Jiji la Kampala linaweza kufananishwa na mji gani wa Tanzania kwa uzuri na maendeleo?

Nimefika Kampala na pia nimeishi Nairobi. Tofauti ya huko na hapa bongo bana ni kuwa ikifika weekend ni weekend kweli. Yani watu wanakula bata haswa. Utaona magari ambayo weekdays huyaoni utaona pisi ambazo hazionekani weekdays.

Yani wao siku za bata ni bata kweli na siku za kazi ni kazi kazi.
 
Picha ziko wapi? Labda Arusha au Dodoma
 
Kwenye miundombinu ya barabara na usafiri wa umma bado tumewapita pakubwa....barabara za mjini ndo kwanza wameanza kupanua zilikuwa ndogo/mbovu....Ila kwa bodaboda Kampala ni wengi hadi kero😂
Barabara ya Mutukula kwenda Kampala utagundua kwa nini viongozi wanapendelea MAV8! Japo ni lami lakini kwa hivyo "vishimo" utatamani bodaboda
 
Ila kweli

Hivi wacha tujaribu kuashumu kuwa hakuna Bandari hapa Dar. Je ingekuwa mstari mmoja na Kampala? Au Kampala nao wangekuwa na Bandari Kama Dar
Kampala wangekuwa na bandari, tena nzuri na kubwa kama ya Dar Es Salaam, wangetuacha mbali sana. Labda ingekuwa inachuana na akina "Durban" au "Cape Town". Waganda wamekaa kijasiriamali. Wangeitumikisha hiyo bandari ipasavyo.
 
Ukiondoa


Ukiondoa bodaboda zinazo sababisha traffic jam si pabaya. Aliyeanzisha boda boda alikuwa na lengo zuri lakini baadaye watu wakafanya isivyo boda to boda ikawa vurugu na kelele
 
labda mwanza? .Ulikaa maeneo gani mkuu owino marketi ulifika?vipi kuhusu Mpererwe na Ntinda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…