Visa ya kusoma anataka na kuzamia?? Ni ngumu, muulize tena.
Pia kwa watumishi wanaoenda kusoma masters huko ,hawawezi kukubaliwa kuunganisha PhD bila muajiri wake kujua.
Kumbuka kuwa barua za udhamini na vigezo vyote muajiri ndio mtu wa kwanza.
Tuseme hiyo phD kajilipia, napo kuna ugumu kwa kuwa inabidi aongeze muda wa kukaa/kusoma huko, na hapo ni lazima muajiri ahusishwe.
Labda useme, kashirikiana na muajiri wake (kitu ambacho SIDHANI)
Mwisho wa uongo wako upo hapa
Huwezi wapelekea barua NSSF eti mafao yako wawape bank, Hapa UMEONGOPA.
Kinachotokeaga ni: bank wanaweza kukupa masharti/form/mkataba ujaze endapo utashindwa kulipa mkopo wao kwa sababu za kushindwa kuendelea na ajira yako, basi inakupasa pesa utayopata ya mafao NSSF wachukue wao.
Lakini sio wewe uwapelekee barua NSSF, kinachotokeaga ni kuna mambo mawili;
- wakati wa kujaziwa taarifa zako za kuchukua hayo mafao na muajiri wako(HR), HR hataweza kukujazia mpaka umalizane na bank kwa kuwa bank ni lazima wawasiliane na HR kuhusu mkopo wako
- NSSF wana utaratibu wa kuhakiki taarifa zako za kibank, na kuna form ya NSSF unaenda nayo bank ili wakujazie taarifa na kuthibitisha taarifa zako. Na hapo bank ni lazima watakubana