Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

.....................

Ulijibiwa hivi:

Pasco,
Ndugu yangu.

Hivi vitisho vya nini?
Wewe si wa kutishika na kalamu yaMohamed Said.

Mtu mmoja mkubwa katika CCM alipata kuniita mimi, "Mbilikimo."

Kisa chake kakasirika kuandika kuwa babu zangu baada ya kuunda African
Association wakaunda Al Jamiatul Islamiyya kisha TANU.

Jamaa zangu wakanambia huyu kakutukana kwa kuwa umemtisha.
Mimi nikauliza nimemtisha kitu gani?

Wakasema unaezua kipaa cha nyumba yake.
Kikiondoka kipaa hicho yeye hana stara tena.
 

Mohamed Said : My brother, you are just rising a FALSE ALARM! Trying to fight against something that does not exist, is to create it. Hakuna udini Tanzania! Tanzania kuna ongezeko la bei za bidhaa na maisha magumu kwa wananchi... Lets concentrate on the concentration!!!
 
LUKUD,
Hakuna tatizo.
 
LUKUD,
Hakuna tatizo.

Hii kitu huwa inanishangaza sana, kwa umri ulionao na elimu inasikitisha kuona mambo unayoyashadadia.

Kwa umri ulionao ni jambo la kheri na busara kutufundisha upendo na mshikamano kwa ujenzi wa taifa hili na si hili jambo uliloshikilia la kutaka kugawa watu kwa itikadi za kidini.

imetosha sasa.
 
Uhuru na Umoja,
Huenda unasema hayo kwa kuwa hujui.

Je ungependa mimi na wewe tujadili mada hii hadharani na mimi
nikupe ushahidi wa tatizo hili nchini petu?

Nimemkwepa LUKUD lakini naona kuna watu wanaipenda mada hii
ijadiliwe.
 
Uhuru na Umoja,
Huenda unasema hayo kwa kuwa hujui.

Je ungependa mimi na wewe tujadili mada hii hadharani na mimi
nikupe ushahidi wa tatizo hili nchini petu?

Nimemkwepa LUKUD lakini naona kuna watu wanaipenda mada hii
ijadiliwe.

Kiukweli kuongelea tu Udini na Dini kwa mtazamo wangu ni Ujinga.

Nadhani nilikuambia ya kua mimi ni ex-mmisionari na nilipoteza muda mwingi sana kwa kutaka kua padri but baada ya masomo zaidi nlikuja elewa kua imani ni kitu/vitu vya/cha kijinga mara nyingi Na imani za Kidini ni moja ya muendelezo huo huo.

Hizi imani nyingi si chaguo letu ni mambo tu yaliopandikizwa vichwani bila ya ridhaa zetu. Watu wengi ni waislam or wakristo simply tu kwakua wamezaliwa kwenye familia za dini hizo hivyo kulelewa katika misingi hiyo ya kidini na mwisho wake wanakua watumwa wa imani hizo za kidini.

Hizi dini zote tumeletewa na watu WAOVU, watu hao walitudhalilisha, walituibia, na waliwauza ndugu zetu kama samaki. Waarabu na dini yao ya Uislam walishiriki katika vitendo vya ukatili pamoja na WAOVU wenzao Wayuropa.

Inasikitisha sana kwa mimi na wewe Africans tunakuwa wajinga kiasi cha kushangaza "eti tunatengana/kutenganishwa na Ujinga uliopandikizwa na watu WAOVU walitenda mambo ya UOVU wa kutisha katika historia ya Mwanaadam.
 
Uhuru na Umoja,
Kila binadamu kaumbwa na uwezo tofauti wa mambo mengi.
Mimi nani hata nikupinge wewe kwa mawazo yako hayo?
 
Salam Mwalimu Mohamed Said

Ningependa kuwa na swali moja tu kwako.

Tumekuwa na Rais Muislamu kwa miaka 10. Tokea 2005 hadi 2015. Huyu ni Muislamu mwenzenu kabisa.

Pia makamu wake alikuwa ni Muislamu msomi tu. Na Mwenye kujua Mambo mengi ya elimu dunia na Qur'an.

Sasa ningependa kufahamu mbona hawa viongozi waislamu wenzenu walishindwa kuivunja Bakwata na kuwapa Taasisi bora na nzuri ambayo ingekuwa mtetezi wenu wa kweli.

Asante.
 
Kuna muislam na muislam jina

Sasa huyu muheshimiwa sijui alikuwa wapi, nadhani jibu unalo.
 
Kwani rais na makamo wake walikuwa madarakani kwa maslahi ya uislam na waislam au kwa maslahi ya wtz wote bila kujali dini zao kabila zao na rangi zao?

Sijui elimu yako na umri wako lakini hili swali lako hata kadada kakazi hawezi kuuliza swali hili.

Samahani kama nimekukwaza maana hapa nilitaka nikujibu zaidi ya hivi lakini naheshimu huu mwezi na hii sheria ya mitandao...
 
Nkuba,
Tusichanganye maudhui.
Ikiwa unataka tujadili BAKWATA fungua uzi In Shaallah nitakuja kujadili.

Lakini ikiwa unataka kuijua historia ya BAKWATA ingia hapo chini:
Mohamed Said: BAKWATA KIBARAKA KIPINDI MAALUM KILICHORUSHWA NA RADIO KHERI, RADIO QUIBLATAIN NA RADIO IMAAN 1 OKTOBA 2012
 
Kiukweli Pascal huwa ananisikitisha kwa posts zake za kikabila na ukanda. Sijui anajaribu kuleta ujumbe gani kwa Taifa?! Wacha tuangalie.
Karibuni na huku mtie neno.
P
 
TANU umeijuwa mwaka 1964 lakini TAA iliyoizaa TANU mwaka 1954 unaijuwa vilivyo mpaka malengo yake!

Hapo sijuwi nishangae, ninune, nicheke au nisepe tu?
 
Soma hiyooo...

 
Soma hiyoo...

 


Huu pia ni urongo, hapa unataka kujenga picha kuwa eti ni Sheikh Takadir ndie aliyemtambulisha Nyerere kwa mara ya kwanza kwa watu wa Dar es Salaam!, sii kweli!, kwenye utambulisho wa Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam, naamini unaujua vilivyo!, labda ungesema, Sheikh Takadir pia alipiga ile 'fatha' yake maarufu kwenye mkutano wa kwanza wa kumtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam, ningekukubalia, lakini siye yeye aliyemtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam!.

Hili pia ni kujazilizia tuu kile Nyerere alichoandikiwa, kama Sheikh Takadir aliyasema haya 1957, alicopy tuu utabiri uliotangulia na kuja kuwa paste hapo kwenye hiyo tafrija ya Taarab, nyota ya Nyerere iliisha anza kung'aa siku nyingi tangu yuko Tabora School, Makerere, Edinburg hadi St. Francis (Pugu) siku nyingi kabla, hivyo utabiri huu wa Sheikh Takadir ilikuwa ni kujazia tuu yaliomo yamo!, usitaka kudanyanga humu eti aliyemtabiria Nyerere ukuu ni Sheikh Takidir!, is just one of them!.


Huu utakuwa ni urongo mwingine, unless wewe ulikuwa bennet na Mwalimu, 24/7 hadi anaingia kaburini, ndio uweze kulisema hili kwa hakika!.

Hapa sasa ndio the Best of Maalim Mohamed Said!, muogope Mola wako!, huwezi kudaid kuwa Sheikh Takadir alikufa kwa kihoro cha kutoswa!, yaani kisababishi cha kifo chake ni kule kutenwa na jamii!. Uhai umeumbwa, na kifo pia kimeumbwa, Sheikh Takadir alijifia natural death siku yake aliyopangiwa na Mungu ilipowadia!. Kwa msio jua!, Malaika mtoa roho, Israel, anampitia kila mmoja wetu mara sabaini fii sabaa kwa siku, ili kuhakikisha muda wake ukifika asizidishe hata sekunde moja!. Hili ni moja ya bandiko jingine la Maalim Mohemed Said lenye kutoa ilmu adimu, but with "ill motive" behind!, ili ilionekane hata kifo cha Shekh Sulemain Takadir, msababishi ni fulani!.

Pamoja na "the ill motive behind", asante kwa simulizi nzuri,
endelea tuu kuipalilia na kuimwagilia na kuitilia mbolea hii "mbegu", soon itamea vilivyo na tutapata mavuno stahiki!
Pasco.

[/QUOTE]
Sukumagang ni ITIKADI iliyoasisiwa na JPM kwa manufaa ya wasukuma ukiwemo wewe Paskali Njalah Mayala, na kwa faida yako Sukumagang

Wasukuma kama hilo ni tatizo fanyeni kazi ya kulifuta maana hata wewe hujawahi kulishutumu huko nyuma!
Mkuu MTK , angalia tuu tarehe ya bandiko ujue watu huu udini, ukanda na ukabila, watu tumeanza kuukemea lini.
P
 
Paskali,
Naomba unifahamishe ikiwa unafahamu.
Tatizo la udini limeanza lini Tanganyika?

Watu gani walioanzisha udini?
Mkuu Maalim Mohamed Said,
Udini Tanzania ulianzishwa na Wakoloni na missionary maeneo yenye mazao ya biashara ndio walijenga makanisa na Shule za misheni, ni watu wa makabila ya maeneo yenye mazao ya biashara ndio walikuwa na uwezo wa kiuchumi kuwalipia watoto wao karo, hivyo wale wa dini nyingine wao walijenga tuu madras.

Uzuri wa Shule za misheni, hawakuwabagua Waislamu, hivyo kuna kundi kubwa la wasomi wa Kiislamu kabla ya uhuru wameokolewa na hizi Shule za Mission.

Tulipopata uhuru, tukajikuta kazi zote za maana za wazungu zinashikwa na Wakristo ubaguzi wa Wabenzi na Makabwela ukaanza.

Mwalimu Nyerere akatangaza elimu bure ili kila Mtanzania apate fursa sawa, ndipo akagundua akili za makabila wanaokula vizuri sio sawa na akili za baadhi ya maeneo, watoto wanaopasi kwenda sekondari ni wa makabila yale yale. Hivyo aka introduce affirmative action kwa baadhi ya maeneo ili Watanzania wote waelimike.

Tukaachana na mitihani ya cambridge tukaanzisha Baraza letu la Mitihani, kisha akaweka different cut of points za ufaulu, ili Watanzania wote wapate fursa sawa.

Ili ndugu zetu Waislamu nao wapate fursa kama za Mission, Mwalimu akaivunja EAMWS
kwa kosa la kuwadumaza na kuwadunisha Waislamu kwa kuitegemea elimu ya madras pekee na kuanzisha kitu kizuri Bakwata ikaanzisha mashule ya Ilim Duniya na kuwaendeleza Waislamu kielimu.

Lakini licha ya Bakwata kuanzisha mazushule bado Shule za Mission ziliendelea kuongoza kwa kufaulisha Div 1 zikiongozana wakati Shule za Kiislamu zikivuta mkia kwa zero kuongozana hivyo idadi ya Waislamu wanaojiunga vyuo vikuu bado ikawa ndogo.

Hivyo zikitangazwa nafasi za ajira, wenye sifa wengi wanakuwa ni watu wa dini moja hivyo Waislamu kujiona kama wanakuwa marginalised!.

Mimi niliwahi kuuliza humu Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!.

Ingefanywa sensa ya dini za vibaka walioko magerezani, wale wadada wanaofanya ile biashara, wanawake wanaoolewa na kuwa ma golikipa, au idadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye umasikini uliotopea, mngeshangaa!.

Ukiondoa mwanzilishi huyo wa udini ambae ni mkoloni, Waislamu waliendelea kujibagua na mpaka kesho bado wanajibagua.

Hata kwenye vyombo vya ulinzi na kazi za ukakamavu niliwahi pia kuuliza humu Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?

Mwalimu Nyerere alikemea sana ubaguzi wowote, mfano ngoja tusubirie akiishamalizana na the Sukuma Gang, tuone nani wanafuatia!.
Pasco
 
Paskali,
Naamini kwa dhati ya moyo wangu tena bila kusita kuwa hakuna mtu aliyetafiti tatizo la udini Tanzania kunishinda.

Naomba radhi ndugu zangu msinione najipigia zumari mimi mwenyewe.

Niliandika makala kuhusu ''Dini'' na kwa makusudi niliacha kuandika ''Uislam,'' (vinginevyo kichwa cha habari kingekuwa Uislam Ulivyowaunganisha Watanganyika Dhidi ya Ukoloni).

Makala ilitolewa matoleo manne katika Raia Mwema.
Huu ni mwezi mzima.

Makala hayo yanaeleza juhudu za Waislam kuleta umoja wa wananchi kupitia TANU ili kupigania uhuru wa Tanganyika na kuondoa kila aina ya ubaguzi.

Uhuru ukapatikana.

Mimi naweza hapa nikaeleza historia ya ubaguzi baada ya Tanganyika kuwa huru lakini nafanya staha kwani imeelezwa kuwa ''Nyerere alikemea udini.''

Sioni kama ni busara kwangu kuingia katika historia hiyo.

Lakini tatizo hili nimelieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Wala tatizo kubwa linalokabili nchi yetu si ukabila wala ukanda.

Hata chini ya ukoloni ukabila na ukanda haukupata kuwa tatizo.
Tatizo la ubaguzi baada ya uhuru lilianzishwa na wale walioshika serikali.

Hawa wanafahamika.

Wanaobaguliwa pia wanafahamika na wameeleza hadharani kuhusu ubaguzi huu.

Hawajaacha kueleza kuhusu ubaguzi huu hadi leo.

Serikali ina hofu kubwa ya kujadili tatizo hili.
Wanadhani na wanategemea tatizo hili litajiondoa lenyewe.

 
Paskali,
Naamini kwa dhati ya moyo wangu tena bila kusita kuwa hakuna mtu aliyetafiti tatizo la udini Tanzania kunishinda.

Naomba radhi ndugu zangu msinione najipigia zumari mimi mwenyewe.
Maalim Mohamed Said , nakuunga mkono na juzi kati nilikuona TBC, nikajisemea wewe ni a very resourceful person, unafaa upewe your own 30 minutes weekly ya kipindi chako kipewe jina lolote, "Masimulizi ya Mohamed Said" na kutuletea vile visa kimoja baada ya kingine ili sio tuu kuwaelimisha Watanzania mengi yasiyofahamika, bali pia kuyahifadhi masimulizi hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Udini, ukanda na ukabila ni tatizo ila tumeamua kutumia njia ya negation kulikabili na uki liongea tuu huchelewi kuitwa mdini, mkanda na mkabila!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…