Nakubaliana na wewe, kuwa sisi kama wana jf, tuko sawa, hakuna mwenye washabiki wala wafuasi, laki pia najua unajijua nguvu uliyonayo humu jf, kuhusiana na hoja unazozipigia nia na unajua fika kuwa sio tuu una washabiki humu, bali hadi wafuasi na unawajua!.
Siku zote kwenye mnakasha, wewe ni mwalimu wa lugha za staha, na sio mara moja wala mbili, umeendesha darsa la mnakasha, ila nimenote wakileta ujinga wajinga wajinga wengine, unakemea, ila wakileta ujinga ujinga wafuasi, wewe kimya!.
Wewe kama mwanazuoni, unapaswa kuwa totally impartial, ila kwa sababu niliwahi kusema humu kuwa 'you are a man with a mission', na 'the motive behind ni some ill motives', tuendelee tuu kuzipanda, tuzimwagilie zitamea, tusiwekee mbolea zimee vizuri, hadi zikomae tupate mavuno mengi!, nazungumzia zile 'mbegu' unazotupandia humu!.
Huyu mzee mi nasoma sana maandiko yake najaribu kumuelewa na sijawahi kukocoment hata siku moja nilikuwa najua labda simuelewi lakini kila akiandika anaandika vitu vilevile style ile ile anabadilisha tu jina la mada then mwenyewe anajisifia utasikia maandiko yangu yako pale yako huku kutafuta legitimacy ile ile na huyu ni mtu mwenye mission na kuna watu anaowalenga wasome, na huwa hatoi solution yeye kazi yake ni kuwafeed watu with his violence doctrine na huyu ni mtu mbaya sana bora hata wale wanaovamia vituo vya Polisi, angekuwa mtu wa kutafuta maridhiano angekuwa amefika hata 2% yake kwa muda wote huo ambao amekuwa akifeed wafuasi wake, nimeona watu wengi wakimsihi aje na proposed solution lakini anawafeed tu wafuasi kama kuku wa kisasa mwisho wake sijui ni nini?
Maturanya,
Ukishaanza na "huyu mzee," basi tayari pana tatizo.
Umehamaki.
Tatizo si kuniita mzee tatizo ni hizo ghadhabu zako.
Hakika mimi ni mtu mzima sana wala hilo si kitu cha kunikera bali cha
kushukuru.
Sijisifu ila inabidi wakati mwingine nikufahamisheni ukweli kuwa msidanganyike
na hilo jina.
Hii nasema kwa uzoefu.
Wengi wamejikwaa kwa jina langu sasa singependa na wewe ukajikwaa.
Mimi sina "hisia kali."
Nilipogundua kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika imepotoshwa niliamua
kuiandika.
Tatizo lipo hapo.
Mimi sina watu wala sina "mission" yoyote.
Usijitishe wala huna haja ya kuwatisha watu.
Akiingia mtu hapa
Majlis akataka kuikebehi historia hii hapo mie huja na kueleza
lile ninalolifahamu.
Mathalan kulikuwa na mjadala hapa
Majlis wa safari ya
Mwl. Nyerere UNO 1955.
Nimeingia na nimeieleza ile safari kama nilivyohadithiwa na wenyewe walioifunga
safari hiyo.
Bahati mbaya wapo ambao hawapendi kusikia kuwa aliyekuwa akikusanya fedha za
safari ile alikuwa
Idd Faiz Mafongo.
Ukweli ni kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwekahazina wa TANU 1955 na ukiangalia ile
picha ya kumuaga
Mwl. Nyerere uwanja wa ndege
Idd Faiz Mafongo amesimama
pembeni ya
Nyerere.
Hiyo "violance doctrine," iko wapi hapo?
Nimeweka "paper" na vitabu vyangu vyote hapa na kuomba kama kuna uchochezi basi
uonyeshwe.
Sasa takriban mwaka wa tatu hakuna aliyekuja na ushahidi.
Badala yake ni kejeli za "huyu mzee."
Huyo aliyesimama katika ya
Zuberi Mtemvu na
Julius Nyerere ndiye
Idd Faiz Mafongo kadi yake ya TANU ni na. 25.
Maturanya,
Nini kimekughadhibisha?
Kule kumrejesha
Idd Faiz katika historia baada ya yeye kufutwa?
Kwako wewe huu ndiyo uchochezi?