijalifikia jiji la Dar Es Salaam, na pia limeyaacha mbali majiji ya Mbeya na Tanga, ni mji upi Tanzania unaweza kulinganishwa nao?
Picha ziko wapi? Labda Arusha au Dodoma
 
Acheni utoto
Yaani Kampala iishinde Dar?

1735752579915.png
 
Kwenye miundombinu ya barabara na usafiri wa umma bado tumewapita pakubwa....barabara za mjini ndo kwanza wameanza kupanua zilikuwa ndogo/mbovu....Ila kwa bodaboda Kampala ni wengi hadi kero😂
Barabara ya Mutukula kwenda Kampala utagundua kwa nini viongozi wanapendelea MAV8! Japo ni lami lakini kwa hivyo "vishimo" utatamani bodaboda
 
Ila kweli

Hivi wacha tujaribu kuashumu kuwa hakuna Bandari hapa Dar. Je ingekuwa mstari mmoja na Kampala? Au Kampala nao wangekuwa na Bandari Kama Dar
Kampala wangekuwa na bandari, tena nzuri na kubwa kama ya Dar Es Salaam, wangetuacha mbali sana. Labda ingekuwa inachuana na akina "Durban" au "Cape Town". Waganda wamekaa kijasiriamali. Wangeitumikisha hiyo bandari ipasavyo.
 
Ukiondoa
Kwa siku chache ambazo nimekuwepo hapa Kampala, nimeweza kujionea, japo ni kwa sehemu ndogo tu, jinsi lilivyo.

Ni jiji kwenye hadhi ya kuitwa jiji. Lina mandhari nzuri na pia hali ya hewa nzuri.

Pamoja na kwamba ni jiji, lakini ukililinganisha na jiji la Dar Es Salaam ni kulionea, na ukisema ulilinganishe na jiji la Tanga au Mbeya ni sawa na kulitukuna.

Ikiwa halijalifikia jiji la Dar Es Salaam, na pia limeyaacha mbali majiji ya Mbeya na Tanga, ni mji upi Tanzania unaweza kulinganishwa nao?

Ukiondoa bodaboda zinazo sababisha traffic jam si pabaya. Aliyeanzisha boda boda alikuwa na lengo zuri lakini baadaye watu wakafanya isivyo boda to boda ikawa vurugu na kelele
 
Kwa siku chache ambazo nimekuwepo hapa Kampala, nimeweza kujionea, japo ni kwa sehemu ndogo tu, jinsi lilivyo.

Ni jiji kwenye hadhi ya kuitwa jiji. Lina mandhari nzuri na pia hali ya hewa nzuri.

Pamoja na kwamba ni jiji, lakini ukililinganisha na jiji la Dar Es Salaam ni kulionea, na ukisema ulilinganishe na jiji la Tanga au Mbeya ni sawa na kulitukuna.

Ikiwa halijalifikia jiji la Dar Es Salaam, na pia limeyaacha mbali majiji ya Mbeya na Tanga, ni mji upi Tanzania unaweza kulinganishwa nao?
labda mwanza? .Ulikaa maeneo gani mkuu owino marketi ulifika?vipi kuhusu Mpererwe na Ntinda?
 
Back
Top Bottom