Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 02:
CHAPTER 15

“A TRUE STORY BY INSIDERMAN”

PREVIOUS:
Tulianza safari ya kwenda Zanzibar na Baada ya kuwasili Zanzibar tulikwenda moja kwa moja hotelini kupumzika maana nilikuwa nishafanya booking ya room mapema sana.

CONTINUE:

Hotelini nilikuwa nimefanya booking ya room 2 tofauti kwaajili yangu na Hilda, sikutaka kufanya ujinga wowote Zanzibar.

Baada ya kuwasili hotelini nilikabidhiwa funguo mbili na tulipewa kampani mpaka room zetu. Nilimwambia Hilda tunapumzika kidogo then baadae tutakwenda kuonana na dada agent ili atupe Abc ya kinachoendelea.

Baada ya kuingia room yangu kitu cha kwanza kabisa nilimpigia simu wife kumpa taarifa kuwa nimefika salama. Na baada ya kuongea na wife nilimpigia simu Iryn kumpa taarifa niko Zanzibar tayari.

Jioni niliwasiliana na Agent ili tuonane na akasema anakuja hotelini niliko ili tuongee vizuri.

Ilimchukua dakika 20 kuwasili pale hotelini na tulitafuta sehemu nzuri ya kukaa pale restaurant ili tufanye mazungumzo. Taarifa alizonipa ni kwamba kila kitu kinakwenda sawa na meli ndo inashusha mzigo na kufikia kesho ambayo ni jumamosi, mzigo utakuwa umewasili Dar. Kuna balance ya pesa nilitakiwa kumpa na nilimkabidhi kisha tukaagana na alisema tunaweza tusionane tena mpaka Dar.

Ukweli toka Iryn abebe mimba yangu nilikuwa niko makini sana kwenye usimamizi wa biashara na sikutaka kuona anapigwa pesa kizembe, na nilijitahidi sana kudhibiti matumizi ya ofisi kwa kiasi kikubwa. Sehemu ambayo sikutaka kuingilia ni upande wa sales maana huku wengi ndo walikuwa wanapatia hela.

Saa 1 usiku nilimgongea mlango Hilda ili tukapate chakula cha jioni palepale hotelini. Hilda alionekana bado kuwa na usingizi, ila alitoka tukaenda kula dinna.

Tuliagiza chakula na wakati tunakula tulikuwa tunapiga story nyingi sana,

HILDA: “Bossy nikuulize kitu?”

MIMI: “Niulize bossy wangu.”

HILDA: “Ulitumia mbinu gani kumpata Iryn?”

MIMI: “Hakuna cha mbinu wala nini ni bahati tu.”

HILDA: “Na anajua una mke na mtoto?”

MIMI: “Yes anajua.”

HILDA: “Insider nyota yako ni kali sana, nawasikiaga wadada pale Salon wanavyo kuongelea, wanakusifia sana.”

MIMI: “Kawaida tu mbona, hata wewe upo vizuri pia.”

HILDA: “Ahsante lakini mimi ni wa kawaida bhana, ulinambia tutakwenda onana na agent imekuaje?”

MIMI: “Tulishaonana na kesho kuna possibility ya kurudi Dar.”

HILDA: “Sawa haina shida.”

Kipindi bado tuko pale restaurant kwa upande mwingine Asmah alikuwa anapiga simu, kutokana na mazingira sikupokea simu zake na alipiga mara 2.

Baada ya kumaliza kula tulirudi room kupumzika, nilikuwa na Hilda room yangu, mimi nilikuwa nachezea laptop na yeye alikuwa kalala kitandani.

Nilianza kupata mawazo ya ngono kichwani maana nilijua Hilda hawezi nikazia kwa haya mazingira. Nilimuangalia na yeye alikuwa busy kuniangalia, macho yake yalionesha anataka something.

Nilifikiri sana nikaona hapa nikifanya ujinga naweza kupoteza vitu vingi kwa tamaa za kijinga, ni bora nitafute siku ya kufanya huu ujinga lakini sio huku Zanzibar.

Muda ulikuwa ni saa 3 za usiku, hivyo nilimwambia Hilda akalale room kwake na kesho asubuhi tutakwenda kutembea kabla ya kuondoka. Hilda aliondoka kwa kunitakia usiku mwema, na aliniomba kama nitawahi kuamka bhasi nimuamshe.

Unajua ni ngumu sana kwa mwanaume rijali kumuacha mrembo kama yule tena kwenye mazingira kama haya. Baada ya Hilda kuondoka, mawazo ya ngono yalipotea kabisa na Asmah alipiga tena simu;

ASMAH: “Wewe na Hilda wote hampokei simu mnashida gani? Na nini kinaendelea huko?”

Nilishangaa sana kuona Asmah akionesha wivu juu yangu;

MIMI: “Tumefika kwa kuchelewa, then mambo yakawa mengi, na ni lini umeanza kuwa na wivu juu yangu?”

ASMAH: “Lazima niwe na maswali why hampokei simu?. Nilitaka kujua maendeleo yako na mmefikia wapi.”

MIMI: “Kila kitu kinakwenda vizuri mummy usiwe na wasiwasi, as long as niko huku hakuna kitakacho haribika.”

ASMAH: “Sawa, ulinambia ukirudi tutaplan kwenda wote Zanzibar au ulikuwa unanidanganya?”

MIMI: “Siwezi kumdanganya mwanamke nayempenda.”

ASMAH: “Okay, I’m in.”

Baada ya kumaliza kuongea na Asmah nilifurahi sana nikajisemea hapa mchezo kwisha na sitochelewesha kwenda naye Zanzibar na huku lazima nimle mpaka hamu iishe.

Haikuchukua hata dakika 5 muda huu simu yangu ilianza kuita tena ni mama kijacho wangu alikuwa anapiga, nilipokea simu yake kwa haraka sana;

IRYN: “Darling za huko Zanzibar na mmefikia wapi?”

MIMI: “Kila kitu kinakwenda freshy mummy, sijui wewe na mwanangu mnaendeleaje?”

IRYN: “Leo nilikuwa clinic, maendeleo ya mtoto ni mazuri, mimba ina miezi 3 tayari.”

MIMI: “I love you guys.”

IRYN: “Baby, nusu saa iliyopita nimeongea na mama mkubwa kuhusu lile jambo nililokwambia. But huwez amini mama amefoka sana kuhusu hii ishu mpaka nimeshangaa, na anasema alihisi kuna kitu hakipo sawa since niende Ethiopia.”

MIMI: “Aisee! Sasa anafokaje wakati wewe ni mtu mzima?”

IRYN: “Ni kweli baby, mimi niko chini ya uangalizi wa mama mkubwa na ndo kama mama yangu. Yeye anasema nilipaswa kupata mimba baada ya kuolewa na sio kiholela kama nilivyofanya, na amechukia sana.”

MIMI: “Sasa mmefikia wapi baby maana nishaanza kupata presha huku.”

IRYN: “Amesema nirudi tena Ethiopia ili tukazungumze hili suala.”

Nilinyamaza kwa sekunde kadhaa hata sikujua najibu nini, na Iryn aliendelea kuongea,

“Baby are you there? Tell me something.”

MIMI: “Mummy hata sijui niseme nini, unakumbuka nilikwambia simuelewi mama mkubwa wako? Naona utabiri unakwenda timia.”

IRYN: “Mama anacho foka ni kupata mimba bila utaratibu na nimekwenda kinyume cha mila na desturi zetu.”

MIMI: “Baby mimi naomba nipromise kuwa huyo mtoto atakuwa salama. Promise me again.”

IRYN: “Baby, I promise nothing is going to harm this child. Like I said before huyu mtoto ni kwaajili yako wewe.”

MIMI: “Sawa mummy na lini unategemea kwenda huko?”

IRYN: “Next week nitapitia Dar kuonana na wewe, then nitaunganisha Ethiopia.”

MIMI: “Sawa baby, I’m waiting for you.”

Moyo wangu ulianza kuumia maana tangu niko Ethiopia niliona kama mama mkubwa wake atakuwa ni tatizo kama atajua hili suala. Niliendelea kuwaza mpaka Iryn ameambiwa aende huko hili jambo sio la kawaida ni kubwa na ukizingatia familia yake wako makini sana kwenye mila na desturi zao.

Sina hela, sina status yoyote hapa nilipo, hivi watakubali binti yao azalishwe tu bila kufunga ndoa?. Niliona ni jambo gumu sana ukizingatia status ya Iryn ni kubwa sana na ndo binti pekee aliyeachwa na mama yake, hawawezi kukubali apotee au awe na mtu ambaye si sahihi. Kwa yale mazingira ya Ethiopia niliyo yashuhudia kwa macho yangu nilisema sitoboi kuna possibility kubwa ya kumkosa mtoto. Kwanza Iryn hana sauti yoyote, just imagine akiwa kwa mama mkubwa wake kama anatoka, lazima aage, yaani anatritiwa kama mtoto. Je ataweza kuongea na akakubalika kwenye familia yake kuhusu mimba aliyobeba?

Mawazo yangu yote yalikuwa ni kwa mtoto wala sio kingine, niliwaza nimempoteza mtoto kwa Prisca na huyu kwa Iryn naweza mpoteza, nisipokuwa makini, ukizingatia mimba bado ndogo. Nilikumbuka maneno ya Jimmy aliyonambia kuwa as long as Iryn ananipenda, hii ndo silaha kubwa kwangu, lakini niliona haimake sense kwangu ni useless.
****
Asubuhi niliamka mapema sana na nilimpigia simu Hilda aanze kujiandaa ili twende Nungwi Beach. Hilda alikuwa kaniomba twende huko akapaone, huwa anaishia kupaona kwa picha na kusimuliwa.

Saa 2 asubuhi tuliondoka pale hotelini na tulitumia kama lisaa na nusu kuwasili maeneo yale, ni kuna ka mwendo karefu kidogo. Nungwi ni beach ambayo inakuwaga na watu wengi sana mpaka watalii, bila kusahau kuna bar na clubs.

Baada ya kuwasili eneo la tukio tulibadilika chap ili kuendana na mazingira ya beach. Kwa upande wake alijichia sana, alijifunga mtandio kiunoni na shepu yake ilikuwa ikionekana vizuri kabisa, afu ndani alikuwa na bikini tu.

Mimi sikuwa na mudi kabisa maana nilifanya kumpa kampani ili afurahie kuja Zanzibar na nilianza kumpiga picha kupitia simu yangu iphone 14 Pro ambayo nilipewa zawadi na Iryn.

Baada ya kumpiga picha alikwenda kuogelea na mimi nilikaa pembeni kwenye bembea nikiendelea kufikiri juu ya Iryn.

Niliwaza kuendelea kufanya kazi chini ya Iryn ni utumwa inabidi nifanye maamuzi magumu ya kuachana na kampuni yake. Kutambulishwa huko kwao kama ni manager wa kampuni yake ni dharau kubwa sana, nitaonekana ni marioo.

Nilikuwa deep sana, kwani nilikuwa nina jiuliza na kujijibu mwenyewe,

Kama watataka nimuoe Iryn nitagoma sitokubali kabisa kwa hili na vipi sasa kuhusu mtoto sindo nitamkosa?. Daah! bladifakeni hapa nikileta mchezo nitakosa vyote, lakini Jimmy alinihakikishia usalama kwa hili.”

Kwa mbali nilimwona Hilda akija usawa wangu na shepu yake ilikuwa imechoreka barabara, michirizi ya maji ilikuwa ikichuruzika kwenye paja zake na alisogea mpaka usawa wangu.

HILDA: “Insider upo sawa kweli? Tangu muda mrefu nakuona una mawazo, ni kitu gani kinakuchanganya akili? Niambie bhasi.”

Hilda alipanda kwenye bembea na tukawa wawili kama wapenzi hivi, na alianza kuchezea mustach,

MIMI: “Kuna jambo linanichanganya akili lakini sio muhimu sana.”

HILDA: “Kuhusu mzigo au jambo lingine?”

MIMI: “Masuala mengine binafsi, niko sawa usijali.”

HILDA: “Sijakuzoea hivi ndomana nimekuja kukuuliza kama kuna shida.”

MIMI: “Ahsante kwa kujali.”

HILDA: “Twende beach kama upo sawa, ukigusa maji ya bahari maybe utakuwa sawa.”

Hilda alinibembeleza nikaamua kwenda naye beach na tukaanza kuswim wote.

Saa 9 mchana tuliondoka kurudi hotelini ili tujiandae na safari ya kurudi Dar. Njiani nilimuomba dereva akimbize sana gari, kwani tulikuwa tunatarajia kuondoka na boti ya saa 16:30 jioni.

Tulipitia hotelini kuchukua mabag yetu na tukaelekea bandarini kwaajili ya kuanza safari, nakumbuka tulichelewa kama dakika 10 hivi, lakini boti ilikuwepo.

Baada ya kuwasili Posta nilimwambia Hilda twende Samakisamaki tukamalizie siku, lakini tunakwenda kwake kuweka mabag na kupumzika kidogo, maana ndo kwanza ilikuwa saa 1 kasoro za usiku.

Kimbembe ilikuwa kwenye kurequest usafiri maana simu zetu hazikuwa na chaji, njia ya haraka ilibidi tuchukue Tax ya kuturudisha.

Baada ya kuwasili kwa Hilda bila kuchelewa niliingia kuoga na nikalala kupunguza uchovu.

Nilishtuka mida ya saa 3 kasoro na Hilda alikuwa bado kalala afu kanizungushia mikono yake kwa nyuma. Mawazo ya ngono yalianza kunijia tena kichwani muda huu, hivyo niliamua kutoka kitandani na kwenda seblen.

Nilicheki simu yangu nikakutana na missed call nyingi tu ikiwemo ya Kizoka, Lucy na Asmah. Nilianza kwanza kumpigia Asmah na alikuwa anauliza kama nimerudi, then nikampigia simu Kizoka na yeye alinipa taarifa kwamba amerudi mjini, tukakubaliana tuonane kesho jumapili.

Nilimwambia Hilda ajiandae ili tuondoke mapema na nilikumbuka kumcheki jamaa yangu Allen ili tuonane maeneo yale anipe na maokoto yangu.

Wakati tuko njiani tukielekea Masaki kwa upande mwingine Iryn alianza kupiga simu na Hilda aliona maana tulikuwa close sana.

Bila kusita nilipokea simu yake,

IRYN: “Darling, hunajipa feedback umefikia wapi?”

MIMI: “Tumekamilisha na tumerudi Dar tayari.”

IRYN: “Wow nice, sikutarajia ungerudi leo Dar, kulikoni?”

MIMI: “Sijaona sababu ya kuendelea kubaki kule wakati kazi imekwisha ni kuchezea pesa za ofisi.”

IRYN: “Hahahaha! Kama manager ninaye, ushafika home?”

MIMI: “Home sijafika bado nitarudi badae kidogo.”

IRYN: “Muda huu bado hujarudi? Una ratiba gani za usiku? Unanipa stress tu.”

MIMI: “Nakwenda Samakisamaki kupoteza muda, then nitarudi home kulala.”

IRYN: “Okay sawa, kesho tutaongea vizuri nenda kaenjoy.”

MIMI: “Sawa mummy kesho nitakucheki mapema.”

Tuliwasili pale Samakisamaki kwa upande mwingine Allen alikuwa kashawasili tayari na baada ya kuingia ndani na kuonana, tuliishia kusalimiana kwa kugonga, na pale mezani alikuwa na dem mmoja. Walikuwa wanakunywa Hennessy na sisi tukaagiza moet na story zingine ziliendelea na alinikabidhi cash yangu mapema, ili akilewa asisahau.

Tulikaa mpaka saa 8 za usiku ndo tuliondoka lakini jamaa tulimuacha na sisi tulifanya kurequest Bolt ya kuturudisha home. Kipindi tuko njiani niliwaza sijui nikalale na Hilda kwake? Maana wife alikuwa hana taarifa kama nimerudi Dar. Nilifikiri sana nikaona hakuna haja, nimevumilia tukiwa Zanzibar nije niharibu mwishoni? Acha nirudi home nikaonane na mama J wangu.

Tulianza kumdrop Hilda Morocco pale kwake na tukaendelea na safari ya kwenda home Mbezi Beach.
***
Kutokana na uchovu nilichelewa sana kuamka na kucheki muda ilikuwa ni saa 5 asubuhi, kwa upande mwingine hapakuwa na mtu yoyote ndani zaidi yangu, nilihisi hawa wamekwenda church.

Baada ya dakika 10 nilipokea simu kutoka kwa Kizoka na aliuliza tunakutana wapi maana anataka kuja mapema ili tuweke mambo sawa, bhasi nikamwambia aje home ili apajue.

Kizoka alikuwa anatokea Kawe, hakuwa mbali sana na kwangu. Ilimchukua nusu saa kufika home na baada ya kuonana tuliishia kusalimiana maana ilikuwa ni kitambo sana hatujaonana.

MIMI: “Karibu sana brother hapa ndo home.”

KIZOKA: “Mzee unaishi kama Paris, kodi unayolipa hapa kwa mwezi mimi ndo mwaka mzima.”

MIMI: “Hahahaha hamna afu kawaida tu.”

KIZOKA: “Familia iko wapi naona pametulia sana.”

MIMI: “Hawa wamekwenda church sio muda watarudi.”

KIZOKA: “Hongera sana kama una mke anayekumbuka kusali, kaka upo kwenye mikono salama.”

MIMI: “Nashukuru Mungu kwa hili. Nilikuwa Zanzibar mara moja na nimerudi jana usiku sana. Nilikutafuta sana ujue ukawa hupatikani mpaka nikaenda kwa dada Madaki shule ndo kunipa namba ya wife wako.”

KIZOKA: “Nakubali sana brother kwa kujali kweli nimeamini wewe ni ndugu. Baada ya kuona mambo hayaeleweki sipati gari, niliamua kwenda shambani kulima.”

MIMI: “Twende ukaione gari kama kuna maboresho ya kufanywa bhasi useme mapema kabla ya kukukabidhi.”

Tulitoka nje kumuonesha gari na yeye aliishia kuisifia sana,

KIZOKA: “Mzee hii gari imesimama naona kila kitu kipo mahala pake, huyu njiwa nitamtunza sana.”

Sikutaka kumwambia Kizoka kuwa gari ni yangu na nilimwambia ni gari ya wife ila mimi ni kama msimamizi tu. Na uzuri usajili wa gari ulikuwa unasoma jina la wife na nilimsisitiza kuilinda gari.

Tulikubaliana nitamkabidhi gari next week ili aanze kazi na mimi nitafute gari ya kutumia.

Kizoka hakutaka kupoteza muda na tuliondoka pale home na mimi mawazo yangu kichwani niende Upanga kwa Asmah.

Tulielekea na usawa wa Mwaikibaki Road na nilimdrop Kizoka pale roundabout ya kwenda Kawe na nikaendelea na safari yangu. Nilikuwa nakwenda kwa Asmah bila kumpa taarifa na nilitaka iwe surprise, nilijesemea kama nitamkuta fresh na nikimkosa fresh pia.

Nilipitia Shoppers ya Mikocheni nikanunua mazaga ya kutosha ya kumpelekea maana nilijua lazima ataulizia zawadi za kutoka Zanzibar.

Baada ya kuwasili pale kwake niligonga mlango na nilishtuka sana kufunguliwa na mtu mwingine ambaye baadae alinitambulisha kuwa ni kama dada yake.

Kwa upande wake alishangaa sana mimi kwenda bila taarifa maana sio kawaida yangu na nilimwambia nimefanya makusudi ili nimfumanie kwani ananidanganya sana kuwa yuko single.

Tulianza kupiga story pale seblen na alionesha kufurahia ujio wangu na kubwa aliuliza safari ya Zanzibar na aliishia kulalamika kwanini sijampa taarifa wakati narudi. Pia alikuwa anahisi maybe kuna something fishy kilikuwa kinaendelea kati yangu na Hilda tukiwa Zanzibar. Nilichofanya nilitoa simu nikamuonesha booking za rooms 2 yenye jina langu na Hilda na hapo akawa na amani.

Dada yake hakukaa sana na aliondoka na sisi tulikwenda jikoni kupika na nilikuwa nikimsaidia kazi kama kusaga nyanya, kukata vitunguu, karoti nknk. Nilikuwa nikimpa viutani vya hapa na pale, nilikuwa namwagia sifa na yeye alikuwa akitabasamu tu.

Ukweli mimi nilikuwa nawaza kumla tu, hata sikuwa na jambo lingine zaidi ya hili maana ndo liliniketa huku Upanga na nilijisemea leo itafahamika. Niliendelea kumshika shika japo mara ya kwanza alikuwa analalamika ila alikuwa mpole, kwani hakuwa na jinsi tena.

Baada ya kumaliza kazi zangu nilirudi seblen na nilikutana na missed call 5 za Iryn, nikakumbuka alisema leo tutaongea na sikumtafuta. Palepale nilimpigia simu na haikuchukua muda akapokea tukaanza maongezi,

IRYN: “Baby, mbona hupokei simu zangu unashida gani?.”

MIMI: “Simu nilisahau kwa gari.”

IRYN: “Na upo wapi?”

MIMI: “Niko Sinza.”

Ilibidi nimdanganye maana sikuwa na jinsi,

IRYN: “Okay naomba uende Masaki Sea cliff hotel, kuna mtu ukaonane nae atakupa mzigo wangu, soon nakutumia namba zake.”

MIMI: “Baby now?”

MIMI: “Yes now, anaondoka na ndege ya saa 10 jioni so ukichelewa utamkosa.”

Niliona Iryn ananikatili na anataka kuharibu mipango yangu kwa Asmah, lakini sasa sikuwa na jinsi ilibidi niwe mpole niende huko Masaki.

Nilimuaga Asmah natoka nakwenda Masaki mara moja then narudi, hata yeye aliuliza kuna nini? Nikakwambia kuna mtu muhimu sana nakwenda onana naye.

Nilitumia muda mfupi kuwasili pale Seacliff hotel na nilikutana na jamaa ambaye hakuwa mgeni kwangu, ni yule ambaye tulikutana naye Johari Rotana hotel, kipindi Iryn anarudi South Africa.

Jamaa alianza kuniuliza maswali ya kejeli na nilimsoma kama anadharau hivi na mimi nilimdharau pia,

JAMAA: “Who are you?”

MIMI: “I think she told you about me. I'm not here to waste my time, so I expect the same from you. Getting to know me is not the business here.”

Jamaa aliniangalia na akanipa bahasha pale,

“What is inside?”

JAMAA: “Just look.”

Nilicheki na nikaona kuna hela zilikuwa ni noti za dollar 100 bunda 5, huyo nikaondoka kurudi parking niliko park gari.

Nilikuwa nimepark gari nje kabisa na bango la Casino na kwa mbali nilimuona Masai mmoja ambaye ni rafiki wa Elias. Mostly wanakuwa pamoja, hata yeye baada ya kuniona alinitambua na akasogea mpaka pale kwenye gari.

Nilimuuliza jamaa kama Elias yupo kwani simu zake zilikuwa hazipatikani na alinambia Elias alikwenda Zanzibar baada ya kufiwa na mtoto wake. Nilisikitika sana baada ya kupewa hizi taarifa na nilimwambia Masai afanye namna yoyote nipate mawasilino yake.

Nilimwachia Masai damu nyekundu na tukaagana, niliingia ndani ya gari na nilifungua bahasha kuhesabu ni kiasi gani kabla ya kuondoka. Baada ya kuhesabu jumla zilikuwa ni $50,000 na nikampigia Iryn ili aconfirm na akasema ziko sawa, kesho nitamuwekea kwenye account yake.

Sikutaka kumuuliza yule jamaa ni nani? Na nilisema nasubiri tena mpaka aniambie mwenyewe maana hii ni mara ya pili nakutana na huyu mpuuzi na amempa $50,000, nilihisi kuna kitu kinaendelea.

Nilimpa taarifa nilizopata juu ya Elias na alisikitika sana, akasema kama nitampata nimjulishe. Saa ilikuwa inaonesha ni 11 za jioni, niliwaza nirudi tena kwa Asmah? Lakini niliamua kurudi zangu home.

Sasa baada ya kurudi home wife alianza kufoka;

Yaani umetoka safari umerudi usiku, badala ya kutulia na familia yako wewe unakwenda kuzurura, naona lecture ya mama haikuingia sawasawa.”

Sikutaka maneno naye nikaenda zangu chumbani, na kwa nyuma Junior alikuwa akinifuata.

Mtoto huyo nyuma anakufuata yaani muda wote anaulizia baba! Afu baba mwenyewe don’t care.”

Haikuzidi dakika 10 wife akaja tena chumbani na muda huu nilikuwa nacheza mieleka na Junior. Alikuwa anaona raha sana jinsi navyomuweka mgongoni na kumtupia kitandani, bhasi hapa alikuwa anafurahi sana na aliupenda mchezo.

Mama J baada ya kuona vile alianza kelele tena,

WIFE: “Hivi una matatatizo gani? Ni michezo gani unacheza na mtoto, naona umemchoka mtoto unataka kumvunja mgongo?.”

MIMI: “Anavunjikaje mgongo? Na hapa tuko kitandani sema unatuonea wivu.”

WIFE: “Una matatizo wewe, naomba uache huo mchezo ili tuongee.”

MIMI: “Unataka tuongee nini? Ushaanza mambo yako unataka kuharibu mood yangu na Junior?.”

Wife alinyamaza kimya na alifungua drow akatoa bahasha aliyonipa Iryn ambayo ndani ilikuwa na vile vitu vya kurudisha kwa Muajemi.

WIFE: “Hivi ni vitu vya Iryn, vinafanya nini kwako?. Na wasiwasi huko Kenya mlikuwa wote, na inaonesha alivisahau kwako.”

MIMI: “Kwahiyo unataka kusema nini?, yaani wewe muda wote unaniwazia mabaya tu. Kuna siku ulishawahi kuniwazia mazuri?.”

WIFE: “Nitaanzaje kukuwazia mazuri wakati mwanaume mwenyewe hueleweki na hii siri unayoificha na Iryn kuna siku nitaijua.”

MIMI: “Akili yako inakutuma kufanya hivo ndomana, hivo vitu aliviacha kipindi kile amekuja Dar na mimi sipo. Aliviacha ofisini ili nimpe Ex wake kwani anamsumbua sababu ya hivo vitu. Na ukitaka chats za huyu mtu wakati nachat nae ninazo kama utataka kuziona na hapo umeshika millions of money.”

Mama J alisogea nikamwonesha zile chats na Muajemi ndo kuridhika.

Leo hii mimi ni mwisho kujitetea kwako, next time ukini accuse kwa lolote mimi nitalipokea na hutoniona nikijitetea maana unashindwa kuniamini.”

Wife alinyamaza kimya na alimchukua Junior akaingia nae bafuni ili kumuogesha.

Asubuhi nilikuwa nina miadi ya kuonana na mama Janeth na alisema niende ofisini kwake. Nilianza kupitia ofisi kwake na uzuri pale getini wananijua hivyo huwa hawanisumbui kabisa. Jamaa wakinionaga utasikia “Kijana wa Mrs Carter” naona umekuja msalimia mama yetu.

Nilikwenda moja kwa moja pale ofisini kwake na baada ya kufika kwa secretary wake alimpigia simu kumpa taarifa nimefika na akasema niingie ofisini.

Mama baada ya kuniona aliacha kazi aliyokuwa anafanya na tukaanza maongezi, kubwa aliuliza habari za Zanzibar na tukaendelea na maongezi mengine.

Mama alinipa taarifa ya kufanya kikao siku ya jumamosi pamoja na team zote za Mikocheni na Masaki kwaajili ya kupeana mikakati mipya ya 2023 na kuwapongeza waliofanya vizuri kwa mwaka uliopita.

MIMI: “Ulifaniiwa kuongea na Iryn?”

MAMA: “Yes, ni masomo yana mkeep busy, na nilimtumia clip na picha za mkesha.”

MIMI: “Iryn anakupenda sana, mara ya kwanza nilikuwa najua ni mwanao.”

Mama alicheka sana na akavua miwani yake akaweka mezani,

MAMA: “Iryn ndo mtoto pekee, tuna kazi kubwa sana ya kuhakikisha anafikia malengo ambayo mama yake alitamani afikie.”

MIMI: “Ameshakuwa mkubwa tayari, wewe sahivi inabidi ufocus na Smith.”

MAMA: “Ni kweli lakini mama yake aliniomba sana nimpe uangalizi, ulienda Ethiopia nadhani hakukwambia kuwa mama yake mkubwa yuko strictly sana.”

MIMI: “She told me everything.”

MAMA: “Ni moja ya reason ambayo hapendi kuishi kule sababu hayuko huru.”

MIMI: “Ndomana nilikwambia before, ni mtu mzima tayari hatakiwa kubanwa sana.”

Niliagana na mama na wakati nataka kuondoka alinipa flash disk ambayo alisema ina picha zote pamoja na video za mkesha wa mwaka mpya. Nilimshukuru na nikaondoka kwenda ofisini kuendelea na majukumu yangu.

Baada ya kufika ofisini niliishia reception na nilianza kupiga story na Hilda maana toka tuachane jumamosi hatukuwa na mawasiliano yoyote zaidi alinipigia afu sikupokea.

Hilda alikumbushia picha zake tulizo piga kule Zanzibar na nilimtumia kwa njia ya Airdrop na baada ya kumtumia, nilifuta picha zote mbaya ambazo tulipiga wote na nikaacha zile zenye maudhui mazuri.

Niliendelea kupiga story na Hilda na baadae nilitoka kukaa nje kibarazani. Baadae Rebby alitoka nje na alivyoniona naye alikuja akakaa na mimi.

REBBY: “Nakuona shem umetulia stress free.”

MIMI: “Nambie CIA wa mke wangu.”

REBBY: “Shem unanionea mimi sio CIA bhana.”

MIMI: “Usifanye hivo Rebby, kweli hata mimi unanisnitch?”

REBBY: “Hamna bhana mimi siwezi fanya hivo, kwa dili unazonipa afu nikusnitch haiwezekani.”

MIMI: “Nasikia wewe ndo kigogo wa hii ofisi na umeanza nayo toka enzi hizo.”

REBBY: “Nimeanza na hii kampuni toka 2017 na ofisi zake zilikuwa Msasani. Mwaka 2019 tukahamia Masaki mwisho, hatukukaa sana ndo tukaja hapa ilikuwa 2020 mwezi wa 4.”

MIMI: “Ulipataje kazi hapa?”

REBBY: “Before nilikuwa nafanyia salon X ya Sinza, lakini tulikuwa tunakaziwa sana kwenye maokoto, ndo nikaanza kutafuta kazi sehem nyingine. Kuna mtu alini connect na dada mmoja ambaye alianza kazi na hii kampuni, lakini alishaondoka, ndo nikakutana na mama Iryn kwa mara ya kwanza.”

MIMI: “Kumbe mama Iryn alikupa mchongo, nilijua mama Janeth.”

REBBY: “Mama Janeth kaanza kuonekana baada ya kuhamia hapa. Insider mama Iryn alikuwa na Roho nzuri sana yule mama, Iryn hata nusu hafikii. Yule mama kila mtu alimpenda hata siku ya kusikia taarifa za msiba wake tulilia sana.”

MIMI: “Nimepata taarifa hizi na vipi kuhusu Winny na Asmah?.”

REBBY: “Winny alikuja miezi 2 mbele baada ya mimi kuajiriwa, lakini Asmah alikuja wakati tumehamia hapa. Marehemu alikuwa anampenda sana Asmah kutokana na upole wake na userious kwenye kazi. Ni moja ya mwanamke ambaye anafanya mambo yake na sio mtu wa kujichanganya kabisa. Wewe toka uje ndo umebadilisha life style yake kwa kiasi kikubwa mpaka ameanza kujichanganya na sisi.”

MIMI: “Aisee kumbe wewe una historia na hii kampuni sasa jumamosi tuna kikao, nataka nimshauri mama tufungue website afu tutaweka na historia ya hii kampuni kwenye profile.”

REBBY: “Hii itakua poa sana.”

Katika siku zote ambazo nilipiga story na Rebby bhasi ilikuwa ni hii siku maana nilijua vitu vingi sana kuhusu kampuni.

Niliamua kuingia ndani ili nimsalimie Asmah na ile kuingia tu alianza kulalamika kwanini sikurudi na nilimuahidi ningerudi?. Nilimpa taarifa za kuwa na kikao siku ya jumamosi na atoe taarifa kwa team, then nikampigia simu Lucy kumpa taarifa kwa upande wa Mikocheni.

Hii siku tulikuwa busy sana kuandaa maripoti ya mwaka uliopita na nilikuwa na Asmah mpaka usiku. Mida ya saa 2 nilitoka kuangalia mazingira na hakukuwa na mtu, wafanyakazi wote walikuwa wameondoka.

Nilikumbuka kudeal na simu ya Asmah lakini niliwaza ni process ambayo itachukua muda mrefu kidogo, kunipa simu yake sio shida ila akiona inachukua muda mrefu atauliza na mimi sitaki ajue nachotaka kufanya.

Nilichanganya akili sana nikakumbuka Asmah alisha niomba nimuunganishe na huduma ya Apple music, nikapata sababu ya kueleweka.
Nilimpanga Asmah na akajaa kwa mfumo na akanipa simu yake, bhasi mimi bila kuchelewa nilianza kufanya backup kwanza kwa kuhamishia vitu vyake kwenye Macbook yangu na nikareset simu yake.

Ilinichukua kama dakika 40 kufanya hii kazi, nikarudishia vitu vyake kama zamani na nikamuunganisha na Apple music, then nikamkabidhi simu yake. Nilikamilisha mission yangu kirahisi sana na kwa upande wake aliishia kufurahi na alianza kuplay na kudownload nyimbo pale.

ASMAH: “Insider ahsante sana.”

MIMI: “Muda umekwenda tuondoke, kesho tutaendelea.”

ASMAH: “Nataka nimalizie hizi kazi ili ijumaa niombe likizo hata ya week, twende na Zanzibar.”

MIMI: “Tufanye next week maana weekend hii tuna kikao na mama.”

ASMAH: “Aisee afu nilisahau ujue, kila mwanzoni mwa mwaka tunakuwaga na kickoff meeting.”

MIMI: “Bhasi ndo hivo, waambie na wafanyakazi wako wajue na wajiandae.”

ASMAH: “Kitafanyikia wapi hicho kikao?”

MIMI: “Hatujaongea sana haya ila sidhani kama itakuwa nje na Serena hotel. Sogea hapa kwenye coach tuongee bhasi, umekaa mbali sana mummy.”

ASMAH: “Haya nimesogea nambie.”

Nilimbana vizuri na nikaanza kumpa kashikashi japo alikuwa ananipa upinzani, lakini baadae alitulia na akaanza kunipa ushirikiano. Nilivyotaka kutalii bustani yake alinishika mkono na akasema yuko period, hapa mimi nilikuwa niko fire hatari. Nilikuwa simuamini na nilidhani anatafuta sababu ya kutoliwa na niliendelea kuforce mpaka nika prove ni kweli, hivyo kumuacha.

Muda ulikuwa umekwenda sana na tuliondoka ofisini, wakati tunatoka getini kwa upande mwingine mlinzi alinambia ana maongezi na mimi, siku ambayo nitakuwa na nafasi na ni muhimu.

Baada ya kuachana na mlinzi pale getini, niliwaza jamaa anataka kuniambia kitu gani? Nikapanga kumtafuta kesho ili tuongee ili nijue jamaa ana jambo gani.

****
Jumamosi tulikuwa na kikao cha kampuni nzima na tulifanyia pale Serena hotel. Lengo la kikao ilikuwa ni kufanya review za mwaka uliopita pamoja na kuset goals na mipango ya mwaka mpya.

Kikao chetu kilichukua masaa 4 kutoka saa 10 jioni mpaka saa 2 za usiku ndo tulimaliza. Baada ya kumaliza kikao mama Janeth aliomba nibaki kwani kuna mambo ya kuongea wawili.

Mambo muhimu tuliyozungumza ilikuwa ni pamoja na suala la kupewa dividend/Gawio kutokana na faida, maana Iryn tuliongea na alinambia watanipa gawio la 10% ya faida.

Jambo lingine lililonishtua ni baada ya mama kunambia kuwa mama mkubwa wa Iryn Ethiopia, alimpigia simu kumuulizia information zangu na hapa sasa nikajisemea mambo yashaanza kuwa moto na hakunaga marefu yasiyokuwa na ncha,

MIMI: “Anaulizia taarifa zangu kama zipi? Maana Iryn alimtambulisha kuhusu mimi.”

MA’ JANETH: “Alitaka kujua umeingia lini kwenye kampuni na ufanisi wako kwenye kampuni ni vitu kama hivyo.”

Kidogo nikapata amani,

MIMI: “Ni hivo tu hakuna kingine?”

MA’ JANETH: “Hatukumaliza maongezi yetu na alisema atanirudia tuongee vizuri.”

MIMI: “Sawa mama kama kuna lolote utanijulisha.”

Nilijisemea, nimetoka kuongea na Iryn haya mchana lakini hachukulii maanani kabisa, ona sasa mama soon ataambiwa ukweli.”

Nilinyong’onyea sana kwakweli na tuliondoka pale ukumbini kuelekea parking na njiani tulikuwa tukipiga story za kawaida. Kwa upande mwingine Asmah alikuwa akinisubiri parking ili tuondoke na niseme alikuwa tayari kashajaa kwangu na nilikuwa nasubiri kwenda naye Zanzibar kumaliza kazi.

Tuliagana na mama pale parking na mimi nilielekea kwa Asmah ili tuondoke na baada ya kuingia kwa gari nilimvutia upande wangu na nikaanza kumchapa mate kwa fujo.

Simu yangu ilianza kuita na ile kucheki nani anapiga alikuwa ni Iryn na niliipotezea maana alikuwa kanikera sana mchana hii siku.

Sababu kubwa ni kwamba nilimwambia akija Dar ahakikishe mama Janeth anajua suala la mimba yake na amwambie ukweli kuwa mimba ni yangu. Niliona ni bora amwambie mama Janeth mapema na itakuwa rahisi kuni defend kuliko akiambiwa na mtu mwingine, italeta chuki kwangu. Iryn alisema hawezi fanya hivo maana haoni sababu ya kumuogopa mama, hapa ndo tuliishia kugombana mpaka kukatiana simu.

Asmah alisema suala la sex niwe mvumilivu mpaka tutakavyo kwenda Zanzibar na kuhusu mahusiano yote tutazungumza. Nilianza kumdrop nyumbani kwake na mimi nika endelea na safari ya kurudi home, lakini sasa njiani nilikuwa nawaza yale maneno ya mama Janeth.

Baada ya kuachana na Asmah nilimpigia simu Iryn ili tuongee na ile kupokea alianza kufoka kwanini sipokei simu zake?

IRYN: “Insider una matatizo gani wewe mwanaume?.”

MIMI: “Umeanza kelele tena kama huwezi kuongea kata simu, siko kwenye mood nzuri.”

IRYN: “What did you say?, mimba inisumbue na wewe pia unisumbue?. I’m still reminding you, mambo ya kijinga unayofanya achana nayo before it’s too late.”

MIMI: “Huu wimbo wako nisha uchoka na acha kunitisha.”

IRYN: “The moment ambayo nitachukua action, please usije kuja kulaumu.”

MIMI: “Sawa wewe chukua tu! huna haja ya kujifikiria, nimechoka kelele zako hizi.”

IRYN: “What?”

MIMI: “Kwanza mchana tumeongea kuhusu mama Janeth na sio muda katoka kuniambia kuwa mama mkubwa wako kampigia simu kuulizia taarifa zangu, soon mama anajua kuhusu wewe.”

IRYN: “Hata akijua kwamba nitakufa? Na wewe acha uoga mwanaume gani hujiamini?”

MIMI: “Point yangu, mwambie mama yako mdogo ajue, ni bora umwambie wewe kuliko mtu mwingine.”

IRYN: “Ukweli ni kwamba we f*cked na ukamwagia ndani, leo hii nina mimba yako. Sasa kelele nyingine zinatoka wapi? Ulifikiri nitakaa kipindi chote bila mama kujua?

MIMI: “So! What’s your point?”

IRYN: “Shut your mouth, ulikuwa unaona raha kuniweka style unazotaka? Haya ndo matunda yake.”

MIMI: “Kadri siku zinavyokwenda ndo unazidi kuchanganyikiwa, naomba ufanye kama nilivyo kuelekeza mchana.”

Baada ya kuongea na Iryn nilijisemea, hii mimba inamchanganya huyu mwanamke maana anakuwa kama mwehu kadri siku zinavyokwenda anakuwa anabadilika.

Baada ya kuachana na Iryn, niliwasiliana na Lucy na alinambia kesho Jumapili atakuja home kunitembelea na mdogo wake, ilikuwa ni surprise na nilimkaribisha.

Jumapili home nilikuwa nina ugeni wa Lucy na tulishinda wote home mpaka usiku. Hii siku Lucy alinifungukia kuwa wako kwenye mahusiano na Bob na wana mwezi tayari. Ni taarifa ambazo hazikunishtua sana maana tangu muda mrefu nilishaona dalili za Lucy kumuelewa Bob.

Kwa upande mwingine tuliongea kuhusu suala la Iryn kwenda Ethiopia kwaajili ya suala lake la ujauzito na yeye alinipa moyo kuwa kila kitu kitakwenda sawa na sina haja ya kuwa na wasiwasi.

Jumatatu nilikwenda Masaki ofisini kwa kuchelewa sana, niliingia mida ya saa 5. Pale reception alionekana Hilda na sikumsalimia maana alikuwa anaongea na simu na straight nikaingia ofisini.

Muda huu nilitegemea ninge mkuta Asmah lakini hakuwepo na nilibaini hajafika bado, sikutaka kumpigia simu kabisa kumuuliza alipo.

Baada ya nusu saa Hilda alikuja ofisini kashika mafile na nilishangaa kuona analalamika majukumu yamekuwa mengi,

MIMI: “Una maanisha nini kusema majukumu yamekuwa mengi?”

HILDA: “Bossy ina maana majukumu ya Asmah nani ata cover kama sio mimi?”

MIMI: “Asmah bado hajaanza likizo usiwe na wasiwasi na kama ataanza mimi nitacava.”

HILDA: “Asmah amekwenda likizo au ameachishwa kazi, you guys mbona siwaelewi?”

MIMI: “Hilda mimi ndo nashindwa kukuelewa, kwani Asmah kaja ofisini leo?”

HILDA: “Amekuja asubuhi akaniaga kuwa ameachishwa kazi ila tutakuwa tuna wasiliana.”

MIMI: “Hakuna wa kumuachisha kazi anakuzingua, atakuwa kapewa likizo na mama maana aliomba likizo. Yaani! aachishwe kazi afu mimi nisijue? Hakuna mtu anayeachishwa kazi bila mimi kuaproval.”

HILDA: “Bossy, Asmah anaonekana amelia sana hata macho yake yalikuwa ni mekundu na anaoneka hayuko sawa kabisa. Tangu lini mtu anayekwenda likizo anakuwa na huzuni na sio furaha? Pia namjua Asmah vizuri sana.”

MIMI: “Unataka kusema Asmah kaacha kazi? and how? yaani from nowhere haimake sense ujue.”

HILDA: “Ameniambia kaachishwa kazi, sema alikuwa na haraka sababu ya Uber alinambia tutaongea badae. Kama wewe hujui kinachoendelea bhasi mpigie simu uongee naye, au kaangalie mails zako.”

Nilitoa simu kumpigia na hakupoea simu zangu, maana nilipiga mara tatu bila majibu. Niliamua kufungua mails za ofisi ili nione kama kuna taarifa yoyote kutoka kwake…..

TO BE CONTINUED.
Asante
 
Ukipata kazi fanya kazi
Acha kazi uone kazi
Asmah ameyatimba na genye zake alitakiwa akaze asikuregezee sababu aloshajua toka awali mazoea na wewe yatamfukuzisha kazi.
 
Kabul Pulao Pilau Pendwa La Pakistan.

Ilikuwa Ijumaa Order ya wateja wangu wapo walotaka Biryani wengine Kabul Pulao pembeni ikisindikizwa na Bisbas Chachandu ya Yemen na Sambharo

Gily Gru mwambie wifi soon nakuja tuipike Kabul Pulao nampa na Secret Ingredients ambayo simpi yoyote kila Chef ana secret yake ya chakula kitamu.
 
Attachments

  • BeautyPlus_20240607210129655_save.jpg
    BeautyPlus_20240607210129655_save.jpg
    1.6 MB · Views: 18
  • BeautyPlus_20240607211630102_save.jpg
    BeautyPlus_20240607211630102_save.jpg
    1.7 MB · Views: 16
  • BeautyPlus_20240607152326234_save.jpg
    BeautyPlus_20240607152326234_save.jpg
    1.6 MB · Views: 16
Kabul Pulao Pilau Pendwa La Pakistan.

Ilikuwa Ijumaa Order ya wateja wangu wapo walotaka Biryani wengine Kabul Pulao pembeni ikisindikizwa na Bisbas Chachandu ya Yemen na Sambharo

Gily Gru mwambie wifi soon nakuja tuipike Kabul Pulao nampa na Secret Ingredients ambayo simpi yoyote kila Chef ana secret yake ya chakula kitamu.
Nimefikisha taarifa. Wewe tu njoo ule bata🤩
 
CCTV za kazini zilionesha kijana akifanya yake na Asma eneo la ofisi. Mlinzi alitaka amuambie awe makini, maana kila analofanya boss Iryn anaona. Sasa kibarua kimeota nyasi
 
Smart move ya Iryn ni kuwapa zawadi wafanya kazi wake ya IPhone akiwemo Insider na mke wake. Anaona mawasiliano yao na location alipo.

Insider alimpeleka Asmah akapumzika kidogo hapo lakini akajikuta amelala hadi saa 10 alfajiri. Hapa Iryn aliona simu zikisoma location moja masaa zaidi ya 4 lazima ahisi kuna jambo linaendelea. Halafu Insider huyohuyo alichukua simu ya Asmah na kuindoa scam spy app za Iryn. Hii ilikuwa kengele kuwa mali Italiwa badly na Iryn hatakuwa na chake. Simu alizogawa Iryn kama zawadi kwa wafanyakazi ndio ulinzi wake kibiashara na kwa mtu anayempenda. Gari aliyokuwa anatumia ni ya Iryn je aliikagua kujua kama kuna Camera zile za usalama ambazo mara nyingi ni ngumu kugundua kama sio mtaalamu wa hayo mambo. Pia vipi hiyo gari kama ina GPRS nayo inaonyesha location alipo hata kama kwenye simu ameondoa spy programs?

Kuna mifumo ipo sasa hivi mtu akitaka kujua mliyokuwa mnaongea anawapa pesa vijana wa taasisi fulani wana download maongezi yenu yote wanamtumia.

Bado Hilda na Sumaiya anawatafutia angle ya kuwatimua
 
Smart move ya Iryn ni kuwapa zawadi wafanya kazi wake ya IPhone akiwemo Insider na mke wake. Anaona mawasiliano yao na location alipo.

Insider alimpeleka Asmah akapumzika kidogo hapo lakini akajikuta amelala hadi saa 10 alfajiri. Hapa Iryn aliona simu zikisoma location moja masaa zaidi ya 4 lazima ahisi kuna jambo linaendelea. Halafu Insider huyohuyo alichukua simu ya Asmah na kuindoa scam spy app za Iryn. Hii ilikuwa kengele kuwa mali Italiwa badly na Iryn hatakuwa na chake. Simu alizogawa Iryn kama zawadi kwa wafanyakazi ndio ulinzi wake kibiashara na kwa mtu anayempenda. Gari aliyokuwa anatumia ni Jeep ya Iryn je aliikagua kujua kama kuna Camera zile za usalama ambazo mara nyingi ni ngumu kugundua kama sio mtaalamu wa hayo mambo. Pia vipi hiyo gari kama ina GPRS nayo inaonyesha location alipo hata kama kwenye simu ameondoa spy programs?

Gari alirudisha kitambo. Nahisi ndani ofisini Kuna cctv au kwenye simu kulikua na spy software. Hata yeye mwenyewe Insider Man anaweza kuwa amewekewa kwenye simu yake.
 
Smart move ya Iryn ni kuwapa zawadi wafanya kazi wake ya IPhone akiwemo Insider na mke wake. Anaona mawasiliano yao na location alipo.

Insider alimpeleka Asmah akapumzika kidogo hapo lakini akajikuta amelala hadi saa 10 alfajiri. Hapa Iryn aliona simu zikisoma location moja masaa zaidi ya 4 lazima ahisi kuna jambo linaendelea. Halafu Insider huyohuyo alichukua simu ya Asmah na kuindoa scam spy app za Iryn. Hii ilikuwa kengele kuwa mali Italiwa badly na Iryn hatakuwa na chake. Simu alizogawa Iryn kama zawadi kwa wafanyakazi ndio ulinzi wake kibiashara na kwa mtu anayempenda. Gari aliyokuwa anatumia ni Jeep ya Iryn je aliikagua kujua kama kuna Camera zile za usalama ambazo mara nyingi ni ngumu kugundua kama sio mtaalamu wa hayo mambo. Pia vipi hiyo gari kama ina GPRS nayo inaonyesha location alipo hata kama kwenye simu ameondoa spy programs?

Kuna mifumo ipo sasa hivi mtu akitaka kujua mliyokuwa mnaongea anawapa pesa vijana wa taasisi fulani wana download maongezi yenu yote wanamtumia.

Bado Hilda na Sumaiya anawatafutia angle ya kuwatimua
Gari ya Iryn n audi sio jeep
 
Kwa mkewe yupi?

Hiyo jamaa hajaoa, kazaa na mama J na hawajala kiapo. kisha kamkula bosi wake hadi kumjaza mimba, na huyo hawajala kiapo.

Sasa mkewe ni nani hapo?
Mama J ndio mkewe hiyo haipingwi mzee, ndoa sio yale makaratasi mzee baba!!. Ndio maana hata akae nje mpaka saa 8 za usiku, bado mahala pa kurud ni kwa mama J. Huyo ndio mkewe
 
Kinachomfanya mama J umtambue kuwa ni mke ni kule kuzaa na kuishi nyumba moja na insider man?

Vipi Iryn naye akizaa kisha insider akahamia sauzi kuishi naye atakuwa mkewe?

Walioanzisha ndoa za makaratasi hawakukurupuka jichanganye ule kiapo kisha utelekeze mwanamke ndio utajua maana yake.
 
Ahahahah.
Mama J ndio mke wa jamaa bwana hata iweje. By the way ndio character pekee ninayempenda katika story nzima.
 
Kinachomfanya mama J umtambue kuwa ni mke ni kule kuzaa na kuishi nyumba moja na insider man?

Vipi Iryn naye akizaa kisha insider akahamia sauzi kuishi naye atakuwa mkewe?

Walioanzisha ndoa za makaratasi hawakukurupuka jichanganye ule kiapo kisha utelekeze mwanamke ndio utajua maana yake.
Na ndio maana kulikuwa na kikao kule ukweni kwa insider,kikaja kikao cha mama insider,mama j na insider.
Maana yake pamoja na wao kuzaa na kuishi pamoja bado kuna jambo la msingi linatakiwa lifanyike ( kufunga ndoa).
Ila kibongo bongo mama j ndio mwenye mali na tunaweza kusema ndio mwenye mamlaka na insider au insider kuwa na mamlaka na mama j ,sabaabu ni watu wanaotambulika kwenye familia zao zote mbili kwamba wapo pamoja.ni sawa kusema " mkewe".
 
Back
Top Bottom