Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

.....................

Ulijibiwa hivi:

Pasco,
Ndugu yangu.

Hivi vitisho vya nini?
Wewe si wa kutishika na kalamu yaMohamed Said.

Mtu mmoja mkubwa katika CCM alipata kuniita mimi, "Mbilikimo."

Kisa chake kakasirika kuandika kuwa babu zangu baada ya kuunda African
Association wakaunda Al Jamiatul Islamiyya kisha TANU.

Jamaa zangu wakanambia huyu kakutukana kwa kuwa umemtisha.
Mimi nikauliza nimemtisha kitu gani?

Wakasema unaezua kipaa cha nyumba yake.
Kikiondoka kipaa hicho yeye hana stara tena.
 
scan0026.jpg

Kutoka Kushoto: Sheikh Suleiman Takadir, Mbutta Milando, JohnRupia na Julius Nyerere Hao Waliowazunguka na Silaha za Jadi ni Bantu Group Kundi la Vijana wa TANU lililokuwa linatoa Ulinzi kwa Viongozi wa TANU. Picha Hii Ilipigwa Mwaka wa 1955.

Jina la Sheikh Suleiman Takadir halijapatwa kutajwa popote katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika wala katika historia ya TANU. Hatajwi na hakupata kutajwa baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 na sidhani hata kama atakuja kutajwa au kukumbukwa na hawa viongozi walio katika madaraka hivi sasa. Lakini naamini viongozi hawa walio madarakani hivi sasa ambao wakati wa kudai uhuru walikuwa watoto wadogo lazima watakuwa wamesikia jina hili likitajwa na wazee wao. Sheikh Suleiman Takadir hutajwa kila linapotokea jambo ambalo Waislam huonekana wanadhulumiwa na serikali kwani ilikuwa Sheikh Suleiman Takadir ndiye aliyeweka agenda ya hali ya baadae ya Waislam na Uislam katika Tanganyika huru mwaka 1958. Jambo hili alipolileta lilitishia kuigawa TANU katika misingi ya dini katika wakati amabo umoja wa Waafrika ulikuwa unahitajika sana. Mwaka wa 1958 TANU ilikuwa imeenea nchi nzima na tayari iko katika barabara ya kuelekea kuchukua madaraka ya ndani na kisha Tanganyika kupata uhuru wake kamili.

Sheikh Suleiman Takadir alikuwa nani na nini ulikuwa umaarufu wake? Sheikh Suleiman Takadir kwanza alikuwa ''alim," mwanazuoni kisha alikuwa Mwenyekiti muasisi wa Baraza la Wazee wa TANU kuanzia TANU ilipoundwa mwaka 1954 hadi "alipotoswa" mwaka 1958 kwa kosa la "kuchanganya dini na siasa.'' Sheikh Takadiri alishiriki vilivyo ndani ya Baraza la Wazee wa TANU katika kutayarisha safari ya Nyerere kwenda UNO mwaka 1955. Wapenzi wake katika harakati za kupigania uhuru walimpachika jina la utani wakimwita "Makarios," wakimlinganisha na Askofu Makarios wa Cyprus na Ugiriki aliyekuwa anapambana na ukoloni wa Waingereza wakati yeye alipokuwa anapambana na Waingereza katika ardhi ya Tanganyika. Sasa kwa kuwa Suleiman Takadir alikuwa sheikh na mpambanaji ndipo walimpa jina hilo la "Makarios" na kwa hakika jina hili lilimkaa, likamwenea vyema na yeye akalipenda.

WAZEE%2BWA%2BTANU.jpg

Baraza la Wazee wa TANU
Sheikh Suleiman Takadir wa Pili Chini Kulia, Wa Pili Waliosimama Dossa Aziz,
Wa Sita Julius Nyerere, Wa Saba John Rupia, Wa Tisa Said Chamwenyewe,
Anaefuatia Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate

Mikutano ya mwanzo ya TANU ilikuwa ikifanyika Mnazi Mmoja mbele ya baadae ilipojengwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Wakati ule pale palikuwa hakuna jengo lolote, palikuwa na kiwanja kitupu na ardhi ile ilikuwa mali ya Mzee John Rupia Makamu wa Rais wa TANU. Kiwanja hiki baaadae Mzee Rupia aliwapa TANU na TANU wakaanzisha Chuo Kikuu pale mara baada ya uhuru. Mikutano ya kwanza ya TANU ikifanyika pale Mnazi Mmoja na kabla Nyerere hajapanda juu kwenye jukwaa kuzungumza na wananchi alikuwa kwanza anatangulia Sheikh Suleiman Takadir kusawazisha uwanja na kuwaweka wananchi tayari kumsikiliza kiongozi wao. Kama alivyokuwa Nyerere, Sheikh Suleiman Takadiri alikuwa na kipaji cha kuongea. Leo hii huenda baadhi ya wasomaji wangu wasiamini lakini ukweli ni kuwa Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kabla hajazungumza lolote alikuwa akipiga "fatha," wananchi wakaitika na kwa umoja wao wakasoma, "Surat Fatha," sura ya ufunguzi katika Qur'an Tukufu, kisha Sheikh Takadir akaomba dua na wananchi wakawa wanaitika kwa pamoja, "Amin," Amin," "Amin." Baada ya hapo ndipo atapanda Nyerere na kuanza kuhutubia. (Picha za mwanzo za mikutano hii zipo na zilipigwa na Mzee Shebe ambae katika miaka ile ya 1950 alikuwa na studio yake Mtaa wa Livingstone na Kipata. Picha hizi baadhi nimepata kuziona. Mzee Shebe ndiye alinipiga picha yangu ya kwaza nikiwa na umri wa mwaka mmoja au miwili hivi na picha hii ninayo hadi hii leo. Inaaminika Mzee Shebe ndiye mpiga picha wa kwanza wa TANU na Nyerere).

002_2.JPG

Mwandishi Akiwa na Mwaka Mmoja Au Miwili Picha Aliyopigwa na Mzee Shebe
1952/53 Kwenye Studio Yake Mtaa wa Livingstone na Kipata

scan0027-1.jpg

Nyerere Akihutubia Mkutano wa TANU Siku za Mwanzo

Huyu ndiye Sheikh Suleiman Takadir na huyu ndiye Nyerere kama alivyokuja kutambulishwa kwa watu wa Dar es Salaam na Sheikh Suleiman Takadir kwa mara ya kwanza mwaka wa 1954.Kabla ya hapo Nyerere alikuwa akijulikana na watu wachache katika TAA. Sheikh Takadir alimpenda sana Nyerere kiasi kuwa mwaka 1957 katika hotuba aliyotoa katika tafrija moja ya taarab Mtaa wa Mvita, alimwita Nyerere, "Mtume wa Afrika," aliyetumwa na Mungu kuwaokoa Waafrika. Maneno yale ya Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kama anamtabiria Nyerere makubwa katika mustabali wa Afrika, kwani miaka mingi baadae Nyerere alikuja kusimama mstari wa mbele katika kuikomboa Afrika kutoka makucha ya wakoloni. Nyerere akawa hapungui nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Swahili. Nyumba hii iko jirani na kilabu ya mpira ya Pan Africa. Kutembelewa na Nyerere pale nyumbani kwake ikapelekea baba mwenye nyumba, Jumbe bin Jumaa wa Digosi amuhamishe nyumba Sheikh Takadir asije kumponza kwa kwani Nyerere alijulikana kama adui mkubwa wa Waingereza. Hii kwa muhtasari ndiyo historia ya Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere. Lakini usuhuba huu ulikuja kuvunjika na watu wawili hawa wakawa mahasimu wakubwa, Sheikh Suleiman kafa hasemi na Nyerere na Nyerere kwa upande wake hakupata hata siku moja kumtaja Sheikh Takadir popote hadi anaingia kaburini. Inaaminika Sheikh Takadir alikufa kihoro baada ya kupigwa pande na TANU na wakazi wote wa Dar es Salaam na wanachama wa TANU kwa kosa la "kuchanganya dini na siasa." (Ikiwa msomaji wangu ulisoma makala yangu ya juma lililopita utakuwa umeona kuwa TANU ikiongozwa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir ilipitisha azimio la kupiga vita hisia zozote na chembechembe za Uislam ndani ya TANU). Hakika Uislam ulikuwa na nguvu ndani ya TANU lakini haukuachiwa uvuke mipaka kuwabagua wengine waliokuwa si Waislam.

Kilitokea nini hadi kupelekea Sheikh Suleiman Takadir agombane na Nyerere? Chanzo cha mtafaruku huu ni Uchaguzi wa Kura Tatu wa mwaka 1958. Waingereza waliweka masharti ambayo kwa hakika yalikuwa ya kibaguzi na yalifanya wananchi wengi wasiweze kukidhi sifa zilizowekwa za kuweza mtu kupiga au kupigiwa kura. Kulikuwa na sifa ya elimu, kipato na kazi ya kukubalika na kupiga kura kwa tabaka za rangi. Mpiga kura Mwafrika alitakiwa ampigie kura Mzungu, Muasia na Mwafrika. Masharti haya yalikuwa kisiki kigumu kwa uongozi wa TANU na wanachama wake kutimiza. TANU na viongozi wake wengi hawakuwa na hiyo elimu iliyokuwa ikitakikana wala kipato cha maana. Ili mtu asimame kama mgombea kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria au awe angalau mpiga kura ilibidi azikusanye sifa zote hizo mahali pamoja. Wapiga Kura na wagombea walitakiwa wawe na kisomo cha darasa la 10 au kipato cha pauni 400 kwa mwaka na kuwa na kazi ya maana. Waafrika waliokuwa na sifa hizi hawakuwa wengi katika TANU. Wengi katika TANU kama walivyokuwa wakipenda kujiita wenyewe walikuwa, "Baba Kabwela." Ikawa sasa ili TANU iweze kuweka wagombea ilibidi iwatafute watu nje ya uongozi wa TANU. Hapa ndipo lilipokuwa tatizo.

proxy

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Nyerere Akitia Sahihi Azimio la Tabora[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ilibidi TANU sasa iwalete watu wenye sifa nje yake na wengi wa watu hawa walikuwa Wakristo waliosomeshwa na wamishionari. Jambo hili lilimkera sana Sheikh Takadir na wanachama wengi wa TANU kwa ujumla wao na kwa hakika TANU nzima hawakutaka kabisa kuingia uchaguzi ule kwa masharti yale waliyoyaona ya kibaguzi. Wanachama wa TANU walikuja na kauli mbiu isemayo, "Kuingia Kura Tatu ni sawa na kujipaka kinyesi." Ilikuwapo minong'ono kuwa Wakristo wataichukua nchi lakini kwa muda mrefu hofu hii ilizuiwa kwenye vifua hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kulisema hilo waziwazi kwani jambo la dini lilikuwa mwiko mkubwa katika TANU. Ikawa tatizo lile la kushiriki kwa TANU katika Uchaguzi wa Kura Tatu lijadiliwe kwenye Mkutano Mkuu wa TANU wa mwaka 1958 uliopangwa kufanyika Tabora. Mpinzani mkubwa wa Kura Tatu alikuwa Zuberi Mtemvu, Katibu Mwenezi wa TANU kwa wakati ule. Ukweli ni kuwa Kura Tatu ilitishia uhai wa TANU na zilikuwapo dalili za chama kumeguka pande mbili. Kulikuwa na uwezekano mkubwa sana kuwa Zuberi Mtemvu na Sheikh Takadir wangelikuwa upande mmoja na wangeweza kuja na chama kingine ingawa agenda zao zilikuwa tofauti. Mtemvu yeye alisimama kwenye Afrika kwa Waafrika na Sheikh Takadir kwenye Uislam. Mkutano wa Tabora ni kisa kirefu In Sha Allah tutakitafutia wakati wake makhsusi tukizungumze. (Nimekiandikia kitabu kizima "Uamuzi wa Busara," Abantu Publishers 2007, Dar es Salaam) Sheikh Suleiman Takadir na baadhi ya wazee katika Baraza la Wazee wa TANU walikuwa wajumbe katika mkutano wa Tabora. Kufupisha kisa TANU ilipiga kura kukubali kuingia kwenye Uchaguzi wa Kura Tatu na manusruna kura zifungane kati ya wale wanaounga mkono na wale waliokuwa wakipinga. TANU iliingia katika Uchaguzi wa Kura Tatu na ikapata ushindi mkubwa.

Hofu aliyokuwanayo Sheikh Takadir ilikuwa kuwa watu walioingia katika TANU kuchukua uongozi ni Wakristo. Sheikh Takadir alikuwa anajua nguvu ya madaraka waliyokuwa wanakabidhiwa akawa na hofu kama uongozi huu mpya utakuja kutoa haki kwa Waislam uhuru utakapopatikana. Sheikh Takadir alitaka uhakika wa hali ya baadae ya Waislam katika Tanganyika huru. Katika mkutano wa Halmashauri Kuu Makao Makuu ya TANU, New Street Sheikh Takadir alimkabili Nyerere akamshutumu kuwa hakuwa na nia nzuri na Waislam, atakuja wapendelea ndugu zake Wakristo katika Tanganyika huru. Sheikh Takadir akawageukia wenzake katika Baraza la Wazee wa TANU akasema, "Tuzibe ufa tusije tukajenga ukuta." Jambo lile lilikuwa zito. Nyerere alijiinamia na aliponyanyua uso wake machozi yalikua yanambubujika. Mkutano haukuweza kujadili jambo lile na kikako kile kikavunjika pale pale na wajumbe wakawatawanyika.

Sheikh Takadir ''akatoswa,'' kwani alikuwa amevunja mwiko mkubwa katika TANU. Mzee Iddi Tulio akachaguliwa kushika nafasi yake. Huku ''kutoswa'' na kutengwa na jamii ndiko kulikosababisha kifo cha Sheikh Takadir. Alikuwa hata akitoa salamu hakuna aliyeitika. Akienda sokoni Kariakoo kununua chochote kile hakuna aliyekuwa tayari kupokea hela yake. Haikuchukua muda mrefu Sheikh Takadir akaaga dunia. Kabla Sheikh Takadir hajafa TANU ilifanya mkutano mkubwa sana na Nyerere akamshambulia Sheikh Takadir kwa kutaka kuwagawa Watanganyika katika misingi ya dini. Baada ya mkutano kundi kubwa lilikwenda nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Msimbazi kuzomea huku wakiimba, "Takadir Mtaka Dini." Sheikh Takadir alitoka nje akasimama kizingitini akasema maneno haya, "Ndugu zangu In Sha Allah iko siku mtakuja kunikumbuka." Haukupita muda mrefu Sheikh Takadir akatangulia mbele ya haki na kwa kipindi kirefu katika historia ya uhuru wa Tanganyika hakuna aliyemkumbuka Sheikh Suleiman Takadir, Askofu Makarios wa Tanganyika. Hivi sasa Sheikh Suleiman Takadir anatajwa sana na kizazi cha leo. Utabiri wake kuwa ndugu zake watakuja kumkumbuka umetimia. Swali la kujiuliza ni iweje hii leo baada ya miaka 57 kupita Sheikh Suleiman Takadir anarejeshwa upya katika historia ya kupigani uhuru wa Tanganyika? Hiki ni kitendawili kinachongoja kuteguliwa.

3ngq7mfoNBkDsGoTihZVXo4ZzngGhTG3i5TneJ6bQLk=w409-h207-p-no

Mohamed Said : My brother, you are just rising a FALSE ALARM! Trying to fight against something that does not exist, is to create it. Hakuna udini Tanzania! Tanzania kuna ongezeko la bei za bidhaa na maisha magumu kwa wananchi... Lets concentrate on the concentration!!!
 
LUKUD,
Hakuna tatizo.
 
LUKUD,
Hakuna tatizo.

Hii kitu huwa inanishangaza sana, kwa umri ulionao na elimu inasikitisha kuona mambo unayoyashadadia.

Kwa umri ulionao ni jambo la kheri na busara kutufundisha upendo na mshikamano kwa ujenzi wa taifa hili na si hili jambo uliloshikilia la kutaka kugawa watu kwa itikadi za kidini.

imetosha sasa.
 
Uhuru na Umoja,
Huenda unasema hayo kwa kuwa hujui.

Je ungependa mimi na wewe tujadili mada hii hadharani na mimi
nikupe ushahidi wa tatizo hili nchini petu?

Nimemkwepa LUKUD lakini naona kuna watu wanaipenda mada hii
ijadiliwe.
 
Kiukweli kuongelea tu Udini na Dini kwa mtazamo wangu ni Ujinga.

Nadhani nilikuambia ya kua mimi ni ex-mmisionari na nilipoteza muda mwingi sana kwa kutaka kua padri but baada ya masomo zaidi nlikuja elewa kua imani ni kitu/vitu vya/cha kijinga mara nyingi Na imani za Kidini ni moja ya muendelezo huo huo.

Hizi imani nyingi si chaguo letu ni mambo tu yaliopandikizwa vichwani bila ya ridhaa zetu. Watu wengi ni waislam or wakristo simply tu kwakua wamezaliwa kwenye familia za dini hizo hivyo kulelewa katika misingi hiyo ya kidini na mwisho wake wanakua watumwa wa imani hizo za kidini.

Hizi dini zote tumeletewa na watu WAOVU, watu hao walitudhalilisha, walituibia, na waliwauza ndugu zetu kama samaki. Waarabu na dini yao ya Uislam walishiriki katika vitendo vya ukatili pamoja na WAOVU wenzao Wayuropa.

Inasikitisha sana kwa mimi na wewe Africans tunakuwa wajinga kiasi cha kushangaza "eti tunatengana/kutenganishwa na Ujinga uliopandikizwa na watu WAOVU walitenda mambo ya UOVU wa kutisha katika historia ya Mwanaadam.
 
Kila binadamu kaumbwa na uwezo tofauti wa mambo mengi.
Mimi nani hata nikupinge wewe kwa mawazo yako hayo?
 
Salam Mwalimu Mohamed Said

Ningependa kuwa na swali moja tu kwako.

Tumekuwa na Rais Muislamu kwa miaka 10. Tokea 2005 hadi 2015. Huyu ni Muislamu mwenzenu kabisa.

Pia makamu wake alikuwa ni Muislamu msomi tu. Na Mwenye kujua Mambo mengi ya elimu dunia na Qur'an.

Sasa ningependa kufahamu mbona hawa viongozi waislamu wenzenu walishindwa kuivunja Bakwata na kuwapa Taasisi bora na nzuri ambayo ingekuwa mtetezi wenu wa kweli.

Asante.
 
Kuna muislam na muislam jina

Sasa huyu muheshimiwa sijui alikuwa wapi, nadhani jibu unalo.
Mohamed Said : My brother, you are just rising a FALSE ALARM! Trying to fight against something that does not exist, is to create it. Hakuna udini Tanzania! Tanzania kuna ongezeko la bei za bidhaa na maisha magumu kwa wananchi... Lets concentrate on the concentration!!!
 
Salam Mwalimu Mohamed Said

Ningependa kuwa na swali moja tu kwako.

Tumekuwa na Rais Muislamu kwa miaka 10. Tokea 2005 hadi 2015. Huyu ni Muislamu mwenzenu kabisa.

Pia makamu wake alikuwa ni Muislamu msomi tu. Na Mwenye kujua Mambo mengi ya elimu dunia na Qur'an.

Sasa ningependa kufahamu mbona hawa viongozi waislamu wenzenu walishindwa kuivunja Bakwata na kuwapa Taasisi bora na nzuri ambayo ingekuwa mtetezi wenu wa kweli.

Asante.
Kwani rais na makamo wake walikuwa madarakani kwa maslahi ya uislam na waislam au kwa maslahi ya wtz wote bila kujali dini zao kabila zao na rangi zao?

Sijui elimu yako na umri wako lakini hili swali lako hata kadada kakazi hawezi kuuliza swali hili.

Samahani kama nimekukwaza maana hapa nilitaka nikujibu zaidi ya hivi lakini naheshimu huu mwezi na hii sheria ya mitandao...
 
Salam Mwalimu Mohamed Said

Ningependa kuwa na swali moja tu kwako.

Tumekuwa na Rais Muislamu kwa miaka 10. Tokea 2005 hadi 2015. Huyu ni Muislamu mwenzenu kabisa.

Pia makamu wake alikuwa ni Muislamu msomi tu. Na Mwenye kujua Mambo mengi ya elimu dunia na Qur'an.

Sasa ningependa kufahamu mbona hawa viongozi waislamu wenzenu walishindwa kuivunja Bakwata na kuwapa Taasisi bora na nzuri ambayo ingekuwa mtetezi wenu wa kweli.

Asante.
Nkuba,
Tusichanganye maudhui.
Ikiwa unataka tujadili BAKWATA fungua uzi In Shaallah nitakuja kujadili.

Lakini ikiwa unataka kuijua historia ya BAKWATA ingia hapo chini:
Mohamed Said: BAKWATA KIBARAKA KIPINDI MAALUM KILICHORUSHWA NA RADIO KHERI, RADIO QUIBLATAIN NA RADIO IMAAN 1 OKTOBA 2012
 
Mkuu Paskali una-instigate uhutu na ututsi katika nchi hii. Please stop this. Haisaidii chochote, watanzania hatutakubali kuona watu wanajaribu kujikuza over others. Take it from me, hatutakuwa tayari kabila moja lijitukuze at the expense ya makabila mengine hapa Tanzania. Kabila la wasonjo ni dogo lakini likiona kuna ndivyo sivyo kwa minajili ya ukabila litafight hadi mwisho. Be composed when writing to mass.
Ndugu Jorojik, Thank you very much kwa ukweli ulituwekea hapa. Ndugu Pascal anaendelea kujivunjia hadhi na heshima, japokuwa ni mwandishi mzuri na mwenye maono mazuri ya kisiasa, lakini naona amejiunga na kundi linalosemekana lina mipango ya kutuletea siasa za kiKENYA nchini kwetu.

Ndugu Pascal yumo kwenye siasa za kidini na kikabila, hili jambo limenishtusha na kunisonesha sana, i was a great follower of his writings, but now am very disappointed.

Ninamuombea mungu amrudishe kwenye fikra za kizalendo na amuepushe na ukabila na udini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu Pascal, I truly hope unasome post zote katika uzi huu.

JEE huoni kama umetukosea sana Watanzania kwa kuutukuza ukabila na udini?

JEE huoni kama kuna wengi hapa JF walikuwa wapenzi wa michango yako mizuri na post zako nyingi zilizokuwa na mafunzo, ukweli na upendo.

I believe you need to sit down na kutafakari na ujirekebishe.

Ndugu Ukabila hauna maendeleo wala faida, nadhani hakuna anayefaidika kwa ukabila , it has never put any food in your plate nor supported your family.

Ndugu tuangalie yaliyotokea Somalia, hii ni nchi yenye watu wa Lugha Moja, dini moja tena madhehebu moja, lakini kilichoiteketeza somalia ni ukabila.

Tusisahau yaliyotokea Rwanda, Burindi, Kenya, Central Africa Republic, Myanmar na yanayo endelea leo India, bila kusahau Iraq na Syria.

Jee utafurahia hayo yakitokea Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli Pascal huwa ananisikitisha kwa posts zake za kikabila na ukanda. Sijui anajaribu kuleta ujumbe gani kwa Taifa?! Wacha tuangalie.
Karibuni na huku mtie neno.
P
 
Huo ni mtizamo wako binafsi. Usilazimishe mtizamo wako kihistoria uwe ndiyo msimamo "official". Mada zako nyingi zimejikita katika Uislamu na Pwani ya Tanganyika. Nikutaarifu tu kwa mimi niliyetoka "interior" Tanganyika kwa mara ya kwanza nimekutana na waislamu (sisi kule kwetu tunaita "Waswahili") mwaka 1970 ukichukulia maanani nimezaliwa miaka ya 50. Lakini chama cha TANU nimekisikia mwaka wa 1964. Waswahili walikuwa confined to the coastal belt na vision yao kabla ya Nyerere sidhani kwamba ilikuwa kubwa kwa sababu malengo yao yalikuwa ni ya kijamii zaidi kuliko kisiasa. TAA ilibadilika sana Nyerere alivyoingia kwa sababu ailibadilisha vision na mission ya TAA kuwa political rather than social. The very fact kwamba mtu mmoja alileta mabadiliko makubwa kiasi hicho wakati kundi la waswahili hawakuweza kufanya hivyo mpaka Nyerere alipofika, ndicho kinachokukwaza sana na unafikiri labda Nyerere aliwakandamiza. Historia imejaa mifano mingi tu ya namna mtu mmoja anavyoweza kuhamasisha watu kwa lengo fulani. Hivyo mantiki yako ni very narrow na hii haishangazi sana kwa kuwa "Religion has never been the best argument to base on, unless mtu umefilisika kabisa kifikra".
TANU umeijuwa mwaka 1964 lakini TAA iliyoizaa TANU mwaka 1954 unaijuwa vilivyo mpaka malengo yake!

Hapo sijuwi nishangae, ninune, nicheke au nisepe tu?
 
Inaonekana umejitoa ufahamu maswali unayajuwa na unakwepa kwepa

Naona unajivunia kuchapicha Oxford University press mimi nimefanyanao kazi ila kwa sasa ninakampuni yangu mimi nimejikita zaidi kwenye UCHUMI na Upatanishi kuliko dini nawengi wamefaidika na mimi pia nimetembea bara la Ulaya kwenye nchi zaidi 15 Afrika zaidi ya nchi 20 America asia na kwingineko
Huko kote nimealikwa kwenye midahalo yakuikomboa Dunia hasa mwafrika kutoka kwenye utumwa wakimawazo nakujenga uchumi imara

Dunia yaleo sio kuzungumzia dini fulani au utawala wa dini fulani maana hauna tija
Kunachi zinaongozwa kwa imani za kidini kama
Misri,Irak,Iran,Libya nanyinginezo hakuna utulivu zaidi ya ugomvi

Nadhani ifike sehemu dini zibaki misikitini na makanisa huku tuubiri upendo amani basi
Soma hiyooo...

Sheikh Mohamed Said wewe kuniweka katika ile s.... list wala sikosi usingizi kamwe laiti ungelijua mimi nimekuweka katika list gani ungekaa kimya.Histohisia zako kuchapwa Oxford University Press,New York... wala si hoja laiti ungelijua wazungu wanatuwazia nini sisi waAfrika usingejitapa katu.Wazungu unaowasifia wanatamani sana kuona Tanzania inaingia kwenye mifarakano ili iwe rahisi kutuibia Dhahabu,Gas,Tanzanite..... watafurahi sana kumpata mchochezi wa udini kama wewe itawarahisishia kuliharibu taifa alilolijenga Mwl Nyerere kwa miongo mitatu.
Soma hiyoo...

Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza asante kwa kisa hiki cha Mzee wako, Sheikh Suleiman Takadir, ila sio kweli kuwa Mzee huyu hatajatwa popote kwenye historia ya Tanu, kwa sababu mimi nimelisikia jina la Sheikh Suleiman Takadir siku nyingi, kabla sijakusoma wewe, hivyo lazima kuna mahali alitajwa hadi mimi kumjua!, na sio kutajwa tuu, nadhani ia kuna namna alienziwa, sikumbuki vizuri, lakini nahisi niliwahi kulisikia jina la Mtaa fulani ukiitwa Takadiri japo sikumbuki vizuri!.

Kama hii ndio ilikuwa sifa kuu ya Sheikh Takadir, "kuongea sana na kupiga 'fatha' kwenye mikutano ya Tanu!, connotation meaning ya para hii ni kuwa Mkiristo Nyerere, alikuwa hawezi kupanda jukwaani kuwahutubia Waislamu wa Tanu, mpaka kwanza Sheikh Takadir atangulie kuwapooza kwa 'fatha'!, jambo ambalo sii kweli!, ili ukweli ni kuwa Maeneo mengi ya Uswahilini, walijaa Waislamu, hivyo hizo 'fatha' ni kikolezo tuu cha kujengea hamasa, kama alivyoakifanya Salum Tambalizeni kwenye mikutano ya CCM, yaani kazi ya uhamasishaji, hivyo inawezekana kwa sasa, usimsikie Tambalizeni ekienziwa popote!, kama ambavyo alivyotoswa Sheikh Takadir!, msingi wa mtu yeyote kuenziwa ni mchango wake kuthaminiwa kwenye jambo fulani!, kama mchanga wake ni uhamasishaji tuu, then alivyothaminiwa hata kwa kutajwa tuu hadi mimi kumfahamu, ni thamani tosha!. Wako wengi walioisaidia sana Tanu, na wengine hadi kufungwa gerezani kuipigania Tanu kama kina Robert Makange na Kheri Bagdelalah lakini sikumbuki kuwasikia ni wapi walienziwa!. Kuna mamia wengine huko mikoani, wamefanya makubwa kwa Tanu, lakini sikupata kuwasikia mfano Dr. Kyaruzi, mimi ndio nimemsikia juzi juzi tuu baada ya kufariki kimya kimya huko kwao Bukoba!. Hivyo kuna wengi waliofanya makubwa kwa Tanu, hawajatajwa, ila wewe unajenga picha kwa Wazee wako tuu kuwa hawajatajwa kwa Uislamu wao!, kitu ambacho sii kweli, na haitakuwa kweli hata siku moja!.

Huu pia ni urongo, hapa unataka kujenga picha kuwa eti ni Sheikh Takadir ndie aliyemtambulisha Nyerere kwa mara ya kwanza kwa watu wa Dar es Salaam!, sii kweli!, kwenye utambulisho wa Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam, naamini unaujua vilivyo!, labda ungesema, Sheikh Takadir pia alipiga ile 'fatha' yake maarufu kwenye mkutano wa kwanza wa kumtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam, ningekukubalia, lakini siye yeye aliyemtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam!.

Hili pia ni kujazilizia tuu kile Nyerere alichoandikiwa, kama Sheikh Takadir aliyasema haya 1957, alicopy tuu utabiri uliotangulia na kuja kuwa paste hapo kwenye hiyo tafrija ya Taarab, nyota ya Nyerere iliisha anza kung'aa siku nyingi tangu yuko Tabora School, Makerere, Edinburg hadi St. Francis (Pugu) siku nyingi kabla, hivyo utabiri huu wa Sheikh Takadir ilikuwa ni kujazia tuu yaliomo yamo!, usitaka kudanyanga humu eti aliyemtabiria Nyerere ukuu ni Sheikh Takidir!, is just one of them!.

Huu utakuwa ni urongo mwingine, unless wewe ulikuwa bennet na Mwalimu, 24/7 hadi anaingia kaburini, ndio uweze kulisema hili kwa hakika!.

Hapa sasa ndio the Best of Maalim Mohamed Said!, muogope Mola wako!, huwezi kudaid kuwa Sheikh Takadir alikufa kwa kihoro cha kutoswa!, yaani kisababishi cha kifo chake ni kule kutenwa na jamii!. Uhai umeumbwa, na kifo pia kimeumbwa, Sheikh Takadir alijifia natural death siku yake aliyopangiwa na Mungu ilipowadia!. Kwa msio jua!, Malaika mtoa roho, Israel, anampitia kila mmoja wetu mara sabaini fii sabaa kwa siku, ili kuhakikisha muda wake ukifika asizidishe hata sekunde moja!. Hili ni moja ya bandiko jingine la Maalim Mohemed Said lenye kutoa ilmu adimu, but with "ill motive" behind!, ili ilionekane hata kifo cha Shekh Sulemain Takadir, msababishi ni fulani!.

Pamoja na "the ill motive behind", asante kwa simulizi nzuri,
endelea tuu kuipalilia na kuimwagilia na kuitilia mbolea hii "mbegu", soon itamea vilivyo na tutapata mavuno stahiki!
Pasco.

[/QUOTE]
Sukumagang ni ITIKADI iliyoasisiwa na JPM kwa manufaa ya wasukuma ukiwemo wewe Paskali Njalah Mayala, na kwa faida yako Sukumagang

Wasukuma kama hilo ni tatizo fanyeni kazi ya kulifuta maana hata wewe hujawahi kulishutumu huko nyuma!
Mkuu MTK , angalia tuu tarehe ya bandiko ujue watu huu udini, ukanda na ukabila, watu tumeanza kuukemea lini.
P
 
Jina la Sheikh Suleiman Takadir halijapatwa kutajwa popote katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika wala katika historia ya TANU. Hatajwi na hakupata kutajwa baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 na sidhani hata kama atakuja kutajwa au kukumbukwa na hawa viongozi walio katika madaraka hivi sasa. Lakini naamini viongozi hawa walio madarakani hivi sasa ambao wakati wa kudai uhuru walikuwa watoto wadogo lazima watakuwa wamesikia jina hili likitajwa na wazee wao. Sheikh Suleiman Takadir hutajwa kila linapotokea jambo ambalo Waislam huonekana wanadhulumiwa na serikali kwani ilikuwa Sheikh Suleiman Takadir ndiye aliyeweka agenda ya hali ya baadae ya Waislam na Uislam katika Tanganyika huru mwaka 1958. Jambo hili alipolileta lilitishia kuigawa TANU katika misingi ya dini katika wakati amabo umoja wa Waafrika ulikuwa unahitajika sana. Mwaka wa 1958 TANU ilikuwa imeenea nchi nzima na tayari iko katika barabara ya kuelekea kuchukua madaraka ya ndani na kisha Tanganyika kupata uhuru wake kamili.
Paskali,
Naomba unifahamishe ikiwa unafahamu.
Tatizo la udini limeanza lini Tanganyika?

Watu gani walioanzisha udini?
Mkuu Maalim Mohamed Said,
Udini Tanzania ulianzishwa na Wakoloni na missionary maeneo yenye mazao ya biashara ndio walijenga makanisa na Shule za misheni, ni watu wa makabila ya maeneo yenye mazao ya biashara ndio walikuwa na uwezo wa kiuchumi kuwalipia watoto wao karo, hivyo wale wa dini nyingine wao walijenga tuu madras.

Uzuri wa Shule za misheni, hawakuwabagua Waislamu, hivyo kuna kundi kubwa la wasomi wa Kiislamu kabla ya uhuru wameokolewa na hizi Shule za Mission.

Tulipopata uhuru, tukajikuta kazi zote za maana za wazungu zinashikwa na Wakristo ubaguzi wa Wabenzi na Makabwela ukaanza.

Mwalimu Nyerere akatangaza elimu bure ili kila Mtanzania apate fursa sawa, ndipo akagundua akili za makabila wanaokula vizuri sio sawa na akili za baadhi ya maeneo, watoto wanaopasi kwenda sekondari ni wa makabila yale yale. Hivyo aka introduce affirmative action kwa baadhi ya maeneo ili Watanzania wote waelimike.

Tukaachana na mitihani ya cambridge tukaanzisha Baraza letu la Mitihani, kisha akaweka different cut of points za ufaulu, ili Watanzania wote wapate fursa sawa.

Ili ndugu zetu Waislamu nao wapate fursa kama za Mission, Mwalimu akaivunja EAMWS
kwa kosa la kuwadumaza na kuwadunisha Waislamu kwa kuitegemea elimu ya madras pekee na kuanzisha kitu kizuri Bakwata ikaanzisha mashule ya Ilim Duniya na kuwaendeleza Waislamu kielimu.

Lakini licha ya Bakwata kuanzisha mazushule bado Shule za Mission ziliendelea kuongoza kwa kufaulisha Div 1 zikiongozana wakati Shule za Kiislamu zikivuta mkia kwa zero kuongozana hivyo idadi ya Waislamu wanaojiunga vyuo vikuu bado ikawa ndogo.

Hivyo zikitangazwa nafasi za ajira, wenye sifa wengi wanakuwa ni watu wa dini moja hivyo Waislamu kujiona kama wanakuwa marginalised!.

Mimi niliwahi kuuliza humu Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!.

Ingefanywa sensa ya dini za vibaka walioko magerezani, wale wadada wanaofanya ile biashara, wanawake wanaoolewa na kuwa ma golikipa, au idadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye umasikini uliotopea, mngeshangaa!.

Ukiondoa mwanzilishi huyo wa udini ambae ni mkoloni, Waislamu waliendelea kujibagua na mpaka kesho bado wanajibagua.

Hata kwenye vyombo vya ulinzi na kazi za ukakamavu niliwahi pia kuuliza humu Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?

Mwalimu Nyerere alikemea sana ubaguzi wowote, mfano ngoja tusubirie akiishamalizana na the Sukuma Gang, tuone nani wanafuatia!.
Pasco
 
Naamini kwa dhati ya moyo wangu tena bila kusita kuwa hakuna mtu aliyetafiti tatizo la udini Tanzania kunishinda.

Naomba radhi ndugu zangu msinione najipigia zumari mimi mwenyewe.

Niliandika makala kuhusu ''Dini'' na kwa makusudi niliacha kuandika ''Uislam,'' (vinginevyo kichwa cha habari kingekuwa Uislam Ulivyowaunganisha Watanganyika Dhidi ya Ukoloni).

Makala ilitolewa matoleo manne katika Raia Mwema.
Huu ni mwezi mzima.

Makala hayo yanaeleza juhudu za Waislam kuleta umoja wa wananchi kupitia TANU ili kupigania uhuru wa Tanganyika na kuondoa kila aina ya ubaguzi.

Uhuru ukapatikana.

Mimi naweza hapa nikaeleza historia ya ubaguzi baada ya Tanganyika kuwa huru lakini nafanya staha kwani imeelezwa kuwa ''Nyerere alikemea udini.''

Sioni kama ni busara kwangu kuingia katika historia hiyo.

Lakini tatizo hili nimelieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Wala tatizo kubwa linalokabili nchi yetu si ukabila wala ukanda.

Hata chini ya ukoloni ukabila na ukanda haukupata kuwa tatizo.
Tatizo la ubaguzi baada ya uhuru lilianzishwa na wale walioshika serikali.

Hawa wanafahamika.

Wanaobaguliwa pia wanafahamika na wameeleza hadharani kuhusu ubaguzi huu.

Hawajaacha kueleza kuhusu ubaguzi huu hadi leo.

Serikali ina hofu kubwa ya kujadili tatizo hili.
Wanadhani na wanategemea tatizo hili litajiondoa lenyewe.

242088131_1025265708220807_2512999011382367468_n.jpg
 
Paskali,
Naamini kwa dhati ya moyo wangu tena bila kusita kuwa hakuna mtu aliyetafiti tatizo la udini Tanzania kunishinda.

Naomba radhi ndugu zangu msinione najipigia zumari mimi mwenyewe.
Maalim Mohamed Said , nakuunga mkono na juzi kati nilikuona TBC, nikajisemea wewe ni a very resourceful person, unafaa upewe your own 30 minutes weekly ya kipindi chako kipewe jina lolote, "Masimulizi ya Mohamed Said" na kutuletea vile visa kimoja baada ya kingine ili sio tuu kuwaelimisha Watanzania mengi yasiyofahamika, bali pia kuyahifadhi masimulizi hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Udini, ukanda na ukabila ni tatizo ila tumeamua kutumia njia ya negation kulikabili na uki liongea tuu huchelewi kuitwa mdini, mkanda na mkabila!.
P
 
Back
Top Bottom