Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
cacuteeSEASON 02
EPISODE 30
“BY INSIDER MAN”
CONTINUE:
Niliondoka na Shabiby ya saa 4 asubuhi na niliwasili Dodoma jioni, Aggy alikuja kunipokea na tukapitia Golden fork kupata dinner;
MIMI: “Unapenda sana vyakula vya kudownload kwa mtoto wa kike haipendezi.”
AGGY: “Sometimes kuchoka na uvivu unachangia.”
MIMI: “Ukiolewa itakuwaje?”
AGGY: “Lazima niingie jikoni.”
MIMI: “This time nataka unitambulishe shem wangu maana unamficha sana.”
AGGY: “Insider kuwa na subira bro! Mambo mazuri hayataki haraka.”
MIMI: “Ausioo ila mahusiano yangu ulikuwa unayafuatilia sana.”
AGGY: “Insider yaishe bhana.”
MIMI: “Kuanzia jumatatu mimi nitaondoka kwako nataka nihamie kwangu.”
AGGY: “What? Yaani ukapange na kwangu sehemu ya kulala ipo?. No! siwezi kuruhusu hili litokee.”
MIMI: “Nafikiri unasahau kuwa mimi ni mwanaume na wewe ni mwanamke.”
AGGY: “Unamaanisha unakosa uhuru wa kufanya mambo yako? Au nimekuelewa vibaya?”
MIMI: “Unaweza kuwa sahihi, mimi naanza harakati zangu kurudi usiku kwako sio busara, pia wewe ni mtoto wa kike nataka kukupa uhuru wa kufanya mambo yako, hata mimi nahitaji uhuru wa kufanya mambo yangu. Kuendelea kukaa kwako kwa muda mrefu sio sawa kabisa, au wewe unaonaje ni sawa?”
AGGY: “Mimi naelewa unataka uhuru wa namna gani na sikushangai maana hata mdogo wangu anaonaga bora alale hotelini kuliko kulala kwangu.”
MIMI: “Kumbe somo limekuingia haya nipe tano.”
AGGY: “Shenzi zako ni uhuni tu hakuna lolote.”
MIMI: “Sio uhuni toka nifike kwako sijawahi kumuona shem akija kumaliza shida zako au wewe ukienda kwake kumaliza shida zake, sababu unaniogopa mimi.”
AGGY: “Hahahaa! Ila Insider mpaka leo siaminigi uliwezaje kukaa na mwanamke ndani inawezakana wifi yangu anavumilia mengi tu. Naomba nikuulize, hivi bado mnawasiliana na Angel?”
MIMI: “Hahahaa! Sijui umewaza nini mpaka umekumbuka Angel, huyo b*tch mimi nilishamsahau kitambo sana. Tulikutana 2022 mwishoni pale Karambezi, alinipa namba zake, lakini nilifuta.”
AGGY: “Anapost sana Instagram, nilim-DM tukachati kidogo akasema nikupe hi, nikamwambia Insider ana mke sahivi utamuharibia. Mpaka leo hukuwahi kunambia sababu ya kuachana kwenu, naona uliamua iwe siri yako.”
MIMI: “Sikia, Angel alinipiga tukio ndiyo sababu ya kuachana, ndomana sikukwambia kipindi kile, tuachane na huyu malaya hana umuhimu kwangu.”
Baada ya kupata dinner tuliondoka kurudi home kulala nami nilifanya kuwasiliana na Dalali aanze kunichekia chumba ili nihamie haraka iwezekanavyo.
Kwa upande mwingine Pesa ilikuwa imekata tayari, nilikuwa nimefulia sina pesa na balance iliyokuwa imebakia ni 340,000 tu. Nilipiga hesabu napata wapi Pesa?, sikutaka kumshirikisha Aggy juu ya hili maana alikuwa analalamika sana kuwa anakatwa makato makubwa kwenye kulipia mkopo wake, alikopa kwaajili ya kufanyia ujenzi kwao.
Nilipiga hesabu nipate million 2 kama akiba ili niweze kupanga geto na kununua baadhi ya mahitaji na nyingine inisaidie kuendesha ofisi. Baada ya kuwaza sana nikakumbuka wapangaji wangu wanamaliza mwezi wa 4 mikataba yao, hivyo niliona nimtafute Maggy nimuombe anilipe kabisa.
Nilimpigia simu Maggy kuomba kuonana naye na alisema tuonane jumamosi asubuhi maana kwa kesho ana safari ya kwenda Arusha kwenye kikao na atarudi jioni.
Siku ya jumamosi iliwadia na Maggy alinipigia simu kunipa taarifa yuko home, hivyo naweza kwenda. Saa 4 asubuhi niliwasili pale kwake na baada ya kuonana nilimueleza shida yangu inayonikabili kwa kipindi hiki. Maggy bila hiyana alisema nimpe account yangu ili afanye kutransfer hiko kiasi na niliishia kumshukuru, kisha nikaenda kuonana na Dalali.
Dalali alinionesha vyumba vyote alivyokuwa amepata na niliipenda masta ambayo ilikuwa meneo ya Uzunguni. Mazingira yalikuwa mazuri sana na kwenye compound zilikuwepo nyumba 5, Master ilikuwa moja tu ambayo ni yangu zilizobaki zilikuwa ni chumba sebule na moja ina vyumba 2.
Master ilikuwa ni nzuri na niliona itanifaa sana kwa kipindi chote nitakacho kuwepo huku. Baada ya kufanya malipo nilienda kununua Godoro na mashuka ya kujifunika kwaajili ya baridi, bila kusahau mito.
Sikutaka mbwembwe za kununua kitanda nilijisemea godoro tu linatosha cha muhimu na sehemu ya kulala, sijaja Dodoma kula bata. Kuhusu kula nilipanga nitakuwa nakula kwa mama ntilie, hivyo hakuna haja ya kununua jiko.
Jumatatu ndo nilihamia geto rasmi na ndio siku ambayo tulianza kazi rasmi na dogo kwenye upande wa service, gari ya kwanza kuanza nayo kazi ilikuwa ya Aggy ‘BMW X1’.
Pale geto nilikuwa nina ishi maisha yangu sikuwa na habari na mtu zaidi ya jamaa yangu Michael ambaye tulitokea kuelewana kwa haraka sana. Michael alikuwa kapanga chumba na sebule ndo mtu pekee aliyenikaribisha mazingira ya pale, kutokana na ucheshi wake tulitokea kuelewana sana.
Pale ofisini yule dada ambaye alinipokea na kuandikishiana mikataba tulitokea kuzoeana kwa haraka sana, na alikuwa kama mtani wangu maana nilikuwa namuita ‘Sanchi’ sababu kabarikiwa makalio.
Sanchi alikuwa zaidi ya rafiki wa kazini, ilikuwa haipiti siku bila kutaniana labda asije kazini. Kila mchana, nilijikuta nikienda ofisini kwake kupumzika, ambapo yeye alikuwa meneja wa kile kituo cha mafuta.
Siku moja, nilimuomba aniruhusu kuzungusha kamera ili iweze kuangalia upande wangu, kwani ilikuwa imeelekezwa sehemu isiyokuwa na umuhimu. Aliniambia, "Tutaifanya hiyo kazi Jumatatu, mpaka fundi aje na kuiset kwenye mfumo."
Jumatatu ikafika, na Sanchi hakutokea kazini.
Jumanne ilipowadia, Sanchi alichelewa kufika ofisini. Lakini alipowasili, alikuja moja kwa moja kuniangalia kama nipo. Akanikuta nikiwa namwaga oil ya gari la mteja, na aliniita kwa sauti laini, na akaanza matani yake;
SANCHI: “Bossy hata wewe unafanya hizi kazi? Kuna haja gani ya kumuajiri fundi?”
MIMI: “Sema umebarikiwa sana, hilo Bunango ukienda Bank wanakupa mkopo bila riba.”
SANCHI: “Umefanya nisahau hata nilichotaka kukwambia nitarudi badae.”
MIMI: “Usiondoke bhana si unajua wewe ni mtani wangu? Haya nambie ulitaka kusema nini?”
SANCHI: “Hio camera kama unaweza izungushe imulike upande wako, halafu mimi nitaangalia kama imekaa sawa haina haja ya fundi kuja.”
MIMI: “Hayo ndo maneno, hapo sasa naweza kuwa na jeuri ya kukutoa out ukale dinner.”
SANCHI: “Wewe huyo na ulivyo bahiri hata hauendani na muonekaneno wako, hujawahi hata kunipa offa ya lunch utaweza kunitoa out?”
MIMI: “Kukutoa out sio shida, tatizo nahofia uhai na usalama wangu mali unayomiliki hio ni balaa.”
SANCHI: “Yaani wewe nishakuzoea una matani sana.”
MIMI: “Sasa bossy wangu soon nakucheki.”
Habari mbaya Sanchi mwaka huu alitangulia mbele ya haki, ni moja ya watu ambao walinisaidia sana kupata wateja tena wale madon. May her soul rest in peace! AMEN.
Mwezi wa tatu ulipita, na licha ya biashara kusuasua kwa pande zote, kulikuwa na dalili za matumaini. Huku nikiwa na matumaini mapya, niliendelea kupambana kwa bidii, nikitumia mbinu mbalimbali ili kuvutia wateja.
*****
Kuanzia mwezi wa nne, biashara ilianza kuimarika, na matumaini yakaanza kuchanua. Hakukuwa na siku iliyopita bila kuuza pale dukani au kufanya service ya gari, kwa siku za weekend kazi zilionekana. Kujaza upepo kwenye tairi za gari kulifanya tusikose pesa ya lunch, maana nilijitahidi kuwa na vipimo imara ili kuleta ulinganifu wa tairi zote.
Watu walikuwa wameanza kuzoea mazingira na niliwashirikisha watu wangu wote wa karibu wa pale Dodoma wanisaidie kwa hili. Biashara ni connection ya watu na sikuzote watu wa karibu ni moja ya key agents wa kukufanikisha.
Dogo alikuwa akipiga sana kazi kwa upande wake pamoja na kujituma kwa bidii sana. Kutokana na mazingira yetu kuwa mazuri na ya kuvutia tulianza kupigiwa simu na kupata wateja kutoka sehemu mbalimbali.
Nilipata wazo nifungue kampuni ili niweze kuomba tenda mbalimbali hasa kwenya makampuni na serikali. Niliamua kuelekeza akili yangu kwenye biashara na ili niweze kupata hizi tenda, bila kampuni kutoboa ni ngumu.
Nilianza process za kufungua kampuni Brela, tatizo lilikuwa nani nimuweke awe Director? Maana kampuni sheria ni lazima kuanzia directors wawili. Nilikuwa napata ukakasi kumuweka mama J sababu sikuwa na imani naye kama tutaendelea kuwa pamoja, licha ya yote, nilikuwa nishamsajili kwenye mali nyingi sana kama nyumba na magari.
Baada ya kujifikiria sana niliona ni bora nimuweke mama yangu mzazi, mabadiliko mengine nitafanya hata hapo baadae. Nilianza process online na nilifanya mwenyewe kasoro kwenye kuandaa memorandum ndo nilihitaji msaada kutoka kwa Wakili.
Mnamo tarehe 6 April, kampuni yangu ndo ilisajiliwa rasmi, baada ya hapo nikaanza process za kusajili TIN ya biashara TRA, bila kusahau kununua mashine ya EFD maana walikuwa washaanza kunisumbua pale dukani.
Baada ya kumalizana na TRA ilibidi nianze process za kufuatilia leseni ya biashara manispaa, kisha nikaja na watu wa OSHA, Mara taka, fire nknk. Mambo ni kibao sio poa.
Baada ya kumalizana na mamlaka za serikali nilianza kufikiri namna ya kuandaa mkakati bora wa kupata tenda mbalimbali ili niwe na uhakika wa kazi. Akili yangu niliielekeza kwenye biashara sikutaka masikhara kabisa, nilikaa mbali na wanawake pamoja na starehe.
Ndugu yenu nilianza kufubaa na kupauka, mnajua hali ya hewa ya Dodoma, sivyo? Kwangu mimi, hali hiyo hainifai kabisa. Jua lile ni kama Jehanam ndogo, na maji ya chumvi ni balaa. Kuishi Dodoma ni kama kuteseka.
Yale maisha ya Dar es Salaam ya kwenda migahawa ya gharama na hadhi nilisahau kabisa. Sehemu yangu ya kula ilikuwa ni kwa mama ntilie “Mama Gire” huyu mama kanilisha sana. Asubuhi nilikuwa napata soup safi, mchana napata wali wangu wa nguvu, usiku ndo nilikuwa mara nyingi nakula karibu na mazingira ya geto.
Jumamosi ya wiki hii ya kwanza ya mwezi Aprili, niliamua kuwasiliana na dada yangu ili nijue kama kuna taarifa yoyote mpya kutoka kwa mama J. Tangu nilipofika Dodoma, sikuwa nimezungumza na dada yangu, kwa hiyo nikaona ni muhimu kuwasiliana naye.
Baada ya kumpigia simu alipokea na tukaanza mazungumzo na habari kubwa alisema mama J ananitafuta sana;
SISTER: “Wifi kachanganyikiwa huko karudi home kakuta haupo, amenipigia simu anaanza kulalamika umehama bila kumpa taarifa, na hupatikani kwenye simu. Anahisi umeenda kupanga sehemu nyingine na mwanamke mwingine. Mimi nikamuuliza kwani ulikuwa haupo nyumbani? Na kwanini ahame bila kukupa taarifa, nini kinaendelea?.”
MIMI: “Ehe! akasema nini?”
SISTER: “Huwezi amini hajasema chochote, zaidi kasema aliondoka mkiwa hampo kwenye maelewano mazuri. Ndipo nikamwambia suala la kuhama ulinishirikisha, lakini mimi sijui kinachoendelea kati yenu maana hata wewe hajanambia.“
MIMI: “Nilimpigia simu hakupokea sasa analalamika nini?”
SISTER: “Mtafute wifi yangu, anaonekana anataka kurudi home, tumeongea haya since jumatatu, lakini kwenye simu nikawa sikupati.”
MIMI: “Nilikuwa busy sana hapa katikati maana siko mjini kama tulivyoongea, lakini sahivi kidogo mambo yanaenda.”
SISTER: “Safi sana nafurahi kusikia hivo.”
MIMI: “Bhasi poa, ngoja nimcheki sahivi nimsikie anasemaje.”
SISTER: “Fanya hivo yule ni mke wako hata kama hamjafunga Ndoa, siku ambayo atachoka kuvumilia utampoteza na utajutia sana.”
MIMI: “Leo namaliza dada yangu acha kuninanga.”
Baada ya kuongea na sister niliamua kumpigia simu wife ili tuongee, ikiwezekana niyamalize kabisa. Simu iliita kwa mara ya kwanza ikakata bila kupokelewa, nikapiga tena kwa mara ya pili ndo kupokea.
MAMA J: “Nani?”
MIMI: “Ahh mke wangu ni mimi baba watoto huna haja ya kuwa na wasiwasi. Nimekumiss sana ujue, nimekupigia kukujulia hali pamoja na mtoto.”
MAMA J: “Umenimiss wapi au sababu wifi amekupa taarifa nakutafuta?”
MIMI: “Hapana sijaongea naye muda mrefu sana maana sahivi napatikana kwa hii namba mpya.”
MAMA J: “Mimi nilifikiri umeamua kuhama na kubadilisha namba ili usipatikane, tusikusumbue.”
MIMI: “Nipo Dodoma kuna project nimekuja ifanya, ikikaa sawa nitarudi huko Dar. Vipi unataka kurudi home nikuelekeze kwenye makazi yetu mapya?”
MAMA J: “Sitamani kurudi kuendelea kuishi na wewe na kama unataka mimi nirudi njoo nichukue home.”
MIMI: “Nakutumia pesa ya Uber urudi home sawa?”
MAMA J: “Aliyekwambia mimi sina nauli ni nani?”
MIMI: “Kukuhudumia ni jukumu langu hata kama una hela.”
MAMA J: “Haya kwaheri.”
Ilipita dakika 10 hivi akanitumia text message…
“Umehamia sehemu gani?”
“Mbezi chini karibu na kota za BOT.”
“Sizijui.”
“Bhasi karibu na Sea breeze hall. Ukiwa tayari nambie nikupe namba ya Dullah akupe funguo za pale home.”
“Okay! Send me his contact.”
Nilimtumia namba ya Dullah na tukaagana pale, kwa upande wangu nikajisema case closed.
Baada ya hapo niliwasiliana na Jane ili kumjulia hali maana toka niondoke Dar hatukuwa na mawasiliano kabisa, pia nilikuwa sipatikani kwa simu. Simu iliita kwa muda mfupi na akapokea pale;
MIMI: “Hello shem! Ni mimi Insider.”
JANE: “Oh! I can’t believe, nimekuwazia sana leo nikipiga simu yako hupatikani.”
MIMI: “Pole sana, nilikuwa busy sana huku ndomana ukaona kimya, halafu hii ndo namba yangu inayopatikana kwasasa.”
JANE: “Hukunipa hii namba ndomana.”
MIMI: “Sorry! Unaendeleaje lakini pamoja na mtoto?”
JANE: “Niliumwa sana hapa katikati mpaka nikalazwa, lakini namshukuru Mungu nilipona salama.”
Taarifa za Jane zilinishtua sana na nilianza kujiona na hatia maana sikuwahi mtafuta wala kumpa namba yangu mpya;
MIMI: “Shem pole sana na pia naomba nisamehe kwahili.”
JANE: “Usijali, jambo jingine, kwanini uliondoka pasipo kumuaga Mary? Unakosea sana shem, Mary ni moja ya familia yetu usimtenge, uwe unamshirikisha mambo yako.”
MIMI: “Ni kweli shem! Nilisahau tu kwa bahati mbaya nitamcheki kumuomba msamaha juu ya hili.”
JANE: “Sawa! Fanya hivo.”
Baada ya kumalizana na Jane niliendelea kuwaza pale kitandani kwa dakika kadhaa, kisha nikalala zangu ili kesho niwahi kwenda church.
*****
Mwezi ulikuwa umewadia tayari tangu nizamie Dodoma. Kuhusu upande wa biashara mambo yalianza kuwa mazuri wanasema ‘When one door closes another opens’.
Pesa nilizokuwa napata kwenye biashara nilikiwa nazideposit bank kwenye akaunti ya kampuni. Nilikuwa makini sana hasa kwenye kufanya cost minimization stategies ili niweze kupata Profit kubwa.
Katikati ya mwezi wa nne siku ya jumapili mama J alirudi home na alinipa taarifa kabla ya kurudi home. Taarifa nyingine aliyonipa ni kuhusu mama wawili, alisema alimpigia simu kuniulizia, na akamwambia mimi nimesafiri ndomana sipatikani.
Nilikumbuka ahadi ambayo nilimpa Pili kuhusu kwenda kwenye mahafali yake ya kidato cha sita maana ndo mwezi wa 4 ulikuwa katikati na mahafali nyingi huwa zinafanyika mwezi huu. Niliwaza sana kuhusu hili jambo nikaona haina haja ya kwenda wacha niendelee na harakati zangu, niliona natakiwa kukaa mbali na mama wawili, nimuache na maisha yake.
Zilipita siku mbili, na asubuhi hiyo nikiwa kazini, Mary alinipigia simu. Nilipogundua ni yeye, nikaamua kuipokea. Kama ilivyo kawaida yake, alianza kunilaumu kwamba nimeondoka bila kumpa taarifa.
MIMI: “Mary I’m so sorry niliondoka kwa haraka, na baada ya kufika huku mambo yakawa yamenibana sana.”
MARY: “Kama ulikumbuka kumuaga dada Jane, why me?”
MIMI: “Ndiyo maana nimekuomba unisamehe kwa hili. Tafadhali elewa, sifanyi kwa kusudi; kuna mambo mengi yanayonisumbua sana akili yangu kwa sasa.”
MARY: “Dada Jane kaumwa sana, wewe hupatikani mpaka tukaanza kuingiwa na wasiwasi.“
MIMI: “Tumeongea juzi hapa, ahsante sana kwa yote uliyofanya.”
MARY: “Ujue ninakujali na kukuthamini, lakini wewe unanitupa sana mpaka huwa nawaza labda kuna kitu nilikukosea.”
MIMI: “Mary I really appreciate kwa yote unayofanya, naomba utambue nina pitia mambo magumu sana kipindi hiki.”
MARY: “Sawa pole! I’m not here to complain mengi tutaongea nikija huko.”
MIMI: “Unakuja Dodoma?”
MARY: “Yes! Ninatarajia kuja jumamosi nitakucheki.”
MIMI: “Una mishe gani huku tena?”
MARY: “Nikija haya yote tutaongea, byee and takecare.”
Baada ya kuagana na Mary, nilibaki nikiyatafakari maneno yake. Nilihisi hatia kubwa kwa kumkosea, na nikaamua kuwa si sahihi kuendelea kumfanyia hivyo. Pia, mawazo yangu yalizidi kuzunguka huku nikijiuliza, 'Mary anakuja kufanya nini Dodoma?'"
Hilda tulikuwa tunawasiliana sana na habari kubwa alinambia kwamba Asmah ananiuizia sana mpaka anapata wasiwasi juu ya mahusiano yetu. Hilda hakuishia hapo, alisema Asmah kama anachanganyikiwa juu yangu, hivyo akanishauri nimtafute maana anamsumbua sana.
Mimi nilijua Asmah ananitafuta sababu ya lile jambo la sikuile usiku pale kwake wala sio kitu kingine. Suala la kumtafuta kwasasa halikuwa kipaumbele changu, hivyo nilijisemea nikirudi Dar nitamtafuta, lakini sio sasa.
****
Jumamosi asubuhi, Mary alinipigia simu kunijulisha kuwa yuko njiani kuelekea airport, na alisema kwamba kufikia saa 7 mchana atakuwa amefika Dodoma. Nilimkaribisha kwa furaha na kumwambia aniambie akifika mjini ili niweze kumfuata.
Jumamosi ilikuwa siku yenye shughuli nyingi sana kwangu, kiasi kwamba nilisahau kabisa kuhusu miadi yangu na Mary. Aliniambia angetua Dodoma saa 7 mchana, lakini nilipokumbuka ilikuwa tayari saa 9 kasoro. Simu yangu ilikuwa ofisini kwa Sanchi, na nikajiwazia, 'Hakika Mary atakuwa amepiga simu mpaka akachoka.'"
Baada ya kuchukua simu, kweli nikakutana na missed call nyingi kutoka kwake. Ikabidi nimpigie haraka ili kujua alipo. Alipopokea, aliniambia kuwa kuna mtu tayari amekuja kumwona mara tu baada ya kuona sipokei simu zake.
Mary alisema kuwa kufikia saa 12 jioni atakuwa amemaliza mazungumzo na huyo mtu, na atanipigia ili tuonane. Nilijiuliza, Mary ana shughuli gani huku, na ameja kuonana na nani? Maana ni mgeni na hajawahi kufika Dodoma.
Niliendelea na ratiba zangu, na kwa mara nyingine nikaacha simu ofisini kwa Sanchi. Nilikuwa naiweka huko kwa sababu sikuwa naitumia, na hakuna mtu wa kunitafuta kwani namba yangu ni mpya. Muda wa mapumziko, kama wakati wa kula lunch, ndiyo nilikuwa nikiichukua.
Kuhusu wateja, nilikuwa nawasiliana nao kupitia simu ndogo na nilisajili laini maalum kwa ajili ya hili. Sikutaka kuchanganya mambo ya kazi na mambo yangu binafsi, ndiyo maana nikasajili laini maalum kwa matumizi ya ofisi.
Saa 10 jioni, nilitoka kwenda dukani kwa ajili ya kupiga mahesabu na kuangalia namba za lubricants ambazo zimeisha, ili nifanye kuagiza mzigo mwingine kutoka Dar es Salaam. Supplier alikuwa akisubiri odda yangu ili aanze kuandaa mzigo na autume mapema.
Ilikuwa saa 12 kasoro tayari, nikasema ni bora nirudi haraka kwani Mary maana alisema atanicheki muda huu. Baada ya kurudi ofisini, Sanchi alitoka nje na akaanza kuniita. Aliniambia simu yangu ilikuwa inaita sana, kuangalia ni Mary alikuwa amepiga mara 5, nikampigia haraka.
MIMI: “Hello mummy ushamaliza?”
MARY: “Yeah muda mrefu hupokei simu.”
MIMI: “Ulisema saa 12 utanicheki.”
MARY: “Nilisema kufikia saa 12 nitakuwa tayari, hivyo muda wowote ningekujulisha.”
MIMI: “Ok! tulishindwa kuelewana haya nambie ulipo.”
MARY: “Tukutane Golden fork huyu mtu ananiacha hapo, nataka nile kabisa nahisi njaa.”
MIMI: “Sawa mummy nitakukuta hapo.”
Baada ya kukata simu nilijisemea ‘Mary anakwenda Golden Fork anataka kunitia gharama tu.’ Kwa upande wa pili Sanchi alikuwa akiniangalia sana, uvumilivu ulimshinda akaanza kuongea pale;
SANCHI: “Wacha wee! Naona una appointment na mrembo, amekupigia sana simu.”
MIMI: “Appointment gani na hali hii niliyonayo unaona ina make sense?”
SANCHI: “Kwani si unakwenda kuoga na kujiandaa kwanza, uzuri hapa bafu zipo kazi kwako.”
Niliamua kupotezesha mada;
MIMI: “Vipi leo si unakuja kulala kwangu.?”
SANCHI: “Hahahaa! Usinichekeshe mie kulala tu.?”
MIMI: “Kwani umesikia neno lingine zaidi ya kulala?”
SANCHI: “Najua huwezi kuniacha salama shenzi zako.”
MIMI: “Haya bhana acha mimi nikukimbie mama, tutaonana jumatatu.”
SANCHI: “Jumatatu tutaongea kuhusu simu nataka ninue iphone kama yako, utanipa connection.”
MIMI: “Imeisha hio hata bure utapata usiwe na wasiwasi.”
SANCHI: “Toka zako wahi ulikopigiwa simu.”
Nilikuwa nimechafuka sana oil zimegandia kwenye jeans, na mikononi. Kurudi geto niliona mbali, hivyo niliishia kunawa vizuri na kujipukuta ili niwahi kuonana naye maana alikuwa keshapiga simu kwamba amefika ananisubiri mimi tu.
Nilichukua bodaboda mpaka Golden fork na nilianza kuingia huku nikizungusha macho yangu vizuri na nilimuona amekaa pembeni akinitizama na ile kusogea aliinuka akaja akanikumbatia.
“Wow Insider I have missed you.”
Watu waliokuwa maeneo yale walikuwa wakituangalia sana maana Mary alikuwa kapendeza ukizingatia ni mzuri. Kama mnavojua Dodoma hakuna warembo wakali kabisa, kwa mrembo kama Mary akija maeneo haya anakuwa kivutio kwa wenyeji.
Tulianza story pale na bila kuchelewa mhudumu alikuja kutusikiliza Mary aliagiza chips na kuku, mimi nikaagiza juice. Mary alinikata jicho kali sana;
MARY: “You can’t be serious muda huu umekula wapi?”
MIMI: “Usijali mimi nitaenda kula home juice inanitosha.”
MARY: “No! Agiza chakula.”
Muda huu dada alikuwa akitabasamu tu;
MIMI: “Dada niletee wali mweupe na makange ya kuku local.”
“Sawa bossy.” dada akaondoka,
MARY: “Insider umepungua sana, halafu umepauka shida ni nini?”
MIMI: “Ni maisha mama halafu mimi ni mtoto wa kiume. Embu niambie huku unamishe gani, halafu ulikuwa na nani?”
MARY: “Huku nina ishu za research ndiyo zimenileta, mtu niliye onana naye atanisaidia kwenye hili.”
MIMI: “Ulikuwa na plan za kuja huku au baada ya kusikia niko huku ndo ukaamua uje?”
MARY: “Actually nilikuwa nina mipango toka muda mrefu.”
MIMI: “Sawa, na itachukua muda gani?”
MARY: “Itategemea makadirio ni week mbili mpaka tatu.”
MIMI: “Sawa na utafikia wapi? Nakuona na bag.”
MARY: “Nafikia kwako, tukimaliza kula tunaenda wote.”
MIMI: “What? Sikuelewi huwezi kuja kulala kwangu, kwanza naishi geto moja, halafu sio mazingira mazuri ya kulala mwanamke, acha nikitafutie hotel au lodge nzuri uwe unalala.”
MARY: “Hizo gharama ni kubwa sana…”
Nikamkatisha;
MIMI: “Kuna ndugu yangu yupo huku ni mwanamke kama wewe hana shida utalala kwake.”
MARY: “Insider nisikilize kwa makini, mimi sitaki kwenda sehemu nyingine zaidi yako. Kama hutaki nije kwako nambie sitaki ijulikane moja, lakini sio kunipeleka sehem ambazo sizijui.”
Nilikuwa mpole ghafla hata sikuwa na usemi tena, ilinibidi nikubaliane na matokeo. Niliwaza kule gheto naishi kisera sana kuna godoro la 4x6 halafu liko chini. Nilijisemea pale, ‘mtoto kautaka acha niende nae tukifika huko itajulikana’.
TO BE CONTINUED
Kwani wachaga tumekukosea nini mjomba?Wanawake wa kichaga wana D ya mapenzi mzee baba...
Wachache sana wapo romantic wa kuhesabu mno...
Shule nimeanza October 2023.Oya insider, kipindi uko dom ulikuw likizo au ulikuwa unasoma online?
Una maamuzi ya haraka ndio maana yanakugharimu sana
Nyingine isichelewe sana mzee hapo ulipoishia Pana mengi.Shule nimeanza October 2023.
Mr ShermanAsante kaka kwa kutukumbukaaa
Ni kweli, mshahara unaweza kuwa mkubwa, lakini utatosha vipi kulipa uhuru wangu?.
Kusajili kampuni natakiwa kuwa na kiasi gani? INSIDER MAN
Mkuu hii ni Kwa wanawake wengi, yaani akishaolewa anaanza dharau na mengine ambayo yanasababisha wanaume kuwaza plan BUkiwa unasoma utaona kama nilikuwa namkosea sana Mama J ila hamjui tu niliyovumilia. Mengi nilishayaandika nyuma, yeye ndo chanzo cha mimi kuanza kuchepuka.