Tabia za kike, ukitetea basi na wewe utakuwa nazo hizo tabia .
Mwanaume unanukia ili iweje kwa mfano. Wanaume asili yake alienda na anaenda porini akawinde alete kitoweo. Alipigana vita ku conquer others tribe cattle and land.
Na hizi bado zinaendelea in very modern way Sasa na wewe unawaza kunukia ni lini utafanya hayo.
Mwanamke ni ua inabidi anukie amridhishe ama amfurahishe mmewe.
Ndo maana me nawakubali UMUGHAKA n Analyse wakianzisha story inaenda kwa mtiririko na kwa muda muafaka inaisha. Sio hii story inakuwa ndefu kama isidingo af msimuliaji anasimulia kama hataki😂😂😂😂
Huu ni mkasa unaoendelea kwenye maisha yake ya kila siku mbona ngumu kuelewa?kuelewa mkuu akikaa na kukusanya matukio ya mwezi mzima huoni story inakuwa kwenye mtiririko mzuri?
SEASON 02
CHAPTER 29
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
PREVIOUS:
Saa 12 jioni nilianza safari ya kwenda Dodoma na nilichukua bodaboda wa kunipeleka Magufuli stand. Muda wa jioni mabus huwa yanasumbua hivyo, nilisogea pale darajani kwa Yusuph nikapata private inayokwenda Dodoma.
CONTINUE:
Safari ya kwenda Dodoma ilianza pale na gari ilikuwa ni Harrier. Tulikuwa jumla ya watu sita, pamoja na dereva. Tulikaa wanne nyuma ya seat, tukiwa tumebanana kimtindo—wanaume wawili na wanawake wawili.
Nilipokuwa barabarani, nilikuwa kimya sana, hata sikushirikiana na wenzangu katika mazungumzo. Nilikuwa nikiwaza mipango yangu ya biashara Dodoma na kupanga kumpigia simu dalali kumkumbusha kuhusu jambo letu.
Lengo langu la kwenda Dodoma ni kufungua biashara ya kuuza lubricants za magari na kufanya services. Nia yangu hapo baadae nipanue biashara hii kwa kuuza bidhaa kama vipuri vya magari, urembo, rims, na matairi.
Niliweka lengo kwamba ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo, nitakuwa tayari nimeanza biashara yangu. Nilidhamiria kwa dhati kuanzisha biashara. Pia, nilipanga kuwa na nidhamu ya fedha kwa kipindi chote nitakachokuwepo Dodoma.
Saa 7 za usiku, tulipowasili Dodoma, baridi kali lilikuwa limetanda. Nilipata lodge iliyoko karibu na Chuo cha CBE na kwenda kupumzika.
Asubuhi baada ya kuamka jambo la kwanza niliwasiliana na Aggy kumpa taarifa niko Dodoma. Kwa upande wake alishangaa sana kusikia nimekuja bila kumtaarifu mapema na alisema baada ya nusu saa atakuwa around.
Baada ya hapo, nilimpigia simu dalali ili anipe mrejesho pamoja na ratiba zake. Lengo langu lilikuwa kuanza leo hii kutafuta frem za biashara ili mipango yangu iende kama ilivyopangwa. Dalali aliniambia tukutane baadae, na akanihakikishia kwamba bado anaendelea kutafuta frem zingine ili tuwe na chaguo la kutosha wakati wa kuangalia.
Ndani ya nusu saa, Aggy alikuwa tayari amewasili, nami nikatoka kwenda kuonana naye ili tuondoke. Tulipokutana, tulisalimiana kwa furaha na tukakumbatiana kwa upendo, kisha safari yetu ya kuelekea nyumbani kwake ikaanza.
Aggy alionesha kuwa na furaha sana maana mara ya mwisho kuonana ilikuwa ni October kipindi nimeenda na Iryn. Aggy aliulizia kuhusu maendeleo ya nyumbani na hakumsahau Iryn, ndipo mazungumzo yakaanza;
AGGY: “Yule mrembo yupo?”
MIMI: “Yupo mama ila sio Tanzania hii.”
AGGY: “Na kwanini unakuja bila kunipa taarifa na unafikia lodge?”
MIMI: “Nilitaka nikusurprise au hujapenda?”
AGGY: “Tufanye umeshinda.”
MIMI: “Naona unazidi kuwa mrembo nipe siri ya mafanikio au mama anamwaga pesa mingi huko maofisini.”
AGGY: “Hahahahaa hali mbaya Insider bora hata wewe uliejiajiri.”
MIMI: “Hamjawahi kukubali kuhusu hili, sawa bhana.”
Ndani ya muda mfupi tuliwasili nyumbani kwake na alinikaribisha seblen kisha akaniandalia na chai ili ninywe. Aggy alitamani sana kujua sababu iliyonileta Dodoma, nami nilimwambia mipango yangu yote na aliishia kunipongeza. Nilimwambia nitakuwepo Dodoma kwa muda mrefu mpaka pale ambapo nitaona biashara imesimama na haihitaji tena usimamizi wangu.
Aggy aliniaga anarudi ofisini na kutoa ahadi atawahi kurudi, kwa upande wangu nilimpa ratiba zangu za kutoka jioni kwenda kuonana na dalali, na alisema atakuwa karudi tayari, hivyo atanipa kampani ya kwenda.
Saa 10 jioni tulikutana na dalali maeneo ya Sabasaba, kisha tukaanza kuangalia frem zote alizokuwa nazo. Baada ya kuzunguka sana niliipenda frem moja ipo katikati ya mjini ilikuwa location nzuri sana.
Muda ulikuwa umeenda sana, na mhusika wa hii frem alituambia tukutane kesho asubuhi ili kuweka mambo sawa. Baada ya hapo, Aggy alipendekeza tupitie sehemu kwaajili ya kupata chakula cha jioni, tutakapokarudi nyumbani, ni kulala moja kwa moja.
Wakati tulipokuwa tunakula chakula, mazungumzo yaliendelea pale, ambapo Aggy alisema kwamba mwezi ujao anatarajia kusafiri kwenda mkoani kuwasalimia wazazi wake. Nami niliona wazo lake lilikuwa zuri sana, hivyo lilinipa hamasa ya kwenda kumtembelea mama, na tukakubaliana kwamba tutaenda pamoja.
Kama nilivyowahi kusema hapo awali, mimi na Aggy tulisoma katika chuo kimoja, tukichukua course moja. Zaidi ya hilo, tulipitia shule moja ya O-Level, na wazazi wetu pia wanatoka mkoa mmoja.
Baada ya kurudi nyumbani, nilimpigia simu Maggy kumtaarifu kuwa nipo Dodoma, isinge kuwa busara kula buyu ukizingatia ananisaidia sana kuangalia nyumba yangu. Hata hivyo, baada ya kumpigia hakupokea simu zangu, kwa vile muda ulikuwa umekwenda, nilijisemea kwamba akiziona missed call atanipigia.
Aggy alikuwa amepanga nyumba ya vyumba viwili, hivyo alinionesha chumba changu cha kulala, kisha akaniga anakwenda kulala na tutaonana kesho.
Asubuhi baada ya kuamka nilikuwa na ratiba ya kukutana na dalali ili kwenda kufanya malipo kwa fremu iliyokuwa kwenye mipango yetu. Lakini, dalali alinijulisha kuwa kuna fremu nyingine mpya imepatikana na iko kwenye eneo la Sheli, tukakubaliana tuanze kwanza kuiangalia hio frem.
Baada ya kuliona eneo lilikuwa lina mvuto mkubwa, na nikawaza kuwa litakuwa na faida kubwa kama likitumika kama sehemu ya kufanyia service, huku eneo la mjini likiwa kama showroom. Nilionana na mhusika na baada ya maongezi ya muda mrefu akasema wanapangisha kwa 350,000, hivyo nilichukua namba zake za simu na tukaondoka.
Dalali alinishauri kama naweza nichukue eneo la sheli maana nitapata wateja wengi sana wa service, kwani sehemu ni nzuri sana. Tulishauriana sana na nikamwambia anipe muda nijifikirie, na alisema kuhusu fundi yupo dogo anamjua na anacheti cha VETA naweza kufanya naye kazi.
Tulienda straight kuonana na landlord ili tufanye malipo ya frem ya jana na baada ya kukutana na mhusika nilifanya malipo ya 2.4M kwa miezi 6. Sikutaka kupoteza muda nikatafuta fundi wa kuanza kutengeneza shelves ili nianze biashara.
Niliandaa mipango yangu nikaona kuna haja ya kurudi Dar kwaajili ya kuchukua mzigo wa lubricants/vilainishi. Habari njema hii biashara nina uzoefu nayo, hivyo haikuwa shida kwangu kuifanya na kuwatafuta suppliers maana machimbo yote nayajua na nina namba zao.
Niliwaza kutafuta chumba cha kupanga kwa kipindi chote nitakachokuwa Dodoma. Kuendelea kukaa kwa Aggy sikuona jambo la busara ukizingatia mimi ni mtoto wa kiume, nahitaji uhuru.
Mipango yangu ilikuwa kufikia jumatatu niwe nimenza biashara, pia niwe nimeondoka kwa Aggy tayari. Lakini jambo la kwanza nitaanza kwenda Dar, kisha baada ya kurudi nianze mchakato wa kutafuta geto.
Jumamosi frem ilikuwa imekamilika tayari kwa kuingia na kuanza bishara, hivyo nikaona kesho jumapili nirudi Dar, ili jumatatu niwe Kariakoo kuchukua mzigo.
Jioni nilienda kumsalimia Maggy nyumbani kwake maana ilikuwa ni kitambo kimepita bila kuonana. Baaada ya kuwasili pale kwake alinikaribisha, lakini nilianza kwanza kukagua nyumba.
Mazingira ya nyumba yalikuwa mazuri na yakivutia, kwani palikuwa pamepandwa maua maua na miti ndani na nje ya fenzi. Pia nilimsalimia jirani yake ambaye ni mpangaji wangu, baada ya hapo tukaingia ndani kuendelea na maongezi mengine;
MAGGY: “Karibu sana baba mwenye nyumba, sijui nikuletee kinywaji gani?”
MIMI: “Maji yanatosha.”
Alimuagiza dada aniletee maji na story zikaendelea;
MAGGY: “Umekuja lini huku? Halafu kimya kimya.”
MIMI: “Nilitaka nikufumanie una bahati sana.”
MAGGY: “Huhuuu! Yule dada mrembo yupo?”
MIMI: “Yupo masomoni ni muda hatujaonana.”
MAGGY: “Kwa uzuri tu amebarikiwa asee, kuna watu walipendelewa.”
MIMI: “Mbona wewe umependelewa mahips au hujioni?”
MAGGY: “Insider ni mshenzi wewe! Mimi nimefurahi sana kukuona, sijui wifi yangu anaendeleaje na mtoto.”
MIMI: “Wako poa nashukuru Mungu. Bado wewe sijui unasubiri nini.?”
MAGGY: “Wanaume waoaji kama wewe hawapo siku hizi.”
MIMI: “Naamini shemeji yupo ila unamfichaficha.”
MAGGY: “Insider tuachane na haya, nimekumiss sana Dar.”
MIMI: “Karibu sana kwenye mji wetu.”
Tuliongea mambo mengi likiwemo suala langu lililonileta Dodoma, pia kwa upande wake alisema ana mpango wa kutafuta kiwanja aanze ujenzi taratibu. Tulipata dinner ya pamoja na baada ya hapo nilimuaga maana Aggy alikuwa akinipigia sana simu.
Baada ya kuagana na Maggy nilimpigia simu Aggy na alisema ananisubiri ili tukale dinner, nikamwambia nimeshakula tayari, akaomba nimpelekee chips yai na mishikaki.
Baada ya kurudi home nilimtaarifu Aggy kuhusu kurudi Dar siku ya kesho kwaajili ya kuchukua mzigo na nitarudi jumatatu na nikamuaga nikaingia chumbani kulala.
Jumapili asubuhi, niliondoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam na nilifika nyumbani jioni kwenye makazi mapya. Mara baada ya kufika, mazingira yalikuwa tulivu sana kiasi kwamba nilianza kumkumbuka Junior wangu, kwa jinsi nilivyozoea fujo zake ndani, mara agombane na mama yake au dada yake kwa sababu ya utundu wake.
Mazingira ya home yalianza kuniboa mpaka nikatamani kwenda Mbweni kwa Ghati, zile siku mbili nilizolala kwake zilinidatisha sana. Baadae nikaona wacha niende Upepo garden kupoteza muda kwanza nilikuwa jirani na mazingira ya huku.
Nilikwenda nikakaa sehemu ambayo mara ya mwisho nilikuwa na Prisca na nilijukuta namkumbuka tena. Niliagiza bia zangu nikawa nakunywa huku napanga mipango yangu taratibu nikipulizwa na upepo wa bahari.
Jumatatu nilienda Kariakoo nikanunua mzigo wa kutosha, kisha nikauepeleka transporter kwaajili ya kuusafirisha kwenda Dodoma. Gari huwa zinasafiri usiku, hivyo kufikia kesho asubuhi mzigo ungekuwa umefika tayari.
Baada ya kumaliza taratibu zote, nilianza kufanya utafiti kuhusu bei za spares za magari, hasa kwa bei za jumla. Kwa bahati nzuri, Kariakoo nina kaka yangu ambaye anauza spares za magari na yuko mtaa wa MAFIA/SIKUKUU. Amekuwa msaada mkubwa kwangu katika sekta hii, na ana duka lake kubwa sana, anauza kwa jumla, jambo ambalo limenisaidia sana.
Niliwasiliana na Dullah ili tuweze kuonana na lengo nimkabidhi funguo za nyumba incase kama mama J atahitaji kurudi home na tulikutana pale breakpoint Makumbusho japo alifika kwa kuchelewa sana;
MIMI: “Naelewa bro! Kama unavyoniona niko busy na mipango yangu hapa.”
DULLAH: “Dadeki kitu Macbook Air hii dukani inakwendaje?”
MIMI: “Mahali uliyolipa kwa Latifah zidisha mara 4.”
DULLAH: “Mseng** wewe unataka kusema ina thamani ya Million 8?”
MIMI: “Ndo maana yake au huamini?.”
DULLAH: “Niambie naona umebadili namba ya simu tayari na ukaondoka bila taarifa, nakutafuta kwa simu sikupati mpaka nikahisi labda dada amekufungia ndani.”
MIMI: “Daah aisee sio poa, halafu unajua ile manzi ina mtoto? Japo anadai baba mtoto alikufa.”
DULLAH: “Mhh! Becareful mzee, umeomba akuoneshe kaburi la baba mtoto?”
MIMI: “Tuachane na haya kaka, mwanamke mwenyewe sina mpango naye ilitokea bahati mbaya wewe ndo uliniforce niende. Unajua nilikuwa Dodoma na nimepata frem tayari?, halafu nimerudi jana kufuata mzigo na kesho mapema naondoka.”
DULLAH: “Hongera sana kaka, itabidi nije Dodoma siku moja maana sijawahi fika kabisa.”
MIMI: “Karibu uje uangalie fursa. Mzee mimi sina story leo, nilichokuitia hapa nilitaka nikupe taarifa ya kuanza biashara na pia nimehama pale home, nimehamia mbezi chini kabisa.”
DULLAH: “Kwanini umehama sehem nzuri kama ile?”
MIMI: “Nimehama kwasababu maalumu, pia naomba nikukabidhi funguo endapo wife akihitaji atawasiliana na wewe.”
DULLAH: “Haina shida bro usiwe na wasiwasi.”
MIMI: “Nashukuru sana, mimi sikai nataka niwahi home nikalale, kesho niwahi kuondoka kwenda Dodoma kupokea mzigo. Baada ya hapo nina safari nyingine tena ya kwenda mkoani kumsalimia mama yangu.”
DULLAH: “Naona unataka ukachukue baraka kwa bimkubwa.”
MIMI: “Muhimu kaka si unajua biashara zina mazingaombwe sana.”
DULLAH: “Naelewa kaka wewe wahi mengine tutaendelea kuwasiliana.”
Baada ya kuachana na Dullah niliondoka straight kuelekea home na baada ya kufika, nilifanya mawasiliano na Aggy anisaidie kumtafuta dada wa kushinda dukani.
Kesho yake nilirudi Dodoma mapema maana nilitumia usafiri wa anga, pia nilikuwa nina safari nyingine ya kwenda mkoani. Baada ya kuwasili nilienda moja kwa moja kufuatilia mzigo wangu na baada ta kuupata nilitafuta usafiri wa kuupeleka dukani.
Baada ya kupeleka mzigo dukani, nilimpigia Aggy simu kumtaarifu kwamba naenda mkoani kumsalimia mama yangu. Aggy alishangaa kwanini haraka sana? Hata sijapata muda wa kupumzika?, nikamwambia ni muhimu sana kwenda, na nikaondoka kwa private.
Niliingia mkoani usiku kwa upande wa pili, mama hakuwa na taarifa za ujio wangu, hivyo nilitaka kumsaprize. Nilipofika home geti lilikuwa tayari limefungwa, ikabidi nigonge, mbwa walikuwa karibu wakaanza kubweka pale, na walikoma mara moja waliponitambua.
Moja ya Mbwa wetu anaitwa Askari, alisogea getini kwa furaha kubwa muda huu. Alianza kutoa kelele za furaha kuniona huku akitikisa mkia wake kwa nguvu na kurukia geti kwa msisimko. Askari ni mbwa ambaye nimemlea tangu akiwa mdogo, na licha ya kwamba naweza kutokuwepo nyumbani kwa muda mrefu, kila ninaporudi, daima ananikumbuka kwa upendo wa kipekee.
Dada alikuja kufungua geti na kunikaribisha ndani na ile kuingia seblen mama alikuwa na wadogo zangu wakiangalia tamthlia na baada ya kuniona aliishia kufurahi na kuja kunikumbatia kwa nguvu.
“Ooh mwanangu nimetoka kukuwazia sio muda mrefu, mbona unakuja bila kutoa taarifa huko umefukuzwa?”
“Sijatokea Dar nilikuwa Dodoma.”
“Kuna nini huko?”
“Kuna biashara nataka kuianza ndiyo imenileta hapa home.”
“Niambie nakusikiliza mwanangu.”
Tulianza maongezi na mama, ambapo nilimshirikisha kuhusu biashara ninayotaka kuanzisha. Mama alifurahi sana na alinipongeza, kisha akasema tutafanya maombezi ya nguvu kabla ya kwenda kulala. Pia, tulizungumza kuhusu mimi kuwa Zambia, na mama alifurahi sana baada ya kupata taarifa kutoka kwa baba.
Baada ya maongezi marefu, nilimkabidhi mama yangu zawadi maalum, simu ya Samsung niliyonunua Dar es Salaam. Mama alifurahi sana kwa zawadi ya simu na bila kuchelewa akaweka line.
Kabla ya kwenda kulala kama familia tulifanya maombi juu ya biashara nayoenda kuianza kwa kufunga Roho za chuma Ulete, tukimwomba Mungu kuondoa maadui watakaojaribu kunikwamisha katika safari yangu ya kibiashara. Tuliiomba pia msaada wa kupata wateja, ili biashara yetu iweze kustawi kwa mafanikio.
Baada ya maombi nilimuaga mama nakwenda kulala na masuala mengine mengi tugaongea kesho panapo majaliwa. Lakini zawadi ya simu ilimgusa sana mama yangu maana alifurahi sana na alizidi kunishukuru.
*****
Jumatano nilirudi Dodoma na niliwasili jioni, nilikuwa nimechoka, lakini nilikuwa na matumaini makubwa ya kuanza biashara siku inayofuata. Kwa bahati nzuri, Aggy alikuwa tayari amempata dada ambaye angeweza kunisaidia dukani. Huyu dada alikuwa ni mfanyakazi wake wa zamani, kabla Aggy hajafunga biashara yake.
Aggy alinihakikishia kuwa huyu dada ni mchapakazi, mwelewa, na mwenye uaminifu, hivyo atanifaa sana katika biashara yangu. Bila kusita, nilimuomba Aggy amfahamishe ili kesho tukutane kwa ajili ya mazungumzo zaidi na kupanga jinsi ya kuanza kazi pamoja.
Mnamo Alhamisi, tarehe 16/03/2023, nilifungua rasmi biashara yangu. Nilianza kwa kuwajulisha watu wa karibu na kuwaomba waniunge mkono. Nilitembelea garage mbalimbali na kuwaeleza kuhusu biashara yangu, huku nikiwapatia punguzo maalum la bei.
Jumapili, nilimtembelea Mzee Mollel nyumbani kwake ili kumsalimia na kumshirikisha kuhusu biashara mpya niliyofungua. Mzee Mollel ni rafiki wa karibu wa baba yangu, na ninamheshimu sana kama mzazi wangu mwenyewe.
Mzee Mollel alifurahi sana kusikia hizi taarifa na hakuishia hapo akaniashauri nifanye na service kabisa za magari. Alikuwa mulemule kwenye mipango yangu.
“Sasa hivi Dodoma imekua sana na magari yameongezeka kwa wingi. Kama utaweza fanya na service za magari, mteja akija kupata huduma unamuuzia na oil, hivyo mzunguko wa hela utaonekana kwa urahisi. Wewe umetoka Dar es Salaam, basi onyesha utofauti na wafanyabiashara wa hapa. Ukifanya hivyo kwa ufanisi, baada ya mwezi mmoja utaanza kuona mafanikio."
“Ahsante mzee hili la kufanya service lipo kwenye mipango yangu na kuna sehemu nilipata acha nikalifanyie kazi.”
“Wewe ukikamilisha nijulishe wateja nitakuletea wengi sana hili ondoa wasiwasi, cha muhimu kama nilivyokwambia awali onesha utofauti na wengine.”
“Ahsante kwa ushauri wako mzee.”
Mzee alinipongeza sana kwa maamuzi niliyoyachukua na alisema atanisapoti kwa kadri ya uwezo wake. Nilishinda pale kwake mpaka usiku nikapata na dinner, kisha nikaaga na kuondoka kurudi kwa Aggy.
Niliona umuhimu mkubwa wa kulisimamia suala la biashara kwa bidii na umakini wa hali ya juu, kwani kufeli kwangu kutanirudisha katika ajira, jambo ambalo sitaki kabisa. Kwa upande wangu, kuajiriwa ni sawa na kujifunga katika utumwa wa hofu na mashaka ya maisha. Ni kweli, mshahara unaweza kuwa mkubwa, lakini utatosha vipi kulipa uhuru wangu?.
Niliporudi nyumbani, niliwasiliana na dalali na kupanga tukutane kesho na yule kijana ambaye aliniambia angeweza kunifaa kwenye masuala ya service. Pia, tulikubaliana tuwahi kuonana ili tuende kwenye eneo husika, na ikiwezekana, tufanye malipo kabisa
Kesho yake tulikutana na dalali akiwa ameongozana na dogo, nilimfanyia usaili kidogo na niliona yuko vizuri ana uwezo, pia alionesha nia ya kufanya kazi pamoja nami. Baada ya kumalizana na dogo, tulienda kukutana na mhusika mkuu ili kupata muongozo wa namna ya kufanya malipo.
Tulikutana na dada ambaye alionekana kuwa msimamizi wa eneo hilo, na mara ya kwanza, tulikutana na kaka, lakini leo hali ilikuwa tofauti. Dada huyu alikuwa na mvuto wa kipekee maana alikuwa kafungasha vizuri, alitupa muongozo na nikafanya malipo ya miezi sita kwa kiasi cha shilingi 2,100,000.
Baada ya hapo nilikaa chini na dogo ili tupange mipango kuhusu vifaa vya kazi atakavyohitaji maana kama eneo alikuwa keshaliona tayari. Dogo alisema ninunue compressor, mashine kwaajili ya wheel balancing, Automatic tyre changer, stand jack, bila kusahau sare/uniform na buti akiwa kazini na vifaa vingine vingi.
Dogo aliahidi kuwapa taarifa wateja wake wote wa zamani ili waje kwenye ofisi mpya, nami nilimuahidi kumpa bonasi kwa kila mteja mpya atakayeleta. Kuhusu mshahara, tulikubaliana kuwa nitaanza kumlipa 250,000 kwa mwezi, ambapo chakula na nauli zitakuwa juu yangu. Pia, nilimwambia kwamba mambo yakianza kwenda vizuri, atapata bonus kwa kila gari atakaloifanyia service.
Tuliagana kwa makubaliano ya kukutana pindi nitakapokuwa nimekamilisha kununua vifaa vya kazi, na nilimwambia kuwa ndani ya siku mbili vitakuwa tayari, hivyo ajiandae muda wowote nitampigia simu.
Nilipanga hesabu zangu kwa umakini na kugundua kuwa kuna umuhimu wa kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya kununua vitendea kazi. Hata hivyo, biashara kule dukani ilikuwa bado ngumu, hasa kwa kuwa duka lilikuwa jipya. Aidha, nilikuwa nikimfundisha dada kuhusu aina za lubricants ili aweze kutoa huduma bora kwa wateja.
Baada ya siku mbili kupita nilirudi tena Dar es Salaam kwaajili ya kununua vifaa na nilienda Posta mtaa wa India. Kuna fundi wangu ndo aliniongoza kwa moja ya supplier ambaye anamjua na amenyooka.
Baada ya kufika dukani niliwaelekeza vifaa navyotaka pamoja na kupewa discount, baada ya kufanya malipo walisema watanitumia na nitapigiwa simu namna ya kupata mzigo wangu.
Nilimaliza mapema sana kisha nikarudi home kupumzika na nilipanga jioni nionane na Hilda kwaajili ya maongezi. Tangu niondoke Dar wiki mbili zilikuwa zimekata tayari, halafu hatukuwa na mawasiliano yoyote
Jioni ilipowadia Hilda alinipigia simu na kuuliza tunakutania wapi? Nami nilimjibu asogee mpaka Mikocheni ‘Triple 7’. Nilianza kujiandaa pale kwa haraka na baada ya nusu saa nilitoka home kuelekea eneo la tukio.
Baada ya kuonana tulianza mazungumzo pale na aliishia kulalamika kwanini sipatikani kwenye simu? Maana amekuwa akinipigia bila mafanikio;
MIMI: “Nilisahau kukupa namba mpya, halafu nilikuwa busy sana kule Dodoma hata hapa unaniona sababu kuna vifaa nimefuata.”
HILDA: “Insider usifanye hivo, uliniahidi utakuwa available pindi nakuhitaji, hata Lucy anakutafuta sana bila mafanikio unatuacha kwenye mataa wenzako.”
MIMI: “Pole mummy ndomana leo nimekutafuta ili tuongee, pia nimekumiss sana ujue.”
HILDA: “Don’t say that, mimi naona ofisi ni chungu, nilishazoea kukuona, kunitania muda wote nakuwa na furaha ofisini, umeniacha mpweke.”
MIMI: “Nollie si yupo?”
HILDA: “Sawa yupo, lakini hatuwezi kuwa na ukaribu kama wako.”
MIMI: “Embu niambie ni nini kiliendelea tangu tuachane kipindi kile ni week 2 tayari.”
HILDA: “Thanks God mzigo tulipata week iliyopita na tumelipa deni tayari, mama alirudi aka clear deni.”
MIMI: “Good news na anasemaje yeye?”
HILDA: “Nothing! Ila alikuulizia nikamwambia bado upo likizo.”
MIMI: “Kuna taarifa yoyote kutoka kwa Iryn?”
HILDA: “Hapana sijasikia ni muda mrefu sana na kila mtu anamuulizia pale ofisini.”
MIMI: “Ahsante kwa mrejesho mzuri bila shaka kwasasa huna stress kila kitu kipo kwenye track huna haja ya kuwa na wasiwasi tena.”
HILDA: “Ripoti zangu si unazipata lakini?”
MIMI: “Niwe mkweli sijawahi hata kuangalia ila tukiachana hapa nikirudi home nitaziangalia.”
HILDA: “Halafu umenikumbusha, Lucy alikuja kwako akaambiwa umehama, hapa ndo amechanganyikiwa anakuwa na wasiwasi sana juu yako.”
MIMI: “Nimehamia jirani hata sio mbali na nilikokuwa naishi zamani.”
HILDA: “Asmah pia anakuulizia sana, anahisi mimi na wewe tuna mawasiano ya siri ila namficha.”
MIMI: “Asmah hana taarifa wala sikumuaga pamoja na Lucy, hivyo hawajui niliko. Kama tulivyokubalina before usimpe mtu namba yangu bila kupata idhini yangu.”
HILDA: “Sawa hili ondoa wasiwasi Insider.”
Tuliendelea na maongezi mengine, lakini nilipata wazo la kwenda kumsalimia Asmah pale kwake kabla sijaondoka kurudi Dodoma kuendelea na mishe zangu.
Nilimdrop Hilda Morocco nami nikaendelea na safari ya kwenda Upanga na nilitumia barabara ya Kawawa ili nikaunge na barabara inayokwenda Makaburini, sikumwambia Hilda kama nakwenda kwa Asmah.
Baada ya kuwasili kwa Asmah nilipark gari usawa wa apartment yake, lakini kwa leo kulikuwa na utofauti maana kuna Crown nyeusi ilikuwa imepark pale.
Baada ya kushuka kutoka kwenye gari, nilipanda hadi ghorofa ya kwanza na kugonga mlango. Sikumpigia simu kwa sababu nilitaka iwe saprize, nilijua kuwa kwa nyakati za usiku, mara nyingi huwa nyumbani. Huu ulikuwa utaratibu wangu wa kawaida, kwenda bila kutoa taarifa.
Asmah alifungua mlango na ile kuniona alishtuka sana na alitoka nje akarudishia mlango;
ASMAH: “Insider what are you doing here?”
MIMI: “What? Mimi ndo wakuniuliza hivo? Hata salamu hakuna.”
ASMAH: “Kwanini unakuja bila taarifa?”
MIMI: “Mara ngapi nakuja hapa kwako bila taarifa?”
ASMAH: “Please naomba uende nitakucheki badae niko na kaka yangu akiona hivi atachukia.”
MIMI: “Ahh! Hayo unaleta wewe mimi nimekuja ili nikusalimie sasa wasiwasi wako ni nini?.”
Niliamua kuondoka sikutaka kuendelea kupoteza muda, lakini nili smell something fishy kinaendelea. Niliwasha gari yangu ili niondoke, lakini Crown iliyokuwa imepaki pembeni ilinipa mashaka, nikahisi Asmah atakuwa amepata mhuni.
Nilivyofika getini ilibidi nimpige maswali mlinzi kuhusu ile Crown na alisema hii mara ya pili anaiona ikiingia na kutoka. Niliondoka kurudi home ili nikajiandae na safari yangu ya kurudi Dodoma nikaendelee na harakati zangu.
Baada ya kurudi home kutokana na mazingira kuwa ya kimya na upweke nilifikiri nikaona kuna umuhimu wa wife kurudi home. Niliwaza pale nimpigie simu tuongee arudi home, lakini niliona ni heri arudi mwenyewe ili kutunza heshima yangu.
Niliingia Shabiby Online na kukata tiketi yangu ya bus mapema. Pia nilianza kufikiri namna ya kutoka pale kwa Aggy na nikaona pindi nitakapo rudi Dodoma, nianze kutafuta gheto. Nilijiuliza sana, Aggy ni binti na kuna uwezekano kwamba kuna mwanaume anayemlipia kodi, kuendelea kukaa pale kwake ni sawa na kumuumiza. Hata kama tumekuwa marafiki wa muda mrefu, lakini kwa hatua tuliyofikia sasa, kuna baadhi ya mambo yanahitaji kupeana nafasi.
Mkuu umeongea point nzito sana. Mikasa ipo Mikali sana tunaogopa codes.. Matukio ya INSIDER ni ya kawaida kwa Wanaume flani flani hivi...ndio maana tunakufa mapema. Juzi tu tumeamua case moja matata...mtu unawatoto tisa na wanawake wakali mbaya😀😀😀😀😀😀 Shetani atusamehe... Shetani tena
SEASON 02
EPISODE 29

AGGY: “What? Yaani ukapange na kwangu sehemu ya kulala ipo?. No! siwezi kuruhusu hili litokee.”
MIMI: “Nafikiri unasahau kuwa mimi ni mwanaume na wewe ni mwanamke.”
AGGY: “Unamaanisha unakosa uhuru wa kufanya mambo yako? Au nimekuelewa vibaya?”
MIMI: “Unaweza kuwa sahihi, mimi naanza harakati zangu kurudi usiku kwako sio busara, pia wewe ni mtoto wa kike nataka kukupa uhuru wa kufanya mambo yako, hata mimi nahitaji uhuru wa kufanya mambo yangu. Kuendelea kukaa kwako kwa muda mrefu sio sawa kabisa, au wewe unaonaje ni sawa?”
AGGY: “Mimi naelewa unataka uhuru wa namna gani na sikushangai maana hata mdogo wangu anaonaga bora alale hotelini kuliko kulala kwangu.”
AGGY: “Hahahaa! Ila Insider mpaka leo siaminigi uliwezaje kukaa na mwanamke ndani inawezakana wifi yangu anavumilia mengi tu. Naomba nikuulize, hivi bado mnawasiliana na Angel?”
MIMI: “Hahahaa! Sijui umewaza nini mpaka umekumbuka Angel, huyo b*tch mimi nilishamsahau kitambo sana. Tulikutana 2022 mwishoni pale Karambezi, alinipa namba zake, lakini nilifuta.”
AGGY: “Anapost sana Instagram, nilim-DM tukachati kidogo akasema nikupe hi, nikamwambia Insider ana mke sahivi utamuharibia. Mpaka leo hukuwahi kunambia sababu ya kuachana kwenu, naona uliamua iwe siri yako.”
MIMI: “Sikia, Angel alinipiga tukio ndiyo sababu ya kuachana, ndomana sikukwambia kipindi kile, tuachane na huyu malaya hana umuhimu kwangu.”
Baada ya kupata dinner tuliondoka kurudi home kulala nami nilifanya kuwasiliana na Dalali aanze kunichekia chumba ili nihamie haraka iwezekanavyo.
Kwa upande mwingine Pesa ilikuwa imekata tayari, nilikuwa nimefulia sina pesa na balance iliyokuwa imebakia ni 340,000 tu. Nilipiga hesabu napata wapi Pesa?, sikutaka kumshirikisha Aggy juu ya hili maana alikuwa analalamika sana kuwa anakatwa makato makubwa kwenye kulipia mkopo wake, alikopa kwaajili ya kufanyia ujenzi kwao.
Nilipiga hesabu nipate million 2 kama akiba ili niweze kupanga geto na kununua baadhi ya mahitaji na nyingine inisaidie kuendesha ofisi. Baada ya kuwaza sana nikakumbuka wapangaji wangu wanamaliza mwezi wa 4 mikataba yao, hivyo niliona nimtafute Maggy nimuombe anilipe kabisa.
Nilimpigia simu Maggy kuomba kuonana naye na alisema tuonane jumamosi asubuhi maana kwa kesho ana safari ya kwenda Arusha kwenye kikao na atarudi jioni.
Siku ya jumamosi iliwadia na Maggy alinipigia simu kunipa taarifa yuko home, hivyo naweza kwenda. Saa 4 asubuhi niliwasili pale kwake na baada ya kuonana nilimueleza shida yangu inayonikabili kwa kipindi hiki. Maggy bila hiyana alisema nimpe account yangu ili afanye kutransfer hiko kiasi na niliishia kumshukuru, kisha nikaenda kuonana na Dalali.
Dalali alinionesha vyumba vyote alivyokuwa amepata na niliipenda masta ambayo ilikuwa meneo ya Uzunguni. Mazingira yalikuwa mazuri sana na kwenye compound zilikuwepo nyumba 5, Master ilikuwa moja tu ambayo ni yangu zilizobaki zilikuwa ni chumba sebule na moja ina vyumba 2.
Master ilikuwa ni nzuri na niliona itanifaa sana kwa kipindi chote nitakacho kuwepo huku. Baada ya kufanya malipo nilienda kununua Godoro na mashuka ya kujifunika kwaajili ya baridi, bila kusahau mito.
Sikutaka mbwembwe za kununua kitanda nilijisemea godoro tu linatosha cha muhimu na sehemu ya kulala, sijaja Dodoma kula bata. Kuhusu kula nilipanga nitakuwa nakula kwa mama ntilie, hivyo hakuna haja ya kununua jiko.
Jumatatu ndo nilihamia geto rasmi na ndio siku ambayo tulianza kazi rasmi na dogo kwenye upande wa service, gari ya kwanza kuanza nayo kazi ilikuwa ya Aggy ‘BMW X1’.
Pale geto nilikuwa nina ishi maisha yangu sikuwa na habari na mtu zaidi ya jamaa yangu Michael ambaye tulitokea kuelewana kwa haraka sana. Michael alikuwa kapanga chumba na sebule ndo mtu pekee aliyenikaribisha mazingira ya pale, kutokana na ucheshi wake tulitokea kuelewana sana.
Pale ofisini yule dada ambaye alinipokea na kuandikishiana mikataba tulitokea kuzoeana kwa haraka sana, na alikuwa kama mtani wangu maana nilikuwa namuita ‘Sanchi’ sababu kabarikiwa makalio.
Sanchi alikuwa zaidi ya rafiki wa kazini, ilikuwa haipiti siku bila kutaniana labda asije kazini. Kila mchana, nilijikuta nikienda ofisini kwake kupumzika, ambapo yeye alikuwa meneja wa kile kituo cha mafuta.
Siku moja, nilimuomba aniruhusu kuzungusha kamera ili iweze kuangalia upande wangu, kwani ilikuwa imeelekezwa sehemu isiyokuwa na umuhimu. Aliniambia, "Tutaifanya hiyo kazi Jumatatu, mpaka fundi aje na kuiset kwenye mfumo."
Jumatatu ikafika, na Sanchi hakutokea kazini.
Jumanne ilipowadia, Sanchi alichelewa kufika ofisini. Lakini alipowasili, alikuja moja kwa moja kuniangalia kama nipo. Akanikuta nikiwa namwaga oil ya gari la mteja, na aliniita kwa sauti laini, na akaanza matani yake;
SANCHI: “Bossy hata wewe unafanya hizi kazi? Kuna haja gani ya kumuajiri fundi?”
MIMI: “Sema umebarikiwa sana, hilo Bunango ukienda Bank wanakupa mkopo bila riba.”
SANCHI: “Umefanya nisahau hata nilichotaka kukwambia nitarudi badae.”
MIMI: “Usiondoke bhana si unajua wewe ni mtani wangu? Haya nambie ulitaka kusema nini?”
SANCHI: “Hio camera kama unaweza izungushe imulike upande wako, halafu mimi nitaangalia kama imekaa sawa haina haja ya fundi kuja.”
MIMI: “Hayo ndo maneno, hapo sasa naweza kuwa na jeuri ya kukutoa out ukale dinner.”
SANCHI: “Wewe huyo na ulivyo bahiri hata hauendani na muonekaneno wako, hujawahi hata kunipa offa ya lunch utaweza kunitoa out?”
MIMI: “Kukutoa out sio shida, tatizo nahofia uhai na usalama wangu mali unayomiliki hio ni balaa.”
SANCHI: “Yaani wewe nishakuzoea una matani sana.”
MIMI: “Sasa bossy wangu soon nakucheki.”
Habari mbaya Sanchi mwaka huu alitangulia mbele ya haki, ni moja ya watu ambao walinisaidia sana kupata wateja tena wale madon. May her soul rest in peace! AMEN.
Mwezi wa tatu ulipita, na licha ya biashara kusuasua kwa pande zote, kulikuwa na dalili za matumaini. Huku nikiwa na matumaini mapya, niliendelea kupambana kwa bidii, nikitumia mbinu mbalimbali ili kuvutia wateja.
*****
Kuanzia mwezi wa nne, biashara ilianza kuimarika, na matumaini yakaanza kuchanua. Hakukuwa na siku iliyopita bila kuuza pale dukani au kufanya service ya gari, kwa siku za weekend kazi zilionekana. Kujaza upepo kwenye tairi za gari kulifanya tusikose pesa ya lunch, maana nilijitahidi kuwa na vipimo imara ili kuleta ulinganifu wa tairi zote.
Watu walikuwa wameanza kuzoea mazingira na niliwashirikisha watu wangu wote wa karibu wa pale Dodoma wanisaidie kwa hili. Biashara ni connection ya watu na sikuzote watu wa karibu ni moja ya key agents wa kukufanikisha.
Dogo alikuwa akipiga sana kazi kwa upande wake pamoja na kujituma kwa bidii sana. Kutokana na mazingira yetu kuwa mazuri na ya kuvutia tulianza kupigiwa simu na kupata wateja kutoka sehemu mbalimbali.
Nilipata wazo nifungue kampuni ili niweze kuomba tenda mbalimbali hasa kwenya makampuni na serikali. Niliamua kuelekeza akili yangu kwenye biashara na ili niweze kupata hizi tenda, bila kampuni kutoboa ni ngumu.
Nilianza process za kufungua kampuni Brela, tatizo lilikuwa nani nimuweke awe Director? Maana kampuni sheria ni lazima kuanzia directors wawili. Nilikuwa napata ukakasi kumuweka mama J sababu sikuwa na imani naye kama tutaendelea kuwa pamoja, licha ya yote, nilikuwa nishamsajili kwenye mali nyingi sana kama nyumba na magari.
Baada ya kujifikiria sana niliona ni bora nimuweke mama yangu mzazi, mabadiliko mengine nitafanya hata hapo baadae. Nilianza process online na nilifanya mwenyewe kasoro kwenye kuandaa memorandum ndo nilihitaji msaada kutoka kwa Wakili.
Mnamo tarehe 6 April, kampuni yangu ndo ilisajiliwa rasmi, baada ya hapo nikaanza process za kusajili TIN ya biashara TRA, bila kusahau kununua mashine ya EFD maana walikuwa washaanza kunisumbua pale dukani.
Baada ya kumalizana na TRA ilibidi nianze process za kufuatilia leseni ya biashara manispaa, kisha nikaja na watu wa OSHA, Mara taka, fire nknk. Mambo ni kibao sio poa.
Baada ya kumalizana na mamlaka za serikali nilianza kufikiri namna ya kuandaa mkakati bora wa kupata tenda mbalimbali ili niwe na uhakika wa kazi. Akili yangu niliielekeza kwenye biashara sikutaka masikhara kabisa, nilikaa mbali na wanawake pamoja na starehe.
Ndugu yenu nilianza kufubaa na kupauka, mnajua hali ya hewa ya Dodoma, sivyo? Kwangu mimi, hali hiyo hainifai kabisa. Jua lile ni kama Jehanam ndogo, na maji ya chumvi ni balaa. Kuishi Dodoma ni kama kuteseka.
Yale maisha ya Dar es Salaam ya kwenda migahawa ya gharama na hadhi nilisahau kabisa. Sehemu yangu ya kula ilikuwa ni kwa mama ntilie “Mama Gire” huyu mama kanilisha sana. Asubuhi nilikuwa napata soup safi, mchana napata wali wangu wa nguvu, usiku ndo nilikuwa mara nyingi nakula karibu na mazingira ya geto.
Jumamosi ya wiki hii ya kwanza ya mwezi Aprili, niliamua kuwasiliana na dada yangu ili nijue kama kuna taarifa yoyote mpya kutoka kwa mama J. Tangu nilipofika Dodoma, sikuwa nimezungumza na dada yangu, kwa hiyo nikaona ni muhimu kuwasiliana naye.
Baada ya kumpigia simu alipokea na tukaanza mazungumzo na habari kubwa alisema mama J ananitafuta sana;
SISTER: “Wifi kachanganyikiwa huko karudi home kakuta haupo, amenipigia simu anaanza kulalamika umehama bila kumpa taarifa, na hupatikani kwenye simu. Anahisi umeenda kupanga sehemu nyingine na mwanamke mwingine. Mimi nikamuuliza kwani ulikuwa haupo nyumbani? Na kwanini ahame bila kukupa taarifa, nini kinaendelea?.”
MIMI: “Ehe! akasema nini?”
SISTER: “Huwezi amini hajasema chochote, zaidi kasema aliondoka mkiwa hampo kwenye maelewano mazuri. Ndipo nikamwambia suala la kuhama ulinishirikisha, lakini mimi sijui kinachoendelea kati yenu maana hata wewe hajanambia.“
MIMI: “Nilimpigia simu hakupokea sasa analalamika nini?”
SISTER: “Mtafute wifi yangu, anaonekana anataka kurudi home, tumeongea haya since jumatatu, lakini kwenye simu nikawa sikupati.”
MIMI: “Nilikuwa busy sana hapa katikati maana siko mjini kama tulivyoongea, lakini sahivi kidogo mambo yanaenda.”
SISTER: “Fanya hivo yule ni mke wako hata kama hamjafunga Ndoa, siku ambayo atachoka kuvumilia utampoteza na utajutia sana.”
MIMI: “Leo namaliza dada yangu acha kuninanga.”
Baada ya kuongea na sister niliamua kumpigia simu wife ili tuongee, ikiwezekana niyamalize kabisa. Simu iliita kwa mara ya kwanza ikakata bila kupokelewa, nikapiga tena kwa mara ya pili ndo kupokea.
MAMA J: “Nani?”
MIMI: “Ahh mke wangu ni mimi baba watoto huna haja ya kuwa na wasiwasi. Nimekumiss sana ujue, nimekupigia kukujulia hali pamoja na mtoto.”
MAMA J: “Umenimiss wapi au sababu wifi amekupa taarifa nakutafuta?”
MIMI: “Hapana sijaongea naye muda mrefu sana maana sahivi napatikana kwa hii namba mpya.”
MAMA J: “Mimi nilifikiri umeamua kuhama na kubadilisha namba ili usipatikane, tusikusumbue.”
MIMI: “Nipo Dodoma kuna project nimekuja ifanya, ikikaa sawa nitarudi huko Dar. Vipi unataka kurudi home nikuelekeze kwenye makazi yetu mapya?”
MAMA J: “Sitamani kurudi kuendelea kuishi na wewe na kama unataka mimi nirudi njoo nichukue home.”
MIMI: “Nakutumia pesa ya Uber urudi home sawa?”
MAMA J: “Aliyekwambia mimi sina nauli ni nani?”
MIMI: “Kukuhudumia ni jukumu langu hata kama una hela.”
MAMA J: “Haya kwaheri.”
Ilipita dakika 10 hivi akanitumia text message…
“Umehamia sehemu gani?”
“Mbezi chini karibu na kota za BOT.”
“Sizijui.”
“Bhasi karibu na Sea breeze hall. Ukiwa tayari nambie nikupe namba ya Dullah akupe funguo za pale home.”
“Okay! Send me his contact.”
Nilimtumia namba ya Dullah na tukaagana pale, kwa upande wangu nikajisema case closed.
Baada ya hapo niliwasiliana na Jane ili kumjulia hali maana toka niondoke Dar hatukuwa na mawasiliano kabisa, pia nilikuwa sipatikani kwa simu. Simu iliita kwa muda mfupi na akapokea pale;
MIMI: “Hello shem! Ni mimi Insider.”
JANE: “Oh! I can’t believe, nimekuwazia sana leo nikipiga simu yako hupatikani.”
MIMI: “Pole sana, nilikuwa busy sana huku ndomana ukaona kimya, halafu hii ndo namba yangu inayopatikana kwasasa.”
JANE: “Hukunipa hii namba ndomana.”
MIMI: “Sorry! Unaendeleaje lakini pamoja na mtoto?”
JANE: “Niliumwa sana hapa katikati mpaka nikalazwa, lakini namshukuru Mungu nilipona salama.”
Taarifa za Jane zilinishtua sana na nilianza kujiona na hatia maana sikuwahi mtafuta wala kumpa namba yangu mpya;
MIMI: “Shem pole sana na pia naomba nisamehe kwahili.”
JANE: “Usijali, jambo jingine, kwanini uliondoka pasipo kumuaga Mary? Unakosea sana shem, Mary ni moja ya familia yetu usimtenge, uwe unamshirikisha mambo yako.”
MIMI: “Ni kweli shem! Nilisahau tu kwa bahati mbaya nitamcheki kumuomba msamaha juu ya hili.”
JANE: “Sawa! Fanya hivo.”
Baada ya kumalizana na Jane niliendelea kuwaza pale kitandani kwa dakika kadhaa, kisha nikalala zangu ili kesho niwahi kwenda church.
*****
Mwezi ulikuwa umewadia tayari tangu nizamie Dodoma. Kuhusu upande wa biashara mambo yalianza kuwa mazuri wanasema ‘When one door closes another opens’.
Pesa nilizokuwa napata kwenye biashara nilikiwa nazideposit bank kwenye akaunti ya kampuni. Nilikuwa makini sana hasa kwenye kufanya cost minimization stategies ili niweze kupata Profit kubwa.
Katikati ya mwezi wa nne siku ya jumapili mama J alirudi home na alinipa taarifa kabla ya kurudi home. Taarifa nyingine aliyonipa ni kuhusu mama wawili, alisema alimpigia simu kuniulizia, na akamwambia mimi nimesafiri ndomana sipatikani.
Nilikumbuka ahadi ambayo nilimpa Pili kuhusu kwenda kwenye mahafali yake ya kidato cha sita maana ndo mwezi wa 4 ulikuwa katikati na mahafali nyingi huwa zinafanyika mwezi huu. Niliwaza sana kuhusu hili jambo nikaona haina haja ya kwenda wacha niendelee na harakati zangu, niliona natakiwa kukaa mbali na mama wawili, nimuache na maisha yake.
Zilipita siku mbili, na asubuhi hiyo nikiwa kazini, Mary alinipigia simu. Nilipogundua ni yeye, nikaamua kuipokea. Kama ilivyo kawaida yake, alianza kunilaumu kwamba nimeondoka bila kumpa taarifa.
MIMI: “Mary I’m so sorry niliondoka kwa haraka, na baada ya kufika huku mambo yakawa yamenibana sana.”
MARY: “Nikija haya yote tutaongea, byee and takecare.”
Baada ya kuagana na Mary, nilibaki nikiyatafakari maneno yake. Nilihisi hatia kubwa kwa kumkosea, na nikaamua kuwa si sahihi kuendelea kumfanyia hivyo. Pia, mawazo yangu yalizidi kuzunguka huku nikijiuliza, 'Mary anakuja kufanya nini Dodoma?'"
Hilda tulikuwa tunawasiliana sana na habari kubwa alinambia kwamba Asmah ananiuizia sana mpaka anapata wasiwasi juu ya mahusiano yetu. Hilda hakuishia hapo, alisema Asmah kama anachanganyikiwa juu yangu, hivyo akanishauri nimtafute maana anamsumbua sana.
Mimi nilijua Asmah ananitafuta sababu ya lile jambo la sikuile usiku pale kwake wala sio kitu kingine. Suala la kumtafuta kwasasa halikuwa kipaumbele changu, hivyo nilijisemea nikirudi Dar nitamtafuta, lakini sio sasa.
****
Jumamosi asubuhi, Mary alinipigia simu kunijulisha kuwa yuko njiani kuelekea airport, na alisema kwamba kufikia saa 7 mchana atakuwa amefika Dodoma. Nilimkaribisha kwa furaha na kumwambia aniambie akifika mjini ili niweze kumfuata.
Jumamosi ilikuwa siku yenye shughuli nyingi sana kwangu, kiasi kwamba nilisahau kabisa kuhusu miadi yangu na Mary. Aliniambia angetua Dodoma saa 7 mchana, lakini nilipokumbuka ilikuwa tayari saa 9 kasoro. Simu yangu ilikuwa ofisini kwa Sanchi, na nikajiwazia, 'Hakika Mary atakuwa amepiga simu mpaka akachoka.'"
Baada ya kuchukua simu, kweli nikakutana na missed call nyingi kutoka kwake. Ikabidi nimpigie haraka ili kujua alipo. Alipopokea, aliniambia kuwa kuna mtu tayari amekuja kumwona mara tu baada ya kuona sipokei simu zake.
Mary alisema kuwa kufikia saa 12 jioni atakuwa amemaliza mazungumzo na huyo mtu, na atanipigia ili tuonane. Nilijiuliza, Mary ana shughuli gani huku, na ameja kuonana na nani? Maana ni mgeni na hajawahi kufika Dodoma.
Niliendelea na ratiba zangu, na kwa mara nyingine nikaacha simu ofisini kwa Sanchi. Nilikuwa naiweka huko kwa sababu sikuwa naitumia, na hakuna mtu wa kunitafuta kwani namba yangu ni mpya. Muda wa mapumziko, kama wakati wa kula lunch, ndiyo nilikuwa nikiichukua.
Kuhusu wateja, nilikuwa nawasiliana nao kupitia simu ndogo na nilisajili laini maalum kwa ajili ya hili. Sikutaka kuchanganya mambo ya kazi na mambo yangu binafsi, ndiyo maana nikasajili laini maalum kwa matumizi ya ofisi.
Saa 10 jioni, nilitoka kwenda dukani kwa ajili ya kupiga mahesabu na kuangalia namba za lubricants ambazo zimeisha, ili nifanye kuagiza mzigo mwingine kutoka Dar es Salaam. Supplier alikuwa akisubiri odda yangu ili aanze kuandaa mzigo na autume mapema.
Ilikuwa saa 12 kasoro tayari, nikasema ni bora nirudi haraka kwani Mary maana alisema atanicheki muda huu. Baada ya kurudi ofisini, Sanchi alitoka nje na akaanza kuniita. Aliniambia simu yangu ilikuwa inaita sana, kuangalia ni Mary alikuwa amepiga mara 5, nikampigia haraka.
MIMI: “Hello mummy ushamaliza?”
MARY: “Yeah muda mrefu hupokei simu.”
MIMI: “Ulisema saa 12 utanicheki.”
MARY: “Nilisema kufikia saa 12 nitakuwa tayari, hivyo muda wowote ningekujulisha.”
MIMI: “Ok! tulishindwa kuelewana haya nambie ulipo.”
MARY: “Tukutane Golden fork huyu mtu ananiacha hapo, nataka nile kabisa nahisi njaa.”
MIMI: “Sawa mummy nitakukuta hapo.”
Baada ya kukata simu nilijisemea ‘Mary anakwenda Golden Fork anataka kunitia gharama tu.’ Kwa upande wa pili Sanchi alikuwa akiniangalia sana, uvumilivu ulimshinda akaanza kuongea pale;
SANCHI: “Wacha wee! Naona una appointment na mrembo, amekupigia sana simu.”
MIMI: “Appointment gani na hali hii niliyonayo unaona ina make sense?”
SANCHI: “Kwani si unakwenda kuoga na kujiandaa kwanza, uzuri hapa bafu zipo kazi kwako.”
Niliamua kupotezesha mada;
MIMI: “Vipi leo si unakuja kulala kwangu.?”
SANCHI: “Hahahaa! Usinichekeshe mie kulala tu.?”
MIMI: “Kwani umesikia neno lingine zaidi ya kulala?”
SANCHI: “Jumatatu tutaongea kuhusu simu nataka ninue iphone kama yako, utanipa connection.”
MIMI: “Imeisha hio hata bure utapata usiwe na wasiwasi.”
SANCHI: “Toka zako wahi ulikopigiwa simu.”
Nilikuwa nimechafuka sana oil zimegandia kwenye jeans, na mikononi. Kurudi geto niliona mbali, hivyo niliishia kunawa vizuri na kujipukuta ili niwahi kuonana naye maana alikuwa keshapiga simu kwamba amefika ananisubiri mimi tu.
Nilichukua bodaboda mpaka Golden fork na nilianza kuingia huku nikizungusha macho yangu vizuri na nilimuona amekaa pembeni akinitizama na ile kusogea aliinuka akaja akanikumbatia.
“Wow Insider I have missed you.”
Watu waliokuwa maeneo yale walikuwa wakituangalia sana maana Mary alikuwa kapendeza ukizingatia ni mzuri. Kama mnavojua Dodoma hakuna warembo wakali kabisa, kwa mrembo kama Mary akija maeneo haya anakuwa kivutio kwa wenyeji.
Tulianza story pale na bila kuchelewa mhudumu alikuja kutusikiliza Mary aliagiza chips na kuku, mimi nikaagiza juice. Mary alinikata jicho kali sana;
MARY: “You can’t be serious muda huu umekula wapi?”
MIMI: “Usijali mimi nitaenda kula home juice inanitosha.”
MARY: “No! Agiza chakula.”
Muda huu dada alikuwa akitabasamu tu;
MIMI: “Dada niletee wali mweupe na makange ya kuku local.”
“Sawa bossy.” dada akaondoka,
MARY: “Insider umepungua sana, halafu umepauka shida ni nini?”
MIMI: “Ni maisha mama halafu mimi ni mtoto wa kiume. Embu niambie huku unamishe gani, halafu ulikuwa na nani?”
MARY: “Huku nina ishu za research ndiyo zimenileta, mtu niliye onana naye atanisaidia kwenye hili.”
MIMI: “Ulikuwa na plan za kuja huku au baada ya kusikia niko huku ndo ukaamua uje?”
MARY: “Actually nilikuwa nina mipango toka muda mrefu.”
MIMI: “Sawa, na itachukua muda gani?”
MARY: “Itategemea makadirio ni week mbili mpaka tatu.”
MIMI: “What? Sikuelewi huwezi kuja kulala kwangu, kwanza naishi geto moja, halafu sio mazingira mazuri ya kulala mwanamke, acha nikitafutie hotel au lodge nzuri uwe unalala.”
MARY: “Hizo gharama ni kubwa sana…”
Nikamkatisha;
MIMI: “Kuna ndugu yangu yupo huku ni mwanamke kama wewe hana shida utalala kwake.”
MARY: “Insider nisikilize kwa makini, mimi sitaki kwenda sehemu nyingine zaidi yako. Kama hutaki nije kwako nambie sitaki ijulikane moja, lakini sio kunipeleka sehem ambazo sizijui.”
Nilikuwa mpole ghafla hata sikuwa na usemi tena, ilinibidi nikubaliane na matokeo. Niliwaza kule gheto naishi kisera sana kuna godoro la 4x6 halafu liko chini. Nilijisemea pale, ‘mtoto kautaka acha niende nae tukifika huko itajulikana’.
Kwa mazingira ya Insider na nature ya kazi yake ya Uber nadhani sio sahihi kumwita malaya, amekwepa vishawishi vingi sana; mnamkumbuka yule Dada aliye achana nae Sinza akiwa hana nauli? Alimpotezea though mwanamke mwenyewe was ready na nguo alianza kuvua kwenye gari but "muhuni" akakomaa na...
SEASON 02
EPISODE 29
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
PREVIOUS:
Saa 12 jioni nilianza safari ya kwenda Dodoma na nilichukua bodaboda wa kunipeleka Magufuli stand. Muda wa jioni mabus huwa yanasumbua hivyo, nilisogea pale darajani kwa Yusuph nikapata private inayokwenda Dodoma.
CONTINUE:
Safari ya kwenda Dodoma ilianza pale na gari ilikuwa ni Harrier. Tulikuwa jumla ya watu sita, pamoja na dereva. Tulikaa wanne nyuma ya seat, tukiwa tumebanana kimtindo—wanaume wawili na wanawake wawili.
Nilipokuwa barabarani, nilikuwa kimya sana, hata sikushirikiana na wenzangu katika mazungumzo. Nilikuwa nikiwaza mipango yangu ya biashara Dodoma na kupanga kumpigia simu dalali kumkumbusha kuhusu jambo letu.
Lengo langu la kwenda Dodoma ni kufungua biashara ya kuuza lubricants za magari na kufanya services. Nia yangu hapo baadae nipanue biashara hii kwa kuuza bidhaa kama vipuri vya magari, urembo, rims, na matairi.
Niliweka lengo kwamba ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo, nitakuwa tayari nimeanza biashara yangu. Nilidhamiria kwa dhati kuanzisha biashara. Pia, nilipanga kuwa na nidhamu ya fedha kwa kipindi chote nitakachokuwepo Dodoma.
Saa 7 za usiku, tulipowasili Dodoma, baridi kali lilikuwa limetanda. Nilipata lodge iliyoko karibu na Chuo cha CBE na kwenda kupumzika.
Asubuhi baada ya kuamka jambo la kwanza niliwasiliana na Aggy kumpa taarifa niko Dodoma. Kwa upande wake alishangaa sana kusikia nimekuja bila kumtaarifu mapema na alisema baada ya nusu saa atakuwa around.
Baada ya hapo, nilimpigia simu dalali ili anipe mrejesho pamoja na ratiba zake. Lengo langu lilikuwa kuanza leo hii kutafuta frem za biashara ili mipango yangu iende kama ilivyopangwa. Dalali aliniambia tukutane baadae, na akanihakikishia kwamba bado anaendelea kutafuta frem zingine ili tuwe na chaguo la kutosha wakati wa kuangalia.
Ndani ya nusu saa, Aggy alikuwa tayari amewasili, nami nikatoka kwenda kuonana naye ili tuondoke. Tulipokutana, tulisalimiana kwa furaha na tukakumbatiana kwa upendo, kisha safari yetu ya kuelekea nyumbani kwake ikaanza.
Aggy alionesha kuwa na furaha sana maana mara ya mwisho kuonana ilikuwa ni October kipindi nimeenda na Iryn. Aggy aliulizia kuhusu maendeleo ya nyumbani na hakumsahau Iryn, ndipo mazungumzo yakaanza;
AGGY: “Yule mrembo yupo?”
MIMI: “Yupo mama ila sio Tanzania hii.”
AGGY: “Na kwanini unakuja bila kunipa taarifa na unafikia lodge?”
MIMI: “Nilitaka nikusurprise au hujapenda?”
AGGY: “Tufanye umeshinda.”
MIMI: “Naona unazidi kuwa mrembo nipe siri ya mafanikio au mama anamwaga pesa mingi huko maofisini.”
AGGY: “Hahahahaa hali mbaya Insider bora hata wewe uliejiajiri.”
MIMI: “Hamjawahi kukubali kuhusu hili, sawa bhana.”
Ndani ya muda mfupi tuliwasili nyumbani kwake na alinikaribisha seblen kisha akaniandalia na chai ili ninywe. Aggy alitamani sana kujua sababu iliyonileta Dodoma, nami nilimwambia mipango yangu yote na aliishia kunipongeza. Nilimwambia nitakuwepo Dodoma kwa muda mrefu mpaka pale ambapo nitaona biashara imesimama na haihitaji tena usimamizi wangu.
Aggy aliniaga anarudi ofisini na kutoa ahadi atawahi kurudi, kwa upande wangu nilimpa ratiba zangu za kutoka jioni kwenda kuonana na dalali, na alisema atakuwa karudi tayari, hivyo atanipa kampani ya kwenda.
Saa 10 jioni tulikutana na dalali maeneo ya Sabasaba, kisha tukaanza kuangalia frem zote alizokuwa nazo. Baada ya kuzunguka sana niliipenda frem moja ipo katikati ya mjini ilikuwa location nzuri sana.
Muda ulikuwa umeenda sana, na mhusika wa hii frem alituambia tukutane kesho asubuhi ili kuweka mambo sawa. Baada ya hapo, Aggy alipendekeza tupitie sehemu kwaajili ya kupata chakula cha jioni, tutakapokarudi nyumbani, ni kulala moja kwa moja.
Wakati tulipokuwa tunakula chakula, mazungumzo yaliendelea pale, ambapo Aggy alisema kwamba mwezi ujao anatarajia kusafiri kwenda mkoani kuwasalimia wazazi wake. Nami niliona wazo lake lilikuwa zuri sana, hivyo lilinipa hamasa ya kwenda kumtembelea mama, na tukakubaliana kwamba tutaenda pamoja.
Kama nilivyowahi kusema hapo awali, mimi na Aggy tulisoma katika chuo kimoja, tukichukua course moja. Zaidi ya hilo, tulipitia shule moja ya O-Level, na wazazi wetu pia wanatoka mkoa mmoja.
Baada ya kurudi nyumbani, nilimpigia simu Maggy kumtaarifu kuwa nipo Dodoma, isinge kuwa busara kula buyu ukizingatia ananisaidia sana kuangalia nyumba yangu. Hata hivyo, baada ya kumpigia hakupokea simu zangu, kwa vile muda ulikuwa umekwenda, nilijisemea kwamba akiziona missed call atanipigia.
Aggy alikuwa amepanga nyumba ya vyumba viwili, hivyo alinionesha chumba changu cha kulala, kisha akaniga anakwenda kulala na tutaonana kesho.
Asubuhi baada ya kuamka nilikuwa na ratiba ya kukutana na dalali ili kwenda kufanya malipo kwa fremu iliyokuwa kwenye mipango yetu. Lakini, dalali alinijulisha kuwa kuna fremu nyingine mpya imepatikana na iko kwenye eneo la Sheli, tukakubaliana tuanze kwanza kuiangalia hio frem.
Baada ya kuliona eneo lilikuwa lina mvuto mkubwa, na nikawaza kuwa litakuwa na faida kubwa kama likitumika kama sehemu ya kufanyia service, huku eneo la mjini likiwa kama showroom. Nilionana na mhusika na baada ya maongezi ya muda mrefu akasema wanapangisha kwa 350,000, hivyo nilichukua namba zake za simu na tukaondoka.
Dalali alinishauri kama naweza nichukue eneo la sheli maana nitapata wateja wengi sana wa service, kwani sehemu ni nzuri sana. Tulishauriana sana na nikamwambia anipe muda nijifikirie, na alisema kuhusu fundi yupo dogo anamjua na anacheti cha VETA naweza kufanya naye kazi.
Tulienda straight kuonana na landlord ili tufanye malipo ya frem ya jana na baada ya kukutana na mhusika nilifanya malipo ya 2.4M kwa miezi 6. Sikutaka kupoteza muda nikatafuta fundi wa kuanza kutengeneza shelves ili nianze biashara.
Niliandaa mipango yangu nikaona kuna haja ya kurudi Dar kwaajili ya kuchukua mzigo wa lubricants/vilainishi. Habari njema hii biashara nina uzoefu nayo, hivyo haikuwa shida kwangu kuifanya na kuwatafuta suppliers maana machimbo yote nayajua na nina namba zao.
Niliwaza kutafuta chumba cha kupanga kwa kipindi chote nitakachokuwa Dodoma. Kuendelea kukaa kwa Aggy sikuona jambo la busara ukizingatia mimi ni mtoto wa kiume, nahitaji uhuru.
Mipango yangu ilikuwa kufikia jumatatu niwe nimenza biashara, pia niwe nimeondoka kwa Aggy tayari. Lakini jambo la kwanza nitaanza kwenda Dar, kisha baada ya kurudi nianze mchakato wa kutafuta geto.
Jumamosi frem ilikuwa imekamilika tayari kwa kuingia na kuanza bishara, hivyo nikaona kesho jumapili nirudi Dar, ili jumatatu niwe Kariakoo kuchukua mzigo.
Jioni nilienda kumsalimia Maggy nyumbani kwake maana ilikuwa ni kitambo kimepita bila kuonana. Baaada ya kuwasili pale kwake alinikaribisha, lakini nilianza kwanza kukagua nyumba.
Mazingira ya nyumba yalikuwa mazuri na yakivutia, kwani palikuwa pamepandwa maua maua na miti ndani na nje ya fenzi. Pia nilimsalimia jirani yake ambaye ni mpangaji wangu, baada ya hapo tukaingia ndani kuendelea na maongezi mengine;
MAGGY: “Karibu sana baba mwenye nyumba, sijui nikuletee kinywaji gani?”
MIMI: “Maji yanatosha.”
Alimuagiza dada aniletee maji na story zikaendelea;
MAGGY: “Umekuja lini huku? Halafu kimya kimya.”
MIMI: “Nilitaka nikufumanie una bahati sana.”
MAGGY: “Huhuuu! Yule dada mrembo yupo?”
MIMI: “Yupo masomoni ni muda hatujaonana.”
MAGGY: “Kwa uzuri tu amebarikiwa asee, kuna watu walipendelewa.”
MIMI: “Mbona wewe umependelewa mahips au hujioni?”
MAGGY: “Insider ni mshenzi wewe! Mimi nimefurahi sana kukuona, sijui wifi yangu anaendeleaje na mtoto.”
MIMI: “Wako poa nashukuru Mungu. Bado wewe sijui unasubiri nini.?”
MAGGY: “Wanaume waoaji kama wewe hawapo siku hizi.”
MIMI: “Naamini shemeji yupo ila unamfichaficha.”
MAGGY: “Insider tuachane na haya, nimekumiss sana Dar.”
MIMI: “Karibu sana kwenye mji wetu.”
Tuliongea mambo mengi likiwemo suala langu lililonileta Dodoma, pia kwa upande wake alisema ana mpango wa kutafuta kiwanja aanze ujenzi taratibu. Tulipata dinner ya pamoja na baada ya hapo nilimuaga maana Aggy alikuwa akinipigia sana simu.
Baada ya kuagana na Maggy nilimpigia simu Aggy na alisema ananisubiri ili tukale dinner, nikamwambia nimeshakula tayari, akaomba nimpelekee chips yai na mishikaki.
Baada ya kurudi home nilimtaarifu Aggy kuhusu kurudi Dar siku ya kesho kwaajili ya kuchukua mzigo na nitarudi jumatatu na nikamuaga nikaingia chumbani kulala.
Jumapili asubuhi, niliondoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam na nilifika nyumbani jioni kwenye makazi mapya. Mara baada ya kufika, mazingira yalikuwa tulivu sana kiasi kwamba nilianza kumkumbuka Junior wangu, kwa jinsi nilivyozoea fujo zake ndani, mara agombane na mama yake au dada yake kwa sababu ya utundu wake.
Mazingira ya home yalianza kuniboa mpaka nikatamani kwenda Mbweni kwa Ghati, zile siku mbili nilizolala kwake zilinidatisha sana. Baadae nikaona wacha niende Upepo garden kupoteza muda kwanza nilikuwa jirani na mazingira ya huku.
Nilikwenda nikakaa sehemu ambayo mara ya mwisho nilikuwa na Prisca na nilijukuta namkumbuka tena. Niliagiza bia zangu nikawa nakunywa huku napanga mipango yangu taratibu nikipulizwa na upepo wa bahari.
Jumatatu nilienda Kariakoo nikanunua mzigo wa kutosha, kisha nikauepeleka transporter kwaajili ya kuusafirisha kwenda Dodoma. Gari huwa zinasafiri usiku, hivyo kufikia kesho asubuhi mzigo ungekuwa umefika tayari.
Baada ya kumaliza taratibu zote, nilianza kufanya utafiti kuhusu bei za spares za magari, hasa kwa bei za jumla. Kwa bahati nzuri, Kariakoo nina kaka yangu ambaye anauza spares za magari na yuko mtaa wa MAFIA/SIKUKUU. Amekuwa msaada mkubwa kwangu katika sekta hii, na ana duka lake kubwa sana, anauza kwa jumla, jambo ambalo limenisaidia sana.
Niliwasiliana na Dullah ili tuweze kuonana na lengo nimkabidhi funguo za nyumba incase kama mama J atahitaji kurudi home na tulikutana pale breakpoint Makumbusho japo alifika kwa kuchelewa sana;
MIMI: “Naelewa bro! Kama unavyoniona niko busy na mipango yangu hapa.”
DULLAH: “Dadeki kitu Macbook Air hii dukani inakwendaje?”
MIMI: “Mahali uliyolipa kwa Latifah zidisha mara 4.”
DULLAH: “Mseng** wewe unataka kusema ina thamani ya Million 8?”
MIMI: “Ndo maana yake au huamini?.”
DULLAH: “Niambie naona umebadili namba ya simu tayari na ukaondoka bila taarifa, nakutafuta kwa simu sikupati mpaka nikahisi labda dada amekufungia ndani.”
MIMI: “Daah aisee sio poa, halafu unajua ile manzi ina mtoto? Japo anadai baba mtoto alikufa.”
DULLAH: “Mhh! Becareful mzee, umeomba akuoneshe kaburi la baba mtoto?”
MIMI: “Tuachane na haya kaka, mwanamke mwenyewe sina mpango naye ilitokea bahati mbaya wewe ndo uliniforce niende. Unajua nilikuwa Dodoma na nimepata frem tayari?, halafu nimerudi jana kufuata mzigo na kesho mapema naondoka.”
DULLAH: “Hongera sana kaka, itabidi nije Dodoma siku moja maana sijawahi fika kabisa.”
MIMI: “Karibu uje uangalie fursa. Mzee mimi sina story leo, nilichokuitia hapa nilitaka nikupe taarifa ya kuanza biashara na pia nimehama pale home, nimehamia mbezi chini kabisa.”
DULLAH: “Kwanini umehama sehem nzuri kama ile?”
MIMI: “Nimehama kwasababu maalumu, pia naomba nikukabidhi funguo endapo wife akihitaji atawasiliana na wewe.”
DULLAH: “Haina shida bro usiwe na wasiwasi.”
MIMI: “Nashukuru sana, mimi sikai nataka niwahi home nikalale, kesho niwahi kuondoka kwenda Dodoma kupokea mzigo. Baada ya hapo nina safari nyingine tena ya kwenda mkoani kumsalimia mama yangu.”
DULLAH: “Naona unataka ukachukue baraka kwa bimkubwa.”
MIMI: “Muhimu kaka si unajua biashara zina mazingaombwe sana.”
DULLAH: “Naelewa kaka wewe wahi mengine tutaendelea kuwasiliana.”
Baada ya kuachana na Dullah niliondoka straight kuelekea home na baada ya kufika, nilifanya mawasiliano na Aggy anisaidie kumtafuta dada wa kushinda dukani.
Kesho yake nilirudi Dodoma mapema maana nilitumia usafiri wa anga, pia nilikuwa nina safari nyingine ya kwenda mkoani. Baada ya kuwasili nilienda moja kwa moja kufuatilia mzigo wangu na baada ta kuupata nilitafuta usafiri wa kuupeleka dukani.
Baada ya kupeleka mzigo dukani, nilimpigia Aggy simu kumtaarifu kwamba naenda mkoani kumsalimia mama yangu. Aggy alishangaa kwanini haraka sana? Hata sijapata muda wa kupumzika?, nikamwambia ni muhimu sana kwenda, na nikaondoka kwa private.
Niliingia mkoani usiku kwa upande wa pili, mama hakuwa na taarifa za ujio wangu, hivyo nilitaka kumsaprize. Nilipofika home geti lilikuwa tayari limefungwa, ikabidi nigonge, mbwa walikuwa karibu wakaanza kubweka pale, na walikoma mara moja waliponitambua.
Moja ya Mbwa wetu anaitwa Askari, alisogea getini kwa furaha kubwa muda huu. Alianza kutoa kelele za furaha kuniona huku akitikisa mkia wake kwa nguvu na kurukia geti kwa msisimko. Askari ni mbwa ambaye nimemlea tangu akiwa mdogo, na licha ya kwamba naweza kutokuwepo nyumbani kwa muda mrefu, kila ninaporudi, daima ananikumbuka kwa upendo wa kipekee.
Dada alikuja kufungua geti na kunikaribisha ndani na ile kuingia seblen mama alikuwa na wadogo zangu wakiangalia tamthlia na baada ya kuniona aliishia kufurahi na kuja kunikumbatia kwa nguvu.
“Ooh mwanangu nimetoka kukuwazia sio muda mrefu, mbona unakuja bila kutoa taarifa huko umefukuzwa?”
“Sijatokea Dar nilikuwa Dodoma.”
“Kuna nini huko?”
“Kuna biashara nataka kuianza ndiyo imenileta hapa home.”
“Niambie nakusikiliza mwanangu.”
Tulianza maongezi na mama, ambapo nilimshirikisha kuhusu biashara ninayotaka kuanzisha. Mama alifurahi sana na alinipongeza, kisha akasema tutafanya maombezi ya nguvu kabla ya kwenda kulala. Pia, tulizungumza kuhusu mimi kuwa Zambia, na mama alifurahi sana baada ya kupata taarifa kutoka kwa baba.
Baada ya maongezi marefu, nilimkabidhi mama yangu zawadi maalum, simu ya Samsung niliyonunua Dar es Salaam. Mama alifurahi sana kwa zawadi ya simu na bila kuchelewa akaweka line.
Kabla ya kwenda kulala kama familia tulifanya maombi juu ya biashara nayoenda kuianza kwa kufunga Roho za chuma Ulete, tukimwomba Mungu kuondoa maadui watakaojaribu kunikwamisha katika safari yangu ya kibiashara. Tuliiomba pia msaada wa kupata wateja, ili biashara yetu iweze kustawi kwa mafanikio.
Baada ya maombi nilimuaga mama nakwenda kulala na masuala mengine mengi tugaongea kesho panapo majaliwa. Lakini zawadi ya simu ilimgusa sana mama yangu maana alifurahi sana na alizidi kunishukuru.
*****
Jumatano nilirudi Dodoma na niliwasili jioni, nilikuwa nimechoka, lakini nilikuwa na matumaini makubwa ya kuanza biashara siku inayofuata. Kwa bahati nzuri, Aggy alikuwa tayari amempata dada ambaye angeweza kunisaidia dukani. Huyu dada alikuwa ni mfanyakazi wake wa zamani, kabla Aggy hajafunga biashara yake.
Aggy alinihakikishia kuwa huyu dada ni mchapakazi, mwelewa, na mwenye uaminifu, hivyo atanifaa sana katika biashara yangu. Bila kusita, nilimuomba Aggy amfahamishe ili kesho tukutane kwa ajili ya mazungumzo zaidi na kupanga jinsi ya kuanza kazi pamoja.
Mnamo Alhamisi, tarehe 16/03/2023, nilifungua rasmi biashara yangu. Nilianza kwa kuwajulisha watu wa karibu na kuwaomba waniunge mkono. Nilitembelea garage mbalimbali na kuwaeleza kuhusu biashara yangu, huku nikiwapatia punguzo maalum la bei.
Jumapili, nilimtembelea Mzee Mollel nyumbani kwake ili kumsalimia na kumshirikisha kuhusu biashara mpya niliyofungua. Mzee Mollel ni rafiki wa karibu wa baba yangu, na ninamheshimu sana kama mzazi wangu mwenyewe.
Mzee Mollel alifurahi sana kusikia hizi taarifa na hakuishia hapo akaniashauri nifanye na service kabisa za magari. Alikuwa mulemule kwenye mipango yangu.
“Sasa hivi Dodoma imekua sana na magari yameongezeka kwa wingi. Kama utaweza fanya na service za magari, mteja akija kupata huduma unamuuzia na oil, hivyo mzunguko wa hela utaonekana kwa urahisi. Wewe umetoka Dar es Salaam, basi onyesha utofauti na wafanyabiashara wa hapa. Ukifanya hivyo kwa ufanisi, baada ya mwezi mmoja utaanza kuona mafanikio."
“Ahsante mzee hili la kufanya service lipo kwenye mipango yangu na kuna sehemu nilipata acha nikalifanyie kazi.”
“Wewe ukikamilisha nijulishe wateja nitakuletea wengi sana hili ondoa wasiwasi, cha muhimu kama nilivyokwambia awali onesha utofauti na wengine.”
“Ahsante kwa ushauri wako mzee.”
Mzee alinipongeza sana kwa maamuzi niliyoyachukua na alisema atanisapoti kwa kadri ya uwezo wake. Nilishinda pale kwake mpaka usiku nikapata na dinner, kisha nikaaga na kuondoka kurudi kwa Aggy.
Niliona umuhimu mkubwa wa kulisimamia suala la biashara kwa bidii na umakini wa hali ya juu, kwani kufeli kwangu kutanirudisha katika ajira, jambo ambalo sitaki kabisa. Kwa upande wangu, kuajiriwa ni sawa na kujifunga katika utumwa wa hofu na mashaka ya maisha. Ni kweli, mshahara unaweza kuwa mkubwa, lakini utatosha vipi kulipa uhuru wangu?.
Niliporudi nyumbani, niliwasiliana na dalali na kupanga tukutane kesho na yule kijana ambaye aliniambia angeweza kunifaa kwenye masuala ya service. Pia, tulikubaliana tuwahi kuonana ili tuende kwenye eneo husika, na ikiwezekana, tufanye malipo kabisa
Kesho yake tulikutana na dalali akiwa ameongozana na dogo, nilimfanyia usaili kidogo na niliona yuko vizuri ana uwezo, pia alionesha nia ya kufanya kazi pamoja nami. Baada ya kumalizana na dogo, tulienda kukutana na mhusika mkuu ili kupata muongozo wa namna ya kufanya malipo.
Tulikutana na dada ambaye alionekana kuwa msimamizi wa eneo hilo, na mara ya kwanza, tulikutana na kaka, lakini leo hali ilikuwa tofauti. Dada huyu alikuwa na mvuto wa kipekee maana alikuwa kafungasha vizuri, alitupa muongozo na nikafanya malipo ya miezi sita kwa kiasi cha shilingi 2,100,000.
Baada ya hapo nilikaa chini na dogo ili tupange mipango kuhusu vifaa vya kazi atakavyohitaji maana kama eneo alikuwa keshaliona tayari. Dogo alisema ninunue compressor, mashine kwaajili ya wheel balancing, Automatic tyre changer, stand jack, bila kusahau sare/uniform na buti akiwa kazini na vifaa vingine vingi.
Dogo aliahidi kuwapa taarifa wateja wake wote wa zamani ili waje kwenye ofisi mpya, nami nilimuahidi kumpa bonasi kwa kila mteja mpya atakayeleta. Kuhusu mshahara, tulikubaliana kuwa nitaanza kumlipa 250,000 kwa mwezi, ambapo chakula na nauli zitakuwa juu yangu. Pia, nilimwambia kwamba mambo yakianza kwenda vizuri, atapata bonus kwa kila gari atakaloifanyia service.
Tuliagana kwa makubaliano ya kukutana pindi nitakapokuwa nimekamilisha kununua vifaa vya kazi, na nilimwambia kuwa ndani ya siku mbili vitakuwa tayari, hivyo ajiandae muda wowote nitampigia simu.
Nilipanga hesabu zangu kwa umakini na kugundua kuwa kuna umuhimu wa kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya kununua vitendea kazi. Hata hivyo, biashara kule dukani ilikuwa bado ngumu, hasa kwa kuwa duka lilikuwa jipya. Aidha, nilikuwa nikimfundisha dada kuhusu aina za lubricants ili aweze kutoa huduma bora kwa wateja.
Baada ya siku mbili kupita nilirudi tena Dar es Salaam kwaajili ya kununua vifaa na nilienda Posta mtaa wa India. Kuna fundi wangu ndo aliniongoza kwa moja ya supplier ambaye anamjua na amenyooka.
Baada ya kufika dukani niliwaelekeza vifaa navyotaka pamoja na kupewa discount, baada ya kufanya malipo walisema watanitumia na nitapigiwa simu namna ya kupata mzigo wangu.
Nilimaliza mapema sana kisha nikarudi home kupumzika na nilipanga jioni nionane na Hilda kwaajili ya maongezi. Tangu niondoke Dar wiki mbili zilikuwa zimekata tayari, halafu hatukuwa na mawasiliano yoyote
Jioni ilipowadia Hilda alinipigia simu na kuuliza tunakutania wapi? Nami nilimjibu asogee mpaka Mikocheni ‘Triple 7’. Nilianza kujiandaa pale kwa haraka na baada ya nusu saa nilitoka home kuelekea eneo la tukio.
Baada ya kuonana tulianza mazungumzo pale na aliishia kulalamika kwanini sipatikani kwenye simu? Maana amekuwa akinipigia bila mafanikio;
MIMI: “Nilisahau kukupa namba mpya, halafu nilikuwa busy sana kule Dodoma hata hapa unaniona sababu kuna vifaa nimefuata.”
HILDA: “Insider usifanye hivo, uliniahidi utakuwa available pindi nakuhitaji, hata Lucy anakutafuta sana bila mafanikio unatuacha kwenye mataa wenzako.”
MIMI: “Pole mummy ndomana leo nimekutafuta ili tuongee, pia nimekumiss sana ujue.”
HILDA: “Don’t say that, mimi naona ofisi ni chungu, nilishazoea kukuona, kunitania muda wote nakuwa na furaha ofisini, umeniacha mpweke.”
MIMI: “Nollie si yupo?”
HILDA: “Sawa yupo, lakini hatuwezi kuwa na ukaribu kama wako.”
MIMI: “Embu niambie ni nini kiliendelea tangu tuachane kipindi kile ni week 2 tayari.”
HILDA: “Thanks God mzigo tulipata week iliyopita na tumelipa deni tayari, mama alirudi aka clear deni.”
MIMI: “Good news na anasemaje yeye?”
HILDA: “Nothing! Ila alikuulizia nikamwambia bado upo likizo.”
MIMI: “Kuna taarifa yoyote kutoka kwa Iryn?”
HILDA: “Hapana sijasikia ni muda mrefu sana na kila mtu anamuulizia pale ofisini.”
MIMI: “Ahsante kwa mrejesho mzuri bila shaka kwasasa huna stress kila kitu kipo kwenye track huna haja ya kuwa na wasiwasi tena.”
HILDA: “Ripoti zangu si unazipata lakini?”
MIMI: “Niwe mkweli sijawahi hata kuangalia ila tukiachana hapa nikirudi home nitaziangalia.”
HILDA: “Halafu umenikumbusha, Lucy alikuja kwako akaambiwa umehama, hapa ndo amechanganyikiwa anakuwa na wasiwasi sana juu yako.”
MIMI: “Nimehamia jirani hata sio mbali na nilikokuwa naishi zamani.”
HILDA: “Asmah pia anakuulizia sana, anahisi mimi na wewe tuna mawasiano ya siri ila namficha.”
MIMI: “Asmah hana taarifa wala sikumuaga pamoja na Lucy, hivyo hawajui niliko. Kama tulivyokubalina before usimpe mtu namba yangu bila kupata idhini yangu.”
HILDA: “Sawa hili ondoa wasiwasi Insider.”
Tuliendelea na maongezi mengine, lakini nilipata wazo la kwenda kumsalimia Asmah pale kwake kabla sijaondoka kurudi Dodoma kuendelea na mishe zangu.
Nilimdrop Hilda Morocco nami nikaendelea na safari ya kwenda Upanga na nilitumia barabara ya Kawawa ili nikaunge na barabara inayokwenda Makaburini, sikumwambia Hilda kama nakwenda kwa Asmah.
Baada ya kuwasili kwa Asmah nilipark gari usawa wa apartment yake, lakini kwa leo kulikuwa na utofauti maana kuna Crown nyeusi ilikuwa imepark pale.
Baada ya kushuka kutoka kwenye gari, nilipanda hadi ghorofa ya kwanza na kugonga mlango. Sikumpigia simu kwa sababu nilitaka iwe saprize, nilijua kuwa kwa nyakati za usiku, mara nyingi huwa nyumbani. Huu ulikuwa utaratibu wangu wa kawaida, kwenda bila kutoa taarifa.
Asmah alifungua mlango na ile kuniona alishtuka sana na alitoka nje akarudishia mlango;
ASMAH: “Insider what are you doing here?”
MIMI: “What? Mimi ndo wakuniuliza hivo? Hata salamu hakuna.”
ASMAH: “Kwanini unakuja bila taarifa?”
MIMI: “Mara ngapi nakuja hapa kwako bila taarifa?”
ASMAH: “Please naomba uende nitakucheki badae niko na kaka yangu akiona hivi atachukia.”
MIMI: “Ahh! Hayo unaleta wewe mimi nimekuja ili nikusalimie sasa wasiwasi wako ni nini?.”
Niliamua kuondoka sikutaka kuendelea kupoteza muda, lakini nili smell something fishy kinaendelea. Niliwasha gari yangu ili niondoke, lakini Crown iliyokuwa imepaki pembeni ilinipa mashaka, nikahisi Asmah atakuwa amepata mhuni.
Nilivyofika getini ilibidi nimpige maswali mlinzi kuhusu ile Crown na alisema hii mara ya pili anaiona ikiingia na kutoka. Niliondoka kurudi home ili nikajiandae na safari yangu ya kurudi Dodoma nikaendelee na harakati zangu.
Baada ya kurudi home kutokana na mazingira kuwa ya kimya na upweke nilifikiri nikaona kuna umuhimu wa wife kurudi home. Niliwaza pale nimpigie simu tuongee arudi home, lakini niliona ni heri arudi mwenyewe ili kutunza heshima yangu.
Niliingia Shabiby Online na kukata tiketi yangu ya bus mapema. Pia nilianza kufikiri namna ya kutoka pale kwa Aggy na nikaona pindi nitakapo rudi Dodoma, nianze kutafuta gheto. Nilijiuliza sana, Aggy ni binti na kuna uwezekano kwamba kuna mwanaume anayemlipia kodi, kuendelea kukaa pale kwake ni sawa na kumuumiza. Hata kama tumekuwa marafiki wa muda mrefu, lakini kwa hatua tuliyofikia sasa, kuna baadhi ya mambo yanahitaji kupeana nafasi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.