Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

Mzee Mohamed Said,

Hebu msome Prof Karim F Hirji, MuIslam mwenzako bila shaka, kwenye #RaiaMwema ya leo, pengine kuna utakaloambulia ili wajuze na mashabiki wako humu. Huyu ni msomi na mtafiti zaidi yako anayelitakia mema TAIFA hili.

Kumbe ulisoma St. Joseph Convent, moja ya shule alizotaifisha Mwalimu ili nanyi mpate nafasi ya kusoma!
 
Last edited by a moderator:
Mods bwana!! wanaporuhusu muzi kama huu wenye mhadhara wa ku-propagate chuki wanaona wanajeeenga!!
 
Mods bwana!! wanaporuhusu muzi kama huu wenye mhadhara wa ku-propagate chuki wanaona wanajeeenga!!

Haya mabadiliko ya ghafula ya hisia za kidini tunayoyashuhudia katika mitandao mbalimbali ya kijamiiyanatoka kweli chini katika jamii yetu au yanatoka mahali wengi tusipopajua.Yanaaksi hali halisi ya mahusiano tuliyonayo katika jamii? Posts nyingi zimesheheni chuki na hisia kali za kidini. Muislamu anamuonamkristu kama adui yake mkubwa, na mkristo anamuona muislamu kama adui yakemkubwa. Lakini ukweli halisi mitaani uko hivyo? Nadhani jibu la haraka hatakukaribia bado. Lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna wachache wanaotakakutupeleka huko. Kwa maslahi gani, ni vigumu kujua bila kufanya utafiti. Inakuwaje tunakuwa maadui katika mitandao ambako mara nyingihata majina tunayotumia niyakuazima, na tunakuwa marafiki makazini, mashuleni,majumbani, michezoni, siasani na katika sehemu nyingine za harakati zakimaisha? Leo Hamisi na Jonh wanapanga katika nyumba moja. Asubuhi wakiendakazini wanapeana lifti katika magariyao, wakiwa kazini wake zao wanaombana chunvi na viberiti, lakini leo katikamitandao ya kijamii wakiwa katika miwani yao ya mbao wanapeana majina mabaya nakuchafuana kwa hisia za kidini. Hii kwahesabu ya kawaida inatoa jibu kwamba chuki hizi za mitandaoni hazitokani nahali halisi ya maisha tuliyonayo wala tuliyokuwa nayo huko nyumba, bali nitaswira ya hali ya maisha ambayo wachache baadhi yetu wanataka tuyaishi hukombeleni. Tuharibu historia yetu ya Tanzania. Tuharibu upendo wetu wa kiasili wakitanzania na amani yetu na hatimaye wao wapate hicho wanachokitaka na kutuachakatika maisha ya porini. Wachache wanataka kutumia dini kufanikisha hilo. Wamejaribukutumia siasa hawakufanikiwa na ukabila pia. Mafanikio yao yanataka kupatikanakatika dini. Nijuavyo mimi, dini, iwe uislamu au ukristo, kwa asili yakeinafundusha amani na upendo katika jamii. Ukriso unafundisha falsafa ya “shavula kushoto kwa la kulia”, neno “islamu” maana yake ni amani. Sasa haya yakuchukiana kwa misingi ya dinitunayapata wapi? Kwa nini nadharia zachuki zinazidi kupata nguvu kadiri muda unavyokwenda? Watanzania hatuwezi kujifunza kwa uzoefu wa nchinyingine zilizogawanyika kidini kama Nigeria, Afrika ya Kati na kwingineko? Ni nani ananufaika na atharizinazotokea katika nchi hizo kwaajili ya chuki za kidini, bila shaka ni watuwengine wasionekana. Ushauri wangu kwa watanzania wenzangu na hasa vijana nikwamba tuwe makini kwa kila tunachokisikia. Tuchukuwe tahadhari kubwa maanakuna uwezekano wa kuwepo kwa watu wasioitakia mema nchi yetu. Wasijewakafanikiwa mambo yakaharibika tukabaki majuto watoto wa wajukuu. Hizo dinitunazodai kuwa tunazitetea tukashindwa kuzitekeleza na maisha ya duniatunayoyapigania tutashindwa kuendelea kuyafaidi na watoto na wajukuu zetu watabakikuyasoma katika vitabu vya historia. Watanzania tuache kucheza na hisia za kidini “michezo yenu nimauti kwetu”.
 
Well said mkuu
 
Kaka uko vizur sana mzalendo, yan mi inanishangaza sana unakuta mtu anadai kwamba watu wa dini flan wanaonewa na kuna mkakati wa kuwafelisha eti na yeye kafelishwa, hatak mfumo kristo lakini anaongea kiingereza, mi kwa maoni yangu watu tuache jazba zisizo na msingi na tusipende kujihalalisha kidini pale tunapokuwa tumefeli kwenye maisha,

mimi nimeshuhudia wakristo wakisema wamefekishwa mitihan wakatudia tena miaka kusoma ila hawajawah sema kuwa ilikuwa kwa sabau ys ukristo wao.

watu tujiamini na kamwe mimi naamini mawazo yoyote yenye hila mbaya tanzania hayata fanikiwa.....

Mungu pishilia mbali..
 
scan0026.jpg

Kutoka Kushoto: Sheikh Suleiman Takadir, Mbutta Milando, JohnRupia na Julius Nyerere Hao Waliowazunguka na Silaha za Jadi ni Bantu Group Kundi la Vijana wa TANU lililokuwa linatoa Ulinzi kwa Viongozi wa TANU. Picha Hii Ilipigwa Mwaka wa 1955.

Jina la Sheikh Suleiman Takadir halijapatwa kutajwa popote katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika wala katika historia ya TANU. Hatajwi na hakupata kutajwa baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 na sidhani hata kama atakuja kutajwa au kukumbukwa na hawa viongozi walio katika madaraka hivi sasa. Lakini naamini viongozi hawa walio madarakani hivi sasa ambao wakati wa kudai uhuru walikuwa watoto wadogo lazima watakuwa wamesikia jina hili likitajwa na wazee wao. Sheikh Suleiman Takadir hutajwa kila linapotokea jambo ambalo Waislam huonekana wanadhulumiwa na serikali kwani ilikuwa Sheikh Suleiman Takadir ndiye aliyeweka agenda ya hali ya baadae ya Waislam na Uislam katika Tanganyika huru mwaka 1958. Jambo hili alipolileta lilitishia kuigawa TANU katika misingi ya dini katika wakati amabo umoja wa Waafrika ulikuwa unahitajika sana. Mwaka wa 1958 TANU ilikuwa imeenea nchi nzima na tayari iko katika barabara ya kuelekea kuchukua madaraka ya ndani na kisha Tanganyika kupata uhuru wake kamili.

Sheikh Suleiman Takadir alikuwa nani na nini ulikuwa umaarufu wake? Sheikh Suleiman Takadir kwanza alikuwa ‘’alim,” mwanazuoni kisha alikuwa Mwenyekiti muasisi wa Baraza la Wazee wa TANU kuanzia TANU ilipoundwa mwaka 1954 hadi “alipotoswa” mwaka 1958 kwa kosa la “kuchanganya dini na siasa.’’ Sheikh Takadiri alishiriki vilivyo ndani ya Baraza la Wazee wa TANU katika kutayarisha safari ya Nyerere kwenda UNO mwaka 1955. Wapenzi wake katika harakati za kupigania uhuru walimpachika jina la utani wakimwita “Makarios,” wakimlinganisha na Askofu Makarios wa Cyprus na Ugiriki aliyekuwa anapambana na ukoloni wa Waingereza wakati yeye alipokuwa anapambana na Waingereza katika ardhi ya Tanganyika. Sasa kwa kuwa Suleiman Takadir alikuwa sheikh na mpambanaji ndipo walimpa jina hilo la “Makarios” na kwa hakika jina hili lilimkaa, likamwenea vyema na yeye akalipenda.

WAZEE%2BWA%2BTANU.jpg

Baraza la Wazee wa TANU
Sheikh Suleiman Takadir wa Pili Chini Kulia, Wa Pili Waliosimama Dossa Aziz,
Wa Sita Julius Nyerere, Wa Saba John Rupia, Wa Tisa Said Chamwenyewe,
Anaefuatia Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate

Mikutano ya mwanzo ya TANU ilikuwa ikifanyika Mnazi Mmoja mbele ya baadae ilipojengwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Wakati ule pale palikuwa hakuna jengo lolote, palikuwa na kiwanja kitupu na ardhi ile ilikuwa mali ya Mzee John Rupia Makamu wa Rais wa TANU. Kiwanja hiki baaadae Mzee Rupia aliwapa TANU na TANU wakaanzisha Chuo Kikuu pale mara baada ya uhuru. Mikutano ya kwanza ya TANU ikifanyika pale Mnazi Mmoja na kabla Nyerere hajapanda juu kwenye jukwaa kuzungumza na wananchi alikuwa kwanza anatangulia Sheikh Suleiman Takadir kusawazisha uwanja na kuwaweka wananchi tayari kumsikiliza kiongozi wao. Kama alivyokuwa Nyerere, Sheikh Suleiman Takadiri alikuwa na kipaji cha kuongea. Leo hii huenda baadhi ya wasomaji wangu wasiamini lakini ukweli ni kuwa Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kabla hajazungumza lolote alikuwa akipiga “fatha,” wananchi wakaitika na kwa umoja wao wakasoma, “Surat Fatha,” sura ya ufunguzi katika Qur’an Tukufu, kisha Sheikh Takadir akaomba dua na wananchi wakawa wanaitika kwa pamoja, “Amin,” Amin,” “Amin.” Baada ya hapo ndipo atapanda Nyerere na kuanza kuhutubia. (Picha za mwanzo za mikutano hii zipo na zilipigwa na Mzee Shebe ambae katika miaka ile ya 1950 alikuwa na studio yake Mtaa wa Livingstone na Kipata. Picha hizi baadhi nimepata kuziona. Mzee Shebe ndiye alinipiga picha yangu ya kwaza nikiwa na umri wa mwaka mmoja au miwili hivi na picha hii ninayo hadi hii leo. Inaaminika Mzee Shebe ndiye mpiga picha wa kwanza wa TANU na Nyerere).

002_2.JPG

Mwandishi Akiwa na Mwaka Mmoja Au Miwili Picha Aliyopigwa na Mzee Shebe
1952/53 Kwenye Studio Yake Mtaa wa Livingstone na Kipata

scan0027-1.jpg

Nyerere Akihutubia Mkutano wa TANU Siku za Mwanzo

Huyu ndiye Sheikh Suleiman Takadir na huyu ndiye Nyerere kama alivyokuja kutambulishwa kwa watu wa Dar es Salaam na Sheikh Suleiman Takadir kwa mara ya kwanza mwaka wa 1954.Kabla ya hapo Nyerere alikuwa akijulikana na watu wachache katika TAA. Sheikh Takadir alimpenda sana Nyerere kiasi kuwa mwaka 1957 katika hotuba aliyotoa katika tafrija moja ya taarab Mtaa wa Mvita, alimwita Nyerere, “Mtume wa Afrika,” aliyetumwa na Mungu kuwaokoa Waafrika. Maneno yale ya Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kama anamtabiria Nyerere makubwa katika mustabali wa Afrika, kwani miaka mingi baadae Nyerere alikuja kusimama mstari wa mbele katika kuikomboa Afrika kutoka makucha ya wakoloni. Nyerere akawa hapungui nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Swahili. Nyumba hii iko jirani na kilabu ya mpira ya Pan Africa. Kutembelewa na Nyerere pale nyumbani kwake ikapelekea baba mwenye nyumba, Jumbe bin Jumaa wa Digosi amuhamishe nyumba Sheikh Takadir asije kumponza kwa kwani Nyerere alijulikana kama adui mkubwa wa Waingereza. Hii kwa muhtasari ndiyo historia ya Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere. Lakini usuhuba huu ulikuja kuvunjika na watu wawili hawa wakawa mahasimu wakubwa, Sheikh Suleiman kafa hasemi na Nyerere na Nyerere kwa upande wake hakupata hata siku moja kumtaja Sheikh Takadir popote hadi anaingia kaburini. Inaaminika Sheikh Takadir alikufa kihoro baada ya kupigwa pande na TANU na wakazi wote wa Dar es Salaam na wanachama wa TANU kwa kosa la “kuchanganya dini na siasa.” (Ikiwa msomaji wangu ulisoma makala yangu ya juma lililopita utakuwa umeona kuwa TANU ikiongozwa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir ilipitisha azimio la kupiga vita hisia zozote na chembechembe za Uislam ndani ya TANU). Hakika Uislam ulikuwa na nguvu ndani ya TANU lakini haukuachiwa uvuke mipaka kuwabagua wengine waliokuwa si Waislam.

Kilitokea nini hadi kupelekea Sheikh Suleiman Takadir agombane na Nyerere? Chanzo cha mtafaruku huu ni Uchaguzi wa Kura Tatu wa mwaka 1958. Waingereza waliweka masharti ambayo kwa hakika yalikuwa ya kibaguzi na yalifanya wananchi wengi wasiweze kukidhi sifa zilizowekwa za kuweza mtu kupiga au kupigiwa kura. Kulikuwa na sifa ya elimu, kipato na kazi ya kukubalika na kupiga kura kwa tabaka za rangi. Mpiga kura Mwafrika alitakiwa ampigie kura Mzungu, Muasia na Mwafrika. Masharti haya yalikuwa kisiki kigumu kwa uongozi wa TANU na wanachama wake kutimiza. TANU na viongozi wake wengi hawakuwa na hiyo elimu iliyokuwa ikitakikana wala kipato cha maana. Ili mtu asimame kama mgombea kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria au awe angalau mpiga kura ilibidi azikusanye sifa zote hizo mahali pamoja. Wapiga Kura na wagombea walitakiwa wawe na kisomo cha darasa la 10 au kipato cha pauni 400 kwa mwaka na kuwa na kazi ya maana. Waafrika waliokuwa na sifa hizi hawakuwa wengi katika TANU. Wengi katika TANU kama walivyokuwa wakipenda kujiita wenyewe walikuwa, “Baba Kabwela.” Ikawa sasa ili TANU iweze kuweka wagombea ilibidi iwatafute watu nje ya uongozi wa TANU. Hapa ndipo lilipokuwa tatizo.

scan0023.jpg

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Nyerere Akitia Sahihi Azimio la Tabora[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ilibidi TANU sasa iwalete watu wenye sifa nje yake na wengi wa watu hawa walikuwa Wakristo waliosomeshwa na wamishionari. Jambo hili lilimkera sana Sheikh Takadir na wanachama wengi wa TANU kwa ujumla wao na kwa hakika TANU nzima hawakutaka kabisa kuingia uchaguzi ule kwa masharti yale waliyoyaona ya kibaguzi. Wanachama wa TANU walikuja na kauli mbiu isemayo, “Kuingia Kura Tatu ni sawa na kujipaka kinyesi.” Ilikuwapo minong’ono kuwa Wakristo wataichukua nchi lakini kwa muda mrefu hofu hii ilizuiwa kwenye vifua hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kulisema hilo waziwazi kwani jambo la dini lilikuwa mwiko mkubwa katika TANU. Ikawa tatizo lile la kushiriki kwa TANU katika Uchaguzi wa Kura Tatu lijadiliwe kwenye Mkutano Mkuu wa TANU wa mwaka 1958 uliopangwa kufanyika Tabora. Mpinzani mkubwa wa Kura Tatu alikuwa Zuberi Mtemvu, Katibu Mwenezi wa TANU kwa wakati ule. Ukweli ni kuwa Kura Tatu ilitishia uhai wa TANU na zilikuwapo dalili za chama kumeguka pande mbili. Kulikuwa na uwezekano mkubwa sana kuwa Zuberi Mtemvu na Sheikh Takadir wangelikuwa upande mmoja na wangeweza kuja na chama kingine ingawa agenda zao zilikuwa tofauti. Mtemvu yeye alisimama kwenye Afrika kwa Waafrika na Sheikh Takadir kwenye Uislam. Mkutano wa Tabora ni kisa kirefu In Sha Allah tutakitafutia wakati wake makhsusi tukizungumze. (Nimekiandikia kitabu kizima “Uamuzi wa Busara,” Abantu Publishers 2007, Dar es Salaam) Sheikh Suleiman Takadir na baadhi ya wazee katika Baraza la Wazee wa TANU walikuwa wajumbe katika mkutano wa Tabora. Kufupisha kisa TANU ilipiga kura kukubali kuingia kwenye Uchaguzi wa Kura Tatu na manusruna kura zifungane kati ya wale wanaounga mkono na wale waliokuwa wakipinga. TANU iliingia katika Uchaguzi wa Kura Tatu na ikapata ushindi mkubwa.

Hofu aliyokuwanayo Sheikh Takadir ilikuwa kuwa watu walioingia katika TANU kuchukua uongozi ni Wakristo. Sheikh Takadir alikuwa anajua nguvu ya madaraka waliyokuwa wanakabidhiwa akawa na hofu kama uongozi huu mpya utakuja kutoa haki kwa Waislam uhuru utakapopatikana. Sheikh Takadir alitaka uhakika wa hali ya baadae ya Waislam katika Tanganyika huru. Katika mkutano wa Halmashauri Kuu Makao Makuu ya TANU, New Street Sheikh Takadir alimkabili Nyerere akamshutumu kuwa hakuwa na nia nzuri na Waislam, atakuja wapendelea ndugu zake Wakristo katika Tanganyika huru. Sheikh Takadir akawageukia wenzake katika Baraza la Wazee wa TANU akasema, “Tuzibe ufa tusije tukajenga ukuta.” Jambo lile lilikuwa zito. Nyerere alijiinamia na aliponyanyua uso wake machozi yalikua yanambubujika. Mkutano haukuweza kujadili jambo lile na kikako kile kikavunjika pale pale na wajumbe wakawatawanyika.

Sheikh Takadir ‘’akatoswa,’’ kwani alikuwa amevunja mwiko mkubwa katika TANU. Mzee Iddi Tulio akachaguliwa kushika nafasi yake. Huku ‘’kutoswa’’ na kutengwa na jamii ndiko kulikosababisha kifo cha Sheikh Takadir. Alikuwa hata akitoa salamu hakuna aliyeitika. Akienda sokoni Kariakoo kununua chochote kile hakuna aliyekuwa tayari kupokea hela yake. Haikuchukua muda mrefu Sheikh Takadir akaaga dunia. Kabla Sheikh Takadir hajafa TANU ilifanya mkutano mkubwa sana na Nyerere akamshambulia Sheikh Takadir kwa kutaka kuwagawa Watanganyika katika misingi ya dini. Baada ya mkutano kundi kubwa lilikwenda nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Msimbazi kuzomea huku wakiimba, “Takadir Mtaka Dini.” Sheikh Takadir alitoka nje akasimama kizingitini akasema maneno haya, “Ndugu zangu In Sha Allah iko siku mtakuja kunikumbuka.” Haukupita muda mrefu Sheikh Takadir akatangulia mbele ya haki na kwa kipindi kirefu katika historia ya uhuru wa Tanganyika hakuna aliyemkumbuka Sheikh Suleiman Takadir, Askofu Makarios wa Tanganyika. Hivi sasa Sheikh Suleiman Takadir anatajwa sana na kizazi cha leo. Utabiri wake kuwa ndugu zake watakuja kumkumbuka umetimia. Swali la kujiuliza ni iweje hii leo baada ya miaka 57 kupita Sheikh Suleiman Takadir anarejeshwa upya katika historia ya kupigani uhuru wa Tanganyika? Hiki ni kitendawili kinachongoja kuteguliwa.

3ngq7mfoNBkDsGoTihZVXo4ZzngGhTG3i5TneJ6bQLk=w409-h207-p-no

Mi naomba kuuliza hivi katika hili suala la kupendelea wakristo waliosoma shule za mishen za kikristo je ni wangapi waliokuwa wamesoma shule zq mission zq kiislam walioachwa?,

Na kabla ya uhuru we unadhan watu gani waliokuwa wanafungua na kueneza elim kama siyo makanisa, tatizo hapa siyo waislam ambao hawakuwa wamesoma wengi na ama wakristo waliokuwa wamesoma wengi

tatizo hapa ni wale walioleta dini ndiyo wenye tatizo, huwa najiulizq hivi ni kwa niji hasa mahala ambapo kukikuwa na uislam sana, yan hukuti shule, hospitali na mambo mengine ya huduma za kijamii?....

anyway naweza elewa pia kuhusu gharama za usambazaji ni kubwa lakin pia hata uislam ulikuja anzishwa miaka 600 baada ya ukristo mi nadhan kulikuwa na mengi ya kujifunza kwani sitaki kuamini kuwa sisi ndiyo waanzilishi wa hiz dini, yan kila mtu kwa muda wake ama babuzake ama yeye mwenyewe alijikuta anatembelewa na wageni asiofaham, na wao wakampa ama uislam ama ukristo sasa kosa hapo ni la nani?,

yan kifupi sisi hapa tulipo sawa tunashukur tumepata mwanga toka kwenye upafani ila ki ukweli haya si mawazo ama akili zetu, yan tumetengenezwa na watu wa kuja toka ama mashariki ama kaskazini hivyo hatuna sababu ya kuchukiana kiasi hicho....

Mi naamin hata waislam wa zaman hawakuwa wanyonge kias hicho kama baadhi ya waislam wa sasa wanavyoonyesha, yan wao wanajiona ndiyo wanaijua sana thaman ya dini kuliko wale wa zaman hili si la kweli, hata wale wa zaman naamin dini pia waliijua na hao ndiyo walio warithisha hawa wa sasa

ila wale walijari zaidi amani juliko machafuko na fujo na hiyo ndiyo dini inavyotaka...

siamini kama kuna Mungu anayependa watu wauane ama wachukiane basi asinhereta dini za kukataza maovu, dini zote lengo lake ni kukataza wizi, zinaa, magomvi na mengineyo kwani hayo hupelekea kuuana na macjafuko katika jamii na Mungu aliyajua hayo..

Sasa sisi tunatakiwa kutokubali uchonganishi wa namna yeyote ile na hizi story za kutunga zisizo na mashiko kisa mtu alikosa madaraka ama alishindwa kwa point sasa anajificha nyuma ya dini hilo hatulikubali hata kidogo..

kwa nini sasa baada ya miaka 57 ni kwa sababu nchi kwa sasa haina voongozi madhubuti ambao watakemea uchochezi kama huu, viongozu wetu ni hawa wanaopenda kujipendekeza hata kama ni kwa kudanganya ili tu kuwafurahisha watu flan....

tanzania itabaki kuwa tanzania na kamwe haitavurugwa kirahisi kama baadhi ya watu wanavyotamani, yan kuna baadhi ya watu kwa sababu za kukosa madaraka kipindi cha kupigania uhuru yan wanataman hata hii amani iliyojengwa waiondoe kwa ajiri ya kuwakomoa akina nyerere, mi naomba tusikubali kwan akina nyerere wenyewe washakufa tayari yan vita yao itasababisha mauti kwetu tuliohai halaf historia ni historia tuu hata ukiizika leo ipo siku hata ipite miaka mia saba kuna mtu atakuja kufukua na kusema mwk nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa tanzania na tanyika na alisaidia kutengeneza nchi yenye aman......sina haja ya kumtukuza mtu bali najaribu kuongea ukweli.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Hivi waislamu ni wao ndio vichaa au huyo jamaa Allah wanaemuabudu ndio fyatu? Maana wao ni shida, kulalamika, vurugu, ugaidi, kukandamiza wanawake, ubaguzi wa watu, majini, mauaji, puuu! Mbaya zaidi hata waislamu walioenda shule elimu imekataa kuwaingia kabisa
 
George Jinasa,
Penye dhulma hapawezi kuwa na amani.

Kilichotufikisha hapa ni pale baada ya uhuru tu ukawekwa mkakati
wa kuukandamiza Uislam.

Ni katika kutekeleza mkakati huu ndipo hata historia ya kudai uhuru
ambao mchango wa Waislam ulikuwa mkubwa ukafutwa.

Ikiwa kwa hakika una nia ya kuujua ukweli jiulize ni ujasiri gani
uliowapelekea Waislam kutembea nchi nzima na kufanya mikutano
ya wazi kuitahadharisha serikali kuwa nchi yetu inaendeshwa na
Mfumokristo?

Unaweza ukapata habari zaidi kwa kusoma kitabu changu:
"Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes..."
 
Jembepori,
Ulikuwa ukiijua historia hii kabla sijaiandika?
Historia hii ilifichwa.

Sasa jiulize kwa nini ilifichwa?
Nini kilikuwa kinaogopwa?
 
Mpinga Shetani,
Unaandika ukiwa huchukui tahadhari ya lugha yako.
Unaandika ukiwa tayari ushajizonga na propaganda dhidi ya Uislam.

Kabla hujaandika tena waulize wenye kujua wakufahamishe nini Uislam.
Leo Kanisa linanasibishwa na kila uchafu kuanzia ushoga hadi mengine nk.

Sasa jiulize haya ndiyo mafunzo ya Yesu? Jibu ni hapana.

Hii ndiyo hali inayokabili Uislam kunasibishwa na yale ambayo hayamo katika
mafunzo yake kama ugaidi nk.
 
Jembepori,
Ulikuwa ukiijua historia hii kabla sijaiandika? Historia hii ilifichwa. Sasa jiulize kwa nini ilifichwa? Nini kilikuwa kinaogopwa?

Mkuu hii historia nilikuwa naijua maana haya malalamiko si ya leo, yapo na kuna waliotangulia kulalamika hata enzi za utawala wa mwl..nilipara kusoma kitabu cha "uhuru na maendeleo" by Julius K Nyerere...

kunamahala alitahadharisha akasema nchi hii kunawatu wanaeneza chuki, akasema na wanasemasema kana kwamba si mawazo yoa tu ila hatari iliyopo ni kuwa watu wataamin kama serikali ikikaa kimya, akasema kama kunamtu ajamfaham mtu aliyenyimwa kazi kwa sababu ya dini yake ama sababu nyingine aliwapa wstu ruhusa kwenda ikulu na kuripoti....

na kama hamna basi asije akasikia mtu anasema mambo ambayo hayana ukweli....ukweli ni kwamba hakuna hata mtu mmoja kwa mujibu wa kitabu kile aliyejitokeza kwa kukosa kazi za kitaalam kwa sababu ya dini....

naamini kwa kulionahilo la tofauti ya wasomi na kujua kuwa litakuja kutupa shida baadae mwl nyerere aliamua kufanya maamuzi magum ambayo si ya kawaida kwa kuchukua shule zote za wakristo na kuzifanya shule za serikali ili hata kama waislam watu wazima kipindi kile kuwa walikuwa hawajasoma kwenye mission bas sasa watoto na wajukuu zao waende shule ili kuweza kushindana kisawa kwebye ajira za tanzania...

jambo ambalo siamini kama mapadre na wachungaji kama walilifurahia, kwa hiyo jitihada ya ku balance mambo mi naamini ilikuwepo tanguwanzo wa tanzania kuwepo, ukiachilia mbali kipindihiki cha rushwa, ila hata sasa ajira majeshini na polisi zinatolewa sawa kwa wilaya na mikoa yote ya kitaifa....bila kujali mkoa gani unawasomi wala upi usio na wasomi,

ukija kwenye shule kunamikoa ilikuwa inapendelewa ki viwango vya ufaulu, nakumbuka nikiwa shule ya msingi nilikuwa wilaya ya kinondoni maana nilisoma pale ubungo nh primary, ila ufauru kwa wilaya hii ulikuwa mgumu sana kwani maksi zetu kwa mtu kwenda azania kulinganisha na mtu anayesoma akitokea ilala ama temeke zetu zilikuwa juu sana yaani kwa masomo yote matatu ilikuwa uwe na maksi angalau 121 wakati wale wenzetu wa temeke na ilala ni maksi 90 tu unaingia aza boy,

ukiuliza unaambiwa watu wa kule wengi hawapendishule na ni wachache wanaosoma, yan ukiangalia saaaana unaona ni nia ileile ya serikali kutaka kutoweka matabaka bali kuchukua watu wote kwenye kila jambo jema...

jaman mi ninachotakw kusema hapa ni kwamba ni hatari sana kwa mtu kutumia madhaifu machache yakiutendaji yaliyofanywa bila dhamira ama mkakati na kuyageuza kuwa ya kimkakati, sidhani kama nyerere alipomteua rais mwinyi ilikuwa ni mkakati flan, hili hatulisemi sana ila naamin kama mtu mzima alijua hiz changamoto za ukristo na uislam kwa utashi tuu akaamua pia muislam atawale na kama angeamua kuwauliza wakristo sidhan kama wangemruhusu amuachie nchi mwislam

nataka kujenga hojakuwa tusieneze chuki zisizo na sababu ndugu zangu, mi nafurahi sana ninapoona mtu anapinga mfumo kristo huku anazungumza kiingereza kwani ni dalili njema kuwa sasa uwanja wa mapambano kwa maana ya kazi, nafasi za uongozi na nyinginezo ambazo huwa ni njoz kwa binadam yeyote yule hata kama hana dini kutakuwa na uwanja sawa kuliko watu wanapokataa kusoma shuke linakuwa ni tatizo jingine...

hii elimu dunia ikiyoenezwa na warumi baadae na makanisa yao hapo awali ilibuniwa na wagikiki, wengi wa wanafalsafa za elimu za kila sampuli kama ni sayansi, uchumi na nyingineza hawakuwa na dini, wao walikuwa wanafalsafa tuuu, siamini kama plato alikuwa mkristo ama aristotle, tena waroma walimuua galileo kwa kusema kuwa dinia ni duara ila baada ya miaka mia moja mbele dunia ilimkubali

yan hii elimu ni yetu sote wala si ya dini flan, ni maarifa tu ya kuujua ulimwengu na viumbe vyake na mwenye nayo atakuzidi tuu hata kama hana dini.....

hebu tupendane watanzania na tumuombe mwenyezi Mungu atupe moyo wa kulazimisha kumpenda mtu asiye wa dini moja na wewe, haya mambo ni ya kulazimisha kwani hata wanademokraria tunao wajua waliamua kuwa na demokrasia hiyo ingawa nafsi zao bado huwa zina ubinafsi.....

na ndiyo maana hawakuacha ibada ili mwenyezi Munhu awasaidie wasije wakajisahau na kuzifuata nafsi zao, na ndiyo maana inatupasa tusali sana tusijejikuta tunafuata nafsi zetu ambazo kiasili zinaubinafsi sana....

jiulize ukiwa kituoni unasubiri usafiri na daladala ikaja watu huwa wanagombania kwa nini?, ni kuwahi siti ya kukaa, na pale hakuna mzee mtu wa makamo wala kijana, yan kila mtu anawaza siti, yeye kwanza na akishakaa ndiyo anamkumbuka kama anajamaa ama rafiki , yan unaweza msahau hata mwenza wako usipokuwa makini na hiyo ndiyo nafsi ilivyo....

Mungu pishilia mbali...

wasalaam!
 
Jembe Pori,
Hujaujua ukweli wenyewe.
Wa kutujibu Waislam wako kimya.
 
Hivi waislamu ni wao ndio vichaa au huyo jamaa Allah wanaemuabudu ndio fyatu? Maana wao ni shida, kulalamika, vurugu, ugaidi, kukandamiza wanawake, ubaguzi wa watu, majini, mauaji, puuu! Mbaya zaidi hata waislamu walioenda shule elimu imekataa kuwaingia kabisa

Tatizo huanzia mbali sana Mkuu.

MAFUNDISHO YA MADRASA UTOTONI.

Niwalimu wachache hufundisha upendo, kweli na amani.

Wengi wao hupotosha watoto kabisa nakuwajengea chuki na visasi, na mafundisho ya utotoni hukaa kichwani daima ndiyo maana wapo waliosoma lakin ukimfikisha kwenye ufia din - JIHAD hajielewi.

Mfano mzuri wa waalimu wapotoshaji na wachochezi ni huyu msomi fake 'MOHAMED SAID'

Elimu yake hainamsaada kwa watanzania, yeye kwake umoja, upendo, amani na mshikamano si lolote si chochote, kutwa-kucha niuchochezi na kushawishi vijana kuvuruga amani ni udin, udin mada zake zote, popote na maisha yake yote.

Huyu ni muathilika wa elimu ya utotoni alopewa madrasa na hatabadilika mpaka kaburini.
 
Jembe Pori,
Hujaujua ukweli wenyewe.
Wa kutujibu Waislam wako kimya.

Mkuu mimi nimejaribu kujenga hoja na kwa kutumia midano dhahili, unadhan kwa nini uislam unaungwa mkono sana maeneo ya Borno Nigeria ama kule Garissa kenya ama maeneo eneo katika nchi za secural kama tanzania?.

Ni sababu zile nchi hazikulitibu hili suala tangu mwanzo, na ndiyo maana majimbo yaliyoendelea tanguukoloni yameendelea mpaka leo, mikoa yenye shule tangu mwanzo na ndiyo inazidi kutoa wasimi kila kukicha..

tanzania hapa sivyo, hapa hakuna mkoa kipaumbele wala kabiala bora, hapa shule zote serikali ilichukua na kila mwenye uwezo wa kusoma amesoma....

yan ndiyo maana mawazo ya kijihad kwa waislam wa tanzania ni ndoto sababu hawaoni logic hata kwa hapa waseme nini sababu wanafaham jinsi walivyotumia uwezo wao navkufika walipofika........

Hiv utamwambua Saad na Sabri Sadiq marafiki zangu wale niliosoma nao pale makongo na wao kupata divisssion one na kuwapita hata wakristo kuwa leo eti watakwambia mwislam huwa anafelushwa?...

hawa ni mfani tu nawajua akina issa jassim ba wengineo wengi ambao mnapiga nao buku na anakutoa "knok out" mpaka unamkubal RIP sir....

yan ninachojitahid kueleza hapa kaka ni ubadili mfumo wa mawazo, tynajua kuna ndugu na jamaa za watu kama akina Takadir na usikute na wewe ni mmoja wao na unataka kyfanya revange sasa uusitake kuchafua hali ya nchi kwa kupandikizabchuki baina ya watu walio oleana tayari

Unapoongea hapa kuhusu waislam yan watu wanawaza mengi, hiv leo mimi naanzaje kumkata panga rajabu mtoto wa mama yangu mdogo ama aisha, qma zubeda? yan kuna kazi sana lakuni huzi chuki zikiendelezwa utashangaa kuona sikumoja ndugu zangu hawa hawaji tena kututembelea hapa dar, ama tukafika mahala pa kuuana kabisa kitu ambacho mi siombei....

tafadhal naomba kama mtu ana chuki na mtu usitumue mlango wa dini kwani hii nu hatari sana tunaomba kaka mohamed tusaidiane, huyu nyerere huyu alikuwa mtu tuu, tena mlugaluga hiv wa kuja so alikuwa na mapungufu yake, tutajadili mapungufu yake kama yeye na wala si mfumo wa kidini na mema yake tunayakubali pia mfano tunajua kuna tetesi kuwa nyerere alikuwa tajiri kweli lakini wqnaosema sema hivyo hawatoi ushahid zaidi ya kusema kwa malikia kuna ardhi yake, sawa pia ni mawazo lakini ukweli utabaki palepale ksti ya viongozi wotr mpaka sasa tanzania hapa hakuna wavkumlinganisha ki uadilifu hasa ule wa kutumia madaraka ya nchi kiuadikifu ama bila kuingiliwa na ndugu na jamaa na marafiki ama kutolewa madaraka na kuumiza wananchi na sera uchwara........

kunamifumo aliyoikuta tangu ukoloni kama hili la kusali jumapili na jumamosi kupumzika..Pia kuna suala la chama....hili la TANU nalo lina mbwembwezake maana kunawatu wanauchukia ukristo kwa sababu ya nyerere na TANU kuwa aliwanyang'anya waislam chama chao, mi sidhan kama ni kweli na hays yanasemwa yeye akiwa hayupo na ndiyo mbaya zaidi ila ninachokijua kutoka kwenye vitabu hasa cha Nyerere of tanzania na Willium Edget Smith kinaeleza jinsi alivyo acha kazi ya ualimu nabkuingia kwenye siasa rasmi, kakin ukisoma kwa makini utaona nyerere hakuwa kimkakati kwamba afanye harakaharaka kuchukua nafadi ya uongozi na kuburuza wenzake ........

alitoka kwenye ualimu akaenda kwao butiama, akakiaacha chama na watu wooote wa chama walikuwa hapa dar es salaam mwaka ule wa 1954 woote npaka chama kikawa kama kinataka kufa ndipo walipomtuma Kambona kwenda butiama na ndipo nyerere akarudi mwaks unaofuata......

haikuwah ki mkakati kiiiivyo kama watu wengi wanavyosema na waidlam waliokuwa wakimpenda na kumpa uongozi waliangalia uwezo wake tu wabkiuongozi na si ukristo wake.....

yan watu walidhachoka na utawala wa kikoloni na mtu angalau aliyeonekana kuwrza kuwakabiri waingereza alikuwa Julius...
Sipo kumtetea mtu ila nachosema ni bora kuwa wakweli wa nafsi zetu kuliko kupotosha ukweli ilihali tunajua tunachofanya..

ukieneza chuki sikuzote chuki itakufuata wanasema "something goes around is something comes around"

Salaaam!
 
Ha ha ha ha Ustadh Mohamed Said kwanza nimefurahi sana umejitahidi kujibaraguza na hoja dhaifu eti mimi niko DAB lakini mwisho wa siku unajionyesha ulivyomjinga.Kwa taarifa yako Wakoloni hawakupenda kuondoaka Afrika wanajitahidi kutumia mbinu mbali mbali kurudi Afrika moja wapo ni kuangalia sababu zipi zinazoweza kutugawa kubwa ni ukabila na udini.Bahati mbaya wakitaka kutugawa kupitia udini tayari wana mtu anaitwa Ustadhi Mohamed Said.

Ngongo,
Hiyo si hoja.

Labda nami nikuulize.

Kwa nini kitabu changu hakisomeshwi Chuo Kikuu cha St. Augustine lakini
kinasomeshwa vyuo vyote Marekani na Ulaya?

Sasa wewe si wa kutoa jibu.

Jibu wacha litolewe na Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mbona hujagusa matawi ninayokalia?

Yanakutisha?

Hivi unajua kama mimi nimo kwenye list ya Dictionary of African Biography?

Hivi unajua huu maradi ulikuwa wa Harvard na Oxford Univeristy Press,
New York?

Ikiwa hawa huwajui uliza utaambiwa hawa ni nani katika duru za kisomi na
uchapaji.

Wewe uko kwenye s...list.

Hahahahahahahahahahahah!
Jamani mbavu zangu.

Ngongo,
Niangalia hapa chini:

CIMG0424.JPG

Unapajua hapo?
Hapo ni BBC.

Siyo BBC London, Bush House.
Hapana.

Hapo ni BBC Glasgow.
Unajua nafanya nini?

Nafanya kipindi cha historia ya Afrika.
Unajua ni lini?

1991.
Si unaona nilikuwa mdogo.

Kufa kwa roho yako mbaya ya choyo na wivu.
Ati mbona kitabu changu hakisomeshwi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

My foot!

Usithubutu kurudi na utumbo wako hapa jamvini.
Ndiyo nitakumaliza kabisa.

Ngongo,
Hunijui.

Nataka leo unijue.

Si tu "The Life and Times of Abdulwaid Sykes..." kimepigwa pande
hakisomwshwi hapa nchini.

Nina kitabu kingine kilichochapwa na mabingwa wa uchapaji nacho
vilevile kimekataliwa hakisomeshwi.

Kitabu hiki kinaitwa, "Torch on Kilimanjaro," Oxford University Press,
Nairobi, 2006.

Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe, kuwa sisi kama wana jf, tuko sawa, hakuna mwenye washabiki wala wafuasi, laki pia najua unajijua nguvu uliyonayo humu jf, kuhusiana na hoja unazozipigia nia na unajua fika kuwa sio tuu una washabiki humu, bali hadi wafuasi na unawajua!.

Siku zote kwenye mnakasha, wewe ni mwalimu wa lugha za staha, na sio mara moja wala mbili, umeendesha darsa la mnakasha, ila nimenote wakileta ujinga wajinga wajinga wengine, unakemea, ila wakileta ujinga ujinga wafuasi, wewe kimya!.

Wewe kama mwanazuoni, unapaswa kuwa totally impartial, ila kwa sababu niliwahi kusema humu kuwa 'you are a man with a mission', na 'the motive behind ni some ill motives', tuendelee tuu kuzipanda, tuzimwagilie zitamea, tusiwekee mbolea zimee vizuri, hadi zikomae tupate mavuno mengi!, nazungumzia zile 'mbegu' unazotupandia humu!.

Huyu mzee mi nasoma sana maandiko yake najaribu kumuelewa na sijawahi kukocoment hata siku moja nilikuwa najua labda simuelewi lakini kila akiandika anaandika vitu vilevile style ile ile anabadilisha tu jina la mada then mwenyewe anajisifia utasikia maandiko yangu yako pale yako huku kutafuta legitimacy ile ile na huyu ni mtu mwenye mission na kuna watu anaowalenga wasome, na huwa hatoi solution yeye kazi yake ni kuwafeed watu with his violence doctrine na huyu ni mtu mbaya sana bora hata wale wanaovamia vituo vya Polisi, angekuwa mtu wa kutafuta maridhiano angekuwa amefika hata 2% yake kwa muda wote huo ambao amekuwa akifeed wafuasi wake, nimeona watu wengi wakimsihi aje na proposed solution lakini anawafeed tu wafuasi kama kuku wa kisasa mwisho wake sijui ni nini?
 
Katika historia kuna mengi yaliyotokea na mimi nisingependa kujielekeza zaidi katika hayo. Historia itakuwa na maana kama itatujulisha wapi tulipo na wapi tunakwenda. Itakuwa haina maana zaidi kama itakuwa inaturudisha tulikotoka au kutupeleka kusiko na manufaa. Tatizo langu sio katika uchambuzi wa historia katika mtizamo wa kawaida wa kifalsafa hata kama kutakuwa na tofauti katika kuhitimisha. Tatizo langu kubwa ni hizi hisia kali na chuki za kidini zinazojitokeza kwa wachangiaji wengi bila kujali kama ni wakristu au waislamu. Na sio tu chuki zinazojionesha katika mada tunayojadili hapa bali katika mada zingine katika majukwaa mbalimbali. Naharia ya chuki za kidini inaota mzizi. Hoja yangu ni kwamba licha ya yote, hamna namna tunavyoweza kuepuka mazungumzo yoyote yanayochochea chuki za kidini kati yetu?
 
Mpinga Shetani, haya mafundisho ya watoto katika madrasa yamekuwepo toka toka hata kabla ya ukoloni na bado vijana na wazee waliyosoma katika madrasa hizo wameishi kwa amani na upendo na ndugu zao wa dini zingine. Hapakuwepo na majibizano ya chuki na hisia kali za kidini kama tunavyoziona leo katika mitandao. Suala la kujiuliza ni je waislamu na wakristu wa leo walikuwa ni waumini safi kuliko wa miaka ya zamani? Matukio mengi ya uhalifu, ufisadi na dhuluma katika muda huu tunaoishi yanaweza kutupa jibu la hapana. Sasa ni nini kilichotubadilisha? Sikubaliani na wewe kwamba ni mafundisho ya dini kwa watoto. Kama ingekuwa ndivyo chuki zingeanza toka zamani ambako mafundisho ya dini yalikuwa yanazingatiwa hata kuliko sasa

MAFUNDISHO YA MADRASA UTOTONI.

Niwalimu wachache hufundisha upendo, kweli na amani.

Wengi wao hupotosha watoto kabisa nakuwajengea chuki na visasi, na mafundisho ya utotoni hukaa kichwani daima ndiyo maana wapo waliosoma lakin ukimfikisha kwenye ufia din - JIHAD hajielewi.

Mfano mzuri wa waalimu wapotoshaji na wachochezi ni huyu msomi fake 'MOHAMED SAID'

Elimu yake hainamsaada kwa watanzania, yeye kwake umoja, upendo, amani na mshikamano si lolote si chochote, kutwa-kucha niuchochezi na kushawishi vijana kuvuruga amani ni udin, udin mada zake zote, popote na maisha yake yote.

Huyu ni muathilika wa elimu ya utotoni alopewa madrasa na hatabadilika mpaka kaburini.[/QUOTE]
 
Kaka siamini kwamba unawatendea haki waislamu katika maneno yako haya makali. Maneno na majibizano ya namna hii yanachochea na kutia mafuta katika chuki miongoni mwetu jambo ambalo sote na kwa faida yetu tunapaswa kujiepusha. Ni vizuri kila mtu akaheshimu imani ya mwenzie. "Allah" nijuavyo mimi ni jina la Mwenyezi Mungu kwa lugha ya kiarabu. Mungu wanayomuabdu waislamu ni huyo huyo wanaemuabdu wakristo japo kutakuwa na tofauti katika kuelezea sifa zake. Nashangaa muislamu na mkristu ambao wote wanaamini uwepo wa Mwenye Mungu na siku ya mwisho wanakuwa na chuki kali na wakati huo huo hawanachuki na wale wanaoabdu mizimu. Hapa ndipo suala linapokuja kama chuki hizi ni chuki halisi za kidini au zinachochewa na vitu vingine. Ushauri wangu kwa wote, kwa kadiri tutakavyojadili tujiepushe na maneno ya chuki na dharau kwa misingi ya dini zetu.
 
Mashara yao kifo chetu....waambie kabisa
 
Back
Top Bottom