Jinsi biashara ya forex ilivyonifilisi na kuniacha na madeni

Jinsi biashara ya forex ilivyonifilisi na kuniacha na madeni

Mkuu. Naomba utoe ushauri kulingana na mazingira. Hebu tafakari kwanza: Kuna robot lenye uwezo wa ku-download mpaka dola 10,000 kwa wiki, na mwenye hilo robot analiuza kwa dola 2500. Swali: Kwanini aliuze badala ya kulitumia? Na kama anayo mengi, kwa nini hayatumii yampe fedha nyingi zaidi kuliko hizo anazopata kwa kuuza? Yale yale ya mganga wa kienyeji anayelala kwenye kibanda anakulipisha fedha ili akufanye uwe tajiri.
kwa mfano mtu akinifata akaniambia weka mia utapata mia 2 na ili upate hiyo namna nilipe shilingi tano
sitakubali kwa sabab kama kuna uwezekano wa kuipta mia asingenifata mimi
awekeze mwenyewe
ni simple logic ambayo ukipenda shirtcut ipo kila mahali
kuanzia mr kuku and soo on
watu wengi hawapendi kuumia
hwapendi mchakato ndo maana wanapigwa kirahisi

nimempongeza jamaa kwa sabbu alidhubutu kuijua forex ila pia nimemwambia asipende kufanyiwa mambo
alitakiwa afanye deep search kuhusu hizo mambo za roboti
ajifunze kwa mchakato
ila yeye alitaka shortcut

ila nimeongea pia coment nyingi watu wengi ni waoga sana wa kujribu hta kuijua hiyo forex
hawaijui kabisa ila wanaiongelea sana
kwa upande wa utapeli ili hali hawajajishuhulisha kuijua
jamaa amejaribu
na hiyo ni ajali katika upambanaj
 
Uliwahi kujiuliza kwanini yeye hatumii hilo robot kutengeneza hiyo 100k dollars? Badala yake anaitaka 2.5k dollars yako?
 
Habari zenu wana jamvi,

Nimependa leo niweze kushare hapa changamoto ninayopitia ambayo imenifanya nipoteze Kila kitu kwenye maisha yangu kupitia hii biashara ya forex

Mimi ni mhitimu kutoka UDSM chuo ambacho kina magenius wengi sana na ma TO wengi sana wamemaliza hapo

Biashara ya forex niliifahamu mwaka 2022 wakati naingia mwaka wa kwanza chuoni hapo na niliifahamu Kuna mtanzania mmoja maarufu sana (aliwahi kua na brokerage yake) alikua na mkutano hapo chuoni kuhusu maswala ya fedha na biashara

Na ndipo nilipo fahamu kwa mara ya kwanza kabisa kuhusu hii biashara inayoitwa forex

Tangu mwaka huo 2022 niliwahi kulipia forex kujifunza kwake lakini sikuzingatia sana sababu bado chuo kilikua kinanibana hivyo nilielewa juu juu tu

Mwaka 2023 mwezi wa 7 ndipo nilianza kuichukulia biashara ya forex serious hapa nililipia darasa kwa wasouth Africa wanaitwa FX GOAT walikua na course yao ya $75

Kwa kweli safari ya kujifunza imekua ngumu sana toka 2023 mpaka leo niseme nimepotesa pesa nyingi sana hapa namaanisha maboom,hela za intern pia nilikua winga wa simu hivyo zile ganji ganji nilikua nazitumia kudeposit na kulipia training tofauti tofauti

Kwa hapa Tanzania nimesoma kwa watu wengi kama Jeff,pipstorm,TraderMT na liquidator lakini nilianza kuona mwanga kwa kweli nikawa na withdraw na at least pesa ya kula ikawa sio shida

Matatizo yangu makubwa yalianza 2025 mwezi wa tatu nilikutana na mtu anaitwa noebilion alikua anauza robot linaitwa TINGATINGA ROBOT na alikua analiuza $2500 pia alikua anafanya flipping za $1000 mpaka $100,000 ndani ya wiki 2

Kwa kweli niliona hapa ndipo sehemu naenda kutoboa kwenye haya maisha, nikiangalia maisha yangu yalivyokua na maisha yake lifestyle ya Dubai nilivutiwa mno

Nikamtafuta kuhusu kununua hilo robot linalofanya flipping ili niweze kununua, lakini mimi uwezo wa kupata $2500 yote sikuwa nao kabisa na njia iliyobaki ilikua ni kutafuta namna yoyote ya kupata hio pesa sababu nimeambiwa ndani ya wiki 2 tayari nitakua na pesa nyingi mno

Kwa wakati huo nilikua na kama 3.3M jumla kwenye mpesa na benki na pesa iliyokuwa inatakiwa jumla ya 9.2M hivi ($2500 ya robot na $1000 ya kudeposit kuflip)

Kwa sababu sikuwa na sehemu yoyote ya kupata pesa njia pekee ilikua ni kutafuta sehemu za kukopa na nilikua na ujasiri sababu nilijua baada ya wiki 2 nitaweza kulipa madeni yote

Nilimwambia mama akanichukulia 2.5M kwenye kikundi chao, nyingine nikaazima kwa rafiki zangu na ndugu wengine pia niliuza pia fridge yangu kuongezea kupata pesa yote

Kwa kweli baada ya wiki tatu niliweza kukamilisha pesa yote $3500 ambayo nilijua naenda kubadilisha maisha yangu completely kumbe naenda kuteketeza maisha yangu kwa ujumla

Kwa kweli nilimtafuta jamaa na nikaweza kulipia $2500 na $1000 nikadeposit kwenye akaunti yangu ya FBS

Nakumbuka nilifanya malipo ijumaa jioni na jumamosi akaweza kunifanyia set-up ya bot kwenye PC yangu ambapo jumatatu ilikua tuanze zoezi Zima la flipping kutoa $1000 mpaka $100,000 kwa kutrade XAUUSD tu

Aisee ndani ya siku 2 tu lile robot lilichoma ile $1000 yote 😭😭😭, pesa ambayo ndio ilikua imebeba hatima ya maisha yangu

Nikamtafuta jamaa nikamwambia robot limechoma akaunti yangu na aliniambia kama likichoma basi atanirudishia hela niliyodeposit na pesa ya bot na $500 za usumbufu atanipa ila nilicho ambulia ilikua ni kula BLOCK Instagram na Whatsapp

Mpaka hapo nilihisi kuzimia nikiwaza mama nyumbani ijumaa natakiwa kutuma hela ya rejesho, bado watu wengine nilio wakopa pesa asee kutaka story isiwe ndefu nilifilisika

Nilikua na iphone 14 niliuza,nimeuza kitanda,kabati na vitu vyangu vingi mno kuweza kumaliza madeni lakini mpaka sasa nimemaliza madeni yote ila Sina tena chochote, Sina tena nuru usoni nimechakaa sababu ya njia mbaya niliyochagua ya kupata utajiri

Kwa sasa nachotaka nipate ni nauli tu ya kurudi kwetu Buhigwe sababu huku Dar Sina tena sababu ya kuendelea kuishi, bora nyumbani Kuna mashamba ya urithi nianze kujitafuta upya kwenye kilimo

Kwa sasa kama unataka Kuni-support Kuna hii monitor yangu imebaki naiuza bei ya hasara pitia kwenye huu uzi 👇


Kama Kuna mtu yoyote anaitaka please nipigie simu niwashukuru sana

Mpaka sasa nataka nirudi nyumbani kwetu Buhigwe nikaanze maisha upya niliyopitia hapa Dar yanatosha
Polee naijua vizuri
 
Hawa wajinga wakishafeli baada ya kutapeliwa wanakuja mitandaoni kujiliza ili kupata attention ya kuwahurumia wakati huo wanajiunga walikuwa kimya, hawa ndio wanaichafua trading ionekane scam sababu ya ujinga wao.

Kuna fursa nyingi ktk trading zenye lower risk lakini ni potential vile vile, sasa mtu anapo invest in highly volatility assets bila kuwa na maarifa lazima apigwe aje kutoa vilio humu.

Mimi huwa siwaachi hawa wapuuzi wanaoichafua trading lazima niwashushie nondo wajifunze waache upuuzi
nakuelewa!
 
Change your mindset

Sio betting hiyo kuweni na akili basi, tatizo la hizi shithole countries zilizochelewa kuyajua mabadiliko ya maendeleo ya kitechnolojia zinaishia kuumia kila siku sababu ya kukurupuka wenzio wakiwa wameshaamka.

Forex&Cryptocurrency sio utapeli wala aihusiani na betting, ni vile opportunity hii iliingia bongo bado watu wakiwa ktk mindset ya ujima kwamba, ili ufanikiwe lazima uvuje jasho na kujihusisha na kazi za kutumia nguvu akili kidogo, baada ya watu kuanza kuijua biashara hii kuna wachache waliitumia kama chance ya kuwatapeli wengi wajinga wasioijua.

Tofauti na hivi leo maendeleo ya internet yameleta ufahamu mkubwa wa watu kwa vitu walivyokuwa wakitapeliwa sababu ya ujinga wa kutokuvijua, the same thing utapeli uliokuwa ktk mitandao ya simu, leo hii elimu inatolewa kila mahala mitandaoni, tofauti na miaka 5 iliyopita.

Hivi leo kuna Contents creators kwenye social media wamejaa wakiwaelimisha kuhusu fursa za mitandaoni, trading channels kila mahala kuanzia TikTok, Facebook, Instagram, Whatsapp kote huku kuna walimu wa kutoa maarifa ya hizi opportunities, bila kusahau siku hizi kuna institutes nyingi mijini na nje ya miji zinatoa huduma ya kielimu kuhusu hii biashara, sasa mtu unafeli wapi?.

La mwisho kwa sasa kuna uhuru wa kupata elimu kwa njia rahisi kupitia simu yako yenye internet kupitia searching engines(google,) pia kuna AI zinazotoa maelezo ya kila jambo, je mtu unafeli wapi kupata mwanga wa jambo kabla ya kuanza lawama?.

Kwa kila jambo lazima skills(knowledge+experience) itumike ili upate ufaulu ktk jambo hili, mnaosema forex ni betting hamna tofauti na wale wanaokimbilia biashara/kilimo kisa trending wanayoona kwa wenzao waliofanikiwa/kuwashawishi wakihisi watafanikiwa kama wao.

Hauwezi kufanikiwa over night kwa jambo lolote lile haiwezekani, sasa nyie vilaza kwanini mnataka trading iwatajirishe kirahisi wakati kazi zingine hazitajirishi kirahisi hivi?.

Lack of exposure ndio inasababisha hii nchi tubaki nyuma kwa kila jambo, wenzetu nchi jirani kama Kenya, fursa za mitandaoni zinaboresha maisha ya watu sababu ya raia wao kujielimisha kwa kufuata dunia inataka nini kwa kuendana na technology, sisi tuko bize na siasa za kupigana, simba+yanga, kilimo cha mkono na upuuzi wa kila aina wakati huo fursa za maana zikitupita then baadae zikitufikia tunaita utapeli sababu ya kukurupukia.
Umemaliza kilakitu
 
Forex shikamooo hawa vijana tunawona wanamaisha kupitia forex tuwe makini nao mara nyingi hakuna ukweli juu yao

Kama hukuwahi kupita kwenye madrasa mengi ya forex akili inakuonyesha hela ipo nyeupee ukiingia sasa ndo utajua.

Pole kijana ni kukosea ni kujifunza
 
Forex shikamooo hawa vijana tunawona wanamaisha kupitia forex tuwe makini nao mara nyingi hakuna ukweli juu yao

Kama hukuwahi kupita kwenye madrasa mengi ya forex akili inakuonyesha hela ipo nyeupee ukiingia sasa ndo utajua.

Pole kijana ni kukosea ni kujifunza
Shukrani sana mkuu
 
Back
Top Bottom