The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Jiji la Tanga limepitisha rasimu ya bajeti ya Tsh. bilioni 25 kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.491 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/2024, ambayo ilikadiriwa kukusanya Tsh. bilioni 21 kutoka mapato ya ndani.
Akizungumza wakati wa kufunga baraza hilo, Mwenyekiti na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Ndugu Abdul-Rahman Shiloo, amesema kuwa katika mwaka wa fedha uliopita, baraza lilipanga kukusanya Tsh. bilioni 78, na kwa mwaka huu wa fedha 2025/2026, lengo limeongezeka hadi Tsh. bilioni 83, sawa na ongezeko la asilimia 3.2.
Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Baadhi ya madiwani wamesema imani yao kwa bajeti hiyo, kuwa italeta maendeleo katika Jiji la Tanga. ikiwa ni pamoja na kubainisha , kuwa asilimia 40 ya mapato hayo yataelekezwa moja kwa moja kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi, jambo linalotarajiwa kuboresha maisha ya wakazi wa jiji hilo.