SEASON 03
CHAPTER 6
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
PREVIOUS:
Ilikuwa ni saa moja usiku, ghafla nikasikia mlango ukigongwa. Niliposogea kufungua, nikakutana na Hilda na Sumaiya, wakiwa wamesimama mlangoni kwa tabasamu na, wakiomba kuingia ndani.
CONTINUE:
Sikuwa nimefungua mlango wote, bali kidogo tu, kwa ajili ya kuzungumza nao. Kabla sijasema neno, Hilda akawa wa kwanza kufungua mdomo;
“Insider, hupokei simu, kwanini? Nimekupigia sana baada ya kutoka meeting.” Alinena huku akinitazama moja kwa moja machoni.
“Nilikuwa naoga, guys nisubirini kidogo nivae ili tuondoke.”
Niliwaacha nje wakisubiri kwa subira, nami nikajiandaa upesi kwa ajili ya kuondoka nao kwenda kupata chakula cha jioni. Ghati alikuwa bado amelala fofofo, na sikuona sababu ya kumuamsha. Kwahiyo, safari yetu ya kuelekea dinner ikaanza na njiani tulikuwa tukitaniana sana.
Tulipofika dining, na tukiwa tumekaa mezani tukisubiri chakula kiletwe, Hilda hakuweza kujizuia tena. Uvumilivu ulimshinda, aliniangalia kwa makini, kisha akaniuliza kwa sauti yenye msisitizo na mashaka:
“Yule dada uliyekuwa ukiongea naye leo. Ni nani hasa kwako? Mbona nilikuona mkiwa karibu sana, hata mkibadilishana namba za simu? Umeshampenda?”
Nilihisi swali hilo lilitoka moyoni mwake kwa uzito. Nilimtazama, nikabaki kimya kwa sekunde chache, nikitafuta maneno sahihi ya kumjibu. Pembeni yetu, Sumaiya alikuwa kimya kabisa, akimtazama Hilda kwa mshangao, na hakutaka kuchangia wala kuharibu hali iliyokuwepo.
Kwa upande wa Hilda, niliona wazi aliumia moyoni. Pengine alihisi nimewatelekeza ili niwe karibu na Savinna. Ukweli ni kwamba, mawazo yao yalikuwa mbali na hali halisi, mimi sikuwa nimekimbia kwa ajili ya Savinna, ila nilikuwa na mipango yangu mingine ya kukutana na Ghati.
Tulianza maongezi mengine ambapo, mazungumzo yetu yalijikita zaidi kwenye mkutano wa leo. Hilda na Sumaiya walikuwa wananisifia kwa namna nilivyoweza kutoa speech nzuri, wakiniambia nimeonesha kujiamini na mvuto wa hali ya juu. Maneno yao yalinitia moyo, nikahisi kweli juhudi zangu hazikuwa bure.
Wakati tunazungumza, Ghati alinipigia simu na kwa sauti ya kudeka, aliniuliza nilipo, kisha akasema anahisi njaa sana. Nikamtuliza haraka, nikimwambia kuwa mhudumu atamletea chakula, hivyo asiwe na wasiwasi.
Baada ya chakula kuletwa, Hilda alikula kwa haraka sana kisha akatuaga akielekea kulala. Alisema amechoka mno na anahitaji kupumzika. Mimi na Sumaiya tulibaki tukijadiliana kwa kina kuhusu maandalizi ya hotuba aliyotarajia kutoa kesho kuhusiana na kampuni ya Cleaning. Lengo letu kuu lilikuwa ni kuwashawishi wateja wapya, kushinda tender mbalimbali na kukuza kampuni kwa kiwango kikubwa zaidi.
Kwa upande mwingine, Iryn naye hakuwa mbali nasi. Alitupa ushirikiano mkubwa pamoja na mbinu muhimu za namna bora ya kutoa hotuba yenye mvuto. Kwa kuwa Iryn amebobea sana katika masuala haya, mchango wake ulikuwa msaada wa kipekee uliotupa ujasiri na imani zaidi.
Baada ya kumaliza mipango hiyo muhimu, mazungumzo yetu yakabadilika na kuingia kwenye stori za kawaida. Hapo ndipo Sumaiya akanishtua na habari mpya, alikuwa na mpango wa kununua gari nyingine. Kwa tabasamu na hamasa kubwa alisema gari anayolitamani kwa muda mrefu ni Mazda CX-5, na akaahidi kwamba kabla mwaka huu kuisha atahakikisha anaimiliki.
Kwa upande mwingine, nilimtaarifu Dullah kuhusu ujio wa Ghati Zanzibar. Alinisihi sana jambo moja la msingi, nihakikishe namwambia ukweli wangu wote. Maana kwa jinsi mambo yalivyo, Ghati alikuwa anaonesha wazi kabisa kwamba anatamani kuanzisha mahusiano na mimi. Dullah aliona ni vyema nimweleze mapema kwamba tayari nina mke na mtoto, ili baadaye mambo yasiwe magumu.
Baada ya kumalizana na Sumaiya, tuliagana kwa ahadi ya kukutana kesho mapema. Nilirudi chumbani kwangu nikiwa nimechoka, nilipofungua mlango, nilistuka kidogo, Ghati hakuwa ndani. Nilipoangaza kitandani, niliona nguo zake zimetupwa juu yake na nilipofungua mlango wa nyuma, nikamuona yuko kwenye swimming pool.
Nlisogea na kukaa kimya kwenye pool lounger nikimwangalia. Ghati alikuwa naked, na uzuri wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu ulijitokeza mbele yangu bila chenga. Pamoja na kwamba alikuwa ameshawahi kunyonyesha, mwili wake ulikuwa bado na mvuto wa pekee. Nilijikuta nikimtizama sana, nikishindwa kuondoa macho yangu. Baada ya muda si mrefu, alitoka majini, akaja kukaa karibu nami, kisha nikamkabidhi taulo, akajifunika taratibu.
MIMI: “Umekula?”
GHATI: “Yes, thank you.”
MIMI: “You’re so beautiful and you look sexy.”
Ghati alitabasamu tu, akinitazama kwa macho ya mahaba. Sekunde zikapita kimya, kisha akavunja ukimya kwa kuuliza:
GHATI: “Mna event gani huku?”
Nilianza kumueleza kwa kifupi kuhusu event iliyotuletea Zanzibar, nikamwambia pia kwamba sipo peke yangu, nina wenzangu wawili. Baada ya maongezi hayo, ghafla Ghati akaanza kulalamika. Alisema nimekuwa nambania muda, sipokei simu zake wala kujibu message zake. Malalamiko yake yalikuwa ya moja kwa moja, hivyo sikuwa na budi bali kumfungukia ukweli wote.
Nilimwambia kwa utulivu kwamba,
“Nina mwanamke ninayeishi naye na tuna mtoto mmoja wa kiume. Ukiachana na huyo, bado nina mwanamke mwingine nimezaa naye South Africa. Kipindi nilipokuwa kimya huku ukinitafuta sana, nilikuwa huko, maana amejifungua mwezi uliopita. Ndiyo maana simu nilikuwa sizipokei wala meseji sizijibu, nilikuwa busy kulea. Samahani sana kama nakupa taarifa hizi sasa, lakini napenda ujue ukweli kuhusu mimi, kwa sababu hatujawahi kuzungumza kwa undani, na hukuwahi kuniuliza.”
Ghati alitulia kwa muda mrefu, kimya. Uso wake haukuwa na furaha, na nilijua taarifa hizo hazikumwingia vizuri. Baadaye akasema kwa sauti ya taratibu;
GHATI: “Ahsante kwa kufahamu ila kuhusu mtoto, nafahamu unaye.” Na akaniacha pale kwenda ndani;
Kauli yake ilinifanya niwe kama nimepigwa na butwaa. Nilikaa nikijiuliza, nani kamwambia? Sikumbuki kama tulishawahi kuzungumza naye kuhusu mtoto. Je, huenda Dullah ndiye alimwambia? Lakini moyoni mwangu nilihisi haiwezekani.
Nilipokuwa bado nadumbukia kwenye fikra hizo, ghafla Ghati alitoka ndani akiwa amebeba simu yangu mkononi. Akanisogelea, akaniambia kwa sauti ya upole:
GHATI: “Shika, simu yako inaita sana.”
Nilipoichukua, tayari ilikuwa imekatika. Nikaangalia ni Prisca, na alikuwa amenipigia mara tatu mfululizo. Bila kupoteza muda, nikampigia na simu yake iliita kwa sekunde chache, kisha akapokea. Baada ya kusalimiana, alinipa taarifa kwamba amemaliza mitihani yake na alikuwa na shauku kubwa tuonane, akasema ana jambo muhimu la kuniambia. Nilimwahidi nitakaposhuka Dar es Salaam nitamtafuta, ni jambo lililomfurahisha mno.
Sikutaka kupoteza muda pale nje hivyo nikaona bora niingie ndani kulala ili niwahi kuamka kwaajili ya kikao cha kesho. Nilipoingia chumbani, nilijaribu kuzungumza naye, lakini hakuwa na mwitikio mzuri. Nikaamua kulala kimya kimya, nikiacha moyo wangu ukibeba maswali na hisia zisizo na majibu.
Asubuhi ilipofika, niliamka mapema sana na kuanza kujiandaa, nilihitaji kuwahi venue na kuanza kuandaa nondo zangu kwa ajili ya kikao. Ghati bado alikuwa amelala kitandani, amejifunika vizuri kana kwamba usingizi wake ulikuwa mzito. Nilitazama kwa sekunde chache kisha nikatoka, niliacha maelekezo kwa wahudumu kuhakikisha anapewa chochote anachohitaji.
Nilipofika venue nilijikuta nipo peke yangu. Nikaona huu ndio muda mzuri wa kuendelea kuandaa business plan kwa ajili ya biashara yangu na Jane. Bila kupoteza muda nilianza kazi mara moja, nikiwa na umakini.
Baada ya kama nusu saa kupita, Mr. George aliingia ukumbini na moja kwa moja akaja kukaa pembeni yangu. Tukaanza kuzungumza kwa urafiki, na alipogundua kwamba nilikuwa naandaa business plan, alionesha utayari wa kunisaidia. Kwa uzoefu na maarifa yake makubwa, alinipatia mawazo mapya yaliyoniwezesha kuboresha na kufanya plan iwe bora zaidi na ya kitaalamu.
Wakati huo huo, watu walikuwa wanaanza kujaa taratibu kwenye eneo la tukio. Kulikuwa na shamrashamra za salamu, watu wakitambulishana, wengine wakibadilishana maneno ya kujuana.
Saa mbili kamili, Kikao kiliendelea kwa siku ya pili. Leo ilikuwa siku yenye uzito maalumu ambapo kila kampuni ilipewa nafasi ya kujitambulisha, kuelezea huduma zao na fursa walizokuwa nazo. Hii ilikuwa ni golden chance kwa makampuni yote yaliyoshiriki kuonyesha ubora wao. Lengo kuu ilikuwa ni kujenga mtandao wa kibiashara, kutengeneza fursa mpya, na kuimarisha mahusiano kati ya makampuni yote yaliyoshiriki.
Kwa upande wetu, Sumaiya ndiye aliyebeba jukumu la kutuwakilisha. Na kwa dhati kabisa, Sumaiya alituwakilisha kwa kiwango cha juu kuliko nilivyowahi kutarajia. Hii siku ndiyo nilikuja kugundua kwamba Sumaiya si mfanyakazi wa kawaida tu! ni hazina ya kampuni. Mara nyingi tumekuwa tukimjua kwa utani na masihara yake ya ofisini, lakini leo alionyesha uwezo wake tena ule wa kitaalamu.
Hotuba yake ilikuwa ya kupendeza mno, kwani aliipanga vizuri, hakubabaika, wala kuuma maneno. Alizungumza kwa ufasaha na kwa lugha iliyonyooka, huku akionyesha kujiamini kwa hali ya juu. Bado, hakuacha kuvutia kwa mwonekano wake, kwa jinsi alivyokuwa amependeza.
Baada ya kikao, wakati wa chakula cha mchana, mimi, Sumaiya, na Mr. George tulikaa pamoja tukila, lakini Hilda hakukuwa nasi kama ilivyo kawaida. Badala yake, alikuwa amekaa na jamaa mmoja ambaye ni moja ya washiriki wa hii event. Nilipomkonyeza Sumaiya kuhusu hili, alitabasamu tu baada ya kuona jinsi Hilda na Jamaa walivyokuwa busy wakicheka na kujiachia pale kwa meza yao.
Cha kushangaza ni kwamba tangu asubuhi, Hilda na yule jamaa walikuwa karibu sana, walikaa pamoja toka mwanzo wa kikao, wakionekana kufurahia kila wakati. Sikuweza kuelewa walifahamianaje, lakini ukaribu wao ulinipa mashaka. Na kwa jinsi hali ilivyokuwa, ilionekana wazi kuwa Hilda alikuwa ameelewa mziki tayari kutoka kwa yule jamaa.
Saa kumi na moja jioni , baada ya kikao kumalizika, hali ya ukumbi ilibadilika kabisa. Watu wengi walimfuata Sumaiya kumpongeza kwa hotuba yake ya kuvutia. Kulikuwa na wengine waliotaka kumpa mikono ya shukrani, baadhi wakitaka namba yake ya simu kwa mawasiliano ya baadaye, huku wengine wakiahidi kushirikiana naye kikazi. Nilimtazama Sumaiya akicheka na kuzungumza kwa ujasiri, na wadau mbalimbali na pale nilitambua tena thamani yake kwenye kampuni, kwani alikuwa amefungua milango mingi mipya kwa bidii yake ya siku moja tu.
Baada ya muda, Sumaiya aliniaga na kuondoka. Mimi nilibaki ukumbini, nikiona bado sina haraka ya kwenda room mapema kupumzika. Nilijua fika nina mambo yangu mengi binafsi ya kufanyia kazi, hivyo niliamua kutumia muda huo kukamilisha mipango yangu, ikiwemo na safari. Nilipanga kwenda South kumsalimia binti yangu Aria, kisha nipitie Zambia kuonana na mzee. Ratiba ilikuwa tight sana, lakini sikuwa na jinsi ilibidi nifanye hivyo.
Nilimpigia simu mama Aria nikamweleza mpango wangu, na kwa sauti yenye furaha alinihakikishia kuwa litakuwa jambo kubwa kwake. Baadaye nilimpigia mzee kumtaarifu kuhusu safari hiyo, lakini yeye alisema, “Hapa ni nyumbani, hakuna haja ya taarifa nyingi. Karibu wakati wowote.”
Muda ulisogea, na ilipotimia saa mbili usiku ndipo niliamua kuelekea chumbani. Lakini kabla ya hapo nilipitia dining kupata chakula cha jioni kwanza. Baada ya kushiba, nilienda moja kwa moja chumbani. Nilipofungua mlango, nilimkuta Ghati amelala kitandani kizembe, kisha akageuka kunitazama kwa macho yaliyobeba hisia tofauti. Tulibaki tukitazamana kimya kwa sekunde chache kabla sijasogea na kukaa pembeni yake.
Nilianza kuzungumza naye taratibu, nikijaribu kusoma hali yake. Nilihisi maneno niliyomwambia usiku uliopita bado yanamkera au pengine hayakumkaa vizuri. Yeye kwa upande wake alidai yuko sawa, hakuna shida, lakini niliona wazi tofauti kwenye mienendo yake, hasa mazungumzo hayakuwa kama kawaida, majibu yake yalikuwa mafupi, na hata furaha alikuwa hana.
Nilipogundua hali hiyo, niliamua kutoendelea kumsumbua. Nilitoka nje, nikakaa kwenye kibaraza nikifurahia upepo mwanana wa bahari ukipiga taratibu. Nilifanya kumpigia simu simu Dullah nikamweleza yote yaliyotokea. Yeye kwa sauti ya kistaarabu alinishauri nisiwe na haraka na alisema “Umefanya kitu sahihi mpe muda, atapanga na kuamua mawazo yake mwenyewe. Usifanye chochote sasa.”
Nilikaa pale kwa muda mrefu, nikitafakari mambo mbalimbali, hasa kuhusu safari ya Zambia na jambo kubwa lililokuwa likinisumbua kichwani. Nilifanya uamuzi wa kwenda kumweleza mzee kuhusu suala langu na Iryn na mtoto. Nilijua si jambo dogo, lakini niliamua nitaweka wazi kila kitu pindi nitakapotua Zambia.
Nilifanya maongezi na Mary, tulijikita kwenye mipango ya kuzaa pamoja mtoto. Kama nilivyosema awali, niliona Mary anafaa kuwa mama wa mtoto wangu na ni mtu sahihi. Kwa upande wake, yeye alikuwa tayari, lakini kwa condition.
Nilinyamaza kwa sekunde kadhaa kisha nikamuuliza;
“Condition gani?”
Mary akasema kwa sauti ya utulivu lakini yenye uzito,
“Kabla hatujaendelea, lazima umalize historia yote na mdogo wangu Prisca. Sitaki nifanye kitu kisicho wazi, kisha aje kujua baadaye. Insider ni lazima ujue kwamba kuna siku ukweli utajulikana tu, bora aje ajue kutoka kwako kuliko apate kupitia njia nyingine.”
Nikavuta pumzi kwa nguvu,
“Mary, what’s your point?”
Akasema kwa msisitizo;
“Naomba umwambie Prisca ukweli kwamba mimi na wewe tunadate, ili isijekuleta shida hapa nyumbani au mimi kugombana na dada yangu. Afu kuhusu suala lako la kuwa na mke mimi nitadeal nalo. We have a deal or not?”
Nilinyamaza kimya kwa muda mrefu. Kwa kweli nilihisi Mary ananichanganya, alianza kuniletea mambo ambayo kamwe hayakuwahi kupita kwenye ubongo wangu. Mwisho wa siku, sikuwa na jibu la haraka. Nilimuaga kwa upole nikamwambia:
“Tutaongea vizuri nikirudi Dar.”
******
Jumamosi ilikuwa ni siku ya mwisho ya mkutano wetu, ile asubuhi baada ya kuwasili kwa ajili ya meeting, nilimkuta Hilda tayari ameshafika. Niliposogea kumpa hi, hakunionyesha hata chembe ya uchangamfu kama ilivyokuwa siku za nyuma. Hivyo, niliona heri nimuage tu kwa heshima, kisha nikaenda kukaa karibu na Savinna.
Tukiwa tumekaa na Savinna, nilimwomba kama ingewezekana tukutane jioni kwenye bar tupate kinywaji na kufurahia kidogo. Lakini alinijibu kwa kusema;
“Mimi situmii kilevi, labda tutafute sehemu nyingine nzuri ya kuongea.”
Niliheshimu msimamo wake, nikakubali.
Mchana ulipowadia, wakati wa lunch, nilijikuta nimekaa na Sumaiya. Tulipiga story kwa muda mrefu, na katika mazungumzo nilimwambia kuwa Jumatatu nitaondoka kuelekea South Africa kwenda kumsalimia binti yangu. Naye akanijulisha kuwa kesho Jumapili ataondoka pamoja na Hilda.
Kilichotushangaza zaidi ni mabadiliko ya ghafla ya Hilda. Tofauti na awali, sasa alionekana kututenga kabisa. Alikuwa busy muda mwingi na yule yule jamaa mmoja, akatufanya tuone kana kwamba amejitenga na sisi.
Sumaiya akaniuliza kwa mashaka:
“Kuna nini kati yako na Hilda Mmegombana?”
“Hapana, hakuna shida yoyote.”
Lakini Sumaiya, kwa mtazamo wake, alisema huenda mimi kutompa attention ndio sababu iliyomfanya Hilda abadilishe mwenendo. Mimi kwa upande wangu nilimwambia, tumuache Hilda afanye mambo yake na tusimuingilie.
Ilipofika saa kumi jioni, event ilifungwa rasmi kwa mafanikio makubwa. Tulikuwa tumepata fursa ya kipekee ya kutengeneza mtandao mpana wa kibiashara na kushirikiana mawazo na watu wenye ushawishi mkubwa. Hali ya jioni ilikuwa tulivu sana, upepo ukipuliza taratibu kutoka baharini, na nje ya ukumbi wa mikutano nilijikuta nikiwa na Mr. Graham tukipiga story, tukichanganya mazungumzo ya kibiashara na mambo binafsi.
Mr. Graham alinieleza kuwa mama Janeth ni rafiki yake wa karibu sana. Aliniambia kwamba alipofahamishwa na mama kuhusu nia yake ya kutaka wageni wake wahudhurie mkutano huu, hakusita kuongeza idadi ya watu kwa ajili yetu. Na kwa gharama za kuhudhuria mkutano huu kuwa $1,200 kwa mtu mmoja, ilikuwa wazi huu haukuwa mkutano wa kawaida bali wa kiwango cha juu kabisa.
Tulipoendelea kuzungumza, Mr. Graham ghafla aliniuliza kuhusu mipango yangu ya kitaaluma. Alionekana kuniamini sana kwa sababu alisema ananiona nikiwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa kimataifa. Nilimweleza kuwa nina mpango wa kuanza masomo ya Masters pamoja na CPA, lakini bado sijafanya maamuzi ya mwisho kuhusu aina ya Masters nitakayosoma. Nilimweleza kuwa nipo dilemma kati ya MBA in Finance, Masters in Accounting & Finance, na Masters in Finance & Investment.
Kwa tabasamu la kujiamini, Mr. Graham alisema, “Kama unataka kufanya CPA, basi MBA in Finance & Investment itakufaa zaidi. Itakupa upeo mpana na kukuweka vizuri kwenye soko la kimataifa.”
Kwa kuwa niliona ni mtu mwenye uzoefu mkubwa, sikuwa nyuma kuuliza zaidi kuhusu historia yake ya kitaaluma. Hapo ndipo alipoeleza kuwa yeye ana vigezo vya hali ya juu na vya kimataifa kama CFA, ACCA, FRM, na CFP, na amejikita kwenye financial markets, business analysis, financial analysis, na investment analysis, alikuwa na wasifu wa kuvutia sana.
Hata zaidi, alinishauri niachane na CPA na badala yake nichukue ACCA kama nataka kufungua milango ya kimataifa. Baada ya ACCA, alisema, CFA itakuwa silaha yangu ya mwisho ya maangamizi, hivyo niiweke kwenye mipango yangu. Maneno yake yalionekana kuwa na uzito mkubwa na nilijikuta nikimsikiliza kwa makini mno. Kwanza unapata wapi ujasiri wa kutomsikiliza mtu kama huyu ambaye anakwenda kila sehemu hapa duniani kutoka mafunzo?.
Mwisho wa mazungumzo yetu, nilimuahidi kuwa nitayafanyia kazi mawazo yake. Tukacheka kidogo, tukabadilishana namba za simu, na kisha tukaachana pale kwa mawasiliano zaidi.
Baada ya kurudi chumbani, nilianza kujiandaa haraka kwa ajili ya kutoka. Savinna tayari alikuwa kashanitumia ujumbe akisema yuko tayari na angependa sana tuongozane pamoja. Tulikuwa tumepanga kwenda mgahawani uliokuwa mbali kidogo na mazingira ya hoteli, sehemu tuliyoambiwa ina chakula kizuri na mazingira ya kupendeza sana.
Ilipofika saa kumi na mbili jioni, nilitoka na kuelekea sehemu tuliyopanga kukutana. Savinna alifika akiwa amevalia kwa heshima lakini mvuto wake ulikuwa wa hali ya juu, mtu ambaye anaonekana kujiamini na kujiheshimu sana. Tuliendelea na safari ya kuelekea mgahawani huku mazungumzo madogo madogo yakiendelea njiani, mengi yakihusu jinsi event ya leo ilivyokuwa ya mafanikio.
Tulipofika restaurant, tulipokelewa kwa utulivu na kuonyeshwa sehemu nzuri ya kukaa. Tulipoweka oda zetu, kulikuwa na ukimya kidogo, yaani ule ukimya wa watu wawili ambao bado wanajitafuta maneno ya kuanza. Baada ya muda mfupi, nilivunja ukimya huo:
MIMI: “Hivi ni kweli hutumii alcohol? Au unanipiga tu sound.”
SAVINNA: “Ni kweli kabisa, siwezi kukudanganya. Sijawahi kutumia tangu nizaliwe.”
MIMI: “Hongera sana, si jambo rahisi. Kwa kweli nimeheshimika sana kusikia hivyo.”
Baada ya hapo niligeukia mada nyingine.
MIMI: “Kampuni yenu ni kubwa na maarufu sana. Uliwezaje kupata nafasi ya kazi pale?”
SAVINNA: “Mama yangu anamiliki hisa nyingi sana pale, kwa hiyo ana nguvu kubwa kwenye maamuzi. Uwepo wangu pale ni sehemu ya urithi na pia kujifunza.”
MIMI: “Asee! Safi sana, kama mama ana hisa nyingi hivyo, basi kampuni kwa sehemu kubwa ni yake. Na kuhusu baba yako je? Anajishughulisha na nini?”
Savinna alinyamaza kwa sekunde chache, kisha akajibu kwa utulivu lakini kwa sauti ya chini kidogo:
SAVINNA: “Mzee wangu na mama walitengana tangu mama akiwa mjamzito. Tangu siku hiyo hajawahi kumtafuta mama, na mimi sijawahi kumjua kabisa.”
Nilihisi kauli hiyo ina uzito wake, nikajikuta nikisema kwa sauti ya polepole,
MIMI: “Samahani sana, sikuwa na nia ya kukuumiza.”
SAVINNA: “Usijali, niko sawa, haya ni maisha tu. Na vipi kuhusu kampuni yenu je?”
MIMI: “Mbali na kampuni ya usafi, kampuni mama inahusika na masuala ya beauty na salon. Tunauza nywele za asili, tunafanya makeups na huduma nyingine nyingi. Ofisi yetu ipo Masaki, na nitafurahi sana ukija kutembelea bidhaa zetu.”
SAVINNA: “Ahsante, lazima nitafute muda nifike. Nitakupigia simu.”
MIMI: “Pia unaweza kutembelea tovuti yetu,” nikamtajia jina pale pale.
Tulicheka kidogo kisha mazungumzo yakahamia kwenye biashara nyingine nilizo nazo Dodoma. Nilimweleza kuwa huenda siku moja nikahitaji huduma zake, hasa upande wa mikopo na yeye alijibu kwa kujiamini;
SAVINNA: “Hakuna shida kabisa, tutashirikiana.”
Baada ya muda, nilimuuliza kuhusu maisha yake ya mahusiano. Alijibu kwa upole kwamba yuko kwenye mahusiano, lakini hawajakuwa kwa muda mrefu sana. Nilipojaribu kuuliza kama huyo jamaa ana malengo makubwa naye, alicheka tu na kusema:
“Hayo bado, tupo kwenye hatua za awali sana.”
Saa moja kasoro usiku, Sumaiya alinipigia simu kuniarifu kuwa wanaelekea kwenye bar na kunialika niwafuate. Nilimwambia wanaweza kutangulia na nitaungana nao baadae.
Ilipofika saa mbili usiku, niliamua kuondoka pamoja na Savinna ili turudi hotelini. Njia tulipokuwa tunatembea ilikuwa kimya, lakini ilikuwa iliyojaa utulivu. Savinna, ambaye chumba chake kilikuwa cha kwanza, alifika kabla yangu. Tuliposimama mlangoni kwake, tuliagana kwa kukumbatiana, nikamtakia safari njema, naye akaahidi kuwa atanitafuta baadaye ili tuendelee kuwasiliana.
Baada ya kufika chumba changu, Ghati aliionekana amejilaza kitandani akichezea simu yake. Ghati ghafla akaanza kunishambulia kwa maneno, akilalamika kwamba narudi na kuondoka bila hata kumuaga kana kwamba hana thamani. Aliendelea mbele zaidi na kusema anajuta kuja Zanzibar, maana mimi sijali uwepo wake, na zaidi akasisitiza kuwa ninazitesa hisia zake, na kwamba sizithamini kabisa.
Kwa upande wangu, nilijikuta nikifurahi kimoyomoyo kuona Ghati akilalamika vile. Nilijua kabisa somo limeeleweka vizuri, na kwa namna alivyozungumza, niliona kama amenipa green light kwamba yuko tayari kwa hatua yoyote kutoka kwangu.
Sikutaka kuingia kwenye mabishano. Badala yake nilisogea karibu naye kimya kimya, nikamkumbatia. Ghati, akiwa mfupi kwangu, alilaza kichwa chake taratibu kwenye kifua changu. Nilihisi joto la pumzi yake likipenya kwenye shati langu huku mimi nikianza kumpapasa nywele zake taratibu. Ilikuwa ni ishara yangu ya kuonyesha kuwa huu si muda wa maneno marefu, bali vitendo.
Baada ya ukimya mfupi, nilimnong’oneza na kumwambia;
“Jiandae, tutoke tupoteze muda kidogo kwenye moja ya bar za hapa hotelini.”
Bila pingamizi, alitabasamu taratibu, akaenda bafuni kuoga.
Kwa kweli, Ghati ni moja ya mwanamke mzuri sana. Sifa zake nilishazieleza kitambo kwenye season ya pili pale Mbweni, carwash, siku ile tulipokutana kwa mara ya kwanza. Zaidi ya uzuri, tuna gap ya miaka sita, yeye ni mkubwa kwangu, lakini mwili wake bado ni top tier, haonekani kama mtu aliyezaa. Halafu anajiweza kiuchumi, kitu ambacho kwa upande wangu ni muhimu sana. Mimi siwezi kuwa na mwanamke ambaye hana shughuli yoyote wala hana malengo, nahitaji mtu ambaye anaweza kucontribute zaidi ya sex.
Baada ya kutoka kuoga, alianza kujiandaa taratibu. Alipomaliza kuvaa, alionekana stunning hasa mavazi, harufu ya perfume, kila kitu kilikuwa sawa. Tulipotoka chumbani, Sumaiya alikuwa ameshapiga simu mara kadhaa akiuuliza niko wapi, na alisema kafika tayari wananisubiri.
Baada ya kufika bar, hali ilianza kuwa ya kuvutia, kila aina ya rangi tofauti za watu ilikuwa inaonekana hapa. Picha linaanza naanza kukutana na baadhi ya wadau tuliokuwa tumekutana na kufahamiana nao kwenye mkutano. Niliwasalimia baadhi yao kwa heshima, kisha macho yangu yakarudi kumkagua Sumaiya, na alikuwa amekaa nyuma kabisa, kwenye kona ya bar, akitazama kwa utulivu.
Lakini Sumaiya hakuwa peke yake, alikuwa pamoja na Hilda na dada wawili ambao tulikuwa nao kwenye mkutano. Niliposogea karibu yao, hali ilibadilika mara moja maana wote walianza kumtazama Ghati kwa macho ya mshangao, kasoro Hilda alimtizama kwa jicho kali, na sura yake ilibadilika ghafla, ikionyesha tahadhari.
Niliwasalimia wote kwa heshima, na Ghati akafanya hivyo pia. Na muda huu mhudumu alikuwa ameshafika kusikiliza odda zetu;
”Mnataka kunywa nini? “ niliuliza.
“Tuchafulie meza bhana,” Sumaiya alisema kwa utani, lakini kwa msisitizo,
Kisha nilimgeukia Hilda;
“Hilda, bossy wangu, uko kimya sana.”
Hilda alijibu kwa tabasamu dogo, tena la kujilazimisha:
“Wewe sio mgeni na mimi niko huru.”
Niliagiza tuletewe Moët kubwa mbili, wine na redbull. Wakati huu, Hilda na Ghati walianza kuangaliana kwa macho tu, na taratibu Ghati akaninong’oneza:
“Huyu dada alikuja jana pale room kukuulizia, nikamwambia hujarudi kutoka seminar.”
Nilishtuka kwa maneno haya, sikutegemea kutoka kwa Ghati.
“Mbona sasa hukuniambia?”
“Nakumbuka ulinambia unawafanyakazi wenzako uko nao hapa, pia nilihasahau na nililala mapema.”
Hapo sasa ndipo nilipapata picha halisi na sababu ya Hilda kuninunia, sababu alimkuta Ghati room. Nilipokuwa nikiongea na Ghati, ghafla Mr. George alifika kutujoin, na sasa tukawa jumla saba kwenye meza. Hali ilibadilika kidogo, lakini bado ilikuwa na vibe ya utulivu na story zikaendelea.
Sumaiya uvumilivu ulimshinda, alitumia ujumbe mfupi kwenye simu yangu. Ujumbe ulisomeka hivi:
“Who is she?”
Nikareply kwa utulivu,
“One of my old friends lives here in Zanzibar.”
Baada ya kumwangalia kwa macho kidogo, Sumaiya aliishia kunibetulia mdomo. Ilikuwa ni ishara ya kimya kati yetu wawili tu, kitu ambacho hakuna mwingine aliyekuwa akijua kilichokuwa kinaendelea.
Baada ya kupita takribani masaa mawili, Hilda alionekana kuchoka na kuamua kuaga ili apumzike kwa ajili ya safari yake ya kesho. Kabla hajaondoka, nilimjulisha kuhusu mpango wangu wa safari ya kwenda South, na tukakubaliana kuwa tutaendelea kuwasiliana.
Sisi tuliendelea kukaa pamoja hadi majira ya saa saba usiku ndipo tulipoamua kuondoka na kila mmoja kurudi kulala. Njiani nilitembea na Ghati kwa utulivu, kwa kuwa alikuwa amelewa na kuonekana mchovu.
Nilipomfikisha chumbani, niliheshimu hali yake na nilihakikisha amelala vizuri. Japo nilikuwa na upwiru sana, lakini niliamua kuvumilia na kuwa mpole, lasivyo ningekuwa ninabaka.
****
Saa nne asubuhi, Sumaiya na Hilda waliondoka kurudi Dar es Salaam. Mimi, kwa upande wangu, niliungana na Ghati na kuamua kwenda beach kuburudika na upepo wa bahari pamoja na kutalii maeneo ya jirani. Tulikaa huko mchana mzima tukifurahia mandhari na hatimaye kurudi hotelini jioni.
Wakati tukiwa ufukweni, nilitumia nafasi ile kumfanya Ghati ajisikie vizuri. Nilihakikisha tunacheka, tunazungumza kwa uhuru na kuenjoy kila dakika tuliyokuwa pamoja. Ghati alionekana kufurahia muda huo kwa namna ya pekee, na ilikuwa siku ya kipekee kwetu wote.
Katika hali ya kutulia na kuaminiana, Ghati alinifungukia mambo mengi kuhusu maisha yake. Aliniambia siri na mambo ya ndani kabisa ambayo, kwa kauli yake mwenyewe, hajui ni kwa nini aliamua kuniambia, isipokuwa kwa sababu ametokea kuniamini kwa kiwango cha juu sana.
Nilipomdadisi kuhusu mipango yake ya baadaye, hasa kuhusu ndoa, aliniambia kwa uwazi kuwa kwa kiwango alichofika hajawahi hata kufikiria kuwa na mume au kuolewa. Alisema ameridhika na maisha yake ya sasa na kwasasa anataka kujikita zaidi kwenye malengo yake binafsi na maisha yake kwa ujumla.
Katika mazungumzo hayo, Ghati aliniomba nimuonyeshe picha za wake zangu pamoja na watoto. Bila kusita, nilianza kumwonesha picha za mama J na Junior, ambazo alizipenda sana na kumsifia mama J kwa namna alivyokuwa. Lakini, ilipofika kwenye picha za Iryn, Ghati alionekana kupagawa kabisa kwa jinsi alivyoona uzuri wake. Mara moja akaanza kuniuliza maswali ya kina kuhusu jinsi nilivyokutana na Iryn, namna tulivyoanza kufahamiana hadi kuwa wapenzi. Nilimjibu kwa uaminifu na kumweleza kila kitu bila kuficha. Tulimaliza siku yetu kwa kupiga picha nyingi za pamoja kwa kutumia simu yake iPhone 14 Pro Max.
Kwa upande mwingine, nilimueleza Ghati kwamba kesho tungeondoka wote kurudi Dar es Salaam, ila mimi ningepanda ndege kuelekea Afrika Kusini. Alipolisikia hilo, alinitazama kwa tabasamu kisha akaniambia ameufurahia sana muda wetu pamoja kule Zanzibar. Alinipongeza na kunishukuru kwa kampani niliyompa, akisema ilikuwa kama tiba kwake.
Jioni tuliporudi hotelini, miili yetu ilikuwa imechoka kutokana na siku ndefu ya kutalii na kustarehe ufukweni. Tulipoingia chumbani, tuliamua kuoga kwa pamoja kwenye jacuzzi, na hapa alinipa greenlight ya kucheza na body yake. Nilitumia nafasi hii kucheza na maeneo mbalimbali ya hatari ya mwili wake, na alikuwa akionesha ushirikiano wa hali ya juu. Nilianza kuendesha gari taratibu, yaani! Slowly sikuwa na haraka ya kuwahi, nilitaka kuenjoy vizuri utamu wa hii safari. Baadaye sasa nilianza kukanyaga gas kwa nguvu na spidi ilianza kuongezeka kwa kasi, huku kelele za milio ya gari ikirindima kwa sauti ya juu. Baada ya safari ndefu, hatimaye safari yetu ilifika tamati kwa Ghati kulala huku kichwa chake kimeegamia kwenye kifua changu.
Usiku nilipata nafasi ya kuwasiliana na Iryn, na kubwa aliuliza muda ambao ningeingia South Africa ili aje kunipokea. Nilimwambia kwa upole kwamba hakukuwa na haja ya yeye kuja, na kwamba Samantha angeweza kunipokea badala yake. Kauli hiyo haikumfurahisha hata kidogo, na alionesha kukasirika waziwazi.
*****
Asubuhi ilipofika, baada ya kuamka nilianza kujiandaa kwa safari yangu ya kwenda South. Nilikuwa napanga nguo zangu taratibu, na Ghati kwa upande wake alijitolea kunisaidia, nilimuomba abaki na baadhi ya nguo zangu, ambazo nilitumia kwenye mkutano. Nilimwambia aondoke nazo na kwamba nitazichukua baada ya kurudi kutoka South.
Wakati huo huo, sikuwa na budi kumuaga mama J. Nilijua wazi kuwa kama ningeondoka bila taarifa yoyote, ingeibua tafaruku kubwa. Hata hivyo, sio kwamba tulikuwa hatuwasiliani, ukweli ni kwamba mawasiliano yetu yalikuwa ya kila siku. Nilimpigia simu tukaanza kuzinguana pale kama kawaida yetu na kwa sauti ya upole nikamwambia:
“Mke wangu, nina mpango wa kwenda Zambia kuonana na mzee. Kuna mambo ninahitaji kuyashughulikia.”
Alikaa kimya kwa sekunde chache kisha akanijibu, akionyesha mshangao:
“Kuna nini tena huko Zambia?”
“Nina mpango wa kuacha kazi kwa Iryn. Safari hii ni sehemu ya kwenda kuangalia fursa nyingine ambazo naweza kufanya huko.”
Alisita, kisha akaniuliza kwa sauti yenye uzito:
“Kwanini unaacha kazi, Baba Junior? Na Iryn anasemaje juu ya uamuzi huu?”
“Mke wangu, tutazungumza vizuri nikirudi. Kwa sasa nataka tu mambo yaende taratibu. Kama vipi, unaweza kubaki huko na wifi yako ili utulize akili. Nitakutumia pesa uende Serengeti na mwanangu, mkapumzike hata siku tatu, muenjoy maisha.”
“Sawa, tutashukuru sana.”
“I love you.”
Baada ya hapo nikakata simu, nikasema kwa sauti ya juu, case closed. Ghati alikuwa akifuatilia maongezi yangu na mama J na aliishia kutabasamu.
Kufikia saa nne asubuhi tulikuwa tumeweka kila kitu sawa, kila bag likiwa limepangwa na kila kitu kikiwa kimekaa tayari. Ratiba yetu ya kuondoka hotelini ilikuwa ni saa 8 mchana, hivyo tulibaki na masaa kadhaa ya utulivu kabla ya kuanza safari rasmi. Tulitumia muda huu kupeana mahaba motomoto, tukianzia kwenye swimming na kisha tukahamia kitandani kwa shughuli ya mwisho
Saa 8 mchana tuliondoka hotelini tukielekea Stone Town kwa usafiri wa hoteli, tayari kwa safari ya kurudi Dar es Salaam kwa kupitia boat. Tulipofika Dar, niliagana na Ghati ambaye alichukua bolt kuelekea Mbweni, huku mimi nikipanda bolt nyingine kunipeleka JNIA, tayari kuanza safari yangu ya kuelekea South
TO BE CONTINUED
SUNDAY