Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Hope mpo salama.

Niliamua kujipa short break kidogo, ili kutoa nafasi kwa watu kuzungumza na kutafakari masuala muhimu ya nchi yetu.

That day was heavy, terrible things happened, poleni sana. Hata kwangu binafsi, nilipoteza mmoja wa watu wa karibu sana moyoni mwangu 💔.

Kwa sasa hali inaanza kurudi back to normal. Kesho, tutaendelea na our story, pale tulipoishia.
Ni sahihi
 
Hope mpo salama.

Niliamua kujipa short break kidogo, ili kutoa nafasi kwa watu kuzungumza na kutafakari masuala muhimu ya nchi yetu.

That day was heavy, terrible things happened, poleni sana. Hata kwangu binafsi, nilipoteza mmoja wa watu wa karibu sana moyoni mwangu 💔.

Kwa sasa hali inaanza kurudi back to normal. Kesho, tutaendelea na our story, pale tulipoishia.
good to hear that
 
SEASON 03

CHAPTER 12

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

CONTINUE:

Jioni ilipowadia, tuliondoka kuelekea The White Sands Hotel. Tulikuwa watatu tu ambao ni mimi, wife, na Sanchi. Junior pamoja na dada zake tuliwaacha nyumbani; tuliona hakuna ulazima wa kuambatana wote.

Tulipowasili hotelini, tulipokelewa na mandhari ya kuvutia na upepo mwanana wa Bahari ya Hindi ukipuliza taratibu. Tulitembea taratibu hadi Jet Bar, sehemu ambayo imejengwa ndani ya bahari.

Sanchi, aliyekuwa akifika maenao haya kwa mara ya kwanza, alishindwa kuficha furaha yake. Macho yake yalikuwa yakizunguka kila upande kwa mshangao, akifurahia utulivu na uzuri wa mazingira.

Baada ya kupata sehemu nzuri ya kukaa, tuliagiza vinywaji na kuendelea na mazungumzo. Nilimwelezea mama J kuhusu nafasi kubwa ambayo Sanchi anayo katika kusimamia biashara zetu kule Dodoma, na jinsi alivyochangia mafanikio mengi tuliyoyapata.

Wife alikuwa tayari anasikia mengi kuhusu Sanchi, lakini hii ilikuwa mara ya kwanza kumwona uso kwa uso. Alimshukuru kwa mchango wake mkubwa, akionyesha upendo na heshima ya dhati. Kisha akapendekeza, mwisho wa mwezi tutoke wote kwenda Dodoma, tuone biashara zetu huko.

Mazungumzo yalikuwa ni mengi sana, pia hali ya utulivu na ubaridi unaotokana na upepo wa Bahari ulituvuta pamoja na kufanya story ziwe tamu zaidi huku tukipata ladha ya muziki wa mbali.

Ilipofika saa nne usiku, tulipanga kuondoka. Sanchi alionekana mwenye furaha kubwa sana na alishukuru kwa nafasi ya kumwona mama J na kumfahamu, na aliahidi kwamba kila anapokuwa Dar es Salaam kwa shughuli za kampuni, atahakikisha anampitia kumsalimia.

Tuliondoka pale, nikianza kumshusha mama J nyumbani. Baada ya hapo, nikaondoka kumpeleka Sanchi hotelini. Njiani, alionekana kimya, akiniangalia kwa makini kama mtu aliye na kitu cha kuzungumza lakini hawezi kupata maneno.

Tulipofika hotelini, nilimsindikiza hadi kwenye room yake. Alinikaribisha ndani, kisha akasema kwa upole lakini kwa uthabiti:

“Usiondoke subiri.”

Nilikuwa nimesimama nikiwa nimeganda, bado sijielewi kabisa alitaka kusema nini. Muda ulikuwa umeenda sana, na hata lile wazo la kumpeleka hotelini lilikuwa kama nimejilazimisha tu.

“Sanchi, kuna jambo? Nina haraka sana,”
nilimuuliza kwa sauti ya utulivu.

Aliniangalia kwa tabasamu la ajabu na kusema,

“Karibu ukae kitandani, I want to show you something.”

Nilimtazama Sanchi kwa jicho la mzaha, lakini ndani ya kichwa changu mawazo yakaanza kunijia vibaya maana nilihisi anataka mashine, si kitu kingine. Hata hivyo, kwa upande wangu sikuwa na mpango wa kumtamani Sanchi. Nilimuheshimu sana, na nilishajiapia moyoni kwamba sitawahi kufanya kitendo kama hicho naye, haijalishi mazingira yatakuwaje.

Baada ya Sanchi kuona bado nimesimama nikimwangalia, aliendelea kuongea kwa sauti ya upole,

“Insider, nimekuita kwa sababu nataka kuongea na wewe jambo, tafadhali.”

Nilijikuta nikichukua hatua chache na kukaa pembeni yake, nikisubiri kuona ni nini hasa anataka kuniambia. Sanchi akatabasamu kidogo, kisha akasimama taratibu, akaenda kufungua begi lake. Alitoa bahasha ndogo ya kaki na kunipatia, akisema kwa sauti ya utulivu, “Fungua hii, tafadhali.”

Nilianza kupata hamu ya kujua ni nini kilichokuwa ndani ya ile bahasha ndogo ya kaki. Ilikuwa nzito kidogo, jambo lililonifanya niwe na shauku zaidi. Taratibu nilianza kuifungua, nikatoa kitu kilichong’aa chenye umbo la mstatili. Nilipotazama kwa karibu, nikaona maandishi yaliyosomeka 100g, palepale nikatambua ni dhahabu.

“Gold?” niliuliza kwa mshangao, nikimwangalia Sanchi usoni.

“Yes, wala hujakosea,” alijibu Sanchi huku akinikazia macho kwa namna isiyoelezeka.

Nilibaki nikiiangalia kwa mshangao. Mara ya mwisho kushika dhahabu ilikuwa enzi za marehemu Mzee Pama ilikuwa ni kumbukumbu ya zamani kidogo. Niligeuka nikamtazama Sanchi kwa uso wa kuuliza, nikasema kwa sauti ya chini:

“Hii umeipata wapi mama?”

Alitulia kidogo, akavuta pumzi kisha akaniambia,

“Ngoja nikwambie jinsi nilivyoipata hii dhahabu, lakini kabla sijafika huko, nataka nikupe historia kidogo ya maisha yangu. Insider, it’s a long story.”

Nilikaa kimya nikimsikiliza kwa makini. Akaanza kunieleza maisha yake, kutoka alipotoka, changamoto alizopitia, na namna alivyojenga ujasiri wake. Ni story ambayo ilinigusa sana moyoni kwakweli na nilijikuta nikianza kupatwa na huruma juu yake.

Baada ya muda, akaja kwenye sehemu ya dhahabu. Aliniambia aliikuta ndani ya begi la jamaa yake, baada ya kumuachia pamoja na nguo zake azifue. Kipindi anafanya usafi wa bag ndipo alipokutana na dhahabu hiyo na kuihifadhi kwa siri hadi leo. Aliniambia tayari miezi tisa ilikuwa imepita tangu awe na hii dhahabu, na yule jamaa hajawahi kuulizia, inawezekana kabisa ameisahau.

Nilimtazama kwa mashaka, nikasema,

MIMI: “Sio amekuwekea trap?”

SANCHI: “No, mazingira niliyoikuta hii dhahabu yalikuwa ya kujificha sana. Ndomana nasema huenda ilisahaulika na yeye hajui kinachoendelea, so! Hakuna njama hapo.”

Nikavuta pumzi ndefu, nikaiangalia tena ile dhahabu.

MIMI: “Hii ina gramu 100, ambayo ni zaidi ya milioni thelathini! Sasa kwanini umenionesha mimi hii?”

SANCHI: “Hapo sasa tupo kwenye point. Nataka niiuze, lakini ninaogopa sana. Hata sijui nianzie wapi.”

Nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa kabla ya kumjibu,

MIMI: “Kuhusu kuiuza, hakuna tatizo. Mimi namjua mtu, ni mzee wangu wa kuaminika. Anaweza kukusaidia, ila kwa usalama wako itabidi subiri kwanza. Hata mwaka ukipita, tutatafuta namna sahihi ya kufanya.”

SANCHI: “Poa, lakini nataka nikuachie ukae nayo hadi tutakapoonana tena kwa ajili ya hili.”

Nilinyamaza kwa muda, nikamtazama kwa makini.

MIMI: “Mmh! Hapana, wewe nenda nayo iendelee kuwa mikononi mwako. Usiniamini sana unajua binadamu tunabadilika.”

Ulipita ukimya wa sekunde chache Sanchi bila kujibu na alionesha kufikiria jambo. Simu yangu ilianza kuita muda ule na baada ya kuitoa mfukoni, ni wife alikuwa akipiga. Nilipokea haraka na kumjulisha kuwa niko njiani kurudi nyumbani maana alianza kuuliza maswali mengi sana muda huu. Baada ya kumaliza mazungumzo, nilisimama, nikamkumbatia Sanchi kwa heshima, tukaagana kwa maneno mafupi. Niliondoka pale hotelini kwa kasi nikienda na uelekeo wa home.

Baada ya kufika kwenye mataa ya Namanga, nikiwa naelekea upande wa Ubalozi wa Marekani, nilipigiwa simu na Jimmy. Nilipokea na tukaanza mazungumzo. Alianza kwa kuniomba radhi kwa kushindwa kupokea simu yangu hapo awali, akifafanua kuwa alikuwa bize na mambo ya msiba. Kwa upande wangu, tayari nilikuwa nimeshasahau kuhusu taarifa za msiba ule wa Ethiopia ambazo nilipewa na Iryn.

Nilimpa pole na nikajifanya kusudio langu la kumpigia lilikuwa ni kuwasilisha salam za rambirambi pamoja na kujua maendeleo ya msiba. Baada ya mazungumzo mafupi, nilimueleza wasiwasi wangu juu ya Iryn kwa kuwa amekuwa hapokei simu zangu. Jimmy aliniambia kuwa Iryn hakusafiri kwenda Ethiopia kwa sababu ya mtoto, na badala yake walienda bibi pamoja na Samantha.

Jimmy aliongeza kwamba mara ya mwisho kuongea na dada yake ilikuwa jana asubuhi, na alimueleza kuwa atakwenda kumsalimia baba yake. Alinifanya nitulie na kuniambia niondoe wasiwasi, akiahidi kumtafuta Iryn na kunipigia baadaye kunipa taarifa kamili ya kinachoendelea, tukaagana.

Sasa, wakati nipo barabarani kuelekea Kawe kwa mwendo wa kasi kuwahi kurudi nyumbani, simu yangu ilianza kuita. Nilipoangalia, nikaona ni Iryn. Nikapokea haraka, tayari nikiwa na hasira zangu moyoni.

MIMI: “Kwa nini hupokei simu zangu toka jana? Ulikuwa wapi?”

IRYN: “Hubby, hata salamu hakuna?”

Nilishtuka kusikia hiyo “Hubby”. Kwa muda wote tuliokuwa pamoja, hajawahi kunitaja hivyo hata mara moja. Maneno yake yalipunguza joto la hasira yangu ghafla.

MIMI: “Where have you been? Unajua unanipa presha bila sababu?”

IRYN: “I’m sorry… niliondoka kwenda kwa baba, kwa bahati mbaya nikaacha simu. Haikuwa makusudi.”

MIMI: “Kwa nini hukuniambia unaenda kumsalimia baba?”

IRYN: “Babu yake Aria anaumwa. Nilikuwa na haraka sana hadi nikasahau hata simu. Ningekupa taarifa, baby. I’m really sorry.”

MIMI: “Sawa baby, usijali.”

Kutoka hapo mazungumzo yakawa ya upole na akaanza kunisimulia maendeleo ya afya ya baba yake na kuniambia kuwa kwa sasa hali inaendelea vizuri.

Kisha, akarudi kwenye habari za kampuni ile tunayoifuatilia, kampuni ambayo tayari tumeshapoteza muda na nguvu nyingi kuijua undani wake. Aliniambia kuwa yuko karibu kumjua Steve Jobs halisi wa nyuma ya mchezo mzima mchafu unaoendelea. Hakuingia kwenye maelezo marefu sana, bali aliniambia niendelee kuwa na subira. Alisema bado anaendelea kuchimba taarifa taratibu, na muda si mrefu atakuwa na ukweli kamili ulionyooka sawasawa.

Baada ya habari zile, Iryn akanipa taarifa nyingine nzito zaidi. Alianza kuniambia kuhusu mama yake mdogo kama mwanamke ambaye kwasasa anaonekana kuwa kama mwiba kwenye kampuni za mzee wake. Alisema kadri siku zinavyosonga, ndivyo anavyoendelea kugundua mambo ya hovyo aliyokuwa anayafanya nyuma ya pazia.

Alisisitiza kuwa kwa sasa anasubiri Aria afikishe angalau miezi sita ili aweze kuanza kusimamia kampuni zote kikamilifu. Ila, wakati huo huo, tayari ameanza kufanya mageuzi taratibu kama kubadilisha baadhi ya wafanyakazi na kuweka watu wake anaowaamini, ambao wanaweza kufanya kazi kwa uadilifu.

Kwa upande mwingine, aliniambia wazi kuwa yeye na mama yake mdogo hawako kwenye maelewano tena. Sababu kubwa ni kwamba tayari ameshajua siri nyingi za upotevu wa fedha na mianya ya kifedha iliyokuwa ikipigwa kwa ujanja ujanja ndani ya kampuni. Kwahiyo anajaribu kuziba mianya hiyo yote, jambo ambalo linaonekana kumuumiza sana mama yake mdogo.

Niliendelea kumsisitiza Iryn awe makini sana na mama yake mdogo, nikijua wazi kwamba mama yake mdogo angeweza kufanya jambo lolote baya endapo angehisi anapoteza nafasi yake. Hata hivyo, Iryn alinituliza kwa upole, akinihakikishia kuwa anafahamu tabia zake, anajua anachokifanya na yuko makini kila hatua.

Mazungumzo yetu yaliendelea kwa muda mrefu, nikiwa bado barabarani hadi nilipowasili nyumbani. Nilikaa ndani ya gari kwa dakika kadhaa, nikihitimisha mazungumzo hayo ambayo yalikuwa yamenikamata kiakili na kihisia kiasi cha kushindwa hata kushuka mara moja. Baada ya kuagana, ndipo polepole nikaiingiza gari ndani na kurudi kwenye utulivu wangu wa kawaida.

******
Asubuhi baada ya kuamka nakutana na ujumbe kutoka kwa Dullah, ambaye aliomba tukutane jioni kwaajili ya maongezi mafupi. Nilireply ujumbe wake kwa kumwandikia sawa nitafanya hivyo. Niliingia bafuni kuoga, kisha nikajiandaa haraka na kuondoka kwenda ofisini kwaajili ya majukumu yangu ya kila siku.

Baada ya kufika ofisini nilifanya mawasiliano na mama Janeth, nikampa taarifa ya kumalizika kwa kazi yake ambayo alinikabidhi. Mama alifurahi sana kuzisikia taarifa zile na hakusita kunishukuru na akasema ataniwekea vocha kwenye account yangu.

Tuliagana pale na kuendelea na majukumu yangu na baada ya dakika chache kupita aliingia Winny ofisini kwangu kwa lengo la kunipa ripoti ya Zanzibar. Winny ni rafiki yangu sana, hivyo tulianza kuzinguana pale kwa kupeana maneno ya utani, kisha akanipa ripoti ya Zanzibar na ukweli alisema kwamba, alienjoy sana.

Winny aliniaga anakwenda kuendelea na majukumu yake na mimi nikaanza kufungua na kupitia mails za ofisi. Nilikutana na mail kutoka kwa Hilda ambayo ilihusu yeye kwenda likizo fupi ya wiki mbili. Nilibaki nikishangaa na kujiuliza pale mbona ghafla hivi? na hajanipa taarifa?. Niliwaza pale huenda tofauti zetu ndiyo zimepelekea Hilda kwenda likizo bila kunijulisha.

Niliumia moyoni, lakini nikaendelea kupitia mails zingine taratibu, nikakutana tena na mail yake aliyotuma wiki mbili zilizopita akitaarifu kuhusu yeye kwenda likizo fupi ya wiki mbili. Hata hivyo, bado niliendelea kutafakari kuhusu hili la Hilda kushindwa kunipigia simu na kwenda likizo kimya kimya. Niliendelea kutafakari kwa kina na kuona kwamba hatua aliyofikia Hilda kwasasa ni mbaya sana, hivyo lazima nichukue hatua za haraka dhidi yake.

Wakati nikiendelea kutafakari juu ya hili, Lucy aliingia ofisini na baada ya kuniona, kwa sauti ya furaha akaniita ;

LUCY: “Insider….”

Ilibidi niamishie akili yangu kwake sasa;

MIMI: “Nambie mama za kutoka Zanzibar.”

LUCY: “Was very nice kwakweli, licha ya kufanya kazi but tulienjoy sana na Winnie.”

MIMI: “Ningekuwa mimi ndiyo wewe ningeenda na Bob Zanzibar, ulianzaje kwenda peke yako?”

Lucy aliangalia kwa macho ya upole na kutabasamu kwa pamoja;

LUCY: “Yaani wewe Insider sawa bhana, nimekuletea zawadi ya tende, tena hizi ni original kazi kwako.”

MIMI: “Ahsante sana malkia wangu, usingekuwa na ukaribu na Iryn ningekuwa nimeomba unibless sio kwa upendo huu.”

Lucy alicheka kwa sauti ya juu na tukaendelea na story zingine, kubwa ilikuwa kuhusu Iryn. Kwa upande wake alitamani sana kujua kama nilifanikiwa kuwasiliana na Iryn, pamoja na maendeleo yake. Baada ya hayo tukahamia kwa Hilda ambapo Lucy aliuliza sababu ya ugomvi wetu ni ipi ili aweze kutusuluhisha.

Sikuwa tayari kumwambia Lucy sababu ya kutofautiana kwangu na Hilda. Badala yake nikahamisha mada kwa kumuuliza kama anataarifa ya Hilda kwenda likizo. Lucy alisema Hilda alimpa taarifa tangu ijumaa ya kuanza likizo yake.

Licha ya kujaribu kubadilisha mada bado Lucy aliendelea kuzungumzia suala la Hilda na aliniomba sana nikae chini na Hilda tumalize tofauti zetu. Nilimuahidi Lucy aniachie hili suala, nitamtafuta Hilda na tutamaliza tofauti zetu na kurejesha malewano yetu kama awali.

Ilipotimia jioni niliondoka ofisini kwenda kuonana na Dullah Makumbusho kwenye ofisi yake. Nilikuwa nafahamu fika suala atakalokwenda kulizungumzia, ni suala la Ghati wala hana habari nyingine mpya. Ulikuwa ni mwendo wa dakika 15 hadi nawasili pale ofisini kwake, lakini tukatafuta sehemu nyingine ya kukaa kwaajili ya maongezi.

Kama kawaida yetu tulianza maongezi kuhusu harakati na maendeleo ya familia zetu. Habari njema ni kwamba Dullah alinipa habari mpya kabisa kuhusu mke wake Latifah. Ni taarifa ambazo zilinishtua na kunifurahisha kwa pamoja;

DULLAH: “Kaka shem wako Latifah ni mjamzito, mimba ina mwezi sasa.”

MIMI: “Daah! Hongera sana Senior yangu karibu kwenye ulimwengu wa kuitwa baba.”

DULLAH: “Daah! Ahsante sana kaka hapa sasa natakiwa nianze jipanga taratibu hadi anapojifungua niwe vizuri kifedha.”

MIMI: “Ni jambo jema unapaswa kufanya hivyo, uwe unaweka fedha kwaajili ya mama na mtoto.”

DULLAH: “Ni wazo zuri kaka itabidi nifanye hivyo.”

MIMI: “Niambie Senior! Nasubiri kukusikiliza unachotaka kunambia japo najua.”

Dullah alianza kucheka pale na badale yake akaanza mada zingine kabisa;

DULLAH: Bro! Yule dada tuliyekuwa naye juzi Samaki hivi kweli hupigi pale? Maana ni balaa.”

MIMI: “Hamna kaka yule tunaheshimiana sana na ananisaidia sana kuangalia biashara zangu kule Dodoma lazima nicheze kete zangu vizuri.”

DULLAH: “Insider unabalaa sana yaani cycle ya wanawake wanaokuzunguka ni pandemic, umefanya mtoto wa watu Ghati alale kwa shida sana.”

MIMI: “Na ile siku nilipanga kumsindiza dada hotelini, lakini nilibadilisha mpango ule baada ya Ghati kuniganda na kuomba tuondoke wote.”

DULLAH: “Ulifanya vizuri ila sasa Ghati alinicheki na kunambia umemtakia maneno magumu sana.”

MIMI: “Maneno gani?.”

DULLAH: “Anasema umemtakia maneno mabaya kwa kinywa chako kwamba wewe lengo lako sio mahusiano ni kuhit tu.”

MIMI: “Sio kweli kaka sijamwambia hayo maneno, anataka kukuza mambo na ndo kawaida ya wanawake. Halafu Senior ngoja nikwambie kitu kaka inatakiwa tukikutana kama hivi tunaongea masuala muhimu ya biashara, na sio kuwapa airtime wanawake ambao hatuna future nao.“

DULLAH: “Ofcourse ila hapo kwenye kusema hatuna future nao ninakupinga Senior. Kuna wanawake ni potential na Asset, mfano kipindi umepata yale majanga Polisi kumbuka katika Wanawake wote kwenye simu yako, bado ulimtafuta Ghati aje akusaidie. Nataka kusema hivi, usimweke mbali maana alijitoa sana kwako kipindi kile, bado ni potential sana yule mwanamke.”

MIMI: “Unajua Senior Ghati kwasasa ni mshikaji wako na alichofanikiwa ni vile kujiweka karibu sana na wewe. Nataka nikwambie Ghati ataenda jinsi navyotaka mimi na sio anavyotaka yeye. Haya niliyomfanyia jana ni hatua za awali ambazo nazichukua ili kumteka akili yake na kuanza kumpeleka nako taka mimi.”

DULLAH: “Suala la mahusiano ni juu yenu ila jitahidi mmalize tofauti zenu yule ni familia.”

MIMI: “Hili suala niachie kaka.”

Baada ya maongezi kukamilika nilimuomba Dullah kuondoka ili niwahi kurudi nyumbani mapema kukaa na Familia yangu pamoja na kucheza na Junior.

*****
Wiki hii yote nilikuwa na ratiba ngumu sana, nikiweka nguvu kubwa kwenye maandalizi yangu ya kuanza masomo ya Master’s. Hata kazini sikuweza kuhudhuria ipasavyo kwa sababu nilikuwa nafanya ufuatiliaji, michakato na majibu ya maombi niliyowasilisha. Bahati nzuri nilifanikiwa kupata nafasi katika vyuo vitatu tofauti, na ndipo safari ya kuamua kozi sahihi ikaanza.

Kila mtu niliyemshirikisha alinipa ushauri wake wenye uzito. Mama mtoto wangu Iryn alinisisitiza sana nichukue MBA in Finance, akiamini itanijenga zaidi katika eneo la usimamizi wa fedha, maamuzi ya kifedha na mikakati ya kibiashara. Kwa upande mwingine, Mzee Juma yeye alitamani nifuate kozi ya Finance and Investment, kwa mtazamo kwamba italeta manufaa makubwa katika mustakabali wa uwekezaji na ukuaji wa miradi mikubwa. Wakati Kaka Allen yeye alipendelea nijiunge na Masters of Finance & Accounting, akilenga kuniona nikiwa na ustadi mkubwa zaidi katika uhasibu, uchambuzi wa taarifa za kifedha, auditing na financial reporting.

Kwa kifupi, kila mmoja wao alikuwa na hoja zake za msingi kulingana na nafasi, uzoefu na mtazamo wake kuhusu mustakabali wangu wa kitaaluma. Lakini, bado kwa upande wangu sikuwa na maamuzi sahihi na niliendelea kujipa muda kabla ya kufanya maamuzi.

Ijumaa niliamua kurejea kazini. Siku hii pia nilikuwa na ugeni maalum kutoka kwa Sanchi. Alikuwa amemaliza mkutano wa kampuni yao siku ya Alhamisi, hivyo nilimwomba abakie hadi Jumamosi ili Ijumaa tupate muda wa kuwa pamoja ofisini.

Alifika ofisini saa nne asubuhi, nilimtoka kwenda kumpokea na kisha nikaanza kumwonyesha sehemu mbalimbali za ofisi. Nilimtambulisha kwa Lucy pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo wakati huo. Baada ya hapo nikamuacha na Winny, ambaye aliendelea kumpa maelezo kuhusu bidhaa na huduma tunazotoa kama kampuni.

Baada ya kumaliza kuzunguka ofisini, tulitoka nje tukakaa kwenye garden. Hapo ndipo mazungumzo yakawa ya kina zaidi, nilianza kwa kumkumbusha ile simulizi aliyoniambia mara ya mwisho hotelini, kuhusu maisha yake.

MIMI: “Kwahiyo Sanchi, baba wa mtoto wako yuko wapi sasa?”

SANCHI: “Yuko hapa hapa Dar es Salaam, lakini tumekuwa hatuwasiliani kwa muda mrefu sana. Hata jina la ukoo wake kwa mtoto nililazimika kulibadilisha, sababu ya upumbavu wake na jinsi alivyotoka kwenye maisha yetu.”

Nikabaki kimya kwa sekunde kadhaa, nikihisi maumivu yake.

MIMI: “Kwa kweli story yako ilinifanya nijisikie vibaya sana, ulichopitia si kitu rahisi.”

SANCHI: “Ndiyo maisha Insider hata wewe ninaamini kuna mengi umeyapitia siyajui. Nikuambie kitu Insider, niimekaa na mama J, na kwa muda mfupi sana tumeharmonize.”

Nilimkatisha maongezi yake pale;

MIMI: “Sababu nyote ni wachaga basi.”

SANCHI: “Hapana hio sababu. lnsider, tulia na hawa wanawake wawili uliowazalisha, usihangaike na wanawake wa nje tena. Una wanawake wazuri, wanaojitambua, wachapakazi. Ukiwekeza nguvu zako kwa hawa wanawake, utaenda mbali sana. Trust me.”

Nikatabasamu huku nikitikisa kichwa,

MIMI: “Naona leo umekuja na lecture ya mahusiano eeh?” Tukaishia kucheka.

Saa saba mchana, Lucy alikuja kutuchukua twende kula lunch. Lengo la Lucy ilikuwa, turudi mapema ofisini aweze kumhudumia Sanchi kama nilivyoahidi. Nilikuwa nimempa Sanchi ofa ya kuchagua huduma yoyote atakayoenda kufanyiwa.

Wakati tuko kwenye lunch, nilimueleza Lucy kwa utulivu na uwazi kuhusu nafasi ya Sanchi katika maisha yangu, jinsi anavyonisaidia kusimamia mambo yangu Dodoma, na namna walivyofahamiana na Iryn. Lucy alibaki kushangaa, akisema hakujua kama mambo yalikuwa yamefika huko, na tukacheka sana tukibadilishana stories nyingine za maisha.

Ile siku nilishinda na Sanchi hadi usiku na tukagana pale na nikampa ahadi ya kumuona soon Dodoma na nilimwambia nitaenda na mama J. Sanchi aliishia kunishukuru sana kwa yote na akasema nimpe taarifa mapema kabla hatujaenda Dodoma.

Baada ya Uber kufika ili kumchukua na kumpeleka hotelini, nilitoa bahasha ndogo ya kaki nikampa kama zawadi yangu na tukaishia kukumbatiana kama ishara ya kuagana, akapanda na kuondoka. Wakati huo, Lucy naye alikuwa tayari kabisa kuondoka. Bila kupoteza muda, tulianza safari ya kurudi nyumbani.

****
 
SEASON 03
CHAPTER 13


CONTINUE:
Jumamosi asubuhi, nilipokea simu kutoka kwa Sanchi. Aliniambia kuwa anaondoka kuelekea Dodoma, nami nikamtakia safari njema. Baada ya mazungumzo naye, nilimpigia Savinna, dada tuliyefahamiana Zanzibar ili tukubaliane muda wa kukutana. Tangu tuachane Zanzibar tayari mwezi ulikuwa umeshapita, lakini ratiba zangu zilizokuwa zikigongana mara kwa mara zilikuwa zinatufanya tushindwe kukutana kwa urahisi.

Baada ya kuwasiliana, Savinna aliniambia atakuwa ofisini kuanzia saa tano asubuhi, na kwamba muda huo naweza kufika. Mimi nikaingia bafuni kuoga na kujiandaa mapema, nikisubiri saa zisonge.

Ilipofika 10:00 AM, niliamua kuondoka na kuelekea Nyerere Road, karibu na TCC ambako Ofisi Kuu (Head Office) ya kampuni yao ilipokuwa. Kichwani mwangu nilikuwa na mpango mkubwa wa kukuza biashara yangu, jambo lililonifanya nianze kuangalia uwezekano wa kupata mkopo ili kuongeza nguvu ya mtaji.

Kitaalamu, kampuni au wataalamu wa fedha hushauri kutumia 50% equity (hisa) na 50% debt (mkopo) ili kupata uwiano bora wa gharama na usalama wa kifedha (optimal capital structure). Faida kubwa ya mkopo ni kwamba riba unayolipa huwa tax deductible, hivyo inapunguza kiasi cha kodi kinacholipwa.

Biashara yangu ikiwa bado ni mpya, nilijua kupata mkopo benki kungekuwa kizungumkuti, hasa ukizingatia nimesajili kampuni. Kwa hiyo nilihitaji microfinance ambayo ingeweza kunisaidia kufikia hatua ya pili ya maendeleo ya biashara bila mimi kutoa pesa kutoka mfukoni tena.

Niliendesha gari mpaka ofisini kwao, mkabala na jengo lililokuwa karibu na TCC. Nilipowasili, nilipokelewa vizuri sana. Tuliingia ndani, akanikaribisha kuketi kwenye sofa na kunipatia kikombe cha kahawa. Nikiwa nimekaa, macho yangu yalikuwa yanazunguka kila kona kama mwizi anayechunguza mazingira, ukweli ile ofisi ilikuwa imetulia, ni ya kisasa, na ya kuvutia kweli, executive kabisa.

Savinna alikaa kisha akanigeukia taratibu:

SAVINNA: “Karibu sana Investor, what can I help you with?”

Alisema kwa sauti ya utani na madaha. Mimi nilitabasamu tu.

MIMI: “Waoh! You look so beautiful in this office.”

Alijikuta akitabasamu na tukacheka wote.

SAVINNA: “Insider una mambo! Za tangu Zanzibar? Maana simu zangu hupokei, mara hupatikani, message nazo hujibu kwa kubahatisha. Nilianza kuhisi kama tayari nimempoteza Investor wangu.”

MIMI: “Hahaha! Pole. Baada ya kuachana Zanzibar nilienda South Africa, kisha Zambia, ndo nikarudi. Ratiba zilikuwa ngumu sana kwangu.”

SAVINNA: “Pole sana na karibu tena, hii ndiyo head office yetu. Hebu nieleze, biashara zako zinaendeleaje?”

MIMI: “Namshukuru Mungu zinaenda vizuri. Na kilichonileta kwanza ni kufahamu huduma mnazotoa aina za mikopo, riba, na masharti mengine.”

Savinna alinielezea kwa utaratibu huduma zote wanazotoa kwenye kampuni yao. Alinionyesha nia ya kunisaidia ili tuweze kufanya kazi pamoja, jambo lililonipa faraja. Baada ya kumaliza mazungumzo ya msingi, tulibadilisha mada na kuzungumza masuala mengine ya kawaida. Pia aliahidi kwamba siku moja atakuja kutembelea ofisi yetu Masaki.

Baada ya kuwa wote kwa zaidi ya saa moja, tuliagana, kisha nikaanza safari ya kuelekea Madale kwa Mama Wawili. Mimi na mama wa2 tulikuwa tukijuliana hali mara kwa mara lakini muda ulikuwa umepita bila kuonana. Nilikuwa nimempa ahadi kwamba Jumamosi hii nitapita kwake, hivyo nikaona ni wakati mzuri kutimiza hilo.

Safari ya kuelekea Madale haikuwa fupi, ulikuwa ni mwendo mrefu sana mpaka nawasili nyumbani kwa Mama Wawili. Nilipofika, dada mmoja mgeni ambaye sikuwahi kumuona hapo awali alinipokea kwa tabasamu na kunikaribisha kwa kufungua geti, na kunikaribisha hadi ndani sebleni. Aliniambia nisubiri kidogo kwani Mama Wawili alikuwa ndani akijiandaa.

Niliketi kwenye sofa nikichezea simu yangu, huku nikisubiri kwa utulivu. Baada ya muda mfupi, yule dada aliniletea juisi kwenye glass, nikapokea kwa shukrani. Haikuchukua dakika kumi, Mama Wawili alitokea sebleni akiwa na uso wa furaha ulionyesha wazi amefurahi kuniiona, na kunikumbatia kwa nguvu.

MAMA 2: “Insider karibu sana, nilikumiss sana wewe mwanaume.”

Akakaa pembeni yangu kwa ukaribu na tukaanza kuangalia pale, na maongezi yakaendelea;

MIMI: “Ahsante sana, nasikitika sana mke wangu Pili kuondoka kwenda masomoni bila mimi kumuaga.”

MAMA 2: “Kipindi anaondoka ulikuwa South Africa. Atakaporudi likizo utamuona, usiwe na shaka.”

MIMI: “Alinitumia ujumbe lakini siku jibu, nilikuwa nimebanwa sana. Nitamtafuta baadae nimsalimie na nijue anaendeleaje.”

MAMA 2: “Fanya hivyo, lakini tangu litokee lile jambo kule shuleni, Pili ananilaumu sana. Anasema kaka Insider ameamua kukutenga kwa sababu ya lile tukio.”

MIMI: “Hapana bwana! Yale mambo tulishamaliza na hakuna haja ya kuyafufua tena. Mimi na wewe tumetoka mbali sana, hivyo usijipe mashaka yasiyo na msingi.”

Mama wawili akanitazama halafu akatabasamu kidogo, kama mtu aliyehisi faraja.

MAMA 2: “Lakini vipi, naona unazidi kunawiri, umekuwa handsome mno siku hizi.”

Nilihisi aibu baada ya kusikia maneno haya, maana sikuyategemea kabisa kuyasikia;

MIMI: “Ahsante sana, Mungu anaendelea kunibariki. Lakini mke wangu Rachel yuko wapi? Simuoni.”

MAMA 2: “Rachel yupo, ila kaenda mjini na mama yake mdogo.”

MIMI: “Kwa kweli njaa inanibana. Kama kuna chakula nitashukuru sana.”

MAMA 2: “Ngoja nikuandalie mkwe wangu, siwezi kukuacha na njaa.”

Aliposimama kuelekea jikoni, macho yangu yakagota kwenye tumbo lake. Lilikuwa limejionyesha kiasi ambacho mtu wa kawaida hawezi kupuuzia. Sikuwa na uhakika asilimia mia, lakini kila dalili zilikuwa wazi kwamba Mama Wawili alikuwa mjamzito.

Baada ya muda aliniita kwenye dining kwaajili ya kupata chakula, hivyo nikahama kutoka sebleni. Nilipoketi mezani, sikutaka kupita bila kuuliza:

MIMI: “Mama mkwe, usiniambie una mpango wa kuniongezea mke mwingine. Naona utukufu umeanza kuonekana kwa mbali au nakosea?.”

Alinitazama kwa aibu, hakutegemea mimi ningejua kuhusu hali yake. Sura yake ikaanza kuchanua tabasamu laini;

MAMA 2: “Ndio Insider nategemea mtoto mwingine.”

MIMI: “Hongera sana! Nimefurahi kusikia hiyo taarifa. Ila baba yake… huyu ni mtu mwingine tena?”

Mama wawili alinitazama kimya, akatingisha kichwa taratibu kuashiria ndio, bila kusema neno zaidi.

MIMI: “Basi kuanzia leo nitakuita Mama Watatu.”

Mara akacheka sana, mpaka akashika tumbo lake. Tuliendelea kuzungumza mambo mengine ya kawaida. Aliniuliza pia kuhusu Iryn pamoja na Maggy, nami nikamwambia kuwa wote wanaendelea vizuri, ila kwa sasa Iryn ana mtoto na yuko South Africa. Mama Wawili alishangaa sana, akaniomba nimsalimie.

Nilikaa pale kwa zaidi ya masaa mawili tukaongea, tukacheka, na kweli alifurahia sana ujio wangu. Niliamua kuagana pale maana nilikuwa na ratiba nyingine tena, hivyo nikaelekea Mbweni. Lengo lilikuwa kwenda kuonana na Jane, lakini kabla sijafika nikaamua nipitie kwa Ghati kwanza. Tangu nikiwa kwa Mama Wawili nilikuwa nikiwasiliana naye na nikamtaarifu kuwa nitapitia kumsalimia.

Wakati nipo njiani mawazo yangu yalirudi kwa Mama Wawili. Kitendo cha kuwa na watoto watatu, kila mmoja na baba tofauti, kilinichanganya sana. Nikaanza kuwaza kuhusu binti zake, kwani mabadiliko ya tabia yanaanzia nyumbani, na niliogopa huenda akawarithisha tabia ambazo zinaweza kuwaharibu mbele ya safari. Mawazo haya yalinisumbua sana nikiwa barabarani.

Nilipofika kwenye apartment ya Ghati, nikamtumia ujumbe kuwa nimefika ili afungue geti. Baada ya kuingiza gari ndani, nikaingia sebleni nikisubiri. Alikuwa anaongea na simu tangu nilipofika, hivyo nikakaa kimya nikisubiri amalize. Dakika 10 zikapita, 20… hadi nusu saa. Bado alikuwa anaongea na simu. Ukweli hili lilinikasirisha na niliona dharau waziwazi.

Nikaamua kuinuka na kwenda kibarazani alikokuwa. Nikamwambia,

MIMI: “Ninaondoka.”

Kauli ile ndiyo ilimfanya hatimaye aache kuongea na simu.

GHATI: “Insider sasa unaondoka kwenda wapi wakati unaona nilikuwa naongea na simu?” aliuliza kwa mshangao.

MIMI: “Baada ya kukwambia naondoka ndiyo umeamua kuacha kuongea na simu?. Nimekuja hapa, hujanikaribisha, hujanipa hata muda wako kama hii sio dharau, ni nini?”

GHATI:, “Mimi naona unacomplain bila sababu za msingi wakati unaona fika naongea na simu.”

MIMI: “Sijacomplain concern yangu ni moja tu, ulipaswa kunambia ningoje kama simu ni ya muhimu. Angalau ningeona unaniheshimu na kujali uwepo wangu, hatujasalimiana halafu bado unaniacha sebleni peke yangu. Ni mpaka niseme ninaondoka ndiyo unanisikiliza?”

Nilipoanza kuondoka, alianza kunivuta nisiondoke. Nikamwambia

“Ghati nipishe niondoke bhana kabla sijaharibu siku yako.”

Baada ya kuona ananisumbua, nilimsukumia kwa nguvu kidogo akakaa kwenye sofa, nami nikaondoka kwenda kwa Jane. Kutoka kwake hadi kwa Jane haikuwa mbali, ndani ya dakika 10 tayari nilikuwa nimefika.

Baada ya kuwasili nyumbani kwa Jane nilingia ndani sebleni, ghafla nikakutana uso kwa uso na Mary akiwa amembeba Johnson. Tulitazamana sekunde kadhaa kila mmoja akiwa hajategemea kumkuta mwenzake pale. Sikumsemesha, nikaenda moja kwa moja kukaa kwenye sofa. Mara nikasikia Vicky akinipigia kelele kutoka jikoni, kisha akaja sebleni.

VICKY: “Wewe mwanaume unamaringo sana! Hivi ukipokea simu zangu utakufa?”

MIMI: “Hahaha Vicky, kwa kulalamika hujambo. Kama ningekuwa mwanaume wako si ungenitesa sana?”

VICKY: “Insider, ubadilike. Ukipigiwa simu pokea, na kama uko busy, call back baada ya kumaliza. Hivi juzi nilikupigia sana nikupe taarifa kuhusu hawa mbwa, hukupokea simu kabisa. Nilimind kweli.”

Vicky alionekana kuchukizwa kweli na tabia yangu ya kutopokea simu zake. Mary, ambaye muda wote alikuwa akijifanya kucheza na Johnson, ghafla alitulia kana kwamba anataka kusikia kila neno.

MIMI: “Vicky, pole mke wangu. Kwa kweli niliona simu zako lakini nilikuwa nimebanwa sana, ubaya nikasahau kukurudia. Nakuomba msamaha, haitajirudia. Sometimes ukiona sipokei, nitext WhatsApp.”

VICKY: “Wewe huyo utafikiri unajibugi message, kwanza angalia message nazokutumia kama huwa unazijibu. Wewe mwanaume hapana kwakweli, sijakutana na mwanaume mwenye maringo kama wewe, hadi huwa najiuliza ni mimi tu unanifanyia hivi au na wengine pia.?”

Kauli ile ilimfanya Mary atulie zaidi, kana kwamba anasubiri jibu langu kwa hamu.

MIMI: “Vicky, yaishe basi. Nimeomba msamaha, mumy. Sasa twende tukawaone mbwa.”

Tuliinuka wote kwa pamoja kwenda kwenye nyumba ya mbwa na Vicky alinambia Storm (Shepherd) alikuwa kama kapatwa na homa, alikuwa anakula chakula kwa tabu sana. Vicky aliendelea kunieleza kwamba baada ya dokta kuja kumtibu ndo kurudi katika hali yake ya kawaida.

Kwa upande mwingine, mbwa walizidi kukua kwa kasi na sisi tuliendelea na mazungumzo na Vicky. Habari iliyokuwa ikitawala ni kuhusu Mary, kwani Vicky alionekana kujua kila kitu kinachoendelea kati yangu na yeye.

VICKY: “Mmegombana na mpenzi wako Mary?”

MIMI: “Hapana, tuko sawa… na kwa taarifa yako Mary sio mpenzi wangu.”

VICKY: “Unadhani sijui? Mary alikuwa anamueleza dada Jane kuwa hamko sawa. Nilikuwa jikoni, niliwasikia wakiongea.”

MIMI: “Acha umbea basi… naona unazidi kunawiri mtoto, nipe siri ya mafanikio.”

Sikutaka kuendeleza mada ile, ikabidi nibadilishe mazungumzo haraka.

VICKY: “Ah! ni likizo tu, chuo huwa kina-nichakaza sana.”

Kwa mbali nilisikia Jane akiniita, nikamuacha Vicky na kwenda sebleni. Sababu kubwa ya kwenda kwake ilikuwa kuendelea na mipango yetu ya biashara. Kwa upande wangu tayari nilikuwa nimeshakamilisha usajili wa kampuni, na fremu ya biashara ilikuwa imepatikana. Jane alitaka kufahamu kwa undani kuhusu bei na mtaa fremu ya biashara ilipo.

Nilimweleza kila kitu kuhusu bei ya fremu na location yake ilipo na nikamsisitiza kwamba eneo lile ni zuri sana kwa biashara. Baada ya mazungumzo yale tulikubaliana kuwa kesho, siku ya Jumapili, tutaenda Kariakoo kwenda kuikagua na kufanya malipo moja kwa moja.
Wakati tunajadili haya, Mary alikuwa ametoka nje ni kama alitaka kutupa nafasi ya kuongea mambo yetu kwa uhuru.

Baada ya kumaliza maongezi ya kibiashara, Jane akaanza kuniuliza kuhusu mahusiano yangu na Mary. Alisema Mary kamwambia kwamba hatuko sawa, ingawa hakutaka kueleza sababu.

Sikutaka kuzungumzia kuhusu haya na niliishia kumwambia kwamba ni masuala ya mapenzi na kugombana ni jambo la kawaida ila tutakaa sawa. Mazungumzo yetu yalikatishwa na kelele za Johnson aliyeanguka na kuanza kulia kwa sauti ya juu. Hivyo nikamnyanyua na kuanza kumbembeleza pale.

Johnson alikuwa anakua kwa kasi sana, na umri wake ulipofika hatua ya kuanza utundu wa kushika na kusimamia vitu, hivyo alitaka usimamizi kila dakika. Niliishia kucheza naye sebuleni na baadae Jane alipoomba amnyonyeshe, mimi nikatoka nje kumtafuta Mary. Lakini sikumkuta pale kwenye kibaraza, ikanilazimu kuzunguka upande wa pili wa nyumba na ndipo nikamuona amesimama peke yake, akiongea na simu. Nilipomsogelea tu, alitaka kuondoka. Nikamzuia taratibu kwa mkono, ndipo akaanza kuongea:

MARY: “Insider, leave me alone. Nipishe nipite.”

Nikambana katikati ukutani, mikono yangu ikipita ubavuni mwa kiuno chake huku yeye akiwa katikati.

MIMI: “Kwanini umeniblock?”

MARY: “It’s over, Insider.”

MIMI: “Naelewa… lakini hatuwezi kuachana kwa namna hii. Ni utoto, kama mtu ambaye bado hajakomaa.”

MARY: “Hayo ni maamuzi yangu, si yako. Nimeamua kuishi hivyo. Sitaki hata kukuona kwenye mboni zangu, nakuchukia sana.”

MIMI: “Si kila mfungwa gerezani ana hatia, wapo waliobebeshwa mizigo ya uonevu na maamuzi ya bahati mbaya. Ukinihukumu bila kunisikia, jua unafuata nyayo za hakimu aliyekosea na unatoa hukumu kwa pupa.”

MARY: “Okay… let me go.”

MIMI: “Sawa Mary, nakuacha uende. Ila sikuwahi kufikiria kama kuna siku mahusiano yetu yangekuja kuisha kwa namna hii. Ulikuwa mmoja wa wanawake muhimu sana niliowahi kuwa nao, umeniachia kumbukumbu nyingi. Nakutakia kila la heri.”

Mary aliondoka kwa haraka, nilibaki nikimkata jicho mpaka alipopotea kwenye kona. Niliishia kung’ata meno kwa hasira na maumivu yaliyojificha ndani. Baada ya kukaa nje kwa dakika kadhaa, niliingia ndani kumuaga Jane, kisha nikaondoka eneo lile nikiwa mzito moyoni.

Barabarani nilikuwa nimeshikwa na mawazo mazito kuhusu Mary. Nilijua wazi nimempoteza, maana vile alivyoongea na kunitazama tu sikuweza kudanganya nafsi yangu, Mary alikuwa serious sana. Nilikuwa nawaza namna ambayo ningeweza kukaa naye chini, tuzungumze, tuyamalize na tuendelee na mahusiano yetu kama awali. Nilihitaji mtu wa kunipa mwanga, mtu wa kunisaidia kutupatanisha ambaye ni Jane angeweza, lakini sikutaka kabisa kumhusisha. Niliona bora nitafute njia zingine.

Nilipofika nyumbani sikuona mtu yeyote. Nilimpigia simu mama J, akaniambia wako Mlimani City wameenda matembezini. Nikaamua kuoga ili kupunguza msongo wa mawazo uliokuwa unanizidi. Lakini nilipotoka bafuni, nilikuta missed call mbili kutoka kwa dada yangu. Roho ilinirudia, nilifurahi sana kuona amenitafuta.

Bila kuchelewa nikampigia na yeye alipokea simu haraka, na mazungumzo yakaanza. Kwanza maongezi yalianza ambapo tulimaliza tofauti zetu pale ambapo Dada alinieleza kwa upole kwamba mimi ni mtu mzima, hivyo natakiwa kufanya maamuzi bila kushinikizwa na mtu.

Niliamua kumueleza ukweli kuhusu azma yangu ya kumwambia mzee kile kinachoendelea, lakini sikuweza kufanya hivyo maana moyo wangu ulinizuia. Dada yangu alinisikiliza, kisha akasisitiza kwa mara nyingine kwamba nisubiri angalau miezi sita ipite kabla ya kuwaambia wazazi. Alisema ipo siku nitayakumbuka maneno yake na nitaona busara yake.

Kisha mada ikahamia kwenye jambo lililokuwa linanisumbua kwa muda, kuhusu safari yangu ya kwenda Ethiopia na Iryn. Ilikuwa lazima niende kuzuru kaburi la mama yake, na pia ilikuwa sehemu ya kutambulishwa rasmi upande wa kwao. Lakini moyoni mwangu swali moja lilibakia kuniumiza, hivi Inawezekanaje kwenda kutambulishwa ukweni kabla ya kutambulisha kwetu? Haikuleta mantiki.

Dada yangu akasema wazi kuwa si sahihi kuanza kumpeleka Aria kwao kabla ya kumtambulisha kwetu sisi. Alisema hilo ni jambo la msingi, na kwamba anataka alishughulikie mwenyewe ili kuhakikisha linaenda kwa mpangilio sahihi. Mazungumzo yakawa marefu sana, yenye uzito na yenye kugusa familia nzima.

Kabisa mwisho, dada akanitahadharisha kuhusu mama J. Alisema tangu walipokutana Arusha, mama J alikuwa akimdokezea maswali ambayo yalionyesha anahisi mimi na Iryn tuna uhusiano wa siri. Dada aliniambia niwe makini sana kipindi hiki, na akasisitiza kwamba mpango wangu wa kuacha kazi kwa Iryn ni wa busara, na niumalize haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajachukua sura nyingine.

Tuliongea sana kuhusu masuala ya familia, maisha, na mambo ambayo nilikuwa nimeyabeba moyoni siku nyingi. Baada ya kuagana, nilihisi pumzi imenirudia kidogo, ni kama furaha yangu ilikuwa imerudi moyoni.

****
Jumapili saa tano asubuhi tulikutana na Jane tayari kwa safari ya kuelekea Kariakoo kuangalia fremu na kufanya malipo. Jane hakuwa peke yake bali alikuwa ameongozana na Vicky, na walinipitia barabarani kunichukua kabla hatujaendelea na safari.

Tulipofika Kariakoo, tulikutana na dalali aliyekuwa anatusubiri. Tukaanza kukagua fremu moja baada ya nyingine, na ile tuliyokuwa tumelenga kutoka muda mrefu ilimvutia sana Jane. Baada ya hapo tukatafuta fundi, tukaeleza mpango mzima wa marekebisho na decoration, naye akatupa gharama. Jane alisikiliza kila kitu kwa makini, akauliza maswali ya msingi, kisha akasema yupo satisfied.

Mara moja tukafanya malipo ya fremu kwa mwaka mzima, tukasaini mikataba, na tukamaliza rasmi hatua ya kwanza ya biashara. Tulikaa Kariakoo hadi majira ya saa kumi jioni, tukiendelea kupanga mipango midogomidogo na kupangilia hatua zitakazofuata.

Wakati tunaondoka, tukaamua kupitia Golden Fork pale Mikocheni ili kupata chakula. Tulipokuwa pale, simu yangu iliendelea kuita mara kwa mara, ni Ghati alikuwa anapiga, na sikupokea hata moja. Baadaye akanitumia ujumbe mrefu, ambao ulikuwa umejaa hisia na msisitizo kwamba tunapaswa kumaliza tofauti zetu na akaomba niende kwake moja kwa moja.

Mimi sikuwa tayari kwenda kwake, mawazo yangu hayakuwa kwenye kukutana kwake nyumbani. Nikamjibu kwamba tungeweza kukutana sehemu nyingine. Baada ya majadiliano ya haraka, tukakubaliana tukutane saa kumi na mbili jioni Ununio Beach.

Baada ya kumaliza kula, tukakaa pale kwa muda tukipumzika, kisha tukaondoka. Jane alinidropi Ununio, karibu na shule, na kwa upande wao walitamani sana kujua ni mishe gani nilikuwa nayo Ununio kwa wakati ule? Na niliishia kuwadanganya kwamba nina rafiki yangu naenda kukutana naye.

Nilitembea taratibu hadi Ununio Beach, hewa ya bahari ikiwa baridi na upepo ukipiga taratibu uso wangu. Ghati alinijulisha kwa ujumbe kuwa yuko Dynasty Beach, amekaa akinisubiri. Nilipofika karibu na eneo alilotaja, nilimwona amekaa kwenye kona akitazama bahari ya Hindi. Upepo ulipeperusha nywele zake kwa taratibu, na miwani yake meusi iliongeza mguso wa mvuto wake.

Alikuwa amevalia pant ya kijeshi aina ya American cargo, iliyo kaa vizuri kiunoni, na juu akavaa pluneki nyeupe iliyombana kiasi cha kuonyesha vizuri umbo la kifua chake. Alionekana kuvutia sana kwa mbali na kadri nilivyozidi kumsogelea, ndivyo sura yake ilivyozidi kujichora vizuri mbele ya macho yangu.

Nilimsalimia, nikaketi upande wa pili wa meza, tukitizamana. Mhudumu alikuja, nikafanya order ya maji ya kunywa pamoja na Red Bull.

Tulianza kutizamana pale bila kusemeshana kwa muda, nikaamua kuvunja ukimya;

MIMI: “Nambie mama, mambo ya tangu jana?”

GHATI: “Mbaya tu, jana uliondoka kwa hasira, sikupenda. Halafu simu hukupokea kabisa.”

MIMI: “Mimi nilijua utaomba msamaha kwa ulichokifanya, kumbe bado unataka kuendelea kubishana?”

GHATI: “Hapana, jana nilikuwa naongea na mtu aliyenitafutia dada wa kazi. Dada alitakiwa afike jana lakini ikashindikana, na nauli nilimtumia kumbe ameila. Nilikasirika sana.”

MIMI: “Pole sana, ila jana ulichonifanyia kwangu kilionekana dharau, ndo maana nikaondoka. Tuachane na hayo nimetii wito wako na nimekuja kukusikiliza, kuna jambo gani?”

GHATI: “Yale maneno uliyoniambia kuhusu hali yetu mimi na wewe sikuyapenda. Ulinivunjia heshima sana.”

MIMI: “Na kati ya yale maneno yangu, kuna neno lolote la uongo nililosema?”

GHATI: “Sio kwamba ni uongo, lakini maneno uliyosema nimeyachukulia tofauti. Uliongea kama vile… kama vile unaniona mimi ni malaya. Lakini na-appreciate uliniambia ukweli kuhusu mahusiano yako kabla hatujaenda mbali. Mimi nilikubali uhalisia huo kwa sababu kupata mwanaume wa kweli siku hizi ni ngumu.”

MIMI: “Wanaume wa kweli wapo, labda kama unakuwa too selective. Sasa twende kwenye point… dhumuni la kuniita hapa ni nini?”

GHATI: “Dhumuni ni kujadili mustakabali wa mahusiano yetu. Kama ulivyosema, tumekuwa na intimacy bila kukaa chini na kujadili hili suala.”

MIMI: “Sawa! kwanza, nikuulize. Umeridhia kuwa na mahusiano na mimi nikiwa kwenye hali niliyo nayo sasa?”

GHATI: “Nimeridhia, sina tatizo.”

MIMI: “Kama umeridhia, basi nataka nikupe misingi yangu ya kufuata. Moja, mimi nina wivu sana sitaki kukuona ukiwa karibu na mwanaume mwingine zaidi yangu. Pili, nahitaji uje unizalie mtoto. Si leo, lakini nataka ujue mapema kwamba ipo siku nitaomba mtoto kutoka kwako.”

GHATI: “La kwanza sina shida nalo, la pili, mtoto nitakuzalia but sio kwa sasa.”

MIMI: “Sijasema kwa sasa, ila weka hilo kwenye akili yako.”

GHATI: “Nimekuelewa.”

Tuliongea kwa muda mrefu, tukapitia kila kona kuhusu mustakabali wa mahusiano yetu. Tulitumia muda mrefu sana pamoja na hatimaye nikaamua kumwambia kuwa muda wa kuondoka umefika, maana nilitaka kuwahi nyumbani. Pamoja na kwamba Ghati alionesha kunihitaji sana kihisia, kimoyo, na hata kimwili, na aliomba sana tuende kulala wote, bado nilisimama kwenye msimamo wangu. Nikamwambia lazima nirudi nyumbani, na kwamba tutatafuta siku nyingine ya kuwa pamoja.

Tuliondoka pamoja yeye akienda kwenye gari yake nami nikachukua bodaboda wa kunirudisha home. Baada ya kufika home na kuingia sebuleni, nilimkuta wife akiwa na wageni wawili. Alinitambulisha kuwa ni rafiki zake wa chuo waliokuja kumsalimia. Baada ya salamu za haraka, sikuona sababu ya kukaa pale muda mrefu, nikajifanya nina uchovu mwingi na moja kwa moja nikaelekea chumbani kupumzika.

Nilipowasha simu na kuingia WhatsApp, nikakutana na ujumbe wa Iryn uliotumwa takribani dakika 40 zilizopita. Alikuwa ananiambia kuwa hali ya baba yake imeendelea kuwa mbaya zaidi na kwamba kesho ata hamia rasmi kwa baba yake kwa muda ili awe karibu kumuangalia na kumuuguza.

Ujumbe ule ulinibana moyo ghafla, nikahisi huzuni na wasiwasi kwa wakati mmoja. Bila kupoteza muda, nikaamua kumpigia simu ili niweze kujua kinachoendelea kwa undani.

Nilipiga video call na lipita sekunde kadhaa bila majibu, kisha akapokea. Mara tu skrini ilipofunguka nilishtuka kumuona akiwa uchi, vifua wazi, akicheka kama mtu aliyekusudia kunifanyia vile.

IRYN: “Baby… surprise!”

MIMI: “Wewe ndo nini hivi sasa? Kama ningekuwa na mama J au sehemu yenye watu ingekuwaje?”

IRYN: “Ndomana nilianza kwa kuficha camera ili kwanza nione mazingira uliyopo.”

MIMI: “Unanipa mizuka tu na unajua fika hali yako ilivyo.”

IRYN: “Good news…doctor amesema nimepona vizuri. But next month atatoa recommendation if we can start sex or not.”

Alisema hivyo huku akitabasamu, macho yakicheza kwenye kamera kana kwamba anataka kunijaribu.

Baada ya kumaliza utani wetu wa mwanzo, tulirudi kwenye mada ya msingi kuhusu afya ya baba yake. Iryn aliniambia hali ya mzee haikuwa nzuri kabisa, ndiyo maana ameamua kwenda kukaa naye kwa muda ili awe karibu, amuangalie na kufuatilia maendeleo ya matibabu yake kwa umakini.

Tulipokuwa katikati ya maongezi, nikasikia wife akija kuelekea chumbani. Nikamwambia Iryn haraka:

MIMI: “Mama J anakuja chumbani, usikate simu.”

Nikaweka simu chini ya mto, nikajifanya nimelala. Wife aliingia, akafungua droo ya kabati, akachukua funguo za gari, bila kusema chochote, kisha akaondoka. Mara tu niliposikia hatua zake zikififia, nikamtoa Iryn chini ya mto.

MIMI: “Baby, tuendelee…”

Lakini cha kushangaza, Iryn hakurudi kwenye mada ya afya ya baba yake. Badala yake akabadilisha kabisa mwelekeo wa maongezi:

IRYN: “Baba Aria, hivi una mpango gani na mimi?”

MIMI: “Motive ya hili swali ni nini?”

IRYN: “Nataka tu kujua. It’s better ukajibu.”

MIMI: “Wewe si mke wangu jamani?”

IRYN: “Na Mama J je?”

MIMI: “Wote nyie ni wake zangu.”

Akasimama kimya sekunde mbili, kisha akaja na swali lililolenga penyewe:

IRYN: “Kama ni hivyo, sasa mbona hujanitambulisha kwenu?”

Nilivuta pumzi ndefu ukizingatia suala hili ndilo lililokuwa likiniuma kichwani muda mrefu.

MIMI: “Nitakutambulisha mama… better late than never.”

IRYN: “Law No.21-Play a sucker to catch a sucker.”

Nikacheka kidogo, nikamjibu naye:

MIMI: “Law No.35- Master the art of timing.”

IRYN: “Lol! Insider ahadi zako zote ziko hewani, ni muda utafika na nitakukumbusha.”

MIMI: “I know what I’m doing. Why teaching me what to do?”

IRYN: “December sio mbali… na najua utakuwa hujatimiza. I’ll be there no matter what.”

MIMI: “Why talking like you already have answers?”

IRYN: “You’re so annoying.”

Akasema hivyo kwa hasira kisha papo hapo akakata simu. Nilibaki nikitazama screen ikififia mwanga taratibu, nikijua wazi kuwa mazungumzo yale hayajamalizika bali yameahirishwa.

****

Jumatatu nilikuwa na ratiba ya kukutana na Asmah Oysterbay kwa ajili ya makabidhiano ya ofisi, kazi ambayo nilikuwa nafanya kwa niaba ya Iryn mwenyewe. Tulikutana saa nne asubuhi. Baada ya kukabidhi ofisi, nilimwacha ndani akiwaaga wafanyakazi, nami nikaenda kumsubiri kwenye gari.

Dakika 10 baadaye, Asmah alitoka na akaingia ndani ya gari. Tukaendelea na mazungumzo, makubwa yakiwa juu ya safari yake, alisema anatarajia kuondoka Jumamosi. Niliondoa gari maeneo yale na kwenda kupark uwanja wa Farasi, mbali kidogo na ofisi, ili tuendelee kuongea kwa utulivu zaidi.

Nilimwomba anipe “blessing” ya mwisho kabla hajaondoka, lakini alikataa kabisa. Alisema amejiahidi hatalala tena na mimi, hataki kutenda dhambi, na hataki kurudia historia. Nilimbembeleza sana, nikamkumbusha tulikotoka, nikamwambia itakuwa mara ya mwisho-halafu tufunge ukurasa. Bado aligoma na mwishowe nikamuomba basi tukutane Alhamisi kwa dinner ya mwisho kabla ya safari yake, hilo akalikubali.

Asma awali alitaka kwenda nyumbani, lakini kutokana na muda tuliokaa pamoja, akaghairi. Tukaondoka wote kwenda ofisini.

Tulipofika, niligundua kuwa Lucy hayupo. Mimi na Asmah tuliendelea kupiga stori mpaka Lucy alipowasili, akasema ametoka kwa wateja. Kwa upande wa Asmah alikuwa akimuangalia Lucy kwa macho makali, niliona amebadilika ghafla hakuwa tena mchangamfu, hata salamu zao zilipita juu juu.

Lucy hakukaa sana ofisini, akaaga na kuondoka, ndipo nikamuuliza Asmah kuhusu tabia ile aliyokuwa akiionesha,

MIMI: “Asmah, kuna shida gani? Mbona unamtizama Lucy kwa macho makali sana. Bado unaamini kuwa yeye ndio informer wa Iryn?”

ASMAH: “Insider, Lucy ndiye mtu wa karibu zaidi na Iryn. Ndiye aliajiriwa na Iryn, na ndiye informer namba moja. Be careful.”

Sikutaka kuamini maneno ya Asmah nilihisi labda kuna tofauti zao binafsi. Lakini bado, ndani yangu niliona kuna haja ya kufanya uchunguzi wangu wa siri, kwa sababu kama walivyosema, adui huwa hatoki mbali.

Hata hivyo, muda wa lunch ulikuwa umefika, hivyo tukaondoka kwenda kula. Nilikuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza kuhusu shutuma zake juu ya Lucy, na nilipanga kumhoji mara baada ya kufika restaurant. Tulipowasili, tulikaa sehemu tulivu na kuagiza chakula, ndipo mazungumzo yetu yakaanza upya.

MIMI: “Asmah, kwa nini unamuwazia mabaya Lucy? Kuna wakati mlipata kutofautiana?”

ASMAH: “Mimi sina shida yoyote na Lucy. Lakini nachokuambia ni ukweli mtupu ni vile tu hutaki kunielewa kwa sababu ya ukaribu wenu. Lucy ndiye mtu wa karibu zaidi na Iryn, na ndiye aliajiriwa na Iryn. Sasa unataka kuniambia hawezi kuwa informer wa Iryn? Yaani awe upande wako na si wa Iryn? Be serious.”

MIMI: “Unajua kwamba Lucy ndiye mtu aliyenishawishi sana nianzishe mahusiano na Iryn?”

ASMAH: “Hiyo siyo sababu. Na kwa sasa Lucy anafaidika sana kupitia mahusiano yako na Iryn kama ulikuwa hujui.”

Kauli yake ilinipa kumbukumbu kipindi Lucy ananisukuma sana nianze mahusiano na Iryn, alishawahi kuniambia waziwazi kuwa kama nitakuwa kwenye mahusiano na Iryn, bhasi hata yeye ataweza kutoboa. Sikuielewa sana ile kauli wakati ule.

Nikiwa bado nikiwa nimezama kwenye mawazo yangu nikikumbuka maneno ya Asmah, yeye aliendelea kuzungumza kwa sauti ya uhakika:

ASMAH: “Halafu mimi najua kitu kimoja, Iryn alikupenda wewe kama Insider, na inawezekana kabisa Lucy alitumika kama daraja tu la kufikia malengo yake. Hivi, Insider, unamchukuliaje Iryn? Mwanamke mzuri kama yule akazaa mtoto na wewe ghafla tu? Bila hata kusukumwa na potential aliyoiona ndani yako?”

MIMI: “Unamaanisha nini sasa?”

ASMAH: “Iryn alishakuona wewe ni mtu muhimu sana kwenye maisha yake na hata kwenye biashara zake. Njia pekee aliyohisi itamfunga karibu na wewe, ilikuwa ni kukupa mtoto. Na hapo, Insider, alishavuna alichokitaka.”

Maneno yake yalikuwa makali, lakini cha ajabu ni kwamba sikuwa mgeni nayo. Nilikuwa nikiyafikiria moyoni mwa muda mrefu. Hata hivyo, ilibidi nijifanye kama yote haya ni mapya ili kujua zaidi yale ambayo Asmah alikuwa bado hajaniambia kuhusu Iryn.

MIMI: “Sawa, hebu niambie, wewe unajua mambo gani ya Iryn ambayo mimi sijui?”.

Asmah alinisogelea kidogo na kusema kwa sauti ya chini kama anayetoa siri nzito:

ASMAH: “Nitakwambia, lakini tafadhali iwe siri yako. Nakuamini sana, Insider. Unajua mbali na mambo mengine, Iryn ana biashara zake za massage. Pia ana bwana wake Mfaransa, but sijui kama bado wako pamoja. Hayo alishawahi kukwambia?”.

Nilikuwa najua kila neno alilolitamka, lakini nililazimika kuendelea kucheza mchezo wangu.

MIMI: “Hapana, sijui kitu. Hebu niambie vizuri, wewe ulijuaje?”.

Asmah akaanza kuelezea kwa utulivu pale. Alisema kuwa yeye na marehemu mama yake Iryn walikuwa marafiki wa karibu sana. Mara nyingi alikuwa akienda nyumbani kwao kumtembelea mama yake, na Iryn alikuwa mtu wa kuja kumsalimia mama yake na kuondoka, hapo ndipo walipofahamiana.

Siku moja, alipokwenda kumwona mama yake, alimkuta Iryn na wakaingia kwenye mazungumzo. Katika mazungumzo hayo, Iryn akamueleza kuhusu biashara yake ya massage-biashara ambayo, kwa mujibu wake, ilikuwa inamuingizia pesa nyingi sana. Alimshawishi hata Asmah aingie kwenye hiyo biashara, akimwambia ni rahisi, inalipa, na angemtafutia wateja.

Asmah alimwuliza Iryn kama mama yake alikuwa anajua kuhusu hiyo biashara ya massage. Iryn akamjibu kwa msisitizo kwamba mama yake hajui, na hata akijua hatakubali kabisa kwa sababu zake mwenyewe.

Asmah aliendelea kuniambia kuwa hata yeye aliwahi kuvutiwa na hiyo biashara baada ya kusikiliza maelezo ya Iryn. Alisema mara ya kwanza aliichukulia kama biashara za wanawake kujiuza ili kujipatia kipato, lakini baada ya kumsikiliza Iryn kwa makini, akagundua kuwa ni biashara kama nyingine tu ni mtazamo tu wa Waafrika kutazama mambo tofauti na wenzetu.

Kisha akagusa suala la Griezmann, mwanaume ambaye Iryn alimpenda sana. Asmah alisema alifahamu kuhusu Griezmann kupitia Iryn mwenyewe, kwani aliwahi kumtambulisha kwake. Hata hivyo, Asmah alisema kwa sasa hajui kama bado wako pamoja au kama Iryn bado anaendelea na zile biashara zake za massage.

Baada ya hapo, Asmah alinieleza mambo mengi kuhusu marehemu mama yake Iryn. Alisema mama yake alikuwa mtu mzuri kupindukia, mwenye roho safi na upendo mwingi. Alimpenda Iryn kupita kiasi na, cha kushangaza zaidi, bado alikuwa na pesa nyingi sana. Asmah alisisitiza kuwa ingawa yeye anajua machache tu, kama ningependa kuijua dunia ya Iryn kwa undani zaidi, basi ningekuwa karibu na Mama Janeth, au nimbane vizuri Sumaiya, ambaye naye anajua mambo mengi sana kumhusu Iryn.

Tulichukua muda mrefu sana pale restaurant tukiongea, hadi tukachelewa kurudi ofisini. Tuliporudi, Asmah alionekana kuchoka sana na mara moja akalala kwenye sofa, wakati mimi nikaendelea na majukumu yangu ya kiofisini.

Tulikaa na Asmah pale ofisini tukipiga story za hapa na pale hadi usiku ulipoingia. Hatimaye, Asmah aliaga na aka-request Uber ya kumrudisha nyumbani. Baada ya yeye kuondoka, nami pia niliamua kuondoka kurudi kwangu.

Safari ya kurudi nyumbani ilikuwa kimya, lakini kichwa changu kilikuwa na kelele nyingi. Maneno ya Asmah yalikuwa yakijirudia, nilifikiria sana, na nikahisi huenda Asmah alikuwa na pointi kubwa kuhusu Lucy that maybe, kweli, hakuwa mtu wa kumuamini kupita kiasi. Uwezekano wa yeye kuwa snitch haukuondoka kichwani mwangu kabisa.

Nilipofika nyumbani, nilijikuta nikiingia kwenye ugomvi na wife. Ugomvi ambao sikutarajia hata kidogo. Alianza kusisitiza kwamba tunapaswa kufunga ndoa kabla mwaka haujaisha na msisitizo wake ulikuwa wa ajabu, wa ghafla. Nilishindwa kuelewa pressure hii imetoka wapi, hasa ukizingatia kuwa tulishajadili suala hili na kufikia makubaliano tayari.

Mama J alizidisha moto zaidi, alisema hataki ndoa yenye shamrashamra nyingi wala za gharama. Kwa mujibu wake, cha msingi ni pete tu kidoleni, mengine yote hayana umuhimu. Lakini mimi niliendelea kusimama kwenye msimamo wa makubaliano yetu ya awali, na ndipo ugomvi ulipotikisa nyumba nzima.

Kesho yake nilichelewa kuamka, sikuwa na mood ya kwenda kazini na badala yake cha kwanza nilichofanya ni kumpigia simu Ghati. Nilimueleza kuwa najisikia kutulia, na kuwa naye pamoja siku ya leo. Yeye akaniambia yuko ofisini, lakini ataomba ruhusa ya kurudi home kwaajili yangu, hivyo ningeweza kwenda nyumbani kwake nikapumzike na kufikia saa tano atakuwa karudi, alisisitiza.

Sikupenda yale makelele ya wife maana alimka na kuendeleza mada ya jana kuhusu ndoa. Niliondoka kuelekea Mbweni, na break yangu ilikuwa nyumbani kwa Jane. Vicky alikuwa pale nyumbani na akanipa taarifa kwamba Jane ametoka kwenda dukani, kwahiyo inaonekana tulipishana kidogo tu.

Nikaingia ndani na kukaa sebleni tukipiga story na Vicky. Nilianza kwa kumuuliza kuhusu hali ya mahusiano yake kwa ujumla, maana kwa muda wote tuliokuwa tunajuana hakuwahi kufunguka kuhusu upande huo wa maisha yake. Niliona hanitaki kuingia humo, hivyo nikaachana nalo na kuendeleza story nyingine za kawaida.

Vicky alianza kunipa habari za Mary, zile ambazo hakuwahi kuniambia siku ile tulipoachana ghafla mezani. Aliniambia kwamba baada ya mimi kuondoka, alisikiliza kwa makini mazungumzo ya Mary na dada yake, Jane. Katika mazungumzo hayo, Mary alimwambia Jane moja kwa moja kwamba mimi na yeye tumeachana.

Kitu kilichonistua zaidi ni sababu aliyoitoa. Kwa mujibu wa Mary, tuliachana kwa sababu amegundua nina wanawake wengi na sijatulia.

Maneno hayo yalinigusa vibaya sana yalinikuna kwenye sehemu ambayo sikutegemea. Niliingiwa na hofu kubwa, maana mara moja tu mawazo yangu yakakimbilia kwa Jane. Nikawaza pale Kama Mary kaweza kumwambia Jane hivyo, je, inawezekana pia kamwambia kuhusu mahusiano yangu na Iryn?. Nilijisemea kama Mary atakuwa alithubutu kusema hili, bhasi nami nitamwambia Prisca ukweli kuhusu mahusiano yetu ya siri na dada yake.

Wakati huu niliona sina tena sababu ya kuendelea kumficha Vicky ukweli kuhusu mimi na Mary. Nilijikuta nikimwambia moja kwa moja kwamba Mary ana wivu usio na sababu, na kwamba sina mahusiano na mwanamke yeyote zaidi yake na mama J tu. Nikazidisha kumhakikishia kwa kumwambia kwamba kama kweli mimi ni mtu wa aina ile ambayo Mary anasema, basi hata yeye (Vicky) ningekuwa nimesha-mtongoza muda mrefu maana mazingira yalishawahi kutokea, lakini sikufanya chochote.

Baada ya maneno hayo, Vicky alitabasamu tu, alionekana kama mtu aliyeanza kuyaamini maneno yangu. Akaamua kupotezea mada nzima mara moja akanigeukia kwa swali la kawaida:

“Halafu siku moja tutoke out tangu nianze likizo hadi inaisha sijawahi kutoka.”

Nikamuondolea wasiwasi na nikamwambia hakuna tatizo kabisa, tutapanga tu.

Saa 6 mchana Ghati alinipigia simu akaniambia yuko Boko na kuniuliza ningetamani kula nini mchana. Nilimwambia ningependa kula wali na samaki, naye akajibu: “Sawa, baby, I will cook for you.”

Dakika ishirini tu baada ya hapo, alinitumia ujumbe akiniarifu kuwa amefika tayari nyumbani. Sikutaka kupoteza muda, hivyo nikamuaga Vicky pale na kuondoka. Tuliongozana nje, Vicky akanifungulia geti na kuniomba sana nimfundishe kuendesha gari. Nilimwambia kipindi hiki cha likizo aanze na shule ya udereva, kisha nitamsaidia baadae. Alikubali na nilimuomba asijaribu kumwambia Jane kwamba mimi nilienda pale nyumbani.

Nilitumia muda mfupi sana kufika kwenye apartment ya Ghati. Nilikuwa tayari ni mwenyeji, hivyo nilifungua geti na kuingiza gari ndani. Nilimkuta jikoni akipika chakula, na baada ya kuniona aliishia kutabasamu na kunikaribisha kwa furaha, nami nikaishia kuslap kalio lake ‘Paah’.

Nilianza kumsaidia kupika huku tukipiga story mbalimbali. Katika wakati huo, kulikuwa na ugeni wa dada mpya ambaye alinitambulisha kama dada wa kazi. Ofcourse aliniona siko sawa na alitamani sana kujua ni nini kinanisumbua, lakini niliishia kumdanganya kwa kumwambia ni mambo ya ofisi. Ukweli suala langu na mama J, lilikuwa ni heavy sana na lilinipa mawazo.

Baada ya chakula cha mchana, tulihamia kwenye shughuli nyingine ya mapenzi na mahaba motomoto, ambayo yalikuwa yasiyo na kikomo hadi jioni. Kwa mahaba niliyopewa nilijikuta nikisahau shida zote za dunia hii, hata stress za wife zikawa zimenipotea. Saa 12 jioni tuliondoka kwenda supermarket kununua mahitaji ya nyumbani, na nilimwambia anunue kila kitu kilichohitajika.

Baada ya shopping, tulipita filling station na nikamjazia gari mafuta full tank, kisha tukarudi nyumbani kuandaa chakula cha usiku. Njiani, nilimwambia nikifika nyumbani nitaondoka, lakini yeye alitaka nile chakula cha usiku kwanza, hapo ndio ataweza kuniruhusu niondoke.

Muda wa saa 3 usiku, baada ya kula, niliaga na kuondoka kurudi nyumbani. Nilipofika, sikutaka kupiga story pale sebleni, hivyo nikajikuta nikingia chumbani na kumkuta wife akipanga nguo kabatini.

WIFE: “Kwanini hupokei simu zangu?”

MIMI: “Nilikuwa nina drive ndomana.”

WIFE: “Ulikuwa wapi? Hii sio harufu yako kabisa… kuna mwanamke ulikuwa naye.”

Nilikubali kimoyoni kuwa nilinukia harufu ya perfume ya Ghati, na nikahisi huenda alipuulizia T-shirt yangu.

MIMI: “Yaani wewe mwanamke hupendagi amani, nilijipulizia perfume ya mtu ofisini. Sitaki kelele sasa, niache ninalale nimechoka sana.”

WIFE: “Ukitoka kwa mwanamke mwingine mimi nitajua tu.”

MIMI: “Sawa, nimetoka kwa mwanamke mwingine, is that what you would like to hear?”

WIFE: “Kwahiyo unakubali ulikuwa na mwanamke mwingine?”

MIMI: “Mama J, embu niache akili yangu imevurugwa sasa.”

Wife aliishia kunisonya pale, mimi sikujali sana, nikapanda kitandani na kulala. Baada ya kuondoka, nilimtumia Ghati ujumbe kumkanya na kumsisitiza asijaribu tena kupulizia perfume nguo zangu.

Dakika chache baadaye, Ghati alinipigia simu akiniomba msamaha, akasema alifanya kwa nia njema. Nilimwambia kufanya hivyo ni hatari, kwani ni kuniletea matatizo na mama wa mtoto wangu. Ghati aliendelea kuomba msamaha na kuahidi kwamba hatorudia tena kitendo hicho, hatimaye tukaagana.
******

Siku ya alhamisi asubuhi, kabla sijaondoka kwenda kazini, nilikuwa na maongezi na wife wangu. Nilimkumbusha aanze maandalizi ya safari yetu ya kwenda Dodoma, kama tulivyokuwa tumepanga awali.

Baada ya kuingia kwenye gari nikakuta ujumbe wa Prisca kwenye simu nyingine akinisalimia. Nikaamua kumpigia ili kujua kama yuko dukani kama kawaida. Aliponijibu kuwa yupo dukani, nilimwambia napita soon kumsalimia.

Safari ikaanza pale na nilipitia Bagamoyo Road kuelekea Mwenge, nikakata kona hadi Mlimani City kisha kushoto kuelekea Makaburini Road. Lengo langu la kumfuata Prisca halikuwa tu salamu, nilitaka pia kumchunguza kidogo kuhusu Mary.

Nilipokaribia, nilimpigia tena anielekeze lilipo duka lake. Akanipa maelekezo hadi nikafika na kupark gari karibu na lango la kuingia dukani.
Prisca baada ya kuniona nikiingia dukani kwake alikuja kwa upesi kwa furaha na kunikumbatia kwa nguvu. Hakukuwa peke yake, bali alikuwa ameambatana na mdogo wake Ivy, ambaye naye alikimbia kunikumbatia kwa bashasha ile ile. Pembeni yao alikuwepo rafiki yake kipenzi, Eva.

Nilijisikia vizuri sana hasa ile warm welcome kutoka kwa Prisca na mdogo wake ilinigusa. Ivy alikuwa na furaha isiyo kifani kuniona wakati ule. Nilikaa pembeni ya Emmy tukasalimiana, kisha nikaanza kuzungumza na Ivy.

Lakini Ivy, kama kawaida yake, alianza na maswali magumu ambayo sikuwa tayari kuyajibu pale papo hapo.

IVY: “Uncle Insider, mbona siku hizi huji nyumbani kumsalimia dada Prisca kama zamani?”

Nilimtazama Prisca aliyekuwa amesimama mbele yetu, akitabasamu tu bila kusema lolote.

PRISCA: “Insider, karibu.”

MIMI: “Ahsante. Ivy nitakuja, eeh! Nilikuwa nimesafiri. Leo hujaenda shule?”

Prisca akaingilia mazungumzo akijibu kwa niaba yake.

PRISCA: “Yuko likizo, ndiyo maana nakuja naye dukani. Tangu Jumatatu nashinda naye hapa ananisaidia kuuza.”

Nilimuangalia Ivy na kutabasamu tu, kutokana na ucheshi wake. Prisca na mdogo wake huyu wanapendana sana hili niliwahi kulisema tangu Season 1. Zaidi ya hapo, mama yao anawapenda kupita kiasi, hawa watatu, Prisca, Ivy na mama yao, wana upendo wa ajabu. Lakini upande wa pili, kuna Mary, mdogo wao wa tatu Loraine (anayemfuata Prisca) na baba yao hawa nao wako karibu sana, kama vile familia imegawanyika katika makundi mawili ya upendo.

Mazungumzo yaliendelea kwa bashasha na muda ukaenda bila kujua. Baada ya kama nusu saa, nilimuaga Prisca kuwa naondoka kuelekea ofisini. Ivy alikataa kabisa niondoke bila yeye, aling’ang’ania twende wote na nimrudishe baadaye. Prisca hakuwa na pingamizi, akakubali nimchukue tu.

Tulipofika ofisini, nilimkabidhi Ivy kwa Winny. Nikamwomba Winny amsuke Ivy nywele kwa mtindo mzuri na wa kuvutia. Niliwaachia maagizo yote, kisha nikaondoka kwenda kukutana na kaka Allen ofisini kwake kwa mazungumzo ya kampuni.

Tulikaa na Allen hadi saa 10 jioni tukipanga mipango mbalimbali na maongezi mengine ya hapa na pale. Niliporudi ofisini kumchukua Ivy, nilimkuta amebadilika kabisa na alikuwa kapendeza kupindukia. Winny alikuwa amefanya kazi ya mikono ya dhahabu, kwani Ivy alionekana mrembo zaidi.

“Waoh! umependeza Ivy you are so beautiful,” nilimwambia.

Akatabasamu, akajibu kwa adabu,

“Thank you, Uncle Insider. May God bless you.”

“Thank you, Ivy. Let’s go,” nikamwambia.

Kabla hatujaondoka, nilimgeukia Winny kuulizia gharama. Akanijibu kuwa jumla ni TZS 100,000/=. Nikamlipa, nikamshukuru kwa kazi nzuri aliyomfanyia Ivy, kisha mimi na Ivy tukatoka kuelekea Sinza, lakini tukaanza kupitia Mikocheni kufanya shopping ya nguo.

Baada ya kununua nguo chache nzuri za kumfanya Ivy aang’ae zaidi, tulielekea moja kwa moja Sinza kwa Prisca.

Prisca alipomwona Ivy, alibaki akimtazama bila kupepesa macho. Kwa upande wake alishangaa kuona mdogo wake amependeza kiasi kile, halafu akaniangalia mimi kwa tabasamu la shukrani lisilohitaji maneno.

Kabla hata Prisca hajatoa neno, nilimwambia anitolee vipodozi nilivyomnunulia wife na nikamwambia tuongozane hadi kwenye gari ili nimpe pesa yake. Tulipoingia ndani ya gari, mazungumzo yakaanza papo hapo.

PRISCA: “Insider, leo umemsurprise Ivy, kafurahi mwenyewe mpaka basi.”

MIMI: “Sijawahi kumfanyia surprise ya aina hii. Leo ilikuwa bahati yake tu.”

Prisca akavuta pumzi kwa upole, akaniangalia kwa macho yale ya kumaanisha.

PRISCA: “Nikikuonaga hivi huwa nakuwa na amani sana. I miss you, Insider.”

Nilibaki kimya kwa sekunde chache, kisha nikabadili mwelekeo wa mazungumzo.

MIMI: “Mary anaendeleaje? Ni muda mrefu sijamuona.”

PRISCA: “Dada Mary yuko busy na shule. Jana alikuwa hapa dukani.”

MIMI: “Msalimie sana. Mwambie Insider anampa hi.”

PRISCA: “Usijali, zitafika, na home utakuja lini kumsalimia mama? Anakuulizia sana.”

MIMI: “Nitakuja, usijali.”

Nilimshika mkono taratibu, na kuchezea vidole vyake kwa utulivu. Alitabasamu bila kusema neno, na baada ya muda mfupi, tuliagana.

Wakati ninaondoka, saa yangu ilikuwa inasoma saa 12 jioni. Nikachukua njia ya kuelekea Masaki kukutana na Asmah, na mwendo wangu ulikuwa wa kasi sikupenda kumchelewesha.

Upande wa pili, Asmah alinijulisha kuwa amechukua Uber na tayari yuko njiani kuelekea eneo tulilokubaliana Barometer Bistro. Ni miongoni mwa maeneo aliyoyapenda sana kutokana na utulivu wake na hadhi ya watu wanaokuja humo.

Asmah alinitangulia kufika eneo la tukio, na nilimwambia asishuke kwenye Uber, anisubiri ili tuingie pamoja. Baada ya dakika kama tano, nami nilifika. Baada ya kuonana nilimshukuru dereva Uber kwa maneno ya ucheshi, kisha nikamshika mkono Asmah, hao tukaingia kwenye lift kuelekea kwenye restaurant.

Asmah alikuwa amependeza sana kweli alijitahidi. Kazi yangu ilikuwa ni moja tu, kumpa sifa njiani kote hadi tunafika restaurant, na yeye alibaki akitabasamu njiani kote. Tulipokelewa vizuri sana na mhudumu, tukapelekwa kwenye angle nzuri ya utulivu. Kila mmoja akaagiza kile kilichomvutia.

Tulianza mazungumzo pale na mada kubwa ilikuwa maisha na masomo yake Qatar. Nilimuuliza kama akimaliza masomo anapanga kurudi Tanzania, akaniambia kuwa hana uhakika. Akipata fursa nzuri kule, hatakuwa na mpango wa kurudi Bongo kirahisi.

Baada ya chakula, tuliagiza wine na hapa mazungumzo yalipamba moto zaidi. Asmah akaanza kunieleza mambo mengi, ikiwemo siri za ofisini kabla sijaingia kazini. Alinisisitiza tena na tena kuwa niwe makini na Lucy, pia nisimweleze mambo yangu muhimu, kwani Lucy ndiye “informer namba moja” wa Iryn.

MIMI: “Hili la Lucy nitalifanyia kazi. Na wewe umeshamuaga Iryn na mama Janeth?”

ASMAH: “Iryn tumewasiliana jana tu, na akanitumia pesa ya safari.”

MIMI: “Kiasi gani kakutumia?”

ASMAH: “$2,000. Iryn ana roho nzuri sana kama mama yake.“

MIMI: “Rebby alinambia Iryn hafikii hata nusu ya roho ya mama yake.”

ASMAH: “Rebby anaongea kutokana na mtizamo wake. Lakini mimi nilikuwa karibu sana na mama yake. Kwa ukweli, Iryn kanifanyia mambo mengi mazuri kwa muda mfupi kuliko hata mama yake-nisiseme uongo. Tulianza tu kupishana pale ulipoingia wewe, na kuanza kuwa na interests kwako.”

MIMI: “Kwa hiyo mimi ndiyo sababu hadi mkawa na cold war?”

Asmah akanitazama, akatikisa kichwa huku akicheka kwa uchungu laini.

ASMAH: “Insider, umebadilisha maisha yangu wewe mwanaume! Kwa kweli wewe ndiye chanzo changu cha mimi kuanza kuishi maisha ya ki-huni. Hata Iryn mwenyewe ananiambia, ‘Asmah umebadilika umekuwa hivi kwa sababu ya Insider.’”

Nilijikuta natabasamu.

MIMI: “Haya ndiyo maisha uliyoandikiwa kuishi, si mengine, lakini vipi si tunaondoka wote?”

Asmah akakataa kimyakimya, akitingisha kichwa polepole.

ASMAH: “Insider, nilishakuambia haiwezekani. Tafadhali.”

MIMI: “Asmah, haiwezekani uondoke bila kuagana. But I promise this will be the last. It won’t happen again. Naomba leo iwe ya mwisho mwisho tufunge ukurasa.”

Alinitazama kwa macho laini ya mahaba. Hatimaye, akakubali kimya kimya.

Sasa tukaanza kujadiliana tutaenda wapi. Nyumbani kwake haingewezekana, alikuwa na dada yake. Nikaamua kufanya booking Peninsula Hotel, Masaki. Tukaelekea huko na pale ndipo Asmah aliniachia moja ya unforgettable memories ile ya mwisho, ya kufunga ukurasa. Mpaka leo ninavoandika, hatujawahi kukutana kimwili tena.
 
Hope mpo salama.

Niliamua kujipa short break kidogo, ili kutoa nafasi kwa watu kuzungumza na kutafakari masuala muhimu ya nchi yetu.

That day was heavy, terrible things happened, poleni sana. Hata kwangu binafsi, nilipoteza mmoja wa watu wa karibu sana moyoni mwangu 💔.

Kwa sasa hali inaanza kurudi back to normal. Kesho, tutaendelea na our story, pale tulipoishia.
Good to see you back buddy. Stay safe Bro.
 
SEASON 03
CHAPTER 14

A TRUE STORY BY INSIDER MAN

CONTINUE:

Ijumaa asubuhi nilikuwa nimelala usingizi mzito hadi wife alinistua kwa kunigusa taratibu, akinihimiza nikaoge ili tuanze maandalizi ya safari. Tulipaswa kufika mapema AirPort kwenye check-in saa 3 asubuhi kabla ya safari yetu ya Dodoma kuanza. Kabla hatujaondoka, tulikaa kikao kifupi kuhusu Junior. Wife alitamani twende naye Dodoma, lakini mimi niliona abaki nyumbani. Kwa mazingira ya Dodoma tuliyotarajia, Junior angekuwa mzigo mkubwa na angepunguza uhuru wetu wa kumaliza kazi zetu kwa utulivu.

Tuliondoka kwenda JNIA na nikiwa njiani nilipigiwa simu na mama Prisca (Mary), ambaye alijitambulisha mara tu nilipopokea. Baada ya utambulisho wake, nilipatwa na butwaa kwa sababu sikuwa nimewahi kufikiria kama kuna siku angenipigia simu. Baada ya kusalimiana na maongezi mafupi, mama alisema dhumuni la kunipigia simu ni kunishukuru kwa kile nilichomfanyia binti yake, Ivy, na hakusita kusema kuwa Ivy alipendeza kuliko kawaida. Furaha yake ilikuwa dhahiri sana, jambo lililonifanya hata mimi nijisikie vizuri.

Mama aliomba sana kuwa siku nikipata nafasi niende kumsalimia nyumbani, akisisitiza kuwa ni muda mrefu umepita bila kuonana. Nilinyamaza kwa sekunde chache, lakini nilimhakikishia kuwa nitafanya hivyo, na nikamwambia kuwa nitawasiliana na Prisca ili tuweze kupanga.

Baada ya simu kukatika, nilibaki nikitafakari pale, nikaanza kuwaza kuhusu binti zake Prisca na Mary. Niliwaza pale nimechezea moyo wa binti yake Prisca, lakini mama anaonekana hana shida na mimi. Niliendelea kuwaza pale, hivi itakuwaje siku akijua nina mahusiano na binti yake Mary?. Mawazo yalinichukua mbali, na bila kujitambua nikajikuta natabasamu mwenyewe, hadi kupelekea wife kuuliza kinachonifurahisha.

Baada ya kuwasili airport na tukisubiri ndege ya kwenda Dodoma, Asmah alinipigia simu kuniaga. Aliniambia kuwa anatarajia kuondoka kwenda Qatar saa saba mchana. Mimi nilimtakia safari njema na nikamkumbushia kumbukumbu nzuri ya usiku uliopita, hasa memory nzuri ya sex aliyonipa. Sikusahau pia kumshukuru tena, na nikampatia ahadi kwamba tutaendelea kuwasiliana.

Tulipowasili Dodoma, tulikwenda kupumzika Chako ni Chako na tukapata chakula cha mchana hapo. Tukiwa mezani, Iryn alinipigia video call lakini sikuipokea badala yake nilimtumia ujumbe nikamjulisha kuwa niko na wife. Haikupita muda akanijibu:

IRYN: “What do you mean?”


MIMI: “Let’s chat baby.”


IRYN: “Asmah ameondoka leo, amekuaga?”

Nilihisi swali lake lina ukakasi, kama mtego fulani.

MIMI: “What do you think? Kwamba aondoke bila kuniaga?”


IRYN: “Can’t be possible.”


MIMI: “Wewe ndiyo sababu ya Asmah kuondoka, ujue.”


IRYN: “Na mimi ndiyo sababu ya wewe kujuana na Asmah.”

Nilibaki kimya kwa muda, sikuwa na la kuongeza.

MIMI: “Niko Dodoma na mama J.”


IRYN: “What’s the deal?”


MIMI: “Nimekuja aone project mpya nilizoanzisha.”


IRYN: “Vizuri.”


MIMI: “Mzee anaendeleaje lakini?”


IRYN: “Not bad, anaendelea vizuri.”


MIMI: “Mama mdogo mnaishi vizuri?”


IRYN: “Mmh… Kanichukia sana. Ila kwa sababu mimi nakaa upande mwingine wa nyumba, tuna sebule yetu, jiko na kila kitu, kuonana ni mara chache. Mara nyingi mzee anakuwa na mimi.”

MIMI: “Be careful, see you soon.”

Baada ya kumaliza kula, tulichukua bajaji ya kutupeleka nyumbani. Tulipowasili, nilifungua mlango na kumkaribisha wife ndani. Wakati huo alikuwa anatazama mazingira ya pale kwa mshangao na udadisi.

“Hii nyumba… kama vile umempangia mtu. Inavyoonekana inaendelea kufanyiwa usafi,” alisema huku akichungulia kila kona.

“Nina dogo wangu wa ofisini anayeishi kwenye geto la nje. Mara nyingi hupenda kutumia jikoni humu ndani au kusaidia kufanya usafi.” nikamjibu

Ingawa jibu langu halikumwingia moja kwa moja, alikubali kimya kimya kwa sababu hakuwa na la kufanya. Niliamua kubadili mada na nikamwambia tupumzike ili baadaye tuende kutembelea miradi yetu. Wakati huo huo, nilimtumia ujumbe Aggy kumtaarifu kuwa nipo Dodoma na mama J, akanijibu kuwa akitoka ofisini atanitafuta.

Ilipofika jioni, tuliamua kuondoka na kuelekea kuangalia miradi yetu, tukianza na dukani. Tulikaa hapo kwa muda mfupi tu kabla ya kuendelea kwenye ofisi nyingine ya Sanchi. Tulipofika, nilianza kwa kuwasalimia ndugu na jamaa waliokuwa nje, kisha tukaelekea moja kwa moja ndani.

Baada ya kufungua mlango wa ofisi, nilimwona Sanchi akiwa busy, amejikita kwenye kazi zake. Mara tu alipotuona, alionekana kushangaa sana kwa sababu hakuwa na taarifa yoyote kuhusu ujio wetu wa Dodoma, hivyo ilikuwa ni surprise kubwa kwake.

Alisimama haraka, akaja kutukumbatia na kutukaribisha kwa furaha iliyojaa usoni.

“Karibu sana wifi yangu, wewe Insider ni mwenyeji hapa, sina hata haja ya kukukaribisha,” alisema huku akitabasamu.

Baada ya salamu na mazungumzo ya mwanzo, niliwaacha wakiongea ndani na mimi kutoka nje kuonana na team yangu.

Upande wa ofisi yangu kulikuwa na shughuli nyingi, kama kawaida ya weekend ambapo watu wengi hufika garage kwa ajili ya kufanya service za magari. Vijana wangu walikuwa busy sana, na sikutaka kuvuruga mudi yao ya kazi. Niliwasalimia tu kisha nikaingia ndani kuonana na kiongozi wao ambaye ndiye cashier wangu.

Baada ya kusalimiana, nilimuomba aniandalie ripoti zote kuanzia, idadi ya wateja, mauzo, pamoja na taarifa nyingine muhimu. Nilipomaliza kupitia ripoti na kujiridhisha, nikaenda pia kukagua store. Baada ya hapo, nilirudi ndani kuendelea na mazungumzo mengine.

Huyu dada cashier, Aggy, ndiye aliyeniunganisha ni mdogo wa rafiki yake mkubwa na wanafanya kazi ofisi moja. Ninamchukulia kama mdogo wangu kabisa, ni mchapakazi, mjanja na mwepesi kujituma. Ufanisi wake kazini ulikuwa ukinivutia kila siku, kiasi kwamba nilishawishika kumuongezea mshahara.

Zilipita takribani dakika 15 kabla ya Sanchi na Mama J kufika ofisini kwangu kuangalia mazingira. Mama J aliendelea kushangazwa na jinsi ofisi ilivyopangika, huku akizungumza na dada. Baadaye tukatoka nje na kuelekea upande wa workshop ambako alijionea kazi zikifanyika kwa ufanisi mkubwa, kwa kweli, alionekana kuvutiwa sana.

Muda mfupi baadaye, Aggy alipomaliza kazi zake alipitia ofisini. Alipomuona wifi yake, Mama J, walikumbatiana kwa furaha s sana tena isiyofichika. Aggy na Mama J ni marafiki wa siku nyingi, niliwakutanisha tangu tunaanza mahusiano, na tangu wakati huo uhusiano wao umeendelea kuwa wa karibu sana. Aggy ndiye mtu wa kwanza kabisa niliyemtambulisha kwa Mama J.

Baada ya salamu na furaha zote, Aggy aliniangalia na kuanza kunilalamikia kwa safari yangu ya kuja Dodoma kimyakimya bila kumpa taarifa. Nikamcheka kidogo na kumjibu kuwa nilitaka iwe “surprise”.

“You guys, naona leo mmefurahi sana,” Sanchi alisema huku akitembea kuja upande wetu.

“Kwanini tusitoke tukapate dinner pamoja? I will pay,” akaongeza.

Kabla sijasema chochote, Aggy akashauri,

“Insider, mcheki na Maggy kama vipi, na yeye ni familia.”

Wazo lao lilinivutia, hivyo nikampigia Maggy na kumwambia aje Golden Fork. Alionekana kushangaa kwa sababu ilikuwa ghafla, lakini akaniambia ndani ya nusu saa angekuwa ameshafika.

Sisi tuliendelea na story zingine huku tukimsubiri Maggy aanze kutoka nyumbani. Baada ya kunipa taarifa kuwa tayari anaanza kuja, sisi pia tukaanza safari ya kuelekea Golden Fork kwa ajili ya dinner. Tulifika mapema na tukabaki ndani ya gari tukimsubiri Maggy ili tuingie wote kwa pamoja.

Baada ya Maggy kuwasili eneo la tukio, alionekana kushangaa sana kutuona tukiwa wengi kama kamati. Mawazoni mwake, alitarajia angenikuta mimi peke yangu. Baada ya kusalimiana kwa furaha pale kwenye parking, tuliingia ndani kwa pamoja na tukaketi kwenye meza nzuri iliyokuwa huru.

Mhudumu alikuja kutusikiliza, akachukua order za kila mmoja. Kila mtu aliagiza chakula alichotaka, ila mimi nikaishia kuagiza chipsi yai na kuku.

Mara tu baada ya mhudumu kuondoka, Sanchi akanigeukia:

SANCHI: “Insider, kumbe unatumiaga chipsi? Kwa mara ya kwanza kukuona ukiagiza.”

Nilibaki nikitabasamu tu kwa sababu sikutarajia kama swali kama hilo lingeibuka.

MIMI: “Yeah, natumia. Ila ni mara chache sana.”

AGGY: “Hivi mnaelewa kinachoendelea hapa?”

Sote tulimgeukia tukitaka kusikia anachotaka kusema. Lakini yeye alikuwa kimya, akitabasamu kana kwamba anaandaa kitu cha kusema.

SANCHI: “Hivi unajua tunakusikiliza?”

AGGY: “Ni hivi, guys mnaelewa kwamba wote tuko hapa sababu ya Insider?”

SANCHI: “Sijakuelewa… unamaanisha nini?”

AGGY: “Namaanisha kwamba sisi wote tumefahamiana kupitia yeye. Bila Insider, sidhani kama tungekuwa hapa meza moja tukila pamoja.”

SANCHI: “Sasa nimekuelewa. Ni kweli, mimi nimewajua wote kupitia Insider.”

Maneno ya Aggy yaligusa mioyo ya kila mmoja. Kila mtu alikubali kwamba kwa namna moja au nyingine, njia zetu zimekutanishwa na mimi. Lakini nikaona wanapaka chumvi sana, nikaamua kuwanyamazisha kwa kuingilia kati:

MIMI: “You guys, mbona mnadanganyana? Wanasema everything happens for a reason. Kujuana kwetu si jambo la kubahatisha ni mpango wa Mungu. Hata kama asingetumia mimi, bado mngekutana tu. It is written.”

MAGGY: “Sawa, lakini tuseme Mungu alikufanya wewe kuwa daraja letu. Kwa hiyo bado tunarudi palepale kwenye point ya Aggy.”

Kauli yake ikafanya meza yetu izidi kujaa furaha. Mazungumzo yakawa mengi vicheko, utani, na kila aina ya story zilizotufanya tuendelee kuwa pamoja usiku ule. Tulikaa pale hadi saa nne usiku, kisha tukaagana na kila mmoja kuelekea kwenda kulala.

Aggy alitupa kampani hadi home. Kabla hajaondoka, nikamuomba aniazime gari yake kwa siku ya kesho ili nifanye mizunguko yangu bila usumbufu. Akakubali, akaniambia atalipitisha asubuhi wakati wa kwenda ibada ya jumuiya.

Asubuhi ilipofika, niliamka pamoja na Mama J, na tulianza kufanya usafi wa nyumba nzima. Baada ya kumaliza sehemu ya ndani, nikaona niitumie nafasi hiyo pia kumtembelea kaka Bonny-yule kaka mkubwa niliyemfahamu kupitia Michael.

Baada ya kukutana na kaka Bonny, alionekana kufurahi sana maana mara ya mwisho nilipofika pale nikitokea South Africa yeye hakuwepo, alikuwa safarini. Nikamwambia twende kwenye apartment yangu kwa sababu kulikuwa na mgeni. Tulipofika, nikamtambulisha mama J kwake, yeye alibaki akishangaa pale, kwani nyuma nilikuwa tayari nimemtambulisha Iryn na Mary.

Baada ya salamu na utani wa kawaida, tulitoka nje na kukaa kwenye kibaraza chake. Hapo ndipo mazungumzo ya moja kwa moja yakaanza, kama ilivyo tabia yake ya kupenda kwenda straight kwenye point.

BONNY: “Kaka, spidi yako ni kali sana. Huyu sasa ndiyo mama familia?”

Huku nikicheka;


MIMI: “Yeah, kaka, huyu ndiyo mwenyewe kabisa.”

Akanigeukia kwa macho ya mshangao yanayoonyesha hamu ya kujua mengi.

BONNY: Yule dada mzuri mjamzito… na Mary je?”

Kwa sekunde kadhaa nikabaki kimya nikitafakari jinsi ya kuanza kumjibu. Ukweli ni kwamba Mary alishajulikana sana pale home, kwa sababu niliwahi kukaa naye muda mrefu sana, jambo lililowafanya wapangaji wengi wawe karibu naye. Hivyo swali lake lilikuwa la kawaida, lakini uzito wake ulikuwa mwingine.

MIMI: “Yule dada mjamzito tayari kashajifungua, ni kama mke wangu wa pili na Mary yeye ni mchepuko tu. Na kitu usichokijua, mahusiano yangu na Mary yalianza hapa kabisa, kipindi nahamia gheto.”

Kaka Bonny alishtuka kidogo, akakodoa macho.


BONNY: Mkuu, ngoja kwanza, hawa wote wanajuana?”

Nikavuta pumzi ndefu,


MIMI: “Yaani situation ipo hivi… Wife hajui chochote. Iryn anajua nina mke ambaye ndiye huyu hapa. Na Mary, yeye anawajua wote wawili, na aliridhia mwenyewe.”

Kaka Bonny alishika kichwa, akacheka kwa mshangao.


BONNY: Mdogo wangu, you have something special! Hivi inawezekanaje mrembo kama yule anakubali kuwa mchepuko na anakuzalia mtoto? What the f*ck!”

MIMI: “Hahaha, kaka relax ni story ndefu sana. Na si kwamba napenda mambo haya, lakini ni mazingira yalitufikisha hapa. Sometimes huwa naamini ni mipango wa Mungu tu.”

Mazungumzo yetu yaliendelea kwa dakika chache zaidi na yalikoma baada ya kupokea simu kutoka kwa Aggy. Akanitaarifu kwamba tayari amefika nje getini, akiomba nimfungulie geti. Nikaaga haraka, nikamshukuru kaka Bonny kwa muda wake, kisha nikaenda kumkaribisha Aggy.

Saa 5 kamili tuliondoka na wife kuelekea Mtumba, ambako nilikuwa na appointment ya kukutana na mtu kuhusu kununua plot. Tulipofika maeneo yale nilipaki gari pembeni tukamsubiri. Baada ya dakika kama 10, dada ambaye tulikuwa tukiwasiliana alifika na kutupeleka kuona viwanja.

Safari haikuwa ndefu, tukafika kwenye kiwanja cha kwanza alichotuonyesha. Tulipofika kwenye kiwanja cha kwanza, tulivutiwa nacho mara moja sababu eneo lake lilikuwa zuri, tambarare, na karibu kabisa na barabara. Tulipoangalia mazingira yake, hatukuona sababu ya kutembea kuangalia vingine, tukafanya uamuzi hapo hapo. Nikamwambia dada aendelee na hatua zinazofuata na kwamba tutakutana tena kwa ajili ya malipo, na sisi tukaelekea Iyumbu.

Tulipofika kwenye plot yetu nyingine kule Iyumbu, nilimpigia jamaa anayehusika na kumwagilia miti. Miti ilikuwa imekua vizuri sana yenye kijani kibichi, yenye afya, na ilionekana wazi kuwa inatunzwa kwa umakini.

Baada ya muda mfupi jamaa alifika, tukasalimiana na kuanza kuongea.

MIMI: “Naona miti inakuwa vizuri, ahsante sana.”

JAMAA: “Hasa huu mti wa yule dada unakuwa sana,” alisema huku akiwa ameushika.

Mama J alikuwa karibu na kak sasa ile kauli yake ilifanya wife adakie haraka na kuuliza;

MAMA J: “Dada gani kaka?” Wife aliuliza kwa mshangao.

MIMI: “Anamsemea Iryn.”

Nikajibu haraka wakati huo huo nikamtupia jamaa jicho kali sana, jicho la kumuonya kwamba ameteleza vibaya. Na kweli, alijishtukia mara moja, kwani alijua katema boko.

MAMA J: “Iryn alikuja hapa?”

MIMI: “Yeah, alikuja kipindi kile nilipoacha kazi na kuja kujichimbia huku. Alinifuata kuniomba nirudi kazini.”

Mama J hakuridhika na majibu ya haraka, akawa bado anauangalia ule mti.

MAMA J: “Sasa kaka anavyosema huu ni mti wake, anamaanisha nini?”

Nikavuta pumzi ndefu kidogo.

MIMI: “Tulikuja wote siku ile, na akauchagua huu mti kama wake, akampa kaka kazi ya kuumwagilia kila siku, na akamlipa pesa zake zote. Ndiyo maana unaona mti huu ni mkubwa kuliko yote sababu unapata maji mengi kuliko mingine.”

Mama J akatingisha kichwa polepole, akionyesha hisia za kuchanganyikiwa, alihisi something fishy is going on.

MAMA J: “Mhhh! Wewe na Iryn mnasiri nyingi sana. Kama kaka angekaa kimya nisingejua kabisa kinachoendelea.”

MIMI: “Swahiba kweli hata hili ni la kukwambia? Come on, be serious.”

Furaha yake ilipotea ghafla ni kama wingu jeusi limetanda kwenye uso wake. Mazingira yakawa kimya zaidi, bila kuongea. Hatukukaa muda mrefu, tukaondoka na kuelekea mitaa ya Mipango kwa mzee Mollel.

Baada ya kufika kwa Mzee Mollel, tulikaribishwa ndani sebleni na mama. Kwa upande wake alionekana kufurahi sana kutuona, na furaha yake ilizidi zaidi alipomuona mkamwana wake, mama J. Baada ya salamu za hapa na pale pamoja na maongezi mafupi, mama alituambia kuwa tuna bahati mbaya kwani baba alisafiri leo asubuhi kwenda mkoani kikazi.

Mazungumzo yaliendelea pale sebleni, yakijikita zaidi kwenye maisha kwa ujumla. Mama alionyesha hamu kubwa ya kujua maendeleo ya mjukuu wake Junior, na akalalamika kwa upole kwanini hatukusafiri naye mpaka Dodoma.

Sebleni walikuwepo pia watoto wake wakubwa wawili, mmoja akiwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni, na mwingine aliyemaliza kidato cha sita akisubiri kuanza chuo. Yule wa chuo nilikuwa namfahamu, ila huyu wa kidato cha sita sikuwa nimewahi kukutana naye kwa sababu ya kuwa shule muda mwingi.

Ilipofika saa 10 jioni, Sanchi alinipigia simu kunikumbusha mpango tuliozungumza siku zilizopita-kukutana na mdau mmoja pale Morena Hotel. Nilikuwa na appointment na mdau ambaye alikuwa tayari kunisaidia katika kubid tenda mbalimbali, hasa za serikali. Kwa kweli nilikuwa nimesahau kabisa kuhusu hili. Baada ya mazungumzo mafupi na Sanchi, nilitafuta namna nzuri ya kumuaga mama na tukaondoka.

Siku tatu nyuma niliwasiliana na yule mdau ambaye nilimfahamu kwa jina la Mr Ando na tukakubaliana tukutane Jumamosi saa 12 jioni pale Morena Hotel kwa ajili ya masuala ya corporate. Wazo la kwenda na Sanchi lilinijia ili kuongeza attention kutokana na mvuto wake. Nilipomshirikisha Sanchi kuhusu mpango huu, alikubali mara moja na akaahidi kunipa kampani.

Tuliporudi nyumbani, nilijiandaa haraka kisha nikaondoka kwenda kumchukua Sanchi tuende Morena Hotel.

Tulipowasili hotelini, bado tukiwa kwenye parking, nilimpigia simu yule mdau kumjulisha kuwa tumeshafika. Hakuweza kupokea, lakini alinitumia ujumbe kunieleza kuwa bado yuko kwenye kikao na kwamba tumsubiri kidogo, wanatarajia kumaliza muda si mrefu.

Nilimwambia Sanchi tuingie ndani tukakae restaurant ili tuendelee ku-buy time, tukimsubiri jamaa. Tuliposhuka kwenye gari ndipo nilipomuona vizuri kwa namna alivyopendeza. Alikuwa amevaa suruali ya kitambaa rangi ya dark blue, shati jeupe lililomkaa vizuri, chini akiwa na heels safi na usoni miwani meusi. Hakika Sanchi alikuwa amependeza kupita maelezo, shepu lake lilikuwa limechoreka barabara-mwonekano ulioteka macho yangu na watu wengine waliokuwa around.

Kama kawaida yangu sikukosa kumsifia hapo hapo parking, na tabasamu lake la wazi lilidhihirisha namna alivyofurahia maneno yangu. Nilimshika mkono, tukatembea taratibu kuelekea ndani, na hadi tunaingia watu walikuwa wanatuangalia sana. Kweli kumuita Sanchi hakukua kosa hata kidogo.

Tulienda kukaa upande wa restaurant na tukaagiza maji ya kunywa. Nikaweka MacBook juu ya meza ili kuongeza mvuto na professional presence. Tukaanza kupiga stori huku tukisubiri jamaa afike. Baada ya takribani dakika 45, jamaa alinipigia simu kuuliza nilipo, nikamwambia nipo restaurant.

Kwa kuwa sikuwahi kukutana naye uso kwa uso, nilitegemea tu kumuona akitafuta meza niliyokaa. Dakika tano baadaye alifika pale restaurant, na nilimgundua kuwa ni yeye, nikamnyooshea mkono kama ishara, na akaja moja kwa moja kwenye meza yetu.

Kabla hata hatujasalimiana, simu yake iliita na akaipokea hapo hapo. Mimi na Sanchi tulikaa kimya tukisubiri. Baada ya kumaliza maongezi ya simu, ndipo alisema:

MR. ANDO: “Nisameeni jamani, kuna simu zingine huwezi kuzikaushia.”

MIMI: “Yeah sure! Lakini uko poa? Hatujapata hata nafasi ya kusalimiana.”

MR. ANDO: “Aisee ni kweli! Dadeki mambo vipi lakini? Bila shaka wewe ndiyo Insider. Mimi ni Mr. Ando, leo tumeonana live sasa.”

MIMI: “Nashukuru sana kukutana nawe leo. Maana ulipokuja Dar tulikosa kuonana.”

MR. ANDO: “Unajua mishe mishe mdogo wangu… siku napanga kukutana na wewe nikaamrishwa safari ya Mtwara.”

Kisha nikamtambulisha Sanchi:

MR. ANDO: “Huyu anaitwa Sanchi, operation manager wa kampuni. Mimi nikiwa Dar, yeye ndiye anayesimamia ofisi.”

MR. ANDO: “Ahsante dada kwa kukufahamu,”

Baada ya utambulisho tukaanza mazungumzo rasmi ya biashara. Ando alieleza namna ambavyo anaweza kunisaidia kupata tenda mbalimbali, hasa upande wa serikali. Alisisitiza cha muhimu ni kuhakikisha kampuni imekamilisha nyaraka zote pamoja na kuwa na VRN (VAT). Nikamwambia tayari nimeshaanza process, na soon mambo yatakuwa sawa.

Kisha tukafika kwenye suala la malipo. Ando alisema ili kushirikiana vizuri, anataka apewe asilimia 20% ya shares za kampuni na akahakikisha ataleta kazi nyingi. Hili suala sikutegemea kutoka kwake maana nilijua malipo yangekuwa kwa kamisheni, hivyo nikamwambia atanipa ruhusa nikaongee na Director mwenzangu kabla ya kufanya uamuzi.

Baada ya mazungumzo yale, Ando alituaga kwa haraka kwa sababu alikuwa na ratiba nyingine. Tulikubaliana kwamba tutaendelea kuwasiliana pindi nitakapofikia uamuzi kuhusu suala la kumpa nafasi kwenye kampuni.

Mara tu Ando alipoondoka, Sanchi alinitazama kwa wasiwasi.

SANCHI: “Huyu jamaa anaonekana ni nyoka(Code) kabisa 🐍, na connections anazo, ila kumpa 20% ya hisa siyo sahihi hata kidogo.”

MIMI: “Mmh… kama analeta kazi hakuna shida. Mfano kampuni ikipata faida ya 10M, basi 2M tu ndiyo itakuwa yake.”

SANCHI: “Lakini anaweza kukupora kampuni. Be careful.”

MIMI: “Hawezi kuwa na power hiyo. Mimi ninamiliki 80% ya shares nina control ya financial na operational policies zote.”

SANCHI: “Insider tuliza akili kwanza. Usiangalie kupata kazi tu, angalia na risk.”

MIMI: “Sawa mama, nimekuelewa, let’s go.”

Nilimrudisha Sanchi kwake, na kwa kuwa sikuwa nimewahi kufika kwake, niliingia ndani kidogo. Akanitambulisha kwa binti yake wa kike, kisha tukaenda dining kula chakula tukipiga stori. Maongezi yetu yalijikita juu ya yule baba wa mtoto ambaye walizaa mtoto na kumtelekeza mtoto na majukumu yote. Sanchi hakupenda kuzungumzia haya, sababu alisema ni story ambazo huwa zina muumiza na hataki kukumbuka alikotoka. Baada ya kula sikuchelewa niliaga na kuondoka. Wakati huo mama J alikuwa anapiga simu mfululizo akitaka kujua nilipo.

Kesho yake, siku ya Jumapili, Sanchi alikuja nyumbani kushinda na mama J, wakati mimi nilielekea ofisini kuwahi kuonana na vijana wangu. Kwa upande mwingine nilikuwa nawasiliana na Erica-mrembo wangu mpya wa mjini Dodoma. Tulikuwa tunapanga kukutana usiku kwa ajili ya mazungumzo.

Nikiwa ofisini, nikiwa busy na mipango, Iryn alinipigia video call. Nikapokea.

MIMI: “Hey baby.”

IRYN: “Let me guess… hapo ni ofisini kwa Sanchi, right?”

MIMI: “Hahaha… unapafahamu ndomana. Baby, nataka nikushirikishe jambo.”

IRYN: “What is it?”

Nikamsimulia mkasa mzima kuhusu suala la Mr. Ando na mpango wake wa kutafuta tenda za kampuni kisha kutaka kupewa 20% ya hisa. Baada ya kumaliza, alinitazama bila kusema, huku akitafuna crisps kwa maringo yake ya kawaida.

IRYN: “Unampa 20% ya shares za kampuni? Kwa lipi? Analipia hizo hisa?”

MIMI: “Hilo bado hatujaingia ndani. Tulikubaliana tukutane tena kwa maongezi.”

IRYN: “Hebu fikiria jambo moja… kama atashindwa kukuletea kazi lakini tayari umempa hisa, itakuwaje?”

MIMI: “Tutakuwa tumeandikishiana. Kama hataleta kazi narudishiwa hisa.”

IRYN: “Sikiliza, ngoja nikupe mbinu rahisi kabisa. Mwambie mlipane kwa commission kulingana na kazi anazoleta. Mfano akikupa deal ya 10M, mpe 30%. Utaumia kidogo mara ya kwanza, lakini utakuwa umepata customer wa uhakika anayeleta pesa kwa muda mrefu. What do you think?”

MIMI: “Wazo lako ni zuri, ila sidhani kama atakubali. Anasisitiza ataleta kazi nyingi.”

IRYN: “Lakini bado siyo busara kumruhusu mtu usiyemfahamu achukue umiliki wa kampuni ni hatari. Commission ndiyo njia pekee inayotumika duniani kote.”

MIMI: “Sawa, tutakutana naye na tuzungumze kwa kina zaidi.”

IRYN: “Sawa baby, be careful. Ninaanza kupika, lakini usikate simu. Nitakuwa napika huku tunaendelea na story. Leo nimekumiss.”

Tukaendelea na mazungumzo, yeye akipika na mimi nikiendelea na kazi zangu. Baadaye, alipomaliza kupika, tukamalizia maongezi na kuagana.

Saa moja jioni nilitoka kuelekea Rafiki Hotel kuonana na Erica. Nilichagua eneo hilo kwa ajili ya chakula cha jioni kwa sababu sehemu nyingine nyingi nimekuwa nikienda mara kwa mara na ninafahamika sana. Mimi ndiye niliyetangulia kufika, na Erica alinijulisha kuwa tayari alikuwa njiani.

Baada ya dakika kama kumi, alifika na akanipigia simu kunithibitishia kuwa amewasili, nilimuelekeza nilipokaa. Nilimuona kwa mbali akiingia, macho yake yakizunguka kutafuta nilipo, wakati huo wote nilikuwa namtazama kimya kimya. Aliponiona, alitabasamu taratibu, nami nikaendelea kumfuatilia kwa macho mpaka alipokaribia meza. Alikuwa amependeza kupita maelezo, na alipoketi nilijikuta tu nikimsifia.

ERICA: “Nisamehe sana, nimechelewa.”

MIMI: “Hamna shida hata mimi nimefika muda si mrefu. Nimefurahi sana kukuona tena, maana hatujawahi kukaa pamoja kama hivi.”

ERICA: “Yeah, sure hata mimi nimefurahi kukuona, Insider. Vipi, mambo yako kwa ujumla?.”

MIMI: “Nashukuru Mungu, mambo yako poa. Pole na majukumu ya Serikali.”

Erica aliishia kucheka kwa aibu na mhudumu alikuwa kawasili pale kutusikiliza. Tuliagiza chakula na mazungumzo yakaendelea pale, na mada kubwa ilikuwa kuhusu mipango yangu ya biashara. Nilimuelezea hatua mpya ninazotarajia kuchukua hivi karibuni kwa utulivu na kwa mpangilio. Kisha nikamueleza pia kuhusu eneo moja ambalo nilihitaji msaada wake, jambo lililokuwa ndani ya uwezo wake na ambalo lingeweza kunisaidia kutimiza malengo yangu.

Lengo langu kubwa katika mazungumzo yetu ya awali lilikuwa kuhakikisha kuwa biashara zangu zinafanyika kwa kufuata taratibu na sheria zote za nchi, bila kuvunja hata moja. Erica alionesha uelewa wa kina pamoja na nia ya dhati ya kunisaidia katika jambo nililomwomba. Aliniomba nimpe muda akapime namna bora ya kunisaidia bila kukiuka sheria wala taratibu.

Baada ya kumaliza mazungumzo ya masuala ya kampuni, tuligeukia upande wa mahusiano yetu ambayo, kumbuka, bado yalikuwa mapya. Na kwa jinsi alivyokuwa akinitazama, ilikuwa wazi kabisa kuwa alibeba maswali na mashaka kadhaa moyoni.

Tulipomaliza kula, niliagiza vinywaji. Nikaomba dada mhudumu atuletee wine.

ERICA: “Dada, mimi naomba maji.”

MIMI: “Dada, na mimi niletee maji, acha wine.”

DADA: “Sawa, haina shida.”

Niligeuka nikamuuliza taratibu,

MIMI: “Hutumii alcohol au leo hauko sawa?”

ERICA: “Mimi situmii kabisa alcohol.”

MIMI: “Oh, sorry… sikujua.”

ERICA: “Lakini wewe kuwa comfortable. Kwa nini umeghairi ghafla?”

MIMI: “Siwezi kunywa alcohol mbele yako kama wewe hutumii. Haipendezi.”

Alitabasamu kidogo, akaituliza sauti yake,

ERICA: “I believe unatumia alcohol, but kwa kiasi, na sio mlevi.”

MIMI: “Natumia vinywaji laini kama hizi wine occasionally. So… baada ya hapa si tunaenda home ukapajue?”

Nilimuuliza hilo kama mtego, nilihitaji tu kuona majibu yake, ingawa nilijua fika kuwa haiwezekani kwenda naye home sio kwa sababu nyingine yoyote bali kutokana na ukweli kwamba mke wangu alikuwa nyumbani.

Erica hakujibu mara moja. Alinyamaza, akatafakari, kisha akaamua kujibu kwa uangalifu,

ERICA: “Kwako nitakuja lakini siyo leo.”

Nilimshika mikono yake juu ya meza, nikamwangalia moja kwa moja machoni.

MIMI: “Unataka kuja lini wakati mimi kesho naondoka kurudi Dar? Hutaki upajue nakaoishi?”

ERICA: “Next time ukija Dodoma nitakuja kwako, and I promise.”

MIMI: “Promise me kwamba utalala kabisa.”

Aliniangalia kwa aibu kidogo, akatikisa kichwa taratibu.

ERICA: “Nitajitahidi… lakini unajua bado naishi kwa Uncle na ni mkali sana. Siwezi kukupromise hilo asilimia mia, but I’ll try.”

Baada ya mazungumzo hayo marefu tulipanga kuondoka, tuliinuka na kuelekea kwenye parking nilipokuwa nimepark gari. Tukawa tumebaki hapo kwa muda mfupi tukipunguza ukimya kwa romance ndogo ya kuagana. Baadaye, Uber yake ilifika, akapanda, na mimi nikabaki nikimtazama hadi mlango unafungwa kabla ya kuanza safari ya kumrudisha nyumbani.

Baada ya kurejea nyumbani, nilimkuta Aggy pamoja na mama J sebleni wakipiga stori zao. Niliingia nikaketi nao, tukaendelea na mazungumzo ya kawaida kama hakuna kitu chochote kilichotokea muda mfupi uliopita.

Haikuchukua muda mrefu, simu yangu ilianza kuita. Nilipoangalia, nikaona jina la Erica liking’aa kwenye screen. Sikuwa na namna ya kupokea simu hiyo pale ndani, kwa hiyo nikaamua kutoka nje kidogo ili kumsikiliza vizuri, moyo wangu ulihisi kwamba kulikuwa na jambo muhimu alitaka kusema.

Nilipoipokea simu, sauti yake ilikuwa ya utulivu na ya heshima. Kwanza, alinijulisha kuwa amefika nyumbani salama, kisha akashukuru kwa dinner tuliyokula pamoja. Baada ya hapo, akaingia kwenye hoja ambayo nilihisi ndiyo ilimfanya apige simu hiyo, alinieleza nisijisikie vibaya kwamba alikataa kuja kwangu. Alisema sababu iliyopelekea kukataa kwake ni kuwa nyumbani kwao alitakiwa kurudi mapema, na hakutaka kuonekana kama anachelewa bila sababu.

Nilimtoa wasiwasi mara moja na nilimwambia,

“Usijali kabisa mimi sina shida. Wakati utakapofika, utapafahamu tu.”

Kauli hiyo ilimfanya apumue kwa utulivu na akaendelea kuongea, akaniambia kwamba atahakikisha analishughulikia jambo nililomwomba mpaka litakapofanikiwa. Tuliendelea kuongea maongezi mengine kuhusu familia yake ya Dodoma anakoishi na baadae tuliagana na mimi kurudi ndani.

Niliporudi sebleni, muda huo Aggy alisimama na kuaga, alisema kuwa kesho asubuhi atakuja kutuchukua kutupeleka airport. Tukamsindikiza hadi nje, nikafunga mlango baada ya kuondoka, kisha mimi na wife tukaendelea na stori za hapa na pale na kubwa alisema anajipanga kununua gari itakayomsaidia kwenye mishe zake.

Saa nne asubuhi, Aggy alikuja nyumbani kutuchukua ili atusindikize airport, akitokea moja kwa moja kazini. Safari ilianza mapema, hewa ya asubuhi ikiwa tulivu na barabara zikiwa bado hazijachangamka sana. Tukiwa njiani, Aggy alimwambia mama J kuwa kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuja Dar es Salaam kikazi mwezi ujao. Nilikuwa nasikia mazungumzo yao waziwazi, lakini sikutaka kuwaingilia, wote walikuwa wamekaa mbele, na Aggy alikuwa akiendesha gari.

Tulipitia ofisini kwanza, ambapo tulimkuta Sanchi. Mama J aliagana naye, nami nikapata nafasi ya kuwaaga vijana wangu. Takribani dakika tano zilipopita, Sanchi alikuja nilipokuwa na kuniomba tusogee pembeni kidogo ili tuzungumze kwa faragha.

Nikaanza kwa utani:

MIMI: “Nambie bossy wangu, umefika hapa kuniaga kwa kuni-hug?”

Sanchi alicheka tu, tukatabasamu kwa pamoja.

SANCHI: “Insider, unapenda sana kunichokoza, ila kilichonileta ni ile ishu ya dhahabu. Tafadhali usisahau kuniulizia kwa yule mtu uliyeniambia, ili kama itawezekana, mwishoni mwa mwezi nije Dar tukamalize.”

Nilimtazama huku natabasamu, nikamshika kidevu chake kwa utani.

MIMI: “Usijali, hilo limekaa sawa.”

Tuliendelea kuzungumza mambo mengine kwa muda mfupi, na baada ya dakika chache Aggy na Mama J walikuja kunijulisha kuwa muda wa kuondoka umefika. Kabla ya kuondoka, tulipiga picha ya pamoja na Sanchi kisha tukaelekea airport kwa ajili ya safari.

Tulipofika airport na kumaliza taratibu za check-in, Aggy aliniomba nimsindikize hadi parking. Tulipokuwa tukitembea, alianza kuniuliza maswali kuhusu Iryn. Kitu kikubwa alichotaka kujua ni kama mimi na Iryn tuko kwenye mahusiano au laah!. Nilishangaa kidogo, maana nilidhani suala hilo tulishalizungumza zamani.

AGGY: “Nakuuliza hivi kwa sababu wifi kaniuliza kuhusu huyo Iryn.”

Nilishtuka kidogo na nikampa umakini wote.

MIMI: “Amekuuliza nini hasa?”

AGGY: “Aliuliza kama tulionana kipindi kile Iryn alipokuja Dodoma.”

MIMI: “Na ulimjibu nini?”

AGGY: “Lilikuwa swali gumu sana, hata sikujua nijibu ndiyo au hapana.”

MIMI: “Mwisho ukamjibu nini?”

AGGY: “Nilimwambia tulionana, ila ilikuwa kwa haraka sana, na hatukupata muda wa kuzungumza sana baada ya Insider kunitambulisha kuwa ni bossy wake.”

Nikatikisa kichwa kwa kukubaliana naye.

MIMI: “Umefanya vizuri kumwambia ukweli.”

Nikamsimulia Aggy tukio lililotokea tulipoenda kuangalia plot yetu, na nikamweleza kuwa kwa bahati mbaya mama J hakupata nafasi ya kumuuliza maswali zaidi, japokuwa kulikuwa na jambo lililokuwa linamsumbua kichwani. Aggy akanishauri kwa msisitizo mkubwa niwe makini, kwa sababu mama J ana hisia kuwa huenda mimi na Iryn tuko kwenye mahusiano ya siri.

Tulizungumza kwa kina, nami nikamhakikishia wazi kuwa mimi na Iryn hatuna mahusiano yoyote zaidi ya yeye kuwa bossy wangu. Baada ya hapo, tukaagana, nami nikarudi ndani ya airport kujiandaa kwa safari.

Tulipowasili Dar es Salaam, tulichukua Uber hadi nyumbani. Uchovu wa safari ulinishika, nikaamua kupumzika kwa kulala.

Saa kumi na moja jioni, nilienda Masaki kukutana na kaka Allen. Kulikuwa na masuala ya kujadiliana kuhusu TRA, na tulihitaji kuyajadili kwa kina. Allen alikuwa tayari ananisubiri pale Samaki Samaki, na alinijulisha kwa ujumbe kuwa tayari kafika.

Baada ya kufika eneo la tukio na kuonana, tulianza mjadala mzito kuhusu suala hilo hadi tukafikia muafaka. Baada ya hapo, mazungumzo yakahamia upande mwingine, habari kubwa ikiwa ni kuhusu Hilda. Nilikuwa na shauku kubwa kujua amefikia hatua gani. Allen aliniambia kuwa kwa sasa mambo yako vizuri, hata wikiendi iliyopita walikuwa pamoja na walitoka out.

Baada ya kupata taarifa hizo, sikutaka kuendelea kuchimba zaidi. Haikupita muda mrefu nikamuaga Allen kuwa naondoka na lengo niwahi kwenda kwa Mary. Kwa upande wake alishangaa kuona naondoka mapema, lakini nikamwambia ni uchovu wa safari, ilhali kiuhalisia mawazo yangu yote yalikuwa kwa Mary.

Baada ya kuachana na Allen, niliendesha gari kwa kasi kuelekea apartment ya Mary. Sikumpa taarifa ya ujio wangu, lengo langu lilikuwa ni kumaliza tofauti zetu na kurejesha uhusiano wetu katika mstari. Nilikuwa tayari nimejipanga, nikijiandaa na majibu ya kumpa endapo angeniuliza maswali.

Nilipofika, nilipaki gari na kupanda moja kwa moja hadi kwenye apartment yake. Nilipiga hodi kwa kugonga taratibu, nikisikiliza kwa makini kwa sababu mazingira yalionekana kuwa kimya sana.

Mhh, Mary atakuwepo? niliwaza kimoyomoyo.

Ghafla nikasikia kitasa kikigeuzwa, mlango ukafunguliwa. Nilipatwa na mshangao mkubwa aliyekuwa amesimama mbele yangu hakuwa Mary, bali ni jamaa mwingine, tena mwenye mwonekano wa kunizidi hata mimi kwa umbo. Nilisimama pale kwa mshangao, nikijiuliza kimoyomoyo kama nimekosea apartment.

Jamaa akaanza kuongea kwa sauti tulivu:

“Bro, karibu, nakusikiliza.”

Nikajibu kwa tahadhari,

“Samahani, sijui kama nimekosea apartment… hapa ni kwa Mary?”

“Ndiyo, hujakosea kaka. Unahitaji nini?”

Hapo ndipo nilihisi hali ya dharau ikianza kujitokeza kutoka kwa Jamaa. Sababu alikuwa anaendelea kuniuliza maswali tena ananionesha dharau za waziwazi. Nikatambua wazi kuwa hapa sikuwa na nafasi tena, nilikuwa nimeingia kwenye himaya ya mtu mwingine. Bila kuongeza neno, nikaamua ni bora niondoke haraka kabla mambo hayajaharibika zaidi.


TO BE CONTINUED
 
Back
Top Bottom