Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Attachments

  • Screenshot_20260103-040732.png
    Screenshot_20260103-040732.png
    262.4 KB · Views: 44
ARY: “Insider, nishamove on, sitaki tena kuwa kwenye mahusiano na wewe. Nikikaa karibu na wewe nitakuwa nakupa nafasi ya kuendelea kuniumiza.”
Kuna demu wangu (mchepuko) anaitwa marry naye ananisumbua sana nana maneno yake ni kama haya haya, nilimwambia jamaa yangu akaniambia tafuta hela hawezi kukuacha. ila kama hadi nyie matajiri munakataliwa kama sisi imenipa faraja sana hii
 
SEASON 03
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
CHAPTER 16

Ukweli ni kwamba nilibaki nimesimama kama nimerogwa nilipousoma ule ujumbe, nilipigwa na butwaa. Sikuamini kabisa nilichokiona, wala sikutarajia hata kidogo kwamba Hilda angefikia hatua ya kuchukua uamuzi mzito kiasi kile, ilikuwa nje ya mawazo yangu.

What the fck!* Ndani ya sekunde chache, lawama zote nilijipa mimi. Nilianza kujilaumu kwa nini nilichelewa kumtafuta, kwa nini nilishindwa kumaliza tofauti zetu mapema. Moyoni nilijua wazi kabisa chanzo kikubwa cha haya yote ni mimi kushindwa kumpa Hilda ile attention aliyokuwa akiihitaji.

Nilijiuliza pale nafanya nini sasa? Maana
Sikuona njia nyingine zaidi ya kwenda kwake. Nilijua lazima atakuwa nyumbani, hasa ukizingatia muda haukuwa umeenda sana tangu aondoke ofisini. Bila kufikiri mara mbili, niliwasha gari na kuondoka kwa fujo pale ofisini.

Njiani, mawazo yalikuwa yanapishana kichwani. Nilijisemea, naenda kumpa Hilda anachotaka, lakini siyo kumuacha aondoke, hasa kwenye kipindi hiki ambacho namuhitaji sana ofisini.

Haikuchukua muda mrefu nikawa tayari nimefika kwenye apartment yake, sikumpa taarifa yoyote ya ujio wangu. Nilipaki gari nje ya uzio, nikasogea getini na kugonga. Bahati nzuri, jirani yake ni dada aliyekuwa anafua nguo alinifungulia geti.

Baada ya salamu chache, nilienda moja kwa moja hadi kwenye mlango wa apartment ya Hilda na kugonga. Kulikuwa na ukimya wa sekunde kadhaa, kisha nikasikia mlango unafunguliwa. Alishtuka kuniona, alibaki amesimama akinitazama, ugeni wangu haukuwa kwenye matarajio yake.

“Ooh! Insider… karibu sana.”

Sikujibu chochote na ilimtazama tu, kisha nikaingia moja kwa moja sebuleni. Mezani kulikuwa na nyaraka kadhaa, na nilianza kuzipekuapekua bila hata kuuliza, mpaka nikajikuta nimeshika CV yake mkononi na kuisoma.

MIMI: “Ninaona umeanza kuandaa documents za ofisi mpya. Hilda, kwa nini unaacha kazi hasa kwenye kipindi hiki ambacho nakuhitaji? Tafadhali niambie, kuna kitu ofisi imekutreat vibaya?”

Hilda alinyamaza kimya kwa sekunde kadhaa kabla hajajibu..

HILDA: “Hapana, nimeamua tu kubadili mazingira ya kazi. Samahani sikutoa taarifa mapema.”

Nilisimama kutoka nilipokuwa nimekaa, nikamkaribia na kushika mikono yake yote miwili, na nilimtazama machoni.

MIMI: “Acha kunidanganya bhana sababu kuu unaondoka ni mimi. Tangu turudi Zanzibar hujawahi kuwa sawa. Ndiyo maana nimekuja hapa uniambie unataka nikufanyie nini?”

HILDA: “No! No! Noo! You are not the reason it happened.”

Lakini mwili wake ulikuwa unasema kitu tofauti, nilimshika kiunoni taratibu, nikamsogeza karibu yangu. Hakunipa upinzani wowote na ukimya wake ulikuwa mzito kuliko maneno. Nilimvuta kwangu, nikambana vizuri, nilihisi joto lake la asili na nikaanza kupapasa hips zake taratibu. Alianza kuhema kwa shida huku akitoa sauti ya chini na miguno..

“Insider please, niache.”

Na alianza kujinasua kutoka kwenye mikono yangu na mimi nikamuachia kwa muda. Alianza kuelekea chumbani, nikamfuata kwa nyuma kisha nikamvuta tena na kumpa tongue akapokea kwa pupa. Baada ya kuona sipati tena upinzani na akitoa ushirikiano nikaanza kutalii maeneo mengine ya hifadhi ya Serengeti. Ukweli nilianza kupagawa na maajabu niliyokuwa nina yaona kwenye ile mbuga, nilikuwa nashuhudia uumbaji wa dhahabu uliotukuka.

Hilda alikuwa na pupa ya ajabu, kiasi kwamba alikuwa akisubiri hii neema kwa muda mrefu sana. Ndani ya muda mfupi, hisia zilikuwa zimeshachukua usukani, alikuwa chapachapa tayari kwa kuanza safari ya kwenda dunia nyingine ya mahaba. Ilikuwa ni burudani ambayo ilichukua muda mrefu sana kabla ya kupitiwa na usingizi fofofo.

Nilipozinduka, kichwa kilikuwa kizito, macho yakiwa bado hayajakaa sawa. Nilipochukua simu ndipo mkanganyiko ulipoanza rasmi, saa ilikuwa ikisoma ni saa 8 kasoro za usiku. Kwenye screen, kulikuwa na msururu wa missed calls za kutosha kutoka kwa Mama J, na kutoka kwa Iryn. Jambo la kunishtua zaidi, karibu wanawake wote waliokuwa sehemu ya maisha yangu kipindi hicho kuanzia Erica, Ghati na Prisca walikuwa wamepiga simu pia.

Moyo ulianza kwenda mbio na mapigo ya moyo yakibadilika;

Nilifungua ujumbe mmoja kutoka kwa Mama J. Ulikuwa mfupi lakini mzito:

“Baba J, hivi kwanini unapenda kuniumiza moyo wangu? Kama hao wanawake unaona ni wa muhimu, kwanini usiishi nao?”

Nilikaa kimya nikitazama screen kwa sekunde kadhaa. Swali moja tu lilikuwa likinipiga kichwani-imefikiaje nimelala hadi muda huu? Mara ya mwisho niliangalia saa ilikuwa ni saa tano usiku. Nilikuwa nimepanga kupumzika kidogo tu kwa sababu ya uchovu wa sex, halafu ningeondoka. Kuja kuamka saa nane kasoro za usiku kuliniacha nikiwa nimeshikwa na butwaa kabisa, sikuelewa hata kidogo kilichotokea.

Hilda alikuwa kalala uchi fofofo na muda huu nilianza kuview nyashi yake vizuri maana alikuwa kalalia tumbo. Pale kitandani palikuwa pa hovyo sana, maana shuka lilikuwa limelowa kila sehemu. Nilianza kufikiri kama naoga au laah! Na kuondoka bila kuoga ingekuwa ajabu ukizingatia harufu ya sex ilikuwa imenitapakaa.

Hilda aliamka pale, aliniita kwa sauti ya uvivu,

“Insider…”

Alinisogelea na kuanza kunipapasa mgongoni polepole.

HILDA: “Kwa nini unaondoka? Nilidhani tunalala pamoja.”

Nilimwambia huku nikimuonyesha simu;

MIMI: “Hilda, ni saa nane sasa, hata sielewi nimelalaje. Angalia hizi missed calls za wake zangu.”

Hilda naye kwa upande wake alibaki akishangaa jinsi muda ulivyokwenda na alianza kutoa shuka pale kitandani;

HILDA: “So what are you doing?”

MIMI: “Naondoka narudi nyumbani.”

HILDA: “Basi kaoge kwanza.”

MIMI: “Najifikiria hapa kuhusu kuoga, humjui Mama Junior wangu vizuri. Yule mwanamke ni mpekuzi sana akigundua nimeoga usiku huu, atajua nimetoka kwa mwanamke mwingine.”

Niliamua kuingia bafuni na badala yake niliishia kunawa na kujifuta kwa taulo vizuri, kisha nilimuaga Hilda naye akatoka kunisindikiza hadi nje getini.

Njiani kurudi nyumbani, mawazo yangu yalikuwa hayakai sehemu moja maana kila kona ya barabara ilinirejesha kwa Iryn. Simu zake za mara kwa mara zilinipa ishara kuwa huenda alikuwa na tatizo, labda alihitaji msaada wangu. Lakini kwa wakati ule, sikuwa na nguvu ya kumpigia sababu ulikuwa ni usiku sana, pia ningeweza kutengeneza matatizo mengine.

Nilikuwa nakiendesha gari kwa spidi kuliko kawaida. Nilipofika mitaa ya Mikocheni, karibu na Palm Village, wazo moja lilinijia ghafla la kununua bia. Nilihitaji kuonekana kama nimetoka kunywa, labda hiyo ingetengeneza mazingira fulani kwa wife.

Nikasimama pale Triple 7, nikanunua Heineken mbili. Nilipofika nyumbani, sikuharakisha kuingia, nilibaki nje ya geti, nikafungua chupa moja na kuanza kuinywa polepole hadi ikafika nusu. Ndipo nikaingiza gari ndani na kuingia sebleni nikiwa na chupa mkononi.

Namkuta sebleni Mama J alikuwa amelala kwenye sofa, amejifunika kwa mtandio mwepesi. Nilisimama kidogo nikimtazama, nilijiuliza pale nimuamshe au niende kuoga kwanza?. Ukweli ni kwamba sikuwa comfortable hata kidogo, kile kilichotokea kwa Hilda kiliniacha nikiwa na hisia nzito, na hata kuwa karibu na mke wangu sikuwa natamani.

Lakini nilijua pia kumuacha pale na kwenda chumbani kuoga kungezaa matatizo zaidi. Hivyo nikaamua ni bora nimuamshe, angalau tuzungumze. Niliketi kwenye mkono wa sofa, nikasogea karibu naye, nikamuita kwa sauti ya upole iliyochanganyika na uigizaji;

“Swahiba… baby…”

Mama J aliamka na kukaa huku akiniangalia kwa macho makali sana, na mimi nikaendelea kupretend kama nimelewa;

“Mke wangu nimekuletea na wewe bia unywe maana najua una kiu.”

Alininyang’anya ile chupa na kuiweka mezani, na akaanza kuongea pale;

“Baba J ndo nini hivi unanirudia usiku wa manane na umelewa, kwanza ulikuwa wapi na nani?”

“Hahahaa! Nilikuwa na walevi wenzangu ambao wake zetu wanatupa stress, wacha me nikalale.”

Nikaanza kusogea kuelekea chumbani, nikijaribu kukwepa mazungumzo zaidi. Sauti ya wife ikanifatia nyumba;

“Baba J shenzi.”

Baada ya kufika chumbani niliingia bafuni kuoga chap na ile natoka nakuta amekaa kitandani.

“Our conversation is not over yet, ulikuwa wapi usiku wote huu na simu zangu hupokei.”

“Swahiba mimi nimechoka sana hata sikuelewi, kesho bhana.”

Mimi nilipanda kitandani kulala na yeye aliendelea kukaa pale kitandani na alionekana akitafakari mambo.

Baada ya kuamka ile asubuhi, mawazo yangu yalirudi moja kwa moja kwa Hilda na kile kilichotokea usiku uliopita. Nilijikuta nikirejea tukio hilo hatua kwa hatua, nikitafakari kila kilichofanyika usiku wa jana. Kadiri nilivyozidi kukumbuka, ndivyo nilivyozidi kujiridhisha kuwa ilikuwa ni halali kulala vile.

Maneno ya Hilda nayo yakaanza kunirudia akilini. Mara nyingi alikuwa akiniambia kuwa kwa muda mrefu amekuwa single. Sikuwahi kuyaamini maneno hayo, moyoni nilijua kuna kitu alikuwa ananificha. Lakini baada ya yale yaliyotokea, nilijikuta sina budi ila kuyaweka maneno yake katika mizani mpya ya ukweli.

Ukweli sisi wanaume huwa tunamtambua mwanamke ambaye hajaguswa kwa muda mrefu wakati wa tendo. Sasa kipindi naingiza gari yangu uwanja wa mapambano kwa mara ya kwanza, licha ya barabara kuwa safi na kumwagiliwa vizuri. Lakini bado nilipata shida sana kuingia, pia alikuwa akilalamika mno.

Niliendelea kulifikiria tukio hilo kwa muda, lakini sikutaka kujilaumu kupita kiasi. Nilijipa sababu zangu kuwa nilifanya kwa maslahi ya kampuni, na kwa kufanya hivyo, niliamini nisingempoteza Hilda. Hata hivyo, swali moja zito lilibaki likining’inia akilini mwangu, What is next?.

Niliingia bafuni kuoga, wakati najiandaa kutoka, wife aliingia chumbani na bila kupoteza muda akaanzisha mazungumzo yale yale tulipoishia niliporudi nyumbani usiku.

MAMA J: “Baba J, naomba uniambie kwa nini ulikuwa hupokei simu zangu. Ulikuwa na nani?”

Nikavuta pumzi kidogo kabla ya kujibu.

MIMI: “Nilisahau simu kwenye gari, na lilikuwa mbali.”

Alinitazama kwa jicho la kutoamini.

MAMA J: “Una maana gani? Na ulikuwa na nani?”

MIMI: “Nilikuwa na Dullah.”

MAMA J: “Mpigie simu niongee naye.”

MIMI: “Uongee naye nini?”

MAMA J: “Ni-confirm kama mlikuwa wote. Mimi nachojua jana ulikuwa na mwanamke mwingine.”

MIMI: “Kama ningekuwa na mwanamke mwingine, ningerudi hapa home kweli? Si ningetafuta sababu ya kukudanganya na kutorudi?”

Alinisogelea kidogo.

MAMA J: “Call him, please.”

MIMI: “You already know I can’t do that, hata Dullah atanidharau. Yaani nianze kumpigia Dullah na umuulize ujinga wako? You can’t be serious.”

Nikafungua droo kuchukua funguo ya gari niondoke, lakini sikuiona nilijua wazi lazima atakuwa nayo.

“Naomba funguo yangu ya gari, please.”

MAMA J: “Junior anayo seblen.”

Nilihisi hasira ikipanda.

MIMI: “Ulienda kukagua gari yangu? Bila shaka hata bia yangu utakuwa umenisaidia kuitoa.”

Alinisonya kwa sauti ya juu, lakini mimi hata sikujali nikaondoka.

Nilianza safari kuelekea Masaki. Njiani, Lucy alinipigia simu akiniomba nimpitie pale Mwenge. Wakati huohuo, nilimpigia Iryn mara tatu mfululizo, lakini hakupokea nikapanga nitamtafuta baadaye.

Baada ya kumchukua Lucy, tuliendelea na safari ya Masaki. Mazungumzo yakageukia moja kwa moja kwenye suala la Hilda.

LUCY: “Manager, Hilda amekutaarifu kuwa ameacha kazi?”

Nilicheka kidogo.

MIMI: “Hilda hawezi kuacha kazi kirahisi bhana.”

Lucy alinitazama kwa makini.

LUCY: “Kanitumia message kuwa ameacha kazi. Nilimpigia hapokei, na wewe pia ulikuwa hupokei simu.”

Nikataabasamu kimoyomoyo, nikikumbuka kuwa muda ule mimi na Hilda tulikuwa kwenye dunia nyingine kabisa.

MIMI: “Hilda hajaacha kazi, trust me.”

LUCY: “Insider, unachukulia mambo simple sana. Kama kweli Hilda ameacha kazi, ni kwa uzembe wako.”

MIMI: “So ulitaka nimtongoze kama yeye anavyotaka?”

LUCY: “Hiyo sio concern yangu ila ungeweza kukaa naye chini mkamaliza tofauti zenu. Wewe ni meneja you know how to handle all this bullshit.”

MIMI: “Kama Hilda kaacha kazi, tutaajiri mtu mwingine mwenye uzoefu. Asijifanye yeye ni mkubwa kuliko kampuni.”

LUCY: “Duuh!”

Tulipitia sehemu tukasimama kunywa supu kidogo, kisha tukaelekea moja kwa moja ofisini. Tulipofika na kuingia ofisini, Lucy alisimama ghafla, macho yake yakatanuka kwa mshangao. Hilda alikuwa amekaa kwenye kiti chake, tena akiwa na tabasamu pana usoni-alionekana mwenye furaha isiyo ya kawaida. Nikavunja ukimya.

MIMI: “Hilda mambo! Lucy alikuwa ananiambia eti umeacha kazi.”

Hilda akatabasamu kwa kujiamini kidogo.

HILDA: “Lucy siwezi kuacha kazi bhana.”

Lucy akatikisa kichwa kwa tabasamu la kushangaa.

LUCY:” Nimefurahi kukuona, maana njiani kote nilikuwa ninagombana na Insider kuhusu wewe.”

HILDA: “Nipo dear, siwezi kuwaacha kizembe.”

Lucy akaniangalia kwa macho yaliyokuwa yamejaa maswali kama mtu ambaye bado hajaridhika na majibu aliyopata. Ilikuwa wazi anahisi kuna mkono wangu umehusika katika kurudi kwa Hilda, lakini hakuwa na pa kuanzia kuniuliza. Baada ya sekunde chache za ukimya, aliaga akisema anaenda kuonana na mteja wake, akatuacha mimi na Hilda ofisini.
Hilda akavunja ukimya kwa sauti ya chini.

HILDA: “Niliogopa hata kukupigia simu muda ule. Nilikuwa na imani kila kitu kilienda sawa na wife.”

MIMI: “Yeah, but anahisi nilikuwa na mwanamke mwingine. Tuachane na haya, unaonekana mwenye furaha sana leo, siri ni nini?”

Hilda akacheka kidogo kwa aibu, macho yakikwepa yangu, hakusema neno.

“Nimefurahi kukuona ofisini. You look so beautiful.”

Hilda akatabasamu kwa upole.

HILDA: “Thank you, Insider.”

Nilihisi wazi kwamba alikuwa ameanza kunionea aibu. Alikuwa kama mtu aliyepoteza kujiamini kidogo, tofauti kabisa na Hilda niliyemzoea. Kabla sijaongeza neno lingine, simu yangu ikaingia, ilikuwa ni video call kutoka kwa Iryn. Nikatoka nje haraka kwenda kuipokea;

MIMI: “Baby, I’m really sorry for…”

Hakunipa nafasi ya kumaliza.

IRYN: “Hivi baba Aria una shida gani? Jana nimeanza kukutafuta kuanzia saa 1 usiku hadi saa 5 usiku hupokei simu zangu. Halafu bila mimi kukutafuta, hujali hata kupiga simu kujua maendeleo ya mwanao. Aria ni mtoto wako wa damu usipomjali, unataka nani amjali?”

Nilihisi uchungu na hasira iliyochanganyika na maumivu ikimtoka moyoni, nikajaribu kumtuliza.

MIMI: “Baby, sorry jana…”

Akanikatisha tena.

IRYN: “Jana nilikupigia simu kukupa taarifa kwamba Aria anaumwa. Nimeshinda naye hospital tangu jana usiku, hadi sasa bado tuko hospital.”

Maneno hayo yalinichoma moyo, nilinyamaza kwa sekunde kadhaa kabla ya kuzungumza.

MIMI: “Aria anaumwa nini, baby?”

IRYN: “Insider, am not okay, hata kuongea na wewe hapa najilazimisha.”

MIMI: “Pole sana, najua umechoka. Tafadhali mpe Samantha simu niongee naye kama yuko karibu.”

IRYN: “Okay.”

Samantha akapokea simu na kuniambia Aria ana homa kali, mafua makali, na alikuwa anatapika sana. Alijaribu kunituliza kwa kuniambia hali yake inaendelea kuimarika na kuna uwezekano wakaruhusiwa leo kama afya itaendelea kuwa vizuri.

Nilimuomba awe ananipa taarifa kupitia namba yake, lakini akasema atanipigia kupitia namba ya dada yake. Alisisitiza kuwa dada yake hajamruhusu kuwa na namba yangu, hivyo mawasiliano yatakuwa yakipitia kwake.

Baada ya kumaliza maongezi yetu, nilibaki na mawazo mengi kichwani. Kitendo cha Iryn kumzuia mdogo wake kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mimi kilinizingua sana. Nilishindwa kabisa kuelewa sababu yake ni nini. Je, alikuwa anaogopa nitamtongoza? Au kulikuwa na jambo jingine nyuma ya pazia? Maswali yalikuwa mengi, majibu hayakuwepo.

Kwa ujumla, maneno ya Iryn yaliniuma sana. Aliongea kwa uchungu mwingi, na ukweli ni kwamba alikuwa na haki ya kusema vile ukizingatia nilikuwa nimezembea kupita kiasi. Wakati wote huo ambao alikuwa ananipigia simu, mimi nilikuwa na Hilda tukipenzika.

Nilibaki pale kibarazani kwa muda, nikitafakari maisha yangu na mawazo yangu mengi yalikuwa yanamzunguka Hilda. Nilikuwa, bila hata kutarajia, nimeanza kufungua ukurasa mpya naye. Niliogopa sana na nilijiambia moyoni kwamba nisipokuwa makini, yale yaliyotokea kwa Asmah yanaweza kujirudia tena kwa sura ile ile.

Mawazo yangu yakakatizwa ghafla na simu iliyoingia kutoka kwa Erica Dodoma. Alinieleza kuwa Jumatatu angefanya visit ofisini, hivyo nilihitajika kuwapa taarifa wahusika wote watakaokuwepo. Nilimwambia nitamtumia namba ya mtu wa kuwasiliana naye atakayemwelekeza mpaka afike ofisini bila shida. Baada ya kukata simu, nikamtumia namba za Sanchi kama nilivyoahidi.

Jioni ilipowadia, nilijiandaa kuondoka kuelekea Kariakoo kuangalia maendeleo ya biashara dukani. Nilipokuwa natoka kuelekea eneo la maegesho ya magari, Lucy aliniita akionesha kuwa na jambo la kuzungumza. Nilimpa ishara anifate hadi parking ili tuweze kuzungumza kwa uhuru, naye akafanya hivyo.

Nilimwambia kuwa ninaondoka na kama kutakuwa na jambo lolote tunaweza kuonana Jumatatu. Wakati huo alikuwa akitabasamu sana. Nikachukua nafasi hiyo kumuuliza kuhusu maendeleo ya mahusiano yake na Bob. Alitabasamu tena kisha akaniambia kuwa wamerudiana na kwa sasa mambo yanaenda vizuri. Kwa kweli, zilikuwa habari njema sana kwangu.

MIMI: “Mna muda gani tangu mrudiane?”

LUCY: “Tunaenda mwezi sasa.”

MIMI: “Kwahiyo umekubali kutoa tunda sahivi… safi sana.”

Lucy alicheka sana na akaishia kunisikitia kwa pamoja;

LUCY: “Ila Insider.”

MIMI: “Ee! Usimkazie sana mwanangu hiyo kitu, haondoki nayo.”

LUCY: “Aya bhana, tuachane na hayo. Hebu niambie, umetumia mbinu gani hadi Hilda akarudi ofisini? Leo yuko na furaha kama zote.”

MIMI: “Nilikwambia suala la Hilda niachie. I told you I know how to deal with her and I did.”

Lucy akatikisa kichwa kwa mshangao.

LUCY: “Mmh! Aisee sawa baba. Mimi sina usemi, ila kwa hili umetisha sana nakupa nyota tano.”

Nikiwa bado nazungumza na Lucy, Hilda alitoka nje na kusimama kibarazani, akituangalia tukiongea. Baada ya kumaliza mazungumzo yangu na Lucy, nilimpa ishara ya mkono wa heri, naye akanijibu kwa kunipungia mkono. Kisha nikaondoka kuelekea Kariakoo dukani kuangalia maendeleo ya biashara.

Nilipofika dukani, kama ilivyokuwa kawaida, Vicky alikuwepo na akanieleza kuwa biashara inaendelea vizuri. Nilikaa dukani hadi muda wa kufunga, ndipo nikaondoka na Vicky. Nilimpa lift hadi Mbezi Beach, ambako alishuka na kupanda daladala ya kuelekea Mbweni.

Niliporejea nyumbani niliishia nje getini, nilipiga simu South Africa kufuatilia hali ya mwanangu Aria. Simu ilipokelewa na Samantha, ambaye alinieleza kuwa Aria yuko vizuri na kwamba wanasubiri kauli ya daktari ili kujua kama wanaweza kuruhusiwa kuondoka au la. Baada ya mazungumzo marefu, nilimwambia amsalimie mke wangu na amwambie kuwa nime-mmiss sana. Samantha alibaki akicheka, akasema haina shida salamu zimefika, nami nikakata simu.

Nilipoingia sebuleni, nilimkuta mama J akiwa amekaa na mgeni, ambaye ni dada yake mkubwa. Tulisalimiana kwa furaha, kisha tukaendelea na mazungumzo ya hapa na pale kuhusu maisha. Shem wangu alilalamika kwa utani mzito kuwa nimewatupa sana, maana ilikuwa muda mrefu sijaonekana kwao.

Aliniambia amekaa sana, hivyo nimekuja muda ambao anataka kuondoka ili awahi kurudi nyumbani. Nikasimama nikapendekeza tuondoke ili nimpe lift hadi Mbezi kwa Zena, kisha hapo tungetafuta Uber ya kumrudisha nyumbani.

Tuliondoka wote na njiani tuliendelea kuzungumza mambo mengi sana , pia alinishirikisha mpango wake wa kufungua biashara hivi karibuni. Nikaendelea kumtania ni lini atahama nyumbani akaanze kujitegemea, naye akajibu kwa kicheko kuwa ataondoka kwao siku ya ndoa tu.

Huyu alikuwa ni dada wa kwanza kabisa wa mama J, na licha ya kuwa na kazi nzuri bado aliishi nyumbani. Sikushangaa sana, maana nilimfahamu baba mkwe wangu kuwa ni mtu makini na mkali kidogo kwa binti zake. Hata mimi, kipindi nilipompa mimba mama J, alinipa presha ya kutosha.

Tulipofika kwa Zena, nilimwambia arequest Uber ya kumrudisha nyumbani, nikampa nauli, kisha mimi nikaelekea Shoppers kununua vinywaji. Lengo langu lilikuwa ni kukaa na mama J, tuzungumze mambo ya kifamilia, kumtuliza kwa yaliyotokea jana, na pia kuimarisha ukaribu wetu. Dada yangu alikuwa amenisisitiza sana niwe karibu na mama J, na ikiwezekana nimpe mapenzi ya kutosha ili asipate nafasi ya kunichunguza au kufuatilia mambo yangu.

Niliporudi nyumbani, nilitoa viti na meza nikapanga nje bustanini kwa mpangilio mzuri. Kisha nikamwita mama J tukae tuzungumze. Alishangaa sana kwa kitendo kile, kwa sababu ilikuwa mara ya kwanza kufanya hivyo tangu tuhamie pale. Alikuwa surprised kweli, lakini tabasamu lake lilionyesha alifurahia.

Nikaanza kwa upole:

MIMI: “Leo ungependa kunywa kinywaji gani mke wangu? Agiza chochote, ila isiwe pombe kali. Niko na stock ya kutosha.”

Vinywaji vyote vilikuwa vimepangwa pale nje, naye alibaki akinitazama kwa mshangao huku akitabasamu.

WIFE: “Leo umepatwa na nini?”

MIMI: “Siku moja moja tunatakiwa kukaa hivi, tu-enjoy.”

WIFE: “Eeh! Kuna vinywaji gani hapo?”

MIMI: “Wewe tu! Hapa kuna Moët na wine.”

Mazungumzo yalianza rasmi ambapo nikaanza kumuuliza kuhusu biashara zake na kama ana changamoto zozote. Aliniambia kwa sasa biashara zinaenda vizuri na hana changamoto yoyote kubwa.

Nikahamia kwenye mipango yake ya baadaye.

MIMI: “Vipi ule mpango wako wa kununua gari ulliyeyuka hewani?. Nataka nikusupport Pesa ya clearing.”

WIFE: “Kuna pesa naisubiria, lakini kama uko tayari kunisupport clearing, niagize gari kupitia hiyo hela. Kufikia linafika bandarini nitakuwa nimeshapata pesa ya clearing.”

MIMI: “Hakuna shida, na unataka gari gani?”

WIFE: “Nataka gari isiyo na mambo mengi-IST itanitosha.”

MIMI: “Umekosa gari ya kununua hadi ukaishia IST?”

WIFE: “Leo umepata gari kali unasahau ulikotokea na IST hadi kukufikisha hapa. Mimi nataka gari ya kawaida tu kwa ajili ya delivery na mishe mingine. Tuna mpango wa kufungua biashara ya bakery mimi na dada yangu. Leo tumepanga bajeti na mahitaji yote muhimu.”

MIMI: “Shem alinigusia ana mpango wa kufungua biashara, lakini hakusema kama ni ubia.”

WIFE: “Ndio hivyo. Mungu akijalia, mwezi ujao tunaanza.”

Wakati mazungumzo yanaendelea, nilikuwa nikifungua tovuti mbalimbali. Tukaingia BeForward, tukaangalia magari kadhaa, kisha tukapitia na websites nyingine. Tulipofika Enhance Auto, ndipo tukakutana na IST moja kali sana. Ilimvutia sana, akaipenda papo hapo, lakini gharama yake ilikuwa juu kidogo. Nikamwambia aniachie mimi, nitabargain na wao na tukifikia muhafaka nitailipia.

Baada ya kumaliza suala la gari, mama J alihamia kwenye mada ya kampuni. Alitaka kufahamu taarifa za Directors wa kampuni, hasa kwa sababu nilisajili kampuni bila yeye kushirikishwa. Kwa utulivu, nilimkumbusha kuwa kipindi hicho tulipokuwa tunaandaa usajili wa kampuni, hatukuwa kwenye maelewano mazuri, na ndipo mama yangu alichukua nafasi ya kuwa mkurugenzi.

Nilimtoa hofu kwa kumhakikishia kuwa nitafanya marekebisho ya taarifa za kampuni, nitamuweka kama Director na kumpa hisa asilimia 50. Pia nilimweleza kuwa biashara zake zote zingehamishiwa chini ya kampuni ili ziendeshwe kwa pamoja.

Niliendelea kumhakikishia kuwa sina mwanamke mwingine zaidi yake, na kwamba sijawahi kuona mwanamke kama yeye maishani mwangu. Nilimuomba awe na subira kuhusu suala la ndoa, nikimweleza kuwa ninaandaa mpango wa kufunga ndoa nzuri na ya heshima, lakini kwa sasa kuna masuala muhimu ya shule yanayohitaji kukamilika kwanza. Nilimthibitishia kuwa ndoa ipo na itafungwa kwa wakati wake.

Tulizungumza mambo mengi sana, tukapanga mipango ya pamoja, na muda uliposonga tukaingia ndani chumbani kuendelea na maongezi mengine ya vitendo kitandani.

Asubuhi ilipofika, niliamka mapema kujiandaa kwenda kanisani, nikamwamsha mama J ili tuondoke pamoja. Alionekana kuchoka sana na hakuwa tayari kwenda, lakini nilisisitiza kuwa tuondoke kama familia. Tulielekea kanisani pamoja, na siku hiyo niliitumia kama muda wa kutafakari, kuomba msamaha, na kujiweka sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya kutoka kanisani mchana, nilipokea simu kutoka kwa mama Aria. Mazungumzo yetu ya kwanza yalihusu afya ya mwanangu Aria. Alinieleza kuwa maendeleo yake ni mazuri na waliruhusiwa kurudi nyumbani tangu usiku uliopita. Nilimuomba radhi kwa kushindwa kupokea simu zake siku ya Ijumaa, na tukaendelea na mazungumzo mengine.

Mazungumzo yetu yakahamia kwenye suala la kwenda nyumbani kwetu ili awafahamu wazazi wangu. Alitaka kujua hatua niliyofikia, hasa ikizingatiwa kuwa muda ulikuwa unaenda na Desemba haikuwa mbali.

Nilimweleza kuwa hilo ni suala nyeti linalohitaji busara kubwa, na kwamba nilihitaji kulishughulikia taratibu kwa wakati muafaka ili kuepuka mtafaruku. Hata hivyo, nilimhakikishia kuwa nitalifanyia kazi kama nilivyoahidi, maana ni haki ya mtoto wetu kuwafahamu babu na bibi yake. Alisikiliza kwa utulivu na kusema kuwa muda utafika na ataninikumbusha ahadi zangu.

Baada ya mazungumzo marefu, tuliagana, nami nikabaki nikitafakari kwa kina. Ukweli ni kwamba hili lilikuwa mojawapo ya masuala niliyokuwa nikiyakwepa sana, kwa sababu nilijua ndani yangu kuwa bado sikuwa nimechukua hatua yoyote ya maana.

Suala la kuwajulisha wazazi wangu kuhusu mtoto na mama yake lilinipa msongo mkubwa wa mawazo. Sikuwa najua nianzie wapi wala watalipokeaje. Mawazo yalikuwa mengi, majibu hayakuwepo.

Jioni, Bob alinipigia simu kunijulia hali na pia akanieleza kuwa yeye na Lucy walikuwa wamerudiana. Nilifurahi kusikia hilo, maana hata Lucy alionekana kuwa na furaha kazini tofauti na kipindi walipokuwa wamegombana.

Nilimuuliza swali la kizushi;

MIMI: “Vipi umekula mzigo?”

BOB: “Hapana kaka, bado naenda naye taratibu kumbuka ulinishauri hivi kaka.”

Nilicheka kwa sauti kubwa sana;

MIMI: “Lucy kafanikiwa kukukamata, huna ujanja wewe fala.”

BOB: “Hapana kaka sitaki kurush mambo, Lucy yuko serious sana.”

MIMI: “Lucy sio bikra utambue hilo, kama hakupi yeye anamaliza vipi shida zake? Kuna bwege anapewa halafu wewe husband material unazungushwa, dadeki.” Niliamua kumchana ukweli.

BOB: “Insider acha us**nge bhana, sidhani kama Lucy anaweza kufanya hivyo.”

MIMI: “Nisikilize, najua hupendi kuambiwa ukweli, wewe muulize haya maswali Lucy. Moja, shida zake anamalizia wapi?, pili, anampango wa kukupa tunda lini?, na tatu Je anakuamini?”

BOB: “Bro huko nitafika mbali sana, sasa unanishauri nini?.”

MIMI: “Kaka sisi ni wanaume kuna mambo lazima tuambiazane ukweli. Lucy ni mshikaji wangu sana tambua hilo, lakini anazingua. Mimi nakushauri fanya hivi, kama kweli unampenda tafuta demu pembeni wa kupunguza arosto. Au kama vipi unaweza kumpiga chini mazima ukatafuta mwanamke mwingine, machaguzi ni yako kaka.”

BOB: “Kaka unanishauri nimuache?.”

MIMI: “Sasa kuna haja gani ya kuwa na mahusiano na mtu ambaye hakupi tunda na sio bikra, camon man. Ndomana nimekupa option mbili wewe chagua moja hapo, ila hakikisha unamuuliza hayo maswali 3.”

BOB: “Bro hapo kwenye kumuacha hapana aisee!”

Nikamkatisha pale;

MIMI: “Bro tuachane na hii mada, leo ndo nimejua kwanini Lucy anakusumbua. Kumbe ushamba wako wa wanawake bado hujaacha tangu tuko jeshi.”

Bob aliishia kucheka na akakata simu pale na mimi niendelea kutafakari yale maongezi na sikutegemea kuona Lucy akimsumbua Bob kwa namna ile. Mwisho niliona ni bora kuwaacha waendelee na mahusiano yao maana hayanihusu.

Niliamua kuondoka na Junior kwenda Mlimani City ili kupoteza muda kidogo, huku yeye akipata nafasi ya kucheza na watoto wenzake. Nilishiriki naye kwenye michezo mbalimbali kama baba, jambo lililomfanya afurahi sana. Ilipofika saa mbili usiku, tuliamua kuondoka na kurejea nyumbani, maana alikuwa amechoka sana kutokana na michezo na pilikapilika za siku nzima.
*********
Wiki mpya ya mwezi wa kumi ilikuwa imeanza. Jumatatu asubuhi na mapema, baada ya kumaliza jogging, nilienda moja kwa moja ofisini. Jambo la kushangaza ni kwamba tangu ni sex na Hilda, hatukuwa tena na mawasiliano yoyote hakunitafuta wala mimi sikumtafuta.

Hii wiki nzima kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, Hilda asingekuwepo ofisini, kwani kulikuwa na semina ya wanawake ambako alikuwa akiiwakilisha kampuni.

Majira ya saa tano asubuhi, Sanchi alinipigia simu na kuniarifu kuwa amepigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Erica, aliyetoa taarifa kuwa angefika ofisini siku hiyo. Nikakumbuka sikuwa nimemjulisha Sanchi kuhusu ugeni huo, hivyo nikamtoa wasiwasi kwa kumwambia kuwa huyo dada ni familia na ampe ushirikiano wa kutosha.

Baada ya kumaliza mazungumzo na Sanchi, nilijikuta nikitafakari kwa kina kuhusu hatima yake ndani ya kampuni. Alikuwa anajituma sana, na kwa dhati nilitamani kumpa hata asilimia 10 ya hisa za kampuni. Baada ya kufikiria kwa makini, nikaona ni busara zaidi nimteue rasmi kuwa Secretary wa kampuni na nianze kumlipa mshahara stahiki.

Jumatano jioni, nilikuwa Mikocheni @theWheel, nikisubiri gari langu likifanyiwa service. Ghafla simu yangu ikaanza kuita, nilipoitoa mfukoni, nikaona ni Iryn aliyekuwa anapiga. Nilipokea bila kusita, lakini kwa mshangao sauti niliyoisikia haikuwa ya Iryn bali ilikuwa ni ya Samantha.

Tangu aanze kuzungumza, ilionekana wazi kabisa kuwa mambo hayakuwa sawa. Sauti yake ilikuwa nzito, ikibeba hofu na wasiwasi mkubwa. Akanijulisha kuwa dada yake, Iryn, alikuwa anaumwa sana na tayari amelazwa hospitali tangu jana usiku. Kwa mujibu wa alivyoniambia, hali yake haikuwa nzuri kwa wakati huo.

“Shida ni nini?”

“Dada Vivian ndiye anayejua kila kitu.”

“Na vipi kuhusu Aria?”

“Aria amelala, lakini yuko sawa, hana tatizo.”

“Okay shem, ahsante kwa taarifa. See you soon.”

Baada ya simu kukatika, nilihisi uchungu mkubwa moyoni mwangu kwa kipindi kigumu walichokuwa wakikipitia. Sikujiona nina option nyingine zaidi ya kuondoka kuelekea South Africa. Kilichokuwa kinanitatiza zaidi ni kuelewa kwa nini Iryn na Aria walianza kuumwa tangu walipotoka kwa baba yao.

Nikamwambia Kalanje, mmoja wa jamaa zangu pale @thewheel, nikamwomba aharakishe service ya gari langu kwa sababu nilikuwa nimepatwa na dharura na nilihitaji kusafiri haraka. Wakati huohuo, nikaanza kuwasiliana na agent ili anitafutie tiketi ya kwenda South Africa.

Baada ya dakika kumi tu, gari lilikuwa tayari. Nikaanza safari ya kurudi nyumbani ili kujiandaa kwa safari ya South Africa. Nikiwa njiani, simu ya Dullah ikaingia. Niliipokea na kuiweka kwenye loudspeaker, tukaanza mazungumzo.

MIMI: “Senior vipi kaka?”

DULLAH: “Aisee poa chief. Upo pande zipi? Kuna sehemu nataka twende.”

MIMI: “Kaka, nimepigiwa simu kuwa mama mtoto anaumwa kule South Africa. Mtoto alianza kuumwa, akalazwa, na sasa ni yeye mwenyewe. Hapa naelekea nyumbani kujiandaa niondoke.”

DULLAH: “Pole sana kaka. Ningependa sana kukupa kampani ndugu yangu, ila kwa sasa hali yangu ya kifedha sio nzuri.”

MIMI: “Uko tayari kwenda nikulipie nauli?”

DULLAH: “Ndio kaka, niko tayari kukupa kampani.”

MIMI: “Sawa basi, nenda kajiandae, tuondoke wote.”

Baada ya kuagana na Dullah, kulikuwa na jambo moja tu muhimu la ku-takecare. Sikujua nitawezaje kulitatua, na ndilo lililoanza kunisumbua sana akili yangu.
 
SEASON 03
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
CHAPTER 16

Ukweli ni kwamba nilibaki nimesimama kama nimerogwa nilipousoma ule ujumbe, nilipigwa na butwaa. Sikuamini kabisa nilichokiona, wala sikutarajia hata kidogo kwamba Hilda angefikia hatua ya kuchukua uamuzi mzito kiasi kile, ilikuwa nje ya mawazo yangu.

What the fck!* Ndani ya sekunde chache, lawama zote nilijipa mimi. Nilianza kujilaumu kwa nini nilichelewa kumtafuta, kwa nini nilishindwa kumaliza tofauti zetu mapema. Moyoni nilijua wazi kabisa chanzo kikubwa cha haya yote ni mimi kushindwa kumpa Hilda ile attention aliyokuwa akiihitaji.

Nilijiuliza pale nafanya nini sasa? Maana
Sikuona njia nyingine zaidi ya kwenda kwake. Nilijua lazima atakuwa nyumbani, hasa ukizingatia muda haukuwa umeenda sana tangu aondoke ofisini. Bila kufikiri mara mbili, niliwasha gari na kuondoka kwa fujo pale ofisini.

Njiani, mawazo yalikuwa yanapishana kichwani. Nilijisemea, naenda kumpa Hilda anachotaka, lakini siyo kumuacha aondoke, hasa kwenye kipindi hiki ambacho namuhitaji sana ofisini.

Haikuchukua muda mrefu nikawa tayari nimefika kwenye apartment yake, sikumpa taarifa yoyote ya ujio wangu. Nilipaki gari nje ya uzio, nikasogea getini na kugonga. Bahati nzuri, jirani yake ni dada aliyekuwa anafua nguo alinifungulia geti.

Baada ya salamu chache, nilienda moja kwa moja hadi kwenye mlango wa apartment ya Hilda na kugonga. Kulikuwa na ukimya wa sekunde kadhaa, kisha nikasikia mlango unafunguliwa. Alishtuka kuniona, alibaki amesimama akinitazama, ugeni wangu haukuwa kwenye matarajio yake.

“Ooh! Insider… karibu sana.”

Sikujibu chochote na ilimtazama tu, kisha nikaingia moja kwa moja sebuleni. Mezani kulikuwa na nyaraka kadhaa, na nilianza kuzipekuapekua bila hata kuuliza, mpaka nikajikuta nimeshika CV yake mkononi na kuisoma.

MIMI: “Ninaona umeanza kuandaa documents za ofisi mpya. Hilda, kwa nini unaacha kazi hasa kwenye kipindi hiki ambacho nakuhitaji? Tafadhali niambie, kuna kitu ofisi imekutreat vibaya?”

Hilda alinyamaza kimya kwa sekunde kadhaa kabla hajajibu..

HILDA: “Hapana, nimeamua tu kubadili mazingira ya kazi. Samahani sikutoa taarifa mapema.”

Nilisimama kutoka nilipokuwa nimekaa, nikamkaribia na kushika mikono yake yote miwili, na nilimtazama machoni.

MIMI: “Acha kunidanganya bhana sababu kuu unaondoka ni mimi. Tangu turudi Zanzibar hujawahi kuwa sawa. Ndiyo maana nimekuja hapa uniambie unataka nikufanyie nini?”

HILDA: “No! No! Noo! You are not the reason it happened.”

Lakini mwili wake ulikuwa unasema kitu tofauti, nilimshika kiunoni taratibu, nikamsogeza karibu yangu. Hakunipa upinzani wowote na ukimya wake ulikuwa mzito kuliko maneno. Nilimvuta kwangu, nikambana vizuri, nilihisi joto lake la asili na nikaanza kupapasa hips zake taratibu. Alianza kuhema kwa shida huku akitoa sauti ya chini na miguno..

“Insider please, niache.”

Na alianza kujinasua kutoka kwenye mikono yangu na mimi nikamuachia kwa muda. Alianza kuelekea chumbani, nikamfuata kwa nyuma kisha nikamvuta tena na kumpa tongue akapokea kwa pupa. Baada ya kuona sipati tena upinzani na akitoa ushirikiano nikaanza kutalii maeneo mengine ya hifadhi ya Serengeti. Ukweli nilianza kupagawa na maajabu niliyokuwa nina yaona kwenye ile mbuga, nilikuwa nashuhudia uumbaji wa dhahabu uliotukuka.

Hilda alikuwa na pupa ya ajabu, kiasi kwamba alikuwa akisubiri kwa muda mrefu. Ndani ya muda mfupi, hisia zilikuwa zimeshachukua usukani, alikuwa chapachapa tayari kwa kuanza safari ya kwenda dunia nyingine ya mahaba. Ilikuwa ni burudani ambayo ilichukua muda mrefu sana kabla ya kupitiwa na usingizi fofofo.

Nilipozinduka, kichwa kilikuwa kizito, macho yakiwa bado hayajakaa sawa. Nilipochukua simu ndipo mkanganyiko ulipoanza rasmi, saa ilikuwa ikisoma ni saa 8 kasoro za usiku. Kwenye screen, kulikuwa na msururu wa missed calls za kutosha kutoka kwa Mama J, na kutoka kwa Iryn. Jambo la kunishtua zaidi, karibu wanawake wote waliokuwa sehemu ya maisha yangu kipindi hicho kuanzia Erica, Ghati na Prisca walikuwa wamepiga simu pia.

Moyo ulianza kwenda mbio na mapigo ya moyo yakibadilika;

Nilifungua ujumbe mmoja kutoka kwa Mama J. Ulikuwa mfupi lakini mzito:

“Baba J, hivi kwanini unapenda kuniumiza moyo wangu? Kama hao wanawake unaona ni wa muhimu, kwanini usiishi nao?”

Nilikaa kimya nikitazama screen kwa sekunde kadhaa. Swali moja tu lilikuwa likinipiga kichwani-imefikiaje nimelala hadi muda huu? Mara ya mwisho niliangalia saa ilikuwa ni saa tano usiku. Nilikuwa nimepanga kupumzika kidogo tu kwa sababu ya uchovu wa sex, halafu ningeondoka. Kuja kuamka saa nane kasoro za usiku kuliniacha nikiwa nimeshikwa na butwaa kabisa, sikuelewa hata kidogo kilichotokea.

Hilda alikuwa kalala uchi fofofo na muda huu nilianza kuview nyashi yake vizuri maana alikuwa kalalia tumbo. Pale kitandani palikuwa pa hovyo sana, maana shuka lilikuwa limelowa kila sehemu. Nilianza kufikiri kama naoga au laah! Na kuondoka bila kuoga ingekuwa ajabu ukizingatia harufu ya sex ilikuwa imenitapakaa.

Hilda aliamka pale, aliniita kwa sauti ya uvivu,

“Insider…”

Alinisogelea na kuanza kunipapasa mgongoni polepole.

HILDA: “Kwa nini unaondoka? Nilidhani tunalala pamoja.”

Nilimwambia huku nikimuonyesha simu;

MIMI: “Hilda, ni saa nane sasa, hata sielewi nimelalaje. Angalia hizi missed calls za wake zangu.”

Hilda naye kwa upande wake alibaki akishangaa jinsi muda ulivyokwenda na alianza kutoa shuka pale kitandani;

HILDA: “So what are you doing?”

MIMI: “Naondoka narudi nyumbani.”

HILDA: “Basi kaoge kwanza.”

MIMI: “Najifikiria hapa kuhusu kuoga, humjui Mama Junior wangu vizuri. Yule mwanamke ni mpekuzi sana akigundua nimeoga usiku huu, atajua nimetoka kwa mwanamke mwingine.”

Niliamua kuingia bafuni na badala yake niliishia kunawa na kujifuta kwa taulo vizuri, kisha nilimuaga Hilda naye akatoka kunisindikiza hadi nje getini.

Njiani kurudi nyumbani, mawazo yangu yalikuwa hayakai sehemu moja maana kila kona ya barabara ilinirejesha kwa Iryn. Simu zake za mara kwa mara zilinipa ishara kuwa huenda alikuwa na tatizo, labda alihitaji msaada wangu. Lakini kwa wakati ule, sikuwa na nguvu ya kumpigia sababu ulikuwa ni usiku sana, pia ningeweza kutengeneza matatizo mengine.

Nilikuwa nakiendesha gari kwa spidi kuliko kawaida. Nilipofika mitaa ya Mikocheni, karibu na Palm Village, wazo moja lilinijia ghafla la kununua bia. Nilihitaji kuonekana kama nimetoka kunywa, labda hiyo ingetengeneza mazingira fulani kwa wife.

Nikasimama pale Triple 7, nikanunua Heineken mbili. Nilipofika nyumbani, sikuharakisha kuingia, nilibaki nje ya geti, nikafungua chupa moja na kuanza kuinywa polepole hadi ikafika nusu. Ndipo nikaingiza gari ndani na kuingia sebleni nikiwa na chupa mkononi.

Namkuta sebleni Mama J alikuwa amelala kwenye sofa, amejifunika kwa mtandio mwepesi. Nilisimama kidogo nikimtazama, nilijiuliza pale nimuamshe au niende kuoga kwanza?. Ukweli ni kwamba sikuwa comfortable hata kidogo, kile kilichotokea kwa Hilda kiliniacha nikiwa na hisia nzito, na hata kuwa karibu na mke wangu sikuwa natamani.

Lakini nilijua pia kumuacha pale na kwenda chumbani kuoga kungezaa matatizo zaidi. Hivyo nikaamua ni bora nimuamshe, angalau tuzungumze. Niliketi kwenye mkono wa sofa, nikasogea karibu naye, nikamuita kwa sauti ya upole iliyochanganyika na uigizaji;

“Swahiba… baby…”

Mama J aliamka na kukaa huku akiniangalia kwa macho makali sana, na mimi nikaendelea kupretend kama nimelewa;

“Mke wangu nimekuletea na wewe bia unywe maana najua una kiu.”

Alininyang’anya ile chupa na kuiweka mezani, na akaanza kuongea pale;

“Baba J ndo nini hivi unanirudia usiku wa manane na umelewa, kwanza ulikuwa wapi na nani?”

“Hahahaa! Nilikuwa na walevi wenzangu ambao wake zetu wanatupa stress, wacha me nikalale.”

Nikaanza kusogea kuelekea chumbani, nikijaribu kukwepa mazungumzo zaidi. Sauti ya wife ikanifatia nyumba;

“Baba J shenzi.”

Baada ya kufika chumbani niliingia bafuni kuoga chap na ile natoka nakuta amekaa kitandani.

“Our conversation is not over yet, ulikuwa wapi usiku wote huu na simu zangu hupokei.”

“Swahiba mimi nimechoka sana hata sikuelewi, kesho bhana.”

Mimi nilipanda kitandani kulala na yeye aliendelea kukaa pale kitandani na alionekana akitafakari mambo.

Baada ya kuamka ile asubuhi, mawazo yangu yalirudi moja kwa moja kwa Hilda na kile kilichotokea usiku uliopita. Nilijikuta nikirejea tukio hilo hatua kwa hatua, nikitafakari kila kilichofanyika usiku wa jana. Kadiri nilivyozidi kukumbuka, ndivyo nilivyozidi kujiridhisha kuwa ilikuwa ni halali kulala vile.

Maneno ya Hilda nayo yakaanza kunirudia akilini. Mara nyingi alikuwa akiniambia kuwa kwa muda mrefu amekuwa single. Sikuwahi kuyaamini maneno hayo, moyoni nilijua kuna kitu alikuwa ananificha. Lakini baada ya yale yaliyotokea, nilijikuta sina budi ila kuyaweka maneno yake katika mizani mpya ya ukweli.

Ukweli sisi wanaume huwa tunamtambua mwanamke ambaye hajaguswa kwa muda mrefu wakati wa tendo. Sasa kipindi naingiza gari yangu uwanja wa mapambano kwa mara ya kwanza, licha ya barabara kuwa safi na kumwagiliwa vizuri. Lakini bado nilipata shida sana kuingia, pia alikuwa akilalamika mno.

Niliendelea kulifikiria tukio hilo kwa muda, lakini sikutaka kujilaumu kupita kiasi. Nilijipa sababu zangu kuwa nilifanya kwa maslahi ya kampuni, na kwa kufanya hivyo, niliamini nisingempoteza Hilda. Hata hivyo, swali moja zito lilibaki likining’inia akilini mwangu, What is next?.

Niliingia bafuni kuoga, wakati najiandaa kutoka, wife aliingia chumbani na bila kupoteza muda akaanzisha mazungumzo yale yale tulipoishia niliporudi nyumbani usiku.

MAMA J: “Baba J, naomba uniambie kwa nini ulikuwa hupokei simu zangu. Ulikuwa na nani?”

Nikavuta pumzi kidogo kabla ya kujibu.

MIMI: “Nilisahau simu kwenye gari, na lilikuwa mbali.”

Alinitazama kwa jicho la kutoamini.

MAMA J: “Una maana gani? Na ulikuwa na nani?”

MIMI: “Nilikuwa na Dullah.”

MAMA J: “Mpigie simu niongee naye.”

MIMI: “Uongee naye nini?”

MAMA J: “Ni-confirm kama mlikuwa wote. Mimi nachojua jana ulikuwa na mwanamke mwingine.”

MIMI: “Kama ningekuwa na mwanamke mwingine, ningerudi hapa home kweli? Si ningetafuta sababu ya kukudanganya na kutorudi?”

Alinisogelea kidogo.

MAMA J: “Call him, please.”

MIMI: “You already know I can’t do that, hata Dullah atanidharau. Yaani nianze kumpigia Dullah na umuulize ujinga wako? You can’t be serious.”

Nikafungua droo kuchukua funguo ya gari niondoke, lakini sikuiona nilijua wazi lazima atakuwa nayo.

“Naomba funguo yangu ya gari, please.”

MAMA J: “Junior anayo seblen.”

Nilihisi hasira ikipanda.

MIMI: “Ulienda kukagua gari yangu? Bila shaka hata bia yangu utakuwa umenisaidia kuitoa.”

Alinisonya kwa sauti ya juu, lakini mimi hata sikujali nikaondoka.

Nilianza safari kuelekea Masaki. Njiani, Lucy alinipigia simu akiniomba nimpitie pale Mwenge. Wakati huohuo, nilimpigia Iryn mara tatu mfululizo, lakini hakupokea nikapanga nitamtafuta baadaye.

Baada ya kumchukua Lucy, tuliendelea na safari ya Masaki. Mazungumzo yakageukia moja kwa moja kwenye suala la Hilda.

LUCY: “Manager, Hilda amekutaarifu kuwa ameacha kazi?”

Nilicheka kidogo.

MIMI: “Hilda hawezi kuacha kazi kirahisi bhana.”

Lucy alinitazama kwa makini.

LUCY: “Kanitumia message kuwa ameacha kazi. Nilimpigia hapokei, na wewe pia ulikuwa hupokei simu.”

Nikataabasamu kimoyomoyo, nikikumbuka kuwa muda ule mimi na Hilda tulikuwa kwenye dunia nyingine kabisa.

MIMI: “Hilda hajaacha kazi, trust me.”

LUCY: “Insider, unachukulia mambo simple sana. Kama kweli Hilda ameacha kazi, ni kwa uzembe wako.”

MIMI: “So ulitaka nimtongoze kama yeye anavyotaka?”

LUCY: “Hiyo sio concern yangu ila ungeweza kukaa naye chini mkamaliza tofauti zenu. Wewe ni meneja you know how to handle all this bullshit.”

MIMI: “Kama Hilda kaacha kazi, tutaajiri mtu mwingine mwenye uzoefu. Asijifanye yeye ni mkubwa kuliko kampuni.”

LUCY: “Duuh!”

Tulipitia sehemu tukasimama kunywa supu kidogo, kisha tukaelekea moja kwa moja ofisini. Tulipofika na kuingia ofisini, Lucy alisimama ghafla, macho yake yakatanuka kwa mshangao. Hilda alikuwa amekaa kwenye kiti chake, tena akiwa na tabasamu pana usoni-alionekana mwenye furaha isiyo ya kawaida. Nikavunja ukimya.

MIMI: “Hilda mambo! Lucy alikuwa ananiambia eti umeacha kazi.”

Hilda akatabasamu kwa kujiamini kidogo.

HILDA: “Lucy siwezi kuacha kazi bhana.”

Lucy akatikisa kichwa kwa tabasamu la kushangaa.

LUCY:” Nimefurahi kukuona, maana njiani kote nilikuwa ninagombana na Insider kuhusu wewe.”

HILDA: “Nipo dear, siwezi kuwaacha kizembe.”

Lucy akaniangalia kwa macho yaliyokuwa yamejaa maswali kama mtu ambaye bado hajaridhika na majibu aliyopata. Ilikuwa wazi anahisi kuna mkono wangu umehusika katika kurudi kwa Hilda, lakini hakuwa na pa kuanzia kuniuliza. Baada ya sekunde chache za ukimya, aliaga akisema anaenda kuonana na mteja wake, akatuacha mimi na Hilda ofisini.
Hilda akavunja ukimya kwa sauti ya chini.

HILDA: “Niliogopa hata kukupigia simu muda ule. Nilikuwa na imani kila kitu kilienda sawa na wife.”

MIMI: “Yeah, but anahisi nilikuwa na mwanamke mwingine. Tuachane na haya, unaonekana mwenye furaha sana leo, siri ni nini?”

Hilda akacheka kidogo kwa aibu, macho yakikwepa yangu, hakusema neno.

“Nimefurahi kukuona ofisini. You look so beautiful.”

Hilda akatabasamu kwa upole.

HILDA: “Thank you, Insider.”

Nilihisi wazi kwamba alikuwa ameanza kunionea aibu. Alikuwa kama mtu aliyepoteza kujiamini kidogo, tofauti kabisa na Hilda niliyemzoea. Kabla sijaongeza neno lingine, simu yangu ikaingia, ilikuwa ni video call kutoka kwa Iryn. Nikatoka nje haraka kwenda kuipokea;

MIMI: “Baby, I’m really sorry for…”

Hakunipa nafasi ya kumaliza.

IRYN: “Hivi baba Aria una shida gani? Jana nimeanza kukutafuta kuanzia saa 1 usiku hadi saa 5 usiku hupokei simu zangu. Halafu bila mimi kukutafuta, hujali hata kupiga simu kujua maendeleo ya mwanao. Aria ni mtoto wako wa damu usipomjali, unataka nani amjali?”

Nilihisi uchungu na hasira iliyochanganyika na maumivu ikimtoka moyoni, nikajaribu kumtuliza.

MIMI: “Baby, sorry jana…”

Akanikatisha tena.

IRYN: “Jana nilikupigia simu kukupa taarifa kwamba Aria anaumwa. Nimeshinda naye hospital tangu jana usiku, hadi sasa bado tuko hospital.”

Maneno hayo yalinichoma moyo, nilinyamaza kwa sekunde kadhaa kabla ya kuzungumza.

MIMI: “Aria anaumwa nini, baby?”

IRYN: “Insider, am not okay, hata kuongea na wewe hapa najilazimisha.”

MIMI: “Pole sana, najua umechoka. Tafadhali mpe Samantha simu niongee naye kama yuko karibu.”

IRYN: “Okay.”

Samantha akapokea simu na kuniambia Aria ana homa kali, mafua makali, na alikuwa anatapika sana. Alijaribu kunituliza kwa kuniambia hali yake inaendelea kuimarika na kuna uwezekano wakaruhusiwa leo kama afya itaendelea kuwa vizuri.

Nilimuomba awe ananipa taarifa kupitia namba yake, lakini akasema atanipigia kupitia namba ya dada yake. Alisisitiza kuwa dada yake hajamruhusu kuwa na namba yangu, hivyo mawasiliano yatakuwa yakipitia kwake.

Baada ya kumaliza maongezi yetu, nilibaki na mawazo mengi kichwani. Kitendo cha Iryn kumzuia mdogo wake kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mimi kilinizingua sana. Nilishindwa kabisa kuelewa sababu yake ni nini. Je, alikuwa anaogopa nitamtongoza? Au kulikuwa na jambo jingine nyuma ya pazia? Maswali yalikuwa mengi, majibu hayakuwepo.

Kwa ujumla, maneno ya Iryn yaliniuma sana. Aliongea kwa uchungu mwingi, na ukweli ni kwamba alikuwa na haki ya kusema vile ukizingatia nilikuwa nimezembea kupita kiasi. Wakati wote huo ambao alikuwa ananipigia simu, mimi nilikuwa na Hilda tukipenzika.

Nilibaki pale kibarazani kwa muda, nikitafakari maisha yangu na mawazo yangu mengi yalikuwa yanamzunguka Hilda. Nilikuwa, bila hata kutarajia, nimeanza kufungua ukurasa mpya naye. Niliogopa sana na nilijiambia moyoni kwamba nisipokuwa makini, yale yaliyotokea kwa Asmah yanaweza kujirudia tena kwa sura ile ile.

Mawazo yangu yakakatizwa ghafla na simu iliyoingia kutoka kwa Erica Dodoma. Alinieleza kuwa Jumatatu angefanya visit ofisini, hivyo nilihitajika kuwapa taarifa wahusika wote watakaokuwepo. Nilimwambia nitamtumia namba ya mtu wa kuwasiliana naye atakayemwelekeza mpaka afike ofisini bila shida. Baada ya kukata simu, nikamtumia namba za Sanchi kama nilivyoahidi.

Jioni ilipowadia, nilijiandaa kuondoka kuelekea Kariakoo kuangalia maendeleo ya biashara dukani. Nilipokuwa natoka kuelekea eneo la maegesho ya magari, Lucy aliniita akionesha kuwa na jambo la kuzungumza. Nilimpa ishara anifate hadi parking ili tuweze kuzungumza kwa uhuru, naye akafanya hivyo.

Nilimwambia kuwa ninaondoka na kama kutakuwa na jambo lolote tunaweza kuonana Jumatatu. Wakati huo alikuwa akitabasamu sana. Nikachukua nafasi hiyo kumuuliza kuhusu maendeleo ya mahusiano yake na Bob. Alitabasamu tena kisha akaniambia kuwa wamerudiana na kwa sasa mambo yanaenda vizuri. Kwa kweli, zilikuwa habari njema sana kwangu.

MIMI: “Mna muda gani tangu mrudiane?”

LUCY: “Tunaenda mwezi sasa.”

MIMI: “Kwahiyo umekubali kutoa tunda sahivi… safi sana.”

Lucy alicheka sana na akaishia kunisikitia kwa pamoja;

LUCY: “Ila Insider.”

MIMI: “Ee! Usimkazie sana mwanangu hiyo kitu, haondoki nayo.”

LUCY: “Aya bhana, tuachane na hayo. Hebu niambie, umetumia mbinu gani hadi Hilda akarudi ofisini? Leo yuko na furaha kama zote.”

MIMI: “Nilikwambia suala la Hilda niachie. I told you I know how to deal with her and I did.”

Lucy akatikisa kichwa kwa mshangao.

LUCY: “Mmh! Aisee sawa baba. Mimi sina usemi, ila kwa hili umetisha sana nakupa nyota tano.”

Nikiwa bado nazungumza na Lucy, Hilda alitoka nje na kusimama kibarazani, akituangalia tukiongea. Baada ya kumaliza mazungumzo yangu na Lucy, nilimpa ishara ya mkono wa heri, naye akanijibu kwa kunipungia mkono. Kisha nikaondoka kuelekea Kariakoo dukani kuangalia maendeleo ya biashara.

Nilipofika dukani, kama ilivyokuwa kawaida, Vicky alikuwepo na akanieleza kuwa biashara inaendelea vizuri. Nilikaa dukani hadi muda wa kufunga, ndipo nikaondoka na Vicky. Nilimpa lift hadi Mbezi Beach, ambako alishuka na kupanda daladala ya kuelekea Mbweni.

Niliporejea nyumbani niliishia nje getini, nilipiga simu South Africa kufuatilia hali ya mwanangu Aria. Simu ilipokelewa na Samantha, ambaye alinieleza kuwa Aria yuko vizuri na kwamba wanasubiri kauli ya daktari ili kujua kama wanaweza kuruhusiwa kuondoka au la. Baada ya mazungumzo marefu, nilimwambia amsalimie mke wangu na amwambie kuwa nime-mmiss sana. Samantha alibaki akicheka, akasema haina shida salamu zimefika, nami nikakata simu.

Nilipoingia sebuleni, nilimkuta mama J akiwa amekaa na mgeni, ambaye ni dada yake mkubwa. Tulisalimiana kwa furaha, kisha tukaendelea na mazungumzo ya hapa na pale kuhusu maisha. Shem wangu alilalamika kwa utani mzito kuwa nimewatupa sana, maana ilikuwa muda mrefu sijaonekana kwao.

Aliniambia amekaa sana, hivyo nimekuja muda ambao anataka kuondoka ili awahi kurudi nyumbani. Nikasimama nikapendekeza tuondoke ili nimpe lift hadi Mbezi kwa Zena, kisha hapo tungetafuta Uber ya kumrudisha nyumbani.

Tuliondoka wote na njiani tuliendelea kuzungumza mambo mengi sana , pia alinishirikisha mpango wake wa kufungua biashara hivi karibuni. Nikaendelea kumtania ni lini atahama nyumbani akaanze kujitegemea, naye akajibu kwa kicheko kuwa ataondoka kwao siku ya ndoa tu.

Huyu alikuwa ni dada wa kwanza kabisa wa mama J, na licha ya kuwa na kazi nzuri bado aliishi nyumbani. Sikushangaa sana, maana nilimfahamu baba mkwe wangu kuwa ni mtu makini na mkali kidogo kwa binti zake. Hata mimi, kipindi nilipompa mimba mama J, alinipa presha ya kutosha.

Tulipofika kwa Zena, nilimwambia arequest Uber ya kumrudisha nyumbani, nikampa nauli, kisha mimi nikaelekea Shoppers kununua vinywaji. Lengo langu lilikuwa ni kukaa na mama J, tuzungumze mambo ya kifamilia, kumtuliza kwa yaliyotokea jana, na pia kuimarisha ukaribu wetu. Dada yangu alikuwa amenisisitiza sana niwe karibu na mama J, na ikiwezekana nimpe mapenzi ya kutosha ili asipate nafasi ya kunichunguza au kufuatilia mambo yangu.

Niliporudi nyumbani, nilitoa viti na meza nikapanga nje bustanini kwa mpangilio mzuri. Kisha nikamwita mama J tukae tuzungumze. Alishangaa sana kwa kitendo kile, kwa sababu ilikuwa mara ya kwanza kufanya hivyo tangu tuhamie pale. Alikuwa surprised kweli, lakini tabasamu lake lilionyesha alifurahia.

Nikaanza kwa upole:

MIMI: “Leo ungependa kunywa kinywaji gani mke wangu? Agiza chochote, ila isiwe pombe kali. Niko na stock ya kutosha.”

Vinywaji vyote vilikuwa vimepangwa pale nje, naye alibaki akinitazama kwa mshangao huku akitabasamu.

WIFE: “Leo umepatwa na nini?”

MIMI: “Siku moja moja tunatakiwa kukaa hivi, tu-enjoy.”

WIFE: “Eeh! Kuna vinywaji gani hapo?”

MIMI: “Wewe tu! Hapa kuna Moët na wine.”

Mazungumzo yalianza rasmi ambapo nikaanza kumuuliza kuhusu biashara zake na kama ana changamoto zozote. Aliniambia kwa sasa biashara zinaenda vizuri na hana changamoto yoyote kubwa.

Nikahamia kwenye mipango yake ya baadaye.

MIMI: “Vipi ule mpango wako wa kununua gari ulliyeyuka hewani?. Nataka nikusupport Pesa ya clearing.”

WIFE: “Kuna pesa naisubiria, lakini kama uko tayari kunisupport clearing, niagize gari kupitia hiyo hela. Kufikia linafika bandarini nitakuwa nimeshapata pesa ya clearing.”

MIMI: “Hakuna shida, na unataka gari gani?”

WIFE: “Nataka gari isiyo na mambo mengi-IST itanitosha.”

MIMI: “Umekosa gari ya kununua hadi ukaishia IST?”

WIFE: “Leo umepata gari kali unasahau ulikotokea na IST hadi kukufikisha hapa. Mimi nataka gari ya kawaida tu kwa ajili ya delivery na mishe mingine. Tuna mpango wa kufungua biashara ya bakery mimi na dada yangu. Leo tumepanga bajeti na mahitaji yote muhimu.”

MIMI: “Shem alinigusia ana mpango wa kufungua biashara, lakini hakusema kama ni ubia.”

WIFE: “Ndio hivyo. Mungu akijalia, mwezi ujao tunaanza.”

Wakati mazungumzo yanaendelea, nilikuwa nikifungua tovuti mbalimbali. Tukaingia BeForward, tukaangalia magari kadhaa, kisha tukapitia na websites nyingine. Tulipofika Enhance Auto, ndipo tukakutana na IST moja kali sana. Ilimvutia sana, akaipenda papo hapo, lakini gharama yake ilikuwa juu kidogo. Nikamwambia aniachie mimi, nitabargain na wao na tukifikia muhafaka nitailipia.

Baada ya kumaliza suala la gari, mama J alihamia kwenye mada ya kampuni. Alitaka kufahamu taarifa za Directors wa kampuni, hasa kwa sababu nilisajili kampuni bila yeye kushirikishwa. Kwa utulivu, nilimkumbusha kuwa kipindi hicho tulipokuwa tunaandaa usajili wa kampuni, hatukuwa kwenye maelewano mazuri, na ndipo mama yangu alichukua nafasi ya kuwa mkurugenzi.

Nilimtoa hofu kwa kumhakikishia kuwa nitafanya marekebisho ya taarifa za kampuni, nitamuweka kama Director na kumpa hisa asilimia 50. Pia nilimweleza kuwa biashara zake zote zingehamishiwa chini ya kampuni ili ziendeshwe kwa pamoja.

Niliendelea kumhakikishia kuwa sina mwanamke mwingine zaidi yake, na kwamba sijawahi kuona mwanamke kama yeye maishani mwangu. Nilimuomba awe na subira kuhusu suala la ndoa, nikimweleza kuwa ninaandaa mpango wa kufunga ndoa nzuri na ya heshima, lakini kwa sasa kuna masuala muhimu ya shule yanayohitaji kukamilika kwanza. Nilimthibitishia kuwa ndoa ipo na itafungwa kwa wakati wake.

Tulizungumza mambo mengi sana, tukapanga mipango ya pamoja, na muda uliposonga tukaingia ndani chumbani kuendelea na maongezi mengine ya vitendo kitandani.

Asubuhi ilipofika, niliamka mapema kujiandaa kwenda kanisani, nikamwamsha mama J ili tuondoke pamoja. Alionekana kuchoka sana na hakuwa tayari kwenda, lakini nilisisitiza kuwa tuondoke kama familia. Tulielekea kanisani pamoja, na siku hiyo niliitumia kama muda wa kutafakari, kuomba msamaha, na kujiweka sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya kutoka kanisani mchana, nilipokea simu kutoka kwa mama Aria. Mazungumzo yetu ya kwanza yalihusu afya ya mwanangu Aria. Alinieleza kuwa maendeleo yake ni mazuri na waliruhusiwa kurudi nyumbani tangu usiku uliopita. Nilimuomba radhi kwa kushindwa kupokea simu zake siku ya Ijumaa, na tukaendelea na mazungumzo mengine.

Mazungumzo yetu yakahamia kwenye suala la kwenda nyumbani kwetu ili awafahamu wazazi wangu. Alitaka kujua hatua niliyofikia, hasa ikizingatiwa kuwa muda ulikuwa unaenda na Desemba haikuwa mbali.

Nilimweleza kuwa hilo ni suala nyeti linalohitaji busara kubwa, na kwamba nilihitaji kulishughulikia taratibu kwa wakati muafaka ili kuepuka mtafaruku. Hata hivyo, nilimhakikishia kuwa nitalifanyia kazi kama nilivyoahidi, maana ni haki ya mtoto wetu kuwafahamu babu na bibi yake. Alisikiliza kwa utulivu na kusema kuwa muda utafika na ataninikumbusha ahadi zangu.

Baada ya mazungumzo marefu, tuliagana, nami nikabaki nikitafakari kwa kina. Ukweli ni kwamba hili lilikuwa mojawapo ya masuala niliyokuwa nikiyakwepa sana, kwa sababu nilijua ndani yangu kuwa bado sikuwa nimechukua hatua yoyote ya maana.

Suala la kuwajulisha wazazi wangu kuhusu mtoto na mama yake lilinipa msongo mkubwa wa mawazo. Sikuwa najua nianzie wapi wala watalipokeaje. Mawazo yalikuwa mengi, majibu hayakuwepo.

Jioni, Bob alinipigia simu kunijulia hali na pia akanieleza kuwa yeye na Lucy walikuwa wamerudiana. Nilifurahi kusikia hilo, maana hata Lucy alionekana kuwa na furaha kazini tofauti na kipindi walipokuwa wamegombana.

Nilimuuliza swali la kizushi;

MIMI: “Vipi umekula mzigo?”

BOB: “Hapana kaka, bado naenda naye taratibu kumbuka ulinishauri hivi kaka.”

Nilicheka kwa sauti kubwa sana;

MIMI: “Lucy kafanikiwa kukukamata, huna ujanja wewe fala.”

BOB: “Hapana kaka sitaki kurush mambo, Lucy yuko serious sana.”

MIMI: “Lucy sio bikra utambue hilo, kama hakupi yeye anamaliza vipi shida zake? Kuna bwege anapewa halafu wewe husband material unazungushwa, dadeki.” Niliamua kumchana ukweli.

BOB: “Insider acha us**nge bhana, sidhani kama Lucy anaweza kufanya hivyo.”

MIMI: “Nisikilize, najua hupendi kuambiwa ukweli, wewe muulize haya maswali Lucy. Moja, shida zake anamalizia wapi?, pili, anampango wa kukupa tunda lini?, na tatu Je anakuamini?”

BOB: “Bro huko nitafika mbali sana, sasa unanishauri nini?.”

MIMI: “Kaka sisi ni wanaume kuna mambo lazima tuambiazane ukweli. Lucy ni mshikaji wangu sana tambua hilo, lakini anazingua. Mimi nakushauri fanya hivi, kama kweli unampenda tafuta demu pembeni wa kupunguza arosto. Au kama vipi unaweza kumpiga chini mazima ukatafuta mwanamke mwingine, machaguzi ni yako kaka.”

BOB: “Kaka unanishauri nimuache?.”

MIMI: “Sasa kuna haja gani ya kuwa na mahusiano na mtu ambaye hakupi tunda na sio bikra, camon man. Ndomana nimekupa option mbili wewe chagua moja hapo, ila hakikisha unamuuliza hayo maswali 3.”

BOB: “Bro hapo kwenye kumuacha hapana aisee!”

Nikamkatisha pale;

MIMI: “Bro tuachane na hii mada, leo ndo nimejua kwanini Lucy anakusumbua. Kumbe ushamba wako wa wanawake bado hujaacha tangu tuko jeshi.”

Bob aliishia kucheka na akakata simu pale na mimi niendelea kutafakari yale maongezi na sikutegemea kuona Lucy akimsumbua Bob kwa namna ile. Mwisho niliona ni bora kuwaacha waendelee na mahusiano yao maana hayanihusu.

Niliamua kuondoka na Junior kwenda Mlimani City ili kupoteza muda kidogo, huku yeye akipata nafasi ya kucheza na watoto wenzake. Nilishiriki naye kwenye michezo mbalimbali kama baba, jambo lililomfanya afurahi sana. Ilipofika saa mbili usiku, tuliamua kuondoka na kurejea nyumbani, maana alikuwa amechoka sana kutokana na michezo na pilikapilika za siku nzima.
*********
Wiki mpya ya mwezi wa kumi ilikuwa imeanza. Jumatatu asubuhi na mapema, baada ya kumaliza jogging, nilienda moja kwa moja ofisini. Jambo la kushangaza ni kwamba tangu ni sex na Hilda, hatukuwa tena na mawasiliano yoyote hakunitafuta wala mimi sikumtafuta.

Hii wiki nzima kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, Hilda asingekuwepo ofisini, kwani kulikuwa na semina ya wanawake ambako alikuwa akiiwakilisha kampuni.

Majira ya saa tano asubuhi, Sanchi alinipigia simu na kuniarifu kuwa amepigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Erica, aliyetoa taarifa kuwa angefika ofisini siku hiyo. Nikakumbuka sikuwa nimemjulisha Sanchi kuhusu ugeni huo, hivyo nikamtoa wasiwasi kwa kumwambia kuwa huyo dada ni familia na ampe ushirikiano wa kutosha.

Baada ya kumaliza mazungumzo na Sanchi, nilijikuta nikitafakari kwa kina kuhusu hatima yake ndani ya kampuni. Alikuwa anajituma sana, na kwa dhati nilitamani kumpa hata asilimia 10 ya hisa za kampuni. Baada ya kufikiria kwa makini, nikaona ni busara zaidi nimteue rasmi kuwa Secretary wa kampuni na nianze kumlipa mshahara stahiki.

Jumatano jioni, nilikuwa Mikocheni @theWheel, nikisubiri gari langu likifanyiwa service. Ghafla simu yangu ikaanza kuita, nilipoitoa mfukoni, nikaona ni Iryn aliyekuwa anapiga. Nilipokea bila kusita, lakini kwa mshangao sauti niliyoisikia haikuwa ya Iryn bali ilikuwa ni ya Samantha.

Tangu aanze kuzungumza, ilionekana wazi kabisa kuwa mambo hayakuwa sawa. Sauti yake ilikuwa nzito, ikibeba hofu na wasiwasi mkubwa. Akanijulisha kuwa dada yake, Iryn, alikuwa anaumwa sana na tayari amelazwa hospitali tangu jana usiku. Kwa mujibu wa alivyoniambia, hali yake haikuwa nzuri kwa wakati huo.

“Shida ni nini?”

“Dada Vivian ndiye anayejua kila kitu.”

“Na vipi kuhusu Aria?”

“Aria amelala, lakini yuko sawa, hana tatizo.”

“Okay shem, ahsante kwa taarifa. See you soon.”

Baada ya simu kukatika, nilihisi uchungu mkubwa moyoni mwangu kwa kipindi kigumu walichokuwa wakikipitia. Sikujiona nina option nyingine zaidi ya kuondoka kuelekea South Africa. Kilichokuwa kinanitatiza zaidi ni kuelewa kwa nini Iryn na Aria walianza kuumwa tangu walipotoka kwa baba yao.

Nikamwambia Kalanje, mmoja wa jamaa zangu pale @thewheel, nikamwomba aharakishe service ya gari langu kwa sababu nilikuwa nimepatwa na dharura na nilihitaji kusafiri haraka. Wakati huohuo, nikaanza kuwasiliana na agent ili anitafutie tiketi ya kwenda South Africa.

Baada ya dakika kumi tu, gari lilikuwa tayari. Nikaanza safari ya kurudi nyumbani ili kujiandaa kwa safari ya South Africa. Nikiwa njiani, simu ya Dullah ikaingia. Niliipokea na kuiweka kwenye loudspeaker, tukaanza mazungumzo.

MIMI: “Senior vipi kaka?”

DULLAH: “Aisee poa chief. Upo pande zipi? Kuna sehemu nataka twende.”

MIMI: “Kaka, nimepigiwa simu kuwa mama mtoto anaumwa kule South Africa. Mtoto alianza kuumwa, akalazwa, na sasa ni yeye mwenyewe. Hapa naelekea nyumbani kujiandaa niondoke.”

DULLAH: “Pole sana kaka. Ningependa sana kukupa kampani ndugu yangu, ila kwa sasa hali yangu ya kifedha sio nzuri.”

MIMI: “Uko tayari kwenda nikulipie nauli?”

DULLAH: “Ndio kaka, niko tayari kukupa kampani.”

MIMI: “Sawa basi, nenda kajiandae, tuondoke wote.”

Baada ya kuagana na Dullah, kulikuwa na jambo moja tu muhimu la ku-takecare. Sikujua nitawezaje kulitatua, na ndilo lililoanza kunisumbua sana akili yangu.
mapema kabisa 💃
 
Back
Top Bottom