Jiji la Tanga watu wanalala sana

Jiji la Tanga watu wanalala sana

Saa 10alfajiri, ukikutana na watu wametoka kazini na misizi usoni na nyungo zao.
 
Imagine sasa hivi ni saa 10 alfajiri, hakuna hata mishe mishe za bodaboda huko nje, yaani mji umetulia tuliii tofauti na mikoa mingine kama Dar, Arusha na Mwanza.
Kweli, uko sahihi. Sana sana utakutana na mmoja /wawili wanaenda msikitini, tena wazee......
Tatizo lao ukitokea ukafanya kazi wakaona kuna kitu unapata, wanakuharibia muwe sawa na siyo kuwa naye akuige awe kama wewe, hapana.
Ukiwa na pikipiki anaziba njia, anachimba mshimo usipite and the like, Wadigo hao!
 
Mara ya mwisho nilienda Tanga 2019 na niliondoka asubuhi sana nilipta bodaboda kama saa 10 alfajir maeneo ya Duga mwembeni na nilikuta wapo kibao ,sijajua uko maeneo gani hapa naongelea Tanga mjini.
 
Mambo ya mamwinyi mambo ya uswahili Swahili sana.

Mwarabu Effect.

Ulikuwa mji mzuri mno.

Tanga ku nani??????

Jibu ni Mwarabu Effect
 
Imagine sasa hivi ni saa 10 alfajiri, hakuna hata mishe mishe za bodaboda huko nje, yaani mji umetulia tuliii tofauti na mikoa mingine kama Dar, Arusha na Mwanza.
Mamwinyi hao

Hawana tofauti na watu wa Lindi na Bukoba mjini
 
Mbona hata Arusha haichangamki muda huo?
Huko Njiro hiace zinaamka saa 12.. napo ni chache, saa 2 mama mihogo ndo anaichemsha.

Dar hiace hawalali
Walau watu wa Indrive hawalali uki request tu hata kama unawahi Flight ya saa 11 alfajiri anakuja

Dar es Salaam nilishangaa kukuta Mamantilie pale Buguruni anasonga Ugali na kuuza saa 8 usiku 🙌
 
Ukitaka kujua maana ya mishemishe kaishi Gongo la mboto na Mbagala 🤣🤣🤣kuna vurugu masaa 24.
Uko sahihi

Ni miji iliyochangamka sana.

Nachopendea Dar es SAlaam ni hiyo hali ya Kuchangamka, yaani muda wote watu wapo busy kwenye Utafutaji.

Maeneo ya Mikoani huo muda wa saa 8 usiku ni muda wa Wanakijiji kuongeza watoto maana ndiyo zoezi maarufu kwao 🤪
 
Back
Top Bottom