Pole sana kijana. Hongera sana kwa kujifunza kuwa hakuna hela za ku-download. Iwe fundisho kwa mataahira wengine wanaopenda shortcut kwenye maisha.
Change your mindset
Kila siku Tunawashauri Kamari ni Dhambi.
Kubeti ni Dahmbi.
Hakuna aliyewhi kufanikiwa kwenye hizo kamari.
MSICHEZE KAMARI.
Sio betting hiyo kuweni na akili basi, tatizo la hizi shithole countries zilizochelewa kuyajua mabadiliko ya maendeleo ya kitechnolojia zinaishia kuumia kila siku sababu ya kukurupuka wenzio wakiwa wameshaamka.
Forex&Cryptocurrency sio utapeli wala aihusiani na betting, ni vile opportunity hii iliingia bongo bado watu wakiwa ktk mindset ya ujima kwamba, ili ufanikiwe lazima uvuje jasho na kujihusisha na kazi za kutumia nguvu akili kidogo, baada ya watu kuanza kuijua biashara hii kuna wachache waliitumia kama chance ya kuwatapeli wengi wajinga wasioijua.
Tofauti na hivi leo maendeleo ya internet yameleta ufahamu mkubwa wa watu kwa vitu walivyokuwa wakitapeliwa sababu ya ujinga wa kutokuvijua, the same thing utapeli uliokuwa ktk mitandao ya simu, leo hii elimu inatolewa kila mahala mitandaoni, tofauti na miaka 5 iliyopita.
Hivi leo kuna Contents creators kwenye social media wamejaa wakiwaelimisha kuhusu fursa za mitandaoni, trading channels kila mahala kuanzia TikTok, Facebook, Instagram, Whatsapp kote huku kuna walimu wa kutoa maarifa ya hizi opportunities, bila kusahau siku hizi kuna institutes nyingi mijini na nje ya miji zinatoa huduma ya kielimu kuhusu hii biashara, sasa mtu unafeli wapi?.
La mwisho kwa sasa kuna uhuru wa kupata elimu kwa njia rahisi kupitia simu yako yenye internet kupitia searching engines(google,) pia kuna AI zinazotoa maelezo ya kila jambo, je mtu unafeli wapi kupata mwanga wa jambo kabla ya kuanza lawama?.
Kwa kila jambo lazima skills(knowledge+experience) itumike ili upate ufaulu ktk jambo hili, mnaosema forex ni betting hamna tofauti na wale wanaokimbilia biashara/kilimo kisa trending wanayoona kwa wenzao waliofanikiwa/kuwashawishi wakihisi watafanikiwa kama wao.
Hauwezi kufanikiwa over night kwa jambo lolote lile haiwezekani, sasa nyie vilaza kwanini mnataka trading iwatajirishe kirahisi wakati kazi zingine hazitajirishi kirahisi hivi?.
Lack of exposure ndio inasababisha hii nchi tubaki nyuma kwa kila jambo, wenzetu nchi jirani kama Kenya, fursa za mitandaoni zinaboresha maisha ya watu sababu ya raia wao kujielimisha kwa kufuata dunia inataka nini kwa kuendana na technology, sisi tuko bize na siasa za kupigana, simba+yanga, kilimo cha mkono na upuuzi wa kila aina wakati huo fursa za maana zikitupita then baadae zikitufikia tunaita utapeli sababu ya kukurupukia.