njiwa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 13,144
- 6,942
Heshima kwako mwandishi wa makala hii, hakika nilikuelewa hapo awali kwa makala hii japo siyo siri kwa makala kama hii itasababisha mgawanyiko na chuki za kidini hasa ukizingatia kuwa mwisilam kwa asili hampendi mkristo na ndiyo maana humwita kafiri wakati mkristo humpenda mwislam kwakua ukristo huhubiri juu ya upendo na amani kwa watu wote.
Bila shaka nimekuelewa sababu zilizosababisha waislam wasiwe wengi kwenye uongozi wa wakati ule ni kukosa sifa na si kwamba walibaguliwa kama Takadir alivyodhani, nilitegemea wewe ungetoa mtazamo wako juu ya kile kilichofanyika je ilibidi wakate kugira au kupigiwa kura wote kwa ujumla wao? Je nikweli walibaguliwa kwa sababu ya dini zao? Japo kwa upande wa waingereza sina shaka kuwa walikuwa na ubaguzi wa kidini lakini je nyerere alitumia vigezo vya kidini katika kumbagua Takadir? Huhisi nyerere alikuwa sahihi kukemea udini na huwenda angeruhusu agenda ya udini itawale huwenda uhuru ungechelewa? Na pengine wakristo wangenufaika kwa udini kwakua waingereza ni wakristo?
Sina shaka kuwa wapigania uhuru wengi ni waislam na hii nikutokana na mahali walipokuwa yaani DSM.
Nahisi kwa makala za namna hii huweza chochea chuki ya udini hasa kwa watu wenye hisia za udini mioyoni mwao hivyo ningekushauri uwe unatoa historia lakini ukihitimisha kwa kupinga udini maana utalipeleka taifa hili mahala pabaya.
Sidhani kafiri ni chuki au tusi. .. ni jina tu tunalo muita yeyote asiye muislam. ..
Mara nyingi ukweli huwa ni mchungu. ..
