Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 21,593
- 46,759
Story ishaanza kua ya Shigongo.
Una utunzi na mpangilio mzuri sana wa matukio mkuu.
Hongera sana.

Lie over lieSEASON 03
CHAPTER 3
CONTINUE:
MARY: “So, where are you taking me?”
MIMI: “Watch me…” huku nikitabasamu!
MARY: “Remember nilikuambia mzee yuko home.”
MIMI: “Najua, lakini kwani nikispend na wewe hata kwa lisaa moja ni kosa? Au hujanimiss kweli?”
MARY: “Nimekumiss sana, lakini tafadhali usiende mbali sana, sitakuwa na uwezo wa kurudi home kwa wakati. Nielewe, Insider, please.”
Nilisimamisha gari kwenye mchepuko wa barabara inayoelekea Upepo Garden, eneo hili lilikuwa na ukimya sana;
MIMI: “Naona huna hamu na mimi. Sio yule Mary ninaye-mjua. Anyway, I got this. Unaweza shuka na kwenda home kama unavyotaka.”
MARY: “Hapana baby, sikumanisha hivyo. Nimekumiss kweli, lakini pia niko period mwenzio. Naomba uelewe, mzee wangu anaumwa na mama hayupo kasafiri, Prisca yuko kwenye mitihani. I love you, Insider.”
MIMI: “Sasa, wakati ule tulipokuwa tunazungumza, mbona hukusema kama mzee ni mgonjwa? Do you really think nitakuamini?”
Mary alikuwa mpole ghafla, akaanza kuniangalia kwa macho ya mahaba, na hatimaye akaanza kunichezea ndevu.
MARY: “Baby, hadi ijumaa nitakuwa nimemaliza period, nitakupa unachotaka. Sawa baba?”
MIMI: “Sawa, wahi home. Bhasi tutawasiliana.”
MARY: “Hapana baby… hata hatujaongea umerudi lini, na mtoto sijamuona… camon.”
MIMI: “Nimerudi jana, na ukweli nimekumiss tangu niondoke kwenda South. Sijasex kabisa, yaani nina hamu kama zote. We, si unaona jinsi Kingdom ilivyo-arise baada ya kukuona?
MARY: “Ooh baby, kama utaridhia kufanya hivi na hali niliyonayo, twende, nikupe unachotaka.”
MIMI: “Hapana! Unajua siwezi kufanya hivyo. Maliza tu, tutaonana siku nyingine na thanks kwa kujali.”
Nilitoa simu nikaanza kumuonyesha picha za Aria, na Mary aliishia kutabasamu, huku akizitizama picha kwa makini.
MARY: “Waoh! She’s so beautiful. Unajua unanipa hamu, namimi nikuzalie mtoto? Insider, please, natamani pia kuwa na mtoto.”
MIMI: “Tutaongea kuhusu hili. Halafu mdogo wako Prisca akanipigia simu nikiwa na Jane, na kabla sijatoka kwenda South Africa aliomba tuonane.”
MARY: “Prisca anahisi sisi tuko kwenye mahusiano, kamwambia hadi mama eti mimi nimeiba mwanaume wake.”
MIMI: “Ndio, ni kweli umeiba mwanaume wake, lakini fanya iwe siri sana. Akija kujua ukweli, mtakuja ku-uana mle ndani na kunipa mimi matatizo.”
MARY: “Niko makini, umeniletea zawadi?”
MIMI: “Ukweli, sijakuletea zawadi, lakini ijumaa nitakupeleka shopping.”
Mary alioneka kufurahi sana kupita maelezo, na katika hali ya mzuka tukaanza kubadilishana mate kwa pupa. Baada ya dakika chache kupita, akanigeukia na kuniambia nimrudishe kwao, muda ulikuwa umeenda. Nikageuza gari na kumshusha pale Shoppers, na baada ya kushuka akaniangalia tena akitabasamu, kisha akageuka na kuanza kuembea kuelekea nyumbani kwao, nami nikaendelea na safari ya kurejea kwetu, moyo wangu ukiwa mwepesi.
Nilipofika home, nilimkuta Junior sebleni ameketi kwa utulivu, macho yote yako kwenye katuni. Nikamnyanyua juu mabegani kwa furaha, tukaelekea chumbani na kuanza mchezo wetu wa “mieleka.” Huu ni moja ya michezo tunayopenda kucheza tukiwa pamoja, na kila mara huupokea kwa bashasha kubwa.
Baada ya nusu saa kupita wife alirudi home na alionekana kuchoka sana maana alikuwa kwenye mitihani. Nilimpa pole ya mitihani, lakini macho yake yakatua kitandani, kwani mashuka yote yalikuwa yametanduka na kufumuka kutokana na mieleka ya Junior na mimi. Alianza kuwaka pale kwanini nacheza na mtoto kitandani? Na mimi niliamua kumuacha na kwenda sebleni.
Nilipoingia sebleni, nilimkuta sister amekaa kwenye kochi, akikatakata apple vipande vidogo taratibu. Aliponiona, akaniangalia kwa jicho la upole na akaishia kutabasamu.
SISTER: “Mdogo wangu una heka-heka sana, nimekunyooshea mikono asee!”
Nikabaki nacheka,
MIMI: “Kwa nini dada yangu unasema hivyo?”
SISTER: “Napata lawama, ndomana nasema hivyo.”
Nikakaa karibu naye,
MIMI: “Si kweli, huoni nimewahi kurudi leo? Pia kila Jumapili lazima nitoke na familia tupumzike sehemu fulani. Ni haya mambo ya Iryn yalinifanya kuwa busy.”
SISTER: “Tafuta hela, sawa, lakini kumbuka pia kukaa na familia, hasa mtoto.”
MIMI: “Tuachane na hayo, lakini hebu niambie kuhusu suala la jana ulikuwa serious? Ulinikataza nisiongee na mzee kuhusu Iryn. Ulikuwa unamaanisha kweli?”
SISTER: “Au unafikiri mimba inanichanganya mdogo wangu? Nakuambia ukweli. Tafadhali naomba nielewe… na kuna siku utanielewa kwanini nasema hivi.”
MIMI: “Haiko sawa, mimi naona ningemuambia baba kwanza kabla ya mama . Lakini ukiniambia nisubiri sawa, nitafikiria. Ila dada, hili suala limekaa kiume sana, mama nikimwambia ataingia presha bure. Embu think vizuri tena.”
Wakati mazungumzo yetu yakiendelea, ghafla mama J akaja pale seblen huku amembeba junior na maongezi yetu ndo kuishia hapa;
SISTER: “Insider… mdogo wangu, mimi na wewe njia yetu ni moja. Hatuna utofauti. Niamini dada yako.”
Baada ya kusema hivyo, dada alinyanyuka taratibu na kuelekea jikoni. Aliniaga kwa sauti ya upole kwamba anakwenda kumsaidia wife kupika, akaniacha nikiwa nimebaki nikitafakari kama mtu aliyeachwa gizani.
Nilikaa kimya kwa sekunde chache, nikijiambia moyoni: “Hii mimba kweli inamchanganya dada yangu… ndiyo maana anaongea vitu visivyoeleweka.” Lakini hata hivyo, maneno yake yalibaki yakizunguka kichwani. Nilipiga moyo konde na kujisemea: “Zambia nitaenda kwa Mzee, siwezi kumzungumza na mama hili suala kabla yake.“
Wakati huo nikiwa katikati ya mgongano wa nafsi, simu yangu ghafla ikaanza kulia juu ya meza. Niliinyanyua haraka, macho yangu yakakutana na jina lililoandikwa kwenye skrini, Iryn. Bila kusita, niliibeba simu na kuelekea moja kwa moja chumbani, ili niweze kuongea naye pamoja na faragha.
MIMI: “Mummy, I told you not to call me at this time of night.”
IRYN: “Camon… Aria anataka kukuona baba yake. Analialia, sasa angalia mwanao… umemuona, kanyamaza. You don’t like?”
Nilibaki kimya kwa muda mfupi, nikahisi kama sina namna ya kukwepa na nilikuwa mpole ghafla. Nilitazama kwenye skrini, na kweli Aria alionekana akitabasamu. Tabasamu lile dogo la mtoto liliingia moja kwa moja moyoni mwangu, na nikajikuta nikitabasamu pia.
MIMI: “Usimzoeshe kamera za simu mtoto, bado mdogo sana.”
IRYN: “Ni wewe tu huwa nakupigia video call, ili umuone binti yako. Sio mtu mwingine.”
MIMI: “Naona unazidi kunenepa mama mtoto… na umependeza sana.”
Akatabasamu kwa aibu, kisha akasema;
IRYN: “I hate this body, after three months nitaanza gym.”
MIMI: “Nakupenda jinsi ulivyo… hujui tu.”
Alicheka kwa upole, kisha mazungumzo yetu yakaendelea kubadilika na kubwa ilikuwa kuhusu ugeni anaousubiria. Moyoni nilikuwa na shauku kubwa kujua siri ya ugeni huo ni nini hasa, lakini kwa sauti ya utani alisema hata yeye mwenyewe hajui kwa undani.
Baada ya maongezi marefu, Iryn alipeleka simu kwa Momo, bibi yake mpendwa ili nimsalimie. Nilimsalimia kwa heshima na nidhamu, kisha nikapata nafasi ya kumsalimia mdogo wake Samantha.
Baada ya hapo, mazungumzo yetu yakafikia kikomo na nikamuomba kwamba usiku asipige simu, badala yake atume meseji ili tuchat au nitoke nje ili tuongee, lasivyo ataniweka kwenye matatizo na mama J ambaye hatutaki ajue chochote.
Baada ya kukata simu haikuchukua muda Iryn alinitumia video za mwanangu Aria, pamoja na picha zake. Wakati nikiendelea kumwangalia Aria akicheza na vidole vyake vidogo, nikajihisi kuchanganyikiwa zaidi. Upendo kwa mtoto wangu uliniganda kifuani, lakini pembeni yake kulikuwa na ule mzigo wa maamuzi magumu na siri nzito zinazozunguka kwenye nafsi yangu.
Nilijikuta nikizama kwenye mawazo mazito kuhusu siri inayokua taratibu kati yangu na Iryn. Nilijua siku moja itajulikana, maana hakuna marefu yasiyo na ncha.
Nikajiuliza kwa kina: “Itakuwaje Mama J akiona ukimya wa Iryn? Akijaribu kumpigia simu asimpate, au hata WhatsApp akose majibu, bila shaka atanigeukia mimi. Ataanza kuniuliza maswali kuhusu Iryn na mtoto, kisha atataka kuona picha za mtoto au aombe namba anayotumia sasa.
Lakini je, nikimwambia sina picha hizo wala namba ya mawasiliano, ataamini kweli? Hilo haliingii akilini. Ni wazi atashangaa kwa sababu mimi na yeye ni marafiki wa karibu, na zaidi ya hapo nafanyia kazi kampuni yake.
Nikijaribu kusema sina mawasiliano naye, jibu hilo halitakuwa na uzito wowote wa kuaminika. Moja kwa moja ataona kama nimeficha kitu, na hapo nitakuwa nimewasha taa ya kijani ya kuthibitisha mashaka yake kuwa mtoto huyo huenda ni wangu.”
Niliwaza sana, nikagundua kuwa hili jambo ni serious na si jambo la kupuuza hata kidogo. Nikilisukumia pembeni, siku ikifika itakuwa too late na madhara yake hayatakuwa mepesi kuyaziba.
Nilijiambia wazi kuwa nahitaji kuwa smart sana katika kulishughulikia. Hakuna nafasi ya uzembe, na sitakiwi kufanya makosa. Wife wangu hapaswi kujua chochote mpaka siku taarifa kamili zitakapotolewa. Nikiteleza tu kidogo nitaonekana mzembe, sitachukuliwa kwa uzito, na mbaya zaidi, kila mtu atanicheka.
Nilijikuta nikikuna kichwa sana, nikitafuta mbinu ya busara ya kutumia ili wife wangu asijue chochote kabla mipango yangu haijakamilika. Nilijua wazi kuwa kosa dogo tu lingeweza kuvuruga kila kitu nilichopanga.
Nikawaza kwa kina: “Labda njia pekee ya kunusurika ni kumwambia wife kuwa nimeacha kazi kwa Iryn, au kumdanganya kuwa ofisi imefungwa kabisa. Hapo ndipo nitakuwa salama. Ni bora nimdanganye kwa namna hiyo, maana hata siku akija kuulizia kuhusu Iryn, nitaweza kusimama kwa ujasiri bila hofu. Zaidi ya hapo, natakiwa kubadili jina lake kwenye simu yangu, nimwite kwa jina la binti yangu “Aria” ili mambo yote yaende bila shaka yoyote.”
Nikajiuliza tena kwa hofu: “Je, kweli nitadumu kuficha siri hii? Ndio, nitamwita Aria, nitamwambia ofisi imefungwa… lakini itakuwaje siku Mama J akija kusikia habari hizi kutoka kwa mtu mwingine? Au moja ya mtu wangu wa karibu akiamua kusnitch?.”
Nikakumbuka Lucy ana mawasiliano na mama J, hivyo sinabudi kumpanga mapema kuhusu hili, kabla wife hajaanza ujasusi wake.
****
Asubuhi baada ya kuamka nilipiga simu kwa kaka yangu ambaye ni Advocate na pia ni Lecturer pale UDSM. Baada ya mazungumzo mafupi, aliniambia nifike chuoni, kitivo, majira ya saa 9 mchana kwa ajili ya kuongea naye kwa undani zaidi.
Wakati bado nipo kwenye mawasiliano na bro, simu ya Hilda iliingia upande wa pili. Nilipomaliza maongezi, nilikuta ujumbe wake ukiningojea, uliosomeka:
“Good morning bossy, are you coming today?”
Nikajibu kwa haraka, nikiwa na tabasamu dogo usoni:
“Yes mummy, am on my way.”
Wakati nikiwa mezani nikipata breakfast, Sister alifika na kunipa taarifa mpya kabisa. Aliniambia kuwa ameahirisha safari yake ya Ijumaa na sasa ataondoka Jumapili pamoja na mama J. Nilishituka, nikajiuliza kimoyomoyo “Imekuaje tena aondoke na wife? Wameongea nini mpaka wakafikia maamuzi haya?”
Sister akanieleza kwa utulivu kuwa wife alihitaji kupumzika baada ya mitihani yake na akamshawishi waende wote Arusha, kwa sababu hajawahi kufika huko. Niliposikia hivyo, sikuwa na pingamizi. Ukweli ni kwamba wife hajawahi kumtembelea dada yangu kule Arusha, kwa hiyo ilikuwa nafasi nzuri kwake.
Lakini moyoni mwangu nilijikuta nikicheka kimya kimya. Kwa upande wangu nilifurahia, nilihisi upepo wa uhuru ukianza kunipuliza kwa mbali, niliona ni muda wa kuwa peke yangu bila vikwazo. Kwa upande mwingine, nilimwambia Sister kuwa siku ya Jumamosi ningependa tutoke wote twende sehemu nzuri ya kutulia, tupumzike pamoja na tufurahie chakula cha usiku.
Kabla ya kuondoka nilikumbuka kumtadhaharisha kuwa makini sana na simu yake, ahakikishe ipo mikononi mwake muda wote, maana akijisahau akaiacha kwa wife, anaweza kugundua mawasiliano yake na Iryn pamoja na zile picha walizopiga wote.
Sister kwa upande wake alinihakikishia kwamba yuko makini sana na alitoa wasiwasi juu ya hili. Baada ya kunihakikishia hivyo, akanigeukia na kuniuliza hali ya maelewano yetu kwa sasa.
Nilimsogelea taratibu, nikamnong’oneza kwa sauti ya chini huku nikitabasamu, “Jana nimeichapa usiku kucha.” Kisha nikaondoka nikimuacha akicheka kwa kicheko cha kiutu uzima, kwani hakutegema kusikia maneno haya kutoka kwangu.
Nikiwa njiani kuelekea ofisini, simu ya Asmah iliingia. Bila kusita niliipokea na kuweka loudspeaker. Baada ya salamu fupi, Asmah alianza kulalamika kwa sauti yenye ukali wa maumivu kwamba nimemchunia kwa muda mrefu. Nilijitahidi kumtuliza, nikimwambia kwa upole kwamba nilihitaji muda wa kutulia kipindi niko South, kisha nikampa ahadi ya kumuona baadaye ili tuzungumze kwa utulivu.
Kumbukumbu zangu zikanirudisha nyuma, kabla sijaondoka kwenda South Africa. Alikuwa amenidokeza kuhusu suala lake la kuacha kazi na kwenda kusoma. Wakati huo nilimsihi sana asubiri kwanza Iryn ajifungue ndipo ampe taarifa hizo. Niliona ni jambo la busara, maana singependa kumweka Iryn kwenye hali ya msongo wa mawazo katika kipindi chake cha ujauzito.
Kwa sasa niliona umuhimu mkubwa wa kukutana na Asmah, ili tupate muhafaka wa jambo hili. Nilijua wazi kuwa hatua zingine za kuchukua zingetegemea maongezi hayo, na ndani yangu nilitamani sana kuhakikisha kuwa hakuna presha yoyote inayoweza kumgusa Iryn hasa kipindi hiki anacho-hitaji utulivu.
Kituo changu cha kwanza kilikuwa Masaki ofisini kwa kaka Allen, maana sikuweza kuacha bila kutoa shukrani za dhati kwa msaada wake katika kampuni kipindi chote sipo. Nilipofika pale, baada ya kumuulizia pale reception, niliambiwa yupo, na nikatulia palepale nikimsubiri baada ya kumpigia simu.
Kwa upande wake, alishangazwa sana na ugeni wangu pale ofisini kwake. Sikumpa taarifa yoyote kabla, kwani nilitaka iwe surprise. Ndani ya dakika kumi tu, alifika pale reception, tulisalimiana kwa furaha na, kisha tukapanda hadi ghorofani juu kabisa kuongea kwa faragha na kwa utulivu.
Maongezi yalianza kwa upande wa South Africa, ambapo Allen alikuwa na maswali mengi sana. Kwanza kabisa, alitamani sana kujua maendeleo ya mtoto pamoja na mama yake. Pili, alitaka kujua taswira walizoonesha ndugu zake baada ya kukutana huko South Africa.
Nilimweleza kwa uwazi kuwa sina tatizo na ndugu zake, ila tatizo kubwa linaonekana kuwa upande wa mama yake mkubwa. Nilimueleza jinsi tulivyokuwa na kikao cha kina, na maswali aliyoniuliza kuhusu mustakabali wangu na Iryn.
Allen kwa upande wake alisema kwamba mama yake mkubwa amelichukulia hili kama jambo la mzazi, na alikuwa sahihi kwa upande wake, maana anaumia kuona binti yake akizalishwa bila kuwa na uhakika wa ndoa. Aliendelea kusisitiza kwamba ni Iryn pekee anayehitajika kuwekeza juhudi kuhakikisha jambo hili linaeleweka vizuri na ndugu zake, ili kuwe na ufafanuzi na kusawazisha sintofahamu zote zilizopo.
Baada ya maongezi marefu, nilimshukuru Allen kwa kazi yote aliyoifanya ya kusaidia kampuni kipindi nipo mbali. Alinitoa wasiwasi kwa unyenyekevu, akisema kwamba yeye ni NED wa kampuni na hivyo ni moja ya majukumu yake kuhakikisha mambo yanaenda sawa.
Wakati huo huo, simu ya Hilda iliingia. Bila kusita, niliipokea ili kumsikiza, nijue alitaka nini. Hilda hakuwa na point ya msingi, hivyo nilimwambia kuwa ndani ya nusu saa nitakuwa ofisini, na tutapata muda wa kuongea vizuri nikifika pale.
ALLEN: “Huyo ni Hilda?”
MIMI: “Yeah, ni yeye. Hivi mlifikia wapi?”
ALLEN: “Huyo mrembo nimeamua kunyoosha mikono, nimetumia kila mbinu. Ananambia ana mtu wake anampenda, hawezi kumuacha.”
MIMI: “Unajua wewe unataka kumla, nafikiri kashtukia hili.”
ALLEN: “Hapana! Nataka awe mchepuko wangu. Nilimwambia nataka nimpangie nyumba, kila kitu nitampatia. Nikimpata yule, lazima nitulie na mchepuko 1 tu, Hilda atanitosha kabisa.”
MIMI: “Hadi hizo offa amezikataa? Ni wanawake wachache sana wenye jeuri hii.”
ALLEN: “Amini kaka, mnamlipa mshahara mzuri au ana sponsor anayempa jeuri hapa mjini.”
MIMI: “Kuhusu mshahara, nakumbuka nilikwambia, ila kwasasa amekuwa promoted, ataongezewa na atagonga 2M. Ila kuhusu sponsor sidhani kwakweli, nina informer wangu ambaye huwa ananipa taarifa za kila mmoja pale ofisini. Hilda amenihakikishia sana kuwa hana mtu kwa sasa, labda anidanganye.”
ALLEN: “Hilda anakupenda, Insider. Naamini utanikatalia, ila pokea ukweli huu. Na hii ni moja ya sababu kwanini ananisumbua, ni kwamba ana interest na wewe.”
MIMI: “Siwezi kukubali au kupinga hilo, ila tambua Hilda ni mshikaji wangu sana na tunapatana, tuko close sana. Hili hili lisikutoe kwenye malengo yako kaka.”
ALLEN: “Ni vile, huna interest naye, ila anakupenda sana, amini hivyo.”
MIMI: “Hilda ningekupa assist fresh kabisa, ila sitaki kuja kugombana naye baadaye, mkija kuachana au akijua wewe una mke, nitakuwa nimemkatili sana. Ndomana, nakuacha upambane mwenyewe hata mkizinguana, mimi nakuwa sihusiki kabisa.”
Tuliishia kwa kicheko pale, nami nikamwambia kuwa naondoka kwenda ofisini. Nikamkumbusha tena anitumie account yake ya Bank ili niweze kufanya malipo yote kwa urahisi.
Baada ya kufika ofisini, pale reception alikuwepo Nollie. Nilienda kumsalimia na kumtania kidogo, maana si muongeaji sana. Alinipa pole ya safari, na nikaendelea kuwasalimia wafanyakazi wengine ofisi kwa ofisi.
Baada ya kumaliza, nilikwenda ofisini kwangu ili kuendelea na majukumu mengine. Nilipofungua mlango, macho yetu yalikutana na Hilda, na aliishia kutabasamu. Nikapita kuingia na kukaa kwenye sofa, nikimwangalia kwa makini zaidi;
MIMI: “Nambie, assistant wangu, nakuona unazidi kuwa mrembo.”
HILDA: “Insider, kwa kunipamba unajua sana. Mimi niko vilevile, ninanuka shida kila kona.”
MIMI: “That can’t be you.”
HILDA: “Trust me, then why kila mtu anakulalamikia, hupokei simu zao?”
MIMI: “Nani hao tena?”
HILDA: “Asmah na Sumaiya. Huyu Sumaiya jana nilisahau kukwambia, anaomba sana muonane, amesema ni muhimu. Hata simu zake hupokei analalamika.”
MIMI: “We, si unajua movie nzima? Asmah nimewasiliana naye, ila huyo b*tch siwezi mtafuta, alinieletea dharau.”
Hilda alinyanyuka kutoka kwenye kiti chake na kuja kukaa karibu nami kwenye sofa, akionekana mchangamfu na mwenye furaha usoni.
HILDA: “Insider, mama yangu aliumwa sana hapa katikati ukiwa haupo, nimefulia sana.”
MIMI: “Pole sana. Kwanini hujasema hapo awali, mummy? Unajua fika utaratibu wa ofisi.”
HILDA: “Simu zako zilikuwa hupokei ukiwa South, na jana nilijua utarudi, basi tuongee hili.”
MIMI: “Andaa gharama zote ulizotumia. Ofisi itakurefund, na kicoba chetu kitakupa pesa ya pole, hili niachie mimi, meneja wako. Pia, umefanya kazi kubwa sana, hata Iryn alifurahi. Kuanzia mwezi huu utapandishwa mshahara tena.”
Hilda aliniangalia machoni na tabasamu lake lilionyesha furaha tele,
HILDA: “Insider, ahsante sana. Nataka siku tuende wote home, ukamjue na mama yangu.”
MIMI: “Usijali, Hilda. Naomba invoice zote, pamoja na ile ya ndugu zetu wa Website development, ili nianze kufanya malipo yote.”
HILDA: “One more thing… sijasahau lunch yangu.”
Tuliendelea kupiga story na Hilda huku tukicheka, na kubwa nilikuwa na msukumo wa moyoni kuhusu kunidanganya kuwa yuko single, jambo ambalo sikuelewa kama kweli. Hilda aliendelea kushikilia msimamo wake kwamba yuko single kwa sasa na hahitaji mwanaume, kwani ana mambo mengi ya kupanga na kuweka sawa katika maisha yake.
Hilda alinishirikisha story yake kwa kina jinsi ambavyo amekuwa akipitia majaribu na kipindi mgumu wakati wa kazi zake za nyuma, kabla ya kuajiriwa na kampuni yetu. Alieleza kuwa baadhi ya waajiri na maboss walikuwa wakimtaka au kumtamani kimapenzi, jambo ambalo lilimlazimu kuacha baadhi ya kazi zake. Kwa hivyo, alifichua kuwa kabla ya kuja kwetu, alifanya kazi katika moja ya benki kubwa hapa nchini na kampuni nyingine.
Kwa upande wangu, kipindi Asmah anapitia CV yake, hata sikuwa na habari naye wala kupitia taarifa zake, zaidi nilimuachia Asmah amfanyie vetting pamoja na interview.
Baada ya kutoka lunch, nilipigiwa simu na mama Janeth. Aliomba kwa moyo mkunjufu nimsaidie kuwapeleka Airport wageni wake. Nilimuaga Hilda, kisha haraka nikachukua njia ya kwenda nyumbani kwa mama.
Nilipofika pale, tuwakuta mama na wageni wake wakiwa nje. Kabla hata sijasalimia mama, alianza kuongea mara moja:
MAMA: “Insider mwanangu, sorry nimekutoa kwenye majukumu yako.”
MIMI: “Mama, usijali.”
Baada ya salamu fupi, niliwasalimia wageni wote. Mama alifanya utambulisho mfupi kwa ndugu zake wote, ambapo jumla walikuwa wanne:
MAMA: “Hawa ni wageni wangu, walikuwa Zanzibar kikazi, wakaamua kuja kunisalimia. Leo wanaondoka na ndege ya saa 11 jioni. Naomba uniasaidie kuwapeleka Airport.”
MIMI: “Suala dogo hili, naomba tuanze kupanga mabag yao kwenye gari, maana muda umeenda sana.”
MAMA: “Kila kitu kiko sawa. Mtaondoka na ile Audi, maana gari yako ni ndogo isingetosha.”
MIMI: “Na kweli, isingetosha.”
Tulianza safari kuelekea Airport, nikitumia barabara ya Alli Hassan kuelekea Posta. Wakati wa safari, nilikuwa nikipiga sana story na wageni hao wazungu, tukicheka na hadi tulipofika Terminal 3. Kabla hata hatujaanza kutoa mabag, waliomba tupige picha ya pamoja kama ukumbusho, na tulipata mtu mmoja aliyejitolea kutusaidia kupiga picha.
Baada ya hapo, niliwasaidia kukokota mabag yao hadi ndani departure side. Niliwaaga pale na waliishia kunishukuru kwa moyo wote, na mimi nikawatakia safari njema. Wakati naelekea parking ili niondoke nilitoa simu na kumpigia mama kumpa taarifa ya kuwafikisha wageni salama. Kisha, nikamwambia gari yake nitampelekea siku nyingine, lakini yeye akasema niendelee kuitumia, kwani ni muda mrefu haijatumiwa.
Muda ulikuwa umeenda sana, saa yangu ya mkononi ilikuwa ikionesha 10 kasoro za jioni, na nilikuwa na appointment na Advocate. Njiani, nikirejea kwa gari, alipiga simu na tulifanya maongezi mafupi na tukakubaliana kukutana saa 10 kamili, nitamkuta akinisubiri pale UDASA.
Nilitoka Terminal 3 kwa spidi kali sana kuelekea eneo la tukio. Njiani niliendesha kwa fujo na kwa nguvu kidogo, kwa sababu barabara ilikuwa inatengenezwa. Nilifika UDASA, nikiwa nimechelewa kama dakika 15, na Wakili alikuwa akinisubiri pale.
Baada ya kuonana, tulisalimiana kwani ilikuwa imepita muda tangu tukutane mara ya mwisho. Kisha tulianza mazungumzo yetu ya maisha kwa ujumla, harakati zetu na shughuli za kila siku, na hatimaye tukafika kwenye mada iliyoleta tukio letu pale.
Nilianza kumpa mkasa wote kuhusu kampuni ambayo imeporwa na wahuni na tuko kwenye harakati za kuirudisha kwenye umiliki halali. Nilimpa mkasa mzima kuhusu hii kampuni tangu ianzishwe na inajishughulisha na nini.
Baada ya kumaliza kumsimulia, wakili alianza kuongea pamoja na kuniuliza maswali. Kwanza alitaka kujua kama tuna vielelezo vyote vya msingi kama nyaraka za usajili, mkataba/Memorandum, na kumbukumbu za maamuzi ya bodi. Nilichukua faili niliyokuwa nimebeba kwa gari, nikampa na alinza kukagua taratibu, akibaki kimya kwa muda bila kunisemesha.
ADVOCATE: “Kwa maelezo yako na nyaraka hizi, kuna nafasi kubwa ya kushinda kesi hii. Hata hivyo, lazima tuwe makini sana. Hawa watu waliopora kampuni si wa kawaida wanaonekana kuwa na nguvu na connection kubwa.”
MIMI: “Nakusikiliza Wakili.”
ADVOCATES: “Tutaanza kwa kuwasilisha pingamizi la awali, kuhakikisha mahakama inatambua kuwa umiliki uliohamishwa ni batili. Lakini kabla ya hapo, nataka ufanye jambo moja muhimu, nitahitaji majina ya mashahidi, hasa wale waliokuwepo wakati nyaraka za awali za kampuni zilisainiwa ambao ni Directors au shareholders.”
MIMI: “Director mkuu yupo ambaye ndo baba yake mzazi na ndo anamiliki hisa nyingi, Iryn mwenyewe ni moja ya shareholders, kuhusu director mwingine kama yupo atapatikana tu hakuna shida.”
ADVOCATE: “Kama baba yake yupo hii kesi imeisha ila sasa nakupa kazi ya kufanya mdogo wangu but you have to be very careful, kwanza naomba kukuuliza.”
MIMI: “Sawa uliza tu.”
ADVOCATE: “Je, uko tayari kwa lolote litakalotokea? Kwa maana vita ya kurudisha kampuni hii sio tu ya kisheria, ni pia ya kisaikolojia na unaenda weka maisha yako rehani.”
Sikutegemea kusikia haya maneno kutoka kwake, nilikaa kimya kwa sekunde chache kisha nikamwambia,
MIMI: “Niko tayari hii kampuni ni urithi wa mama mtoto wangu, katu sitokubali ipotee mikononi mwa wahuni. Pia, nataka nirudishe fadhila kwa mama mtoto kwa yote alionifanyia, nafikiri hii ndo itakuwa zawadi yangu kubwa kwake.”
Alipiga meza taratibu kwa vidole vyake, kama ishara ya mtu aliyeanza kutengeneza mkakati kichwani.
ADVOCATE: “Sasa, nakupa kazi ya kufanya, ila ifanye kwa umakini sana. Hakikisha hakuna mwingine anayejua kuhusu hili, na ikiwezekana tumia watu unaowaamini kabisa. Nahitaji kujua, kampuni hii ilifanyiwa uhuni lini? Na Directors wa sasa (fake) ni nani? BRELA na TRA inasomekaje? Hadi narudi next week, naamini utakuwa na taarifa zote muhimu. Mimi nitaondoka na file hili ili nianze kulichambua vizuri na taratibu.”
MIMI: “Assignment yako ni easy kwangu. Hatuwezi kuchelewa, soon nitakuwa na taarifa zote. Lakini nakuomba jambo-naomba hilo file ulilinde sana, maana ni original, na documents zote muhimu zipo humo.”
ADVOCATE: “Upo makini sana. Nitatoa copy, kisha tukionana nitakupa original, ondoa shaka kuhusu hili.”
MIMI: “Na vipi kuhusu gharama za hii kazi? Utacharge kiasi gani?.
ADVOCATE: “Next week tutaongea vizuri kuhusu hili, inabidi niende nikaongee na team yangu tushauriane kwanza. Next time tukavyoonana utakuja ofisini kwangu kwenye firm yetu.”
MIMI: “Ahsante sana kaka nakuamini sana juu ya hili naamini tutafanikisha.”
Ni maongezi yaliyochukua takribani masaa 2 na tuliagana kwa kukubaliana kukutana tena wiki ijayo. Mimi niliondoka kuelekea Mlimani City kwaajili ya kufanya shopping ya mahitaji ya nyumbani.
*****
Hatimaye, siku ya Jumamosi ilitimia. Saa 10 jioni tuliondoka nyumbani kwenda kutembea na kisha kupata chakula cha jioni katika moja ya hoteli nzuri. Kabla ya kuondoka, hatukuwa na makubaliano rasmi kuhusu hoteli tutakayokwenda, hivyo nilimwacha Sister achague. Alikuwa katika dilemma kati ya Whitesand Hotel na Ramada Hotel.
“Au niwapeleke Mediteranneo Hotel?” nilidokeza kwa upole.
“Ipo wapi hii hotel? Maana naisikia tu,” Sister aliuliza.
“Ipo Kawe, ni nzuri sana,” nilijibu, nikimjaribu kumtuliza na kumpa taarifa kidogo.
“Twende hio, hizi zingine at least nazijua, nishawahi fika.”
“Hata mimi sijawahi fika kwakweli,” Mama J alidakia kwa kicheko kidogo.
Nilielekea na kuelekeza gari kuelekea Mediterraneo Hotel, na ndani ya muda mfupi tulikuwa pale. Tulipokelewa kwa ukarimu mkubwa, kisha tukatafuta eneo zuri la kukaa, tukifurahia mandhari ya ajabu ya beach na bahari.
Kila mtu aliagiza chakula na kinywaji alichotaka. Wakati tukisubiri chakula, story za hapa na pale ziliendelea kwa furaha. Sister alianza kwa kudokeza kuhusu safari ya kesho pamoja na wife. Nilikuwa na hamu ya kujua wife atatumia muda gani huko Arusha. Wife alisema atakaa wiki moja tu kisha atarudi.
Kwa upande mwingine, Sister hakuridhika na mpango wa Mama J wa kukaa wiki moja tu. Alidai angalau akae wiki mbili, akizingatia kuwa hajawahi kabisa kutia mguu wake Arusha. Hii ilileta mjadala kidogo, lakini pia ilionyesha jinsi kila mmoja alikuwa na mtazamo wake juu ya hili.
Baada ya kumaliza mjadala wa muda wa safari hii, tulianza kuongea na wife kuhusu suala la Elena kwenda shule, kama tulivyokuwa tumemuahidi awali. Nilimwambia aanze process ya kutafuta dada mwingine wa nyumbani, ili kila kitu kiende kwa mpangilio mzuri.
Baada ya kumaliza maongezi marefu na ya kina, tuliomba Elena atupishe pamoja na Junior. Kisha tulianza mazungumzo yetu binafsi, tukijadili kuhusu sisi wawili. Dada kwa upande wake alikuwa ameshafanya kazi kubwa sana tayar, kilichobaki kwa upande wangu ni kucement mambo tu na kuhakikisha kila kitu kiko sawa.
Wife, kwa upande wake, aliongea mambo mengi sana ambayo hapendezwi nayo kutoka kwangu, baadhi yakiwemo mambo mnayajua tayari. Jambo lililotushtua ni pale alipoanza kusema kwamba amewaza sana, ni bora tukafunge ndoa, kwani hakuna tunachosubiri, na ikiwezekana hata kabla ya mwisho wa mwaka huu tuwe tumefanikisha hili.
MIMI: “Ndoa?” Niliuliza kwa mshangao.
Dada alinyamaza kimya, akiniangalia tu.
WIFE: “Ndiyo, kama kiuchumi kidogo tuko vizuri, hatuwezi kusema ni matajiri, ila tunaweza kuishi vizuri na Mungu ametubariki. Hivi Baba J, kinachofanya tuchelewe kufunga ndoa ni nini? Tumekuwa kwenye mahusiano zaidi ya miaka 5, tumetoka mbali sana tukianza zero. Ni kitu au kikwazo gani cha kutuzuia sasa? Nakuuliza.” Wife alikuwa mkali kidogo.
MIMI: “Mimi nina malengo, Mama J, ambayo mengi bado, na yote ni kwaajili ya familia yetu kwa ujumla.”
WIFE: “Malengo hayaishi, as long as tuko pamoja, tutayafanikisha. Kama kweli unanipenda mimi na mwanao, ninaamini hili jambo liko juu ya uwezo wako au maamuzi, wala si kuzingizia vitu vingine unless unamambo yako ya pembeni.”
MIMI: “We agreed kuhusu hili, tukakubaliana kuhusu ndoa hadi umalize masomo yako pamoja na kujenga nyumba yetu. Naona una breach makubaliano yetu.”
WIFE: “Hizo ni sababu ambazo hazina msingi. Mimi nimekubali ndoa, na haiwezi kunizuia kuendelea na masomo yangu. Suala la nyumba, embu tumuulize wifi. Wifi yangu, wewe wakati mnafunga ndoa mlikuwa mmejenga nyumba?”
Sister alitikisa kichwa kwa ishara ya hapana. Mama J akaendelea:
MAMA J: “Sasa, anachofanya Baba J kina make sense? Kwanini awe mgumu sana linapokuja suala la ndoa? Au kuna jambo linaendelea mimi silijui?”
Sister alivuta pumzi ndefu na kuanza kuzungumza:
SISTER: “Wifi yangu, nimechoka kuzungumza na Insider kuhusu ndoa. Kila mara anasema kuna mambo anaweka sawa kabla ya kuoa. Hata sisi tunatamani kuona ndoa yenu na tunasherehekea pamoja na familia zetu. Nakumbuka mimi na mume wangu tulifanya mipango yetu kwanza, tulipanga kila kitu pamoja hadi suala la ndoa. Naomba mkae chini pamoja mpange upya mipango hii, kwa sababu kisaikolojia mnaweza kuforce ndoa halafu ikawa tatizo zaidi.”
WIFE: “Insider ana mwanamke mwingine ndomana anashindwa kumake decision kwamba amuoe nani? ana mgogoro wa nafsi hapo alipo.”
Sister alinigeukia na kuniuliza;
SISTER: “Mdogo wangu, unadhani mipango yako yote itakuwa sawa lini? Ni hivi hamuwezi kuendelea kuishi kwa dizaini hii hata wazazi hawawezi waelewa.”
MIMI: “Mama J, maliza shule, tufunge ndoa. Hata mimi, kwa upande wangu, nitakuwa nimeweka kila kitu sawa.”
Maongezi yetu yalisimama ghafla pale Elena alipokuja akiwa na simu ya wife na kutupa taarifa kwamba mama yake anampigia sana. Mama J alichukua simu na kuondoka kidogo ili kuongea kwa faragha, huku sisi tukibaki kuendelea na mazungumzo yetu.
SISTER: “Insider, Mama J yuko sahihi. Ndoa ni assurance yake kwa sasa. Unajua sisi wanawake huwa tunahisi kama kuna something fishy kinaendelea.?”
MIMI: “Tatizo liko kwa dada zake. Nahisi wanampamba sana kuhusu ndoa, maana tulimaliza hili suala.”
SISTER: “Umefikia hatua nzuri ya mafanikio. Wanahisi unaweza kuacha mdogo wao na kuoa mwanamke mwingine, na asilimia kubwa ya wanaume wako hivi.”
MIMI: “Kwahiyo, dada yangu, nifanyaje? Nipe mbinu, jasusi wangu.”
SISTER: “Anza kuwa naye karibu sana, mfanyie surprise za kila aina kuonesha unampenda. Sidhani hata kama ndoa atakumbuka tena. Mwisho, kama utaweza, mpe mimba, ila make sure humuoi hadi ajue ukweli kuhusu wewe na Iryn.”
Sister aliongea mambo mengi ambayo yalikuwa na mantiki, wakati tukizungumza na sister, simu ya Mary ilikuwa ikiita ila nilikuwa nakausha. Alivyopiga mara ya tatu, nilitoka na kwenda pembeni kuipokea simu yake.
Mary alikuwa akiniuliza niko wapi, kwa kuwa alitamani sana tuonane, alisema amenimiss kweli. Nilimwambia nmetoka na familia, hivyo leo hatutaweza kuonana, lakini tutapata muda kesho, kwani wife atasafiri na tutakuwa na nafasi ya kutosha ya kuwa pamoja.
Mary alianza kunikumbusha ahadi niliyokuwa nimempa ya kumpeleka shopping. Nilimkumbusha kwamba yeye ndiye alizingua jana, ambayo mwishowe iliishia mimi kwenda kushinda na Jane. Mary hakuweza kuonana na mimi kwa sababu alikuwa kamsindikiza baba yake hospitali, hivyo alichelewa kurudi na kushindwa kutimiza ahadi ya kuonana.
Muda ulikuwa umekimbia sana, hivyo tuliondoka na kurudi home. Njiani, Junior alikuwa akitupa story zake na tulikuwa tukicheka sana hadi tulipofika. Baada ya kufika home, mimi niliendelea kukaa na sister pale sebleni, tukipiga story za mwisho-mwisho huku tukipanga mipango mingine ya pamoja.
Baada ya dakika 15, Mama J alikuja sebleni na aliniita chumbani mara moja, kisha akaondoka.
Sister alishtuka kumuona Mama J kwa hali ile na akasema:
“Something wrong, hujasahau kumbukumbu yoyote kutoka South Africa?”
Nilitikisa kichwa kuonyesha hapana na nikanyanyuka kuelekea chumbani.
Ile nilipoingia chumbani, namuona wife kashika tiketi za ndege na akaanza kuongea kwa hasira,
“Baba J, hukuwa China kama ulivyosema, ulikuwa South Africa.”
ITAENDELEA…
Shida ni budget yake tu maana hiyo inahitaji uoneshe uhalisia wa expensive life pia sehemu ya kwenda SA, Ethiopia je wataweza?!Hii story ikichezwa series itakuwa kali sn
Kina lamatta mitaji midogo, labda azam angekuwa anasponsor izo production km showmaxShida ni budget yake tu maana hiyo inahitaji uoneshe uhalisia wa expensive life pia sehemu ya kwenda SA, Ethiopia je wataweza?!
Siku hizi kuna AI. Inaweza kutengeneza fiction story ya aina yoyote hata video ya kuonyesha mandhari ya eneo lolote duniani. Unaweza kukuta hata hii ni fiction!Shida ni budget yake tu maana hiyo inahitaji uoneshe uhalisia wa expensive life pia sehemu ya kwenda SA, Ethiopia je wataweza?!
Hapo kweliKina lamatta mitaji midogo, labda azam angekuwa anasponsor izo production km showmax
Kumbuka Tanzania hata editing tu bado sana unadhani tunao uwezo wa kutumia AI ilihali hata editing bado hatujafikia viwango?Siku hizi kuna AI. Inaweza kutengeneza fiction story ya aina yoyote hata video ya kuonyesha mandhari ya eneo lolote duniani. Unaweza kukuta hata hii ni fiction!
Kumbuka Tanzania hata editing tu bado sana unadhani tunao uwezo wa kutumia AI ilihali hata editing bado hatujafikia viwango?
AI pia inahitaji knowledge kubwa sana ya kutengeneza prompt na pia sidhani kama hata ni AI kama hizi za kawaida so tunahitaji ujuzi zaidi kwenye matumizi ya teknolojia
Unamkumbuka Mahinda my daughter kila siku anasema ametoka marekani ila hatujawahi kuona hata akipanda ndege?! Life la uigizaji lilivyoisha tu jamaa kweli ndo akahamia huko😂View attachment 3450385
Mbona mwamba alikua anaenda hadi states kushoot
Tupatie Muendelezo basi mkuuSEASON 03

Tema mate tumchape 🫲Sio kwa ubaya mkuu tunajua una majukum ila unavuta sana imefika kipingi ukitupia inabidi urejee episode ya Mwisho kwanza ndio uanze mpya kuconnect MUENDELEZO