Milion 100
Member
- Aug 13, 2024
- 10
- 13
Mwaga moto mdau insider manUlikuwa na stress za pepa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwaga moto mdau insider manUlikuwa na stress za pepa
Wanawake wakoje mkuuInsider akiona mwendelezo unasubiriwa sana ndo kwaaanza... huyu jamaa angekuwa mwanamke 🤣🤣
vijana kama wewe mnamchango mdogo kwa taifa. mda wote mnawaza tu muendelezo.Baadae bado haijafika?
27 lini johSEASON 02:
EPISODE 26
“BY INSIDER MAN”
PREVIOUS:
Kesho yake, asubuhi na mapema, tuliwasili JNIA kuanza safari yetu ya kuelekea Afrika Kusini. Baada ya kucheck-in na kukamilisha taratibu zote, tuliingia kwenye ndege. Hata hivyo, tulikaa kwenye viti tofauti, dada yangu alikaa mbele yangu, wakati mimi nilikuwa kwenye kiti cha tatu nyuma kutoka pale alipokaa.
CONTINUE:
Safari ya kwenda South Africa ilianza, lakini sikupenda kitendo cha kukaa mbali na dada yangu. Nilitamani nimuombe mtu wa pembeni yangu ili tufanye kubadilishana, japo nikae pembeni na dada yangu.
Pembeni yangu alikuwa amekaa mzungu, hivyo tulipiga story kadhaa, alisema anakwenda South Africa kwaajili ya Utalii na ametokea Canada.
Mimi nilikuwa bado kwenye mawazo kuhusu suala la Iryn, nilikuwa nilijilaumu sana hasa nikiyakumbuka maneno ya dada yangu, nilianza kujuta kwa kujifanya BEBERU na sasa mambo yameharibika. Kuhusu suala la mtoto ni kama nilikuwa nimeshakata tamaa, hata kitendo cha kwenda South Africa nilikubali tu! sababu ya sister, lakini moyoni sikuwa na imani tena, nilikubali matokeo.
Nilianza kuyakumbuka matukio yote ambayo tulikuwa pamoja hasa lile tukio la kwenda Zanzibar na jinsi tulivyo enjoy ile moment. Nilikumbuka ile trip ya Dodoma mpaka tunaenda kijiji cha Mondo, ilikuwa ni moja ya trip nzuri sana, nilikumbuka ile moment before hajaondoka kwenda South Africa, nilijikuta naanza kummiss tena.
Kuhusu suala la mahusiano niliwaza limefika tamati, upendo ulikuwepo baina yetu ni mimba kwa sasa hakuna kitu cha kusema tuendelee kuwa pamoja, labda biashara. Niliwaza hata ofisi yake nikirudi South Africa niache kazi officially na nitaandika barua.
Nisingeweza kuendelea kufanya kazi katika mazingira haya, ningewezaje kufanya kazi na mama Janeth ambaye kanichukia? Ningewezaje kufanya kazi na Iryn ambaye ametoa mimba yangu?. Solution iliyokuwepo ni kuacha kazi, nianze kufanya harakati zangu, pia nilikumbuka ule msemo unaosema kila jambo hutokea kwasababu.
Kwa upande mwingine Iryn kwa namna moja ama nyingine aliweza kuniinua kiuchumi kutoka chini kupanda juu, na kipindi kile anakwenda South Africa kwaajili ya masomo alinipa pesa ndefu sana.
Niliendelea kuwaza mambo mengi sana kuhusu maisha kwa ujumla na future ya familia yangu. Mipango yangu ya Dodoma ilibaki vilevile na nilipanga nikirudi Dar, lazima niende kule.
Asubuhi na mapema tuliwasili Johannesburg kulikuwa ndo kunakucha kwa pande zile. Tuliongozana na dada yangu kwenda ndani, sasa kipindi tunaingia ndani kuna kaka alikuja mbele yetu na kutusalimia na akajitambulisha kuwa yeye ndo rafiki wa Tyna, ambaye anatupokea.
Sister alimuuliza umejuaje ndio sisi?, Jamaa alisema Tyna alimtumia picha ambayo wamepiga pamoja asubuhi ili iwe rahisi kututambua. Ni kweli asubuhi kabla ya kuondoka, Tyna na Sister walipiga picha nyingi sana.
Jamaa alimsaidia Sister kubeba bag na tukaenda kuendelea na taratibu zingine za pale airport na alitusaidia tukakamilisha taratibu zote kwa haraka sana. Baada ya hapo tuliingia moja ya mgahawa kwaajili ya kupata breakfast, jamaa alikuwa ndo mwenyeji wetu.
Tulianza maongezi pale na kubwa jamaa alitaka kujua dhumuni la sisi kuja South Africa. Tulihitaji mwenyeji wa kutusaidia, hivyo tulimwambia kwa ufupi jambo lililotuleta huku.
Jamaa kwa upande wake alisema atatupa kampani ya kwenda Capetown mpaka chuo anachosoma Iryn. Pia tulishauriana ni heri tukaenda kulala Cape town ili tuwe jirani na eneo la tukio.
Tuliendelea kupiga story zingine na jinsi walivyo fahamiana na Tyna, ndo kufahamu kwamba, masuala ya kikazi ndio yaliyo wakutanisha na kupelekea kujenga urafiki wao.
Jamaa alituaga kwamba anakwenda kutuchekia tiketi na kisha atarudi ndani ya muda mfupi. Tulitumia muda huo kuwasha data zetu kupitia Wi-Fi. Kwa upande wangu, niliangalia watu walionicheki, maana tangu niingie Arusha sikuwa na habari na simu. Kwa upande wa Sister, aliwasiliana na Tyna kumpa taarifa ya kufika salama na kuonana na jamaa.
Baadae tulianza kupiga story nami nilitumia nafasi hii kumshukuru sister kwa kujitoa kwake na kukubali kunisaidia kwa hili jambo, kisha tuliendelea kupiga story za kawaida;
SISTER: “Tumeongea sana jana kuhusu dada, lakini sijui jina lake”
MIMI: “Hahahaa! anaitwa Iryn.”
SISTER: “Nioneshe na picha zake nimuone.”
Bhasi, nilichukua simu yangu ili nimuoneshe picha zake japo picha nyingi zilikuwa kwenye simu ya zamani, ambayo ipo home. Baada ya kumpa simu aangalie picha ambazo nilikuwa nazo, nilimuona sister akiangalia kwa makini sana;
: “She’s so beautiful. Huyu ndo mwanamke ambaye unamfanyia hizi drama zote?”
Na mimi niliishia kutingisha kichwa kukubali;
SISTER: “Mdogo wangu una bahati sana, huyu dada ni mrembo sana, sikutegemea ningemwona mwanamke mzuri kama huyu aliyekamilika kila idara.”
Nami niliishia kunyamaza kimya maana dada aliuelewa mziki wa Iryn;
“Nimekutana na wanawake wazuri, lakini huyu ni hatari kwa kumuangalia tu kwa picha.”
MIMI: “Mzee wake yuko huku pia, sema ndo sina namba zake.”
SISTER: “Kesho tutajua namna ya kudeal na hili suala, usijali bro kila kitu kitakwenda sawa, naamini mtoto atazaliwa wewe ondoa shaka, dada yako nipo.”
MIMI: “Mimi sina imani kabisa na nishakata tamaa ya huyu mtoto.”
SISTER: “Kesho tunaonana na Iryn, hatuwezi rudi mikono mitupu.”
MIMI: “Sawa, acha tuone. Pia, nina wasiwasi kwamba mama J anaweza kuwa anatutafuta na hatutopatikana."
SISTER: “Namjua vizuri sana wifi yangu, niliwasiliana nae jana nikamwambia leo tutaenda Kenya, pia nimeongea na shem wako kama incase mama akipiga simu asimwambie tupo huku.”
MIMI: “Hapa umecheza kama Messi dada yangu.”
SISTER: “Sio Pele?”
MIMI: “Bhasi umecheza kama Maradona.”
Tuliishia kucheka pale, kwa mtu ambaye hatufahamu angeishia kuhisi sisi ni wapenzi maana tulikuwa close sana, huku tumejawa na furaha.
MIMI: “Vipi kuhusu hotel ya kufikia? Tufanye mchakato mapema.”
SISTER: “Nafikiri tutafute hotel ambayo itakuwa kati ya airport na chuo.”
MIMI: “Wazo zuri.”
SISTER: “Tumuulize jamaa atusaidie kwa hili, yeye ndo mwenyeji huku. Tutafanya booking ya room moja tu, ambayo tutashare ili tubane matumizi, hakuna haja ya kuchukua room 2.”
Nilishangaa sana kusikia Sister akisema hivi,
MIMI: “Hapana dada yangu, bajeti itatosha usiwe na wasiwasi.”
SISTER: “Mdogo wangu sisi ni familia, ukienda kuoga unavalia hukohuko, nami itakuwa vivyo hivyo, tusichezee hela bila sababu bro!.”
MIMI: “Sawa haina shida kama wewe umeridhia hili, mimi napingaje?”
SISTER: “Hatujaja kulala huku tambua hili, kazi yetu ni kumtafuta mama kijacho mpaka tumpate, kwanza hamu ya usingizi unaipatia wapi?, utakuwa na matatizo sio bure.”
Baada ya lisaa kupita jamaa alikuja kutupa taarifa amepata ticket tayari, na ndege itaondoka saa 7 mchana. Kuhusu suala la hotel jamaa alitushauri tufanye booking Southern sun Newlands Hotel, kwani ni nzuri, affordabe na ni sehemu salama.
Good news jamaa alikuwa na mtu ambaye anafahamiana naye anafanyia kazi pale hotelini, hivyo alimpigia simu na kumpa taarifa ya booking, akamwambia tutafanya payment tukiwasili hotelini.
Kwa kuwa tulikuwa na muda wa kutosha kabla ya safari, tuliamua kushauriana na kubadilisha sarafu kwanza. Baada ya hapo, tuliamua kuzurura kidogo nje ya uwanja wa ndege ili kutembea, kusafisha macho, na kupiga picha.
Tulienda kukaa moja ya cafe, tukaagiza juice tukaanza kunywa huku tunapiga story. Na story zetu kubwa zilibase namna ya kumpata Iryn na tulipanga lazima tufanikishe hili jambo.
Dada aliendelea kunishauri nitulie kwasasa nifocus na familia. Kwa asilimia kubwa biashara ya Uber ilinibadilisha kitabia, lakini pia ilibadilisha maisha yangu, equation ilikuwa balanced.
Baada ya masaa 2 kupita tuliamua kurudi Airport kwaajili ya kuangalia utaratibu wa safari, na tuliweza kuonana na jamaa ili atupe maelekezo akasema tusubiri nusu saa, kisha tuta check-in.
Tuliendelea na maongezi pale, lakini jamaa alibase sana kuongea na sister, na kubwa aliendelea kutupa ahadi ya kutusaidia jambo letu, hivyo kesho atakuja asubuhi kwaajili ya hili. Sister kwa upande wake alifurahi sana, ila kwangu mimi ilikuwa tofauti, nilihisi huenda jamaa anafanya hayo yote kwaajili ya sister.
Baada ya nusu saa tulianza safari ya kwenda Capetown, na tulitumia masaa 2 na nusu kuwasili Capetown International airport. Kwa upande wa huku airport kuna dada alitupokea ambaye anafahamiana na jamaa, na alitusaidia kupata tax ya kutupeleka hotelini.
Baada ya kuwasili hotelini, dada mwingine tena alitupokea na kujitambulisha yeye ni rafiki wa jamaa na amepokea taarifa ya ujio wetu pale hotelini. Tulikuwa bado hatujalipia room, hivyo tulifanya malipo na tukapelekwa moja kwa moja mpaka room yetu.
Saa ilionesha ni saa 11 jioni tayari, kutokana na uchovu tulipumzika kwanza maana kila mmoja alikuwa na usingizi. Saa 2 za usiku dada aliniamsha nikaoge ili tukapate na dinner, kisha tuanze kupanga mipango kwaajili ya kesho.
Kipindi tunapata dinner mipango ilikuwa inafanyika jinsi tutakavyokwenda chuoni kwa bahati nzuri tulikuwa na mwenyeji, hivyo tulikuwa tunajiamini sana tutafanikiwa hili jambo.
Baada ya kupata dinner nilifanya mawasiliano na Lucy kumuuliza kama kuna lolote na alisema hakuna mpya, nilimpa taarifa niko South Africa, na alinbaki akishangaa juu ya maamuzi magumu niliyoyachukua na aliishia kunipongeza.
Baada ya kuongea na Lucy niliwasiliana na Sumaiya kumuuliza kama amefanya mawasiliano na mama hivi karibuni, alisema mama yuko field na kama atamtafuta, bhasi atanipa taarifa.
****
Asubuhi tulijiandaa mapema kwaajili ya kwenda chuo kisha tulienda kupata breakfast huku tukimsubiri Jamaa. Saa 4 kasoro jamaa ndo aliwasili pale hotelini, kisha tukaanza safari ya kwenda chuo, ndani ya mfupi tuliwasili pale chuoni.
Baada ya kuwasili hatua ya kwanza kabisa tuliulizia ofisi za ‘Dean of student’ na tukaelekezwa ziko jengo la utawala. Mandhari ya chuo ilikuwa ni nzuri sana kwakweli kwa Tanzania hatuna chuo, angalau UDSM kwenye suala la mandhari na mazingira wako vizuri.
Tulifanikiwa kuonana na Dean, kisha tukamwambia lengo la kuja chuo ni kumtafuta Iryn na tulimsimulia mkasa mzima. Huwezi amini, Dean alitukazia na sababu kubwa alisema hatutambui na hatuna uthibitisho wowote. Alienda mbali zaidi akasema anaweza kutuchukulia sheria, kwani kama kuna tatizo alipaswa kuja mzazi wake au mtu baki anayetambulika na chuo.
Dean aliongea ukweli mtupu, hivyo hatukuwa na jinsi ilibidi tushauriane tunachukua hatua gani? maana ni kweli chuo hakitutambui. Kwa upande wangu sina uthibitisho wowote kwamba Iryn ni mpenzi wangu, unaona ukakasi ulivyo hapa;
SISTER: “Yaani kuhangaika kote, tumekuja huku kupoteza muda na Pesa? Impossible. Anasoma MBA nafikiri tujaribu kwenda kwenye kitivo cha Biashara huenda tukafanikiwa.”
JAMAA: “Dean ndo kila kitu, kwenda huko ilitakiwa tupate ruhusa kutoka kwa huyu, tusije tengeneza matatizo, acha niangalie namna nyingine ya kuwasaidia.”
Sister hakuwa anaeleewa kabisa na yeye aliendelea kuforce twende huko kwa kitivo, bhasi ikabidi twende. Baada ya kufika reception tuliomba kuonana na Dean wa kitivo, tukaulizwa kama tuna appointment naye, tukasema hapana ila ni urgent. Tukaambiwa ametoka ana kikao, lakini tunaweza kuonana na mkuu wa Idara (HOD) na tukapelekwa mpaka kwa ofisi zake.
Baada ya kufika ofisini kwake, tulikaribishwa ndani, tukakaa kwenye sofa, na tukaletewa maji ya kunywa huku tukimsubiri HOD.
HOD alikuja pale kutusikiliza, ni mzee wa makamo, tulisalimiana naye na alitukaribisha sana, kisha tukaanza maongezi. Tulimwambia ukweli HOD kuwa sisi ni watanzania na tumekuja South kwaajili ya kumtafuta mpenzi wangu maana hapatikani kwa simu ni mwezi sasa na ni mjamzito.
Pia, tulimwambia ukweli kwamba tulianza kwenda ofisi ya Dean, lakini kutuchomolea. HOD alikuwa mwelewa sana na akasema tuende tukamwone Academic Supervisor wake, ambaye ndiye atakayesaidia vizuri kwa sababu ana taarifa zote za mwanafunzi, ikiwa ni pamoja na anakoishi, ndugu zake, na mambo mengine mengi.
Tulielekezwa kwenda kwenye floor ya juu inayofuata, mpaka ofisi namba C322, na kumuulizia Madam Marlinda.
Baada ya kufika ofisini kwake, tuligonga mlango na kukaribishwa ndani. Tulipoketi, tuliona jina lake likiwa limeandikwa kwenye meza yake, jambo ambalo lilitusaidia kujua moja kwa moja kuwa ndiye yeye, bila ya kumuuliza.
Madam Merlinda ni mzungu. Jamaa alianza na utambulisho, kisha Madam akatuuliza shida yetu ni nini.
JAMAA: “Madam hawa ni ndugu zangu kutoka Tanzania, tunafahamiana kwa miaka 5 sasa ni familia kwangu. Sasa wamekuja hapa wanashida personal na HOD ndiye ametuleta hapa kwako utupe msaada.”
MADAM: “Sawa nawasikiliza.”
SISTER: “Madam sisi tumekuja kumuulizia wifi yangu anaitwa Iryn na huyu ni kaka yangu ndo mpenzi wake. Kilichotuleta huku ni kwamba hatumpati kwenye simu ni mwezi sasa, halafu ni mjamzito, hiki ndo kinatupa wasiwasi.”
MADAM: “Mnavielezo vyovyote juu ya hili?”
SISTER: “Hapana hatuna.”
MADAM: “Mimi ni Academic supevisor wake, lakini sasa mbona nyie siwajui? Ninawaona kwa mara ya kwanza. Ndugu zake wa karibu huwa nawasiliana nao na huwa wanapiga kujua maendeleo yake hapa chuo, mpaka sasa hawajapiga simu kuniuliza hili, who are you guys?.”
SISTER: “Ni kweli madam unachosema maana watu wake wa karibu tunaowajua akiwepo kaka yake naye hapatikani, ndomana tukaona tuje chuo tupate mwanga kidogo, hatujaja hapa kwa kubahatisha..”
MADAM: “Inakuwa ngumu kuwasaidia sababu mzazi/mlezi ambaye anafamika na chuo ndo alipaswa kuja hapa na si mtu baki.”
MIMI: “Naomba nikuoneshe picha zake tukiwa pamoja na uthibitisho wa mimba yake.”
Nilisogea karibu na simu na nikamuonesha picha, pamoja na zile ambazo Iryn alikuwa akipiga maeneo ya chuo. Madam alishindwa kuamini, lakini sasa macho yake hayakumdanganya—aliyekuwa akimuona kwenye picha alikuwa ni Iryn akiwa na mhuni.
Madam alikuwa mpole ghafla na alionesha kutabasamu maana picha nyingi zilionesha tuko kwenye mahaba;
MADAM: “Una bahati sana kupata mwanamke mzuri na clever. Kwa hizi picha hapa sasa nina weza kuwasikiliza vizuri, ni kweli ni mjamzito. Labda niwaambie hivi, Iryn aliandika barua ya kuhairisha masomo yake mpaka semester nyingine kutokana na afya yake.”
Tulishtuka sana kusikia Iryn amepostpone masomo yake maana hatukutegemea kuzipata hizi habari.
SISTER: “Hatujaja kwa nia mbaya, na kumbuka tumetumia pesa kuja huku kwaajili yake kuonesha tunampenda na kumjali, ni wachache sana wangekuwa na huu uthubutu.
Ombi letu utusaidie namna ya kumpata naamini lipo chini ya uwezo wako madam.”
MADAM: “Chakuwasaidia nitapiga simu lakini sio kuwapa namba maana siruhusiwi bila kibali.”
Alianza kupiga simu ya Iryn lakini ikawa haipatikani.
MADAM: “Namba yake haipatikani pia.”
MIMI: “Inaishia na 33?”
MADAM: “Yes! ngoja niwapigie na ndugu zake.”
Kupiga simu walikuwa hawapatikani japo sikuwafahamu hao ndugu zake ni nani.
Madam aliomba namba yangu akasema akifanya nao tena mawasiliano, bhasi atawapa taarifa kuhusu mimi. Kwa upande mwingine sister alimkaribisha madam Arusha na kumpa ahadi ya kumpeleka Ngorongoro na Serengeti, madam alishia kufurahi, kisha wakabadilishana namba za simu.
Madam alitupa moyo juu ya hili na alisema mpaka ameomba kupostpone masomo yake ni dhahiri anataka apate muda wa kutosha kupumzika na mimba yake. Alitupa kampani mpaka nje, kisha tukaagana, nami nilimtania kwamba next time nitamleta Iryn chuo na aliishia kucheka.
Tuliondoka chuo huku tumenyong’onyea sana maana hatukuwa na option nyingine ya kufanya kwa upande wa chuo. Tulirudi hotelini kufikiria next move kuhusu kumpata Iryn na solution ilikuwa tumtafute mzee wake.
Jamaa alifanya kuwasiliana na mwanasheria ambaye anafahamiana nae na majibu aliyotupa ni kwamba, tunapaswa kutoa taarifa
Ubalozi wa Tanzania sababu hili jambo lipo kimkakati sana. Pia, alisema tunapaswa kuwa na evidence au uthibitisho wowote unaonesha mimi na Iryn ni wapenzi au tunatarajia kupata mtoto pamoja.
Baada ya kufikiria sana tukaona pana ukakasi hatuna option nyingine ya kufanya. Jamaa kwa upande wake alisema atatusaidia kuangalia movement za Iryn kwa pale airport kama ametoka au laah! kisha akatuaga na kuondoka.
Moyo wangu kama ulipigwa ganzi maana nilianza kuona freshy tu, nilikuwa nimeshajiandaa kisaikolojia toka muda mrefu ndomana nilianza kuizoea hii hali. Sister kwa upande wake alionekana kuwa na mawazo sana na nilijua lazima anafikiria kuhusu hili wala si kingine, nami nilimuacha.
Saa 12 jioni, jamaa alipiga simu na kutujulisha kwamba Iryn ameondoka kwenda Dubai jana, Jumapili na aliondoka Cape Town saa 2 asubuhi. Baada ya kusikia hizi taarifa sister alipaniki sana na alizidi kuwa mnyonge sana;
SISTER: “Bro! Tumemkosa mtoto tayari, I’m so sorry.”
MIMI: “I told you, wewe ulinipa matumaini. Mimi nimekubali matokeo ninaamini kila kitu ni mipango ya Mungu.”
SISTER: “Kinachonipa mashaka kwanini aende Dubai?, kule watu wanafata starehe, kivipi mjamzito aende kule?”
MIMI: “Dada tuachane na haya, naona yanazidi kuniumiza tu, tuangalie namna ya kuondoka huku, hata jumatano naona ni mbali sana.”
SISTER: “Kama efforts tumefanya za kutosha, lakini hatujafanikiwa. Mungu hawezi kutuacha trust me.”
Usiku tulikuwa tunapiga stori, ambapo tulikubaliana kwamba kesho tutaenda mjini kwa ajili ya kupiga tour na kufanya shopping kulingana na bajeti yetu. Aidha, nilipokea habari nyingine nzuri kutoka kwa dada yangu; alinijulisha kwamba anatarajia kupata mtoto wa tatu, na mimba yake bado ina mwezi mmoja tu.
Kesho yake saa 4 za asubuhi, tuliondoka kwenda kuzurura city centre kwa lengo la kushangaa mji na kufanya shopping. Lakini tulishauriana kwamba, tuanze kwenda moja ya beach nzuri, kisha mipango mingine iendelee.
Tulienda Clifton Beach, mahali ambapo kulikuwa na watu wengi wakifurahia maisha. Tulipiga picha nyingi za kuvutia pale beach kwa sababu ni nzuri sana na ina mandhari ya kuvutia, pamoja na pisi kali za kila rangi ambazo ziliongeza uzuri wa eneo hilo.
Sister alitokea kuipenda sana hii beach, hata kuondoka alikuwa hataki na tulitumia kama masaa 3, kisha tukaondoka kwenda malls mbalimbali kwaajili ya shopping ikiwemo ‘Canal walk shopping centre’.
Sister alikuwa ananunua mazaga yake kama vipodozi, nguo na viatu nami nilifanya surprise ya kumnunulia mazaga mengi tu na aliishia kufurahi kuona nikimpa surprise.
Baada ya kumaliza shopping tulisogea KFC tukapata chakula na tuliondoka kurudi hotelini kupumzika. Kwa upande wetu mimi na dada tulikuwa watu wenye furaha sana, hata suala la Iryn ni kama tulilisahau kwa muda maana tuliamua kufurahia maisha.
Baada ya kurudi hotelini tulibadilika chap tukaenda swimming pool kupoteza muda. Dada yangu anajua sana kuswim, kwahiyo tulikuwa tunashindana pale, japo alikuwa akinishinda maana mimi naogelea kawaida ila yeye yuko vizuri sana.
Tulishinda swimming mpaka giza linaingia, ndo kurudi room kubadilika ili tukapate dinner. Kipindi tuko room sister alikuwa amejilaza kitandani nami niko busy na laptop yangu nikiandika mipango yangu.
Kwa upande wa sister nilimuona akicheka ikabidi nimuulize kuna nini?
MIMI: “Dada yangu umefurahi nini?”
SISTER: “Si huyu mshenzi ananifurahisha hapa, eti ananitongoza.”
MIMI: “Nilijua tu lazima akutongoze nilisha msoma muda mrefu, kwani haoni hio pete uliyovaa?”
SISTER: “Nashangaa labda hajaiona au anafikiri ni urembo.”
MIMI: “Anafanya makusudi tu, anasemaje?”
SISTER: “Anasema yuko njiani anakuja kunichukua twende tukapate dinner na atanirudisha late sana. Nimemwambia siwezi kutoka alone nikamwacha brother peke yake hotelini, nitakuwa dada wa aina gani? Kama vipi twende pamoja na wewe.”
MIMI: “Akasemaje?”
SISTER: “Amesema haiwezekani maana ana mazungumzo private na mimi, haoni sababu ya kuongozana na wewe. Nimemwambia kwa mazingira ya huku sisi ni wageni, pia brother hawezi kubali mimi nitoke alone. So amesema anakuja hotelini tuongee, nimemwambia sawa haina shida.”
MIMI: “Nenda akakupulizie dawa shauri zako.”
SISTER: “Thubutu! hivi unanionaje? Unasahau enzi zangu?.”
MIMI: “Hahahaa sawa bhana, wewe nenda mimi siwezi kukuzuia ila kuwa makini, ukiona dalili zozote mbaya text me.”
Sister alienda hotel lobby kuonana na jamaa, kisha mimi nikaendelea na mambo yangu. Niliendelea kufikiri, pindi nikirudi Dar, jambo la kwanza kabisa nitaandika barua ya kuacha kazi na kuikabidhi kwa Hilda. Halafu nitaondoka kwenda Dodoma, nilijihapia kukaa mbali na mtu anayeitwa mwanamke kasoro mke wangu tu mama J.
Yalipita masaa 2 kimya hakuna dalili za sister kurudi, ikabidi nimtext kama kuna usalama, nikagundua ameacha simu chaji. Nikapata wazo nishuke kuangalia kama kuna usalama maana nilianza kupata wasiwasi asije kuwa ameingia 18 tayari kaamua kuondoka na jamaa.
Nilishuka kwa step kama Rambo ili nisigundulike na nilifanikiwa kuwaona wakiongea, lakini walionekana kuwa deep sana kwenye maongezi. Nilianza kujiuliza hivi ni nini wanaongea karibu masaa mawili? Nilijua lazima jamaa anamtongoza dada yangu. Niliona kabisa dada anashindwa kumpa majibu ya direct kwasababu ya ugeni na ukizingatia jamaa katupa sana kampani huku South Africa.
Sister yangu anajielewa, hivyo niliamua kuwaacha na kurudi room kuendelea na mambo yangu. Baada ya kurudi nilimpigia simu wife ili kumsalimia maana alikuwa anajua sisi tupo Kenya na nilimpa taarifa ya kurudi kesho na nimemnunulia zawadi kibao kutoka Kenya, lakini niliona kama hana furaha kabisa.
Nilihisi something wrong kwanini wife hana furaha? Nilimuuliza tatizo ni nini? Akasema yuko sawa hakuna shida na niwe na amani na tukaagana. Niliwaza pale au wife kajua sisi hatupo Kenya? Kwanini awe hivi? Haya yote nitayajua nikirudi ila kwanza nitaongea na Sister kama kuna lolote.
Baada ya lisaa sister alirudi na ile kumwangalia alinibinulia mdomo juu tukaanza kuongea pale na kubwa alikuwa ananipa ripoti ya kilichokuwa kinaendelea.
MIMI: “Masaa 3 mlikuwa mnaongea nini? Kama hujaingizwa 18 sijui.”
SISTER: “Hahaha hamna jamaa kanitongoza sana weee! Mara anasema tuondoke jumapili na atatulipia hotel. Nikamwambia pesa sio tatizo hata sisi tunatamani tukae mwezi huku ila masuala ya kazi ndo yanatuwaisha Tanzania.”
MIMI: “Nakusiliza dada nipe ubuyu.”
SISTER: “Bhasi bhana, badae kafunguka oh mimi nimetokea kukuelewa tuwe wapenzi, nikawambia pole umechelewa mimi ni mke wa mtu na nina watoto wawili. Unajua alikuwa haamini kabisa, alihisi kama namtania, yeye anasema naonekana sijazaa kwahiyo namdanganya. Ikabidi nimtajie username yangu ya Instagram ajionee mwenyewe ndo kuamini sasa.”
MIMI: “Duuh! Umejilipua kwahiyo hajamind?”
SISTER: “Anaanzaje? Nimemwambia aje Arusha nimpeleke Serengeti akatalii, amekubali atakuja April.”
MIMI: “Umefanya busara, mama J kanipigia simu seems kama hayuko sawa hivi.”
SISTER: “Wifi anashida gani tena au amefahamu hatuko Kenya?”
MIMI: “I don’t know labda nikuulize wewe, usije ukawa umejichanganya huko au umepost picha.”
SISTER: “Hapana, labda ana jambo lingine hata leo tumechati ile asubuhi hakuna lolote. Vipi sasa kuhusu kampuni ya bibie, utaendelea kufanya kazi?”
MIMI: “Nikirudi naandika barua ya kuresign sitaki hata kuisikia, nafanyaje kazi na mwanamke aliyetoa mimba yangu?”
SISTER: “Hatuna uhakika kama katoa ila tunahisi kafanya hivyo, cha kukushauri usiache kwanza moja kwa moja endelea kubuy time kama ulivyofanya sasa. Bibie ndo aliyekuajiri kwahiyo subiri mpaka yeye afanye maamuzi, usifanye maamuzi ya haraka endelea kukaa pembeni huku unaendelea kuisaidia kampuni. Usiache kazi kwenye mazingira magumu kama haya,acha kazi kwenye mazingira mazuri maana kuna kesho pia.
MIMI: “Ahsante kwa ushauri ila naona kama siwezi kuendelea acha nimove on.”
SISTER: “Nisikilize mimi, acha kuwa na maamuzi ya haraka ndomana huwa unaharibu, tumia sana akili kwenye hili jambo, acha wao wakufukuze kwani utapungukiwa na nini? Na usijaribu kuwaibia hata cent.”
MIMI: “Alright, nimekuelewa.”
SISTER: “Usijali mdogo wangu ila kwasasa katulie na familia yako, katubu dhambi kanisani na mfunge harusi haraka iwezekanavyo. Nadhani kwasasa umegundua wanawake wote wanapita ila mama J bado yuko na wewe kwa kipindi chote.”
Tuliongea mambo mengi sana na dada huku tukipanga vitu kwaajili ya safari ya kesho kurudi Tanzania.
TO BE CONTINUED
sijasema amedanganya maeneo, ila nimesema 'story kuhusu zambia' ni kamba!Ni wewe peke yako, maeneo yote nayajua hakuna alikokosea hata moja, kujichanganya kupo kwa mgeni, but yuko sahihi. Nandos restaurant nimeshapata dinna pale, maeneo karibu yote nayajua. Victoria falls amekwenda mlemle,
cacutee my love mzigo mpyaSEASON 02:

naelewa maeneo aliyotaja ni sahihi, ila 'kwenye huu mfululizo' hii story ya zambia imeingizwa tu..... baba yake hayuko zambiaNiliwahi kuwa Zambia maeneo aliyoyataja nimewahi kufika
INAENDELEA… EPISODE 02:
Kiukweli sikuamini kama nikweli maana niliona kama ndoto hivi, nikasema hawa wanaweza kuwa matapeli, inshort sikuwa interested na ile simu. Sikumwambia mtu yoyote juu ya hili jambo hata mama sikumwambia maana niliogopa wasije wakawa matapeli. Hapo nilikua tayari nina miezi 2 niko home, wakati nimefika mzee wangu alikaa siku 3 akarudi Zambia.
Mzee wangu ni engineer kule kuna kampuni anafanyia kazi na pia mzee wangu kurudi home ni nadra sana anaweza kukaa hata miezi 3 na zaidi bila kurudi nyumbani. Nilikua naongea na mama mambo mengi sana hasa alikua anataka kujua pale kwa Uncle kama ninaishi vizuri. Ni kwamba mama yangu anamjua vizuri sana Aunt ni mtu wa namna gani, sikutaka kumwambia mama lolote kuhusu pale kwa Uncle niliamua kuyaweka moyoni. Japo mama alihisi kuna jambo halipo sawa,lakini alinisistiza sana kuwa na adabu na heshima. “Kila siku usiku tulikua tunapiga maombi na mama” mama yangu ni mtu wa dini sana.
mkuu, labda kama aliamua kublow cover ya hii story, otherwise majina ya maeneo lazima ameyabadili ili kulinda 'watu'.....dong yi toka season 1 episode 2 jamaa alituambia baba yake yuko huko. Ingekuwa ni season 2 anatupa hizi habari hapa ndo ningekuamini.
Hahaha proba ni 0.0001 ila code nyingi zipo open.mkuu, labda kama aliamua kublow cover ya hii story, otherwise majina ya maeneo lazima ameyabadili ili kulinda 'watu'.....
jaribu tu kufikilia story za jane, prisca, mary, saloon zilipo, Asma then unadhani ni maeneo halisi hayo? mbona angejiharibia sana!
Sure acha tuenjoy sisi.mkuu, labda kama aliamua kublow cover ya hii story, otherwise majina ya maeneo lazima ameyabadili ili kulinda 'watu'.....
jaribu tu kufikilia story za jane, prisca, mary, saloon zilipo, Asma then unadhani ni maeneo halisi hayo? mbona angejiharibia sana!
HahahaaSterling hafi...subiri Sterling Iryn nxt episode atakavobadili upepo
Asanteee