Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

Jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano siyo Songea Mbano Sultani wa wangoni wakati wa vita vya Majimaji 1905 - 1907

Mtanganyika...
Ghadhabu haziweki mjadala wa tija zaidi zinatanguliza kuitana majina, kukashifiana na kejeli.

Muhimu hapo ilikuwa kusema lolote kuhusu hayo yaliyoandikwa na Ilunga.

Hayo mengine ni maneno ambayo hakika umeyaandika kwa hasira hivyo sitayapatiliza.
 
Mtanganyika...
Ikiwa unaona Tanzania Notes and Records ni kitabu cha hadithi sitakulazimisha kuamini kuwa ni jarida la kisomi.
 
Hivi haya mambo sijui ya fuvu la Mkwawa sijui jina la Abdalah, sijui Sultani Songea Mbano, hivi yanatusaidia nini sasa hivi katika kukabiliana na changamoto za maisha yetu ya kila siku?
 
Yericko,
Katika uandishi dots huwa tatu tu ...

Hili nimekueleza mara nyingi.
Kuwa nisemayo ni ''takataka,'' sitokujibu kwani ni vigumu kujibu matusi.

Lugha yako ni kali umeghadhibika.

Lakini ndani ya nafsi yako unajua kuwa umemnakili Dr. Harith Ghassany.

''Ilisadifu kuwa siku moja Okello alisafiri kwenda Dar es Salaam akifuatana na Jaha Ubwa, aliyekuwa katibu wake. Walipokuwa wanatarajiwa kurudi Zanzibar, Karume, Yusuf Himid, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walikwenda uwanja wa ndege kumsubiri.

Siku hiyo anaikumbuka vizuri Luteni Hashil Seif aliyekuwa ofisa wa zamu kwenye kambi ya jeshi huko Migombani karibu na uwanja wa ndege. Alipigiwa simu akitakiwa aende kwa haraka uwanja wa ndege. Hakuambiwa anaitiwa nini.

Alipofika ndipo alipoambiwa kwamba kuna ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya Mashariki iliyokuwa inakuja kutoka Dar es Salaam ndani yake wakiwemo pia Okello na Jaha Ubwa. Akaelezwa kwamba awaruhusu abiria wote pamoja na Ubwa washuke, lakini amzuie Okello asishuke. Halafu amwambie rubani ampeleke Okello Kenya.

Hashil naye akampigia simu komredi mwenzake Luteni Amour Dugheshina kumwita aende uwanja wa ndege amsaidie. Maluteni wote wawili walikuwa na bunduki za aina ya ‘machine gun’.

Ndege ilipotua walipanda ndani ya ndege, wakampokonya silaha Okello na kutekeleza amri waliopewa. Rubani wa ndege alikasirika sana. ‘Uso wake ulighadhibika, utafikiri mnyama aliyekosewa risasi,’ alieleza Hashil.

Lakini rubani hakuwa na la kufanya ila kuiwasha ndege na kuelekea Kenya.
Huku nyuma Salim Rashid akampigia simu Oginga Odinga, Makamu wa Rais wa Kenya, kumuarifu kwamba wamemfukuza Okello na ‘wanamrejesha’ Kenya. Alifanya hivyo kwa makosa kwa sababu kutokana na jina lake akifikiri kuwa Okello ni Mjaluo kutoka Kenya.

Kumbe alikuwa mtu wa kabila la Acholi aliyezaliwa Uganda na alikwenda Unguja kabla ya kuhamia Pemba ambako alikuwa mwashi, mtiaji rangi nyumba na mpasuaji mawe.
Swali la kujiuliza hapa ni; je, iwapo kweli Okello alikuwa ‘kiongozi mpendwa wa Mapinduzi’ ilikuwaje wafuasi wake na wanamapinduzi wenzake wasimtetee alipoadhiriwa uwanja wa ndege na kufukuzwa nchini? Ilikuwaje akafukuzwa kwa urahisi hivyo?''
 
Son,
Nilichofanya ni kueleza kuwa historia imepindishwa na hii imefanya ipungue.

Nimeeleza hayo ili kuikamilisha na watu wajue ukweli.

Hili si jambo kukukasirisha labda kama unachomwa na ukweli.

Ikiwa ukweli unakuumiza basi ipo sababu.
 
Mohamed Said

Hebu tupatie historia ya waarabu hapa tz, walianza kuja lini, base zao zilikuwa wapi na shughuri kuu zao zilikuwa nini, na nini ulikuwa mchango wao katika kufanikisha ukoloni na utumwa.

Hivi unafikiri ni kwanini majority ya watu wa bagamoyo bado ni waislam kama unavyosema huko iringa songea walikuwa ni waislam.
Shukrani.
 
Shungurui,
Unaweza ukaisoma hiyo historia wewe mwenyewe kwani inafahamika na imeandikwa kwingi sana.
 
Unajua mambo mengine bwana.....hakuna muhehe yoyote ambaye alimfahamu mkwawa kama sijui nani unayemsema wewe....kama alipewa hilo jina sikatai maana ni kweli alikuwa na urafiki na waarabu...lakini waarab walimkuta mkwawa ni mtu mzima na tayari kashakuwa mtwa...ndiyo jina la cheo chake kwa kihehe na si sultan kama unavyomuita wewe....kwahiyo kwa umri huo na cheo chake hakuna sehemu alipowatangazia wananchi zake kwamba kabadili jina..maana kubadili jina kwa muhehe wakati ule ilikuwa lazima ufanye tukio la kishujaa ndipo upewe ruhusa ya kujipa jina au kupewa jina....hata hilo jina la mkwawa alipewa akiwa kijana si la kuzaliwa nalo...hilo jina ni kifupisho cha jina mkwavinyika..yaani mtwaa nchi...hali kafhalika kwa songea mbano wanaandika jina lenye asili ya songea na kabila lake hayo ya kiarabu nayo pia ni matokeo ya ukoloni....ila ukoloni huo kwasababu ni wa kiarabu wewe huuoni kwasababu umepigwa upofu wa iman.....binafsi naona wako sawa kwasababu wameenziwa kwa majina yao haswa na si majina ya kigeni...wangekuwa waliitwa majina ya kizungu hapo ningekusaidia kulaumu
umemuekimisha vizuri sana,ila lazima atagoma kukuelewa
 
Mengi yamejificha hayajulikani, hadi hii leo watu hawajui kama lile fuvu si la Mkwawa. Watafiti wenyewe waliweka shaka, ila walificha tu kwani aibu kwao kueleza wamezidiwa ujanja na mtu mweusi. Lile fuvu wajerumani walikata kichwa kwa kumkuta mtu aliyeangukia kwenye moto baada ya wao kusikia mlio wa risasi, sura haikujulikana maana iliharibika na moto.

Mkwawa alikuwa ni kichwa haswa kimbinu na kila namna, haitosahaulika alivyochukua bunduki ya mjerumani akaifumua na kuunda vifaa vinavyofanana kisha akafunga na kupata bunduki nyingine.

Yule aliyechukuliwa fuvu lake ni mlinzi wake na ndiye aliyekuwa naye mahali ambapo kulisikika mlio wa bunduki kwa mujibu wa kitabu kimoja, aliwachezea akili wajerumani. Eneo hilo hakuwa peke yake walikuwa watatu unaweza kuamini walinzi waliruhusu ajiue, au mlinzi mmoja alitoroka na kumwacha ajiue?
Eneo hilo miili ilikutwa miwili mmoja ndo uso uliangukia kwenye moto, mwingine ulijulikana wazi ni wa mlinzi mmojawapo naye hakuuawa na wajerumani sasa nani kamuua huyo mlinzi mwingine?


Hapo ndiyo utabaini wazungu walichezewa akili, wakaamua kuficha hii aibu
tajajina la hicho kitabu
 
Juan...
Umeghadhibika na kutumia neno, ''upumbavu.''
Hii ni moja ya ibra ya historia hii kila inapoelezwa ghadhabu zinapanda.

Umesema mengi na sitoweza kukujibu yote.
Nina swali moja tu kwako.

Kwa nini historia hii inakukera?
kwa nn hujibu maswali yote?,jibu yote hasa hilo la ugaidi wahusika kuwa na majina ya Kiarabu,je ni sahihi kuwahusisha wao na dini ya Kiislamu kwa sababu ya majina yao?
 
Mtemikwilla,
Kilichonifanya nitaje Uislam ni kuwa baada ya uhuru zilifanyika jitihadi
ya kuifuta historia ya Uislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa ajili hii nikaamua kufanya kuiandika ili watu waamue nani mkweli
kati ya historia rasmi iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni ipi ya kweli
ipi ya uongo:

GImHALCx9nW4x1xJCDWjfSfdEAXf3Tt8nnPGlooNspCrU2qbiCSojJFIhXatI0JXf16eeMHcmUJfe0kFgWtbCB9t3jtIsX4hYeCVhc6HFUn-g7gvmDeUphIWORTEfc4YYOj9hOqipmKsVY71lvI2mU_RPJwEhWCCD9nYTlPyV0vFDTncKmjotLR0IcoabbEr-ODbmHcq26kMgXkGgq0_XZEgg9xcsDCqkgK-wP2J8yv1XYvxZl4KDq6JnVlymth0LrvPVxvd4MF5lpLeu-cgjuxZahg-R8Xhs44xMewTUOZ4YgOCA5TsrBVz_FvswA8ff5X_1OnS5W3K_PGZKOfFV8P7p8r5g_oN74C_IyUm0ZRfy6ZwoDYLWP0JJ9U_Zub5rhgY62Ci4x5-znNvW3-C2Em5socupNhgUxckHYMCMuHeeoeJYwvFYotGYIY58XA1XijGM2Zi1zhmluZoGqcIpUY49xuagCk8V2ukuywA0krXpBzRJCI7bLSdPrw7LUHQNjP7sJGP0ncia2i7AoNNzbzIlpJrp2mTCdY0xAr1ZgvPp488sERgfNNBC4w2GXK88-Rugiq_NkB21wqip7eV6ScLll4kjPly_yxgmQhi=w141-h220-no
Sorry,naomba unijuze,walipigania uhuru kama Waislamu ama kama Watanganyika?,na kama walipigania uhuru kwa mwamvuli wa dini yao nini yalikuwa malengo yao baada ya uhuru kupatikana?
 
Endeleeni kubishania majina wakati wenzenu tunakamuana kuchangishana hela za kujenga shule na hospitali,halafu baadae mtaendelea kuimba wimbo wenu wa mfumo Kristo
 
Unajua mambo mengine bwana.....hakuna muhehe yoyote ambaye alimfahamu mkwawa kama sijui nani unayemsema wewe....kama alipewa hilo jina sikatai maana ni kweli alikuwa na urafiki na waarabu...lakini waarab walimkuta mkwawa ni mtu mzima na tayari kashakuwa mtwa...ndiyo jina la cheo chake kwa kihehe na si sultan kama unavyomuita wewe....kwahiyo kwa umri huo na cheo chake hakuna sehemu alipowatangazia wananchi zake kwamba kabadili jina..maana kubadili jina kwa muhehe wakati ule ilikuwa lazima ufanye tukio la kishujaa ndipo upewe ruhusa ya kujipa jina au kupewa jina....hata hilo jina la mkwawa alipewa akiwa kijana si la kuzaliwa nalo...hilo jina ni kifupisho cha jina mkwavinyika..yaani mtwaa nchi...hali kafhalika kwa songea mbano wanaandika jina lenye asili ya songea na kabila lake hayo ya kiarabu nayo pia ni matokeo ya ukoloni....ila ukoloni huo kwasababu ni wa kiarabu wewe huuoni kwasababu umepigwa upofu wa iman.....binafsi naona wako sawa kwasababu wameenziwa kwa majina yao haswa na si majina ya kigeni...wangekuwa waliitwa majina ya kizungu hapo ningekusaidia kulaumu

[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Luggy,
Inaelekea hujui historia ya Waislam wa Tanzania.

Ungekuwa unajua usingekuja na kauli hiyo.

Baada ya uhuru Waislam waliitisha Muslim Congress 1962 na 1963 na waliamua kujenga shule nchi nzima na Chuo Kikuu.

Nawaachie wengine wakueleze nini kilitokea.
 
Luggy,
Swali lako umelikosea kuuliza.
Ungeuliza hivi.

Nini kiliwasukuma Waislam kuwa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika?
 
Back
Top Bottom