SEASON 03
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
CHAPTER 15
Hapo ndipo nilihisi hali ya dharau ikianza kujitokeza kutoka kwa Jamaa. Sababu alikuwa anaendelea kuniuliza maswali tena ananionesha dharau za waziwazi. Nikatambua wazi kuwa hapa sikuwa na nafasi tena, nilikuwa nimeingia kwenye himaya ya mtu mwingine. Bila kuongeza neno, nikaamua ni bora niondoke haraka kabla mambo hayajaharibika zaidi.
CONTINUE:
Wakati najiandaa kuondoka, Mary alitoka ndani chumbani, kwa wakati huo hakujua kinachoendelea. Sauti yake ilisikika kwa mbali akimuuliza yule jamaa:
“Emma, ni nini kinaendelea? Mbona umesimama mlangoni?”
Yule jamaa akajibu kwa dharau,
“Kuna mgeni wako hapa, njoo umsikilize.”
Mary aliponiona, alibaki amesimama kwa mshangao. Hakutarajia kuniona pale kwake, na wazi kabisa hakufurahishwa na ujio wangu. Uso wake ulionesha sintofahamu na hasira iliyojificha, kisha akauliza moja kwa moja, jamaa akatuacha pale.
MARY: “What do you want here?”
MIMI: “Acha kujifanya hujui kilichonileta hapa.”
MARY: ““I already told you it’s over. So what do you want?”.
Nikavuta pumzi ndefu kabla ya kujibu,
MIMI: “Nimekuja kwa ajili ya maridhiano. Naomba tukae tuzungumze kwa utulivu, tujaribu kurudisha mahusiano yetu kama zamani.”
Mary alitikisa kichwa kwa huzuni, sauti yake ikibeba maumivu;
MARY: “Haiwezekani Insider, hufahamu kiasi gani ulinuumiza. Nililia sana, nikateseka sana hadi leo nimeamua kusahau kila kitu.”
MIMI: “Utajisikiaje ukijua ulilia bila sababu ya msingi? Ndio maana nimekuja hapa tuweke mambo sawa. Nipe nafasi ya kujieleza kabla ya kufanya maamuzi mazito bila kunisikiliza. Mary, nakupenda sana, na ndiyo maana nipo hapa.”
MARY: “Insider, nishamove on, sitaki tena kuwa kwenye mahusiano na wewe. Nikikaa karibu na wewe nitakuwa nakupa nafasi ya kuendelea kuniumiza.”
MIMI: “Sawa, kama umesha move-on, sina pingamizi. Kumbuka tu, wewe ndiye ulikuwa mwanzo wa mahusiano haya na wewe pia umekuwa mwisho wake. Mti ulioupanda kwa mikono yako mwenyewe, umeamua kuuangusha.”
MARY: “Good, now you understand.”
MIMI: “Concern yangu ni hii, hata kama hatutakuwa kwenye mahusiano, tuendelee kushirikiana kama zamani kwenye mambo mengine. Hii hali ya kuninunia kila tukikutana haileti picha nzuri, na inaweza kumfanya Prisca aone kama kulikuwa na kitu kikubwa kati yetu.”
MARY: “I already told you I can’t be close to you again. Please respect my decision.”
MIMI: “Sawa kama umeamua iwe hivyo. Nimekuja kwa nia njema ya maridhiano, lakini umechagua violence. Sikiliza Mary, nikiondoka hapa leo, tambua kuwa kila kitu kuhusu sisi kitabaki kuwa historia, kwaheri.”
Nikaondoka pale nikiwa na mzigo mzito moyoni. Ukweli ni kwamba nilikuwa nimeumia sana. Hata baada ya kufika kwenye gari, nilikaa kwa dakika kadhaa bila kuondoka, mawazo yangu yote yakiwa kwa Mary. Nilishindwa kuelewa kwa nini moyo wangu uliumia kiasi kile kumuacha. Zaidi ya yote, ile kauli yake ya kusema kuwa ameshamove on ilinichoma moyoni na kuniacha na mawazo mengi sana kwa wakati ule.
Kwa upande mwingine, nilianza kuona hii kama green light kamili ya kuachana naye kabisa. Ukweli ni kwamba kuwa kwenye mahusiano na Mary ilikuwa kama kucheza na bomu la nyuklia-wakati wowote lingeweza kulipuka.
Niliwasha gari na kuondoka yale maeneo, nikachukua uelekeo wa Mwaikibaki Road kurudi nyumbani. Hata hivyo, sikuwa na hamu kabisa ya kwenda moja kwa moja home. Ilikuwa ni saa moja usiku, hivyo nikaamua nipitie Upepo Garden Beach nipoteze muda kidogo, nitulize mawazo yangu.
Nilipofika Upepo Garden, nilitafuta kona tulivu yenye upepo mwanana wa bahari, nikakaa na kuagiza wine. Nikiwa nimekaa pale, wazo likanijia, nimtafute Prisca tuzungumze kidogo, hasa kuhusu mama yake. Tangu mimi na Prisca tuachane, karibu mwaka mmoja ulikuwa umepita, lakini bado hakuonesha kabisa kukata tamaa juu yangu. Aliendelea kuamini kuwa ipo siku tutarudiana na kuendeleza pale tulipoishia.
Nilimtumia ujumbe mfupi kumuuliza alipo, na bila kuchelewa akanijibu kuwa yuko dukani. Nikamjulisha kuwa niko Upepo Garden nimetulia, na kama atapata muda basi apitie tuzungumze kidogo. Prisca alifurahi sana kusikia hivyo, akaniambia atapita muda si mrefu kwani alikuwa anajiandaa kufunga duka.
Baada ya kama dakika 40 hivi kupita, Prisca alinipigia simu kunijulisha kuwa amefika na yuko nje getini. Aliniomba nitoke ili aweke mzigo wake ndani ya gari. Nikatoka nje, tukasalimiana kwa tabasamu, akaweka mzigo wake kwenye gari kisha tukarudi ndani kukaa. Naye pia aliagiza wine, na hapo maongezi yakaanza taratibu.
Tulianza kwa kuzungumzia biashara yake. Nilikuwa na shauku ya kujua maendeleo yake kwa ujumla. Prisca aliniambia biashara inaenda vizuri, kwani mauzo yanaongezeka taratibu na wateja pia wanazidi kuongezeka. Nilimpongeza kwa uamuzi wake wa kuanzisha biashara na kwa juhudi anazoendelea kuweka hadi sasa.
Baadaye mazungumzo yakahamia kwa mama yake. Nilikuwa na maswali mengi sana, ni maswali ambayo mara nyingi nikimuuliza Mary alikuwa anashindwa au hakutaka kunijibu.
MIMI: “Mama alinipigia simu Ijumaa, alikwambia?”
PRISCA: “Aliomba namba yako ili akupigie. Baada ya kumuona Ivy amependeza sana, alitaka kukushukuru. Nilijua lazima akupigie, ila hakuniambia kama alikupigia kweli. Vipi, alisemaje?”
MIMI: “Tulizungumza sana kuhusu Ivy, halafu akauliza na masuala mengine ikiwemo lini nitaenda kuwasalimia.”
Prisca akatabasamu kwa hisia,
PRISCA: “Insider, mama anakulizia sana. Unajua kipindi kile ulikuwa kampani yetu sana, hasa kwenye usafiri ulikuwa unatupiga tafu kubwa. Hujui ni vile mama alikupenda sana. Hata baada ya kuachana na wewe, mara nyingi amekuwa akiniambia nilichezea bahati anasema si rahisi kumpata mwanaume kama wewe.”
Nilivuta pumzi ndefu kabla ya kujibu.
MIMI: “Tatizo mama hajui ukweli kwamba nina mke na mtoto. Laiti angelijua hilo, asingesema maneno kama haya. Mama anajua sababu halisi ya sisi kuachana?”
PRISCA: “Mary alimwambia mama kuwa mambo yangu ya utoto ndiyo yaliyosababisha tuachane. Lakini mama yeye anahisi labda mimba iliyoharibika ndiyo sababu kubwa ya sisi kuachana.”
MIMI: “Sasa nikija huko kwenu, huoni nitaanzisha tena mada nzima? Mama atataka kujua kila kitu na pengine atajaribu kutupatanisha. Namuheshimu sana mama, lakini kuja kuwasalimia huku najua ukweli wote ni kama kuishi kwenye uongo.”
PRISCA: “Hapana, mama hawezi kufanya hivyo. Kilichomshangaza yeye ni kuona bado tunawasiliana na hata kutembeleana. Ndiyo maana akauliza kwanini Insider haji nyumbani kama zamani.”
Nikacheka kidogo kwa mshangao.
MIMI: “Mmh! Mtego huu, nitaangalia lakini kuhusu hili.”
Prisca akaongeza kwa sauti ya utani lakini yenye uzito.
PRISCA: “Uje home Insider, mama yangu anakukubali sana kama mkwe, ulipata nafasi adimu sana.”
Nilicheka tu, Prisca akabadili mada na kuanza kunisimulia kuhusu rafiki yake wa karibu, Eva.
“Ile siku uliyokuja dukani, hukumuonesha kumchangamkia Eva, alimind sana,” Prisca alisema.
MIMI: “Kwa nini amind? Hakuwa target yangu kabisa. Nilimsalimia tu, kisha nikaendelea kuongea na nyie, kuna shida?”
PRISCA: “Anasema alijaribu kukuongelesha ukawa unamu-ignore. Anafikiri labda ulimchukia tangu siku ile mkutane Cape Town Fish Market, ukiwa na mwanamke mwingine.”
MIMI: “Sio hivyo kabisa labda sikumsikia, na ile siku nilikuwa busy sana na Ivy, hata wewe uliona.”
PRISCA: “Sawa, huo ndio ulikuwa wasiwasi wake.”
Ilipotimia saa tano usiku, nikamwambia Prisca afanye kurequest usafiri ili arudi nyumbani, lakini alikataa. Alisisitiza kuwa anataka mimi ndiye nimrudishe nyumbani. Sikuona shida, nikamwambia sawa, tuondoke.
Safari ya kutoka Upepo Garden hadi nyumbani kwao ilikuwa kama dakika 10 tu. Nilimshusha nje ya geti lao, tukaagana na mimi kurudi nyumbani.
Baada ya kurudi home niliwakuta akina Elena na mdogo wangu pale seblen, nikawasalimia, sikupoteza hata sekunde, nilielekea moja kwa moja ndani. Chumbani, nilimkuta Mama J, alikuwa bado ana mvuke wa maji ya kuoga, taulo likiwa limefungwa kiunoni, uso wake ukionyesha hali ya mtu aliyekuwa ananisubiri.
Alinitazama kimya kimya kwa sekunde kadhaa zenye maswali mengi kuliko majibu, kisha akavunja ukimya.
MAMA J: “Hatujamaliza mazungumzo yetu ya Dodoma. Nilichagua kunyamaza tu, sikutaka kuharibu lengo letu la safari.”
MIMI: “Unamaanisha nini hasa kwa maneno hayo?”
MAMA J: “Kwanini hukuniambia kuwa Iryn alifika Dodoma, halafu ukaamua kunyamaza kana kwamba hakuna kilichotokea?”
Nilicheka kwa dharau ndogo, nikitikisa kichwa.
MIMI: “Kabla hajafika Dodoma, Iryn alikuja hapa nyumbani, alikutana na wewe. Wewe mwenyewe ulimpa namba yangu niliyokuwa natumia Dodoma. Hukuniambia chochote, lakini ulichagua kunyamaza kama mimi.
So before you start pointing fingers, make sure your hands are clean.”
Kulikuwa na ukimya mzito, mama J alinitazama kwa makini.
MAMA J: “I remember that I told you.”
MIMI: “Anyway sioni sababu ya kuendelea kubishana. Ndiyo maana nataka niachane na kampuni yake nipunguze hizi kelele zisizoisha humu ndani.”
Bila kusubiri majibu, niligeuka na kuelekea bafuni. Nyuma yangu, sauti ya Mama J ilinifuata;
MAMA J: “Nakukumbusha tu hakuna marefu yasiyo na ncha.”
*******
Kesho yake asubuhi, nikiwa njiani kuelekea ofisini, nilipitia kwanza ofisi ya Sumaiya. Kulikuwa na mambo ya kampuni yaliyohitaji majadiliano ya haraka. Tulizungumza kwa kina, tukapanga mikakati muhimu, kisha tukaondoka pamoja kwenda kupata kifungua kinywa.
Tukiwa mezani, Sumaiya aliniangalia kwa umakini wa ajabu.
SUMAIYA: “Weekend hii unitafute, nina taarifa muhimu nyeti, kuhusu Mama Janeth na Iryn.”
Nilinyanyua macho,
MIMI: “Taarifa gani?”
SUMAIYA: “Sio za kuzungumzia hapa cha muhimu ujue tu! Kinachokujia ni confirmed.”
Alisisitiza kuwa ili aweze kuzungumza kwa uhuru, ni lazima asiwe kwenye akili yake kabisa na mazingira yawe huru. Nikamwambia achague mahali pa kwenda na tukakubaliana iwe Jumamosi.
Baada ya kuachana naye, niliendelea na safari yangu hadi ofisini. Nilipoingia ofini, nilimkuta Hilda akiwa busy kwenye kazi. Nilimsalimia, safari hii akaitikia kwa sauti yake juu. Nikaendelea kumuuliza kuhusu likizo yake, akatabasamu akasema ilikuwa nzuri.
Muda huo huo, niliwasiliana na Asmah kupitia video call. Alikuwa mazingira ya chuo, akisubiri lectures, tukazungumza mengi-hasa maisha ya Qatar kwa ujumla. Kwa upande wake alisema kwamba joto kali la kule linamfanya ahisi kama maisha hayawezi. Baada ya maongezi marefu na story za hapa na pale aliniaga kwamba muda wa kuingia darasani umefika, hivyo akakata simu.
Kwa upande wangu, tayari nilikuwa nimefanya uamuzi mzito kuhusu chuo cha kusomea masters. Kilichobaki ilikuwa ni kumjulisha Mzee Juma na kukamilisha bajeti ambayo alisema niiandae. Kumpigia simu moja kwa moja niliona ni jau, nikapata wazo la kuanza na binti yake, Camila. Nilimpigia simu mara mbili ila hakupokea, nikaamua kuendelea na ratiba za ofisini.
Dakika ishirini baadaye, simu ikaita. Jina lake likaangaza kwenye screen na bila kusita nikapokea simu yake;
MIMI: “Binti wa Mzee Juma.”
CAMI: “Insider wewe! Sio muda nimetoka kukuwazia na umepiga.”
MIMI: “Huo ni unafiki ambao siupendi. Kama ni kweli, kwanini hukupiga?”
CAMI: “Nilikuwa na kazi. Really, I was planning to call you.”
MIMI: “Mzee yupo au kasafiri?”
Akaguna,
CAMI: “You always call me ukiwa na shida”
MIMI: “Nijibu basi.”
CAMI: “Sikwambii.”
MIMI: “Like serious?”
CAMI: “Ndio maana yake, si una namba yake? Mpigie umuulize.”
Nikakata simu, na haikuchukua muda, akatuma ujumbe:
“Mzee yupo, lakini ratiba zake hazieleweki. Wasiliana naye kama unapanga kukutana naye.”
Muda mfupi tu baada ya kuzungumza na Cami, simu yangu iliita tena. Safari hii alikuwa ni Sia, aliniomba tukutane jioni Cocobeach ili tujadiliane kwa kina masuala ya biashara. Hakutaja ni mambo gani hasa, lakini ndani ya nafsi yangu nilihisi wazi kabisa-huenda kuna taarifa njema.
Ilipofika saa 11 jioni, nilimuaga Lucy kisha nikachukua njia kuelekea Coco Beach. Sia alikuwa amewasili dakika kama kumi kabla yangu na alinielekeza sehemu aliyokaa. Nilipoingia, niliona gari yake ikiwa imepaki, nikapaki yangu pembeni yake kisha nikaelekea ndani.
Baada ya salamu fupi, hatukupoteza muda. Sia aliingia moja kwa moja kwenye mada na kunithibitishia kile nilichokuwa nakihisi tangu asubuhi, kuhusu mzigo wetu ulikuwa umefika salama na tayari ulikuwa umehifadhiwa stoo. Aliongeza kuwa gharama zote za usafirishaji kutoka bandarini pamoja na malipo ya stoo alikuwa ameshalipia yeye, hivyo hakukuwa na haja ya mimi kulipia chochote kwa sasa. Alipendekeza tukutane kesho kwa ajili ya makabidhiano rasmi na kukagua mzigo kwa umakini.
Baada ya mazungumzo yale, nilichukua simu yangu iliyokuwa mezani na kumpigia Jane kumpa taarifa. Jane alifurahi kupita kiasi aliposikia mzigo umefika salama, akapendekeza tukutane usiku huo huo ili kupanga hatua zinazofuata. Nilijaribu kuomba tukutane kesho kwa sababu ya muda, lakini alisisitiza tuonane na hata akapendekeza aje kwangu ili apajue.
Wazo hilo halikunikaa vizuri kabisa, yani aje kwangu kufanya nini hasa? Nikamshawishi tukutane Mbezi Beach Makonde ‘EB 25’ badala yake, sehemu tulivu na itakayofaa kwa mazungumzo na mipango, hatimaye alikubali.
Nilirudi tena kwa Sia, nikamshukuru kwa mchango wake mkubwa. Akaendelea kunipa mawazo mbalimbali ya biashara, kisha akanitaarifu kuwa wiki inayofuata atasafiri kwenda Turkey. Kabla ya safari hiyo, alisema angepita ofisini kwetu kupata huduma za salon. Tulikaa Coco Beach kwa takribani saa mbili kabla ya kuagana, mimi nikachukua njia kuelekea Mbezi Beach kuonana na Jane.
Jane alikuwa anasubiri nipige simu nimjulishe nikianza safari kutoka Masaki ili naye aanze kusogea eneo la tukio. Nilipofika Mwenge ITV nikampigia simu kumjulisha, akasema yuko Kunduchi na atafika ndani ya muda mchache.
Baada ya dakika 20 hivi ananijulisha kuwa tayari kafika na ananisubiri, muda huu mimi nilikuwa nimekwama vibaya kwenye foleni ya Lugalo hadi mataa ya mchepuko wa kwenda Kawe.
Nilichelewa kama nusu saa kufika pale EB, nilipompigia anielekeze alikokuwa amekaa, simu yake ilikuwa busy. Nikaamua kuingia ndani mwenyewe, ndipo nikamuona amekaa kwenye upande wa restaurant akiongea na simu, nikajumuika naye mezani.
Aliponiona, alitabasamu kisha akanipa tano, huku akiendelea na mazungumzo ya simu. Mhudumu alifika kunisikiliza, nami bila kusita nikaagiza juice. Alipomaliza kuongea ndipo mazungumzo yetu yakaanza rasmi.
JANE: “Insider! Kwanini unaagiza juice? Agiza chakula.”
MIMI: “Nataka amani nyumbani, sitaki vita na wife.”
Jane alicheka sana.
JANE: “Ndiyo maana hukutaka nije kwako nimjue wifi yangu?”
MIMI: “Mipango mikubwa kama hii nyumbani siyo sehemu sahihi, ndiyo maana nikapendekeza tukutane hapa.”
JANE: “Sawa, uko sahihi ila nimefurahi sana kusikia mzigo umefika salama. Sasa biashara tunafungua lini?”
MIMI: “Kesho naenda kuuangalia mzigo, tukimaliza taratibu zingine, kufikia Jumatatu tutaanza biashara rasmi.”
JANE: “Pale dukani tutamweka nani? Nilikuwa nawaza Vicky aanze kushinda dukani, maana kwa sasa analala tu nyumbani.”
MIMI: “Sawa, lakini hata mimi huu mwezi nitakuwa nashinda dukani. Pia ni muhimu tutafute vijana wawili wenye uzoefu, incase Vicky akirudi chuo. Hata Vicky akirudi chuoni bado tutamtumia kwenye uangalizi wa karibu wa duka.”
JANE: “Ni sahihi, lakini vipi upande wa TRA, umemaliza nao?”
MIMI: “Ndiyo, hata ritani nimeanza kutuma. Masuala ya compliance niachie mimi, nitayashughulikia vizuri.”
Tulitumia kama nusu saa kupanga na kusuka mipango ya biashara kwa umakini. Baada ya hapo, kila mmoja wetu alichukua njia yake ya kwenda nyumbani.
*****
Siku tatu zilizofuata nilizitumia kikamilifu kuhakikisha kila kitu dukani kinakwenda sawa. Nilikuwa karibu muda wote na Vicky, tukisaidiana kwa pamoja vizuri, yeye akishughulikia mpangilio wa bidhaa, mimi nikisimamia mambo ya jumla na kuhakikisha kila kitu kipo kwenye mstari. Ilipofika Jumamosi, tulikuwa tumemaliza kila kitu. Duka lilikuwa limepangwa, bidhaa ziko sawa, na kilichobaki ilikuwa ni kusubiri Jumatatu tufungue rasmi.
Kwa upande mwingine, Sia aliendelea kuwa msaada mkubwa. Aliendelea kunipa elimu na mbinu mbalimbali za kibiashara namna ya kuhudumia wateja hadi bei elekezi za soko la Kariakoo. Ushauri wake ulikuwa wazi ambapo alisema tuanze kwanza kudeal na wateja wa rejareja, halafu tukishakuwa na portifolio kubwa na ya kuaminika, ndipo tuanze kuingia kwenye wholesale.
Jumamosi usiku nilikuwa na ratiba ya kukutana na Sumaiya. Ukweli ni kwamba nilikuwa nimechoka kupita kiasi, lakini sikuwa na namna ya kuahirisha. Kabla sijaondoka dukani nilimpigia simu, naye akaniambia niende moja kwa moja kwake nikamchukue. Nikajisemea moyoni, si mbaya njia ni moja, na ikiwezekana nikaoge kabisa kupunguza huu uchovu.
Sumaiya alikuwa amehamia makazi mapya-Kinondoni Makaburini, eneo ambalo unaingia palepale karibu na makaburi. Alinielekeza vizuri hadi nikafika, akatoka nje getini kunifungulia mlango na nikaiingiza gari ndani ya nyumba.
Alinikaribisha jikoni nikaungane naye kuendelea na story, maana alikuwa katikati ya kupika. Kingine kilichonishangaza ni ukimya uliokuwa pale ndani. Nilitegemea kumkuta mtoto wake akizunguka pale, lakini hali ilikuwa tofauti kabisa. Nilipomuuliza, aliniambia mtoto alikuwa ameenda kumsalimia bibi yake akiwa na dada wa kazi.
Baada ya kula chakula cha jioni nilienda kuoga. Nilipotoka, uchovu wote wa siku ulikuwa umetoweka, nikajikuta nimepata nguvu mpya kabisa. Nikakaa sebleni nikimsubiri Sumaiya ajiandae ili tuondoke.
Pamoja na kunihakikishia kuwa anaishi peke yake na hakuna mwanaume anayefika pale, bado moyoni nilikuwa na wasiwasi fulani niliokuwa siwezi kuueleza wazi, mwanamke haaminiki.
Ilipotimia saa mbili usiku, tuliondoka kuelekea Masaki. Njiani tulikuwa tunabadilishana mawazo ya kwenda kiwanja gani kwa usiku ule. Baada ya majadiliano kidogo, tukaamua kuelekea Coco Beach, Wavuvi Camp.
Tulipopaki na kushuka, ndipo nikamtambua vizuri Masai aliyekuwa ananionyesha sehemu ya kuegesha gari. Alikuwa mmoja wa crew ya Elias, yule ambaye walikuwa wanashinda naye sana pale Seacliff. Tukaanza mazungumzo pale pale, na mada kubwa ikawa ni Elias.
Nilitamani sana kujua maendeleo yake kwa ujumla ukizingatia simu yake haikuwa inapatikana, na taarifa za mwisho nilizozipata zilikuwa nzito, niliambiwa kuwa alifiwa na mtoto wake mchanga.
Masai aliniambia hana uhakika Elias alipo kwa sasa, wala hawakuwa wanawasiliana. Ila anajua tu kwa kuambiwa kuwa Elias aliamua kwenda Zanzibar kutafuta maisha. Nilimuuliza kama kuna mtu yeyote anayefikiri anaweza kuwa na mawasiliano naye, akanitajia jina moja-Laibon. Alinishauri nikifika mitaa ya Seacliff, nimtafute jamaa huyo, huenda akanisaidia.
Baada ya maongezi yale, tukaelekea ndani. Njiani, Sumaiya akaanza maswali.
SUMAIYA: “Yule Masai uliyekuwa unamuulizia ni nani?”
MIMI: “Mind your business.”
Sumaiya alinipiga ngumi ya mgongo kwa mzaha, nami nikapitisha mkono wangu kiunoni mwake huku tukiendelea kutembea taratibu kuelekea ndani.
Ndani, hali haikuwa tulivyotarajia, meza nyingi zilikuwa zimewekewa ‘reserved’, zingine zikiwa tayari zimejaa watu. Hatukupata sehemu iliyoturidhisha, tukatazamana bila hata kuongea sana, kisha tukaamua kuondoka kwenda Warehouse.
Tulipofika Warehouse, bahati nzuri tulipata sehemu ya kukaa juu kabisa. Meza tuliyokaa mbele yetu ilikuwa na watu wawili(couple), hivyo meza ikawa na watu wanne kwa jumla. Haikuchukua muda mhudumu akafika kutusikiliza, na mazungumzo yakaanza moja kwa moja kati yake na Sumaiya.
SUMAIYA: “Insider, nataka kuchukua Jameson, unasemaje?”
MIMI: “Sawa! Mimi niletee Heineken nne kwanza, zinanitosha usisahau na mishikaki.”
SUMAIYA: “Wewe naye kwamba hutaki kulewa?”
MIMI: “Sikujua kama siku hizi Heineken imekuwa non-alcoholic.”
SUMAIYA: “Haiya! Mimi leo nataka kulewa kwelikweli.”
MIMI: “Sawa, lakini uwe makini, usije ukafanya mambo ya hovyo.”
Tulianza mazungumzo ya kawaida ya ofisini ambapo Sumaiya alinipa taarifa njema za kupata wateja wawili wapya kutoka kwenye mkutano wa Zanzibar. Alisema mmoja walifanikiwa ku-close deal kwa simu, na mwingine alikuwa amefika ofisini Alhamisi kwa ajili ya mazungumzo ya kazi.
Kadri bia zilivyoendelea kuingia, ndivyo Sumaiya alivyozidi kufunguka. Alianza kuzungumzia mambo mengi mfululizo, hadi pale alipogusa sakata la mama Janeth na Iryn. Hapo ndipo nilipohamisha umakini wangu wote na kuanza kumsikiliza kwa makini.
MIMI: “Naamini hii habari unayotaka kuniambia ina ukweli ndani yake.”
SUMAIYA: “Why nikudanganye? Ila niombe jambo moja, ibaki kuwa siri yako.”
MIMI: “Sasa unadhani nitamwambia nani?”
SUMAIYA: “Namaanisha Iryn asijue haya niliyokuambia.”
MIMI: “Nilikwambia Iryn anajua kiasi chake. Labda kama kuna siri mpya, maana mara ya mwisho ulisema kama Iryn akijua anaweza kumchukia mama yake milele…”
Sumaiya akamalizia kinywaji kilichokuwa kwenye glass yake, kisha akaminina kingine bila kusita. Alikaa kimya kwa sekunde chache kana kwamba anatafuta maneno sahihi, halafu akaanza kuzungumza kwa sauti ya chini lakini nzito.
SUMAIYA: “Ni hivi Insider… kuhusu suala la Smith, ukweli ni kwamba lilikuwa ni mpango wa mama yake mzazi Iryn mwenyewe. Sio kwamba mama Janeth alichepuka na baba yake Iryn kama ambavyo ulikuwa ukiamini.”
Nilishtuka sana baada ya kuzisikia hizi taarifa kutoka kwa kwake,
MIMI: “Kuwa serious, unamaanisha mama yake Iryn ndiye alitaka mama Janeth azae na mume wake? Hiyo haimake sense kabisa, kwanini afanye hivyo?”
SUMAIYA: “Hizo ndizo taarifa nilizonazo hadi sasa hata mimi nina maswali uliyonayo, kwanini na kwa sababu gani?. Lakini kuna jambo lingine ambalo hujui. Ile nyumba anayoishi mama Janeth ilitolewa na baba yake Iryn mahsusi kwa ajili ya kukaa na mtoto wake Smith. Na nyumba yenyewe iko chini ya umiliki wa mama Janeth. Ninaamini hili, Iryn hajui.”
Nilitikisa kichwa taratibu, nikihisi kichwa changu kimejaa maswali mazito kuliko majibu.
MIMI: “Dadeki! Kama haya yote ni kweli, kwanini hadi leo wamekaa kimya? Kwa nini hawajamwambia Iryn ukweli huu wote?”
SUMAIYA: “Labda wanapima upepo kwanza au wanasubiri muda sahihi wa kumwambia.”
Nilivuta pumzi ndefu, nikiegemea kiti changu.
MIMI: “Aisee… nashukuru kwa kunipa taarifa, lakini kwa sasa bado sina imani kabisa na haya unayoniambia.”
SUMAIYA: “Niamini mimi ni mama mwenyewe ndiye aliyenieleza siri hii. Na mimi nimekuambia wewe hizi siri, please naomba ufunge mdomo wako.”
Nilikaa kimya nikifikiria, kichwani nilikuwa napima kila sentensi aliyonieleza Sumaiya, lakini bado haikunikaa sawa. Ilionekana kama hadithi isiyo na mantiki, lakini kwa upande mwingine, kama mama mwenyewe ndiye aliyemwambia Sumaiya, basi kulikuwa na uwezekano fulani wa ukweli ndani yake.
Mwisho wa yote, nilijisemea kimoyomoyo kwamba haya mambo hayanihusu. Kuyachimbua au kuyafuatilia zaidi ilikuwa ni kupoteza muda wangu tu. Sumaiya alikuwa amenisimulia siri nyingi sana, nyingi ambazo nilizibeba na inabaki kuwa siri yangu. Lakini hata hivyo, sikuweza kusema nina imani kamili na taarifa zile. Kama habari ni za kweli bhasi ni suala la muda tu kwa kila kitu kuwa wazi.
Kwa upande mwingine tulizungumza kuhusu Hilda na nilimweleza Sumaiya wazi kuwa mimi na Hilda bado hatujarejea kwenye maelewano mazuri tangu lile sakata la Zanzibar. Kulikuwa na majeraha ya zamani ambayo bado hayajapona.
Sumaiya aliniskiliza kwa makini kisha akanambia jambo lililonishtua. Alisema kwa sasa Hilda yuko kwenye mahusiano na yule jamaa waliyekutana naye Zanzibar. Ingawa Hilda bado hajamwambia ukweli moja kwa moja, Sumaiya alikuwa na uhakika kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao. Sababu wanakutana mara kwa mara, wanatoka pamoja, na ukaribu wao haukuwa wa kawaida.
Kisha Sumaiya akaongea kwa sauti nzito, kama mtu anayetoa onyo la mwisho:
“Insider, kuendelea kumwangalia Hilda kama dada yako kutakugharimu na heshima itashuka. Mpitishe kama ulivyomfanyia Asmah, hapo atakuheshimu otherwise atakusumbua sana. Hilda anakukubali sana, na sasa ameweka chuki moyoni dhidi yako. Suluhisho ni moja tu tembeza sparkles, ili arudi kuwa sawa.”
Maneno yake, kwa upande mmoja, yalikuwa na mantiki. Lakini moyoni sikuwa tayari kutembea na Hilda, sikutaka kuona yale ya Asmah yakijirudia tena. Nilimwambia Sumaiya wazi kuwa siwezi kufanya kitu kama hicho ni bora Hilda aendelee na maisha yake kuliko mimi kuingia kwenye kitanzi.
Tuliendelea kukimbiza vinywaji huku Sumaiya akinionesha ufundi wake wa kucheza na kuzungusha kiuno, na ilipotimia saa 7 usiku, tuliamua kuondoka.
Nikiwa njiani kurudi home, nilikuwa nikiyatafakari sana maneno ya Sumaiya kwa undani. Swali langu lilikuwa ni kwamba, hivi kuna siri gani inaendelea kati ya mama na Sumaiya? Hadi kupelekea Sumaiya kujua siri nyingi za mama?. Niliona kuna haja ya kuchunguza hili taratibu maana nilihisi huu ukaribu wao si bure.
Baada ya kufika nyumbani, nilijikuta nikiingia kwenye ugomvi mkubwa na wife. Sababu ilikuwa moja tu! Nilichelewa kurudi nyumbani, na usiku ukaisha bila amani, yeye alienda kulala chumba kingine.
Kesho yake ilikuwa Jumapili. Niliamka nikiwa nimechelewa, na nikagundua nyumba nzima ilikuwa tayari imekwenda kanisani, kasoro mimi. Kwa kweli, siku nyingi zilikuwa zimepita bila mimi kukanyaga kanisani. Hapo nikajisemea moyoni kuwa lazima nichukue hatua fulani juu ya maisha yangu ya kiroho.
Nilipochukua simu yangu, nilikuta missed call za kutosha pamoja na ujumbe kutoka kwa Prisca. Nilimjibu kwa salamu, kisha nikampigia Sumaiya kuangalia maendeleo yake, maana tangu tuachane Warehouse hatukuwa tumewasiliana tena. Baada ya kuongea aliniambia yuko salama, na alishia kunichamba kwa kumuacha arudi nyumbani salama, na alisema nilipaswa kuondoka naye.
Baada ya hapo, nikarudi kwenye simu yangu na kuanza kuchat na Prisca. Alikuwa anajibu kwa haraka, na mazungumzo yakachukua mwelekeo mzito. Tulichat sana, na ujumbe wake mkubwa alikuwa anaomba turudiane, tuanze upya, na tuendeleze mahusiano yetu kama zamani.
Prisca alinipa wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi. Tayari mimi na Mary tulishavunja mahusiano, hivyo moyoni nikaanza kuona kama huu ulikuwa wakati sahihi wa kumrudisha Prisca kwenye himaya yangu. Tulishawahi kupendana, tulishawahi kushirikiana mengi na zaidi ya yote, kulikuwa na wazo jingine lililonivutia kimya kimya ni kulipiza kisasi kwa Mary. Nilijua fika, nikirudiana na Prisca, basi Mary lazima angeumia sana. Lakini bado nilikuwa dilemma.
Mchana niliondoka kwenda Mbweni kushinda kwa Ghati na ilipotimia saa kumi na moja jioni niliondoka kwenda kukutana na Mzee Juma, Ze Club Silver Pipes, Mikocheni. Lengo la kukutana lilikuwa moja ni kufinalize suala la bajeti ya masomo, maana tayari nilikuwa nimeshapata chuo na kilichobaki kilikuwa ni kuweka mambo sawa.
Nilipofika pale, nikagundua Mzee Juma hakuwa peke yake. Alikuwa ameongozana na mzee mwingine wa makamo. Baada ya salamu chache za heshima, Mzee Juma akanitambulisha kwa yule mzee kuwa ni rafiki yake wa karibu sana. Kisha akanigeukia na kumwambia, “Huyu ni kijana wa marehemu Pama.”
Mazungumzo yetu yakaanza kumzunguka Pama kuhusu historia yake, maisha yake, na mambo aliyoyaacha nyuma. Baada ya maongezi marefu yaliyokuwa na kumbukumbu nzito, Mzee Juma akanigeukia moja kwa moja, safari hii kwa lengo lililotuleta pale.
Tukaanza kuzungumza kuhusu suala la shule. Nilimweleza faculty niliyokuwa nimeamua kusoma pamoja na chuo nilichopata. Tukapitia masuala ya ada, gharama nyingine, na mipango ya jumla. Mwisho wa mazungumzo, Mzee Juma alisema kwa utulivu kuwa angeingiza pesa ya awamu ya kwanza moja kwa moja kwenye akaunti yangu ya bank.
Baada ya kumaliza maongezi yetu tuliendelea na mazungumzo mengine ya kawaida huku nikimalizia kinywaji changu. Niliamua kuwaaga pale maana sikuona kuna sababu ya kuendelea kubaki pale, pia nilitaka kuwaachia nafasi yao ya mazungumzo.
Mzee Juma hakutaka kuona naondoka mapema, lakini hakuwa na jinsi na aliniruhusu. Nilipofika parking, niliingia ndani ya gari lakini sikuondoka mara moja. Nilibaki pale nikitafakari mambo mengi sana, na kama kawaida, mawazo yangu yote yalirudi kwa Mary.
Nilianza kuumia kwa kiwango kingine huku hasira, maumivu, na tamaa ya kulipiza kisasi vilianza kupishana kichwani mwangu.
“Huyu Mary sijui nifanye nini, niendelee kumkamia anisamehe, halafu nimpige tukio la maana ambalo hatalisahau milele? Ila kulia-lia kwa mwanamke ni udhaifu, muhimu tayari nime-fu**k, I don’t care. Bora nirudiane na Prisca hii itakuwa comeback yangu kubwa, najua kabisa itamuumiza sana. Prisca alikuwa mwanamke wangu kabla yake, yeye alivamia boat. Kama Mary alimfanyia mdogo wake ushenzi, basi na mimi wacha nimfanyie.”
Kwa muda huo, moyo wangu ulikuwa umejaa mawazo ya kisasi tu. Lakini ajabu ni kwamba, kuhusu kurudiana na Prisca, bado sikuwa nimeridhika kabisa. Nilikaa pale nikitafakari, nikajiona kama kuna busara ya kuiacha ile familia iendelee na maisha yao. Nilijua wazi, siku moja ningekuwa chanzo cha kuivuruga kama ningeendelea kusogea karibu.
Nikiwa bado nimezama kwenye mawazo hayo, simu yangu ikaita kwa ujumbe. Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Mama J.
MAMA J: “Swahiba upo wapi? Nimerudi church muda mrefu sijakukuta.”
Nilitaka kuupuuzia kabisa, lakini baadaye nikaamua kujibu.
MIMI: “Wewe ndiyo sababu sikai nyumbani, mwanamke kelele nyingi kama tuko club bhana.”
Jibu lake likaja haraka.
MAMA J: “So! Upo wapi huko ambako hakuna kelele?”
Niliposoma huo ujumbe, nilihisi kama ananipotezea muda tu. Nikaweka simu pembeni. Dakika chache baadaye, ujumbe mwingine ukaingia.
“Urudi home, nimekupikia pilau na kuku, na juisi yako pendwa ya tende. Pia nimekumiss sana mwenzio, rudi mapema, nina hamu na wewe.”
Niliposoma huo ujumbe, nilitabasamu tabasamu la kinafiki. Nikaamua kuwasha gari na kurudi nyumbani, japokuwa awali nilikuwa nimepanga kwenda Mlimani City kupoteza muda.
Usiku ulipoingia, mimi na Mama J tulijikuta kwenye mazungumzo mazito. Safari hii mada haikuwa ugomvi wala lawama, bali suala la kuzaa watoto. Kwa kweli, hatukuwahi kukaa chini kuzungumza idadi ya watoto tunaotamani kuwa nao. Nilikuwa na hamu ya kusikia msimamo wake.
Mama J alisema kwa utulivu kuwa kwa sasa hawezi kuzaa hadi amalize chuo. Baada ya hapo, angependa mtoto mwingine, na kwa mtazamo wake, watoto wanne walitosha kabisa kwa familia yetu.
Nikashangaa sana,
MIMI: “Watoto wanne tu? Are you serious?”.
MAMA J: “Kama unaona wachache, basi watano inatosha.”
Nikacheka kwa dharau.
MIMI: “Mimi nahitaji watoto kumi. Kwa sasa upo nusu ya lengo.”
Akanitazama kwa mshangao.
MAMA J: “You have got to be kidding me. Unataka kuniua? Unafikiri kuzaa watoto kumi ni rahisi? Na hao watoto kumi, kwa maisha haya magumu, ni wa kazi gani?”
MIMI: “Watoto ni Asset mama, acha kuuliza swali la kijinga.”
MAMA J: “Watoto ni liability wanahitaji matunzo, kusoma na gharama zingine kibao. Bado hatuna kipato cha kuwahudumia watoto 10 hata mimi sina uwezo wa kuzaa watoto 10, atleast watoto 6 naweza kujitahidi.”
MIMI: “Sawa sio mbaya sana.”
MAMA J: “What do you mean? Na nitazaa mtoto wa pili nikiwa kwenye ndoa, nadhani umenielewa.”
Hapo ndipo nilihisi mazungumzo yameanza kuingia kwenye eneo ambalo sikutaka kabisa. Habari za ndoa? Sasa hivi? Kwangu hilo halikuwa ajenda hata kidogo. Sikutamani hata kulisikia, hasa ukizingatia mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea kwa siri ndani ya maisha yangu.
*****
Tulipoingia wiki mpya, maisha yangu yalichukua mwelekeo tofauti kidogo. Nilianza kushinda dukani Kariakoo nikiwa na Vicky, huku nikijigawa kati ya majukumu mawili muhimu. Asubuhi nilikuwa naanza siku kwa kwenda ofisini kuweka mambo sawa, kuhakikisha mazingira na maendeleo ya ofisi yako katika mstari unaotakiwa. Baada ya hapo, nilielekea Kariakoo kuendelea na shughuli za duka.
Kwa upande wake Vicky alikuwa ameanza mafunzo ya udereva. Hivyo, mchana alikuwa anaondoka kwenda mafunzoni na baadaye kurejea dukani kuendelea na kazi. Pia tulipata vijana wawili waliokuwa wakitusaidia kuhudumia wateja na kushughulikia mambo mengine madogo madogo ya duka, jambo lililopunguza mzigo wetu kwa kiasi kikubwa.
Kukaa muda mwingi dukani na Vicky kulifanya tuzidi kutengeneza connection na chemistry ya kipekee kati yetu. Jane naye alikuwa akipita dukani mara kwa mara, pale alipokuwa anapata nafasi, ingawa hakukaa sana kama sisi.
Ilipofika siku ya Jumamosi, baada ya kufunga duka, mimi na Vicky tuliamua kutoka out, kwani alikuwa akinisumbua sana. Kwa upande wangu, siku hiyo nilikuwa pia na deni moyoni la kumtafuta Elias ili nijue yuko wapi na anaendeleaje. Mara ya mwisho kuzungumza na mmoja wa marafiki zake pale Wavuvi camp, alinishauri nimtafute Masai mmoja anayeitwa Laibon, aliyekuwa akionekana mara kwa mara mitaa ya Seacliff, huenda angekuwa na taarifa kuhusu Elias.
Niliendesha gari kuelekea Seacliff na nikapaki kwenye maegesho ya karibu na bango la Casino. Nikamwambia Vicky anaweza kubaki kwenye gari au anipe kampani, lakini bila kusita alichagua twende wote.
Nilianza kuwatafuta Wamasai waliokuwa wakizunguka maeneo yale. Kwa bahati nzuri, wengi wao nilikuwa najuana nao, hivyo mazungumzo hayakuwa magumu. Hatimaye nilifanikiwa kumpata mmoja aliyemfahamu Elias, lakini alinieleza kuwa ni muda mrefu hajamuona wala hana mawasiliano naye. Nilipomuliza kuhusu Laibon, mmoja wa marafiki wa karibu wa Elias kwenye kundi lao, alinieleza kuwa naye pia hajulikani alipo kwa muda mrefu, na kuna uwezekano mkubwa alikuwa amehamia Zanzibar.
Baada ya kuzungumza na Wamasai kadhaa bila mafanikio, nikagundua kuwa kupata taarifa za Elias au Laibon haikuwa kazi rahisi kama nilivyodhani. Hatimaye niliamua kumuachia yule Masai namba zangu za mawasiliano, nikimuomba endapo atapata taarifa yoyote kuhusu Elias aniwasiliane mara moja.
Nilitoa shilingi laki moja mfukoni nikampa, nikimwambia aitumie kununua simu ya mawasiliano, na nikamuahidi kumpa zawadi nono endapo angefanikiwa kunisaidia kupata taarifa sahihi kuhusu Elias.
Mimi na Vicky tulielekea kwenye gari, Masai akatupa kampani kwa muda mfupi hadi tunafika. Tulipoingia ndani ya gari, alituaga kisha akaondoka zake. Mara tu tulipobaki wawili, Vicky alinigeukia kwa uso uliojaa maswali. Ilikuwa wazi kabisa alikuwa na hamu ya kujua kilichokuwa kinaendelea.
VICKY: “Kwani huyu Masai ni nani? Na huyu Elias unayemtafuta ni nani hasa? Una agenda gani naye?”
Nikavuta pumzi ndefu kabla sijajibu.
MIMI: “Elias ni rafiki yangu wa karibu sana kipindi naendesha Uber. Mara ya mwisho kuonana alinambia amepata mtoto, tangu siku hiyo hatukuwahi kuonana tena. Baadaye nikasikia taarifa kuwa mtoto wake alifariki, na mpaka leo sina mawasiliano naye wala sijui alipo. Ndiyo maana unaniona namtafuta hivi… roho inanuma asee.”
Vicky alitikisa kichwa taratibu.
VICKY: “Pole sana, sasa kama ukimpata una mipango gani juu yake?”
MIMI: “Nikimpata nitakuwa na mipango naye. Alishawahi kuniambia mipango yake ya maisha, ningeweza kumsaidia kadri nitakavyoweza.”
VICKY: “Hapo sawa, naamini utampata tu.”
Nikawasha gari.
MIMI: “Nikupeleke wapi sasa?”
VICKY: “Hata sijui asee… sijui twende wapi… daah!”
Nikacheka kidogo.
MIMI: “Ngoja nikupeleke Wavuvi Camp ukavue, mambo yasiwe mengi.”
Tulipofika pale Wavuvi, nilimpigia simu Jane kumjulisha kuwa niko na mdogo wake ili asiwe na wasiwasi, nikamwambia yuko sehemu salama. Jane hakupinga, ila kwa utani akanisisitiza nihakikishe namrudisha salama kama nilivyosema. Kwa upande wa Vicky, hakufurahia kabisa kusikia nazungumza na dada yake na kumpa taarifa kuwa tuko pamoja. Mara tu nilipomaliza simu, akanigeukia kwa hasira iliyofichika.
VICKY: “Kwanini unamwambia dada Jane kwamba tuko wote? Unajuaje kama nilikuwa napanga kulala kwako?”
MIMI: “Kama ni kulala tu haina shida, tutaenda hata leo usijali, mummy.”
VICKY: “Kwakweli sijapenda ulichofanya. Mimi ni mtu mzima, sio mtoto.”
MIMI: “Unaishi kwa dada yako, lazima uheshimu taratibu na sheria zake. Kama ungekuwa hostel, sawa, nisingempigia simu. Lakini kuwa na wewe usiku halafu uchelewe kurudi na aje ajue tulikuwa wote, unafikiri atanionaje?”
Vicky akatikisa kichwa.
VICKY: “Doesn’t matter, twende ndani nina vibe kama lote.”
Nikacheka tu, nikatabasamu, tukacheka wote wawili. Kisha tukashuka kwenye gari na kuelekea ndani, yeye akiwa nyuma yangu.
Mara tu tulipoingia, ghafla nikahisi mtu ananishika mkono na kuniita kwa sauti ya juu.
“Oyaaa, Insider brother!”
Nilipogeuka nikamtambua ni jamaa tuliyesoma naye chuo na baadaye tukafanya kazi pamoja kwenye taasisi moja, taasisi X. Tulikumbatiana kwa nguvu, salamu za kiume zile zile.
“It’s been a long time, my nigga!”
“Vipi huyu ni shem wetu?” akauliza akimtazama Vicky.
“Relax kijana, ngoja nitafute sehemu ya kukaa, halafu nitakuja tupige story.”
“Ungekaa hapa, ila naona shem hawezi kuwa comfortable, tumejaa wahuni.”
Nikacheka, nikamshika mkono Vicky na tukatafuta sehemu nyingine tulivu zaidi. Tulipokaa, tuliagiza vinywaji na chakula, na muda huu mziki mzuri ulikuwa ukipiga kila kona.
Kama ilivyo kawaida yake, Vicky hakuacha kuuliza, alitaka kujua ni nani yule niliyemsalimia kwa bashasha kiasi kile. Nikamjibu kwa mzaha, nikamwambia kama amempenda aseme tu nimconnect naye.
Alinionya kimya kimya kwa kunisonya, kisha akaanzisha mada nyingine kabisa mada iliyonifanya nipate mashaka.
VICKY: “Hivi Insider, kabla hujaanza mahusiano na Mary, kumbe ulikuwa una-date na mdogo wake?”
Nilimtazama kwa mshangao.
MIMI: “Nani amekuambia story hizo?”
VICKY: “Insider, unanichukuliaje? Nilisikia kwa masikio yangu mwenyewe. Dada Mary alikuwa anamwambia dada Jane.”
Nilinyamaza kwa sekunde chache. Ndani yangu nikahisi wazi kuwa Vicky alikuwa anajua mengi kuliko nilivyodhani. Nikaona ni vyema kutumia nafasi ile kumchimba zaidi.
MIMI: “Ilikuwaje hadi Mary akafikia kuongea maneno kama hayo?”
VICKY: “Dada Jane alikuwa anataka kuwapatanisha. Lakini dada Mary alisema kwa sasa hawezi kurudiana na wewe. Sababu kubwa ni kwamba mdogo wake Prisca akijua mpo kwenye mahusiano, watagombana sana hasa ukizingatia historia yako na Prisca.”
Nikabaki kimya, nikitafuta maneno sahihi ya kusema, Vicky hakusubiri.
VICKY: “Insider, una mpango gani na Mary?”
MIMI: “Hata sijui kwa sasa ila maamuzi aliyoyachukua ni sahihi, na namuunga mkono.”
Vicky aliguna kidogo, akanitazama usoni.
VICKY: “Do you love her?”
MIMI: “Of course I do love her! Unataka kunishauri nini?”
VICKY: “Kama unampenda, mtafute myamalize. Hata yeye anaonekana kuumia kuachana na wewe, ila ana-pretend kama amemove on.”
MIMI: “Mary ana misimamo sana.”
Vicky alicheka kwa dharau ndogo.
VICKY: “Lol! Angekuwa na misimamo, asinge-date na mwanaume aliyekuwa kwenye mahusiano na mdogo wake.”
Ilibidi ninyamaze kimya na nibadili mada haraka sana, niliona ameanza kwenda mbali sana;
MIMI: “Mbali na hayo, hakuna kingine alichomwambia Jane?”
VICKY: “Hakuna ningekwambia. Ila Insider, wewe hapana, umekula mdogo mtu, halafu dada wa mtu naye ukapita. Wewe ni kiwembe hata mimi ningekuwa kwenye nafasi yako, nisingeweza kuwaacha wanawake wazuri kama wale.”
MIMI: “Vicky, acha hizi story. Hujui ni kiasi gani najutia haya yote.”
Baada ya kama saa moja kupita, yule jamaa yangu tuliyekutana awali alikuja mezani kwetu. Tukaanza mazungumzo marefu yaliyojikita zaidi kwenye masuala ya kazi. Alikuwa na hamu kubwa ya kujua kwa nini niliikataa ofa ya kazi na mkataba wa kudumu kutoka taasisi X. Ukizingatia Taasisi X waliwahi kunipigia simu kunipa mkataba wa kudumu, lakini niliupiga chini. Sababu kubwa ilikuwa tayari nilikuwa na kazi nyingine iliyokuwa inanilipa mshahara mzuri zaidi.
Wakati tunafanya internship pale taasisi X, tulikuwa jumla watu wanane tu. Bahati nzuri wote tulipewa ofa za ajira, lakini watatu tu! walikubali ile offa, wengine tulikuwa na kazi tayari, na mmoja wetu kwa bahati mbaya alifariki dunia. Yule jamaa pekee ndiye aliyepangiwa Dar es Salaam, wengine wakaenda mikoani.
Tulipozidi kupiga story, akanikumbusha maisha ya chuo na kuniuliza maendeleo ya Aggy pamoja na Angel moja ya mwanamke aliyekuwa mpenzi wangu kipindi cha chuo.
Angel alikuwa mmoja wa wanawake tuliopendana sana. Alikuwa mwaka mmoja chini yangu chuoni. Tulianza mahusiano yeye akiwa first year, mimi nikiwa mwaka wa pili. Chuo tulikuwa tunaongozana kila kona kama kumbikumbi, tumelala sana pamoja hostel. Hali hiyo ilitufanya tuishi kama mke na mume halali, sababu muda mwingi tulikuwa pamoja.
Angel alifahamika sana kwa watu wangu wa karibu, akiwemo Aggy, ambaye hadi leo haamini kama mimi na Angel tuliachana kweli. Tuliachana baada ya mimi kumaliza chuo, hata baada ya kuachana, Angel aliendelea kuwasiliana sana na dada yangu kipenzi. Alinipa wakati mgumu sana kipindi nilipoanza mahusiano mapya na mama J maana likuwa adui mkubwa wa mama J. Kama mama J angekuwa na moyo mwepesi, huenda leo asingekuwa mama wa watoto wangu. Angel ni mmoja wa wanawake nina historia nzito sana naye maishani. (Season 1 niliwagusia tulikutana Karambezi cafe, nikiwa na Manuel).
Mazungumzo na yule jamaa yalinirudisha nyuma sana hasa maisha ya campus, na kipindi tunafanya kazi taasisi X. Baada ya story nyingi, jamaa aliondoka, akaniacha mimi na Vicky, tukaendelea na mazungumzo yetu wenyewe.
Kwa upande wake, Vicky alionekana kufurahia sana mazingira ya pale Wavuvi. Hakutaka kabisa kurudi nyumbani mapema. Ilipofika saa saba za usiku ndipo tuliamua kuondoka kwenda kulala, japo kwa mbinde sana. Niliendesha gari hadi Mbezi Beach Rainbow, kisha akarequest Uber ya kumpeleka nyumbani Mbweni.
Baada ya kuachana na Vicky, nilielekea nyumbani. Nilipofika getini, nikaangalia simu yangu nyingine na nikakuta missed call za kutosha kutoka kwa Iryn. Nikakumbuka Iryn alisema atakuwa na mazungumzo na mimi kuhusu suala la mtoto. Hata hivyo, kumpigia simu muda ule niliona kunaweza kuleta matatizo, hivyo nikaamua nitamtafuta asubuhi.
******
Wiki ya mwisho wa mwezi wa tisa ilianza kwa kasi ileile ya wiki iliyotangulia. Ratiba yangu ilikuwa ile ile, asubuhi nitaanza ofisini, kisha mchana kuelekea Kariakoo kuendelea na shughuli za duka. Vicky kwa wakati huo alikuwa tayari ameshaizoea kazi, na hata wale vijana wawili walionekana kuimudu vizuri mazingira ya pale dukani.
Siku ya Jumatano, Sia alikuja kunitembelea dukani ili kuangalia maendeleo ya biashara kwa ujumla. Tulikaa pale tukipiga story, tukichambua mambo mbalimbali ya duka, na ilipofika mchana tukaenda kupata lunch pamoja tukiwa na Vicky.
Wiki hiihii siku ya ijumaa niliishinda ofisini Masaki nikiandaa payroll pamoja na malipo mengine ya ofisi. Mama alinipigia simu kunikumbusha juu ya malipo haya, na pia kupitia mazungumzo yale yalinikumbusha jambo muhimu ambalo sikuwa nimemshirikisha rasmi kuhusu mpango wangu wa kuanza shule mwezi ujao, japokuwa nilishawahi kumdokeza hapo awali.
Sikutaka kumwambia suala hilo kwa simu, hivyo nikamuuliza anarudi lini Dar es Salaam kwa kuwa nilikuwa na mazungumzo muhimu naye. Aliniambia anatarajia kurejea mwanzoni mwa mwezi Oktoba, na hapo tukakubaliana tutakutana.
Baada ya hapo niliamua kutoka kuelekea Mlimani City kwaajili ya kufanya malipo, kisha nikaendelea kununua baadhi ya mahitaji muhimu ya ofisi. Baada ya kumaliza nikaondoka maeneo yale nikaendelea na safari kuelekea Masaki. Niliamua kupitia kwanza Texas kuosha gari yangu, na nilitumia masaa mawili pale. Hatimaye nikaendelea na safari yangu ya kurudi Masaki na nilikuja kupark gari kwenye jengo la ofisi za kina Sumaiya na kwenda moja kwa moja ofisini kwake.
Sumaiya, kama kawaida yake, hakukosa story, tuliishia kuongea mambo mengi sana hadi nikajikuta nimetumia muda mrefu pale kuliko nilivyopanga. Nilipotazama saa, ilikuwa ikisoma dakika chache kabla ya 1 jioni. Nikamuaga Sumaiya na kurejea ofisini kwangu kumalizia kuandaa ripoti na baadhi ya nyaraka nilizopaswa kumtumia mama.
Pale ofisini nilimkuta Lucy, lakini Hilda hakuwepo alikuwa ameshaondoka tayari. Nikiwa nimezama kwenye ubusy wa kazi, ghafla sauti ya ujumbe ikasikika, ni message ilikuwa imeingia kwenye simu yangu. Nilihisi hamu ya kuufungua mara moja baada ya kuona mtumaji alikuwa ni Hilda. Bila kuchelewa nikaufungua ule ujumbe ulikuwa mrefu kidogo.
Hilda alikuwa ameandika kuniarifu kuwa ameacha kazi, na kuanzia jumatatu mwezi mpya wa Oktoba hatutakuwa tunafanya kazi pamoja tena. Alieleza kuwa amepata nafasi kwenye kampuni nyingine, nafasi ambayo ingeweza kumsaidia kukuza zaidi taaluma na ndoto zake za kikazi.
Nilikaa kimya kwa muda, nikisoma ujumbe ule tena na tena, nikitafakari uzito wa maneno yale, nilijikuta naishiwa nguvu.
SEE YOU SOON!