Umeongea kama mama J.Leo jumapili jamani baba J tuletee muendelezo INSIDER MAN
Kweli kabisa.Bro yupo busy, chuo, kwa Ghatt, kwa Asma, kwa mchepuko wa Pama, saloon, kwa marry kwa mama J, kufatilia biashara Dom, site la mzee Juma, bado kufatilia kampuni ya baba Ilyn, kuongea na Ilyn... inshort jamaa anamambo mengi
Jamaa ana huruma sana kwa wanawake yaani anaweza kushinda anazunguka majumbani kwa wanawake siku nzima hadi saa sita usiku, alafu yeye hatumiagi condom 😇😇😇yaani nasikia kuchanganyikiwa lakini angalau episodi hii hapokei pokei bahasha na amepunguza kusimamia miradi ya watu.Bro yupo busy, chuo, kwa Ghatt, kwa Asma, kwa mchepuko wa Pama, saloon, kwa marry kwa mama J, kufatilia biashara Dom, site la mzee Juma, bado kufatilia kampuni ya baba Ilyn, kuongea na Ilyn... inshort jamaa anamambo mengi
Na bado misele ya kalambezi na chako ni chako 😂Kweli kabisa.
Muda wa kuandika story ni 1% tumvumilieni INSIDER MANJamaa ana huruma sana kwa wanawake yaani anaweza kushinda anazunguka majumbani kwa wanawake siku nzima hadi saa sita usiku, alafu yeye hatumiagi condom 😇😇😇yaani nasikia kuchanganyikiwa lakini angalau episodi hii hapokei pokei bahasha na amepunguza kusimamia miradi ya watu.
Na wakati huu nilianza kumuwaza Ghati itakuwaje tukifika Zanzibar.
Kama hii ni true story basi uenda hata nafasi ya kuandika hana maana mda mwingi yupo na wanawake, na hili pia mkaliangalieMuda wa kuandika story ni 1% tumvumilieni INSIDER MAN
😂Kama hii ni true story basi uenda hata nafasi ya kuandika hana maana mda mwingi yupo na wanawake, na hili pia mkaliangalie
Next episode will be on...?SEASON 03
CHAPTER 5
Nikaanza kutafakari hatua za kuchukua, nikijaribu kupanga namna ya kushughulikia hali hii. Wakati huo, simu yangu ilianza kuita, ikipiga kelele.
Ni Ghati ndiye aliyekuwa akinipigia simu. Nilipopokea na kuongea naye, aliniarifu kuwa ofisi imempa emergency na tayari alikuwa amejipanga kwa safari.
Safari yenyewe haikuwa rahisi kupanga, hasa pale ilipoibuka hoja ya kwenda na Hilda Zanzibar, hilo lilikuwa kama mtihani kwangu. Kwa Sumaiya, ningeweza kumwambia waziwazi kwamba hawezi kuja kwenye chumba changu, na asingechukulia kwa uzito. Lakini kwa Hilda, jambo kama hilo lingekuwa gumu mno maana asingekubali kirahisi, na mimi nisingeweza kumkatalia. Nilifikiri sana, niliona kuambatana na Ghati ni sawa na kubeba bomu mfukoni, ni jambo lililohitaji uangalifu mkubwa na tahadhari ya hali ya juu.
Baada ya hayo, nilianza kuandaa bajeti ya safari. Mama alinifahamisha kuwa ofisi itagharamia kila kitu muhimu, mavazi rasmi ya kuvaa kwa siku tatu, viatu pamoja na mahitaji mengine ya lazima. Zaidi ya hapo, tulitenga pia bajeti ya matumizi binafsi, sambamba na posho ambazo kila mshiriki aliingiziwa pesa zote moja kwa moja kwenye akaunti yake.
Wakati nikiendelea kuandaa bajeti ya safari, nilisikia sauti ya Lucy kwa mbali ikiniita. Mara akaja moja kwa moja ofisini, na tulipokutana tuliishia kukumbatiana kwa furaha kubwa kwa sababu tulikuwa tumemissiana sana. Nilimpongeza na kumfariji kwa kumaliza mitihani yake, na muda ule alionekana mwenye furaha isiyo na kifani. Tuliamua kutoka nje na kukaa kwenye kibaraza ili tuzungumze kwa utulivu zaidi.
MIMI: “Kwanini umeamua kuja ofisini wakati tumekupa likizo fupi ya kupumzika?”
LUCY: “Nimekuja kwa ajili yako ujue. Halafu, sina hela, unadhani nitapata wapi ujasiri wa kukaa nyumbani bure?”
MIMI: “Mama anaendeleaje lakini?”
LUCY: “Yuko poa kabisa. Hongera sana Insider kwa kupata mtoto, ni jambo zuri mno.”
MIMI: “Asante sana Lucy.”
Tulipoendelea na mazungumzo, nilimpa taarifa kuhusu safari yetu ya kwenda Zanzibar pamoja na Hilda na Sumaiya. Baada ya hapo, tulihamishia mada kwenye mahusiano yake na Bob, nikitaka kufahamu hatima yao. Lucy aliniambia kuwa bado hawako sawa, na hajui kama wataweza kuendelea pamoja. Nilimwangalia vizuri, nikaona maumivu moyoni mwake, japokuwa alijaribu kuyaficha. Nikamuahidi nitamtafuta Bob na kuzungumza naye ili kujua mustakabali wao.
Dakika kama ishirini baadaye, Hilda aliwasili ofisini. Baada ya kutuona pale kibarazani aliishia kutusalimia kwa tabasamu. Nikamweleza kuhusu safari yetu ya kesho kwenda Zanzibar, na aliipokea taarifa hiyo kwa furaha kubwa. Baada ya muda mfupi aliingia ndani, akituacha mimi na Lucy tukiendelea na mazungumzo yetu.
Baada ya Hilda kuondoka, tuligeukia mazungumzo kuhusu Iryn. Lucy alinifahamisha kuwa Iryn amemwambia anataka aende South Africa kwa ajili ya kumsalimia. Tulipiga utani wa hapa na pale, kisha nikarudi ndani ofisini kuendelea na ripoti yangu.
Ilipofika saa kumi jioni, nilitoka ofisini kuelekea Cocobeach kuonana na Sia. Alikuwa amenitangulia kufika, na kabla sijaanza safari alinipa taarifa kuwa tayari yuko Coco, eneo maarufu liitwalo Aslay Mihogo, akinisubiri.
Nilipowasili, niliingia moja kwa moja kuelekea pale alipo. Nilikuwa napepesa macho huku nikimtafuta, na ghafla nikamuona ameketi kwenye kona ya mwisho kabisa, akinipungia mkono kwa tabasamu. Nilipomkaribia, nilihisi kama kuna kitu kimebadilika juu yake. Sia niliyemwona hakuwa yule niliyekutana naye mara ya kwanza, kwani sura yake, mwonekano wake, ulikuwa na upekee mpya. Nilipokaa, nilijikuta nikimtizama kwa makini zaidi, wakati huo yeye akinitazama kwa tabasamu laini lisilo na haraka.
SIA: “Khalid mambo? Za kupoteana.”
MIMI: “Safi tu… lakini kweli ni wewe?”
SIA: “Yeah, kwamba umeshanisaau? Na kwanini ulikuwa hupokei simu, wala hujibu meseji?”
MIMI: “Nilisafiri kidogo, nilikuwa nimebanwa sana, ndio maana.”
Nakumbuka siku ya kwanza kabisa kukutana na Sia pale Cocobeach. Wakati huo nilimwambia jina langu ni Khalid, siyo jina langu halisi. Leo nilipokutana naye tena niliona ni busara kumweleza ukweli kwamba jina langu halisi ni Insider. Aliposhtuka na kuniuliza kwa nini nilimdanganya jina, nilimfafanulia kwamba ni sehemu ya desturi yangu, kwa mtu mgeni ambaye sina mpango naye wa muda mrefu, sipendi kutoa jina langu la kweli mara moja.
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, wahudumu wawili walifika mezani wakiwa na sahani mbili kubwa za mihogo na samaki mzima aliyepikwa vizuri. Waliweka vyote mbele yetu kwa umakini, kisha wakaondoka. Nilipoangalia ule mlo, nilishtuka kidogo kujua kwamba Sia ndiye aliyekuwa ameniagizia tayari, ili tule wote kwa pamoja. Nilibaki nimeduwaa nikimtazama, naye akaendelea kutabasamu, na alinikaribisha.
Baada ya chakula kutufika mezani, tulianza mazungumzo ambayo yalisogea moja kwa moja kwenye biashara. Sia alionekana kuwa na hamasa kubwa, na mazungumzo yetu yakajikita zaidi kwenye biashara ambazo tayari alikuwa na uzoefu nazo. Tulichambua kwa kina kila biashara, gharama za kuanzisha (startup costs), changamoto zake, na namna ya kuvutia wateja.
Mwisho wa mjadala wetu, tuliona kuna nafasi kubwa kwenye biashara ya Home Decoration-ikiwemo mapazia, mapambo ya nyumba, na vitu vya thamani. Kwa kuwa Sia tayari anajuana na suppliers kutoka nje ya nchi kama Uturuki, China na Dubai, tuliona tunaweza kuagiza bidhaa moja kwa moja kutoka huko na kuuza hapa kwa faida kubwa. Connection na uelewa wake wa biashara ulifanya kila kitu kionekane rahisi zaidi ya nilivyowaza awali.
Nilimwambia anipe muda nipange mahesabu yangu vizuri, pia nifikirie kuhusu biashara zingine alizokuwa amenishauri, kisha nimpe majibu hivi karibuni. Alitabasamu kwa utulivu, kisha tukabadili maongezi kwenda kwenye mambo mengine kuhusu maisha kwa ujumla.
Ilipofika saa kumi na mbili jioni tuliagana pale Coco Beach. Nilimsindikiza hadi sehemu ya parking alikokuwa amepark gari lake. Nilipofika karibu, nilishtuka kidogo kuona akimiliki Discovery 4, gari lenye hadhi na usajili wake ni namba E. Tulisimama pale pembeni ya gari lake tukabadilishana maongezi ya haraka kwa dakika chache, kisha tukakumbatiana kwa heshima. Baada ya hapo, kila mmoja aliingia kwenye gari lake, yeye alikuwa wa kwanza kuondoka, akiniacha pale parking.
Nikiwa ndani ya gari, mawazo yangu yalinipeleka kwa Jane. Alikuwa amenikumbusha mara kwa mara kuhusu masuala ya biashara, hivyo nikaona ni busara nimtafute. Nilimpigia simu na akanijulisha kuwa yupo dukani kwake Kunduchi. Nikamjibu haraka kwamba ndani ya nusu saa ningekuwa nimefika.
Wakati naelekea Kunduchi, nilipata nafasi ya kuwasiliana na akina Hilda na kuwajulisha kuhusu safari yetu ya kesho saa 4 asubuhi kuelekea Zanzibar. Hata hivyo, moyoni nilitafakari kuwa kuondoka na Ghati pamoja na kina Hilda kungeweza kunisababishia matatizo. Ili kuepusha maswali na kelele zisizo za lazima, nilipanga kumwambia Ghati asubiri aje kesho kutwa.
Niliendesha gari kwa kasi barabarani nikielekea kwa Jane, lakini bahati mbaya foleni haikuwa rafiki kwangu. Takribani saa moja nzima ilinipotea njiani kabla sijafika dukani kwake. Nilipofika, Jane alinitazama kwa tabasamu na akaniambia:
“Hebu tutafute sehemu tulivu ya kukaa ili tuweze kuzungumza vizuri.”
Tukakubaliana kwenda Budget kwa ajili ya kupata utulivu na nafasi ya mazungumzo. Tulipokaa, nilitoa MacBook Air yangu mezani, nikaiwasha kwa haraka na kumgeukia Jane nikiwa na hamasa kubwa ya kushiriki naye mawazo yangu.
Nilianza kwa sauti ya kujiamini,
MIMI: “Shem, nimetumia muda mwingi kufikiria kuhusu biashara ambayo mimi na wewe tunaweza kushirikiana. Nimepitia wazo moja baada ya jingine, nikalinganisha faida na changamoto, na hatimaye nikafikia biashara moja ambayo naamini itatufaa. Haijachangamana sana, na hata usimamizi wake ni rahisi.”
Jane akaniangalia kwa makini, sura yake ikionesha hamu kubwa ya kujua.
JANE: “Biashara gani hiyo?” aliuliza huku akiinamisha kichwa kidogo kwa shauku.
Nikavuta pumzi ndefu kisha nikasema kwa msisitizo;
MIMI: “Ni biashara ya home and office decoration. Tutauza mapazia ya aina mbalimbali kwa nyumba na maofisi, pamoja na mapambo na urembo wa ndani unaoleta mwonekano wa kisasa na wa kuvutia.”
Uso wa Jane ukaangaza kwa tabasamu, kiasi kwamba wazo hilo liligonga kwenye moyo wake moja kwa moja.
JANE: “Aisee, hii biashara tayari ilikuwa kwenye mipango yangu!” Lakini kwanza tuanze kwa kuipanga vizuri kwenye bajeti, halafu mambo mengine tutayajadili baadaye.”
Tulipoanza kujadili, nilifungua faili langu la budget ambalo tayari nilikuwa nimetoka kulichambua kwa undani pamoja na Sia. Nikaanza kumueleza Jane hatua kwa hatua. Bajeti ya awali iliyohitajika kwa haraka ilikuwa takribani milioni 80, kiasi ambacho kingetumika kulipia gharama zote muhimu za awali, kama kodi ya pango, kuagiza bidhaa za kwanza (stock), pamoja na kupata vibali vyote vinavyohitajika kisheria.
Niliona Jane akibaki kimya kwa muda, kiasi kwamba alikuwa akipima uzito wa jambo hilo. Niliamua kumtoa wasiwasi kwa kumwambia, asihofu, tayari tuna mtu atakayetusadia kupata mizigo kutoka Uturuki, Dubai na China, tena kwa bei nafuu na ubora wa hali ya juu. Hii itapunguza sana gharama zetu za mwanzo na kutupa faida kubwa zaidi.
Maneno yangu yalionekana kumpa faraja sana na aliona ni wazo zuri la biashara. Tulikubaliana kwa pamoja kwamba tutafungua kampuni rasmi (Legal company) na tutagawana hisa kwa usawa (nusu kwa nusu). Baada ya makubaliano hayo, nilimgeukia Jane nikamwambia:
“Naomba unipe muda kidogo ili niandae comprehensive business plan, ambayo itakuwa na mpangilio wa kina utakaogusa maeneo yote muhimu kama, Market analyisis, Operational plan, Financial plan, Risk analysis nakadhalika.”
Jane alikubali bila kusita. Tulipanga kukutana tena baada ya wiki moja, ambapo nitakuwa nimeshakamilisha mpango huo, na hapo tutaanza rasmi hatua za utekelezaji wa biashara yetu mpya.
Baada ya kumalizana na mazungumzo ya biashara, tulibaki tukibadilishana mawazo mengine ya kawaida. Jane akaniambia jambo moja kubwa lililonigusa:
JANE: “Insider, sipendi kabisa kwamba sijawahi kumjua wife wako na mtoto zaidi ya kuwaona tu kwenye simu. Natamani siku moja nije kusalimia nyumbani.”
MIMI: “Karibu muda wowote, shem. Ila kabla hujaenda kwangu, kwanza nitakuja kwako.”
Jane hakusita kuniuliza jambo jingine ambalo alionekana kuliweka moyoni kwa muda:
JANE: “Na vipi kuhusu Mary? Nimekuwa nikiangalia, naona kama unampotezea muda mtoto wa watu.”
Nikavuta pumzi ndefu kisha nikamwambia ukweli:
MIMI: “Mary bado ni mchepuko wangu. Tulishakubaliana kwamba akipata mtu sahihi ataendelea naye, lakini mpaka sasa bado ni mpenzi wangu.”
Jane akanitazama kwa macho ya huruma kisha akatabasamu kwa huzuni:
JANE: “Mary sijui unampa nini, maana haelewi wala hasikii yule mtu. Insider, usifanye hivyo. Kadri siku zinavyopita, Mary anazidi kukolea kwako hadi anashindwa kujicontrol kabisa. Hii hali ikiendelea, hata mdogo wake atajua mna mahusiano, na hapo italeta mtafaruku mkubwa kwenye familia yao.”
Nilijikuna kichwa kidogo kisha nikasema:
MIMI: “Sasa shem, unanishauri nini? Maana hata mimi nampenda sana.”
Jane akaishia kucheka, akionekana kushindwa kuamini.
JANE: “Mimi nilidhani ni kama upepo tu unapita, kumbe mwenzangu umenogewa kabisa na asali.”
MIMI: “Niachie hili. I can handle, usiwe na wasiwasi.”
Wakati bado tunaendelea kuzungumza, simu yangu ikaanza kutetemeka pale mezani, ilikuwa kwenye vibration. Ilikuwa ni simu ya Iryn, ikapiga mara mbili mfululizo. Nilipoona jina lake, nikaamua kutoipokea. Jane akaona hali ile na akaniuliza kwa mshangao:
JANE: “Mbona hupokei simu?”
MIMI: “Huyo ni bossy wangu. Huwa anapenda mazungumzo marefu sana, ngoja nimcheki baadae nikimalizana na wewe.”
Jane akanitazama kwa macho ya kutia shaka, akatoa sauti fupi yenye mashaka:
JANE: “Mhhh….”
Saa zilikuwa zikielekea mbili kasoro usiku tulipoondoka Budget. Nilimchukua Jane nimrudishe dukani kwake, na tulipokuwa njiani, ghafla simu yangu ikaanza kuita tena. Wakati huo mawazo yangu yote yalikuwa kwa Iryn, kwa sababu huo ndio ulikuwa muda wake wa kawaida wa kupiga simu.
Nilipomfikisha Jane dukani kwake na yeye kushuka, simu iliendelea kuita tena. Niliamua sasa nipokee, lakini nilipogeuza macho, nikaona jina lililoibuka kwenye skrini si la Iryn kama nilivyotarajia, bali ni Mary.
Nikavuta pumzi ndefu kisha nikapokea.
MIMI: “Nambie mama.”
MARY: “Kwanini hupokei simu zangu?”
MIMI: “Ooh! Nilikuwa na Jane, tumeachana muda si mrefu. Hebu nambie, mummy.”
MARY: “I need to see you, baby.”
MIMI: “Mummy, kweli unataka nije hadi Msasani? Impossible!”
MARY: “Sipo Msasani, nipo home Mbezi Beach.”
MIMI: “Alright, basi tukutane kwa Zenna.”
Nikaelekeza gari kuelekea eneo tulilokubaliana.
Nilipofika, Mary hakuwa amewasili bado. Niliamua kupaki gari pembeni karibu na POA Supermarket, nikimsubiri. Dakika 10 zikapita, kisha nikamuona kupitia mirrors akija akitembea taratibu, akitazama huku na kule. Alipofika kando ya gari langu, aligonga kidogo kwenye kioo cha upande wa kushoto, kisha nikamfungulia mlango, naye akaingia ndani.
Macho yangu yaliteleza taratibu hadi kiuno chake, yakashuka chini, kukutana na pant fupi na chembamba kilichoukamata mwili wake na kuchora maungo yake barabara. Nikamwangalia kwa makini kisha nikaanza mazungumzo:
MIMI: “Kwahiyo leo hukupata nguo nyingine ya kuvaa?”
MARY: “Unajua kwa nini nimechelewa kuja? Mama bado yupo chumbani kwangu, hana dalili ya kutoka kabisa. Kama ningeingia kubadilisha mbele yake, lazima angeniuliza nataka kwenda wapi usiku huu.”
MIMI: “Lakini sina muda mrefu sana leo…kesho nina safari ya kwenda mkoani.” Nilimdanganya.
MARY: “Wee kweli? Ungeondoka kimya kimya? Hivi kama nisingekutafuta, nisingejua chochote kabisa, si ndio?”
MIMI: “Si safari ya kukaa muda mrefu, ni dharura tu imetokea, Jumapili nitarudi.”
MARY: “Basi kama ulikuwa unajua unaondoka, si ungesema mapema? Tungepanga kukutana vizuri. Unajua nimekumiss sana… na hizi nyege zangu, kama sio wewe, nani mwingine ataweza kunituliza?”
Maneno yake yalinitia hisia kali, nikamshika taratibu kwenye paja huku nikimnong’oneza:
MIMI: “Imetokea tu kwa ghafla mpenzi wangu, lakini nakupenda sana Mary wangu.”
MARY: “Honey, f** me please, hata kama ni kwenye gari. Nimekuona sasa hivi, siwezi kukubali uondoke ukaniacha hivihivi.”
Nikamuangalia kwa utani nikitabasamu.
MIMI: “Uvumilie kidogo basi mpenzi wangu. Hata mimi nimekumiss, huoni Kingdom yangu ilivyosimama, kisa kukuona?”
Mary alicheka kwa aibu ndogo, kisha akanisogelea akanipelekea mdomo wake. Tukaanza kubadilishana ndimi kwa utamu, moto ukizidi kuwaka.
MARY: “Baby… naomba hata kidogo tu, tafadhali.”
MIMI: “Lakini kwenye gari haiwezekani Mary.”
MARY: “Basi tafuta sehemu yoyote, hata kwa quickie…”
Nilipokuwa nimeshawishiwa na sauti ya Mary na joto lake, nilichezesha ubungo fasta nikageuza gari kuelekea Kidimbwi. Nilikuwa najua kuna eneo moja tulivu, mahali ambapo hakuna movement kubwa ya magari wala watu, isipokuwa mara kwa mara wamasai huonekana wakilinda magari ya watu hasa nyakati za wikendi pale Kidimbwi inapokuwa imefurika.
Nilipofika kwenye lile eneo, nikapata spoti nzuri nikapaki gari, na eneo lilikuwa tulivu sana. Tulishuka taratibu, upepo wa usiku ukipiga kwa mbali, niliacha mlango wa gari wa mbele wazi kama guard, ili hata kama mtu atatokea asione kinachoendelea pale. Nilipomuinamisha Mary awe kama analalia kiti cha mbele, huku sehemu ya nyuma ikitokeza nje, moto ulianza kuwaka kwa haraka, niki-hit from the back.
Baada ya kufyatua risasi za moto, ndipo akili ikanirudia, nikagundua hatuko sehemu salama. Nilimnong’oneza Mary kwa sauti tulivu tuingie ndani ya gari, kwani tulitumia kama dakika 20 hivi. Hatukutaka kupoteza muda eneo hili, hivyo nikamrudisha Mary mpaka Shoppers, nikamuaga kwa kumkiss mdomoni.
Baada ya kumshusha, niligeuza gari nikashika njia kurejea nyumbani, na muda huu nikashika simu ili nimcheki Iryn. Macho yangu yakakutana na missed calls mbili mpya kutoka kwake, mama mtoto wangu. Nikavuta pumzi ndefu, nikajua sina budi kumpigia. Mara simu ilipoita kwa sekunde chache tu, akapokea.
MIMI: “Hello, baby mama.”
IRYN: “Can you tell me exactly why you didn’t answer my calls?”
Sauti yake ilisikika na hasira, nilijua kabisa amekasirika.
MIMI: “Sorry mummy, nilikuwa nimetingwa sana. Hivi mama hajakwambia kuwa kesho nasafiri Zanzibar kwaajili ya seminar?”
IRYN: “Hapana, sina taarifa hiyo. So, hiyo ndo sababu ya kupotezea simu zangu?”
MIMI: “Mke wangu, niliacha simu ndani ya gari bila kujua, samahani.”
IRYN: “Alright nimekuelewa darling, nilitaka kujua umefikia l wapi kuhusu ile issue ya kampuni?”
MIMI: “Nilishaonana na Advocate nikampa maelezo ya awali. Akanipa kazi ya kufanya, na wiki hii natumaini kupeleka majibu this we….”
Alinikatisha pale, na kuuliza kwa shauku;
IRYN: “Alikupa task gani?”
MIMI: “Kufuatilia tarehe kamili ambayo umiliki wa kampuni ulibadilishwa, kujua Directors na shareholders wa sasa, na pia status yake kama bado ipo active au la.”
IRYN: “Na umezipata hizo taarifa? Kampuni ilibadilishwa lini?”
MIMI: “September 2021.”
IRYN: “Hmm… sahihi kabisa. Na najua bado iko active, au nakosea?”
MIMI: “Ndio mke wangu, kampuni bado iko active. Directors wako wawili, wote ni wabongo, shareholders wako watatu. Cha kushangaza, mmoja wa Directors amepewa 10%, mwingine 20%, lakini huyu Steve Jobs ni mzungu, yeye ndiye anayemiliki 70%.”
IRYN: “Who the heck is this guy?” Alikuwa haamini.
MIMI: “Hapo ndipo kazi ipo, tunatakiwa kuwafahamu hawa watu vizuri. Nikikutana na kukaa tena na Advocate nitasikiliza ushauri wake juu ya hizi taarifa.”
IRYN: “Huyo Steve Jobs niachie mimi nimfuatilie. Nahisi kuna something fishy kimefanyika, na aliyefanya haya yupo very close kwenye cycle ya mzee. Baby, umefanya kazi nzuri sana and thank you. Lakini naomba uwe makini sana, kila move unayofanya iwe calculated. Hawa watu sio wajinga.”
MIMI: “Usijali, mummy, niko makini sana.”
IRYN: “Na gharama zake zimekaaje?”
MIMI: “Bado hatujaongelea, ila tukikutana tena na Advocate tutazungumza yote.”
IRYN: “Tumekumiss sana.”
MIMI: “Nikitoka Zanzibar nitakuja kuwasalimia. Nimeimiss sana hio nyau.”
IRYN: “Forget it. Hadi December, mpaka nipone vizuri.”
MIMI: “Basi utanipa Samantha, no problem.”
IRYN: “I will kill you.”
Baada ya mazungumzo kumalizika, nilifungua geti na kuingiza gari ndani. Baada ya kuingia ndani nikampasha taarifa Elena kuhusu safari yangu ya kesho, na muda mfupi baadaye nikampigia mama J kumpa taarifa pia.
******
Niliamka mapema asubuhi nikiwa na hamasa ya kuanza safari yangu. Baada ya kuoga na kujitayarisha, nilianza kupakia mizigo yangu kwa umakini. Nilichukua suti tatu classic ambazo nilinunua kwa ajili ya mkutano, kisha nikaweka kwenye begi langu pamoja na mashati matatu safi, viatu pea tatu, na nguo zingine muhimu ambazo ningezihitaji huko Zanzibar.
Ilipofika majira ya saa mbili asubuhi, niliaga nyumbani na kuanza safari yangu kuelekea Morocco kumchukua Hilda. Tayari tulikuwa tumepanga kila kitu kwa umakini. Upande wa Ghati, nilimwambia wazi kuwa atasafiri kesho, siku ya Alhamisi, jambo ambalo alikubaliana nalo bila tatizo. Nilijua wazi kuwa nisingeweza kusafiri naye pamoja na akina Hilda, hali hiyo ingeibua maswali mengi yasiyo na majibu kutoka kwa Hilda na Sumaiya. Zaidi ya yote, ingeweza kuathiri vibaya uhusiano wangu na Iryn, kitu ambacho sikutaka kabisa kihatarike.
Baada ya kufika Morocco kwake, nilimpigia Hilda kumpa taarifa. Haikupita muda akatokea, akikokota begi lake huku akiwa amependeza kweli. Nilijikuta siwezi kuficha furaha yangu na nilimwaga sifa njiani kote, nikimsifia mpaka tukafika ofisini Masaki.
Tulipoingia ofisini, tulikuta Sumaiya bado hajawasili. Tukaamua kukaa ndani tukisubiri huku tukipiga stori mbalimbali, nyingi zikiwa zimezunguka kuhusu safari yetu ya Zanzibar.
Baada ya kama dakika ishirini, Sumaiya naye akawasili na tukaanza kupanga namna ya kuelekea Posta ili tupande boat. Tulijadiliana kuhusu usafiri, na hatimaye tukakubaliana kuwa kutumia Bolt kutakuwa rahisi na haraka zaidi.
Nikawageukia nikasema kwa mzaha:
MIMI: “Wanawake bwana, hivi haya mabegi makubwa yote ya nini? Mmeambiwa mnahamia huko Zanzibar?”
Sumaiya hakusita kujibu kwa kejeli na kujiamini:
SUMAIYA: “Wewe acha mambo ya wanawake, hayakuhusu, tuachie sisi. Nimejipanga kwenda kuongeza danga lingine kule Zanzibar.”
MIMI: “Aisee! Kwa hiyo income yako unategemea hiyo nyau?”
Maneno yangu yakamchekesha Hilda mpaka akashindwa kujizuia,
Bolt ilipofika, tuliaga wenzetu ofisini na safari ikaanza kuelekea Posta. Mimi nilikaa kiti cha mbele nikiongea na dereva, wakati Hilda na Sumaiya walikaa nyuma wakipiga stori kwa sauti kubwa, kiasi kwamba mipango yao ya Zanzibar ilikuwa ikisikika wazi kabisa. Walikuwa wamejaa furaha na shauku ya kusafiri na kufika huko.
Haikuchukua muda mrefu kufika eneo la Ferry. Baada ya taratibu zote, tulipanda boat tayari kwa safari. Nilikaa upande mmoja na Hilda, wakati Sumaiya alikaa upande wa pili. Safari ilipoanza, mimi na Hilda tulikuwa tukipiga story nyingi sana na kubwa ilikuwa kuhusu hali yake ya mahusiano kwasasa.
Hilda kwa upande wake aliendelea kusisitiza kwamba kwasasa bado yuko single na bado hajapata mwanaume anayempenda. Pia, alisema hahitaji kukimbilia mahusiano, kwani ameamua kufocus na maisha yake.
Baada ya lisaa, hatimaye, tuliwasili Zanzibar, gari ya kutufata haikuwa mbali na dereva akatupokea na kutupeleka moja kwa moja hotelini.
Kuna umbali mrefu kiasi kutoka Stone town hadi Kizimkazi Residence Hotel tuliyokuwa tunafikia, na safari ilituchukua takribani saa moja. Njia tuliyopita ilikuwa na mandhari nzuri, tukipishana na mijengo, mitende, na majengo ya kale. Tulipokaribia hoteli, uzuri wa mazingira ulianza kujitokeza waziwazi, kulikuwa na utulivu, bustani na miti iliyopangiliwa vizuri, na hewa safi na upepo wa bahari kwa mbali ukipuliza.
Tuliposhushwa kwenye dropping area, wahudumu wa hoteli walitukaribisha kwa unyenyekevu na tabasamu, jambo lililotufanya tujisikie vizuri. Tukaingia ndani, moja kwa moja hadi sehemu ya reception kuendelea na taratibu za kupewa funguo za room.
Kila mtu alikuwa na chumba chake. Vyumba vya hoteli hii vilikuwa vinajitegemea, vikiwa vimetawanyika kwa mtindo wa cottage. Mimi na Sumaiya tulikuwa eneo moja, yaani upande mmoja, ingawa vyumba vyetu vilitenganishwa kwa umbali wa takribani mita hamsini. Hilda, kwa upande wake, alipata mbali zaidi kwa sababu tulichelewa kufanya booking.
Wakati tunapewa maelezo na funguo za vyumba vyetu, Sumaiya ghafla akaniangalia kwa mshangao:
SUMAIYA: “Insider ndo nini hii? Si ungechukua room moja tu, ingetutosha wote. Hivi si kuchezea hela namna hii?”
Alisema kwa sauti kubwa kiasi kwamba dada wa mapokezi alijikuta akicheka kwa aibu, huku Hilda akitabasamu kimya kimya. Wahudumu waliokuwa karibu nao nao walibaki wakitabasamu kwa upole.
MIMI: “Sawa, basi twendeni kwanza tupumzike. Tuweke mizigo vyumbani, kisha tukutane jioni kwa dinner na kupanga vizuri kuhusu meeting ya kesho.”
Kwa maneno hayo, wahudumu wakachukua mabegi yetu na kutupeleka kwenye vyumba vyetu husika.
Nilipoingia chumbani, jambo la kwanza nililofanya lilikuwa kumpigia mama Janeth kumpa taarifa ya kuwa tumefika salama. Baada ya hapo nilimpigia Iryn kwa video call. Tulizungumza kwa muda mrefu sana, mazungumzo yetu yalikuwa ya furaha, lakini pia yenye maana kwa sababu alinipa mbinu kadhaa za jinsi ya kutoa hotuba nzuri, hotuba itakayoweza kuwavuta kila mtu atakayekuwapo kwenye kikao.
Baada ya kumaliza kuongea naye, nilikaa mezani chumbani na kuanza kupitia agenda ya kikao cha kesho. Ratiba ilionekana imepangwa vizuri, kikao kingeanza saa mbili asubuhi na kuendelea hadi saa nne, kisha tungepumzika kwa muda wa lisaa kwaajili ya breakfast. Baada ya hapo, ratiba ingeendelea kuanzia saa tano hadi saa nane mchana, kisha tungepumzika tena kwaajili ya lunch. Baada ya hapo ratiba ingeendelea tena kutoka saa tisa hadi kumi na moja jioni, ndo tungefunga kikao.
Nilijikita zaidi kuandaa nondo zangu vizuri katika mada muhimu za kuwasilisha, hasa kwenye masuala ya kifedha, mipango ya kampuni, pamoja na corporate social responsibility. Kutokana na Iryn kunipa muongozo mzuri wa kupangilia nondo zangu, sikuwa na wasiwasi kabisa.
Saa moja usiku tulikutana wote kwenye dining room kwa chakula cha jioni. Kila mmoja alichagua chakula alichokipenda, na wakati tunasubiri chakula, muda huu upepo mwanana wa bahari ulikuwa ukipuliza kwa mbali, ukileta ladha ya kipekee. Meza yetu haikukosa vicheko na utani, ni Sumaiya ambaye alikuwa akinogesha story.
SUMAIYA: “Hii hoteli ni nzuri sana, kwa mara ya kwanza nalala kwenye 5 star hotel. Mwanaume akikuleta kwenye hotel kama hii, hata kama sio mpenzi wako, unampea yote tu.”
Tuliishia kucheka pale, na akaendelea kuzungumza;
“Lakini bado sielewi kwa nini hukuchukua room moja. Tungeweza kutosha, kwani unatuogopa nini?”
MIMI: “Yaani tulale chumba kimoja? Unataka threesome ausioo.”
Hilda akaachia kicheko kikubwa:
HILDA: “Ila shoga angu unazingua sana, sema ukweli, Kwan una mpango gani na sisi?”
SUMAIYA: “Na ingekuwa room moja kweli, usingelala?”
MIMI: “Sumaiya sikia, kila kitu kimegharamiwa na kampuni. Huna haja ya kulalamika.”
HILDA: “Halafu, room yangu iko mbali mno na nyinyi. Hii imekaaje?”
MIMI: “Nilikuwa nimeshafanya booking mapema, lakini baada ya mama kutoa taarifa ya safari yako, ikabidi nifanye booking nyingine kwa haraka. Ndiyo maana room yako ikawa mbali kidogo na zetu.”
Sumaiya alitabasamu kwa kejeli na kusema:
SUMAIYA: “We naye huna lolote sema ulitaka uwe karibu na Insider. Analala peke yake unaweza kwenda kumpa kampani hukatazwi.”
Maneno yale yakaleta ukimya wa sekunde chache. Hilda hakujibu chochote, alibaki kimya kana kwamba hajasikia, na alijifanya kuwa busy zaidi na simu yake.
Tuliletewa chakula na wote tukaanza kula huku tukijadiliana kuhusu mipango ya kikao cha kesho. Tulikubaliana kuhakikisha kila mmoja anaonekana nadhifu, anapendeza na “anawaka” vizuri. Kuhusu sehemu ya tukio, tayari kulikuwa na mtu aliyepangwa kutuchukua asubuhi na kutupeleka moja kwa moja kwenye venue. Hivyo basi, tulipanga tukutane mapema ili tuwe pamoja kama timu na kuonekana wenye mshikamano.
Baada ya kumaliza kula, Sumaiya aliaga akielekea kulala, nikabaki na Hilda tukibadilishana mawazo na kucheka kidogo. Baada ya Sumaiya kuondoka, hata sisi hatukukaa sana tukashauriana tuondoke tukalale kwaajili ya kesho. Tulitoka wote na tukaelekea mpaka kwenye chumba changu, kwa sababu Hilda alikuwa na hamu ya kujua hata sehemu ninapolala. Tulipofika, hatukukaa sana, nikamsindikiza mara moja hadi kwenye chumba chake na nikaondoka.
Nilipokuwa nikirejea kutoka room ya Hilda, nilipita mbele ya chumba cha Sumaiya na kuamua kugonga mlango wake. Aliponifungulia, alionekana kustaajabu kidogo kuniona. Wakati huo alikuwa akizungumza kwa simu. Akanipa ishara ya taratibu kunialika ndani, nami nikaingia kimya kimya.
Baada ya kumaliza kuzungumza kwa simu, Sumaiya aliniangalia moja kwa moja machoni na kusema kwa sauti ya kejeli:
SUMAIYA: “Insider, unataka nini usiku huu?”
Nilitabasamu taratibu, nikasogea karibu naye. Wakati huo nilikuwa nimekaa kitandani, na yeye kasimama mbele yangu. Nikamvuta karibu kwa mikono yangu na kuizungusha kwenye kiuno chake.
MIMI: “Hujaelewa bado kilichonileta? Wewe sasa unakuwa kama mtoto.”
Alitoa kicheko cha dharau, akatikisa kichwa kisha akasema:
SUMAIYA: “Haiwezekani na huonekani kuwa serious, ndio maana nakushangaa.”
MIMI: “Take off your dress.” Kwa sauti ya chini.
Nilisimama na kuanza kuviminya vibatani vyake na aliishia kutoa kamlio ka utamu “Aaah”. Na nikamsukumia kitandani.
Nikaendelea kuongea pale,
“Sijaja kwa masihara. Kuna jambo moja muhimu sana nataka kusikia kutoka kwako leo.”
Sumaiya akavuta pumzi kwa nguvu, kisha akaniangalia kwa jicho la kushuku.
SUMAIYA: “Nilitaka kushangaa kwanza ulikuwa na Hilda. Unamuachaje mrembo kama Hilda akilala peke yake, halafu unakuja kwangu?”
MIMI: “Tuachane na Hilda, nakuomba uniambie kile ulichoniahidi na si vinginevyo.”
Akasita kidogo, kisha kwa sauti ya chini akasema:
SUMAIYA: “Kuhusu mama kuwa mpole, nitakwambia kila kitu. Ondoa wasiwasi kabisa.”
(Nilichokifanya kwa Sumaiya ni wanaume wachache wataelewa, kwanini nilifanya vile).
Tulizungumza mambo mengi sana usiku ule. Jambo kubwa ambalo Sumaiya aliniambia ni kuwa ni lazima niwe makini sana na mama Janeth. Alikiri wazi kuwa mama hakufurahishwa kabisa baada ya Iryn kuzaa na mimi. Sababu kuu, kama nilivyowahi kusimuliwa huko nyuma, ni kwamba mama alikuwa amemtafutia Iryn mchumba, ni kijana mmoja ambaye alimpenda sana na alitamani awe mkwe wake. Bahati mbaya, Iryn alimkataa, hadi sasa hakuwahi kujua kuwa ulikuwa mpango wa mama.
Sumaiya aliongeza kuwa kijana huyo alikuwa kipenzi cha mama, na hivyo kitendo cha Iryn kuzaa na mimi ni sawa na kuharibu ndoto yake. Zaidi ya hapo, alisema kwa sauti ya tahadhari, mali ambazo Iryn ameachiwa ni nyingi mno. Hivyo mama lazima awe na kinyongo na mimi.
Kisha akageukia suala la Lucy. Alinionya sana niwe makini naye. Alisema,
SUMAIYA: “Lucy si mtu wa kawaida kama unavyofikiri. Kila kitu chake kimeshikwa na Iryn.”
Nilimkatiza nikiwa na mshangao:
MIMI: “Ni nini kinaendelea? Sababu hata Asmah naye aliwahi kuniambia jambo kama hilo, kwa nini kila mtu ananiambia niwe makini na Lucy?”
SUMAIYA: “Tatizo lako ni kunichukulia kama snitch wako. Ila ukweli ni kwamba, katika watu wachache ninaowaamini, wewe uko pale juu. Umekuwa karibu nami na umetetea sana ugali wangu. Lakini jiulize, Lucy anapata kila kitu kutoka kwa Iryn, soon tu hapa amepewa iPhone 14 Pro Max, analipiwa kodi, anasomeshwa. Kwa akili ya kawaida, unadhani ataegemea upande wako?”
Nilinyamaza kwa muda,
MIMI: “Hapana, sio rahisi… kwakweli siwezi kumuamini kirahisi.”
Akanitazama moja kwa moja machoni.
SUMAIYA: “Hapo ndo nakwambia uwe makini. Na kuhusu wewe na Asmah… usinidanganye. Mimi ndiye wa kwanza kujua mmekulana, na ndio maana nilikuwa nakuuliza mara kwa mara huku ukikanusha.”
MIMI: “Uligunduaje hilo?”
SUMAIYA: “Kupitia simu yako na ulivyo mjinga, hata chat zako huzifuti. Unakumbuka siku ile nilikuomba simu nimpigie mama? Ulinitolea passcode yako mwenyewe. Nilipoingia, moja kwa moja nikaenda kwenye chats zako na Asmah, nikakuta kila kitu. Mpaka chats zako unaomba game kwa mara nyingine, niliziona.”
Nilikaa kimya, nikijaribu kukumbuka, na kweli nikakumbuka tukio lile,
MIMI: “Daah! Nimekumbuka asee, ni nini hasa sababu ya kufanya vile?”
SUMAIYA: “Nilitaka kuthibitisha mahusino yako na Asmah ili nimprove wrong alikuwa anakataa, wakati nilikuwa namsoma anakupenda. Niliona njia rahisi ya kuprove hili ni kupitia wewe na kweli nikafanikiwa. Sasa ninachokuambia ni hiki usiwaamini hawa mabinti kuwa makini, na Iryn anatumia pesa. Hata mimi akinipa hela lazima nikusnitch vizuri tu, cha muhimu wallet isome.”
MIMI: “Hata wewe uko tayari kunichoma kisa Pesa? Kweli nimezungukwa na wanafiki.”
SUMAIYA: “Ili uwateke hawa warembo acha kuwaogopa, kama Hilda, Nollie, Winnie… wote hao ni kuwatembezea mashine. Wewe usijifanye malaika.”
MIMI: “Sio kwamba siwezi, ila ni heshima tu ninayojipa. Ningekuwa mtu wa tamaa hata wewe ningekuweka ile siku.”
SUMAIYA: “Wewe muda wako bado. Lakini nakwambia ipo siku… na siku ambayo utaonja hii nyau yangu, sitakuacha salama, kila siku utaitaka.”
Nilicheka tu, nikampiga kofi la mzaha kwenye kario lake, kisha nikamuaga. Nilirejea chumbani kwangu nikiwa na mawazo mengi kichwani. Maneno ya Sumaiya yalikuwa yanazunguka kichwani mwangu, na kadri nilivyotafakari, ndivyo nilivyoona huenda kweli akawa sahihi. Sasa ilikuwa wazi nilihitaji kuwa makini sana, na huenda imefika wakati wa kuanza kufuatilia kwa karibu kila jambo.
******
Asubuhi ile niliamka mapema mno, nikaanza kujiandaa kwa umakini wa hali ya juu. Nilivaa suti ya dark blue, shati safi la navy blue, viatu vya ngozi vya black, mkanda mweusi uliolingana, na kukamilisha muonekano wangu kwa red tie pamoja na red pocket square. Nilipomaliza kujitazama mbele ya kioo nilijisemea kuwa leo nimependeza kweli kweli. Hata dada aliyekuja kunichukua na kunipeleka kwenye ukumbi alishindwa kujizuia, akabaki kunisifia kwa tabasamu la dhati.
Tulipofika venue, dada yule aliniaga kwa bashasha, nami nikamkonyeza kwa utani mdogo. Hilda, ambaye sikuwa nimemuona akikaribia, alitokeza ghafla na kabla sijapata nafasi ya kuzungumza, alianza kunimwagia sifa kedekede.
“Insider, umependeza sana asee! Hadi sasa hakuna anayekufikia, baba. You look so smart and handsome.”
Nilitabasamu nikimuangalia. Hilda naye alikuwa wa kipekee siku hiyo, kwani alipendeza sana kwa muonekano wake, suti aliyovaa ilionyesha umbo lake vyema, kweli alikuwa mashallah.
“Nashukuru sana mummy, ila na wewe umependeza sana. Leo madirector watapata tabu sana.”
Muda huo ulikuwa saa mbili kasoro asubuhi, wageni wakianza kuingia taratibu ukumbini. Wengi wao walikuwa watu wa hadhi kubwa, wafanyabiashara na sura ambazo huoni kila siku. Na hoteli yenyewe ni five star! What else do you expect?.
Mara tukasikia sauti ya Sumaiya ikituita, akija kwa bashasha tele tulikosimama;
“Good to see you guys!” alisema akitukumbatia kwa pamoja.
Kweli tulikuwa tumependeza kupita maelezo, na hatukusita kuomba tupigwe picha ya pamoja. Baada ya hapo, nilimuomba kupata picha chache za peke yangu, kwa lengo maalum la kumtumia wife na Iryn.
Mara tu baada ya kupigwa picha, nilimtumia Iryn na mama Junior, nikawaandikia ujumbe mfupi “Good morning mama Aria”, kwenda Iryn. Na “Good morning mama Junior” kwenda kwa wife.
Muda huo tulianza kusalimiana na wageni mbalimbali mle ukumbini, kila mmoja akijitambulisha na kufahamiana kwa namna moja au nyingine. Nilipokuwa nikipita katikati ya makundi ya watu, macho yangu yalivutwa na dada mmoja mrembo aliyekuwa amesimama pembeni, peke yake kana kwamba hakuwa na shauku ya kile kilichokuwa kinaendelea. Alionekana mpole, ila muonekano wake ulikuwa na mvuto wa kipekee.
Nikasogea taratibu hadi usawa wake, nikamtolea tabasamu na kumsalimia kwa ucheshi kidogo:
“Good morning, my name is Insider from XX Investment Ltd in Dar es Salaam, and I am the Finance Manager. May I kindly know if we have met before?”
Alinitazama kwa tabasamu la aibu, kisha akajibu kwa sauti ya upole;
“I don’t remember if we have met before, but thank you, Insider. My name is Savinna from ZZ Microfinance in Dar es Salaam, and I serve as the Human Resource Manager.”
“Wow! Am very interested in your company, and I would appreciate the chance to learn more about your services.”
“Don’t worry, Mr. Insider, we will arrange this. I would also like to know more about your company.”
“Bye! Have a nice session ahead of you.”
Thank you!” alijibu akicheka kidogo.
Nilipoanza kuondoka, nilijikuta nikiendelea kumuangalia kwa sekunde chache zaidi, kana kwamba macho yangu hayakutaka kuachana naye haraka. Lakini mara nilipogeuka, nikakutana uso kwa uso na macho ya kina Sumaiya. Walikuwa wakinitazama kwa tabasamu la kutaniana, kwamba walikuwa wameshuhudia mazungumzo yote. Nilitabasamu kwa aibu ndogo, kisha nikaenda moja kwa moja kumsalimia mtu mwingine.
Nilipata nafasi ya kumsalimia Mr. George, ambaye ni Chief Accountant wa Twiga Cement Company. Mazungumzo yetu yalikuwa ya kuvutia sana kiasi kwamba tulijikuta tukipiga story nyingi hadi mwisho tukabadilishana namba za simu. Mpaka sasa ninavyoandika, amekuwa mmoja wa watu wangu wa karibu sana.
Baada ya muda mfupi, kikao kilianza rasmi kwa utambulisho kutoka kwa waandaaji. Walitoa maelezo mafupi kuhusu Agenda kuu ya mkutano, ambayo ilikuwa kutengeneza mitandao ya kibiashara (business connections), kushirikiana uzoefu, na kujadili fursa mpya za ushirikiano.
Kikao hiki kilihudhuriwa na makampuni maarufu kutoka Tanzania, Zanzibar, na maeneo mengine ya Afrika Mashariki kwa ujumla, pamoja na wageni waalikwa kutoka Ulaya na Marekani. Makampuni zaidi ya 60 yalishiriki kwenye mkutano huu, idadi ya mahudhurio ikiwa zaidi ya watu 110. Pia, kulikuwepo wawakilishi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na viongozi mbalimbali kutoka bara.
Mara baada ya utambulisho wa waandaaji kukamilika, ikawa zamu ya kila mshiriki kujitambulisha binafsi pamoja na kampuni anayowakilisha. Kila mmoja alisimama kwa heshima na kutoa maelezo mafupi kuhusu nafasi yake na taasisi aliyoitoka.
Baada ya zoezi hilo kukamilika, kikao kikaanza rasmi kwa utulivu mkubwa na hadhi ya kipekee, kila mmoja akiwa makini kufuatilia na kutarajia kupata jambo jipya lenye manufaa.
Ilipofika saa nne asubuhi, kikao kilisitishwa kwa mapumziko ya breakfast ya takribani saa moja. Wakati huo nilitoa simu yangu kuangalia ujumbe, nikakuta Iryn tayari alikuwa amereply message niliyomtumia awali. Alinionyesha upendo na kunisifia sana kwamba nimependeza, akapamba ujumbe wake kwa makopa mengi ya upendo, kisha akaniambia nikitoka mapumziko nipige simu.
Bila kusita, nilimpigia video call, haikuchukua muda, akaipokea akiwa na tabasamu lake zuri lililonifanya nisisimke. Mara akasema kwa sauti yake nzuri na upole;
“My darling baby daddy, you look like a real gentleman. Leo umenifurahisha sana! Why don’t you wear suits more often? Suits make you look even better, baby.”
Maneno yake yalinifanya nitabasamu kwa furaha isiyo na kifani. Wakati bado tuko kwenye mazungumzo, Hilda na Sumaiya walikuwa wamesogea karibu. Mara Iryn akawaona na akaanza kutupongeza wote, akisema kwa dhati kwamba tumependeza mno siku hiyo.
Kwa upande mwingine, nilipokea taarifa kutoka kwa Ghati kwamba tayari alikuwa Ferry, akisubiri boat ya kuelekea Zanzibar. Nilitumia muda huo kuwasiliana na dereva aliyetupokea jana na kumpa taarifa za ujio wa mgeni wangu, kwa sababu tayari nilikuwa nimempangia mapema jukumu la kumchukua mara atakapowasili.
Kikao chetu cha siku ya kwanza kilimalizika saa 12 kamili jioni. Mara tu baada ya kumalizika, nilitoka kwa haraka kuelekea reception kwa sababu Ghati tayari alikuwa amewasili na amesubiri muda mrefu.
Wakati natoka nje ya ukumbi, ghafla nikakutana na mmoja wa waandaaji wa event, Mr. Graham, mzungu mwenye tabasamu la kibiashara. Tulisimama tukaanza kuzungumza. Aliniambia kwamba alifurahishwa sana na hoja nilizochangia kuhusu uwekezaji, na akasisitiza kwamba baada ya seminar yetu kumalizika angependa tupate muda wa mazungumzo zaidi.
Mazungumzo yetu yalichukua dakika tano tu kabla hatujaagana kwa heshima. Nilipotoka na kutembea hatua chache kuelekea mlango mkuu, ghafla nikasikia mtu akinita:
“Mr. Insider…”
Nilipogeuka, nikamuona Savinna akija kwangu kwa mwendo wa taratibu, nikasimama palepale hadi aliponikaribia.
SAVINNA: “Nakuona upo spidi sana, unawahi wapi?”
Kwa sekunde kadhaa nilibaki kimya, kwanza sikutarajia kumuona tena muda huo, na pili sikutaka ajue haswa nilichokuwa nakimbilia.
MIMI: “Room yangu ipo mbali kidogo, ndiyo maana unaona niko spidi.”
SAVINNA: “Pole sana. By the way, tuliongea lakini hukuacha business card yako.”
MIMI: “Bahati mbaya siko nayo, lakini si vibaya ukinipa simu yako nikuandikie namba yangu.”
Akanipatia simu yake, nikamwandikia namba yangu na mara moja akanipigia ili na mimi niihifadhi yake. Tulipokuwa tukimaliza, macho yangu yakavutiwa mbele, nikawaona Hilda na Sumaiya na wengine wawili wakija kuelekea pale tuliposimama. Walipofika, tukaendelea mazungumzo kwa pamoja kwa dakika chache kabla Savinna kuamua kuaga.
Baada ya wageni kuondoka, Hilda akanigeukia na kwa utani akasema:
“Tunakutafuta kumbe upo huku nje unaongea na mrembo.”
Nilitabasamu tu, lakini hata sikuwa na habari nao maana nilijua nilikuwa na haraka. Ghati alikuwa amenisubiri vya kutosha, na sikutaka kuongeza muda zaidi.
MIMI: “Guys, nawacheki soon kwa ajili ya dinner.”
Niliwaacha pale wakiwa na tafsiri zao, kisha nikaelekea moja kwa moja reception. Umbali haukuwa mrefu, na mara tu nilipofika nikamuona Ghati amekaa kwenye sofa, amejiegemeza kwa utulivu huku akionekana amechoka na safari yake. Tulipokutana macho, alisimama haraka, na tukasalimiana kwa kukumbatiana kwa furaha.
Ghati alikuwa amependeza kupita maelezo. Lakini cha kufurahisha zaidi, yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kunimwagia sifa nyingi. Alishangazwa na muonekano wangu wa suti, kwa hakika hakuwa akitarajia kuniona vile na furaha yake ilidhihirika wazi machoni.
Tulikaa pamoja kwenye sofa pale reception, nikatamani kutumia muda huo mfupi kujua hali ya nyumbani, hali ya mama, mtoto na yeye mwenyewe.
MIMI: “Nilijua kabisa ungekuja na mtoto, umemwachia nani?”
GHATI: “Mkubwa yule, kwasasa yuko kwa dada yangu. Unajua sasa hivi sina dada pale nyumbani.”
MIMI: “Pole sana, Ghati. Pia samahani kwa kukusubirisha sana hapa, kama unavyoona nimetoka kikao muda si mrefu.”
GHATI: “Usijali, Insider. Ulishanieleza mapema kuhusu hili, kwa hiyo sina wasiwasi kabisa.”
Nilimtazama tena, nikashindwa kujizuia kusema kwa dhati:
MIMI: “You look beautiful and sexy.”
Ghati alianza kutabasamu pale na mimi nilimshika mkono wake nikawa nachezea vidole vyake;
GHATI: “Jamani, thank you, Insider. Nimefurahi sana kukuona leo.”
Nikiwa naongea na Ghati simu ya Hilda ilikuwa ikiingia wakati huu, lakini nikaipiga chini sikutaka kuipokea. Nikamwambia Ghati tuondoke, nikampa ishara mhudumu aje kutusaidia kubeba bag hadi chumba changu.
Tulipofika, Ghati aliingia bafuni kuoga, kisha akalala kutokana na uchovu wa safari yake. Mimi, kwa upande mwingine, nilikaa nikishughulika na laptop yangu nikiandaa ripoti ya kikao cha siku ya kwanza (Day 1).
Ilikuwa ni saa moja usiku, ghafla nikasikia mlango ukigongwa. Niliposogea kufungua, nikakutana na Hilda na Sumaiya, wakiwa wamesimama mlangoni kwa tabasamu na, wakiomba kuingia ndani.
ITAENDELEA
Edo kissySEASON 03