Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ahahahah..ajichanganye aoneHapo Lugalo tu ndio anapatikana
Kwahiyo stori au chai?? 😂una amini mkuu?
Dada yako ni Genious 🙌🏿SEASON 02
EPISODE 25
“BY INSIDER MAN”
CONTINUE:
Kesho yake nilichelewa sana kuamka ni Junior ambaye alikuja kuniamsha chumbani kutokana na fujo zake na ile kuangalia muda ilikuwa ni saa 5 asubuhi.
Kwa upande mwingine mzee alikuwa kaningizia pesa ya Junior aliyokuwa ameahidi na alinitumia ujumbe niigawe na kwa mama yake. Sandra naye hakuwa mbali kunitumia message kuuuliza kama nimefika salama na palepale nilimjibu nimefika salama, nikaingia bafuni kuoga.
Kipindi najiandaa simu yangu ilianza kuita alikuwa ni baba mkwe, nilipokea ili nimsikilize, lakini nilijua lazima ni suala la plot. Baada ya maongezi ya muda mfupi tulikubaliana tukutane ili twende huko Mapinga mapema.
Muda mchache mbele niliondoka kuelekea ukweni, kumpitia baba mkwe na bila kuchelewa tulianza safari ya kwenda mapinga ilikuwa ni mbele kidogo ya Bunju. Mhusika mwenye plot muuzaji, alikuwa yupo tayari eneo la tukio akitusubiri, ambaye ni rafiki wa baba mkwe.
Plot ilikuwa nzuri sana, imepimwa tayari, ipo kwenye eneo zuri karibu na Barabara ya Bagamoyo na ina ukubwa wa sqm 1600. Nilipapenda na nikaomba kupewa bei elekezi, mhusika alisema naweza kulipa kwa awamu 4, lakini awamu ya kwanza lazima nilipie nusu ya gharama.
Tuliondoka kwenda kukaa moja ya bar pale Bunju mwisho kwaajili ya maongezi zaidi na tulikubaliana 23M nikafanya malipo nusu kabisa, sikuwa na wasiwasi wa kuita serikali za mtaa sababu biashara ni ya kindugu.
Kuhusu mkataba wa kuandikishana na kukabidhiana hati ya kiwanja, tulikubaliana kuwa mpaka nitakapomaliza kiasi kilichobaki, hati itakuwa chini ya uangalizi wa baba mkwe. Nilikuwa na imani kubwa na baba mkwe kwa kuwa ndiye msimamizi wa kila kitu, hivyo niliamini asingeweza kuniingiza chaka, na alinihakikishia uhakika wa 100%.
Kufikia saa 9 mchana tulikuwa tumemaliza kila kitu, hivyo tuliondoka kurudi home, kisha nikaanza kumshusha baba mkwe nyumbani kwake, lakini aliomba niingie ndani ili tufanye mazungumzo kidogo.
Kwa upande wake alinipongeza sana kwa hatua niliyoichukua na aliendelea kunishauri kwamba, kwenye ile plot nigawe nusu, kisha nijenge sehemu ya kuishi na nusu inayobaki nijenge nyumba za kupangisha. Nilitumia lisaa pale ukweni, kisha nikaanza safari ya kwenda Masaki kuonana na Hilda maana alikuwa ameshaanza kunipigia simu kwa fujo sana.
Niliwasiliana na Hilda tukutane Olive kwaajili ya maongezi na baada ya nusu saa alinipa taarifa kuwa amefika eneo la tukio tayari, hivyo ananisubiri mimi tu. Kwa upande wangu nilichelewa kama dakika 10 hivi kufika eneo la tukio, baada ya kuwasili tulisalimiana na tukaanza mazungumzo pale;
HILDA: “Nambie Insider za huko Zambia, hope umeenjoy.”
MIMI: “Na enjoy wapi wakati umenitoa huko kwaajili yako.”
HILDA: “Pole sana lakini mimi sielewi kabisa, nafikiri hata kuacha kazi, mmenisusia kampuni na sijui kinachoendelea, simu zenu wote hampatikani.”
MIMI: “Pole sana mummy, ni kweli hatuko kwenye maelewano mazuri, lakini sioni sababu ya wewe kuacha kazi hasa kwenye kipindi hiki cha mpito.”
HILDA: “Kampuni ikifeli si lawama zote zitakuja kwangu?, kuhusu suala lako la kwenda likizo si mama wala Iryn aliyenipigia simu na uliezea kuwa kampuni ipo kwenye mikono yangu.”
MIMI: “Najua unachopitia Hilda, nikutoe wasiwasi tuko pamoja na kila kitu kitakwenda sawa.”
HILDA: “Kampuni haina cash nashindwa kufanya manunuzi madogo madogo, stock inaisha na hakuna taarifa yoyote kama mzigo umeagizwa au laah!, mama hapatikani kwa simu na nguvu ya kumpigia Iryn nakosa sababu hausiani na mimi ni wewe ndo wakuwasiliana nae.”
MIMI: “Mama atakuwa field, nimeongea na Sumaiya na yeye ni muda mrefu hawajazungumza, si unajua kazi yake asilimia kubwa anashinda kwenye majanga?.”
HILDA: “Hio ndo changamoto, sasa tunafanyaje?.”
MIMI: “Stock imebaki kiasi gani? na account Receivable inasomaje?.”
HILDA: “Stock iliyobaki asilimia kubwa ni zile product expensive ila kwa bei za kawaida sidhani kama itaweza kufika week 2 na itadepend na volume ya wateja.”
MIMI: “Sawa sasa nisikilize, kuanzia leo ukifanya mauzo ya cash usiweke bank ili hizo pesa zisaidie kurun office, kingine wahimize customers walipe kwa cash ili iwe advantage kwetu.”
HILDA: “How naweza kumwambia mteja asilipe bank na amezoea kutransfer moja kwa moja kwa account?”
MIMI: “Ni simple tu, customers huwa wanapiga simu kufanya booking, kwahiyo palepale mwambie tuna accept na cash pia, inaweza kufanya kazi na kutusaidia.”
HILDA: “Vipi na kuhusu stock?”
MIMI: “Huko tutafika bado sijamaliza, hujanijibu kuhusu madeni tunayodai kwasasa ni kiasi gani? Ambayo wewe umeyaandikia.”
HILDA: “Ni kama million 3 na something hivi.”
MIMI: “Kipindi nakukabidhi office receivables zilikuwa 67M nikijumlisha na hio ni 70M, Kampuni X na Y zimelipa tayari na mara ya mwisho kuangalia deni, limepungua mpaka 24M pamoja na deni lako. Sasa hawa waliobaki mimi nitaongea nao ili walipe kwa cash, hatuwezi kushindwa hili jambo.”
HILDA: “Vipi kuhusu stock?, ikiisha hatutaweza kuendelea na kazi, na mishahara itakuwaje? Mwezi uliopita ilichelewa.”
MIMI: “Kuhusu mishahara kama mambo bado hayaeleweki, nitaangalia means ya kufanya hata cash naweza kuwalipa. Kuhusu stock niachie hili nilifanyie kazi na nitakupa majibu soon, acha niwasiliane na dada agent huenda anamzigo.”
HILDA: “Mmh sawa, lakini nikiangalia interval ya mzigo wa mwisho kuupokea na sasa, naona kama hakuna taarifa yoyote, angekuwa amekupigia simu.”
MIMI: “Upo sahihi, lakini tutajua tunafanyaje ndomana nimekwambia hili niachie mimi.”
HILDA: “Sawa Insider nimefurahi kukuona.”
MIMI: “Mimi pia, naomba tusaidiane hili jambo hii kampuni isifie kwenye mikono yetu.”
Hilda aliishia kufurahi pale sababu nilikuwa nina ratiba zingine ilibidi nimuage lengo niwahi kwa Lucy, tuliongozana mpaka parking tukaagana kwa kumbatiana, kisha nikaondoka kuelekea Mikocheni.
Nilikuwa na ratiba ya kuonana na Lucy tangu asubuhi, ratiba ziliingiliana wakati niko njiani Lucy alipiga simu na kuuliza niliko na alihimiza nifanye haraka tukaongee kuna jambo.
Baada ya lisaa niliingia kwa kuchelewa sana pale ofisini sababu ya foleni na wakati nikishuka kwa gari, nilimuona Lucy anakuja usawa wangu na alikumbatia kwa nguvu sana, nilihisi akilia;
MIMI: “Lucy mbona unalia kuna shida gani?.”
LUCY: “Insider nimeongea na Iryn sio muda mrefu sana, amefanya maamuzi ya kufanya abortion.”
MIMI: “Nini? Sikuelewi amefanya au bado?”
LUCY: “Bado sijui kama amefanya au laah! anasema ameshindwa kabisa kuhandle upinzani anaoupata kutoka kwa familia yake, na wewe pia hueleweki kama upo upande wake na hili ndo linampa wasiwasi, kitu kingine alikupa masharti ya mtoto, lakini umeshindwa kuyafuata na umetembea na Asmah.”
MIMI: “Amekutafuta kwa namba ipi?”
LUCY: “Nimeongea sana na namba yake, nikijaribu kukuombea msamaha, lakini amenigomea. Anasema hawezi kurudisha tena imani yake kwako, hasa baada ya kutarajia kuwa mngekuwa pamoja katika kipindi hiki cha upinzani anachopitia. Lakini wewe umekuwa ukimpa majibu mepesi, ukionesha wazi huna mpango naye tena pamoja na mtoto, hata kama alifanya kwa reason zake. Insider, nimelia sana na nakuonea huruma mshikaji wangu. Sitaki kuamini kwa kipindi chote mlipokuwa na Iryn, mambo yanamalizika kwa njia mbaya hivi. Nimemwambia kuwa, kama atathubutu kufanya ujinga huu, nitaacha kazi."
MIMI: “Jimmy alinambia Iryn anamaamuzi magumu sana na mpaka amesema hivo jua kweli kadhamiria, na huwa habadili mawazo yake, uzuri unamjua ni mtu wa aina gani, ooh shit.”
LUCY: “Hapana embu mpigie before it’s too late, jaribu kuongea nae muda unaenda.”
Nilitoa simu ili nimpigie na nikakutana na ujumbe kutoka kwake ambao umetumwa dakika 5 zilizopita na ulisomeka;
“Hello Insider, it’s been a while. I hope you’re doing well. I want to tell you that I don’t hate you. Please know that you’re the most important man I’ve ever met in this world. I truly appreciate your contribution and everything you have done in my life.
Please understand that I am currently going through a very difficult time due to this pregnancy, especially when it comes to my siblings. All of them have been against me, and even worse, you, who I relied on to be close to me during this period, have distanced yourself from me.
I have chosen the side of my family because I don’t see any future with you, and you have shown no intention of wanting this child. I don’t like doing this, but I also want to avoid the problems that might arise later, especially for your family. I carried this pregnancy for my own reasons, and I am choosing to end it for my own reasons.
I am truly sorry for this and wish you all the best.”
Nilihisi kuishiwa nguvu na niliegemea kwenye gari hata sikujua nafanya nini muda huu na chozi lilianza kunitoka.
Wanasemaga mwanaume hatakiwi kutoa chozi, nikwambie unakuwa bado hujaingia kwenye 18, nilifungua mlango wa gari kwa haraka sana nikaingia ndani, kisha niliwasha gari kuondoka eneo hili.
Lucy alianza kuniita na kunigongea dirishani;
“Insider nini kinaendelea? Mbona umebadilika ghafla sana?”
Sikuwa hata nikimsikia Lucy, zaidi nilianza kuondosha gari na kumwacha kwenye mataa bila kujua afanye nini kwa wakati huu.
Haikukuchukua muda nilisikia simu ikiita, lakini sikuwa na habari nayo na niliendesha gari nikaja kuipark mbele kidogo ya shule ya Alpha, kama unaelekea Cocacola road, kuna maduka pale pamechangamka sana.
Nilipark gari maeneo haya nikatulia maana sikuwa najielewa huku nikihisi mwili kufa ganzi, machozi mazito yalikuwa yametanda kwenye mboni zangu. Nilikuwa kwenye dimbwi zito la mawazo, nilijiona ni mwanaume ambaye sina bahati, maisha yangu ni kama yamejaa na mikosi, ukizingatia nakwenda kumkosa mtoto kwa mara ya tatu.
Niliwaza mbali sana, nikajisemea ‘au Mungu ananiadhibu kwa kuchepuka?‘ Ni mtoto wa tatu sasa kwa jumla namkosa, before Prisca na Iryn, huko nyuma kuna tukio lingine lilitokea.
Nilichukua simu yangu nikaona calls kutoka kwa Lucy, ndo alikuwa akinipigia muda ule na nilitafuta namba ya Iryn, kisha nikafungua whatsapp ili nimpigie, lakini namba ilikuwa deactivated na normal call hapatikani.
Nilikuwa katika wakati ambao sijui nifanye nini maana nilikuwa dilemma, niliwaza nimpigie simu mama Janeth nimuombe anisaidie hili, nikakumbuka nae hapatikani.
Muda huu wazo lilinijia niende kwa sister yangu Arusha, nikamwambie kuhusu hili suala, kumpigia simu na kumwelekeza isingetosha, niliona sinabudi kwenda huko na nilimpigia simu palepale kumpa taarifa.
SISTER: “Nambie kaka yangu unaendeleaje.”
MIMI: “Dada niko njiani nakuja Arusha, nina maongezi na wewe muhimu.”
SISTER: “Mdogo wangu si nilikwambia nikipata likizo ndo uje au umesahau?”
MIMI: “Dada ni muhimu sana haya maongezi, tafadhali.”
SISTER: “Kuna nini kinaendelea mdogo wangu? Umeshagombana na mama J?”
MIMI: “Dada naomba nielewe, nikifika huko utaelewa ni nini nataka kukwambia.”
SISTER: “Sawa karibu, utakuwa unaniambia safari ilipofikia, pole sana.”
Nilijifuta machozi yangu vizuri, kisha nikaondoka kurudi home kwaajili ya kuchukua vitu na kuanza safari ya kwenda Arusha. Nikiwa njiani nilimpigia simu dada Tyna kumuomba kama nitaweza kupata ticket ya kwenda Arusha, akanambia haiwezekani labda kwa kesho asubuhi.
Niliona kwa asubuhi ni mbali sana wacha niondoke hata kwa kuunga cha msingi nifike Arusha. Nilirudi home, kisha niliingia ndani kwa spidi sana, akina wife walikuwa pale seblen hata sikuwasalimia maana nilikuwa na spidi ya hatari.
Wife alikuja chumbani na alinikuta ninaweka nguo kwenye bag kwaajili ya kuondoka na alianza kuniuliza pale;
“Baba J, una safari ya wapi tena?”
“Nakwenda Arusha mara moja kuonana na sister.”
“Are you okay? Mbona kama macho mekundu ulikuwa unalia? Kuna nini kimekupata?”
“Nothing, mummy usiwe na wasiwasi na mimi.”
“Jana tu! Umerudi kutoka Zambia kwanini usingesubiri hata kidogo ukaenda huko siku nyingine?”
“Ni muhimu sana ndomana nakwenda sitakawia kurudi.”
“Kuna jambo gani huko?.”
“Ni masuala ya kifamilia, nikirudi nitakwambia.”
“Mhhh! Sawa.”
Wife alikubali kwa shingo upande nami niliendelea kupanga vitu vyangu kwa haraka sana. Kwenye bag nilikuwa nina balance ya $1,800 ambazo zilibaki kutoka Zambia na nilitembea na cash Tsh 500,000.
Nilichukua bodaboda kwenda Tegeta-Kibo kutafuta gari za kwenda Arusha na ile nafika nabahatika kupata gari ya kwenda Moshi. Saa mbili usiku tulianza safari ya kwenda Moshi na njiani nilikuwa ni mtu mwenye mawazo sana, nilikuwa natamani hata gari ipae ili tu! nifike mapema.
Saa 8 za usiku tuliwasili Kilimanjaro, nikabahatika kupata gari ya tour inayoenda Arusha, sikutaka kabisa kumsumbua sister maana ni mke wa mtu, hivyo niliplan kumpigia simu asubuhi.
Ulikuwa ni mwendo wa lisaa mpaka tunafika Arusha na jamaa alisema anaishia USA river, kutokana na mimi kuwa mgeni alinipeleka kwenye moja ya lodge ili nilale.
Kufika pale reception naambiwa room zipo ila sasa gharama zake ni za ajabu room ni elfu 90, nilishangaa sana, kwa lodge unalipia elfu 90? Ukizingatia nina masaa yasiyozidi 5 kulala. Muda ulikuwa umeenda sana, hata jeuri ya kutafuta lodge zingine sikuwa nayo afu ni mgeni na maeneo ya huku, kwanza niliogopa vibaka maana Arusha ina scandal nyingi sana.
Nilitoa pesa nikalipia na dada pale reception alianza kujichekesha chekesha, lakini mimi sikuwa hata na habari nae zaidi nilikuwa na mawazo kichwani. Nilioneshwa room yangu na kabla ya kulala nilimpa taarifa sister, kuwa nimefikia salama na nipo lodge ya Mzunguu, USA River.
Niliamka saa 2 asubuhi na kabla ya yote nilicheki simu kuangalia kama dada amenipigia maana simu ilikuwa silent. Baada ya kuangalia nilikuta kweli amenipigia mara 2 na alinitumia ujumbe kunambia nikiamka nimpigie. Kwa upande mwingine mama J nae alikuwa amenipigia simu za kutosha na kutuma message juu, kuuliza kama nimefika salama.
Nilianza kwa kumpigia simu sister, akasema yupo ofisini anaweka mambo sawa, atakuja saa 3 kunichukua lodge. Kisha nilimpigia simu wife, lakini hakupokea na nikamtumia ujumbe kumjulisha nimefika salama Arusha.
Niliingia bafuni kuoga kabisa ili sister akija anikute niko tayari, wakati nikijiandaa simu yangu ilianza kuita, ni Lucy alikuwa akipiga na nilipokea simu yake ili nimsikilize na tulianza maongezi pale;
LUCY: “Insider unaendeleaje?”
MIMI: “Salama Lucy, nashukuru Mungu.”
LUCY: “Jana umeondoka ukaniacha niki hang na simu ukawa hupokei, nini kinaendelea?”
MIMI: “Acha tu, kuna ujumbe mbaya alinitumia kwamba anafanya abortion na mpaka sasa hapatikani hata whatsapp ameifunga.”
LUCY: “Pole sana, wewe upo wapi sahivi?”
MIMI: “Naongea na wewe niko Arusha now.”
LUCY: “What? Umeenda muda gani? Na kuna nini?”
MIMI: “Jana baada ya kuachana nilirudi home, kisha nikaanza safari na nimekuja huku kwaajili ya kuonana na dada yangu.”
LUCY: “Jamani, mmeshaonana tayari?.”
MIMI: “Bado Lucy, nimeingia late sana na soon tutaonana.”
LUCY: “Ngoja niendelee kutafuta means ya kumtafuta Iryn kwa namba nyingine, lakini nataka kuacha kazi Insider.”
MIMI: “Uache kazi kwasababu gani?”
LUCY: “Nimemwambia jana naacha kazi kama atatoa mimba, nitakuwa nimekusaliti kama nitaendelea kufanya kazi chini yake.”
MIMI: “Usifanye maamuzi yoyote mabaya mpaka nitakavyo rudi sawa?”
LUCY: “Sawa! see you then.”
Saa 3 ontime sister alikuwa amefika pale lodge na alinipigia simu kunipa taarifa kuwa yuko parking, nami nilitoka kwenda kuonana nae, alishuka kwenye gari na kunikumbatia pale. Ni miaka 2 ilikuwa imepita bila kuonana na sister na mara ya mwisho kuonana ilikiwa siku ya engagement ya mama J.
Nilirudi ndani kuchukua vitu pamoja na kusign out. Baada ya kurudi, sister alisema tunakwenda kwake, lakini mimi nilimgomea.
SISTER: “Unamaana gani hutaki kwenda kwangu?”
MIMI: “Dada yangu naomba tutafute kwanza sehemu tukae, kisha tuzungumze.”
SISTER: “Sawa! Twende Charity hotel tukazungumze pale tupate na breakfast.”
Tulikwenda Charity hotel ambayo ipo Sakina, palikuwa na kamwendo kutoka USA river mpaka hotelini, na baada ya kuwasili tulikaa nje, na kila mtu aliishia kuagiza anachotaka kula.
SISTER: “Mama J kanipigia simu jana, wewe ulimuagaje home?”
MIMI: “Nilimwambia nakuja kuonana na wewe kwaajili masuala ya kifamilia, ulimjibu nini?”
SISTER: “Nilimwambia ukirudi utamwambia, sikujua hata cha kumjibu na sikutaka kumuacha kwenye question mark.”
MIMI: “Ulifanya vema, sasa dada yangu mpaka nimekuja huku naomba utambue napitia kipindi kigumu sana, hili jambo naloenda kukwambia hakuna mtu yoyote kwenye familia anaejua. Kwa bahati mbaya ninakushirikisha leo, lakini mambo yameshaharibika tayari, wish ningekwambia mapema.”
SISTER: “Kuna nini bro! embu niambie hii itabaki kuwa siri yangu na wewe.”
Alikaa mkao kuonesha kwamba yuko tayari kunisikiliza, nami nikaanza kumsimulia mkanda mzima kuhusu Iryn, jinsi tulivyokutana, tukaanza kujihusisha kimapenzi hadi kupelekea kupata mimba, na mambo yanayoendelea sasa, bila kusahau ukaribu wake na mke wangu.
Baada ya kumaliza kumsimulia mkanda mzima, sister alishusha pumzi ndefu sana na aliishia kusikitika pale;
SISTER: “Daah! Hizi habari kweli ni nzito, simpatii picha wifi yangu akija kujua hii siri, sijui kama utanusurika this time. Bro! unashida gani mpaka unashindwa kucontrol hisia zako?unaenda mbali na kumpa mimba, what are you doing?”
MIMI: “Nimekosea ndio, lakini nimeshakueleza kuwa alibeba mimba kwa reason zake, mtoto anabaki kuwa damu yetu, hatuwezi mkataa.”
SISTER: “Hata hivyo, mimi bado nina wasiwasi na zile dawa alizokupa Masai nahisi huenda kuna kitu alikuwekea, umekuwa mtu wa kupenda penda hovyo au sababu ya kuchelewa kuwajua wanawake?.”
Sister yangu kaplay part kubwa sana ya kunifanya kuwa mwanaume rijali, alinisaidia mambo mengi sana mpaka nikawa sawa, miaka 8 nyuma.
SISTER: “Bro! ifike stage ujicontrol, haya yote unayofanya ipo siku yatakurudia wewe na utakuja kujuta kwenye maisha yako yote, mimi kama dada nimeumia sana juu ya mama J. Mtoto wa watu yuko loyal sana kwako, anakupenda, ametulia na hana mambo mengi ila wewe sasa, Mungu akusaidie.”
MIMI: “Ni kweli nimezingua dada yangu hata mimi najisikia vibaya sana, lakini naomba tushauriane juu ya hili suala, haya mambo mengine tutaongea tuanze kwanza na hili, ndomana nimekuja kwako.”
SISTER: “Umefanya ujinga wako afu sahivi unaomba ushauri, mbona hukuomba ushauri kipindi unaanza?. Okay, ulikuwa Zambia kwa baba, why hujamwambia kuhusu hili?. Brother kwa hili sina cha kukushauri na kama anataka kufanya abortion, ni bora akafanya hivo maana huko mbeleni utakuwa kwenye wakati mgumu sana.”
MIMI: “Sawa nashukuru kwa kunipa lawama zote, lakini tambua hakuna binadamu asiyekosea.”
SISTER: “Insider, unavyofanya ujinga kama huu naomba fanya kwa interest zako, lakini kaa ukijua kwamba mambo yakiharibika ni kwa faida yako, dont ever try to contact me again. Wewe tayari ni mtu mzima unajua ni nini unafanya, hufanyi kwa bahati mbaya, tusipotezeane muda. We done here, naenda washroom nikirudi tunaondoka kwenda home.”
MIMI: “Mimi siwezi kwenda home nitarudi Dar maana sijaja huku kwa lengo la kukutembelea.”
Sister alinikataa na hiki kitendo kilizidi kunipa mawazo, ukweli sister na mama J ni marafiki sana na humwambii kitu kuhusu uhusiano wao. Dada yangu alikuwa sahihi kuchukia kwa hili jambo nililofanya, ukizingatia nilishakuwa nimetoa ahadi huko nyuma ya kutofanya tena, huu ujinga.
Niliinamia meza huku nikiendelea kuwaza next move, lakini sikuwa napata jibu, hivyo niliona wacha nirudi Dar nikaendelee na mambo yangu.
Baada ya dakika 15 Sister alirudi kutoka washaroom na alianza tena kuongea na mimi pale;
SISTER: “Bro! nioneshe message aliyokutumia jana, niisome na mimi.”
Nilitoa simu nikamuonesha na alinyamaza kwa dakika 10 bila kusema kitu chochote, kisha akaendelea;
“Kipindi niko washroom nilikuwa nafikiria hili suala, kwa maelezo yote uliyonipa nikweli dada anakupenda, na hii message aliyokutumia amecheza na mind yako, kuna ujumbe hapa amekuandikia ila umeshindwa kuutambua.”
Dada yangu anajua mambo ya saikolojia, maana anafanyia kazi moja ya NGO kubwa ya kimataifa kule Arusha, sasa baada ya kunipa hizi habari nilishindwa kumuelewa na nilichukua simu ili niusome ujumbe tena kwa makini, hata hivyo sikuelewa kitu.
MIMI: “Mimi sioni chochote hapa dada, labda unambie umeona nini?.”
SISTER: “Ujumbe wa hapo upo clear kabisa ni hivi, dada yuko kwenye kipindi kigumu hasa kwa upande wa familia yake, wewe ulishindwa kumshawishi toka mapema, kwa hapa ulifeli. Before unakumbuka nilikwambia kwamba wanawake tunapenda kudanganywa? Ni kosa kubwa sana kumwambia mwanamke ukweli, kwa ufupi hatupendi ukweli.”
MIMI: “Kwahiyo unataka kusema nilikosea kumwambia ukweli? Ningemdanganya namuoa huoni kama ingekuja kuleta matatizo huko mbeleni?”
SISTER: “Hili jambo lilitakiwa kuisha hata hayo mambo ya Ethiopia usingeenda, ndomana nakwambia ulishindwa kucheza na akili yake tu. Na kama ungenishirikisha mapema hili suala lingekuwa limeisha, sahivi tungekuwa tunajadili namna ya kudeal na mama J.”
MIMI: “Nilitakiwa kufanya nini hapo.?”
SISTER: “Nakupa mfano, kisha utanijibu. Una mtoto wako wa kike, anakuja kwako kukwambia ana mimba, na kapewa na mume wa mtu, utamuelewa?”
MIMI: “Hapana siwezi asee, nitamlamba makofi ya kutosha.”
SISTER: “Uli expect na yeye angekuwa na confidence ya kuongea hivo mbele ya familia yake?.”
Nilinyamaza kimya muda huu;
“Brother ulitakiwa kuisoma akili yake inataka nini kwa kipindi hiki, ulipaswa kumuonesha mpo pamoja no matter what, ulipaswa kumuonesha unampenda sana hata kwa kupretend na kitendo cha kumpiga hotelini, hapa pia ulikosea sana.”
MIMI: “Alinipanda sana kichwani ndomana nilimchapa vibao, nilimuomba msamaha lakini.”
SISTER: “Ulishindwa kutambua ni mjamzito, na ile haikuwa sababu ya kumpiga, shida yako unahasira za haraka sana.”
MIMI: “Ni kweli nilikosea ile siku, lakini bado sioni kama sababu ya kufanya abortion.”
SISTER: “Mpaka sasa, dada anaonekana kuwa upande wetu, lakini bado anajifikiria kuhusu kufanya abortion. Inaonekana nguvu ya familia yake ni kubwa zaidi kuliko ya upande wetu, na mara nyingi, upande wenye nguvu zaidi hushinda. Dada ameona kuwa huna future kwa sababu umeshindwa kumjali katika kipindi hiki kigumu anachopitia. Huu ulikuwa wakati mzuri wa kumuonesha upendo, lakini badala ya kumsaidia, wewe umekuwa against naye wakati ulipaswa hata kwenda South Africa kumsalimia kama kweli ungetaka mtoto. Dada alikuamini, lakini sasa anaona unaweza kuharibu future yake na kumfanya apoteze ndugu zake kwa sababu yako, mtu ambaye si wa kutegemewa."
MIMI: “Conclusion ni nini dada yangu? maana nahisi kuchanganyikiwa hapa kuhusu huyo mtoto bora hata angekuwa anapatikana kwenye simu.”
SISTER: “Huo ujumbe dada aliotuma kwako, ameandika kwa kumaanisha, ni kama amekupa last chance ya wewe kumtafuta, sasa tumia akili tunampataje?”
MIMI: “Hapa ndo mtihani kujua aliko kati ya South, Ethiopia na Ufaransa, lakini anapendelea sana kwenda Ufaransa kwaajili ya mapumziko.”
SISTER: “Dada bado yuko South Africa, kwenda Ethiopia kwa familia kwa kipindi hiki ni ngumu, atleast Ufaransa, kama alitumia namba ya South kukutafuta bhasi yupo huko. Tuna siku moja tu imebaki ambayo ni kesho, ya kwenda South Africa kumtafuta ili tuyaweke sawa haya masuala, tukichelewa tutamkosa mtoto.”
MIMI: “What? Twende South Africa?”
SISTER: “Ndo maana yake, we are running out of time, let’s go, tuanze mchakato wa kufanya booking ya flight mapema.”
MIMI: “Sister taratibu kwanza, tukienda huko tunampataje? Anaishi Capetown lakini sijui address zake.”
SISTER: “Come on, tutakwenda kuulizia chuo anachosoma na tutampata, lazima tutapata contacts za watu wake wa karibu.”
Sister alikuwa kaongea point tupu, ukweli mimi nilikuwa sijitambui kabisa muda huu maana akili yangu ilikuwa imevurugwa sana.
MIMI: “Sawa na vipi kuhusu permits tutafanikisha kweli? Ukizingatia leo tuko weekend ofisi zimefungwa.”
SISTER: “South ni Passport yako tu na ticket ya kurudi ila lazima uwe na sababu maalumu ya kuingia kule, tunaweza kutumia barua ya ofisi yangu ikaonesha nakwenda south kikazi, tukatumia hii advantage.”
Na muda huu alikuwa akimpigia simu dada Tyna na aliweka loudspeaker.
“Hello my love”
TYNA: “Yes darling, I have missed you so much.”
SISTER: “Ooh really?, niko na brother hapa tunajitaji ticket 2 za kwenda South Africa leo, ni muhimu sana.”
TYNA: “Insider jana amenicheki alikuwa anahitaji ticket ya kuja Arusha, sikujua kama anakuja kwako, vipi huko south kuna nini tena?”
SISTER: “Dear kuna mambo tunaenda fatilia tutaongea, ila kwasasa tusaidie hili kipenzi, tukicheki bei za flight zipo juu sana.”
TYNA: “Ticket inakuwa cheap ukikata mapema hizi za haraka nyingi ni za maagent, sasa nipe muda nifanye mpango wa kuwachekia, huko South mnabarua yoyote?”
SISTER: “Ndo tunajadili hapa kipenzi, naweza tumia barua ya ofisi.”
TYNA: “Nina rafiki yangu yuko South, anafanyia kazi Airport Johannesburg, ni rahisi kuwasaidia chap na uzuri yuko airport hamtapata tabu.”
Nilimpa Ishara sister akubali maana ilikuwa ni uhakika;
SISTER: “Sawa dear, ongea nae afu tupe jibu.”
TYNA: “Huyuhuyu anaweza kutusaidia na ticket, ila niwashauri mje Dar kwa uhakika zaidi na ni rahisi kupata ndege za kuunga.”
SISTER: “Bhasi tusaidie ticket za kutoka huku ili tuwahi kuja huko.”
TYNA: “Sawa hili ni chap tu hakuna shida.”
Baada ya kumaliza kuongea na Tyna tulianza kupanga bajeti ya kwenda kule South Africa maana hatukujua tunaweza kutumia muda gani. Mimi nilikuwa nina $1,800 na 370k kama cash iliyobakia, kwa upande wa sister alikuwa ana balance ya 2M, bajeti ikawa inatutosha vizuri kabisa.
Sister alimpigia simu shemeji na alimpa taarifa kuwa mimi nipo Arusha na alimuaga anaondoka kwenda South Africa, alimpa ABC kidogo ya kinachoendelea, na pindi akirudi atamsimulia vizuri.
Shem wangu hanaga noma kabisa, aliomba kuongea na mimi tukasalimiana pale na alinipa pole, tukaongea kidogo, pia alimind kwanini nakuja Arusha, halafu naondoka bila kuonana nae? ilibidi nimwambie tukitoka South tutaonana.
Baada ya dakika 2 shem alituma million 1 kwa sister na alimpigia simu kumwambia itatusaidia safarini, na akatutakia safari njema na mafanikio.
Sister alisema anaondoka kwenda home kubadilika haraka pamoja na kuchukua nguo za safari, na baada ya nusu saa atakuwa amerudi, hivyo aliondoka akaniacha hotelini nikimsubiri.
Mpaka sister anaondoka kwenda kubadilika tulikuwa tumetumia karibia masaa 3 pale hotelini, maana tulikuwa na maongezi mengi sana kuhusu hili suala, na hapa nimeandika baadhi tu yale muhimu.
Suala la Asmah sikutaka kabisa kumwambia maana lingeweza kusababisha mambo yawe magumu zaidi na kupoteza uaminifu kwa dada yangu.
Baada ya dakika 40 sister alirudi hotelini huku amependeza sana, alikuwa kavaa skin jeans ya blue, chini ana raba nyeupe, juu ana top nyeupe na sunglasses nyeusi, nywele zake ndefu ambazo hazijasukwa kaziachia kwa pembeni.
Kama nilivyowaambia awali kuhusu dada yangu, ana asili flani ya Kihindi, mweupe na mzuri by nature. Ukweli alikuwa kapendeza sana, na niliishia kujisifia kuwa nina dada mzuri na baada ya kufika usawa wangu nilimsifia tena kwa kupendeza.
Sister alifurahi sana kuona nikimpa sifa za kupendeza na tuliendelea na mazungumzo;
SISTER: “Tyna kanipigia simu, anasema tusogee JRO.”
MIMI: “Sawa haina shida, na kuhusu ticket za south?”
SISTER: “Hili bado hajaongelea, nafikiri tuendelee kumpa muda.”
Ticket online zilikuwa zinapatikana, lakini sasa bei za ticket zilikuwa ziko juu sana, hizi safari za papo kwa hapo tuwaachie matajiri ndo wanaweza kulipia gharama yoyote ile, ila kwasisi masikini tuendelee kukata ticket mapema.
Sister alikuwa amekuja na dereva wa ofisini kwao kwaajili ya kutupeleka airport, sister alisema baada ya kutoa taarifa ya dharura kwa bossy wake, ndo kupewa na gari ya kumpeleka airport.
Hatukuwa na muda wa kupoteza hivyo, tulianza safari ya kwenda JRO na ndani ya lisaa tuliwasili na tuliendelea kumsubiri Tyna atupe direction.
Saa 11 jioni tulifanikiwa kutoka Kilimanjaro kwenda Dar, kwa upande wa Dar dada Tyna alikuwa around akitusubiri na ile kuwasili alikuja spidi akamkumbatia sister. Hawa ni marafiki wa longtime toka enzi za utotoni, wamekua pamoja, kusoma pamoja ni marafiki wa damu.
Tulikaa Cafe tukiendelea kupiga story, kwa upande wake alitaka kujua ni jambo gani linatupeleka South?, sister aliishia kumpa sababu ya uwongo, haya ni mambo ya kifamilia isingekuwa busara kumwambia.
Tyna alimpigia simu rafiki yake ambaye angetupokea kwa kule South Africa na alimpa simu sister akaongea naye. Jamaa wa kule South alitushauri tufikie Johannesburg na wakati wa kurudi tutaondokea Capetown.
Changamoto iliyojitokeza ni kwamba sisi tunakwenda Capetown na tukifikia Johannesburg, kwenda Capetown pana distance si chini ya 1,400km unaona umbali huo. Kwasababu ya ugeni na tulihitaji mwenyeji wa kutopokea kwa kule, hivyo hatukuwa na jinsi ilibidi tukubali.
Kwa upande mwingine jamaa wa South alipiga simu na kumpa taarifa Tyna kuwa amepata ticket 2 kutoka kampuni ya Ethiopian Airlines, hivyo alihitaji tumtumie taarifa zetu haraka, pamoja na muda tutakaotumia kule.
Tulimtumia Jamaa taarifa zetu kwa haraka na kuhusu gharama za tickets tulilipa $1,750 kwa wote wawili ‘Go and return’. Baada ya kukamilisha malipo na taratibu zote, alitutumia ticket zetu. Ndege ilikuwa inaondoka saa 9 usiku kwenda South, kwahiyo ingetubidi tusubiri mpaka muda ufike wa safari.
Muda ulikuwa ni saa 11 jioni tayari, tukaanza kushauriana na sister tunakwenda kulala wapi?. Tyna alisema tukalale kwake, hawezi kukubali kuona tunalala hotelini wakati anauwezo wa kutupeleka kwake, tulikwenda kulala kwa Tyna.
Plan yetu ilikuwa turudi Dar siku ya jumatano, hivyo tungekaa siku 2 kule. Kwa upande wa bajeti ilikuwa imekata kwa upande wa sister maana tulitumia pesa zake kulipia tickets na tuliacha dollar zitusaidie tunakoenda. Nilikuwa sijatembea na card, pia huduma za online sijajiunga, hivyo nilipiga hesabu za haraka nikaona nikope pesa kwa mtu, ili tuwe na akiba ya kutosha.
Kwa hesabu za haraka niliona nimuazime pesa Ghati na ile kumpigia simu na kuongea naye, kwa haraka sana alinitumia million 3 na nikazitoa kabisa kwa wakala.
Kesho yake, asubuhi na mapema, tuliwasili JNIA kuanza safari yetu ya kuelekea Afrika Kusini. Baada ya kucheck-in na kukamilisha taratibu zote, tuliingia kwenye ndege. Hata hivyo, tulikaa kwenye viti tofauti, dada yangu alikaa mbele yangu, wakati mimi nilikuwa kwenye kiti cha tatu nyuma kutoka pale alipokaa.
ITAENDELEA
Tujiinjoi tu mkuuKwahiyo stori au chai?? 😂
Hawa hawa tunaocheza nao pool table ? Ya bukubukuAna bwana mwanajeahi
Tiririka mpenzi wangu.. Episodes mbili mpya hizoAbeeeeeee
We nikatae tuWw hataunisltaki unanijaza uongo tu.
😁😁😁ThawaWe nikatae tu
Kwamba dada atakuwa Hana usemi atafungwa mdomo😂Sister akimuona Iryn lazima afashusha hasira tu...na huyu ndo anatakiwa aende Ethiopia
Nimegundua Insider una utoto mwingi sanaSEASON 02

AsanteeTiririka mpenzi wangu.. Episodes mbili mpya hizo