Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 02:
EPISODE 24

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN.”

CONTINUE:

Kipindi tuko kwenye flight kwa pembeni yangu dirishani alikuwa amekaa mzee wa makamo kwa kumkadiria umri wake kama miaka 60, kwa pembeni yetu opposite walikaa dada wawili, ambao walionekana kuwa busy sana wakijisnap.

Mzee alikuwa anawaangalia sana wale warembo huku akitabasamu, ilibidi nianze kuongea na mzee;

Mzee nakuona unawaangalia bint zako kwa makini sana vipi kuna tatizo?”

“Najaribu kufikiria kizazi chetu enzi hizo tunakua na kizazi hiki kipya, naona mabadiliko makubwa sana.”

“Upo sahihi mzee, sahivi technologia ni kubwa sana.”

“Sahivi unaweza kuwa na mtu pembeni yako na mnaelekea safari moja na hata msijuane wala kusalimiana sababu ya simu, unakuta mtu muda wote yuko busy na simu.“

“Ni kweli kabisa sahivi mtu anacheka na simu kama binadamu mwenzie.”

“Wazungu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kututeka na kucontrol akili zetu, ule ubinadamu naona unakufa kila siku, mtu anathamini simu kuliko binadamu mwenzie.”

“Mzee upo sahihi, hiki kizazi cha sasa Mungu atusaidie, simu zimetukamata akili kiasi kwamba hata ukiishiwa bando unaona kama maisha hayaendi.”

“Kila generation inapita na sifa zake, sijui hii ndo ile tuliyotabiriwa?. Anyway, wewe ni Mtanzania kama mimi, sina haja ya kukuuliza hili, unakwenda Zambia kwaajili ya nini?”

“Nakwenda kumsalimia mzee wangu pamoja na kuangalia fursa za biashara.”

“Safi sana hii ndo akili na umri wako?”

“Miaka 27.”

“Wewe ni kama kijana wangu wa mwisho kwa huu umri wako, bado ni kijana mdogo sana.”

“Hahahaa nashukuru mzee, vipi na wewe Zambia unaharakati gani?”

“Mimi nina deal na biashara za copper, kwahiyo nakwenda kwaajili ya masuala ya kibiashara.”

“Nimekuwa interested na biashara ya Copper unaweza kunipa ABC hata hapo baadae nikitaka kuifanya niwe na idea?.”

Mzee alinipa elimu kuhusu biashara ya Copa na namna ya kuanza pamoja na mtaji, Ila sasa changamoto kubwa niliyoiona ni namna ya kuingia sokoni maana wazee wa system wameshateka soko tayari la Copper.

Nilipiga story nyingi sana na mzee mpaka tunawasili Lusaka Airport, nakumbuka tulifika saa 3 za usiku na tulibadilishana namba za simu, alisema anakwenda hotelini.

Kwa upande mwingine, mzee wangu alikuwa amenisubiri pale uwanja wa ndege, kwani alifika mapema sana kwa ajili ya kunipokea. Alikuwa akisubiri kwenye sehemu ya mapokezi, na nilipotoka nje, alikuwa wa kwanza kuniona.

Baada ya kuonana tulisalimia na tulianza safari ya kwenda home, lakini tulianza kwanza kupitia kwenye moja ya mgahawa mzuri kwaajili ya kupata chakula cha usiku.

Mazingira ya Zambia pamoja na hali ya hewa yalikuwa ni ya tofauti sana, baridi ilikuwa ni kali kwa wakati huu wa usiku. Muda huu tukipata dinna mzee alianza kuniuliza kuhusu maendeleo yangu kwa ujumla, nami nikamuuliza jinsi maisha yalivyo nchini Zambia. Mzee aliishia kusifia maisha ya Zambia, akisema kuwa ni mazuri na sehemu salama ya kuishi.

Tulitumia kama dakika 45 kisha tukaondoka kwenda nyumbani kwake, anakoishi Lusaka, sehemu inayoitwa Roma. Alikuwa anakaa huko, na sehemu anayokaa ni kota nyingi ambazo zimepangiliwa vizuri sana.

Baada ya kuingia ndani hakukuwa na mtu yoyote nami sikutaka kuuliza maswali sana ukizingatia ndo ninafika hapa kwa mara ya kwanza. Tulifanya mazungumzo kidogo sana mambo mengi tulikuwa tumeshaongea njiani, na mzee aliishia kunionesha chumba changu, akasema nilale na mambo mengine tutaongea kesho.

Niliamka kwa kuchelewa ile asubuhi nikihisi njaa, nikajisemea, 'wacha niende jikoni nione kama kuna chochote cha kula.' Nilikuwa na uhakika nisingekosa kitu. Lakini nilipotoka chumbani, nikakutana na dada aliyekuwa amekaa sebuleni akipanga nguo. Sikuwa na wazo la kwamba kuna mtu mwingine ndani, kwa hiyo nilishtuka kidogo.

Hata dada naye alishtuka kuniona, maana hakutegemea kama kuna mgeni humu ndani. Alianza kupoteza ujasiri kwa sababu alikuwa amejiachia sana, mnavyojua jinsi wanawake wanavyovaa wakiwa peke yao. Nilimchunguza haraka na nikaanza kuwaza, ‘Huyu ndiye mamdogo nini?’ Nikamsalimia, na kwa bahati nzuri, dada alikuwa anaongea Kiingereza vizuri kabisa.

MIMI: “My name is Insider. Yesterday, I arrived here late but didn’t see you”

DADA: “Oh, really? What time did you get here?.”

MIMI: “I got here around 10 PM. Were you already gone by then?”

DADA: “Yes, I left around 7:30 PM. I don’t sleep here, I just come to work and then leave. Also, I don’t have any information about your presence here."

MIMI: “Mr. William is my father. I thought he told you everything about my presence."

DADA: “Oh, I didn't know that, maybe he forgot to tell me, and how long will you be here?"

MIMI: “I'm planning to stay for a while.”

DADA: “Nice, do you want to explore the area?"

MIMI: “Yeah! I'm looking forward to it. Do you have any recommendations?"

DADA: “Definitely, there's a great park nearby and some wonderful cafes, I can show you around if you would like."

MIMI: “That sounds great, thank you! I would love to.”

DADA: “Great, let's arrange for this weekend. It should be a lot of fun."

MIMI: “Have been loving our conversation but realize I don't even know your name lol.”

DADA: “Well my name is Sandra.”

Ndani ya muda mfupi nilikuwa nimeshazoena na dada huku tunapiga story na alikwenda kuniandalia chai, muda huu nilikuwa nimekaa sebleni nikishangaa TV.

Niliendelea kuwaza kuhusu dada pale, “ina maana mzee amemuajiri huyu dada awe anafanya usafi wa nyumba, anamfulia nguo na kumpikia afu anaondoka, na anamlipa mshahara kila mwezi?, ni vizuri lakini.

Baada ya kupata breakfast nilirudi chumbani kuendelea na mambo mengine, niliwasha laptop yangu ya Macbook niliyopewa na Iryn kama zawadi na nikaanza kupanga mipango yangu.

Mipango yangu ilikuwa niwekeze kwenye real estate na kufungua biashara kubwa kwa kule Dodoma, hivyo nilipanga nikitoka huku, nitakwenda Dodoma. Nilipata wazo la kuwasaliana na madalali wa kule ili waanze kunichekia fremu za biashara.

Baada ya kumaliza mipango yangu niliishia kulala pale kitandani maana sikuwa na kitu cha kufanya. Mchana nilitoka kupata lunch, nikarudi tena kulala na jioni dada alinigongea mlango, kisha akaniaga anaondoka na tutaonana kesho.

Saa 2 usiku mzee alirudi home na tulianza maongezi, kwa upande wangu nilimwambia sababu nyingine ya kuja Zambia ni kuangalia fursa za kufanya kama zipo.

MZEE: “Fursa nyingi sana kwa huku Zambia zipo ukanda wa Copper belt wanakochimba Copper, kule kuna fursa nyingi na vijana wengi wameaniriwa kule migodini.”

MIMI: “Vipi kuhusu biashara za nguo na mavazi maana naona wazambia wengi wanakuja Kariakoo kununua nguo.”

MZEE: “Biashara ya nguo ukisema ufungue huku itakusumbua ufuatiliaji, labda nikushauri uwe unauza kwa jumla, uwe na mtu wa kushirikiana nae huku, mimi baba yako niko busy sana, muda mwingi nakuwa site.”

MIMI: “Kuna dada nimeshinda nae siku nzima hapa home, umemuajiri awe anakufanyia kazi za humu ndani?”

MZEE: “Hapana, ameajiriwa na kampuni kwaajili ya hili, humu ndani sisi tunaishi wawili tu! mimi na ndugu yangu mmoja amesafiri.”

MIMI: “Na ofisi yako ipo wapi?”

MZEE: “Ipo Lusaka mjini kabisa itabidi kesho twende wote ukaijue.”

MIMI: “Sawa haina shida, jambo jingine naomba msaada wa Wi-fi tangu jana siko online.”

MZEE: “Wifi ilipata hitilafu kidogo, kesho tukienda ofisini tutachukua nyingine.”

Tuliendelea kuongea masuala mengine na nilitamani nimwambie kuhusu suala la Iryn, lakini Roho yangu ilikuwa inagoma katakata kumshirikisha hili suala, nilimuaga nikaenda zangu kulala.

Asubuhi na mapema tuliondoka kwenda kazini kwake, baada ya kuwasili pale ofisini alianza kunitambulisha kwa wafanyakazi wenzake na wao waliishia kumsifia mzee kuwa na kijana mkubwa na walionesha kunifurahia sana.

Kuna mama mmoja alitokea kunionyesha ukarimu na upendo wa hali ya juu sana, mpaka nikaanza kuwa na wasiwasi huenda akawa mchepuko wa mzee maana alikuwa akinijali sana.

Mzee wangu anafanyia kazi kwenye moja ya kampuni kubwa sana ya construction kwa kule Zambia na anafanya kama quantity surveyor, kazi zake nyingi asilimia kubwa ni kwenda site sehemu mbalimbali, ni mara chache sana kuwa ofisini.

Nilishinda na mzee ofisini siku nzima na jioni wakati tunarudi home alisema kesho anasafari ya kwenda kusini mwa Zambia sehemu inaitwa ‘Livingstone’ na angetamani twende wote. Niliona wazo la mzee ni zuri ukizingatia sababu kubwa ya kuja huku ni kutembea na kutuliza akili, kuondoka na mzee niliona ni heri kuliko kulala ndani tu.

Baada ya kurudi home niliingia online kuangalia watu walionicheki maana tangu nije Zambia sikuwasha data kabisa, nilikuta Hilda, Allen, Jane, Lucy, Mary, Wife, Dullah bila kumsahau Asmah walikuwa wamenicheki na wengine wengi.

Nilianza kwa kumpigia simu mke wangu ili kujua maendeleo ya familia, kisha nikajaribu kumpigia Asmah, lakini hakuwa online, hivyo nikamtumia ujumbe kumjulisha kuwa nimefika salama. Baadaye, nikampigia Dullah, ambaye alikuwa anatarajia kufunga ndoa Jumamosi hii. Ilibidi nimpe udhuru wa kutokuweza kushiriki, ingawa alilalamika sana, hatimaye alikubali kwa shingo upande.

Nilituma ujumbe mfupi kwa Hilda, kisha nikampigia simu Lucy, na ndani ya sekunde chache, Lucy alijibu simu yangu;

LUCY: “Wewe Insider kwanini hupatikani kwa simu? unanipa mashaka sana.”

MIMI: “Nimesafiri niko Zambia one time ndomana unaona hunipati kwa simu.”

LUCY: “Zambia? Una mishe gani huko?”

MIMI: “Nimekuja kutembea na kumsalimia mzee wangu.”

LUCY: “Ohh! Sawa, nimekupigia simu sana leo, hupatikani.”

MIMI: “Nambie kuna jambo gani unataka kushare mummy.”

LUCY: “Ni kuhusu Iryn maana hapatikani kwa simu since niongee nae ijumaa.”

MIMI: “Unajua hili suala linaniumiza sana akili ndomana nimekuja huku, nataka nitulize akili yangu kwanza, huenda nitapata solution.”

LUCY: “Solution ni kwenda South kuoanana naye myamalize, Iryn bado anahasira juu yako kwa kitendo cha kumpiga kule hotelini na bado anataarifa zako kuhusu kutembea na Asmah, na hili suala la mimba ndo linampa mawazo sana.”

MIMI: “Mimi niko tayari kufanya hayo yote ila sasa hapatikani, mpaka kaka yake Jimmy nae hapatikani nafanyaje?.”

LUCY: “Jaribu kumtafuta kaka yake kwa mara nyingine tena, huenda utampata.”

MIMI: “Sawa nitamcheki tena.”

Niliagana na Lucy pale, kwa upande mwingine alikuwa kashanikumbusha kuhusu Iryn maana nilikuwa nimeshamsahau tangu nije huku Zambia, nilijikuta naanza tena kufikiri upya kuhusu mambo yote yanayoendelea.

Muda huu simu ya Hilda iliingia na nilipokea tukaanza mazungumzo na kubwa nilitaka kujua maendeleo ya ofisi kwa ujumla, alisema kila kitu kinakwenda vizuri na niliendelea kumtia moyo kwamba awe ananitafuta pindi apatapo changamoto.

Baada ya kuagana na Hilda nilimpigia simu Iryn, hakuwa online, nilimcheki na Jimmy tena hakuwa online, bhasi nikalala zangu kwaajili ya safari ya kesho asubuhi.

Asubuhi na mapema dereva wa ofisi alikuja kutuchukua kwaajili ya safari ya kwenda Livingstone kusini mwa Zambia. Ilikuwa ni safari ya kukaa siku mbili na tungerudi jumapili, hivyo nilitembea na nguo za kubadilisha.

Saa 2 asubuhi ndo tulianza safari yetu, na umbali wa kutoka Lusaka mpaka Livingstone ni kama 450km, barabarani dereva alikuwa anatembea balaa, gari ilikuwa ni Hilux, na jumla ya watu tuliokuwa kwenye gari ni watano.

Saa 6 mchana tuliwasili Livingstone mjini, kingine kilichonishangaza ni vile eneo kuwa busy sana na asilimia kubwa ya watu wanaopatikana huku ni foreigners, wazungu ndo walikuwa wengi sana.

Mzee alinambia huku wazungu ni wengi sababu ya utalii kama unavyoona vile Arusha, na alisema hatupo mbali sana na Victoria falls, mbuga za wanyama, na watalii wengine wanavuka boda kwenda Zambezi National Park ya Zimbabwe.

Tulipofika ofisini kwao, ambapo wana tawi katika eneo hili, walianza kupanga mipango na kisha wakaondoka kwenda kukagua mradi. Kulikuwa na sheli mpya ambayo ilikuwa inaanza kujengwa, na hiyo ndiyo kazi iliyowaleta huku.

Mzee alinambia niende hotelini kupumzika wakati yeye anaendelea na majukumu ya ofisi, na kwamba baadaye tutakutana. Aliagiza dereva anipeleke hotelini, ambapo dereva alinipeleka New Fairmount Hotel. Booking ilikuwa tayari imefanywa, na mara tu nilipofika na kuoneshwa chumba changu, niliishia kulala kutokana na uchovu.

Mnamo saa 1 usiku, mzee alinicheki ili kupata chakula cha usiku pamoja na rafiki zake wawili, ambao tulikuwa wote safarini na tulifika katika hoteli hiyo. Kwa upande mwingine, walionekana watu kutoka mataifa mbalimbali ambao walikuwa wamekuja kwa ajili ya utalii, hotel za huku Livingstone zote ni za kitalii.

*****
Jumapili kabla ya kurudi Lusaka, mzee alinipeleka Victoria falls kushuhudia maajabu yake na alinambia bila kwenda kuona, sitakuwa nimefika Zambia kwa kweli, kwani ndoto ya kila mgeni ni kuona Victoria falls.

Saa 6 mchana tulitoka hotelini kuelekea Victoria Falls, na ilikuwa ni mwendo wa takriban dakika 10. Tulipofika, tulishuka kutoka kwa gari na kuanza kutembea kwa miguu hadi kwenye eneo la maajabu. Kwa mara ya kwanza, macho yangu yaliona maporomoko haya ya maji, na ilikuwa ni jambo la kushangaza kweli. Eneo lile linavutia sana, jinsi maji yanavyoshuka na mvuke unaopanda juu ni jambo la ajabu kabisa.

Tulisogea karibu na maporomoko ya maji kwa sababu kuna njia maalum zilizotengenezwa kwa ajili ya kutembea kwa miguu, ili uweze kushuhudia maporomoko haya moja kwa moja kwenye mto Zambezi. Upande huu tulikutana na watalii wengi sana.

Maajabu mengine Victoria falls imegawanyika kati ya Zambia na Zimbabwe na ndo mpaka unaotenganisha kati hizi nchi mbili. Pia, kuna daraja ambalo linatumika kama mpaka ‘Victoria falls bridge’, mbele kidogo kuna border ya Zimbabwe, ukienda mbele tena 12km unakutana na Zambezi National park, sisi tuliishia palepale border.

Jambo lingine ukifika huku utasikia kuna sehemu inaitwa ‘Devil pool’ ambayo inapatikana juu kabisa kwenye edge za mto Zambezi (Sehemu ambayo maji yanaanza kuanguka chini ndo hii pool inapatikana). Watu au watalii wengi huwa wanapenda sana kuogelea kwenye hio pool, nilijisemea ‘hawa jamaa hawako serious na lazima wana Roho ngumu’.

Tulimia kama masaa 4 kutalii maeneo haya na ndani ya muda mfupi nilitokea kulipenda sana hili eneo maana lilinavutia na mazingira yake ni mazuri, kwa upande mwingine nilikuwa nimeona kitu kipya kwenye mboni zangu, niliishia kupiga picha nyingi sana hii siku.

Saa 1 usiku tulianza safari ya kurudi Lusaka, kazi iliyokuwa imewaleta huku ilikuwa imekwisha tayari. Nakumbuka tuliingia Lusaka saa 6 za usiku maana kuna sehemu tulitumia masaa 2 kwaajili ya kupumzika na kupata dinna.

Kesho yake nilichelewa sana kuamka sababu ya uchovu wa safari na nilikuwa nikihisi njaa sana, niliamka ili nicheki chochote kitu nile. Nilikwenda dining na nilikuta chai ipo kwenye chupa imeandaliwa tayari, na muda huu nilimuona dada akitokea jikoni, baada ya kuniona alitabasamu na tukasalimiana.

SANDRA: “Nimekugongea sana leo, ulichoka sana na safari?”

MIMI: “Umejuaje? Jana tumeingia saa 7 za usiku na kule nilikuwa silali kabisa.”

SANDRA: “Kaka ameniambia mlikuwa Livingstone, hope ulienjoy.”

MIMI: “Nimeenjoy kawaida, nimepapenda pale Victoria falls, wish tungekuwa wote.”

SANDRA: “Hahahaa kaka ataniua akijua niko na kijana wake.”

MIMI: “Mzee hawezi kuharibu furaha yangu, labda wewe ukatae lakini hio sio sababu.”

SANDRA: “Unaondoka lini kwanza?”

MIMI: “Ijumaa nafikiri nitaondoka. Kesho tukatembee mjini bhasi, niyaone na mazingira na fursa za kuwekeza.”

SANDRA: “Sawa.”

Baada ya kupata chai nilimshukuru na nikarudi room kuendelea na mambo yangu, na ile kuwasha data nakutana na message kutoka kwa Mary, alikuwa akilalamika nimeondoka bila kumpa taarifa.

Nilimpigia simu ili tuongee na iliita kwa sekunde kadhaa akapokea;

MIMI: “Mambo Mummy.”

MARY: “Safi, nimekutafuta juzi na hujataka kunitafuta, na kwanini umesafiri bila kunipa taarifa?”

MIMI: “Sorry sana, nilikuwa na haraka mpaka nikasahau, I’m really sorry.”

MARY: “Insider sio kweli, kama uliweza kwenda kumuaga dada Jane?, ulishindwaje kunitumia ujumbe?”

MIMI: “Ndomana nimekuomba msamaha, kichwa changu kwasasa kimevurugwa kina vitu vingi sana, huwezi kunielewa kwasasa.”

MARY: “Not true, it’s just a matter of priorities, have a good day.” Na akakata simu.

Ukweli nilikuwa nimezingua sana kuondoka bila kumpa taarifa na sio kwamba nilifanya kusudi ila nilisahau sababu ya mambo yanayoendelea. Niliwaza ni busara nimtafute pindi kitakavyo rudi Dar ili tuongee, ila kwasasa nimuache atulie maana alionesha kuchukia waziwazi. Nilimpigia simu Jane kumjulia hali pamoja na mtoto na alisema anaendelea vizuri kabisa, na aliuliza nitarudi lini? maana amenimiss tayari.

Kwa upande mwingine wife alikuwa kanitumia ujumbe kwamba kuna plot nzuri ya kununua na tunaweza kulipa kwa awamu, alisema ni connection ambayo kapewa na mzee wake na ameshauri tuichukue maana ni potential sana na ipo Mapinga. Niliwaza pale nikaona wacha nirudi Dar kwanza ili nikaione, baada ya hapo ndo nitakwenda Dodoma kuendelea na mipango yangu.

Nilimpigia simu Iryn kwa mara nyingine tena, lakini hakuwa online na hapa sasa nilianza kupatwa na wasiwasi, nilijiuliza kwanini hapatikani? Kuna shida gani? Ni nini kinaendelea?, Au Iryn katoa mimba kwahiyo hataki usumbufu?.

Nilimpigia simu kaka Allen kumpa taarifa ya kinachoendelea kuhusu Iryn, lakini nae alinipa jibu jepesi sana, ‘eti nisiwe na wasiwasi atanitafuta tu’. Niliona bro! anazingua na sikutaka kumjibu chochote zaidi ningemvunjia heshima, nikamyamaza na kukata simu. Niliona kuendelea kumsikiliza ataniingiza shimoni, wacha nirudi Dar mapema, kisha nionane na Lucy, huenda tukapata solution.

Kuendelea kubaki huku Zambia na wakati sijui afya yake na mtoto, nitakuwa sifanyi jambo la busara, nikirudi Dar nitafanya maamuzi magumu hata ya kwenda huko Ethiopia.”

Niliplan kuongea na mzee badae akirudi ili nimpe taarifa ya kuondoka jumatano, kwa bahati mbaya hii siku alichelewa sana kurudi na kesho yake asubuhi aliwahi sana kuondoka. Niliwaza kumpa taarifa kwa simu, lakini niliona sio heshima, hivyo nilimtumia ujumbe kumpa taarifa kuwa nina maongezi na yeye baadae.

Saa 4 asubuhi tulindoka na Sandra kwenda mjini, nilitembea mfukoni na dolla 200 kwaajili ya kutusaidia njiani, tulipitia moja ya bureau de change nikampa afanye exchange na tulipata kwacha 4,000 na point.

Tulikwenda East Park Mall ambayo ipo Lusaka, kipindi tupo pale nilimpa offa ya shopping ya nguo mpaka viatu, na aliishia kufurahi sana maana hakutegemea hii surprise. Nilienjoy sana kuwa maeneo haya, kisha tulikwenda Manda Hill Mall ipo Lusaka pia, tuliingia moja ya mgahawa jina lake unaitwa Nando’s kwaajili ya kupata lunch.

Kipindi tunapata lunch tuliendelea kupiga story za hapa na pale kuhusu Zambia, kwa upande wangu nilikuwa namdodosa ili nimjue kiundani zaidi. Kupitia story nilibaini ni mkubwa kwangu kwa miaka 2, pia ana degree ya sociology na ameajiriwa na kampuni ambayo ilimpangia kazi pale home, lakini alisema amejishikiza bado anaendelea kutafuta ajira sehemu zingine.

Sandra alinitembeza maeneo mengi sana ya Lusaka na kwa upande wangu nilienjoy sana kampani yake na tulirudi home jioni sana, kwa lengo la kuwahi kupika chakula cha usiku. Baada ya kurudi home tulikuwa wote jikoni nikimsaidia kupika na nilimpa taarifa za kuondoka, lakini bado sijaongea na mzee.

Kwa upande wake alizipokea taarifa vibaya sana maana hakutegemea kuona nikiwahi kuondoka, alitamani sana niendelee kubaki Zambia, kwa kipindi kifupi tumetengeneza mahusiano na ukaribu.

Usiku tukipata chakula cha usiku, niliongea na mzee na kumpa taarifa ya kurudi Dar, ilikuwa ni taarifa ya kushtukiza, lakini nilimwambia ni mambo ya office ndo yanafanya nirudi mapema, pia, nina safari nyingine ya kwenda Dodoma.

Mzee kwa upande wake hakukubali mimi kuondoka kesho na alisema niondoke alhamis maana nimemshtukiza, sababu alijua nitaondoka weekend. Sikuweza kupinga, hivyo ilibidi nikubaliane na mzee niondoke siku ya alhamis, alinambia kesho kuna sehemu tutakwenda wote na tutaanzia kwanza ofisini.

Kesho yake saa 3 asubuhi tuliondoka pamoja kwenda ofisini kwake kuna vitu alisema anakwenda kuviweka sawa, baada ya hapo ndo tutaondoka kwenda hio sehemu.

Baada ya kuwasili ofisini kama kawaida mama alifurahi sana kuniona na aliishia kunikaribisha ofisini kwake kwaajili ya maongezi, yeye yuko department ya marketing.

Mama alikuwa akinijali sana, alinitengeneza kahawa akaniletea, kwa kumkadiria ni mama wa miaka 45 hivi mwenye asili ya Rwanda, alionekana kujipenda kuanzia uvaaji kwa ufupi ni mashallah!.

Tulikuwa tunapiga stori nyingi sana, maana alitokea kunikubali sana. Alisema huwa anakuja sana Dar es Salaam, hivyo atakuwa ananitafuta tuonane. Wakati wa mazungumzo, nilimgusia kuhusu familia yake, na akaniambia ana watoto wawili.

Nilianza kuwaza mbali sana, huenda mzee amejiweka hapa, kukaa Zambia kwa miaka 8 bila mchepuko haikumake sense kichwani, na kile kitendo cha mama kunijali nilikuwa nazidi kupata ukakasi.

Mchana tulitoka kupata lunch tukiwa wote watatu pamoja na mama, tulikwenda moja ya mgahawa wa karibu na ofisi;

MAMA: “Kijana wako ni mstaarabu sana anajitambua.”

MZEE: “Dume langu la kwanza nalitegemea hili, limenipa na mjukuu mkubwa.”

MAMA: “Ulinambia hili, amewahi majukumu maana vijana wengi wa age yake bado wanakaa kwao na wengine hawana direction.”

MZEE: “Kwahili kama baba najivunia sana.”

MAMA: “Insider embu nioneshe picha za mjukuu wangu nimuone.”

Nilitoa simu nikampa azione picha za Junior na aliishia kufurahi pale,

MAMA: “Anaonekana mjanja sana, nikija Dar nitakuja kuwasalimia.”

MIMI: “Karibu sana.”

Baada ya kupata lunch tuliagana pale, mama alikuwa anarudi kazini, alinitakia safari njema, tukapeana namba za simu. Kwa upande wake alitamani sana niende kwake nikapajue, lakini kutokana na muda isingewezekana.

Mimi na mzee tulikwenda moja kwa moja mpaka sehemu inaitwa Leopard hill, ulikuwa ni mwendo wa nusu saa hivi, njiani nilikuwa nashauku ya kujua mzee anataka kunionesha nini?.

Baada ya kufika eneo la tukio mzee alipark gari yake chini ya mti mkubwa, nilikuwa wakwanza kushuka kwa gari, nikaanza kushangaa mazingira. Eneo lilionekana kuwa na utulivu wa hali ya juu sana, nyumba zake zilionekana kuwa ni mpya na nyingine ujenzi ulikuwa ukiendelea.

Mijengo ilikuwa imesimama sana mazingira yake ni mazuri sana, kwa Dar es Salaam tunaweza kufananisha na Mbweni/ Kigamboni, jinsi ambavyo watu wanajenga majumba ya kifahari.

MZEE: “Nimekuleta hapa ili uone kiwanja nilichonunua, nina mpango wa kuanza ujenzi mwezi wa 6 na familia yote itakuja huku.”

MIMI: “What? Unataka umtoe mama kule mkoani aje huku?”

MZEE: “Ni mke wangu yule, hata kukaa nae mbali haitakiwi ndomana nikapata wazo nimalize ujenzi ili nimchukue tuishi huku na wadogo zako wale wadogo.”

MIMI: “Na nyumba ya kule mkoani itakuwaje?”

MZEE: “Tutapangisha au wewe ukitaka ukakae ni sawa, kwasasa wewe sikuhesabii maana unafamilia tayari.”

MIMI: “Ni kweli mzee.”

Tuliendelea kuangalia kiwanja pale na ukubwa wake ulikuwa ni ekari moja na kimezungushiwa senyenge.

“Bei za viwanja huku zikoje? Kwa haya mazingira nahisi bei zitakuwa juu sana.”

MZEE: “Kwa maeneo ya huku viwanja viko juu sana hasa miaka ya hivi karibuni, asilimia kubwa wageni na matajiri ndo wanajenga sana huku. Mimi nilinunua hiki kiwanja toka 2018, huku kulikuwa bado porini, kipindi kile viwanja vilikuwa ni cheap sana, na aliyenisaidia mpaka napata hiki kiwanja ni Manager wetu ila hayupo, amekwenda likizo.”

MIMI: “Ni kizuri sana, kwahiyo maisha yako yote utamalizia huku Zambia?.”

MZEE: “Nimeshakaa miaka 8 huku, tayari ni nyumbani, sioni sababu ya kurudi Tanzania.”

Tulishinda pale mpaka jioni maana mzee alikuwa anafanya vipimo vyake, mimi haya mambo sijui kwakweli, nilikuwa namsaidia tu pale huku tunapiga story za hapa na pale.

Baada ya kumaliza tulikwenda moja ya bar tukatulia kwaajili ya kupata dinna na kupata moja mbili tatu, story na mzee ziliendelea;

MZEE: “Ninafurahi kuona umekua mtu mzima sasa na una akili ya maisha, na ushukuru sana Mungu umepata mke mzuri na anayejitambua. Sikuzote familia bora inaanzia kwenu nyinyi wawili, mkishindwa kuelewana na kuishi vizuri, mtatengeneza kizazi cha hovyo sana.”

MIMI: “Ni kweli mzee kwa hili upo sahihi kabisa.”

MZEE: “Kuwa makini sana na wanawake wa nje, watakuharibia familia yako usipokuwa makini.”

Nikajisemea mzee anaongea nini sasa;

MIMI: “Siwezi kufanya mistake kwenye hili jambo, ahsante kwa ushauri.”

MZEE: “Wewe ushakuwa mtu mzima tayari na unaonesha njia nzuri kwa wadogo zako, naomba muendelee kupendana na kushikamana kama ndugu, hata pindi sisi hatupo duniani, bhasi familia inakuwa ipo sehemu salama.”

MIMI: “Sawa mzee kwa hili ondoa wasiwasi, lazima nihakikishe madogo nao wanatoboa.”

MZEE: “Violet ni dada yenu msimtupe pia, hata kama kaolewa, ni binti yangu, muendelee kuwa pamoja. Nina mpango Pasaka hii au ikishindika Christmas tukutane pamoja kwaajili ya kusherehekea.”

MIMI: “Ni wazo zuri, sisi hatuna shida tunakusikiliza wewe, nina ratiba ya kwenda home na familia Pasaka hii.”

MZEE: “Nitaangalia ratiba zangu, kisha tutawasiliana.”

MIMI: “Ahsante sana mzee mimi nimefurahi sana kukuona na kukaa hivi pamoja, ni muda mrefu sana umepita.”

MZEE: “Huku tumekuwa na muda wa kukaa sana pamoja, kipindi kile Dar nilikuwa nina haraka sana.”

MIMI: “Inshort nime enjoy sana, niwe mkweli na nimetokea kukupenda sana huku.”

MZEE: “Suala la mipango ya kufanya biashara huku, subiri kwanza mama yako aje ili iwe rahisi kukuangalizia project zako na zangu pia.”

MIMI: “Hili wazo zuri sana, tuendelee kuomba uzima naamini penye nia pana njia.”

MZEE: “Nikuombe sana ukawe baba mzuri kwenye familia yako, hakikisha Junior anakua katika misingi yako, malezi ya sasa yanachangamoto sana, ukifananisha na zamani. Heshima ya mwanaume ni familia na watoto ndo baraka, kama mimi navyojivunia sasa kuwa na wewe, badae iwe wewe kwa Junior.”

Tuliongea mambo mengi sana na mzee, kwa upande wangu nilikuwa nimepata kitu kikubwa sana kutoka kwake, na sikujutia kuja Zambia. Mzee alinishauri mambo mengi sana muhimu na ya msingi na tuliishia kuondoka kurudi home ili nikajiandae kwaajili ya safari.

Kesho yake niliwahi kuamka kwaajili ya kujiandaa na safari maana nilikuwa nategemea kuondoka na flight ya saa 8 mchana. Asubuhi Hilda anilipigia simu kunipa taarifa kuwa anaona kampuni inamuelemea sana, kwani anaona ofisi haina muelekeo. Habari nyingine mbaya aliyonipa ni kuhusu stock, ilikuwa inaishia afu hajui kama mzigo umeagizwa au laah, niliona ni changamoto sana, hivyo nilimwambia najiandaa kurudi Dar, na pindi nitakavyo land, nitamtafuta ili tuongee.

Nilimuachia ofisi Hilda katika kipindi kigumu sana ukizingatia hana experience ya kutosha, mbaya zaidi maboss wote mpaka mimi hatuko katika maelewano mazuri. Nilifikiri sana nikaona kuna haja ya kufanya something ili kuinusuru kampuni katika kipindi hiki kigumu.

Mzee aliondoka mapema kwenda kazini, alisema atarudi mapema kunichukua kunipeleka airport, hivyo niendelee kujiandaa. Kwa upande mwingine Sandra alikuwa amefika home na nilianza kupiga nae story za mwishomwisho huku namsubiri mzee.

Sandra kwa upande wake alikuwa haamini kama kweli naondoka leo, ukizingatia ndani ya muda mfupi tuliokuwa pamoja tulishakuwa na mahusiano mazuri sana. Nilimwambia siku aje Dar kutembea na apajue home, aliishia kukubali na alisema atafanya hivo, alisisitiza sana nisimdanganye kwa hili maana hajawahi fika Dar.

Saa 6 mchana mzee alirudi kunichukua, kabla ya kuondoka nilimuaga Sandra kwa kumkumbatia, tukabadilishana namba za simu na nikaondoka. (Sandra ni moja ya marafiki zangu wakubwa sana mpaka sasa, ameshaniconnect na rafiki zake wengi sana ambao wanakuja Dar).

Tuliondoka kwenda airport baada ya kuwasili, mzee aliomba nimpe akaunti yangu ya bank ili aniwekee pesa za matumizi ya mjukuu wake. Nilimpa akaunti ya Junior ili aziweke pesa huko maana zilimlenga yeye hivyo, sikuona sababu ya kuziweka kwangu.

Mzee aliniaga maana alikuwa anawahi kurudi kazini na mimi nikaenda kucheck in, lakini sasa niliambiwa ndege itachelewa kuondoka na itabidi tusubiri kwa masaa 2. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kushangaa pale airport, baada ya masaa 2 na nusu ndo tulianza safari ya kurudi Dar, tuliwasili JNIA saa 2 za usiku, nikarequest bolt na kuanza safari ya kurudi home.

Baada ya kurudi home jambo la kwanza kufanya, nilimpigia simu Hilda kumpa taarifa kuwa nimerudi na kesho tutaonana kwaajili ya maongezi.
*****
cacutee baby love
Watu8 mwana mzigo full huu hapa
 
kiukweli dada yako anaakili sana nami nimeishia kumpongeza sana
 
SEASON 02
EPISODE 25

“BY INSIDER MAN”

CONTINUE:

Kesho yake nilichelewa sana kuamka ni Junior ambaye alikuja kuniamsha chumbani kutokana na fujo zake na ile kuangalia muda ilikuwa ni saa 5 asubuhi.

Kwa upande mwingine mzee alikuwa kaningizia pesa ya Junior aliyokuwa ameahidi na alinitumia ujumbe niigawe na kwa mama yake. Sandra naye hakuwa mbali kunitumia message kuuuliza kama nimefika salama na palepale nilimjibu nimefika salama, nikaingia bafuni kuoga.

Kipindi najiandaa simu yangu ilianza kuita alikuwa ni baba mkwe, nilipokea ili nimsikilize, lakini nilijua lazima ni suala la plot. Baada ya maongezi ya muda mfupi tulikubaliana tukutane ili twende huko Mapinga mapema.

Muda mchache mbele niliondoka kuelekea ukweni, kumpitia baba mkwe na bila kuchelewa tulianza safari ya kwenda mapinga ilikuwa ni mbele kidogo ya Bunju. Mhusika mwenye plot muuzaji, alikuwa yupo tayari eneo la tukio akitusubiri, ambaye ni rafiki wa baba mkwe.

Plot ilikuwa nzuri sana, imepimwa tayari, ipo kwenye eneo zuri karibu na Barabara ya Bagamoyo na ina ukubwa wa sqm 1600. Nilipapenda na nikaomba kupewa bei elekezi, mhusika alisema naweza kulipa kwa awamu 4, lakini awamu ya kwanza lazima nilipie nusu ya gharama.

Tuliondoka kwenda kukaa moja ya bar pale Bunju mwisho kwaajili ya maongezi zaidi na tulikubaliana 23M nikafanya malipo nusu kabisa, sikuwa na wasiwasi wa kuita serikali za mtaa sababu biashara ni ya kindugu.

Kuhusu mkataba wa kuandikishana na kukabidhiana hati ya kiwanja, tulikubaliana kuwa mpaka nitakapomaliza kiasi kilichobaki, hati itakuwa chini ya uangalizi wa baba mkwe. Nilikuwa na imani kubwa na baba mkwe kwa kuwa ndiye msimamizi wa kila kitu, hivyo niliamini asingeweza kuniingiza chaka, na alinihakikishia uhakika wa 100%.

Kufikia saa 9 mchana tulikuwa tumemaliza kila kitu, hivyo tuliondoka kurudi home, kisha nikaanza kumshusha baba mkwe nyumbani kwake, lakini aliomba niingie ndani ili tufanye mazungumzo kidogo.

Kwa upande wake alinipongeza sana kwa hatua niliyoichukua na aliendelea kunishauri kwamba, kwenye ile plot nigawe nusu, kisha nijenge sehemu ya kuishi na nusu inayobaki nijenge nyumba za kupangisha. Nilitumia lisaa pale ukweni, kisha nikaanza safari ya kwenda Masaki kuonana na Hilda maana alikuwa ameshaanza kunipigia simu kwa fujo sana.

Niliwasiliana na Hilda tukutane Olive kwaajili ya maongezi na baada ya nusu saa alinipa taarifa kuwa amefika eneo la tukio tayari, hivyo ananisubiri mimi tu. Kwa upande wangu nilichelewa kama dakika 10 hivi kufika eneo la tukio, baada ya kuwasili tulisalimiana na tukaanza mazungumzo pale;

HILDA: “Nambie Insider za huko Zambia, hope umeenjoy.”

MIMI: “Na enjoy wapi wakati umenitoa huko kwaajili yako.”

HILDA: “Pole sana lakini mimi sielewi kabisa, nafikiri hata kuacha kazi, mmenisusia kampuni na sijui kinachoendelea, simu zenu wote hampatikani.”

MIMI: “Pole sana mummy, ni kweli hatuko kwenye maelewano mazuri, lakini sioni sababu ya wewe kuacha kazi hasa kwenye kipindi hiki cha mpito.”

HILDA: “Kampuni ikifeli si lawama zote zitakuja kwangu?, kuhusu suala lako la kwenda likizo si mama wala Iryn aliyenipigia simu na uliezea kuwa kampuni ipo kwenye mikono yangu.”

MIMI: “Najua unachopitia Hilda, nikutoe wasiwasi tuko pamoja na kila kitu kitakwenda sawa.”

HILDA: “Kampuni haina cash nashindwa kufanya manunuzi madogo madogo, stock inaisha na hakuna taarifa yoyote kama mzigo umeagizwa au laah!, mama hapatikani kwa simu na nguvu ya kumpigia Iryn nakosa sababu hausiani na mimi ni wewe ndo wakuwasiliana nae.”

MIMI: “Mama atakuwa field, nimeongea na Sumaiya na yeye ni muda mrefu hawajazungumza, si unajua kazi yake asilimia kubwa anashinda kwenye majanga?.”

HILDA: “Hio ndo changamoto, sasa tunafanyaje?.”

MIMI: “Stock imebaki kiasi gani? na account Receivable inasomaje?.”

HILDA: “Stock iliyobaki asilimia kubwa ni zile product expensive ila kwa bei za kawaida sidhani kama itaweza kufika week 2 na itadepend na volume ya wateja.”

MIMI: “Sawa sasa nisikilize, kuanzia leo ukifanya mauzo ya cash usiweke bank ili hizo pesa zisaidie kurun office, kingine wahimize customers walipe kwa cash ili iwe advantage kwetu.”

HILDA: “How naweza kumwambia mteja asilipe bank na amezoea kutransfer moja kwa moja kwa account?”

MIMI: “Ni simple tu, customers huwa wanapiga simu kufanya booking, kwahiyo palepale mwambie tuna accept na cash pia, inaweza kufanya kazi na kutusaidia.”

HILDA: “Vipi na kuhusu stock?”

MIMI: “Huko tutafika bado sijamaliza, hujanijibu kuhusu madeni tunayodai kwasasa ni kiasi gani? Ambayo wewe umeyaandikia.”

HILDA: “Ni kama million 3 na something hivi.”

MIMI: “Kipindi nakukabidhi office receivables zilikuwa 67M nikijumlisha na hio ni 70M, Kampuni X na Y zimelipa tayari na mara ya mwisho kuangalia deni, limepungua mpaka 24M pamoja na deni lako. Sasa hawa waliobaki mimi nitaongea nao ili walipe kwa cash, hatuwezi kushindwa hili jambo.”

HILDA: “Vipi kuhusu stock?, ikiisha hatutaweza kuendelea na kazi, na mishahara itakuwaje? Mwezi uliopita ilichelewa.”

MIMI: “Kuhusu mishahara kama mambo bado hayaeleweki, nitaangalia means ya kufanya hata cash naweza kuwalipa. Kuhusu stock niachie hili nilifanyie kazi na nitakupa majibu soon, acha niwasiliane na dada agent huenda anamzigo.”

HILDA: “Mmh sawa, lakini nikiangalia interval ya mzigo wa mwisho kuupokea na sasa, naona kama hakuna taarifa yoyote, angekuwa amekupigia simu.”

MIMI: “Upo sahihi, lakini tutajua tunafanyaje ndomana nimekwambia hili niachie mimi.”

HILDA: “Sawa Insider nimefurahi kukuona.”

MIMI: “Mimi pia, naomba tusaidiane hili jambo hii kampuni isifie kwenye mikono yetu.”

Hilda aliishia kufurahi pale sababu nilikuwa nina ratiba zingine ilibidi nimuage lengo niwahi kwa Lucy, tuliongozana mpaka parking tukaagana kwa kumbatiana, kisha nikaondoka kuelekea Mikocheni.

Nilikuwa na ratiba ya kuonana na Lucy tangu asubuhi, ratiba ziliingiliana wakati niko njiani Lucy alipiga simu na kuuliza niliko na alihimiza nifanye haraka tukaongee kuna jambo.

Baada ya lisaa niliingia kwa kuchelewa sana pale ofisini sababu ya foleni na wakati nikishuka kwa gari, nilimuona Lucy anakuja usawa wangu na alikumbatia kwa nguvu sana, nilihisi akilia;

MIMI: “Lucy mbona unalia kuna shida gani?.”

LUCY: “Insider nimeongea na Iryn sio muda mrefu sana, amefanya maamuzi ya kufanya abortion.”

MIMI: “Nini? Sikuelewi amefanya au bado?”

LUCY: “Bado sijui kama amefanya au laah! anasema ameshindwa kabisa kuhandle upinzani anaoupata kutoka kwa familia yake, na wewe pia hueleweki kama upo upande wake na hili ndo linampa wasiwasi, kitu kingine alikupa masharti ya mtoto, lakini umeshindwa kuyafuata na umetembea na Asmah.”

MIMI: “Amekutafuta kwa namba ipi?”

LUCY: “Nimeongea sana na namba yake, nikijaribu kukuombea msamaha, lakini amenigomea. Anasema hawezi kurudisha tena imani yake kwako, hasa baada ya kutarajia kuwa mngekuwa pamoja katika kipindi hiki cha upinzani anachopitia. Lakini wewe umekuwa ukimpa majibu mepesi, ukionesha wazi huna mpango naye tena pamoja na mtoto, hata kama alifanya kwa reason zake. Insider, nimelia sana na nakuonea huruma mshikaji wangu. Sitaki kuamini kwa kipindi chote mlipokuwa na Iryn, mambo yanamalizika kwa njia mbaya hivi. Nimemwambia kuwa, kama atathubutu kufanya ujinga huu, nitaacha kazi."

MIMI: “Jimmy alinambia Iryn anamaamuzi magumu sana na mpaka amesema hivo jua kweli kadhamiria, na huwa habadili mawazo yake, uzuri unamjua ni mtu wa aina gani, ooh shit.”

LUCY: “Hapana embu mpigie before it’s too late, jaribu kuongea nae muda unaenda.”

Nilitoa simu ili nimpigie na nikakutana na ujumbe kutoka kwake ambao umetumwa dakika 5 zilizopita na ulisomeka;

Hello Insider, it’s been a while. I hope you’re doing well. I want to tell you that I don’t hate you. Please know that you’re the most important man I’ve ever met in this world. I truly appreciate your contribution and everything you have done in my life.

Please understand that I am currently going through a very difficult time due to this pregnancy, especially when it comes to my siblings. All of them have been against me, and even worse, you, who I relied on to be close to me during this period, have distanced yourself from me.

I have chosen the side of my family because I don’t see any future with you, and you have shown no intention of wanting this child. I don’t like doing this, but I also want to avoid the problems that might arise later, especially for your family. I carried this pregnancy for my own reasons, and I am choosing to end it for my own reasons.

I am truly sorry for this and wish you all the best.”

Nilihisi kuishiwa nguvu na niliegemea kwenye gari hata sikujua nafanya nini muda huu na chozi lilianza kunitoka.

Wanasemaga mwanaume hatakiwi kutoa chozi, nikwambie unakuwa bado hujaingia kwenye 18, nilifungua mlango wa gari kwa haraka sana nikaingia ndani, kisha niliwasha gari kuondoka eneo hili.

Lucy alianza kuniita na kunigongea dirishani;

“Insider nini kinaendelea? Mbona umebadilika ghafla sana?”

Sikuwa hata nikimsikia Lucy, zaidi nilianza kuondosha gari na kumwacha kwenye mataa bila kujua afanye nini kwa wakati huu.

Haikukuchukua muda nilisikia simu ikiita, lakini sikuwa na habari nayo na niliendesha gari nikaja kuipark mbele kidogo ya shule ya Alpha, kama unaelekea Cocacola road, kuna maduka pale pamechangamka sana.

Nilipark gari maeneo haya nikatulia maana sikuwa najielewa huku nikihisi mwili kufa ganzi, machozi mazito yalikuwa yametanda kwenye mboni zangu. Nilikuwa kwenye dimbwi zito la mawazo, nilijiona ni mwanaume ambaye sina bahati, maisha yangu ni kama yamejaa na mikosi, ukizingatia nakwenda kumkosa mtoto kwa mara ya tatu.

Niliwaza mbali sana, nikajisemea ‘au Mungu ananiadhibu kwa kuchepuka?‘ Ni mtoto wa tatu sasa kwa jumla namkosa, before Prisca na Iryn, huko nyuma kuna tukio lingine lilitokea.

Nilichukua simu yangu nikaona calls kutoka kwa Lucy, ndo alikuwa akinipigia muda ule na nilitafuta namba ya Iryn, kisha nikafungua whatsapp ili nimpigie, lakini namba ilikuwa deactivated na normal call hapatikani.

Nilikuwa katika wakati ambao sijui nifanye nini maana nilikuwa dilemma, niliwaza nimpigie simu mama Janeth nimuombe anisaidie hili, nikakumbuka nae hapatikani.

Muda huu wazo lilinijia niende kwa sister yangu Arusha, nikamwambie kuhusu hili suala, kumpigia simu na kumwelekeza isingetosha, niliona sinabudi kwenda huko na nilimpigia simu palepale kumpa taarifa.

SISTER: “Nambie kaka yangu unaendeleaje.”

MIMI: “Dada niko njiani nakuja Arusha, nina maongezi na wewe muhimu.”

SISTER: “Mdogo wangu si nilikwambia nikipata likizo ndo uje au umesahau?”

MIMI: “Dada ni muhimu sana haya maongezi, tafadhali.”

SISTER: “Kuna nini kinaendelea mdogo wangu? Umeshagombana na mama J?”

MIMI: “Dada naomba nielewe, nikifika huko utaelewa ni nini nataka kukwambia.”

SISTER: “Sawa karibu, utakuwa unaniambia safari ilipofikia, pole sana.”

Nilijifuta machozi yangu vizuri, kisha nikaondoka kurudi home kwaajili ya kuchukua vitu na kuanza safari ya kwenda Arusha. Nikiwa njiani nilimpigia simu dada Tyna kumuomba kama nitaweza kupata ticket ya kwenda Arusha, akanambia haiwezekani labda kwa kesho asubuhi.

Niliona kwa asubuhi ni mbali sana wacha niondoke hata kwa kuunga cha msingi nifike Arusha. Nilirudi home, kisha niliingia ndani kwa spidi sana, akina wife walikuwa pale seblen hata sikuwasalimia maana nilikuwa na spidi ya hatari.

Wife alikuja chumbani na alinikuta ninaweka nguo kwenye bag kwaajili ya kuondoka na alianza kuniuliza pale;

“Baba J, una safari ya wapi tena?”

“Nakwenda Arusha mara moja kuonana na sister.”

“Are you okay? Mbona kama macho mekundu ulikuwa unalia? Kuna nini kimekupata?”

“Nothing, mummy usiwe na wasiwasi na mimi.”

“Jana tu! Umerudi kutoka Zambia kwanini usingesubiri hata kidogo ukaenda huko siku nyingine?”

“Ni muhimu sana ndomana nakwenda sitakawia kurudi.”

“Kuna jambo gani huko?.”

“Ni masuala ya kifamilia, nikirudi nitakwambia.”

“Mhhh! Sawa.”

Wife alikubali kwa shingo upande nami niliendelea kupanga vitu vyangu kwa haraka sana. Kwenye bag nilikuwa nina balance ya $1,800 ambazo zilibaki kutoka Zambia na nilitembea na cash Tsh 500,000.

Nilichukua bodaboda kwenda Tegeta-Kibo kutafuta gari za kwenda Arusha na ile nafika nabahatika kupata gari ya kwenda Moshi. Saa mbili usiku tulianza safari ya kwenda Moshi na njiani nilikuwa ni mtu mwenye mawazo sana, nilikuwa natamani hata gari ipae ili tu! nifike mapema.

Saa 8 za usiku tuliwasili Kilimanjaro, nikabahatika kupata gari ya tour inayoenda Arusha, sikutaka kabisa kumsumbua sister maana ni mke wa mtu, hivyo niliplan kumpigia simu asubuhi.

Ulikuwa ni mwendo wa lisaa mpaka tunafika Arusha na jamaa alisema anaishia USA river, kutokana na mimi kuwa mgeni alinipeleka kwenye moja ya lodge ili nilale.

Kufika pale reception naambiwa room zipo ila sasa gharama zake ni za ajabu room ni elfu 90, nilishangaa sana, kwa lodge unalipia elfu 90? Ukizingatia nina masaa yasiyozidi 5 kulala. Muda ulikuwa umeenda sana, hata jeuri ya kutafuta lodge zingine sikuwa nayo afu ni mgeni na maeneo ya huku, kwanza niliogopa vibaka maana Arusha ina scandal nyingi sana.

Nilitoa pesa nikalipia na dada pale reception alianza kujichekesha chekesha, lakini mimi sikuwa hata na habari nae zaidi nilikuwa na mawazo kichwani. Nilioneshwa room yangu na kabla ya kulala nilimpa taarifa sister, kuwa nimefikia salama na nipo lodge ya Mzunguu, USA River.

Niliamka saa 2 asubuhi na kabla ya yote nilicheki simu kuangalia kama dada amenipigia maana simu ilikuwa silent. Baada ya kuangalia nilikuta kweli amenipigia mara 2 na alinitumia ujumbe kunambia nikiamka nimpigie. Kwa upande mwingine mama J nae alikuwa amenipigia simu za kutosha na kutuma message juu, kuuliza kama nimefika salama.

Nilianza kwa kumpigia simu sister, akasema yupo ofisini anaweka mambo sawa, atakuja saa 3 kunichukua lodge. Kisha nilimpigia simu wife, lakini hakupokea na nikamtumia ujumbe kumjulisha nimefika salama Arusha.

Niliingia bafuni kuoga kabisa ili sister akija anikute niko tayari, wakati nikijiandaa simu yangu ilianza kuita, ni Lucy alikuwa akipiga na nilipokea simu yake ili nimsikilize na tulianza maongezi pale;

LUCY: “Insider unaendeleaje?”

MIMI: “Salama Lucy, nashukuru Mungu.”

LUCY: “Jana umeondoka ukaniacha niki hang na simu ukawa hupokei, nini kinaendelea?”

MIMI: “Acha tu, kuna ujumbe mbaya alinitumia kwamba anafanya abortion na mpaka sasa hapatikani hata whatsapp ameifunga.”

LUCY: “Pole sana, wewe upo wapi sahivi?”

MIMI: “Naongea na wewe niko Arusha now.”

LUCY: “What? Umeenda muda gani? Na kuna nini?”

MIMI: “Jana baada ya kuachana nilirudi home, kisha nikaanza safari na nimekuja huku kwaajili ya kuonana na dada yangu.”

LUCY: “Jamani, mmeshaonana tayari?.”

MIMI: “Bado Lucy, nimeingia late sana na soon tutaonana.”

LUCY: “Ngoja niendelee kutafuta means ya kumtafuta Iryn kwa namba nyingine, lakini nataka kuacha kazi Insider.”

MIMI: “Uache kazi kwasababu gani?”

LUCY: “Nimemwambia jana naacha kazi kama atatoa mimba, nitakuwa nimekusaliti kama nitaendelea kufanya kazi chini yake.”

MIMI: “Usifanye maamuzi yoyote mabaya mpaka nitakavyo rudi sawa?”

LUCY: “Sawa! see you then.”

Saa 3 ontime sister alikuwa amefika pale lodge na alinipigia simu kunipa taarifa kuwa yuko parking, nami nilitoka kwenda kuonana nae, alishuka kwenye gari na kunikumbatia pale. Ni miaka 2 ilikuwa imepita bila kuonana na sister na mara ya mwisho kuonana ilikiwa siku ya engagement ya mama J.

Nilirudi ndani kuchukua vitu pamoja na kusign out. Baada ya kurudi, sister alisema tunakwenda kwake, lakini mimi nilimgomea.

SISTER: “Unamaana gani hutaki kwenda kwangu?”

MIMI: “Dada yangu naomba tutafute kwanza sehemu tukae, kisha tuzungumze.”

SISTER: “Sawa! Twende Charity hotel tukazungumze pale tupate na breakfast.”

Tulikwenda Charity hotel ambayo ipo Sakina, palikuwa na kamwendo kutoka USA river mpaka hotelini, na baada ya kuwasili tulikaa nje, na kila mtu aliishia kuagiza anachotaka kula.

SISTER: “Mama J kanipigia simu jana, wewe ulimuagaje home?”

MIMI: “Nilimwambia nakuja kuonana na wewe kwaajili masuala ya kifamilia, ulimjibu nini?”

SISTER: “Nilimwambia ukirudi utamwambia, sikujua hata cha kumjibu na sikutaka kumuacha kwenye question mark.”

MIMI: “Ulifanya vema, sasa dada yangu mpaka nimekuja huku naomba utambue napitia kipindi kigumu sana, hili jambo naloenda kukwambia hakuna mtu yoyote kwenye familia anaejua. Kwa bahati mbaya ninakushirikisha leo, lakini mambo yameshaharibika tayari, wish ningekwambia mapema.”

SISTER: “Kuna nini bro! embu niambie hii itabaki kuwa siri yangu na wewe.”

Alikaa mkao kuonesha kwamba yuko tayari kunisikiliza, nami nikaanza kumsimulia mkanda mzima kuhusu Iryn, jinsi tulivyokutana, tukaanza kujihusisha kimapenzi hadi kupelekea kupata mimba, na mambo yanayoendelea sasa, bila kusahau ukaribu wake na mke wangu.

Baada ya kumaliza kumsimulia mkanda mzima, sister alishusha pumzi ndefu sana na aliishia kusikitika pale;

SISTER: “Daah! Hizi habari kweli ni nzito, simpatii picha wifi yangu akija kujua hii siri, sijui kama utanusurika this time. Bro! unashida gani mpaka unashindwa kucontrol hisia zako?unaenda mbali na kumpa mimba, what are you doing?”

MIMI: “Nimekosea ndio, lakini nimeshakueleza kuwa alibeba mimba kwa reason zake, mtoto anabaki kuwa damu yetu, hatuwezi mkataa.”

SISTER: “Hata hivyo, mimi bado nina wasiwasi na zile dawa alizokupa Masai nahisi huenda kuna kitu alikuwekea, umekuwa mtu wa kupenda penda hovyo au sababu ya kuchelewa kuwajua wanawake?.”

Sister yangu kaplay part kubwa sana ya kunifanya kuwa mwanaume rijali, alinisaidia mambo mengi sana mpaka nikawa sawa, miaka 8 nyuma.

SISTER: “Bro! ifike stage ujicontrol, haya yote unayofanya ipo siku yatakurudia wewe na utakuja kujuta kwenye maisha yako yote, mimi kama dada nimeumia sana juu ya mama J. Mtoto wa watu yuko loyal sana kwako, anakupenda, ametulia na hana mambo mengi ila wewe sasa, Mungu akusaidie.”

MIMI: “Ni kweli nimezingua dada yangu hata mimi najisikia vibaya sana, lakini naomba tushauriane juu ya hili suala, haya mambo mengine tutaongea tuanze kwanza na hili, ndomana nimekuja kwako.”

SISTER: “Umefanya ujinga wako afu sahivi unaomba ushauri, mbona hukuomba ushauri kipindi unaanza?. Okay, ulikuwa Zambia kwa baba, why hujamwambia kuhusu hili?. Brother kwa hili sina cha kukushauri na kama anataka kufanya abortion, ni bora akafanya hivo maana huko mbeleni utakuwa kwenye wakati mgumu sana.”

MIMI: “Sawa nashukuru kwa kunipa lawama zote, lakini tambua hakuna binadamu asiyekosea.”

SISTER: “Insider, unavyofanya ujinga kama huu naomba fanya kwa interest zako, lakini kaa ukijua kwamba mambo yakiharibika ni kwa faida yako, dont ever try to contact me again. Wewe tayari ni mtu mzima unajua ni nini unafanya, hufanyi kwa bahati mbaya, tusipotezeane muda. We done here, naenda washroom nikirudi tunaondoka kwenda home.”

MIMI: “Mimi siwezi kwenda home nitarudi Dar maana sijaja huku kwa lengo la kukutembelea.”

Sister alinikataa na hiki kitendo kilizidi kunipa mawazo, ukweli sister na mama J ni marafiki sana na humwambii kitu kuhusu uhusiano wao. Dada yangu alikuwa sahihi kuchukia kwa hili jambo nililofanya, ukizingatia nilishakuwa nimetoa ahadi huko nyuma ya kutofanya tena, huu ujinga.

Niliinamia meza huku nikiendelea kuwaza next move, lakini sikuwa napata jibu, hivyo niliona wacha nirudi Dar nikaendelee na mambo yangu.

Baada ya dakika 15 Sister alirudi kutoka washaroom na alianza tena kuongea na mimi pale;

SISTER: “Bro! nioneshe message aliyokutumia jana, niisome na mimi.”

Nilitoa simu nikamuonesha na alinyamaza kwa dakika 10 bila kusema kitu chochote, kisha akaendelea;

“Kipindi niko washroom nilikuwa nafikiria hili suala, kwa maelezo yote uliyonipa nikweli dada anakupenda, na hii message aliyokutumia amecheza na mind yako, kuna ujumbe hapa amekuandikia ila umeshindwa kuutambua.”

Dada yangu anajua mambo ya saikolojia, maana anafanyia kazi moja ya NGO kubwa ya kimataifa kule Arusha, sasa baada ya kunipa hizi habari nilishindwa kumuelewa na nilichukua simu ili niusome ujumbe tena kwa makini, hata hivyo sikuelewa kitu.

MIMI: “Mimi sioni chochote hapa dada, labda unambie umeona nini?.”

SISTER: “Ujumbe wa hapo upo clear kabisa ni hivi, dada yuko kwenye kipindi kigumu hasa kwa upande wa familia yake, wewe ulishindwa kumshawishi toka mapema, kwa hapa ulifeli. Before unakumbuka nilikwambia kwamba wanawake tunapenda kudanganywa? Ni kosa kubwa sana kumwambia mwanamke ukweli, kwa ufupi hatupendi ukweli.”

MIMI: “Kwahiyo unataka kusema nilikosea kumwambia ukweli? Ningemdanganya namuoa huoni kama ingekuja kuleta matatizo huko mbeleni?”

SISTER: “Hili jambo lilitakiwa kuisha hata hayo mambo ya Ethiopia usingeenda, ndomana nakwambia ulishindwa kucheza na akili yake tu. Na kama ungenishirikisha mapema hili suala lingekuwa limeisha, sahivi tungekuwa tunajadili namna ya kudeal na mama J.”

MIMI: “Nilitakiwa kufanya nini hapo.?”

SISTER: “Nakupa mfano, kisha utanijibu. Una mtoto wako wa kike, anakuja kwako kukwambia ana mimba, na kapewa na mume wa mtu, utamuelewa?”

MIMI: “Hapana siwezi asee, nitamlamba makofi ya kutosha.”

SISTER: “Uli expect na yeye angekuwa na confidence ya kuongea hivo mbele ya familia yake?.”

Nilinyamaza kimya muda huu;

“Brother ulitakiwa kuisoma akili yake inataka nini kwa kipindi hiki, ulipaswa kumuonesha mpo pamoja no matter what, ulipaswa kumuonesha unampenda sana hata kwa kupretend na kitendo cha kumpiga hotelini, hapa pia ulikosea sana.”

MIMI: “Alinipanda sana kichwani ndomana nilimchapa vibao, nilimuomba msamaha lakini.”

SISTER: “Ulishindwa kutambua ni mjamzito, na ile haikuwa sababu ya kumpiga, shida yako unahasira za haraka sana.”

MIMI: “Ni kweli nilikosea ile siku, lakini bado sioni kama sababu ya kufanya abortion.”

SISTER: “Mpaka sasa, dada anaonekana kuwa upande wetu, lakini bado anajifikiria kuhusu kufanya abortion. Inaonekana nguvu ya familia yake ni kubwa zaidi kuliko ya upande wetu, na mara nyingi, upande wenye nguvu zaidi hushinda. Dada ameona kuwa huna future kwa sababu umeshindwa kumjali katika kipindi hiki kigumu anachopitia. Huu ulikuwa wakati mzuri wa kumuonesha upendo, lakini badala ya kumsaidia, wewe umekuwa against naye wakati ulipaswa hata kwenda South Africa kumsalimia kama kweli ungetaka mtoto. Dada alikuamini, lakini sasa anaona unaweza kuharibu future yake na kumfanya apoteze ndugu zake kwa sababu yako, mtu ambaye si wa kutegemewa."

MIMI: “Conclusion ni nini dada yangu? maana nahisi kuchanganyikiwa hapa kuhusu huyo mtoto bora hata angekuwa anapatikana kwenye simu.”

SISTER: “Huo ujumbe dada aliotuma kwako, ameandika kwa kumaanisha, ni kama amekupa last chance ya wewe kumtafuta, sasa tumia akili tunampataje?”

MIMI: “Hapa ndo mtihani kujua aliko kati ya South, Ethiopia na Ufaransa, lakini anapendelea sana kwenda Ufaransa kwaajili ya mapumziko.”

SISTER: “Dada bado yuko South Africa, kwenda Ethiopia kwa familia kwa kipindi hiki ni ngumu, atleast Ufaransa, kama alitumia namba ya South kukutafuta bhasi yupo huko. Tuna siku moja tu imebaki ambayo ni kesho, ya kwenda South Africa kumtafuta ili tuyaweke sawa haya masuala, tukichelewa tutamkosa mtoto.”

MIMI: “What? Twende South Africa?”

SISTER: “Ndo maana yake, we are running out of time, let’s go, tuanze mchakato wa kufanya booking ya flight mapema.”

MIMI: “Sister taratibu kwanza, tukienda huko tunampataje? Anaishi Capetown lakini sijui address zake.”

SISTER: “Come on, tutakwenda kuulizia chuo anachosoma na tutampata, lazima tutapata contacts za watu wake wa karibu.”

Sister alikuwa kaongea point tupu, ukweli mimi nilikuwa sijitambui kabisa muda huu maana akili yangu ilikuwa imevurugwa sana.

MIMI: “Sawa na vipi kuhusu permits tutafanikisha kweli? Ukizingatia leo tuko weekend ofisi zimefungwa.”

SISTER: “South ni Passport yako tu na ticket ya kurudi ila lazima uwe na sababu maalumu ya kuingia kule, tunaweza kutumia barua ya ofisi yangu ikaonesha nakwenda south kikazi, tukatumia hii advantage.”

Na muda huu alikuwa akimpigia simu dada Tyna na aliweka loudspeaker.

“Hello my love”

TYNA: “Yes darling, I have missed you so much.”

SISTER: “Ooh really?, niko na brother hapa tunajitaji ticket 2 za kwenda South Africa leo, ni muhimu sana.”

TYNA: “Insider jana amenicheki alikuwa anahitaji ticket ya kuja Arusha, sikujua kama anakuja kwako, vipi huko south kuna nini tena?”

SISTER: “Dear kuna mambo tunaenda fatilia tutaongea, ila kwasasa tusaidie hili kipenzi, tukicheki bei za flight zipo juu sana.”

TYNA: “Ticket inakuwa cheap ukikata mapema hizi za haraka nyingi ni za maagent, sasa nipe muda nifanye mpango wa kuwachekia, huko South mnabarua yoyote?”

SISTER: “Ndo tunajadili hapa kipenzi, naweza tumia barua ya ofisi.”

TYNA: “Nina rafiki yangu yuko South, anafanyia kazi Airport Johannesburg, ni rahisi kuwasaidia chap na uzuri yuko airport hamtapata tabu.”

Nilimpa Ishara sister akubali maana ilikuwa ni uhakika;

SISTER: “Sawa dear, ongea nae afu tupe jibu.”

TYNA: “Huyuhuyu anaweza kutusaidia na ticket, ila niwashauri mje Dar kwa uhakika zaidi na ni rahisi kupata ndege za kuunga.”

SISTER: “Bhasi tusaidie ticket za kutoka huku ili tuwahi kuja huko.”

TYNA: “Sawa hili ni chap tu hakuna shida.”

Baada ya kumaliza kuongea na Tyna tulianza kupanga bajeti ya kwenda kule South Africa maana hatukujua tunaweza kutumia muda gani. Mimi nilikuwa nina $1,800 na 370k kama cash iliyobakia, kwa upande wa sister alikuwa ana balance ya 2M, bajeti ikawa inatutosha vizuri kabisa.

Sister alimpigia simu shemeji na alimpa taarifa kuwa mimi nipo Arusha na alimuaga anaondoka kwenda South Africa, alimpa ABC kidogo ya kinachoendelea, na pindi akirudi atamsimulia vizuri.

Shem wangu hanaga noma kabisa, aliomba kuongea na mimi tukasalimiana pale na alinipa pole, tukaongea kidogo, pia alimind kwanini nakuja Arusha, halafu naondoka bila kuonana nae? ilibidi nimwambie tukitoka South tutaonana.

Baada ya dakika 2 shem alituma million 1 kwa sister na alimpigia simu kumwambia itatusaidia safarini, na akatutakia safari njema na mafanikio.

Sister alisema anaondoka kwenda home kubadilika haraka pamoja na kuchukua nguo za safari, na baada ya nusu saa atakuwa amerudi, hivyo aliondoka akaniacha hotelini nikimsubiri.

Mpaka sister anaondoka kwenda kubadilika tulikuwa tumetumia karibia masaa 3 pale hotelini, maana tulikuwa na maongezi mengi sana kuhusu hili suala, na hapa nimeandika baadhi tu yale muhimu.

Suala la Asmah sikutaka kabisa kumwambia maana lingeweza kusababisha mambo yawe magumu zaidi na kupoteza uaminifu kwa dada yangu.

Baada ya dakika 40 sister alirudi hotelini huku amependeza sana, alikuwa kavaa skin jeans ya blue, chini ana raba nyeupe, juu ana top nyeupe na sunglasses nyeusi, nywele zake ndefu ambazo hazijasukwa kaziachia kwa pembeni.

Kama nilivyowaambia awali kuhusu dada yangu, ana asili flani ya Kihindi, mweupe na mzuri by nature. Ukweli alikuwa kapendeza sana, na niliishia kujisifia kuwa nina dada mzuri na baada ya kufika usawa wangu nilimsifia tena kwa kupendeza.

Sister alifurahi sana kuona nikimpa sifa za kupendeza na tuliendelea na mazungumzo;

SISTER: “Tyna kanipigia simu, anasema tusogee JRO.”

MIMI: “Sawa haina shida, na kuhusu ticket za south?”

SISTER: “Hili bado hajaongelea, nafikiri tuendelee kumpa muda.”

Ticket online zilikuwa zinapatikana, lakini sasa bei za ticket zilikuwa ziko juu sana, hizi safari za papo kwa hapo tuwaachie matajiri ndo wanaweza kulipia gharama yoyote ile, ila kwasisi masikini tuendelee kukata ticket mapema.

Sister alikuwa amekuja na dereva wa ofisini kwao kwaajili ya kutupeleka airport, sister alisema baada ya kutoa taarifa ya dharura kwa bossy wake, ndo kupewa na gari ya kumpeleka airport.

Hatukuwa na muda wa kupoteza hivyo, tulianza safari ya kwenda JRO na ndani ya lisaa tuliwasili na tuliendelea kumsubiri Tyna atupe direction.

Saa 11 jioni tulifanikiwa kutoka Kilimanjaro kwenda Dar, kwa upande wa Dar dada Tyna alikuwa around akitusubiri na ile kuwasili alikuja spidi akamkumbatia sister. Hawa ni marafiki wa longtime toka enzi za utotoni, wamekua pamoja, kusoma pamoja ni marafiki wa damu.

Tulikaa Cafe tukiendelea kupiga story, kwa upande wake alitaka kujua ni jambo gani linatupeleka South?, sister aliishia kumpa sababu ya uwongo, haya ni mambo ya kifamilia isingekuwa busara kumwambia.

Tyna alimpigia simu rafiki yake ambaye angetupokea kwa kule South Africa na alimpa simu sister akaongea naye. Jamaa wa kule South alitushauri tufikie Johannesburg na wakati wa kurudi tutaondokea Capetown.

Changamoto iliyojitokeza ni kwamba sisi tunakwenda Capetown na tukifikia Johannesburg, kwenda Capetown pana distance si chini ya 1,400km unaona umbali huo. Kwasababu ya ugeni na tulihitaji mwenyeji wa kutopokea kwa kule, hivyo hatukuwa na jinsi ilibidi tukubali.

Kwa upande mwingine jamaa wa South alipiga simu na kumpa taarifa Tyna kuwa amepata ticket 2 kutoka kampuni ya Ethiopian Airlines, hivyo alihitaji tumtumie taarifa zetu haraka, pamoja na muda tutakaotumia kule.

Tulimtumia Jamaa taarifa zetu kwa haraka na kuhusu gharama za tickets tulilipa $1,750 kwa wote wawili ‘Go and return’. Baada ya kukamilisha malipo na taratibu zote, alitutumia ticket zetu. Ndege ilikuwa inaondoka saa 9 usiku kwenda South, kwahiyo ingetubidi tusubiri mpaka muda ufike wa safari.

Muda ulikuwa ni saa 11 jioni tayari, tukaanza kushauriana na sister tunakwenda kulala wapi?. Tyna alisema tukalale kwake, hawezi kukubali kuona tunalala hotelini wakati anauwezo wa kutupeleka kwake, tulikwenda kulala kwa Tyna.

Plan yetu ilikuwa turudi Dar siku ya jumatano, hivyo tungekaa siku 2 kule. Kwa upande wa bajeti ilikuwa imekata kwa upande wa sister maana tulitumia pesa zake kulipia tickets na tuliacha dollar zitusaidie tunakoenda. Nilikuwa sijatembea na card, pia huduma za online sijajiunga, hivyo nilipiga hesabu za haraka nikaona nikope pesa kwa mtu, ili tuwe na akiba ya kutosha.

Kwa hesabu za haraka niliona nimuazime pesa Ghati na ile kumpigia simu na kuongea naye, kwa haraka sana alinitumia million 3 na nikazitoa kabisa kwa wakala.

Kesho yake, asubuhi na mapema, tuliwasili JNIA kuanza safari yetu ya kuelekea Afrika Kusini. Baada ya kucheck-in na kukamilisha taratibu zote, tuliingia kwenye ndege. Hata hivyo, tulikaa kwenye viti tofauti, dada yangu alikaa mbele yangu, wakati mimi nilikuwa kwenye kiti cha tatu nyuma kutoka pale alipokaa.

ITAENDELEA
Nyingine lin??
 
Haya haya ndio movie linachanganya sasa kuelekea uwanja wa final haya tupo na popcorn kama zote
 
Back
Top Bottom