Myoyambend,
Juan Manuel hajasome kitabu changu ndiyo sababu anajisemea tu kuhusu
Kilimanjaro.
Wakati wa ukoloni pakijulikana kama Jimbo la Kaskazini jimbo likiunganisha
sehemu za Arusha na Moshi.
Hebu tumpe Juan Manuel historia kidogo ya pale Moshi mjini na ikiwa hakutosheka
In Sha Allah nitampandisha Mgombani na haya ninayoweka hapa ni kutoka kitabu
cha Abdul Sykes:
"Inasemekana miongoni mwa matawi yote ya TANU nchini Tanganyika, tawi pekee lililoungwa mkono na wanawake na wao kuwa ndiyo nguvu kuu ya chama, lilikuwa tawi la TANU la Moshi mjini. Nguvu kuu ya TANU ilikuwa wanawake waliokuwa wakiuza mbege, pombe maarufu ya kienyeji huko Kilimanjaro. Uuzaji wa pombe huko Kilimanjaro ilikuwa ni kazi ya wanawake tu, wanaume hawakujishughulisha nayo. Mkuu wa kilabu cha pombe alikuwa mwanamke mmoja wa Kimasai, Mama Binti Maalim. Ingawa mume wa Binti Maalim, Jumbe Mohamed, alikuwa mtumishi wa serikali, na kwa hiyo alijitenga na siasa, hili halikumzuia mke wake, Binti Maalim kuwa mwanachama na mwanaharakati wa TANU. Binti Maalim alihakikisha kwamba kila mwanamke aliyekuwa akifanya biashara mahali pale alikuwa mwanachama wa TANU na alikuwa akitoa sehemu katika kipato chake kusaidia harakati za kudai uhuru. Wanachama wa mwanzo kujiunga na TANU walikuwa wale akina mama wauza pombe waliohamasishwa kujiunga na chama na Mama Binti Maalim.
Nafasi ya wanawake katika harakati mjini Moshi inaweza kuonekana katika katika safari yake ya pili ya Nyerere Kilimanjaro. Katika safari hiyo Nyerere alifikia nyumbani kwa Bibi Halima Selengia aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya tawi la TANU Moshi. Safari yake ya kwanza Nyerere alifkia KNCU Hotel (Hoteli ya Kilimanjaro Native Cooperative Union). Wakati huo TANU ilikuwa haijaota mizizi. Lakini katika safari yake ya pili wanachama walidai kwamba lazima Nyerere atayarishiwe malazi yake na TANU."
Mkuu historia yako naikubali maana inazungumzia mambo madogomadogo ambayo ki ukweli historia za nchi huwa hazi ya accomodate, nakumbuka wakqti nipo high school pake Benjamin nilisoma HGL na kwa huu mchepuo ulinifanya kusoma vitabu vingi hasa vya riwaya na tamthiria na kuba kitabu kinoja kiliitea A letter from who reads" mwandishi simkumbiki ila nachotaka kusema hapa ni kwamba kunashairi moja lililokuwa likielezea difa alizopewa mfalme.mmoja wa china aliyeujenga ukuta mkubwa wa nchi ile lakin mwandishi baadae anauliza hivi huyu nfalme alikuwa pekeyake?, anaendelea kuuliza waapi watu waliochanganya udongo wakati wa ujenzi?, wako waapi walioveba kokoto za zege?, je hakuna hata aliyempikia mfalme wakati wa ujenzi?, yan mwandishi anaukiza maswali ambayo majibu take kuyapata ni ndoto.....
hicho ndicho ninachokuona wewe unajaribu jukifnya na mimi kila siku nimejuwa nikivutiwa sana na haya majina unayoyaeleza kama akina abdulsyjes na ally sykes, mzee tambaza mimi hata bado ntafuta kumjua baba yake mzazi wa raisi wetu mzee mrisho kikwete kwenye harakati za uhuru maaana naamini hata kama wewe hujamtaja lakini mimi naamin pia anamchango na uhuru wa hii tanzania yetu.......
mimi nisichokubaliana na wewe ni kwamba wewe unatumia dini kama sababu ya wao kutotajwa kitu ambacho mimi sikikubali.......
huu ni mfumo tu wa ulimwengu kama tunavyo msikia sana marehem Patrice Lumumba Kongo ila kuna watu wliomsaidia mpaka yeye kufika pale ila hatutakuja kuwajua kamwe....leo hii utasikia museven alimtoa Obote madarakani na kushika nchi unadhani alikuwa pekeyake?, mandela huyo hapo anamasifa kibao watu hawajui hata kama kuna mtu anaitwa Otambo kwa maana ya Oliver Tambo ambaye ndiye aliyekuwa mpambanaji mkuu muda woote mandela akiwa jela........
na hawa watu inatokea tu nyota inawawakia kuwa maarufu kuliko wenzao kitu ambacho binafsi sikipendi ila ndivyo inavyoonekana kuwa kila mahali.......na nataman tuachane na mfumo huu kama ikiwezekana
ninachomaanisha ni kwamba kutotajwa kwa ndugu woote waliopigania uhuru au kutoa mchango kwenye hayo mapambano yapaswa kukumbukwa tena kila mkoa na si tu dar........ila kusema kwamba waislam hawatamkwi sababu ya dini yao hilo nalikataa jwa nguvu zangu zote kwani kama ingekuwa ni mkakati hakuna mtu anayewezabkushindana na watu wenye imani...
sasahivi kuna matishio mengi ya ugaidi na bahsti mbayabnikikufauatisha mtindo wa kutumia majina unaoutumia wewe utakuta wengi kama si wote watuhumiwa wa ugaidi huwa na majina ya kiislam na ulishawahi kusikia kiongozi yeyote akisema waislam ni magaidi?, hakuna watasema tu kuwa kuna magaidi wamekutwa na siraha kwenye nyumba ya ibada........
hapa sababu ni ile ile hakuna mtu aliyewahi kupigana kujaribu kuiua imani flani akafanikiwa kwani imani ni kitu kingine..........
nilifurahi kwente mahojiano yako na yule mtu wa studio pale alipokuuliza kwa jazba kuwa TANU ilifika mahala ikamezwa na dini zingine njebya waisam na wakaamua hata kukataza "asalam aleykum"(mniwie radhi kama nimeikosea) kama salaam na wewe ukamjibu jibu zuri sana kuwa waislam wenyewe kwa kuyasoma mazingira hawakutaka tanu kuonekana kama chama cha kiislam......
na ndio waliokuwa hata hatwaitikii wakisalimiwa swali ni je kama watu wenyewe walikataa udini kwenye chama unadhan kwenye serikali si itakuwa zaidi...
kikubwa hapa ni kwamba kwakweli watu walishachoka na ukoloni na walijuwa hawajali ni nani atakaye watoa kwenye hayo makucha bila kujali dini rangi walankabila, yan wao walikuwa hawawazi kabisa huu udiniudini na ndiyo maana nadhan walishinda.....
siyo kwamba wadini hawakuwepo walikuwepo ila walishindwa na baada ya na mambo yana wawia magum wakaamua kujiunga tanu ila mimi siiamini hiyo nia yao kwa dhat kwan naamin walitua zile slogan za "if you cant fight him join him" na kwa staili hii malalamiko hayatakoma na ndito maana tunataka mtu yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu asilete story za uchochezi kama hizi za kwako....
mi ninaamini kwa story kama hizi za kwako kuna mtu mahala alikosa kazi kihalali kabisa ila akisha kukudoma hapa na sababu jinalake ni la kiislam ataanza kuchukia viongozi na watanzania woote wanaopenda amani na mtu huyo itakuwa tahisi hata kwa yeye kujiua huku akiondoka na wengine kitu ambacho si hatari tuu bali ni kibaya.............
kwani duniani kote pepetrous woote wa majanga ama mauaji ya kimbali wao wenyewe huwa hawafi ila wanawasababishia wengine kuangamia kwa ajili ya ambition zao na ndiyo maana sintaacha usemi wangu wa "MCHEZO WAO MAUTI YETU"
hebu acha mr Mohammed.