SEASON 03
CHAPTER 7
CONTINUE:
Saa 8 mchana tuliondoka hotelini tukielekea Stone Town kwa usafiri wa hoteli, tayari kwa safari ya kurudi Dar es Salaam kwa kutumia boat. Tulipofika Dar, niliagana na Ghati ambaye alichukua bolt kuelekea Mbweni, huku mimi nikipanda bolt nyingine kunipeleka JNIA, tayari kuanza safari yangu ya kuelekea South Africa.
Baada ya kufika Airport terminal 3, nilikamilisha taratibu zote za check in na maandalizi mengine, nikiwa tayari kwa safari yangu kwa ndege ya saa 3 usiku.
Niliamua kutulia pale BAO Café, nikijipatia kikombe cha kahawa ili kuuchangamsha mwili huku nikiendelea kusubiri muda wa kuondoka. Wakati nikiwa hapo, nilikuwa naongea na Iryn kwa simu, naye alikuwa anataka kujua muda hasa wa kuondoka kwangu. Nikamwambia kwa utulivu kwamba safari yangu ilikuwa saa 3 usiku.
Baada ya maongezi na Iryn kukoma, nilibaki kimya nikitafakari mambo yangu binafsi. Kitu kilichonichanganya zaidi ni lile suala la mtoto na Mary. Kauli yake ilinisumbua sana, kwani alinisisitiza niongee na mdogo wake, Prisca, ili ajue ukweli na ndipo awe tayari kunizalia mtoto. Nilijiuliza mara nyingi, kwa nini Mary mwenyewe hakuona haja ya kuchukua hatua hiyo badala ya kunisukumia mzigo wa maelezo kwa mdogo wake? Hapo ndipo nilipoona wazi kuwa jambo hilo lingekuwa gumu mno kufanikisha.
Nilimpenda Mary na nilitamani kweli anizalie mtoto. Tayari Iryn alikuwa amenizalia mtoto mmoja, lakini kwa historia ya maisha yake, sikuona kama angeweza kunizalia wa pili. Nami, kwa upande wangu, nilikuwa na ndoto ya kuwa na watoto wengi. Ndiyo maana nikaanza kumwona Mary kama mtu sahihi wa kuwa mama wa watoto wangu.
Lakini kadiri nilivyozidi kutafakari, niliona hatari iliyojificha. Kwa kuwa tayari nilikuwa na historia na mdogo wake, halafu nikazaa na Mary, hali hiyo ingeweza kusababisha mgongano mkubwa wa kifamilia. Niliona mbali mpaka kwenye uwezekano wa uhasama mkubwa ambao ungeweza kuvunja familia yao.
Hatimaye, nikaona huu mpango wa kuzaa na Mary ulikuwa wa hatari na si rahisi. Nikauweka pembeni, na badala yake nikaelekeza mawazo yangu kwa Ghati. Yeye nilimwona ana sifa zote zinazoweza kumfanya awe mama bora wa watoto wangu.
Wakati nikiwa bado nimekaa pale Café, simu ya Dullah iliingia, bila kusita nikapokea.
MIMI: “Hello brother, najua unataka umbeya, huna jipya.”
Dullah alicheka kwa nguvu, kisha akasema:
DULLAH: “Umejuaje Senior? Yule mtoto namuelewa sana, ila sasa hivi ameshakuelewa wewe zaidi.”
MIMI: “Hahaha! Wewe ms*nge, si ungesema kama unamtaka? Mimi ningekuweka kama nilivyofanya kwa Latifah.”
DULLAH: “We acha mchezo, mimi nimeoa tayari. Halafu shemu wako ana mimba, siwezi kujiingiza kwenye upuuzi kwa kipindi hiki.”
MIMI: “Umekula sana pisi za Uber, leo unajiona Padre.”
Dullah hakujali, akabadili mada mara moja,
DULLAH: “Hebu niambie, kimekuaje huko Zanzibar na mtoto Ghati?”
MIMI: “Ahh, oyaa… alininunia kwanza, ila baadaye mwenyewe akaachia, nikapewa niilambe mwenyewe. Lakini ukweli, yule dada ni mtamu sana wallahi. Unajua hata ile siku ya kwanza siku-enjoy kama safari hii ya Zanzibar?.”
DULLAH: “Daah! We ms*nge, kweli mganga wako sio tapeli, una nyota kali sana. Inabidi uongee vizuri na mama yako akufunulie siri.”
MIMI: “Hahaha! Shida ni kwamba kanizidi miaka, na gap kubwa sana six years.”
DULLAH: “We fala nini? Sasa miaka sita ni mingi? Nimeshakueleza mara ngapi, yule manzi ni asset. Muweke kwenye himaya yako, hao akina Prisca na wengine waache tu. Tulia na Ghati, hata kama ni kama mchepuko, lakini ni wa maana.”
MIMI: “Kwa hiyo unanifundisha uhuni sasa?”
DULLAH: “Acha masihara, wewe ni mhuni asili. Na bahati yako kubwa ni hiyo unakutana na warembo wakali kila mara.”
Mazungumzo yetu yaliendelea kwa muda mrefu sana. Nilimueleza kwamba nipo Airport, nikisubiri safari ya kuelekea South Africa kumsalimia mama watoto. Baada ya hapo, nilimwambia mpango wangu wa kupita Zambia kuonana na mzee wangu, ili nimweleze kwa uwazi suala la Iryn. Dullah kwa upande wake alinitakia safari njema, akaniambia niende nikiwa na moyo wa ujasiri, nitafanikiwa na tukaagana pale.
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimaye saa tatu na nusu usiku tulianza safari ya kuelekea South Africa. Nilipata kiti cha dirishani, na upande wangu wa kulia alikaa mama mmoja wa Kitanzania, huku kiti cha mwanzo kabisa kikichukuliwa na kijana ambaye hakuwa Mbongo.
Yule mama alikuwa mchangamfu, na tulianza kuzungumza mara moja. Aliuliza ninakoelekea, nikamweleza kwamba safari yangu ilikuwa Cape Town. Naye akanieleza kwamba yeye anaishia Johannesburg. Mazungumzo yetu yaliendelea, akanitaka nimwambie mishe zilizonileta South Africa. Nikamjibu kwa ufupi kwamba ni masuala ya biashara, naye akasema safari yake ilikuwa ya kumfuatilia kijana wake aliyekuwa akisoma chuo kule.
Katika mazungumzo hayo, niligundua yule mama alikuwa na majonzi makubwa moyoni. Alisema tangu kijana wake aende kusoma South Africa, amebadilika sana na kujiingiza kwenye makundi mabaya, hali iliyompelekea kufeli na ku-discontinue masomo yake. Kwa sauti ya msisitizo na uchungu, alinieleza kuwa lazima tuwe makini sana tunapopeleka watoto kusoma nje ya nchi, kwani wengi huangukia kwenye vishawishi na kuharibika.
Tulizungumza mambo mengi sana, nikamueleza kuhusu kampuni ninayofanyia kazi na shughuli zangu zingine za kibiashara. Kuhusu yeye, nilikuja kugundua kwamba alikuwa mfanyakazi wa serikali, akifanya kazi kwenye moja ya taasisi kubwa iliyoko mkabala na jengo la TPA.
Tulipofika Johannesburg, tulilazimika kuagana pale, kwani mimi na wengine tulikuwa tunaendelea na safari ya Cape Town. Mama alinipa namba yake ya simu na mimi nikampa yangu kisha akaondoka.
Tulipumzika Johannesburg kwa zaidi ya saa moja. Katika kipindi hicho nilipata nafasi ya kukutana na rafiki yake Tyna ni yule jamaa aliyewahi kutusaidia mimi na dada yangu tulipokuwa tukimtafuta Iryn kipindi kile. Alikuwa maeneo haya ya airport, na tulipiga naye stori nyingi sana, kitu kikubwa alichonieleza ni kwamba bado anawasiliana sana na dada yangu. Wakati huo huo nilikuwa nachat na Iryn, ambaye aliniahidi kwamba atakuja kunipokea nikiwa Cape Town. Akanisisitiza nikianza safari nimjulishe.
Baada ya lisaa limoja la kusubiri, safari iliendelea. Baada ya takribani masaa mawili ya ndege kuruka kutoka Johannesburg, hatimaye tulifika salama Cape Town, ambako nilitarajia kukutana uso kwa uso na Iryn baada ya muda mrefu wa ukimya.
Saa 11 alfajiri ndiyo, tunashuka kwenye ndege, na nilichukua takribani dakika 40 kukamilisha taratibu zote za ukaguzi. Wakati nikiwa bado ndani naendelea na taratibu zingine, nilipokea ujumbe wa Iryn akiniambia ameona ndege yetu imetua na kwamba ananisubiri karibu.
Nilipomaliza taratibu na kuelekea kutokea, ghafla nikasikia sauti ya Samantha ikiniita kwa sauti,
“Brother in law…!”
Sauti hiyo ya Samantha iliwavuta watu wengi waliokuwa jirani kutazama upande wake. Nilipomwona, moyo wangu ulijawa furaha, kisha nikasogea haraka hadi alipokuwa, tukakumbatiana kwa furaha. Lakini la kushangaza, Iryn hakuonekana, badala yake, Samantha ndiye aliyekuwa akitumia simu ya Iryn.
“Ndiyo nilikuwa nina-chat na wewe muda wote?”
Samantha akatabasamu huku akitingisha kichwa, kisha akasema kwa upole:
“Dada hataki niwe na namba yako.”
Samantha hakuwa peke yake. Alikuwa ameongozana na dada wa kazi wa nyumbani, na mara moja tukachukua Uber kuelekea nyumbani. Hali ya hewa ilikuwa baridi na manyunyu madogo ya mvua yalikuwa yakinyesha taratibu. Safari haikuwa ndefu, na ndani ya dakika 20 tulikuwa tayari tumewasili.
Nilipokaribishwa ndani, macho yangu mara moja yalivutwa kwa Iryn aliyelala usingizi mzito kwenye kochi la sebule. Nilisogea karibu naye nikamgusa taratibu huku nikimnong’oneza,
“Mummy, wake up daddy Aria is here.”
Samantha alibaki akitabasamu pembeni, huku Iryn akijivuta taratibu kuamka. Alionekana mchovu kama mtu ambaye hakulala usiku kucha.
MIMI: “Mbona umelala hapa sebleni kunisubiri? Mimi ningefika tu ningekuita.”
Alikuwa akihangaika kufumbua macho yake na kwa sauti ya chini alinisalimia,
IRYN: “Hi mbona umechelewa sana?”
MIMI: “Tumechelewa kutoka Dar es Salaam, pia tumekaa muda mrefu sana Johannesburg Airport.”
IRYN: “Twende ndani chumbani ukamuone binti yako.”
Niliposogea chumbani, nilimkuta mwanangu Aria amelala fofofo. Nilishika mashavu yake kwa upole, nikafarijika kuona afya yake njema. Iryn akaniangalia na kusema kwa sauti ya mama mwenye majukumu mazito,
IRYN: “Usione amelala hivi… usiku silali, huyu dogo ananisumbua sana.”
MIMI: “Hayo ndiyo matunda ya kuwa mama. But you look great… and sexy.”
Maneno yangu yalimfanya atabasamu na kulaza kichwa chake mapajani kwangu. Niliendelea kumchezea nywele zake nzuri, nikigusa shingo yake hadi masikioni.
IRYN: “Baby, tulikumiss sana.”
MIMI: “Tangu niondoke, hata wiki mbili hazijapita.”
IRYN: “Kwangu ni kama mwaka mzima.”
MIMI: “Kidonda chako kimepona?”
IRYN: “I’m okay now… mwanzoni kukojoa ilikuwa vita.”
MIMI: “Let me see.”
Alinitazama, kisha akatabasamu kwa aibu na huzuni kwa pamoja. Hatimaye alikubali kuonyesha na nikaridhika kuona maendeleo yake.
IRYN: “Unaikagua mali yako, eeh?”
MIMI: “Naona ushapona, leo najua utanibless niichape.”
IRYN: “Thubutu! Hapo lazima zipite miezi mitatu kwanza, ndo upate mali yako uitumie.”
Tukaishia kucheka wote wawili pale kitandani. Mazungumzo hayakuendelea sana, kwani Iryn alionekana mchovu sana. Hatimaye tukalala wote wawili, nikiwa nimekumbatia, na mwanangu Aria akiwa mbele yake.
Saa nne asubuhi niliamshwa ili niende dining room kupata kifungua kinywa. Nilipokuwa naendelea kunywa chai, Samantha alijiunga nami na akanipa kampani. Tulikaa pamoja, tukipiga stori za hapa na pale huku tukicheka mara kwa mara. Jambo moja lililonifurahisha zaidi ni pale aliposema kwa mzaha kwamba Aria amerithi upole kutoka kwangu. Kauli ile ilitufanya tufurahi sana na tukaishia kucheka kwa muda mrefu.
Haikupita muda mrefu, Momo bibi yake Iryn aliingia sebleni akiwa amembeba mjukuu wake Aria. Muda huu nilikuwa nimemaliza kunywa chai, hivyo nilisimama na kwenda kumsalimia kwa heshima,
MIMI: “Isin attam?”
MOMO: “Nagaa keesani hoo?”
Tulianza maongezi, ingawa ilikuwa ngumu kidogo kwa sababu ya changamoto ya lugha. Bahati nzuri Samantha alisimama kama mkalimani wetu, na kwa msaada wake mazungumzo yetu yaliendelea kwa muda mrefu zaidi.
Wakati tunazungumza, nilikuwa nimembeba mwanangu Aria mikononi. Alikuwa ananitazama kwa macho ya kupendeza huku akijinyosha nyosha kwa tabia za kitoto. Ukweli ni kwamba nilifurahia sana kuwa nae muda ule, nikimuona na kumshika mwanangu, kulinipa furaha kubwa na nikajikuta natabasamu muda wote bila kujizuia.
Baada ya maongezi marefu na Momo, nilimuaga kwa heshima na kwenda kupumzika kidogo, kwani mwili bado ulikuwa na uchovu wa safari na usingizi haukuwa umetulia vizuri.
Siku hiyo yote iliishia kwangu nikicheza na binti yangu Aria na kitendo hiki kilinipa faraja isiyo na kifani. Ndani yangu nilihisi nguvu mpya ya msukumo wa kuhakikisha kila kitu kinakuwa wazi, ili Junior na Aria wajuane na hatimaye wajenge bond ya kindugu.
Kwa upande wa Iryn, alionekana kufurahia sana kuniona nikicheza na binti yetu. Mara kwa mara alikuwa akinitazama kwa tabasamu na kusema kwa sauti ya furaha, “Yes, daddy…”.
******
Kesho yake saa nne asubuhi niliondoka na mama Aria kwenda hospitali kwa ajili ya clinic ya mtoto na yeye pia kuangalia maendeleo yake kiafya kwa ujumla. Hospitali tuliyoenda ni ileile aliyojifungulia siku za nyuma, na tulipofika pale tulipokelewa vizuri sana na wahudumu wa afya kwa tabasamu na ukarimu mkubwa.
Tulianza na clinic ya mtoto ambapo, Aria alipimwa uzito, hali yake ya lishe, na afya kwa ujumla. Aria alionekana kuwa na maendeleo mazuri sana, afya yake ilikuwa salama na daktari alimsifu Iryn kwa jinsi anavyo mnyonyesha mtoto vizuri.
Baada ya kumaliza upande wa mtoto, tulihamia kwa mama Aria. Aliangaliwa kwa makini, wakiangalia hali yake ya jumla pamoja na kidonda chake cha kujifungua. Madaktari waliridhika kuwa anaendelea kupona vizuri. Wakati yote haya yanaendelea, mimi nilikuwa pale pembeni nikishuhudia kila kitu. Kwa mzaha nikamuuliza muuguzi:
“Nurse, you said her wound is healing well, does that mean I can finally put my stick in?”
Yule muuguzi alikuwa mzungu, alinitazama kwa mshangao, akijaribu kujizuia kucheka lakini mwisho wa siku alishindwa na akaishia kutabasamu tu. Hakuwa ametarajia swali la mzaha kama hilo kutoka kwangu. Iryn alibaki akicheka kwa sauti ya chini huku akinitazama kwa tabasamu la aibu. Nikaendelea kuongea,
“Yes baby, you know I miss you so much.”
Muuguzi, alitabasamu kwa furaha kisha akasema:
“I’m really sorry, but please be patient until she makes a full recovery. It won’t be too long, okay?”
Nikajibu kwa sauti ya upole,
“Thank you, doctor, you know how much I love her, and I feel so lucky to have such a beautiful woman in my life.”
Akacheka na kuongeza,
“Of course, and I’m sure she’s really excited to have you.”
Sote tuliishia kucheka pale.
Baada ya kumaliza taratibu zote, tulipimwa damu sisi wote. Japo nilikuwa na wasiwasi ndani kwa ndani, kama matokeo yatakuja hovyo, lakini matokeo yalipokuja yalitufurahisha kwani wote tulikuwa salama kabisa.
Baada ya kutumia karibu masaa mawili pale hospitalini, tuliondoka na moja kwa moja kuelekea supermarket ili kununua mahitaji ya nyumbani. Tulitumia nusu saa kufanya manunuzi na tulipomaliza, tulirudi nyumbani tukiwa tumechoka lakini wenye furaha.
Jioni ilipofika, mimi na Iryn tulikaa kwenye balcony kwa ajili ya mazungumzo. Upepo mwanana ulivuma taratibu, na mandhari ya eneo lote yalionekana vizuri sana kutoka pale juu. Nyumba anayokaa Iryn ipo kwenye eneo la kifahari sana, unaweza kulilinganisha na Masaki kwa hapa kwetu. Nyumba zimepangwa kwa mpangilio mzuri, miti ya kupendeza imepandwa kwa ustadi, barabara ni safi, na hewa ni safi. Nilijikuta nashindwa kuvumilia na kuanza kumuuliza maswali.
MIMI: “Baby, hivi kodi hapa unalipaje?”
IRYN: “Hii ni nyumba yetu, ni moja ya mali za baba.”
Kauli hiyo ilinifanya nikabaki kimya kwa muda mfupi, nikiendelea kushangaa mazingira. Ndani ya fensi kulikuwa na block tatu, kila moja ikiwa na ghorofa mbili, hivyo jumla kulikuwa na apartments sita, zote zikiwa zimekaliwa. Nilichopenda zaidi ni jinsi zilivyojengwa, kila apartment ina privacy yake ya kipekee bila usumbufu wa majirani.
Baada ya sekunde chache za kimya, niliendelea kumuuliza:
MIMI: “Hukunambia ni za baba yako. Sasa gharama zake zikoje kwa mtu anayetaka kupanga apartment hapa?”
IRYN: “Mfano, hapa kwetu sisi tunacharge $5,500 kwa apartment na ni fully furnished, pia bei zinategemea ukubwa wa apartment na location, kama unavyoona Dar.”
MIMI: “Aisee, hii ni investment nzuri kweli. Na wanaoishi hapa ni Wasouth African?”
MIMI: “Hapana, mimi huwa sifuatilii sana maana kuna kampuni maalum inashughulika na mambo yote ya kodi na wapangaji. Ila najua apartment ya kwanza yote imechukuliwa na Waportuguese. Ya pili, chini wanaishi Wanaigeria, juu sijui. Na hii tunayokaa sisi, chini kuna dada black American ambaye anafanyia kazi KFC.”
MIMI: “Baba yako ana nyumba kubwa sana. Kwanini hukutaka kuishi karibu naye?”
IRYN: “Mimi sasa hivi ni mtu mzima. Pia nahitaji uhuru wa kuishi maisha yangu. Fikiria, kama ningekuwa naishi na baba yangu, kweli ungekuwa na confidence ya kuja kunitembelea na kukaa kwa uhuru kama tulivyo hivi sasa?”
MIMI: “Hapana, nisingeweza kuwa na hii confidence.”
IRYN: “Ndiyo maana nikaamua kuishi peke yangu, pia, hii inampa uhuru stepmother. Usiwaze sana, unajua stepmother anapretend sana kunipenda, ukweli, anatamani hata nisiwepo duniani. Ndomana sikutaka hata kujifungulia mtoto pale home sababu najua yule mama asingefanya kitu chochote kwa upendo.”
MIMI: “Kwanini afanye hivyo?”
IRYN: “Mimi ndiye msimamizi wa mali zote za baba. Asilimia kubwa ya urithi ipo chini yangu ikilinganishwa na watoto wake. Unadhani kweli atanipenda? Juzi tu nimegundua alikuwa anakwapua pesa kwenye kampuni bila sababu ya msingi. Nilipomkanya, hasira zikampanda juu, yaani sahivi amenichukia kabisa.”
MIMI: “I understand, naona atakuja kuwa mwiba kwako huko mbeleni. Tuachane na haya embu tuanze kuzunguma mambo muhimu.”
Baada ya kumaliza mazungumzo ya awali, sasa tulihamia kwenye suala la kampuni ambayo tunataka kuirudisha kwenye umiliki halali, na hapa ndipo Iryn alinipa taarifa mpya kabisa ambazo zilinishtua kidogo.
IRYN: “Nisikilize kwa makini, nakupa taarifa nilizonazo hadi sasa, Aprili 2022 kampuni ililipwa TZS 3.2 billion, na mwezi wa Julai 2022 kampuni ililipwa tena TZS 1.9 billion. Malipo yote haya yaliingizwa moja kwa moja kwenye account ya kampuni.”
Alipokuwa akisema hivyo, Iryn alitoa simu yake na kunionesha bank statement zenye ushahidi wa malipo hayo. Nilipoyaona macho yangu yalipanuka kwa mshangao. Kilichonichanganya zaidi ni jinsi alivyoweza kupata taarifa nyeti kama hizo.
MIMI: “Baby, hizi taarifa umezipataje? Kwa kweli unanitia presha.”
IRYN: “Hii ni international bank, kuna mtu ambaye niliwasiliana naye na akanisaudia kuzipata.”
Nilipigwa na butwaa, kwani Iryn alionekana kujiamini sana, kana kwamba anajua kila kitu kinachoendelea.
MIMI: “Na kuhusu hayo malipo, ni kazi gani hasa ilifanyika hadi kupelekea kulipwa kiasi hicho?”
IRYN: “Unakumbuka mwaka jana tulipokuwa pale Coral Beach Hotel? Nakumbuka nilikwambia kuhusu kampuni ambazo baba alikuwa anamiliki. Nilikwambia kampuni alizofunga, na akaiacha hii moja inayohusika na umeme kwa sababu haikuwa inategemea tender za moja kwa moja kutoka serikalini. (SEASON 1, EP10)
Sasa, mwaka 2019, kampuni ilipata tenda kubwa ya kusambaza generators na kuyaunganisha na mfumo wa umeme wa automatic. Generators zilisambazwa kwenye hospitali, taasisi mbalimbali kote nchini. Ilikuwa ni tenda yenye pesa nyingi sana.”
Alinyamaza kidogo kisha akaendelea kwa sauti ya chini zaidi:
“Lakini ghafla, Mr. President aliposhtukia kuwa kulikuwa na upigaji mkubwa kwenye hizi tender, aliamuru malipo yote yasimamishwe hadi uchunguzi utakapo kamilika. Kampuni ya baba yangu nayo ikawa miongoni mwa zilizoathirika.”
MIMI: “Hiyo ndiyo sababu ya kampuni kucheleweshewa malipo au kuna nyingine?
IRYN: “Kabla sijakujibu, Insider, nakupa mfano mmoja rahisi sana. Unajua hizi biashara zina siri nyingi sana. Na wakati mwingine, kama manager au Director, ili kampuni yako iendelee kukua, unaweza kujikuta unakubaliana na masharti yaliyopo mbele yako bila kupenda.
Fikiria hivi: wewe una kampuni yako, unataka tender kubwa, na unahitaji $100 kwa kazi. Kisha mtu anakwambia, ‘Sawa, lakini kwenye invoice zako utaweka $120 badala ya $100.’ Utafanyaje?”
MIMI: “Hapana, siwezi kukataa. Siwezi kuacha tender ipite kisa hiyo sababu ndogo. Kwahiyo kampuni ilifanya huo mchezo ndo kusababisha haya yote?”
IRYN: “Kampuni ilishinikizwa kufanya hivyo kutoka kwa wahusika, mchezo ulijulikana ndo kupelekea malipo yao yote yakawa pending hadi uchunguzi ukamilike.”
Hapa sasa nikaanza kukumbuka matukio mbalimbali ya Mr president kusimamisha miradi mingi sana ambayo ilihisiwa kuwa na upigaji. Nikakumbuka vilio vya makampuni mengi nchini yakidai malipo yao na kupelekea makampuni kufungwa.
MIMI: “Sawa, sasa uhuni ulifanyika 2021, ni nani ambaye alikuwa anafuatilia hadi kulipwa?
IRYN: “Hapo mimi na wewe hatujui, who was the mastermind behind all of this, soon tutajua.”
MIMI: “Swali langu ni kwamba, hadi kampuni inabadilishwa umiliki yeye alikuwa wapi?”
IRYN: “Baba alikata tamaa kwenye hii kampuni, alijua kulipwa itakuwa ngumu kutokana na danadana kuwa nyingi. Walifuatilia kwa nguvu sana mwanzoni, lakini baadaye wakakata tamaa. Mzee akaacha kila kitu mikononi mwa Director mwenzake hata afya yake haikuwa sawa”
Nilimsimamisha haraka mara tu niliposikia Director mwenzake.
MIMI: “Subiri kidogo… Director mwenzake yuko wapi? Maana nilisahau kabisa kukuliza hili siku ile.”
IRYN: “Ni Mzee Michael, yule aliyekuja kumchukua baba pale Coral Hotel tulipokuwa wote. Si unamkumbuka?”
MIMI: “Ndiyo, namkumbuka vizuri. Alikuwa charming sana, akalalamika kwanini huendi msalimia?”
IRYN: “Hujakosea, huyu mzee ndiye alimwambia baba kuwa kampuni inachunguzwa na kwamba kama vipi waiachie tu mambo yatulie, baba akamsikiliza. Sasa sijui unafikiria kile ninachofikiria mimi?.”
MIMI: “Kwamba Mzee Michael anaweza kuwa amehusika kwenye huu mchezo mchafu?”
IRYN: “Absolutely right, japokuwa sitaki kumuwazia mabaya kwa haraka, maana huyu ni rafiki mkubwa sana wa baba. Ndiyo maana hata mimi sijataka kusema chochote mpaka nikamilishe ushahidi wangu. Pia, kwenye Management ya kampuni wabongo walihusika kwenye top position, huenda wanahusika kwenye hili. Ila mimi najua kabisa mhusika wa huu mchezo mchafu hatoki mbali na circle ya mzee.”
MIMI: “Wewe ulijuaje kuhusu huu mchezo mchafu?”
IRYN: “Hili suala halijaanza jana, ni tangu kipindi kile nimekuja South kumuona baba baada ya kusikia hali yake mbaya. So, baada ya hapo tulikaa chini na kuanza kunambia mali zote anazomiliki hadi hii kampuni. Baba baada ya kunambia pesa ambazo kampuni inadai, nilianza kufuatilia taratibu, namna ya kupata haki yetu, na ndo kubaini kampuni imechezewa.”
MIMI: “Na hili uligundua lini?“
IRYN: “Kipindi nimekuja Dodoma na kaka Jimmy, huu ndo mrejesho nilioupata kutoka kwa informer wangu baada ya kutua Dar, japo nilikuwa sina uhakika hadi niliposikia kutoka kwako.”
MIMI: “Nashindwa kuelewa hadi Mzee Michael naye alikuwa hajui kama kampuni imechezewa?”
IRYN: “Mzee Michael aliondoka Tanzania muda mrefu sana, since 2018, na amekuwa akija kuangalia mali zake na kuondoka. Naamini kwenye huu mchezo mchafu kuna mtandao mkubwa nyuma yake. Wamefanya hujuma nzito kumzunguka mzee. Nataka nipate ushahidi wa kutosha kwanza. Ndiyo maana nakusisitiza hili suala libaki kimya kabla hawajashtuka. But soon the truth will prevail.”
MIMI: “Hizi taarifa zote ulikuwa nazo? Kwanini hukunambia mapema? Mimi nilidhani ndio kwanza tunaaanza kuchimba.”
IRYN: “Kwanza nilitaka kuona kama kweli upo tayari kwa hili. Nimegundua tupo pamoja, ndiyo maana sasa nimekuweka wazi kila kitu.“
MIMI: “Sawa, basi hebu niambie next move ni ipi. Mimi niko na wewe kwa kila kitu.”
IRYN: “Kwa sasa napambana kumjua vizuri huyu Steve Jobs. Nikifanikiwa kumfahamu, tutakuwa sehemu nzuri sana, na kesi hii tutakuwa tumeshinda kabla hata haijaanza. Wewe mwambie Advocate atulie kwanza, tusifanye haraka. Tukishapata hizi taarifa muhimu, ndipo tutampa go ahead ya kufungua kesi.”
MIMI: “Nimekuelewa, my genius. Sasa Mzee mpaka sasa hajui lolote kuhusu kinachoendelea?”
IRYN: “Ndiyo, hajui hata kama malipo yalishafanyika. Japokuwa bado napambana kupata zile documents za tender. Baba anasema ilikuwa tender ya billion 7 na point, na document zipo kwake. Kwasasa nashindwa kuitafuta sababu ya mtoto, nitatafuta muda kwenda kuisaka.”
Maongezi yale yalikuwa marefu mno, mimi hapa nimeyafupisha tu, sababu mengine ni ya kibiashara na mengi ni siri haya nnimewapa machache mpate picha.
Baada ya kumaliza mazungumzo makubwa kuhusu kampuni na mpango mzima wa ushahidi, tulibadili mada na kuzungumzia conference ya Zanzibar. Nilimweleza mafanikio yote tuliyoyapata kule, jinsi tulivyoweza kufunga madili muhimu, na namna tulivyopanua mtandao wa biashara.
Kisha tukazungumzia suala la Asmah. Iryn aliniambia kuwa tayari amezungumza naye, na msimamo wake bado uko pale pale, anataka kwenda kusoma. Iryn alisema hatuna budi kutafuta mtu mwingine atakayejaza nafasi yake na pia alisisitiza kwa msisitizo mkubwa kuwa lazima tupunguze wafanyakazi pale Masaki hadi wafikie 12 pekee ili kupunguza gharama zisizo za lazima.
Baadaye, akaulizia kuhusu safari yangu ya Zambia. Sikupenda kumwambia ukweli wa sababu halisi ya mimi kwenda kule, kwa hiyo nikamjibu tu kwa kifupi kuwa “Mzee kaniita mara moja, sijui kuna nini.” Sikutaka kabisa aanguke kwenye ramani zangu za ndani kwa sasa.
Upande mwingine, alinikumbusha tena kuhusu ahadi yangu ya kwenda kwa wazazi wangu. Alisema wazi kuwa “December lazima twende wote Ethiopia, lakini safari haitawezekana bila kuanza kwa wazazi wako kwanza.” Niliona kuna msisitizo mkubwa sana kwenye hili jambo.
Wakati tukiendelea na maongezi hayo, ghafla tuliitwa mezani kwa ajili ya dinner. Mazungumzo yetu yalisimama pale na tukaenda moja kwa moja hadi dining room, ambako tulikuta familia yote ikitusubiri.
Bibi alinitazama kisha akasema kwa Kioromo huku akicheka, “Mume kaja kidogo umefurahi na unadeka.” Wote walicheka sana pale mezani. Mimi nilibaki nikiangalia bila kuelewa chochote hadi Iryn aliponieleza maana ya maneno ya bibi yake.
Baada ya kula, tulihamia sebleni tukaanza kupiga stori za kifamilia. Mimi, kwa vile nilikuwa kidume, nilijikuta nikiunguruma peke yangu nikisimulia matukio na hadithi mbalimbali huku wote wakifurahia uwepo wangu pale. Baadaye, Iryn akanikonyeza na akanipa ishara ya kuwa muda wa kwenda chumbani umefika, na tukaondoka huku nimembeba mgongoni.
Tulipofika chumbani, bila hata maneno mengi, alivua nguo zote taratibu kisha akaniangalia kwa tabasamu laini, akaanza kunivua na mimi. Tukaelekea bafuni tukaanza kuoga, kwa jinsi mwili wake ulivyobarikiwa, hata nilishindwa kujizuia maana niliishia kusimamisha tu. Ila kwa heshima ya hali yake ya kiafya ambayo haikuwa bado imetengamaa vizuri, niliishia kuwa mpole hata yeye kwa upande wake alipatwa sana na huruma ila hakuwa na jinsi.
*******
Kesho yake, siku ya Alhamisi, nilikuwa na safari ya kuelekea Zambia na nilipanga kuondoka kwa ndege ya jioni. Asubuhi ilipokucha, niliamka mapema na kutumia muda wangu vizuri kucheza na binti yangu mpendwa, Aria.
Baadaye, nilipata fursa ya kuzungumza na Mzee na kumjulisha kuhusu safari yangu ya Zambia. Hata hivyo, aliniarifu kuwa alikuwa amekwama Livingstone, na akasisitiza kuwa haingewezekana kurudi mapema kabla ya kesho ijumaa. Licha ya hivyo, Mzee alihakikisha kila kitu kiko sawa na alithibitisha kuwa tayari alikuwa ameacha taarifa zote muhimu kwa Sandra, ili kila jambo liende vizuri hata kwa kutokuwepo kwake.
Mapema kabisa, niliambatana na Iryn kuelekea uwanja wa ndege. Alitaka kunisindikiza ili kunipa kampani katika safari yangu. Wakati tunaondoka nyumbani, Aria alikuwa bado amelala fofofo. Kabla ya kuingia garini, niliwaaga pia akina Samantha pamoja na bibi. Walinilalamikia kwa utani kwamba ninaondoka mapema mno, lakini niliwafariji kwa kuwaahidi nitarejea tena hivi karibuni.
Tulipofika uwanja wa ndege, tulikaa kwenye moja ya migahawa ya ndani, tukibadilishana mawazo huku nikisubiri muda wa kupanda ndege. Katika mazungumzo yetu, Iryn alinieleza jambo lililonishtua sana. Aliniambia kuwa kwa mara ya pili ameota ndoto akimuona mama yake marehemu akimbeba Aria na kumbembeleza.
“Darling,” akaanza kwa sauti ya upole lakini yenye wasiwasi, “mara ya kwanza niliota niko jikoni napika. Ghafla nikasikia Aria analia kwa nguvu, kisha akanyamaza kimya. Nilipotoka haraka kuingia chumbani, nikamuona mama amembeba Aria na nilimuona kasimama pembeni ya kitanda akinitazama. Akanipatia mtoto kisha nikashtuka.”
Alivuta pumzi kisha akaendelea;
“Ndoto ya pili niliota nimeingia chumbani, nikakosa kumuona Aria. Nikaanza kumuita Samantha kwa sauti kali aniletee mtoto nimwogeshe, lakini hakukuwa na jibu lolote. Nikasema wacha nitoke niende sebleni. Nilipofika pale, nikamkuta mama tena amembeba Aria. Aliponiona alinitazama kwa upole, akatabasamu kisha akanipatia mtoto. Ndipo nikashtuka tena.”
Nilisisimuka kusikia maneno haya kutoka kwake na ilibidi nikae vizuri;
“Bibi ulimwambia kuhusu hizi ndoto? Na hii ina maana gani kweli?”
Iryn akanijibu kwa sauti ya chini;
“Baada ya kuota mara ya pili, nilihisi woga sana. Nikamwambia bibi, naye akaniambia nisiwe na wasiwasi. Alisema hakuna shida, ni ndoto za kawaida, hata kipindi kile mama alipofariki, nilikuwa namuota mara kwa mara. Ilikuwa inanitia huzuni sana.”
“Duuh! Kama bibi kasema haina shida, basi mimi pia naamini ni ndoto tu, usijiwekee hofu, mummy.”
“Lakini bibi amesema natakiwa kumpeleka Aria kwenye kaburi la mama kule Ethiopia, nimtambulishe rasmi kama mjukuu wake.”
Nilimshika mkono na nikamwangalia machoni,
“Sawa, mummy, haina tatizo, ninaamini bibi kuna vitu anajua ila hajataka kusema, kama ni vibaya angekwambia sababu anakupenda sana. Naamini hakuna tatizo kuhusu hizi ndoto ulizoota, lakini tafadhali kumbuka, nawapenda sana vipenzi vyangu. Sitaki jambo lolote baya liwatokee wewe na Aria.”
Alinitazama kwa muda bila kusema neno, kisha akatabasamu kwa upole. Nikamwambia kuwa muda wa kuondoka ulikuwa umefika. Alisimama, tukakumbatiana kwa nguvu, hakutaka kuniachia mapema, kisha nikambusu mdomoni. Aliniangalia kimya huku tabasamu hafifu likibaki usoni pake, hadi pale nilipoingia ndani na kupotea machoni pake.
Safari yangu ilianza saa kumi jioni, kuelekea Zambia, na tuliwasili Lusaka majira ya saa nne usiku. Bila kupoteza muda, nilichukua tax moja kwa moja kuelekea Roma, nyumbani kwa Mzee. Hali ya usiku ilikuwa tulivu, na barabara zilikuwa zikionekana kimya huku nikiendelea kufikiria mambo mbalimbali.
Pale nyumbani, nilimkuta Sandra ambaye ndiye aliyenipokea kwa furaha na kunikaribisha ndani. Tulikaa tukipiga story kwa muda mfupi tu, tukifurahia mazungumzo yetu, na baada ya muda, Sandra akaaga, ili kesho aweze kuja kazini mapema. Baada ya Sandra kuondoka, mimi pia sikutaka kupoteza muda; nikaenda chumbani kulala, na mara moja nikamjulishe Iryn kuwa nimefika salama, pamoja na mzee.
Asubuhi, kulipokucha, niliamka na kuandaa chai kwani nilihisi njaa. Wakati nikiwa mezani, simu yangu ilianza kuita, alikuwa ni mzee akipiga, nilipokea simu hiyo, na tukaanza mazungumzo ya kina. Aliniambia atarudi home kesho, ambayo ni siku ya Jumamosi. Nilimweleza kuwa mipango yangu ilikuwa kuondoka Jumamosi, lakini sasa nitaruhusu mpango huo kubadilika hadi Jumapili, kwani jambo nililotaka kumwambia ni muhimu sana.