Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 27

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

Na wakati niko kwa gari nilikuwa mtu mwenye furaha sana na kama nilikuwa nimepata Nguvu mpya na nikajisemea pale “When one door closes another opens.”

CONTINUE….

Niliamua kumpa Iryn alichokuwa anataka na nilijua kwa maamuzi aliyofanya alitumia sana hisia na sio akili. Nilijua Iryn alikuwa ananipenda toka muda mrefu ila alikuwa anahide hisia zake kwangu. Na kile kitendo cha yeye kutambua nina mke na mtoto ndo kilimuumiza zaidi nikama nilimpiga na kitu kizito sana kichwani.

Ukweli ni kwamba baada ya lile tukio nilijiona kama nimetoa mzigo mwilini kwani sikuwa tena na kinyongo wala wasiwasi wowote na palepale niliamua kufuta namba yake ya simu.

Muda ule nikiwa bado pale nje getini nilitoa ile bahasha alokuwa amenipa ili nijue kiasi cha pesa ambacho alikuwa ameweka na ilikuwa milioni 2 cash.

“Hapa nimepata hela ya kodi tayari na ile pesa aliyonipa Mzee milion 3 nitaweka kwaajili ya kuongezea pesa ya kununua Bajaji”

Sasa angalia jinsi ambavyo Pesa ilikwisha kimasihara hapo na kama utani vile, kwani muda huo nilibakiwa na laki 3 tu kama balance afu gari ilikuwa bado inadai service hapo.

Nilitoka Kijitonyama na nikaamua kurudi zangu home muda ule na nilifika mapema sana, nikawa nacheza na Junior na kipindi hiki nilikuwa namfundisha kutembea.

Katika vitu ambavyo navipa kipaumbele katika maisha yangu bhasi ni pamoja na Familia zangu zote, ya kwangu na ile ya nyumbani. Unaweza kufikiri kama nilikuwa mbali sana na Mama Junior ila ni vile sijataka kumuhusisha sana na hii story.

•••••

Asubuhi Mzee Pama alinipigia simu akanambia jioni tuonane kuna mambo mengine muhimu inabidi tuongee, na tulikubaliana tuonane palepale Budget Bahari Beach. Mzee Pama alikuwaga anapapenda sana hapa na mazungumzo na mipango yetu mingi tumeifanyia hapa.

Kwa upande mwingine ilikuwa inakwenda week bila mawasiliano na Mrembo Prisca. Mara ya mwisho kuongea ni siku ile Jumatatu ya Pasaka ambapo tulizinguana. Prisca aliamua kuniblock mazima mpaka Whatsapp na mimi sikutaka kuhangaika naye maana niliona ni utoto anafanya.

Hii siku niliamua kumpigia simu Mary maana naye toka lile sakata la Kidimbwi litokee sikuwai wasiliana naye tena. Nilipiga namba yake na ikaita bila kupokea, lakini baada ya dakika 2 alinirudia na nikapokea simu yake.

MIMI: “Mary mambo.”

MARY: “Safi shemeji yangu Unaendeleaje?”

Nilishangaa sana muda ule kusikia Mary akiniita shemeji

MIMI: “Safi sana Shem wangu mzuri, vipi hujapenda mimi kuwa shem wako?”

MARY: “No Insider I love you guys.”

MIMI: “Hayo ndo maneno, nimekupigia ili nikusalimie maana umenichunia mpaka naogopa.”

MARY: “Hahahahaa hamna Insider sema nilikuwa na test ndomana.”

MIMI: “Na vipi kuhusu lile deal maana huchelewi kumpa kazi mtu mwingine.”

MARY: “Insider nitakwambia usijali siwezi kukupiga chini.”

MIMI: “Sounds great weekend hii nitakutoa out upo tayari?”

MARY: “Yeah I’m ready why not?”

Tuliagana na Mary na alionekana kufurahi sana kumpigia simu. Pia sikutaka kukaa naye mbali maana kila kitu alikuwa anajua tayari hivyo sikuona sababu ya kumkataa maana alikuwa ni mteja wangu muhimu.

Jioni ilinikutia kwa Maggy maana hii siku nilikuwa nimefanya naye kazi siku nzima na baada ya kumaliza mizunguko nilimpeleka pale kwake. Na muda huu ilikuwa jioni tayari saa 12 hivyo nikaona ndo muda muhafaka wa kwenda kuonana na Mzee.

Wakati nataka kumpigia Mzee simu na yeye alikuwa akipiga na alisema tuonane mida ya saa moja, yeye yuko home soon ataanza safari ya kuelekea eneo la tukio.

Nilimuaga Maggy baada ya kunipa malipo yangu na nikaondoka kuelekea Bahari Beach “Budget”.

Nilitumia kama saa moja kufika eneo la tukio na niliikuta gari yake iko parking “BMW X5”, Mzee alikuwa kafika tayari.

Nilikwenda moja kwa moja alikokuwa amekaa, tukasalimiana pale na nikaagiza Heineken mbili na mishikaki.

MZEE: “Kijana unatumiaga hizi kumbe.”

MIMI: “Mzee natumiaga siku moja moja”

MZEE: “Ndo inavyotakiwa, sehemu zako za starehe ni wapi?”

MIMI: “Inategemea ila napenda sana kwenda Samaki samaki.”

MZEE: “Itabidi siku twende wote namimi nikashangae huko.”

MIMI: “Hahahaaa haina shida mzee wewe tu ukiwa tayari tunakwenda.”

MZEE: “Au hutaki kuongozana na Wazee? sema bwana, maana nyinyi vijana mna mambo sana.”

MIMI: “Hahahaha hamna, mbona kuna wazee wengi sana pale afu wewe unaonekana Mjanja.”

Na kipindi hiki Mzee Pama alikuwa hajui kama nina mke na mtoto, maana hakuwai uliza kuhusu maisha yangu.

MZEE: “Sasa nimekuita hapa kuna mambo tuzungumze kama uanvyojua haya mambo nafanya kwa siri sana. Nataka tufanye manunuzi ya fanicha na vitu vingine vya ndani kwenye ile nyumba, nataka wife anavyoingia akute kila kitu kimekamilika.”

MIMI: “Sawa Mzee haina shida mimi nakusikiliza unipe mpango mzima.”

MZEE: “Fanicha tutakwenda wote jumamosi kuangalia madukani na mambo mengine ila nataka uandae logistics na mafundi wa kuweka sawa.”

MIMI: “Hilo ni jambo dogo Mzee halina shida

MZEE: “Ahsante sana kijana.”

Tuliongea pia mambo mengi sana mengine ni siri siwezi kuyaandika, na baada ya hapo tuuliagana na Mzee pale kwa miadi ya kuonana tena jumamosi na pia alisema hii siku tutakwenda Samaki samaki.

Nilirudi home muda ule na nilimkuta Mama J akiwa na furaha sana huu usiku tofauti na siku zingine, ila furaha ya leo ilikuwa kubwa sana kwake.

“Swahiba mbona leo unafuraha sana kulikoni?”

Na muda huu wife alichukua simu yake iliyokuwa mezani na akanionesha ujumbe uliotumwa na CRDB bank.

Naam, ujumbe ulikuwa unasomeka ni kiasi cha pesa kimeingizwa kwenye account yake na kiasi kilichoingizwa ni 5,000,000/=. Na hapo ndo nikajua Mzee wake ndo aliyetuma ile pesa.

“Mzee ndo ametisha bila shaka.”

“Sasa nikupe hizi Pesa afu ukampe yule malaya wako.”

Muda uleule niliwasiliana na baadhi ya watu wangu wa Kariakoo na nikapata moja ya wauzaji wakubwa wa bajaji na akanambia TVS atanifanyia million 7.

Wife pia aliomba ile Bajaj tumpe mtoto wa shangazi yake aiendeshe kwani hana shida na anamuamini sana.

“Wife ukianza kuweka ndugu huoni kama watatusumbua?”

“Baba J hana shida namjua, wewe ndo utamsimamia sitoingilia makubaliano yenu, dada alishawai kumpa bodaboda na alikuwa analeta hesabu vizuri kabisa.”

“Sawa haina shida mwambie kesho aje tuonane ikiwezekana twende wote dukani.”

Asubuhi dogo alifika mapema na mimi nilikuwa bado nimelala. Tuliongea na dogo na nilikuwa nikimpiga maswali mengi sana muda ule.

MIMI: “Dogo Nambie experience yako ya hizi biashara”

DOGO: “Bro mimi nimeendesha sana bodaboda na nimeendesha mpaka ya dada yake Mama J. Niliamua kuachana na bodaboda sababu nilinusurika na kifo kaka ni Mungu tu aliniokoa tu.”

Na muda huu alikuwa akinionesha kovu kwenye mguu wake wa kushoto.

MIMI: “Aisee pole sana, na bodaboda kwa siku ulikuwa unaingiza kiasi gani?”

DOGO: “Bro ilikiwa inategemea kama nimechelewa kuamka siwezi kosa 25,000/= nilikuaa na uwezo wa kuingiza hadi 70,000 kwa siku hasa kwa wekend. Bro mimi sikufichi kitu pesa zipo sana inategemea na unavyojuana na wateja mimi nawateja wengi sana kama nitapata bajaji nitaingiza Pesa nyingi.”

MIMI: “Na nikikupa Bajaji utaweza ingiza kiasi gani kwa siku?”

DOGO: “Kaka naamini nitaingiza Pesa mingi sana siwezi kosa 40,000 kwa siku kama biashara itakuwa mbaya.”

MIMI: “Sasa mimi nataka kusajili Uber na Bolt maana kwasasa ndo kuna hela huko, pia utakuwa unafanya na kazi zako za pembeni.”

DOGO: “Bro! mimi sina shida account ya Bolt ninayo hata hivyo ila Uber ndo sina.”

MIMI: “Upo vizuri, sasa Uber nitakusaidia kuipata, ila mimi nataka kwa siku 25,000/= kama utapata laki, milioni juu yako ila mimi nataka kwa siku hiko kiasi. Kama utalipa kwa siku au wiki ni juu yako.”

DOGO: “Kwa week itakua vizuri zaidi, hata nikipata ya mwezi mimi nitakuwa nalipa kabisa.”

MIMI: “Sawa mimi sinaga mambo ya undugu kwenye kazi nitakupa mkataba na nataka uandae barua ya serikali ya mtaa na barua za wadhamini wa3 na kopi ya kitambulisho chako bila kusahau leseni yako. Na hakikisha moja ya wadhamini wako awe mwanafamilia.”

DOGO: “Bro haina shida hilo ni suala dogo sana naomba uniamini, dada (Mama Junior) namuheshimu sana siwezi kufanya jambo lolote baya.”

Dogo alionekana kuwa na mzuka sana na lile deal ni kama alikuwa haamini amini hivi, na nilijua dogo atakuwa alikuwa anapiga sana hela na bodaboda na alikuwa mjanja pia.

Na baada ya maongezi ilinichukua dakika 20 kujiandaa na kuondoka home kuelekea Kariakoo nikiwa na dogo.

********

Jumamosi ndo siku ambayo nilikuwa namiadi na Mzee na tulionana asubuhi saa 2 kule Mbweni.

Hatukukaa muda sana pale na tuliondoka na gari ya Mzee na dereva nikiwa mimi. Hii ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza naendesha BMW X5.

Tulizunguka maduka mengi sana hii siku lakini tulikuja kuishia GSM Mikocheni. Mzee alizipenda fanicha za hapa na alinunua fanicha za seblen, vyumbani na Dining. Uzuri ni kwamba tulipewa na wataalam wa kuziweka kule kwenye nyumba pamoja na logistic.

Pia tulinunua home appliances zote muhimu za nyumba, tuseme mzee alitoboka sana hii na wala hakuonesha kujali.

Mpaka kufika saa11 jioni kila kitu kilikuwa kimekaa sawa kwenye ile nyumba na ilibaki mtu kuhamia tu, maana nyumba ilikuwa imewaka na imependeza sana.

Tuliondoka Mbweni na break ilikuwa Budget pale Bahari Beach, tulipumzika hapa kwa masaa kadhaa na tulipata chakula, hii siku hata mchana hatukula na Mzee maana tulikuwa busy sana. Na Mzee alikuwa ametokea kunikubali na kuniamini sana kwa kipindi kifupi tu.

MZEE: “Kijana kuna jambo hapa nataka nione ushauri wako.”

MIMI: “Jambo gani Mzee.”

MZEE: “Nataka kununua gari kwaajili ya wife ila bado nafikiri nimnunulie gari ipi.”

MIMI: “Bajeti umeandaa kiasi gani kwaajili ya gari?”

MZEE: “Budget sio shida ila nilipenda kumnunulia Harrier New Model “Macho Panzi”.

MIMI: “Ni gari nzuri, unanunua hapahapa au unaagiza?

MZEE: “Nitanunua hapahapa nina supplier nao waamini gari zangu zote nanunua kwao”

MIMI: “Kama hivyo sawa maana hizi yard sikuhz wanapika sana magari.”

MZEE: “Upo sahihi ila nitaomba unisaidie kumfundisha kuendesha gari naamini wewe unashinda sana barabarani upo vizuri.”

MIMI: “Hilo halina shida Mzee ila ushauri wangu angeanzia Driving school kwanza afu mimi nifanye kumrekebisha na vitu vidogo.”

MZEE: “Wazo lako zuri sana, bhasi angalia Driving school gani nzuri itamfaa afu tumpeleke.”

MIMI: “Niachie hili nitalifanyia kazi na ulisema ni mjamzito, mimba yake ina umri gani?”

MZEE: “Mwezi huu kafunga 3 tayari.”

MIMI: “Bhasi ni ndogo pia kujifunza kuendesha gari itakuwa ni kama moja ya mazoezi ya viungo. Lakini Mzee mimi nilikuwa nataka nikupe ushauri kama hutojali ila samahani.”

MZEE: “Bila samahani wewe endelea.”

MIMI: “Wife bado hana experince na gari wala hajui kuendesha, huoni kumnunulia hio Harrier ya gharama kama itakucost sana?, kwanini usimnunulie gari ya kawaida kipindi hiki ili aendelee kujifunza na kumasta taratibu, baada ya hata miezi 6 ukiona yuko sawa unamnunulia hio gari sasa.”

MZEE: “Ushauri wako mzuri sana kwa hili hata sikufikiri kabisa.”

MIMI: “Yeye bado ni lena kumnunulia hiyo Harrier utaishia kwenda garage kila siku, bora aanze na gari ndogo ya kawaida hata aikiigonga gonga inakuwa haina shida sana.”

MZEE: “Tufanye hivyo unafikir gari gani ndogo itamfaa?”

MIMI: “Kuna Ist kama yangu na Dualis nafikiri kwa hizi zitamfaa maana hata bei hazitofautiani sana.”

MZEE: “Mimi nafikiri tumchukulie Dualis kidogo kubwa.”

MIMI: “Hiyo nayo nzuri tu.”

MZEE: “Kijana Ahsante sana kwa ushauri wako ndomana niliona nikushirikishe hili jambo.”

MIMI: “Usiwe na wasiwasi Mzee vipi nayeye atahamia lini?”

MZEE: “By next week atahamia, lazima nikupigie simu ili unisaidie kwa hili pia.”

MIMI: “Anytime nipigie.”

Tuliongea mambo mengi sana pale na Mzee tukiwa pale, sababu hii siku Mzee alitaka twende Samaki samaki, niliamua kumpigia simu Mary na kumpanga kama angeweza kutoka nili-muahidi. Baada ya kuwasiliana naye alikubali na nilimwambia nitampitia pale kwa Zena.

Saa 1 usiku ndo tulitoka pale Budget na uelekeo wetu ulikuwa Masaki. Nilimpasha habari Mzee kwamba kuna mtu nitamchukua tunaenda naye huko wala hakuwa na pingamizi.

“Tena utakuwa umefanya vizuri maana mimi nitakuacha huko si unajua leo sijashinda home kabisa, itabidi niwai kurudi leo.”

Nilimpick Mary pale kwa Zena na alikuwa kapendeza sana ni kama alikuwa anataka nipagawe sijui. Nilimwona Mzee akimwangalia Mary kwa macho ya kifisi wakati akivuka barabara kuja upande wetu.

Mary aliingia na akakaa siti za nyuma na muda ule ule nilimtambulisha kwa Mzee kama girlfriend wangu na wakasalimiana. Upande mwingine Mary kama hakuamini kuona nikidrive ile BMW afu ilikuwa new Model. Na the way ambavyo tulikuwa na Mzee tukiongea unawaza kufikiri ni mtu na kijana wake.

Break ya gari ilikuwa pale Samakisamaki na tuliingia ndani, na muda huu hapakuwa na watu sana hivyo tulikwenda kukaa upande wa juu ghorofani (mimi napaitaga VIP, ukikaa kule juu unaona kila kitu kinachoendelea mle ndani).

Tuliagiza vinywaji na story zikiendelea kutawala kwenye ile meza yetu.

Saa 4 Mzee aliaga anaondoka hivyo tuliongozana mpaka parking na alinipa laki 8 ambapo laki 5 zilikuwa zangu na laki3 alisema nitalipia bill ya vinywaji. Alindoka maeneo yale na akanipa ahadi ya kunitafuta tena kwaajili ya ununuzi wa gari ya mchepuko wake.

Nilirudi ndani na tuliendelea kunywa na Mary pale na muda huo alikuwa akiniangalia huku akitabasamu.

MIMI: “Mbona unatabasamu umefurahi nini?”

MARY: “Insider yule ni Mzee wako?”

MIMI: “Hapana ni mshikaji wangu tu.”

MARY: “Kweli washikaji mmekutana na mnaendana, nilijua ni Mzee wako.”

MIMI: “Leo umependeza sana muda ule nilishindwa kukupa pongezi ila leo umewaka sana.”

MARY: “Mmmh thank you shem wangu.”

MIMI: “Umeridhika lakini mimi kuwa shemu wako?”

MARY: “Yeah Insider I’m happy for you guys, kwanini sasa mlikuwa mnaficha?”

MIMI: “Prisca ndo alikuficha, mimi nisingeweza kukwambia wakati mdogo wako hajakwambia. Ila naweza kuwa-oa wote kama mtakubaliana, mimi sina shida.”

MARY: “Hahahaa Insider bhana, mimi nishare Mwanaume na mdogo wangu?”

MIMI: “Ndio kwani haiwezekani?”

MARY: “Impossible can’t do that.”

Na muda huu simu ya Mary ilikuwa inaita akanionesha kucheki alikuwa Prisca anapiga.

“Ona mke wako ananipigia atakuwa anataka kujua nilipo”

MIMI: “Kwani hukuaga?”

MARY: “Atakuwa anahisi niko na wewe maana muda ule wakati ukipiga simu, yeye ndo aliyeniletea simu chumbani.“

MIMI: “Mpokelee usikie anasema nini au mtext back chap.”

MARY: “Nimemtext tayari ila ona sasa anauliza niko wapi na nani?”

MIMI: “Mwambie uko na mimi sababu hakuna kibaya tunachofanya hapa.”

MARY: “Mmh sawa”

Tulipiga story sana muda huu na Mary alionekana mtu mzima hata mazungumzo yake tofauti na Prisca mwenye utoto mwingi.

Hatukukaa sana pale saa6 tuliondoka maeneo yale, gari nilikuwa nimeacha kule Mbweni hivyo ilibidi nifanye kurequest Uber na mimi.

Jamaa alikuja kutuchukua na safari ikaanza, lengo langu ilikuwa nianze kumdrop Mary pale kwao afu sisi tungeendelea na safari mpaka Mbweni, njia ilikuwa ndo hiyohiyo moja.

MARY: “Insider unakwenda Mbweni?”

MIMI: “Ndio ila nitaanza kukuacha wewe home.”

MARY: “Usiku huu kuna nini?”

MIMI: “Niliacha gari kule ndo nalifwata afu narudi home.”

MARY: “Bhasi tunakwenda wote.”

MIMI: “Sawa haina shida.”

Na muda huu tulikuwa tumekaa siti za nyuma na Mary alionekana kuchoka sana, bhasi akajilaza kwenye mapaja yangu bila wasiwasi wowote.

Tuliwasili Mbweni na nikafungua geti kuingia ndani maana funguo nilikuwa nazo. Mary muda huu alikuwa akishangaa sana na alikuwa makini sana kuitizama ile nyumba. Hii nyumba ilikuwa imefungwa taa nzuri sana nje na ndanu na usiku ilikuwa inawaka taa za kuvutia sana. Wakati tumeingia ndani nilikwenda washroom na kumuacha Mary seblen.

Nilivyorudi seblen Mary alikuwa amejilaza kwenye coach na alikuwa amejiachia sana na mambo yote yalikuwa hadharani. Nilikuwa nikayaona maungo yake vizuri sana, nilihisi Mary alikuwa akinifanyia makusudi tu.

EPISODE 28[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 



Uwe unatag raia jamani ☺️
 
Next
 
Mle usirembe broh
 
Oya Mpaka lini tena Asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…