Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 03

CHAPTER 4

“
A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

PREVIOUS:

Baada ya dakika 15, Mama J alikuja sebleni na aliniita chumbani mara moja, kisha akaondoka.

Sister alishtuka kumuona Mama J kwa hali ile na akasema:

“Something wrong, hujasahau kumbukumbu yoyote kutoka South Africa?”

Nilitikisa kichwa kuonyesha hapana na nikanyanyuka kuelekea chumbani.

Ile nilipoingia chumbani, namuona wife kashika tiketi za ndege na akaanza kuongea kwa hasira,

“Baba J, hukuwa China kama ulivyosema, ulikuwa South Africa.”

CONTINUE:

Nilimwangalia kwa sekunde kadhaa bila kusema neno, kisha nikaanza kucheka kwa sababu nilihisi alikuwa amechanganyikiwa. Lakini kitendo changu cha kucheka kwa dharau kilimfanya azidi kukasirika na kuongea kwa hasira.

“Baba J, usinione mimi ni mtoto, ninaamini…”

Nilimkatisha kabla hajamaliza.

“Hivi umesahau tulishazungumza kwamba nikitoka China nitakwenda South kumuona Iryn?”

Akanitazama kwa mshangao na kujibu kwa sauti ya ukali zaidi:

“Mimi sikumbuki kama tuliongea hivyo. All I know the kid belongs to you! Kuna siku ukweli utajulikana, na utalipa kwa hili.”

“Pay for what? Kama unaishi na kuniwazia mabaya kila mara, kweli kuna maana gani wewe kuwa mke wangu? Mwanamke ambaye hata siku moja hafikirii mazuri juu yangu?”

Akatulia kidogo, kisha akasema:

“Naomba nione hizo tiketi za China na hoteli ulizofikia.”

Nikavuta pumzi ndefu;

“Unataka turudi kulekule nyuma? Sawa, nitakupa tiketi hizo. Lakini tukubaliane kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa mahusiano yetu, tubaki tu kulea mtoto.”

What’s your point? What do you mean?” aliuliza kwa mshangao.

“Siwezi kuendelea kuwa na mwanamke asiye na imani nami. Wewe mwenyewe ungeweza kuishi hivyo?”

Baada ya maneno hayo, niliamua kuondoka chumbani. Nikamwacha akiwa kimya, hajui aseme nini wala afanye nini.

Nilirudi tena sebleni kuendelea na mazungumzo ya mwisho na dada kabla hajaondoka. Mazungumzo yetu makubwa yalihusu suala la Iryn, jambo ambalo siku zote lilikuwa likizunguka kichwani mwangu bila majibu ya uhakika. Kila mara nilipojaribu kutafakari hatua sahihi za kuchukua, nilijikuta nikipotea kwenye wingu la mawazo na kukosa mwelekeo.

Dada alikuwa akinipa faraja kubwa. Alinisisitiza kuwa tutapita salama katika hili jambo, ilimradi tu kama nitakuwa na utulivu wa hali ya juu katika kulishughulikia. Kwa mtazamo wake, aliendelea kusimamia msimamo wake uleule wa kuwa nivute subira, na baada ya miezi sita ndipo nianze kufikiria hatua za wazi na sahihi.

Tulishauriana mambo mengi sana, na mara kwa mara alinionya kuhusu namna ya kufanya “moves” zangu na hata jinsi ya kutumia simu. Alisisitiza kuwa, nisipokuwa makini, nitakuja kuharibu kila kitu kwa upumbavu mdogo.

Baada ya muda mfupi, Elena na mama J walijiunga nasi. Mazungumzo yakahama kutoka kwenye suala la Iryn na kuelekea kwenye maisha ya Elena, hasa masuala ya shule. Tulitamani kumsikia akieleza ndoto zake mwenyewe. Elena kwa sauti yake ya upole lakini yenye msisitizo, alisema kuwa tangu akiwa mdogo alitamani kuwa daktari.

Nilitabasamu kwa sababu nilihisi ndoto yake ni kubwa na nzuri, lakini nikajikuta pia nikitazama matokeo yake ya shule. Akiwa na Division 3 ya pointi 22, alifanya vizuri kiasi, lakini si kwa kiwango cha masomo ya sayansi ukizingatia alipata D ya mathematics na Physics. Ndipo nikamshauri asomee Accountancy, nikiamini kwa dhati kwamba katika uhasibu angefanya vizuri na kufanikisha ndoto za maisha yake ya baadaye.

MAMA J aliniangalia, kisha akasema kwa sauti yenye hofu na kejeli kidogo:

MAMA J: “We Baba J, unataka kweli mtoto wa watu akafeli?”

MIMI: “Ukilaza wako wa accounts usiulete kwa Elena, hampo sawa.”

DADA: “Mhh! Hebu tumpe nafasi na yeye asikike. Msikilizeni anachosema.”

ELENA: “Mimi niko tayari kusoma course yoyote, cha muhimu iwe nzuri. Najua nyie mnaelewa zaidi kuliko mimi.”

DADA: “Usikubali tu sababu utasomeshwa, unatakiwa useme kutoka moyoni unachopenda.”

MIMI: “Elena atafanya vizuri kwenye uhasibu. Niko tayari kumsapoti kwa kila njia, kwa sababu nataka aje awe msaada mkubwa kwangu hapo baadaye.”

Tulipoendelea na mazungumzo mengine, niligundua kuwa Elena angebaki nyumbani na mimi badala ya kwenda Arusha pamoja na wife. Habari hizo zilinipenya kama mshale, kwani sikupendezwa hata kidogo. Nilijua fika kuwa kukaa naye kungenipunguzia uhuru wangu wa kufanya mambo yangu kwa namna ninavyopenda.

Kwa upande wao, walipanga kuondoka kesho yake asubuhi majira ya saa moja, ili kufika mapema Airport. Dada yangu, akiwa na tabasamu la furaha, alisema anatamani sana kukutana na rafiki yake Tyna, ili wakumbushane mambo yao na kupiga story.

Ilipofika asubuhi, niliamua kuwapa kampani hadi Airport. Safari haikuwa fupi, foleni ya barabarani ikatufanya kutumia zaidi ya saa moja kabla ya kufika. Tulipowasili Airport, niliwasaidia kutoa mabegi yao moja baada ya jingine, huku dada yangu akiwa bize kuwasiliana na Tyna, akionekana mwenye furaha na hamu ya kukutana naye. Kwa upande wangu, sikutaka kupoteza muda kabisa eneo hili sababu nilikuwa nina miadi ya kukutana na Asmah, hivyo niliwaaga na kuwatakia safari njema.

Nilichukua njia kuelekea Upanga, nikiwa na shauku ya kufika kwenye apartment ya Asmah. Kabla sijafika, nilimpigia simu kumtaarifu kuhusu ujio wangu. Nakumbuka vizuri, nilipofika maeneo ya ofisi za Toyota-Nyerere Road, magari yote yalilazimika kusimama pembeni kupisha msafara wa viongozi. Tulikaa hapo zaidi ya saa moja tukisubiri wapite, na muda ukaendelea kuyeyuka taratibu.

Wakati nikiwa kwenye mataa ya Kamata pale Gerezani, simu yangu iliita. Ni Asmah, sauti yake ikiashiria wasiwasi, alihisi nimeghairi kwenda.

“Upo wapi? Saa mbili zimepita na chai huku imeanza kupoa.”

Nilitabasamu kimya kimya, nikamueleza hali halisi ya foleni na msafara uliotuchelewesha.

Hatimaye nilipofika, nilielekea moja kwa moja hadi kwenye apartment yake. Alinipokea kwa tabasamu pana lililong’ara zaidi ya asubuhi yenyewe, kisha akanikaribia na kunikumbatia kwa upole na mahaba, nilijisikia kama nimefika mahali salama.

ASMAH: “Asante kwa kufika, karibu sana”, alisema huku akiniongoza kuelekea sebuleni.

Aliniandalia chai, nami nikasogea hadi kwenye dining table. Yeye alikaa mbele yangu, macho yetu yakakutana na tukaanza kuangaliana pale.

MIMI: “Umezidi kuwa mrembo, mummy.”

Asmah alitabasamu, macho yake yakiangalia yangu kwa utulivu na upendo.

ASMAH: “Thank you… hata wewe umependeza. Vipi mtoto pamoja na mama yake, wanaendeleaje?”

MIMI: “Wanaendelea vizuri tu.”

ASMAH: “Nioneshe picha za mtoto, nimuone Aria.”

MIMI: “Iryn hajakutumia?”

ASMAH: “Sijaongea na Iryn kwa muda mrefu sana. Mara ya mwisho alisema anakaribia kujifungua, kisha hajawahi kujibu texts wala kupokea simu zangu.”

Nilitoa simu yangu mfukoni, nikaanza kumuonesha picha za Aria. Alianza kuzipitia kwa utaratibu, macho yake yakizingatia kila picha kwa makini. Hii mara hii alinyamaza kimya, bila kusema hata neno.

ASMAH: “She is so cute.”

MIMI: “Na wewe bado kunizalia mtoto mzuri.”

ASMAH: “Kweli, natamani kuwa na mtoto, lakini sio kwako, Insider. I need to stay away from you.”

Kauli zake ziligonga moyoni mwangu kama mshale, niliacha kunywa chai, nilimshika mkono kwa upole, kisha tukasogea tukakaa kwenye coach.

MIMI: “Unamaanisha nini kusema hivyo? Unasahau mimi na wewe tumetoka wapi? Leo hii unaniambia unataka kukaa mbali na mimi? Nimekukosea nini, Asmah?”

Asmah alitulia kwa muda kidogo, kisha akazungumza kwa sauti yenye dhahiri ya huzuni na upendo:

ASMAH: “Insider, kuendelea kuwa karibu na wewe ni kuendelea kuumiza hisia zangu. I truly love you, and I do. Inabidi nikubali matokeo ya yanayoendelea, na sitaki kuingia kwenye matatizo na Iryn. Hata kwenda kusoma Qatar, ni kwa ajili yako, si kwa ajili ya hisia zangu.”

Ilibidi nibadili mada na tulianza kuzungumzia sakata lake la kuacha kazi ili aondoke nchini na kwenda Qatar kwa ajili ya kuanza chuo, ambapo masomo yalitarajiwa kuanza mwezi September. Kuhusu kuondoka kwa Asmah, sikuwa nakubaliana na uamuzi huu, kwani nilihisi sitamani kuona akiondoka. Zaidi ya hayo, Iryn hakuwa na taarifa yoyote kuhusu mpango huu, kwani sikumgusia kuhusu nia ya Asmah kuacha kazi kwa ajili ya masomo.

Nilifanya hivi kwa nia ya kumlinda Iryn na afya yake. Sikutaka kuona mama mtoto wangu akikabiliwa na msongo wa mawazo ya ofisi. Nilijikuta nikitafakari kwa kina, nikajaribu kumshawishi Asmah abaki hapa Dar es Salaam na atafute chuo hapa, badala ya kuondoka. Hata hivyo, Asmah aliendelea na msimamo wake kwamba lazima aondoke. Taratibu zote alikuwa amezikamilisha tayari, na alionyesha waziwazi kuwa uamuzi wake hauwezi kubadilishwa. Sikuwa na budi isipokuwa kumkubalia.

Kipindi chote naongea naye, mkono wangu wa kushoto ulikuwa ukimpapasa taratibu kila angle ya mwili wake na kufanya kuwa kwenye mahaba mazito. Hapo tulianza kupeana romance, na hatimaye tukahamia chumbani. Baada ya zoezi refu, tuliishia kulala.

Mimi nilikuwa wa kwanza kuamka na nilienda sebleni kuangalia simu yangu, nilihisi lazima nimepigiwa simu za kutosha. Baada ya kuangalia simu niliona texts na missed calls kutoka kwa Mary na Sumaiya, wote walikuwa wamenipigia zaidi ya mara mbili.

Nilimpigia simu Mary ili tuzungumze, ukizingatia nilikuwa nimempa ahadi ya kukutana leo. Hivyo, nikamwambia tuonane baadaye kwa ajili ya kwenda shopping ili nitimize ahadi yangu. Akasema yuko Msasani na anahitaji nifike kwa wakati, hivyo nisichelewe.

Wakati naongea na Mary kwa upande mwingine nilimsikia Asmah akiniita na baada ya kuona simjibu aliamua kutoka seblen na muda huu nilikuwa nikiagana na Mary;

“Insider…Mbona umeniacha peke yangu?” Na akajitupia kwenye sofa kama mzigo “puuuh”

Nika slap kario lake PAAH, na nikambeba juu juu kuelekea chumbani kuendelea na round 2 maana hii siku Asmah alikuwa ni mtamu sana na tulishinda tukipakuana, siku nzima.

Kitandani tulikuwa tukiongea mambo mengi sana. Asmah aliendelea kunisisitiza kuwa makini sana na Rebby na alisema ndiye “informer” wa Iryn pamoja na Lucy. Baada ya kumtaja Lucy, nilishtuka na sikuamini maneno yake, hivyo nikampinga:

MIMI: “Lucy? Unamuonea kweli? Yuko karibu na Iryn, ila sio snitch.”

ASMAH: “Huwezi kuelewa sasa, ila kuna siku utakuja kuyakumbuka maneno yangu. Lakini kuwa makini.”

Sikuwa na uwezo wa kumpinga zaidi, kwani wanasema rafiki yako ndiye adui wako, na snitch kawaida hufuatana na wewe. Wakati nikifikiria haya maneno ya Asmah, aliendelea kuzungumza:

“Insider, nakushukuru kwa yote hadi sasa. Umejitoa sana kwangu na umekuwa msaada mkubwa. Kipindi kile nilipopata ajali ya pikipiki na kipindi nilipoachishwa kazi, ulikuwa msaada sana kwangu…”

Ilibidi nimkatishe maongezi yake pale:

MIMI: “Kipindi kile, Iryn alikuachisha kazi au ulikuwa wewe mwenyewe?”

ASMAH: “No, aliniachisha, Insider, na wewe baada ya kuwa mkali akaomba niseme vile.”

MIMI: “Okay, Asmah, haya yametokea. Cha muhimu, umeondoka huna shida na mtu, na mimi nitaendelea kuwa pamoja na wewe.”

ASMAH: “Ahsante! Leo nimefurahia kupata muda na wewe pamoja na ‘sweet sex’ kwa ajili ya kuagana. Don’t ever expect it to happen again. Muda wowote kuanzia sasa nitaondoka, Insider. One more thing natamani nikwambie-Iryn truly loves you, don’t play with this opportunity.” Alinikiss shavuni.

MIMI: “Please, before hujaondoka nijulishe mummy. Ukiondoka bila kuniaga naomba unitafute forever na ufute namba yangu.”

Nilishuka kitandani kwa haraka nikaanza kuvaa ili nikaonane na Mary maana alikuwa kashapiga simu za kutosha.

Nilimuaga Asmah na alinikumbatia kwa nguvu. Hali hiyo ikanifanya nisikie upendo na mimi kumkumbatia kwa nguvu. Nilichukua funguo ya gari kiaina na nikamshika mashavu yake mawili na kumkisi kwenye paji lake la uso na akanisindikiza kwa macho hadi nilipopotea mlangoni.

Baada ya kufika parking, nilimuona akinitazama kutoka juu ya ghorofani akiwa akitabasamu na akinipungukia mkono wa ishara ya “bye.” Nilimkonyeza kisha nikawasha gari na kuondoka eneo hilo, kwa spidi kali.

Nikiwa njiani, nilimpigia simu Mary, aliishia kunifokea sana kwa sababu sikuwa napokea simu zake, lakini hatimaye nikaishia kumbembeleza. Akaniambia kuwa alikuwa akijiandaa kuondoka kwenda kwao, kwani walikuwa na kikao cha familia. Nikamwambia niko njiani, nitafika hivi karibuni kwenye apartment yake. Kwa upande wangu, baada ya kusikia kwamba Mary anakwenda kwao, nilifurahi sana, sikuwa na hamu ya kufanya mapenzi tena.

Dakika kumi baadaye, nilikuwa nimefika nje ya geti kuingia ndani ya apartment zao. Nilipark gari nikiweka kuelekea usawa wa apartment yake. Nilipofika mlango, ulikuwa wazi, hivyo nikaingia ndani. Nilimkuta Mary akiwa chumbani, amekaa kitandani na akipanga nguo zake.

MIMI: “Kwanini unaacha mlango wazi? Ukivamiwa au kufanyiwa jambo baya utamlaumu nani?”

MARY: “Mlinzi getini ana kazi gani?”

MIMI: “Mtu akiwa na jambo atafanikisha tu azima yake, anaweza hata kuwa jirani yako. Hili lisijirudie.”

MARY: “Niliacha wazi kwaajili yako. Kwanza, ulikuwa wapi? Nakupigia simu zangu tangu asubuhi na hupokei.”

MIMI: “Baada ya kuongea mchana, nilienda Serena Hotel kuonana na mtu, ni masuala ya ofisi. Jiandae tuondoke, twende shopping.”

MARY: “Nimekusubiri sana nikitegemea utawahi, na unajua nimekumiss na niko horny sana.”

MIMI: “Sorry, ni masuala ya kampuni yamenichelewesha. Hivi home una mpango wa kwenda muda gani?”

MARY: “Kikao ni saa 3 usiku, na sasa ni saa 1.”

MIMI: “Acha nikupeleke shopping Palm Village, tunaweza onana hata kesho tukafurahia baby.”

MARY: “No hunn, nimekumiss sana naomba tufanye hata kidogo. Hio shopping tunaweza arrange hata kesho.”

MIMI: “Mary, nimekumiss mpenzi wangu, ila kwangu mimi lisaa halitoshi ukizingatia nimekumiss. Sitakubali kukuachia mapema na ukachelewa kikao.”

Mary: “Sawa, lets go.”

Muda huu, simu yangu ilianza kuita, na nilipoitoa alikuwa ni Iryn, tena video call. Mary alikuwa makini sana kuniangalia, lakini nilipotezea na nikampa ishara tuondoke.

Tulikwenda moja kwa moja hadi Palm Village, ambapo tuliingia madukani kwaajili ya shopping ya Mary. Tulitumia muda kama lisaa kuchagua na kujaribu nguo, kunua vitu na mwisho nikatoa kiasi cha laki 6 hivi. Mary alifurahi sana kwa shopping hiyo, na baada ya hapo tukaondoka ili nimpeleke kwao.

Tukiwa njiani, nilitamani kujua ni kuhusu nini wanakikao cha familia, lakini Mary alisema hata yeye hajui, kwani wazazi wanataka kuzungumza nao moja kwa moja. Baada ya kufika, nilimdrop pale Shoppers, kisha nikaanza safari ya kurudi home. Sikutaka kwenda sehemu yoyote tena, nikiwa nimefurahi na kuridhika kwa siku nzima.

Nilimpigia simu Iryn ili tuongee, nikaweka loudspeaker ili niweze kuzungumza naye kwa uhuru huku nikiwa na drive. Kwanza kabisa, nilimpa habari kuhusu Asmah kutaka kuacha kazi kwaajili ya masomo na kwenda Qatar. Ni taarifa ambazo hakuzipokea vizuri na aliuliza mbona ghafla sana?. Nilimueleza kwamba Asmah alitoa taarifa hiyo muda mrefu, hata kabla ya kujifungua, ila sikutaka kumshirikisha na kumpa stress zisizo za lazima.

Mama Aria kwa upande wake hakuwa na la kusema zaidi, alisema atamtafuta Asmah ili wazungumze, na akanipa kazi ya kutafuta mbadala pindi Asmah atakapoacha kazi rasmi. Nilikuwa nimeshafika home muda mrefu na nimetulia ndani ya gari, nikiendelea kuongea na mama mtoto.

Iryn alianza kunipa story kuhusu kilichoendelea kule South Africa baada ya ujio wa wageni, ambao alisema wameondoka leo. Jumla ya wageni waliokuwa pale walikuwa 9, wakiwemo mama yake mkubwa, wajomba, mashangazi, na wengine mbalimbali.

Kwa ufupi, ndugu zake bado waliendelea na msimamo wao wa kutofurahishwa na kitendo cha Iryn kuzaa na mimi, mume wa mtu. Yeye kwa upande wake aliwaambia kwamba ilitokea bahati mbaya, ukizingatia Insider alikuwa karibu sana na mimi, na yeye ndiye alieleta furaha ya maisha yangu.

Ndugu zake walitaka kujua kuhusu familia ya upande wangu, wanasemaje kuhusu hili, na je, ameshawafahamu ndugu zangu? Nilimkatisha kwa haraka sana na kumuuliza:

“Eeh, ukawajibu nini?”

“Niliwaambia naongea na mama yako, na Aria akifikisha miezi 3 nitaenda kuwasalimia wazazi wako.”

Jambo lingine walilomuuliza lilikuwa kuhusu msimamo wake wa mila na desturi zao. Swali lilikuwa Je, atanataka kuwa upande gani, wa marehemu mama yake au baba yake? Iryn aliwajibu kuwa hana upande, na atafuata mila zote za baba yake mzazi pamoja na marehemu mama yake.

Mwisho kabisa, walimtaka ahakikishe atakwenda Ethiopia pamoja nami, kwaajili ya kunifahamu vizuri zaidi. Maongezi yote yalikuwa marefu sana, na Iryn alizidi kushinikiza kuhusu suala la kuwajua wazazi wangu haraka iwezekavyo, kwani hatuwezi kwenda wote Ethiopia kama bado hajawajua wazazi wangu, kitu ambacho kilikuwa kigumu kufanikisha.

Tulipiga stori nyingi sana, ikiwemo mkakati wake wa kurudi chuo kuendelea na masomo. Aliniambia kuwa mara tu Aria atakapofikisha miezi mitatu, ataanza kuja naye Dar es Salaam na kutafuta apartment ya kupanga, ambayo itakuwa sehemu yake ya kufikia. Tulikaa muda mrefu sana tukizungumza, tukipeana utani, tukacheka, tukashirikiana mawazo, kisha mwishowe tukaagana pale. Mimi nikaelekea ndani.

Nilipoingia, nilimsalimia Elena ambaye alikuwa akitazama movie sebuleni, kisha nikaenda moja kwa moja hadi chumbani. Nilipoketi kitandani, mawazo yangu yalinirudia. Nikaanza kuyapitia kwa makini yale maongezi yangu na Iryn kuhusu mpango wa kwenda Ethiopia, pamoja na wazo la kwenda naye nyumbani mkoani.

Nilitafakari sana, nikahisi huenda sasa ni wakati wa kuchukua hatua kubwa. Ushauri wa dada yangu niliamua kuuacha pembeni, nikabaki na msimamo wa kiume, safari ya kwenda Zambia kumuona mzee. Niliona huo ndio uamuzi sahihi, kwa sababu wakati mwingine wanawake hutegemea zaidi hisia katika maamuzi, ilhali sisi wanaume tunapaswa kutanguliza akili na uthabiti. Mpango huu niliona ndio “next move” yangu muhimu kwa kuanza kudeal na hili suala.

Kadri nilivyotafakari, wazo lingine likanijia kwa kasi ni kuhusu kuchukua hatua za haraka za “kufake” kuacha kazi katika kampuni ya Iryn, kisha nimpe taarifa hiyo mama J. Yeye hajui kabisa kuhusu siri yangu na Iryn, na mpango huu ungeweza kunipa kinga ya kisaikolojia endapo mambo yangesogea tofauti. Awali nilipomshirikisha dada yangu kuhusu hili, alinipa baraka zake na kuniunga mkono moja kwa moja.

Kipindi niko kwenye dimbwi la mawazo, simu yangu ghafla ikaanza kuita. Niliitazama na kuona jina la mama yangu mzazi likiangaza kwenye kioo. Sikupata jeuri ya kuipuuza, kwani moyoni nilijua fika kwamba mara nyingi nimekuwa nikizikataa simu zake, kwa sababu nilielewa anachotaka kuzungumza nami.

Safari hii nilijiweka sawa na kuamua kuipokea. Niliposalimiana naye, nilianza kwa kumuomba msamaha kwa tabia yangu ya kutopokea simu zake siku za nyuma. Nilimwambia bayana kuwa nilikuwa naelewa anachotaka kusema, na kwamba kwa namna yangu tayari nilikuwa nimejaribu kuyaweka sawa mambo yote yalokuwa yanaendelea.

Mama hakuzungumza mengi, ila sauti yake ilikuwa tulivu lakini yenye uzito wa maneno. Alinisisitiza juu ya mienendo na tabia zangu, akanikanya kwa upendo lakini pia kwa kumaanisha. Kisha akaishia kuniomba jambo moja la msingi ambalo ni kuwa na heshima kwa mama J.

Wakati bado nipo kwenye maongezi na mama, simu ya mama J nayo ilikuwa ikiingia upande mwingine. Nilipomaliza kuongea na mama, nilimpigia mama J mara moja. Tulipoanza mazungumzo, taarifa kubwa aliyokuwa ananipa ni kwamba tayari wamefika salama Arusha. Pia, kwa upole akaomba msamaha kuhusu tukio la jana la kuniomba ticket. Nilim reassure kwa upendo kwamba sina kinyongo naye, jambo lililomfanya atulie.

Baada ya maongezi marefu yenye kujenga, wife alimpa simu Junior. Nikaanza kupiga naye stori pale huku tunacheka maana kuongea vizuri ilikuwa bado. Baada ya kuzungumza naye kwa muda, niliwaaga wote kisha nikalala mapema kwaajili ya harakati za kesho.

*****
Jumatatu, saa 4 asubuhi, mara baada ya kupata kifungua kinywa, niliondoka kuelekea Masaki. Nilikuwa na miadi ya kukutana na Sumaiya pamoja na Immaculate, lakini nilianza kwanza kupitia ofisini kwa Sumaiya.

Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba alikuwa amenitafuta mara kadhaa, na pia kulikuwa na ripoti za fedha ambazo nilipaswa kumuelekeza kabla ya kwenda kushughulikia zabuni zilizokuwa mbele yetu.

Nilipofika ofisini kwake, niliingia moja kwa moja hadi ndani. Aliponiona, alisimama kwa tabasamu kubwa akaja kunisalimia, kisha tukaketi pamoja kwenye sofa ili tuanze mazungumzo yetu.

SUMAIYA: “Wewe mwanaume una maringo na mashauzi sana kama demu.”

Nikamtazama kwa dharau kisha nikamjibu:

MIMI: “Na ukinitibua nitaondoka nikuache.”

SUMAIYA: “Nisamehe Insider, najua nilikukera sana… ila ninaahidi kukwambia kila kitu utakachohitaji kujua.”

MIMI: “Ni lini hio?”

SUMAIYA: “Wewe siku nitoe out, ukaninyweshe, nitakuropokea kila kitu. Na ikiwezekana, unilombe pia.”

Nikacheka huku nikitikisa kichwa, kisha nikamjibu:

MIMI: “Sawa bhana, mimi sina shida na wewe. Ila ukweli ni kwamba nilikuwa nimebanwa, na kulea sikutaka usumbufu.”

Akanitazama kwa jicho la mzaha na kusema kwa sauti ya utani:

SUMAIYA: “Hongera sana, nimekusave ‘Baba Aria’.”

MIMI: “Naona unazidi kuwa mrembo mama… hivi yule yule sponsa bado yupo?”

Akatabasamu kisha akapiga kicheko cha sauti,

SUMAIYA: “Nampa penzi moto moto hadi anapagawa! Ila tatizo lake hana mikiki kitandani. Ana pesa, ndio, lakini kitandani ni zero kabisa.”

MIMI: “Sasa kwa nini unanambia haya maneno? Mimi yananihusu nini?”

Akasogea karibu, akaniangalia kwa macho ya kupepesa kisha akasema kwa sauti ya mzaha lakini yenye msisitizo:

SUMAIYA: “Point yangu ni moja tu… tafuta hela, na pia jiimarishe kitandani Baba. Usije ukalombewa bure.”

Nilijikuta nacheka tu! Sumaiya ni moja ya wanawake ambao hana Soni na nimuongeaji sana, lakini ukimuona huwezi kumdhania hivyo. Ni demu mkali, mwenye sura ya kuvutia na shepu murua ya mbali, wahuni wanasemaga vi-portable.

Baada ya mazungumzo yetu ya awali, nilianza kumuelekeza Sumaiya namna ya kuzifafanua na kuzielezea vizuri taarifa za fedha (financial statements) ambazo alihitaji kwa ajili ya semina aliyokuwa anakwenda kuhudhuria. Pia nilimpa mwongozo wa namna ya kushughulikia zabuni za usafi zilizokuwa mbele yake. Mazungumzo na maelekezo hayo yalichukua takribani saa moja ofisini kwake.

Mara tu baada ya kumaliza, niliagana naye na kuondoka kuelekea kuonana na Immaculate, eneo la Haile Sellassie Road. Ilikuwa ni mwendo mfupi tu kufika ofisini kwake, na kwa kuwa nilikuwa tayari nimempa taarifa ya ujio wangu, alinitokea nje akanikaribisha kwa tabasamu kisha tukapanda hadi ofisini kwake.

Nilimkabidhi hati ya malipo tuliyokuwa tumefanya, na baada ya yeye kujiridhisha kupitia mhasibu wake, alianza mara moja kazi ya kuipandisha hewani website. Nilikaa pembeni nikisubiri, muda ukasogea hadi saa moja kamili wakati akimalizia kazi hiyo kwa umakini mkubwa.

Baada ya kumaliza, aliniomba nijaribu kuingia kwenye website ili nijionee matokeo. Nilipofungua na kuperuzi, nilijikuta nikifurahia mno kazi iliyokuwa imefanyika, kwani iliwasilisha sura ya kampuni kwa namna ya kitaalamu na yenye mvuto.

Kutoka hapo, tuliondoka pamoja kuelekea ofisini kwaajili ya kutoa mafunzo ya namna ya kupakia bidhaa zetu (upload products) pamoja na kuhuisha taarifa mbalimbali. Kwenye jukumu hili, Hilda na Nollie walihusishwa moja kwa moja ili waweze kulimudu kwa urahisi katika shughuli za kila siku.

Baada ya kufika ofisini kwetu, nilimuita Hilda pamoja na Nollie kwa ajili ya kupewa mafunzo. Nilikuwepo pia nikisikiliza kwa makini kila hatua. Immaculate alianza kufundisha, na kwa takribani saa moja alitufundisha jinsi ya kupakia bidhaa kwenye website pamoja na kuhuisha taarifa. Kisha akawapa Hilda na Nollie task ya kufanya mazoezi ya moja kwa moja (practice live), jambo walilolielewa vizuri sana.

Baada ya kila kitu kuwa sawa, Imma alisimama na kusema kuwa ni wakati wake wa kuondoka. Akatupatia maagizo ya mwisho kwamba tukikumbana na changamoto yoyote, tuwasiliane naye moja kwa moja. Wakati huo ilikuwa tayari ni saa nane mchana, hivyo nikamwambia asubiri tupate chakula cha mchana pamoja na kina Hilda.

Nikageuka kwa Hilda na kumwuliza kwa mzaha:

MIMI: “Hilda, tunaenda wapi Bossy wangu?”

Akacheka kwa upole, kisha akajibu haraka:

HILDA: “Salad for Days! Salt tumechoka kila siku, leo tunabadilisha.”

Tulipoingia eneo la tukio, kila mmoja aliagiza chakula alichokitaka. Meza yetu ikawa na vicheko na mijadala, na mada kuu ikaendelea kubaki ileile ya website. Wakati tunakula, Hilda na Nollie walipata maswali mapya yaliyofanya kumvuta tena Immaculate kwenye maelezo ya ziada.

Wakati tukiendelea na mazungumzo meza ya chakula, nilitumia nafasi hiyo kumkumbusha Hilda kuhusu meeting na timu ambao tulipanga kufanyika siku ya jumamosi. Nilimueleza umuhimu wa kuhakikisha anazungumza na wenzake mapema ili kila mmoja awe tayari na hoja zake. Alinikubalia kwa kichwa, akionyesha kuelewa uzito wa jambo hilo.

Baada ya kumaliza kula na mazungumzo ya mwisho, tuliinuka na kuanza safari ya kumrudisha Immaculate kwenye ofisi yake. Tulipomdrop pale, tulishukuru kwa muda na msaada aliotupatia, kisha tukaagana kwa furaha. Mimi, Hilda na Nollie tulirejea ofisini kwetu kuendelea na majukumu ya kila siku.

Jioni, nilipanga kwenda kumuona mama Janeth kwa lengo la kumkabidhi gari lake na mimi kuchukua langu. Nilikuwa tayari nimemfahamisha mapema, na akanihakikishia kuwa jioni angekuwa nyumbani.

Saa 12 kamili, nilitoka ofisini pamoja na Hilda. Tulipofika kwa mama, tulikaribishwa na Jessie hadi sebleni. Dakika tano tu baadaye, mama alitokea akiwa na tabasamu usoni. Mara alipomuona Hilda, alianza kumzingua kwa utani wa mama wa kawaida, jambo lililonishangaza kidogo kuona jinsi walivyopatana kwa haraka.

MAMA: “Karibuni sana, nimefurahi kuwaona.”

Mimi na Hilda tukajibu kwa pamoja: “Ahsante mama.”

Nikaendelea kwa kusema:

MIMI: “Mama, nimekuletea gari lako maana ile siku sikufanikiwa kutokana na muda.”

Mama akatabasamu, kisha akajibu kwa upole;

MAMA: “Hio gari acha ibaki ni ya mpenzi wako Iryn. Ni busara ukaendelea kuitumia, hata yeye atafurahi kusikia iko mikononi mwako.”

MIMI: “Kuitumia siyo shida, mama. Ila tatizo la hapa mjini Dar, bodaboda hawachelewi kuikwangua.”

Mama akabadilisha mazungumzo na kuniletea habari mpya:

MAMA: “Sumaya alinipigia simu mchana kuniambia ulipita ofisini kwake na kumuelekeza kuhusu zile taarifa za fedha. Pia kuna Trade & Investment Meeting ambayo inafanyika Zanzibar kuanzia Alhamisi. Nilitaka wewe na Sumaiya muende mkashiriki, hasa kutafuta fursa mpya kwa kampuni yetu ya usafi.”

MIMI: “Sawa mama, hakuna shida. Ni muhimu sana kuhudhuria hizi meetings kwa ajili ya kutafuta channels mpya za kibiashara. Naomba kufahamu, hii itafanyika wapi na kwa siku ngapi?”

MAMA: “Itakuwa The Residence Hotel na itachukua siku tatu. Andaeni bajeti mapema. Uzuri wake ni kwamba kwa participants mnapata vyumba hapo hapo. Leo nitafanya malipo, na ninakuachia kazi ya kulipia hizo rooms.”

Baada ya kuagana na mama pale nyumbani kwake, mimi na Hilda tuliondoka tukiwa njiani tukizungumza mambo mbalimbali. Ghafla nikapata wazo la kwenda nyumbani kwangu moja kwa moja pamoja naye ili tupate dinner pamoja, na pia aweze kufahamu ninapoishi. Nilipomueleza lengo langu, Hilda alionekana kufurahi na tabasamu lake halikuisha, mazungumzo yetu yaliendelea kwa utulivu.

MIMI: “Na sasa hivi wewe na mama Janeth mmeanza lini utani hadi kuwa karibu namna hii?”

Akanicheka, akatikisa kichwa kisha akajibu;

HILDA: “Aaah, mama ndiyo ameanza kunizoea mwenyewe. Mimi sijaona hata kama ni kitu kikubwa.”

Tulifika nyumbani kwangu, nikamkaribisha Hilda ndani sebleni. Baada ya kukaa, nilimtambulisha kwa Elena, ambaye mara moja akaenda kutuandalia chakula pale dining. Wakati tukisubiri, macho ya Hilda yalielekea ukutani ambapo picha ya wife na Junior ilikuwa imebandikwa.

HILDA: “Na hawa wako wapi? Mbona sijawaona?”

Nikatabasamu na nikamjibu:

MIMI: “Ndio, huyo ni wife na huyu ni Junior, bila shaka unamjua ika kwa sasa wako safarini Arusha.”

Baada ya chakula kuandaliwa, tulikaa mezani na kupata dinner tuliyoandaliwa na Elena. Mazungumzo yaliendelea na kubwa ilikuwa kuhusu safari ya kwenda Zanzibar ambapo Hilda alitamani sana angepata nafasi hiyo. Muda ulisogea hadi saa nne usiku ambapo Hilda aliomba kuondoka kwenda kwake, na aliita Uber ya kuja kumchukua.

****

Asubuhi baada ya jogging, niliporudi nyumbani nilipiga macho kwenye simu yangu na kukutana na missed calls mbili kutoka kwa Ghati. Moyoni nilijilaumu mara moja kwa kutomtafuta siku kadhaa, hasa tangu mazungumzo yangu na Dullah. Nilijua kwa namna moja au nyingine nilikuwa nimemkosea, na hisia za hatia hazikuchelewa kunipenya.

Ghati ni mwanamke wa pekee sana kwangu. Wakati ule mama wawili waliponibana na kunifanya maisha kuwa magumu kule cello, yeye ndiye aliyebaki mstari wa mbele akipambana kwa ajili yangu. Kila nikimkumbuka, nilikuwa najiona nina deni kubwa sana kwake la kulilipa.

Nikampigia simu na iliita kwa sekunde chache, kisha sauti yake ya upole ikasikika sikioni mwangu, ikinirudisha kwenye utulivu:

GHATI: “Hi Insider, za siku?”

MIMI: “Ghati wangu, kwanza naomba nisamehe kwa kutokukujali. Sikuwa na makusudi, ila nil…”

Ghati alinikatisha maongezi yangu kwa sauti yake tulivu, isiyo na lawama:

GHATI: “Insider, don’t be… I understand. Nimefurahi kusikia sauti yako tena, ila mwenzako hapa katikati nilikuwa namuuguza mama yangu-alikuwa anaumwa sana.”

Maneno yake yalinigonga moja kwa moja moyoni. Nilishikwa na huruma na mara moja nikajikuta nikijilaumu zaidi kwa kutomjali wakati yeye alijitoa sana kwangu katika hali ngumu.

MIMI: “I’m really sorry, mama anaendeleaje sasa?”

GHATI: “She’s really fine now.”

Nikasita kidogo, nikavuta pumzi, kisha nikamkumbusha jambo nililokuwa nimemuahidi siku za nyuma:

MIMI: “Ghati, unakumbuka nilikupa ahadi ya kukupeleka Zanzibar?”

Kwa mshangao na furaha, alijibu kwa haraka kana kwamba alikuwa akisubiria maneno hayo:

GHATI: “Yaani! Utakuwa kama upo moyoni mwangu. Natamani sana kwenda sehemu nitulize akili yangu. Niko tayari kabisa, na please usicheleweshe hii safari.”

Nikajibu kwa msisitizo:

MIMI: “Safari itakuwa kesho mummy, na tutarudi Jumapili. Is that okay with you?”

GHATI: “Yes! Niko tayari, acha leo nichukue emergency ofisini.”

MIMI: “Poa mummy, I hope to see you soon. I miss you so much.”

GHATI: “Bye Insider, I miss you too.”

Nilipokata simu, nilihisi maamuzi niliyoyachukua yalikuwa sahihi kabisa. Safari hii ya Zanzibar ingeweza kuwa nafasi nzuri siyo tu ya kumpa Ghati muda wa kupumua na kutuliza akili, bali pia ya kumaliza tofauti zetu na kutimiza ahadi niliyokuwa nimemuahidi kitambo.

Nikiwa barabarani kuelekea ofisini, ghafla nikapata wazo la kumpigia simu Sia, yule dada tuliyekutana naye Coco Beach. Lengo kuu la kuwasiliana naye lilikuwa biashara, tulihitaji kujadili mambo muhimu ya kibiashara. Baada ya mazungumzo mafupi, tulikubaliana kuwa tunakutana jioni pale pale Coco Beach ili kuendeleza mazungumzo zaidi.

Baada ya kufika ofisini, nilipark gari na ghafla nikagundua gari la mama Janeth limefika pale pia. Nilipokuwa nikiingia ndani, namuona amekaa pale reception, sehemu ya kupumzika wateja. Nikamsalimia kwa heshima na tabasamu, na mazungumzo machache yakaanza kwa upole.

Baada ya kuzungumza kwa dakika chache, mama alisema kwa uzito:

MAMA: “Nimeona ni muhimu mkaongozana na Hilda pia kwenda Zanzibar. Atakuwa na fursa ya kupata experience pia.”

Nikakaa kimya, nikitafakari kwa sekunde chache. Kwa kweli, sikuwa na uwezo wa kupinga maamuzi yake, nikakubali, ingawa kwa shingo upande.

Mama hakuchukua muda mrefu, akaondoka baada ya kutoa maamuzi yake, nami nikabaki pale kuandaa bajeti ya safari yetu ya Zanzibar. Safari yetu tungetumia siku tatu pale, na kurudi Jumapili, hivyo kila kipengele cha bajeti kilihitaji kuzingatiwa kuanzia malazi, usafiri, chakula, na gharama za ziada.

Hata hivyo, moyo wangu ulianza kupishana. Nilijikuta nikiona changamoto kubwa ikija na Hilda. Nilijua mpango wangu wa safari ulikuwa kwenda na Ghati, na kuangalia kuwa Hilda angekuwa pale karibu ingekuwa ni kikwazo kwangu. Kwa upande wa Sumaiya sikuwa na wasiwasi naye, kwani ningeweza kumcontrol kirahisi. Hilda, kinyume chake, angekuwa tatizo kwangu, kwakweli ilikuwa changamoto kubwa.

Nikaanza kutafakari hatua za kuchukua, nikijaribu kupanga namna ya kushughulikia hali hii. Wakati huo, simu yangu ilianza kuita, ikipiga kelele…..

BETTER LATE THAN NEVER

THURSDAY
Thanks
 
Razorblade
 
Aisee story inazidi kunoga ninafuatilia sentensi kwa sentensi.Asante Insider Alhamisi tutakuwepo kupata mwendelezo.
 
come on! I ain't female.you are certainly right I have done some schooling in the past and I actually have been following up the story without commenting as you can see I am a new member

The inside man had been going to places I frequented and I once thought I might have encountered him somewhere especially when he mentions places like Rabininsia hospital,Lugalo,Nyuki,Mbweni,Mikocheni,Rainbow,mbezi beach,M city,etc

His is a true story for I scrutinised the authenticity of the narrative to ascetain flaws but upto no avail.The doubts rests on the amount of money he mentions but it doesn't matter so long as the story flows.

I think he need pieces of advice and I thought he might be needing in his treatment of mama J,how hashly he ends relationship.how he jiggles the two affairs etc

He might be busy at the moment that's why the thread has lost traction,I would suggest for him to drops several chapters in quick succession and disappear.The this is the 'bonus'chapter gave away the utamu wa hadithi now we know what happened

Unaandika kama AI
 
Back
Top Bottom