Uchaguzi 2020 Jiji la Mwanza lasimama usiku kwa ujio wa Tundu Lissu - Septemba 25

Mimi nawapa tu tahadhari mboga mboga kwamba mpaka sasa mnazoziona ni rasharasha tu, mvua za vuli bado na msizimie mkisikia mtu kaweka mpira kwapani na kuinua mikono.

Huyu sijui atakimbilia wapi kwani majirani wote hawamtaki isipokuwa labda yule wa Burundi. Mtoto akililia wembe mpe umkate pale pale na akililia moto mpe umchome pale pale...si kalilia mwenyewe?
 
Ungeandika kwa kiswahili maana pale Lumumba watahangaika kutafuta dictionary, aliyesema " siku ya kufa nyani mti yote huteleza aliona" mbali
 
NEC wana taman waseme TL ana fanya kampeni usiku kiinyume cha ratiba

SUBIRI KIDOGO
Hana mabango, hatembei na wasanii, hafungi shule wanafunzi waje, hatishii watumishi wa serikali waje, hajajenga flyover, wala railways, wala kununua ndege.

Lakini MAELFU WANAMFUATA.

LISSU ANAKERA JAMANI?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]

Hata Mimi ningepata HEARTATTACK !!!
 
Magufuli this time anajuta sana maana hiki kinachotokea leo ni mbegu alizopanda!!
 
Huko Mara Watavunja Rekodi ya Tanzania.

Ila kila Siku Lissu anaongeza idadi ya wahudhuriaji kuna uchawi gani?[emoji23][emoji23]
Mwanzo watu bado hawakuelewa somo la Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu. "Sasa sasa sasa" mwl alipogundua hilo na kuanza kufundisha hiyo topic na ikawaingia wanafunzi vilivyo ndo matokeo unayoyaona wanafunzi darasa karibia lote wanaelewa somo. Ndo maana kila kukicha maudhurio yanavunja rekodi kila leo.
 
Jamani Mwanza ya wap??? Hebu tuwekee hata clip moja ya maadamano hao tofaut na wahuni wachache mliowanunulia konyangi,,, Mwanza tushamaliza uchaguz zamani sana ni jpm
 
Aisee yanayoendelea mwanza usiku huu sio Mambo ya kawaida taratiiiiibuu naanza kuiona tahriri square maana kilichowapata watu wa mwanza nashindwa kuelewa na hii ndio inafanya kuwaelewa watanzania iwe ngumu. Yani mtu anachinjiwa nyumbani kwao mchana kweupee.

Aisee lisu sio mtu wa kawaida.

Jioni hii kinachoendelea mwanza siamini Kama ni kweli au naota. Mlioko mwanza tupeni ukweli msitie chumvi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…