Jinsi biashara ya forex ilivyonifilisi na kuniacha na madeni

Jinsi biashara ya forex ilivyonifilisi na kuniacha na madeni

Change your mindset

Sio betting hiyo kuweni na akili basi, tatizo la hizi shithole countries zilizochelewa kuyajua mabadiliko ya maendeleo ya kitechnolojia zinaishia kuumia kila siku sababu ya kukurupuka wenzio wakiwa wameshaamka.

Forex&Cryptocurrency sio utapeli wala aihusiani na betting, ni vile opportunity hii iliingia bongo bado watu wakiwa ktk mindset ya ujima kwamba, ili ufanikiwe lazima uvuje jasho na kujihusisha na kazi za kutumia nguvu akili kidogo, baada ya watu kuanza kuijua biashara hii kuna wachache waliitumia kama chance ya kuwatapeli wengi wajinga wasioijua.

Tofauti na hivi leo maendeleo ya internet yameleta ufahamu mkubwa wa watu kwa vitu walivyokuwa wakitapeliwa sababu ya ujinga wa kutokuvijua, the same thing utapeli uliokuwa ktk mitandao ya simu, leo hii elimu inatolewa kila mahala mitandaoni, tofauti na miaka 5 iliyopita.

Hivi leo kuna Contents creators kwenye social media wamejaa wakiwaelimisha kuhusu fursa za mitandaoni, trading channels kila mahala kuanzia TikTok, Facebook, Instagram, Whatsapp kote huku kuna walimu wa kutoa maarifa ya hizi opportunities, bila kusahau siku hizi kuna institutes nyingi mijini na nje ya miji zinatoa huduma ya kielimu kuhusu hii biashara, sasa mtu unafeli wapi?.

La mwisho kwa sasa kuna uhuru wa kupata elimu kwa njia rahisi kupitia simu yako yenye internet kupitia searching engines(google,) pia kuna AI zinazotoa maelezo ya kila jambo, je mtu unafeli wapi kupata mwanga wa jambo kabla ya kuanza lawama?.

Kwa kila jambo lazima skills(knowledge+experience) itumike ili upate ufaulu ktk jambo hili, mnaosema forex ni betting hamna tofauti na wale wanaokimbilia biashara/kilimo kisa trending wanayoona kwa wenzao waliofanikiwa/kuwashawishi wakihisi watafanikiwa kama wao.

Hauwezi kufanikiwa over night kwa jambo lolote lile haiwezekani, sasa nyie vilaza kwanini mnataka trading iwatajirishe kirahisi wakati kazi zingine hazitajirishi kirahisi hivi?.

Lack of exposure ndio inasababisha hii nchi tubaki nyuma kwa kila jambo, wenzetu nchi jirani kama Kenya, fursa za mitandaoni zinaboresha maisha ya watu sababu ya raia wao kujielimisha kwa kufuata dunia inataka nini kwa kuendana na technology, sisi tuko bize na siasa za kupigana, simba+yanga, kilimo cha mkono na upuuzi wa kila aina wakati huo fursa za maana zikitupita then baadae zikitufikia tunaita utapeli sababu ya kukurupukia.
Acha upotoshaji mkuu
 
Unalipaje mtu akufundishe FOREX na Wakati wewe ni Genius kutoka UDSM

Ukiona unaktiwa fursa jua we ndo fursa

Hiyo forex kwanini hukufanya mwenyewe kutumia P2P au arbitrage method ?

Yaan unaweka kuwa unanua Dollar kwa 2400 ila unauza kwa 2580 simple tu,

Au unauza Tzsh kupata dollars then unauza in Ug sh!

BINANCE AND KU COIN NIMECHEZA NAZO SANA HAKUNA MTU KAWAI NIFUNDISHA
UPati faida
 
Habari zenu wana jamvi,

Nimependa leo niweze kushare hapa changamoto ninayopitia ambayo imenifanya nipoteze Kila kitu kwenye maisha yangu kupitia hii biashara ya forex

Mimi ni mhitimu kutoka UDSM chuo ambacho kina magenius wengi sana na ma TO wengi sana wamemaliza hapo

Biashara ya forex niliifahamu mwaka 2022 wakati naingia mwaka wa kwanza chuoni hapo na niliifahamu Kuna mtanzania mmoja maarufu sana (aliwahi kua na brokerage yake) alikua na mkutano hapo chuoni kuhusu maswala ya fedha na biashara

Na ndipo nilipo fahamu kwa mara ya kwanza kabisa kuhusu hii biashara inayoitwa forex

Tangu mwaka huo 2022 niliwahi kulipia forex kujifunza kwake lakini sikuzingatia sana sababu bado chuo kilikua kinanibana hivyo nilielewa juu juu tu

Mwaka 2023 mwezi wa 7 ndipo nilianza kuichukulia biashara ya forex serious hapa nililipia darasa kwa wasouth Africa wanaitwa FX GOAT walikua na course yao ya $75

Kwa kweli safari ya kujifunza imekua ngumu sana toka 2023 mpaka leo niseme nimepotesa pesa nyingi sana hapa namaanisha maboom,hela za intern pia nilikua winga wa simu hivyo zile ganji ganji nilikua nazitumia kudeposit na kulipia training tofauti tofauti

Kwa hapa Tanzania nimesoma kwa watu wengi kama Jeff,pipstorm,TraderMT na liquidator lakini nilianza kuona mwanga kwa kweli nikawa na withdraw na at least pesa ya kula ikawa sio shida

Matatizo yangu makubwa yalianza 2025 mwezi wa tatu nilikutana na mtu anaitwa noebilion alikua anauza robot linaitwa TINGATINGA ROBOT na alikua analiuza $2500 pia alikua anafanya flipping za $1000 mpaka $100,000 ndani ya wiki 2

Kwa kweli niliona hapa ndipo sehemu naenda kutoboa kwenye haya maisha, nikiangalia maisha yangu yalivyokua na maisha yake lifestyle ya Dubai nilivutiwa mno

Nikamtafuta kuhusu kununua hilo robot linalofanya flipping ili niweze kununua, lakini mimi uwezo wa kupata $2500 yote sikuwa nao kabisa na njia iliyobaki ilikua ni kutafuta namna yoyote ya kupata hio pesa sababu nimeambiwa ndani ya wiki 2 tayari nitakua na pesa nyingi mno

Kwa wakati huo nilikua na kama 3.3M jumla kwenye mpesa na benki na pesa iliyokuwa inatakiwa jumla ya 9.2M hivi ($2500 ya robot na $1000 ya kudeposit kuflip)

Kwa sababu sikuwa na sehemu yoyote ya kupata pesa njia pekee ilikua ni kutafuta sehemu za kukopa na nilikua na ujasiri sababu nilijua baada ya wiki 2 nitaweza kulipa madeni yote

Nilimwambia mama akanichukulia 2.5M kwenye kikundi chao, nyingine nikaazima kwa rafiki zangu na ndugu wengine pia niliuza pia fridge yangu kuongezea kupata pesa yote

Kwa kweli baada ya wiki tatu niliweza kukamilisha pesa yote $3500 ambayo nilijua naenda kubadilisha maisha yangu completely kumbe naenda kuteketeza maisha yangu kwa ujumla

Kwa kweli nilimtafuta jamaa na nikaweza kulipia $2500 na $1000 nikadeposit kwenye akaunti yangu ya FBS

Nakumbuka nilifanya malipo ijumaa jioni na jumamosi akaweza kunifanyia set-up ya bot kwenye PC yangu ambapo jumatatu ilikua tuanze zoezi Zima la flipping kutoa $1000 mpaka $100,000 kwa kutrade XAUUSD tu

Aisee ndani ya siku 2 tu lile robot lilichoma ile $1000 yote 😭😭😭, pesa ambayo ndio ilikua imebeba hatima ya maisha yangu

Nikamtafuta jamaa nikamwambia robot limechoma akaunti yangu na aliniambia kama likichoma basi atanirudishia hela niliyodeposit na pesa ya bot na $500 za usumbufu atanipa ila nilicho ambulia ilikua ni kula BLOCK Instagram na Whatsapp

Mpaka hapo nilihisi kuzimia nikiwaza mama nyumbani ijumaa natakiwa kutuma hela ya rejesho, bado watu wengine nilio wakopa pesa asee kutaka story isiwe ndefu nilifilisika

Nilikua na iphone 14 niliuza,nimeuza kitanda,kabati na vitu vyangu vingi mno kuweza kumaliza madeni lakini mpaka sasa nimemaliza madeni yote ila Sina tena chochote, Sina tena nuru usoni nimechakaa sababu ya njia mbaya niliyochagua ya kupata utajiri

Kwa sasa nachotaka nipate ni nauli tu ya kurudi kwetu Buhigwe sababu huku Dar Sina tena sababu ya kuendelea kuishi, bora nyumbani Kuna mashamba ya urithi nianze kujitafuta upya kwenye kilimo

Kwa sasa kama unataka Kuni-support Kuna hii monitor yangu imebaki naiuza bei ya hasara pitia kwenye huu uzi 👇


Kama Kuna mtu yoyote anaitaka please nipigie simu niwashukuru sana

Mpaka sasa nataka nirudi nyumbani kwetu Buhigwe nikaanze maisha upya niliyopitia hapa Dar yanatosha
mbona umekata tamaa mapema sana?
 
pole sana mkuu, stori yako nmeisoma vema ila pattern nlyoinotice kwako hauna utulivu na subira, unaendeshwa sana na greedy, haukuimasta part ya emotion na ndo basic ya fx iko hapo, hz technical na fundamental ni mantiki, hata huko shamba unakotaka kukumblia ukikosa utulivu na subra utapakimbia, sema mi ni autodidact(nmejfundsha mwnywe) nliacha coz ya mtaji mdg ila ck ntarud kwny game.

Hata kwenye maisha ya kawaida ukikosa Utulivu na Subra . Na pia ukawa na tamaa ya kupata hela nying kwa haraka na wakat mmoja. Basi utapotea mazima.

Mipango iwepo.
hela za mtandaoni inahitaj uwe na utulivu sana kuzila. Na usiendekeze tamaa. Na pia iwe ni side hustle.

Sio uzitegemee moja kwa moja.
 
Change your mindset

Sio betting hiyo kuweni na akili basi, tatizo la hizi shithole countries zilizochelewa kuyajua mabadiliko ya maendeleo ya kitechnolojia zinaishia kuumia kila siku sababu ya kukurupuka wenzio wakiwa wameshaamka.

Forex&Cryptocurrency sio utapeli wala aihusiani na betting, ni vile opportunity hii iliingia bongo bado watu wakiwa ktk mindset ya ujima kwamba, ili ufanikiwe lazima uvuje jasho na kujihusisha na kazi za kutumia nguvu akili kidogo, baada ya watu kuanza kuijua biashara hii kuna wachache waliitumia kama chance ya kuwatapeli wengi wajinga wasioijua.

Tofauti na hivi leo maendeleo ya internet yameleta ufahamu mkubwa wa watu kwa vitu walivyokuwa wakitapeliwa sababu ya ujinga wa kutokuvijua, the same thing utapeli uliokuwa ktk mitandao ya simu, leo hii elimu inatolewa kila mahala mitandaoni, tofauti na miaka 5 iliyopita.

Hivi leo kuna Contents creators kwenye social media wamejaa wakiwaelimisha kuhusu fursa za mitandaoni, trading channels kila mahala kuanzia TikTok, Facebook, Instagram, Whatsapp kote huku kuna walimu wa kutoa maarifa ya hizi opportunities, bila kusahau siku hizi kuna institutes nyingi mijini na nje ya miji zinatoa huduma ya kielimu kuhusu hii biashara, sasa mtu unafeli wapi?.

La mwisho kwa sasa kuna uhuru wa kupata elimu kwa njia rahisi kupitia simu yako yenye internet kupitia searching engines(google,) pia kuna AI zinazotoa maelezo ya kila jambo, je mtu unafeli wapi kupata mwanga wa jambo kabla ya kuanza lawama?.

Kwa kila jambo lazima skills(knowledge+experience) itumike ili upate ufaulu ktk jambo hili, mnaosema forex ni betting hamna tofauti na wale wanaokimbilia biashara/kilimo kisa trending wanayoona kwa wenzao waliofanikiwa/kuwashawishi wakihisi watafanikiwa kama wao.

Hauwezi kufanikiwa over night kwa jambo lolote lile haiwezekani, sasa nyie vilaza kwanini mnataka trading iwatajirishe kirahisi wakati kazi zingine hazitajirishi kirahisi hivi?.

Lack of exposure ndio inasababisha hii nchi tubaki nyuma kwa kila jambo, wenzetu nchi jirani kama Kenya, fursa za mitandaoni zinaboresha maisha ya watu sababu ya raia wao kujielimisha kwa kufuata dunia inataka nini kwa kuendana na technology, sisi tuko bize na siasa za kupigana, simba+yanga, kilimo cha mkono na upuuzi wa kila aina wakati huo fursa za maana zikitupita then baadae zikitufikia tunaita utapeli sababu ya kukurupukia.

Mkuu, anzisha course uwape vijana shule ya kudanlodi hela wakijichanganya wabamize.
 
  • President Donald Trump made 327 stock purchases on April 8, 2025, according to a CNBC analysis of newly released financial disclosures, as markets reeled from his sweeping “liberation day” tariff plan.
  • The next day, Trump posted that it was a “GREAT TIME TO BUY!!!” before announcing a partial tariff retreat that helped send the S&P 500 up roughly 9.5% in one of its best days on record.
  • Trump’s April 8 buying spree focused heavily on mega-cap tech stocks, including Apple, Alphabet, Amazon, Microsoft and Nvidia, which rebounded sharply after his tariff reversal.
 
Hata kwenye maisha ya kawaida ukikosa Utulivu na Subra . Na pia ukawa na tamaa ya kupata hela nying kwa haraka na wakat mmoja. Basi utapotea mazima.

Mipango iwepo.
hela za mtandaoni inahitaj uwe na utulivu sana kuzila. Na usiendekeze tamaa. Na pia iwe ni side hustle.

Sio uzitegemee moja kwa moja.
Tunajifunza kupitia makosa mkuu
 
Uzuri wa forex kila ujinga/kosa unaofanya unalipia kwa CASH no discussion. Unakula za uso mpaka ujifunze kutumia akili. Fx haitaki tamaa na mihemko.
 
Pole sana...lingekuwa hilo robot linaweza kutengeneza pesa zote yeye mwenye robot lake asingeliuza angelitumia tu...Anywa songa mbele litapita tu hilo rudisha nuru
 
Pole sana...lingekuwa hilo robot linaweza kutengeneza pesa zote yeye mwenye robot lake asingeliuza angelitumia tu...Anywa songa mbele litapita tu hilo rudisha nuru
Asante sana ila mwenyewe nimejifunza mtu ukiwa unakalibia kitapeliwa huwezi kushaurika, nimejifunza sana 🙌
 
Back
Top Bottom