Jiko la gesi lilivyozima ndoto na uhai wa Familia ya Abedi Falhum Msangi

Una kiherehere sana....unashindwa kuanzisha Uzi wako ucomment mitazamo yako kadri unavyoweza hadi uvamie nyuzi za watu? Ubishi peleka CHADEMA
Huyu ni mmoja ya wale wenye matusi sana kwenye uzi flani.. mumzoee[emoji3]
 
Poleni sana kwa msiba mzito. Mungu azidi kumjaalia afya mtoto aliyebaki. Kwa kweli hii mitungi ya gesi ni ya kuwa nayo makini.
Binafsi nilishagoma kutumia mitungi mikubwa, ikinilazimu kutumia mtungi mkubwa basi uwe kwenye jiko la nje.
Haya majiko ya plate siyaamini na siyataki kabisa.
Naunga mkono kauli ya Abeid kama unatumia jiko la ndani basi mtungi uwe nje ya nyumba mpira ndio uingie ndani.
 
Daah! poleni sana aisee mkewe alikuwa Classmate wangu Chuo kikuu Cha Mwenge Moshi wapumzike kwa amani
 
Tatizo sio gas bali jamii yetu inatatizo lakutochukua tahadhari.Uzembe ni mwingi sana kwenye maisha yetu.Jamii inapaswa kuelimishwa sana matumizi ya vitu mbali mbali vinavyoweza kuleta maafa.Kuanzia umeme,gas,petrol,vyombo vya moto,barabara,maji na vitu vingine tunavyovitimia kila siku. Wapumzike kwa amani.
 
Yaan mtu yuko ktkt ya moto aingie ndani atoe mke aingie tena atoe mtt aingie tena amtoe mfanyakazi aingie tena atoe mtungi wa ges na kuutupa nje af atoke nje af walale nje kusubiri pakuche duh sio filamu hii kweli!?
 
Kaka hizi ni dudra za mungu ,chukulia mfano ukishaweka mtungi wa gesi nje,je shoti ya umeme utaiweka wapi, je hujawahi kuskia nyumba imeungua kwa sbb ya hitilafu ya umeme, pia utaotoa nje umeme kikubwa ni kumuomba Allah azilinde familia zetu na Mali zetu,.Naunga mkono tahadhari ni muhim, japo alilolipanga Allah lazima litimie narudia lazima litimie tu.
Akili za mwafrica zimejaa makamasi!

Badala uchukue tahadhari unaleta mambo ya Allah na yesu!

Hujui kama ndani ya nyumba iliyofungwa umeme kuna circuit breaker!

Idiot
 
Yaan mtu yuko ktkt ya moto aingie ndani atoe mke aingie tena atoe mtt aingie tena amtoe mfanyakazi aingie tena atoe mtungi wa ges na kuutupa nje af atoke nje af walale nje kusubiri pakuche duh sio filamu hii kweli!?
Sasa unachobisha ni nini mzee huu mkaaa umetokea kweli na ni kweli familia yote imeteketea kwa ajali iyo ya moto wala hakuna uongo wowote apa huu mkasa umetokea kweli kabisa kabisa usipende kubisha bisha kila jambo mzee
 
Naona mtoto aliyekuwa kabaki naye kaumaliza mwendo. Familia yote imeisha.
 
Yaan mtu yuko ktkt ya moto aingie ndani atoe mke aingie tena atoe mtt aingie tena amtoe mfanyakazi aingie tena atoe mtungi wa ges na kuutupa nje af atoke nje af walale nje kusubiri pakuche duh sio filamu hii kweli!?
Utoto unakusumbua, ukikua utajua tu
 
Yaan mtu yuko ktkt ya moto aingie ndani atoe mke aingie tena atoe mtt aingie tena amtoe mfanyakazi aingie tena atoe mtungi wa ges na kuutupa nje af atoke nje af walale nje kusubiri pakuche duh sio filamu hii kweli!?
Hii jeuri ya kushiba na uzima ulionao Leo ndyo unaona Kama umewin maisha Sana ukisoma stor usipoiona haina funzo Kaa kimya.
 
View attachment 2252483
Familia ya Abeid enzi za uhai wao

Habari wakuu ujumbe huu nimeupata kutuko group moja nikaona ni vyema kushare wa Watanzania wenzangu Ili tuchukue tahadhari[emoji24][emoji24][emoji24] Inauma Sana

Ndugu zangu nataka kuwapa uzoefu na ushuhuda wa kifo Cha jamaa na mdogo wangu Abeid falhum,

Asubuhi saa12 ya Tarehe 19, May nimeamka nikashika simu yangu nikakuta Missed Call 08 za Baba yangu. Wakati najiandaa kumpigia nikaona Notification ya msg kuifungua nakuta ujumbe "..abeid na familia yake wamelipukiwa na gesi Jana usiku, wamelazwa Muhimbili.."
Nikampigia Baba, akanambia tu kifupi kuwa taarifa zipo hivyo.
Nikafunga safari muda huo huo kuelekea Muhimbili,

Nikafika Muhimbili haikuwa ngumu Sana kuingia Wodini sababu nilikuwa na kitambulisho kinachonitambulisha kuwa pia ni Medical Personnel.

Mungu wangu naingia wodi ya SEWAHAJI jicho langu linakutana na Ndugu yangu ABEID, ameungua uso wote hauna ngozi, kwa uchungu sana abeid akaanza kulia.

"..akhaa, kaka nimeungua ndugu yangu, nimeungua aisee, niangalie nilivyoungua.." kiukweli Nilishindwa kumkazia Abeid macho yakiwa yamewiva na machozi nikatoka nje ya wodi nikafuta machozi, nilipojiona nipo sawa sawa nikasema sasa naweza kurudi wodini.

Nikamkuta Abeid pia ametulia, nikampa pole kichwani nikasema hapa sina Cha kuongea na Abeid nikatafuta stori ambayo nitazuga nae pale wodini, akatulia! Unajua nilikuwa Nina mawazo na maswali mengi iweje waungue wote watano, nikajisemea hapa Hilo swali ni gumu kuuliza acha akipona atahadithia.

Nikamuaga, nikamwambia naomba nikawaangalie pia Watoto, shemeji na Dada wa kazi.. Iko hivi Abeid alikuwa na familia ya watu wanne na yeye watano. Watoto wawili, Mke na Dada wa kazi, Masikini waliungua woteee.

Kesho nikarudi kumjulia hali mara hii Abeid Wala Hakulia tukawa tunapiga stori pale wodini katikati ya stori bila ya kumuuliza akaanza kunihathia.

"...ilikuwa mida ya saa1 usiku (jumatano) nipo nyumbn wife akiwa jikoni akaniita jiko linasumbua kuwaka ni jiko lile la plate, basi nikaenda jikoni na mwanangu wa mwisho akanifata, nilipofika jikoni Bali kujali harufu ya Gesi nika'switch jiko, kaka! kiasi cha sekunde 0 wote tukawa tunaogelea kwny moto, nikamshika mtoto kukimbia nae nje sabb mlango ulikuwa umerudishwa tu, wote tukiwa tunawaka nikambwaga mtoto nje, ndani zimejaa kelele nikarudi tena ndani, sebule imelipuka pia lkn mtoto mwngn alikuwa chumbani (chumba Cha watoto) nikaingia huko kote kunawaka mwanangu anawaka nikamvuta akiwa analia huku anaungua nikakimbia nae nje, Hilo tukio lote la kuungua ninalokuelezea ni ndani hata dakk 5 hazifiki aisee, Moto mkali nikamtupa mtoto nje, nikawa nimewabakiza Mke na mfanyakazi ndani nikiwa naungua nikaona zoezi la kuingia na kutoka ni gumu nikaenda jikoni sabb jiko na sebule ni karibu, nikaushika mtungi wa Gesi nauburuza kuelekea nje (huku nawaka moto) nikautupa nje. Nikarudi tena ndani moto umepungua nasikia harufu ya ngozi yangu namna inanuka kwa kuungua na moto, Mke wangu na msichana wa kazi wote wameungua sabb ya uoga walikuwa wanagalagala huku wanaungua, nikawavuta nje, Wote tukalala nje tunasubiri msaada wa majirani, wengine wakawa wanatufunika na kutuzima moto wengine wanajaribu kuudhibiti moto kuunguza Nyumba.."

Anamalizia "...braza toa Gesi nje ndugu yangu ni hatari sana, hatari mnoo!!

Baada ya kumaliza kuongea na Abeid, nikamuaga kutembelea SEWAHAJI wanawake kumuangalia Mke wa Abeid na Dada wa kazi, wameungua aisee ingawa wanaongea macho wanaona lakini moto wa Gesi umeunguza miili Yao vibaya sana..

Tarehe 23 Alfajiri mtoto wa Abeid wa miaka miwili Akafariki dunia haraka Saa7 mchana wa siku hiyo hiyo tukamzika, tarehe 24 ikawa ni siku tunayomfariji Abeid huku tukiwa tumemficha taarifa za kifo Cha mtoto wake

Tarehe 25 alfajiri Abeid Akafariki, tukasafirisha kuelekea Moshi- Usangi kumhifadhi Abeid, tupo njiani tarehe 26 May alfajiri tukapigiwa simu Dada wa kazi ambae amelazwa Muhimbili amefariki, tukazika haraka Ili tuwahi taratibu za kumhifadhi dada wa kazi, ikawa ni lazima tusafirishe Mwili wa Dada wa kazi maana ni Mkazi wa Masasi.

Tukasafirisha tukazika tukarudi Dar.

Mind you wodini amebaki Mke wa Abeid, na mtoto wa miaka mitano.
Tarehe 31 May Mke wa Abeid Akafariki.

Familia ya watu watano, wanne wamefariki imebaki na Mtoto mmoja tu, Tunamuombea Mwenyezi ampe Ahueni.

Abeid alipokuwa kitandani NENO ambalo alikuwa akisisitiza tuwe makini na Gesi, tufanye namna Gesi ikae nje ya jiko, mpira wa Gesi ndiyo uingie jikoni hata ikivuja na kulipuka haiwezi kuleta madhara kiasi kile.

UPDATE JUNI 06, 2022: Binti pekee aliyekuwa amebaki Afariki dunia.
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]Rest In Peace

Sent from my V2027 using JamiiForums mobile app
 
Daah huyo jamaa namfahamu sana na alikuwa kamaliza Udsm kwenye 2016 hivi alikuwa anasome uchumi sikufahamu kuwa ni yeye aliyepatwa na mkasa huu

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe
 
Pumziko La Amani wapate.

Ila kwa kweli ukisikia harufu ya gesi usifanye chochote, wote tokeni nje na milango na madirisha yafunguliwe...kama inawezekana kafunge gesi isiendelee kutoka...msubiri mpaka hewa irudi kwenye hali yake.

Kushauri Mitungi kukaa nje ni sawa lakini Nyumba nyingi za kupanga hazijaandaliwa kuwa hivyo, Watumiaji wengi wanalala na Mitungi ndani.
 
View attachment 2252483
Familia ya Abeid enzi za uhai wao

Habari wakuu ujumbe huu nimeupata kutuko group moja nikaona ni vyema kushare wa Watanzania wenzangu Ili tuchukue tahadhari[emoji24][emoji24][emoji24] Inauma Sana

Ndugu zangu nataka kuwapa uzoefu na ushuhuda wa kifo Cha jamaa na mdogo wangu Abeid falhum,

Asubuhi saa12 ya Tarehe 19, May nimeamka nikashika simu yangu nikakuta Missed Call 08 za Baba yangu. Wakati najiandaa kumpigia nikaona Notification ya msg kuifungua nakuta ujumbe "..abeid na familia yake wamelipukiwa na gesi Jana usiku, wamelazwa Muhimbili.."
Nikampigia Baba, akanambia tu kifupi kuwa taarifa zipo hivyo.
Nikafunga safari muda huo huo kuelekea Muhimbili,

Nikafika Muhimbili haikuwa ngumu Sana kuingia Wodini sababu nilikuwa na kitambulisho kinachonitambulisha kuwa pia ni Medical Personnel.

Mungu wangu naingia wodi ya SEWAHAJI jicho langu linakutana na Ndugu yangu ABEID, ameungua uso wote hauna ngozi, kwa uchungu sana abeid akaanza kulia.

"..akhaa, kaka nimeungua ndugu yangu, nimeungua aisee, niangalie nilivyoungua.." kiukweli Nilishindwa kumkazia Abeid macho yakiwa yamewiva na machozi nikatoka nje ya wodi nikafuta machozi, nilipojiona nipo sawa sawa nikasema sasa naweza kurudi wodini.

Nikamkuta Abeid pia ametulia, nikampa pole kichwani nikasema hapa sina Cha kuongea na Abeid nikatafuta stori ambayo nitazuga nae pale wodini, akatulia! Unajua nilikuwa Nina mawazo na maswali mengi iweje waungue wote watano, nikajisemea hapa Hilo swali ni gumu kuuliza acha akipona atahadithia.

Nikamuaga, nikamwambia naomba nikawaangalie pia Watoto, shemeji na Dada wa kazi.. Iko hivi Abeid alikuwa na familia ya watu wanne na yeye watano. Watoto wawili, Mke na Dada wa kazi, Masikini waliungua woteee.

Kesho nikarudi kumjulia hali mara hii Abeid Wala Hakulia tukawa tunapiga stori pale wodini katikati ya stori bila ya kumuuliza akaanza kunihathia.

"...ilikuwa mida ya saa1 usiku (jumatano) nipo nyumbn wife akiwa jikoni akaniita jiko linasumbua kuwaka ni jiko lile la plate, basi nikaenda jikoni na mwanangu wa mwisho akanifata, nilipofika jikoni Bali kujali harufu ya Gesi nika'switch jiko, kaka! kiasi cha sekunde 0 wote tukawa tunaogelea kwny moto, nikamshika mtoto kukimbia nae nje sabb mlango ulikuwa umerudishwa tu, wote tukiwa tunawaka nikambwaga mtoto nje, ndani zimejaa kelele nikarudi tena ndani, sebule imelipuka pia lkn mtoto mwngn alikuwa chumbani (chumba Cha watoto) nikaingia huko kote kunawaka mwanangu anawaka nikamvuta akiwa analia huku anaungua nikakimbia nae nje, Hilo tukio lote la kuungua ninalokuelezea ni ndani hata dakk 5 hazifiki aisee, Moto mkali nikamtupa mtoto nje, nikawa nimewabakiza Mke na mfanyakazi ndani nikiwa naungua nikaona zoezi la kuingia na kutoka ni gumu nikaenda jikoni sabb jiko na sebule ni karibu, nikaushika mtungi wa Gesi nauburuza kuelekea nje (huku nawaka moto) nikautupa nje. Nikarudi tena ndani moto umepungua nasikia harufu ya ngozi yangu namna inanuka kwa kuungua na moto, Mke wangu na msichana wa kazi wote wameungua sabb ya uoga walikuwa wanagalagala huku wanaungua, nikawavuta nje, Wote tukalala nje tunasubiri msaada wa majirani, wengine wakawa wanatufunika na kutuzima moto wengine wanajaribu kuudhibiti moto kuunguza Nyumba.."

Anamalizia "...braza toa Gesi nje ndugu yangu ni hatari sana, hatari mnoo!!

Baada ya kumaliza kuongea na Abeid, nikamuaga kutembelea SEWAHAJI wanawake kumuangalia Mke wa Abeid na Dada wa kazi, wameungua aisee ingawa wanaongea macho wanaona lakini moto wa Gesi umeunguza miili Yao vibaya sana..

Tarehe 23 Alfajiri mtoto wa Abeid wa miaka miwili Akafariki dunia haraka Saa7 mchana wa siku hiyo hiyo tukamzika, tarehe 24 ikawa ni siku tunayomfariji Abeid huku tukiwa tumemficha taarifa za kifo Cha mtoto wake

Tarehe 25 alfajiri Abeid Akafariki, tukasafirisha kuelekea Moshi- Usangi kumhifadhi Abeid, tupo njiani tarehe 26 May alfajiri tukapigiwa simu Dada wa kazi ambae amelazwa Muhimbili amefariki, tukazika haraka Ili tuwahi taratibu za kumhifadhi dada wa kazi, ikawa ni lazima tusafirishe Mwili wa Dada wa kazi maana ni Mkazi wa Masasi.

Tukasafirisha tukazika tukarudi Dar.

Mind you wodini amebaki Mke wa Abeid, na mtoto wa miaka mitano.
Tarehe 31 May Mke wa Abeid Akafariki.

Familia ya watu watano, wanne wamefariki imebaki na Mtoto mmoja tu, Tunamuombea Mwenyezi ampe Ahueni.

Abeid alipokuwa kitandani NENO ambalo alikuwa akisisitiza tuwe makini na Gesi, tufanye namna Gesi ikae nje ya jiko, mpira wa Gesi ndiyo uingie jikoni hata ikivuja na kulipuka haiwezi kuleta madhara kiasi kile.

UPDATE JUNI 06, 2022: Binti pekee aliyekuwa amebaki Afariki dunia.
DUUUH aiseee!!omba yasikukute!!
 
Back
Top Bottom