Uchaguzi 2020 Jimbo la Ubungo: ACT-Wazalendo yadaiwa kumuwekea pingamizi Meya Jacob na madiwani wote wa CHADEMA

Uchaguzi 2020 Jimbo la Ubungo: ACT-Wazalendo yadaiwa kumuwekea pingamizi Meya Jacob na madiwani wote wa CHADEMA

Taifa la mitandaoni wakiandamana kwa malaika wa chadema...

Mnatia aibu aisee
 
Hivi si ni kitila na ZITTO ndio walianzisha ACT?.. Watu wanasahau haraka Sana.. Boniface asishangae sana kuwekewa mapingamizi na ACT.. BEWARE: Politicians at work.
Kwa hiyo wagombea wa CHADEMA ni dhambi kuwekewa pingamizi siyo?

Ufipa ni mfupa wa kichwa
 
Dah inasikitisha sana Zitto naye kubariki hayo Mapingamizi ,,,Upinzani imara ni kupambana na CCM na sio Upinzani mwenzako ,kazi ya kupambana na wapinzani wamepewa Lipumba na Shibuda na wapo kwenye payroll.
Mimi sioni upinzani hapo, naona ushindani tu
 
Hahahahahahaha yeye akiwekea mapingamizi wengine hawakimbiliii mitandaoni lakini kawekewa yeye fasta anakimbilia mitandaoni kulia lia Chadema wameshaona mitandaoni kama ndo HQ yao si Ufipa tena

Chadema wanadanganywa na twakimu za kuwa
Wananchi wenye kuaccess Internet Tanzania ni milion 22.3 sawa na asilimia 41.4 ya wananchi wote sijui kama walishajiuliza Tanzania ni mambo gani au vitu gani vinafatiliwa au kugoogle sana kwenye Internet ?

Watanzania wengi wanaotumia internet hawafatilii siasa kwenye mitandao ni asilimia chache sana hata ukifanya utafiti utagundua ni Twitter na Jamii forum tu ndo wanafatilia siasa but sehemu au mitandao mingine nadhani unajua nn kinafatiliwa sasa jiulize Twitter na JF ni watanzania wangapi wana account au kuijua?

Tanzania bado main stream media(TV,Magazeti,Radio) bado zinanguvu sana na bado zinafatiliwa na watu wengi kwa sababu kupata taarifa huko ni free au cheap kulinganisha na mitandaoni sasa wanapogeuza mitandao kama ndo sehemu muhimu ya kuwapasha habari Watanzania wanatakiwa kujua nilazima uwe na bando kitu ambacho mtu wa mikoani hawezi kununua GB 4 eti kumuangalia Tundu Lissu akiutubia You tube au Chadema wanasema nini mitandaoni .
Maelfu ya wananchi waliojitokeza kumdhamini Lissu walipata wapi taarifa iwapo TBCCM na tv zingine radio na magazeti vililazimishwa kuimba mapambio ya watawala? Nguvu ya social media wala usi under-rate utakuwa unajidanganya katika karne hii.
 
Tatizo hawa ACT si ndio walikuwa wanalilia kuungana na Chadema kuweka mgombea mmoja,sasa leo inakuwaje uwawekee pingamizi partner wako na kumuacha adui wenu Mkuu?
Nadhani kama wangeungana harafu, harafu act akaweka pingamizi sehemu ambayo cdm imesimamisha mgombea, hapo pangekuwa na hoja. Kwasasa act yupo huru.
 
Mlimfukuza Zitto mkafikiri asingefanikiwa kisiasa sasa mnabweka bweka humu JF awabebe
Kama sikosei December 2012 au 2013 alianzisha uzi humu wa kuomba samahani viongozi wenzie wa Chadema wanachama na wapenzi na pia kutoa ushirikiano wa hali ya juu. Kukawa na maswali mengi ikiwemo umefanya kosa gani na maswali kuhusu matukio miezi miwili kabla ya uchaguzi Mkuu 2010 alijikanyaga kanyaga sana nadhani hata mwenyewe alijistukia hivyo akaomba ule uzi ufutwe na ukafutwa.
 
Ben alikuwa na Mbowe baadae ndio tukasikia kapotea
Kwa point hii na yaliyokua yakiendelea in those days, tunayo haki ya kumuuliza Kaka Zitto , Yuko wapi Ben Saanane?? (We all remember their affiliations!)

Tukiamua kutoka nje ya box ili kutatua shida zetu ni wazi fahamu zetu zitafunguka na kutuacha “Uchi” hata sisi wengine!
 
Ukimtaja Jack huwezi kumwacha Mzee Othman!

CCJ ilifia wapi??

Kumbukumbu ni jambo muhimu!
Hiyo na wewe ndio kumbukumbu yako, mi nimetaja cha ACT na ACT ilikua lazima watafute kiongozi "mzuri" aina ya zitto na yule katibu mkuu wa maji ambaye ni mgombea wa ubungo
 
Tuwekane sawa tu, Jacob ameenguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea wa ACT, mgombea wa CCM alimuwekea pingamizi mgombea wa ACT.
 
CCM imechokwa Sana na mgombea wake hana mvuto kabisa. Kumbe hata watu kule Dodoma wamekusanywa kwa nguvu!!
2501931_IMG_20200829_223607.jpg
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom