SEASON 3
CHAPTER 17
Baada ya kuagana na Dullah, kulikuwa na jambo moja tu muhimu la ku-takecare. Sikujua nitawezaje kulitatua, na ndilo lililoanza kunisumbua sana akili yangu.
Nilianza kuumiza kichwa nikijiuliza, nitaaga vipi kwa Mama J? Na nitamwambia naenda wapi? Haya yalikuwa maswali yaliyokuwa yakinijia mara kwa mara, lakini jibu halikupatikana kirahisi. Nilijikuta nikikaa kimya, nikitafakari kwa kina, nikijua wazi kuwa chochote nitakachosema kitakuwa na uzito wake.
Niliamua kumpigia simu wife kwanza, kujua kama yuko nyumbani. Aliniambia alikuwa bado yuko dukani. Nikamwambia arudi mapema, nikamueleza kuwa nimepata emergency na nalazimika kusafiri usiku huo huo. Sikutaka kuingia kwenye maelezo marefu, hivyo nikamwambia tutaongea vizuri atakaporudi nyumbani.
Ndani ya mawazo yangu, wazo moja likanijia, nimwambie ninaondoka na Mzee Juma kwenda Kenya, kuna kazi tunaenda kufanya pamoja, na ikikamilika nitarudi. Kadri nilivyolifikiria, ndivyo lilivyoonekana linaeleweka na ni rahisi kushawishika. Nikajipa moyo, nikahisi hilo ndilo jibu sahihi kwa wakati ule.
Baada ya kurudi nyumbani, niliingia bafuni kuoga haraka, kisha nikaanza kupanga nguo zangu kwenye bag. Ghafla nikakumbuka bado sijamueleza Agent kuhusu Dullah, ilhali tulihitaji tiketi mbili. Nikampigia simu mara moja na kumuelekeza aanze mchakato wa tiketi mbili za ndege. Alinijibu kwa tahadhari, akasema kupata tiketi mbili kwenye ndege moja inaweza kuwa changamoto, lakini akasema tusubiri tuone kitakachotokea.
Saa mbili usiku, wife alirudi nyumbani. Nilimueleza pale pale kuwa ninaondoka na Mzee Juma kwenda Kenya kwa ajili ya kazi fulani. Mama J hakuniuliza maswali mengi. Kinyume chake, alifurahi sana hasa baada ya kumwambia kuwa tayari nimelipia gari yake na taratibu nyingine za shipping zinaendelea vizuri.
Wakati nazungumza na wife, simu yangu ilikuwa ikiita upande wa pili na ilikuwa ni simu ya Dullah. Nilipopokea simu yake na kuzungumza naye, alinijulisha kuwa yuko tayari kabisa kwa safari. Nikamwambia tukutane Airport.
Kabla sijaondoka, nilimuweka wife kimoja cha haraka, kisha nikachukua Uber kuelekea Airport. Njiani, nilikuwa nikiwasiliana mara kwa mara na Agent, aliendelea kuniambia kwamba changamoto kubwa ilikuwa ni kupata ndege ambayo tunaweza kuondoka wote kwa pamoja.
Nilipofika Airport, nilimkuta Dullah tayari ananisubiri Terminal 3. Tuliposalimiana, tukaanza mazungumzo ya haraka,
MIMI: “Senior, ahsante sana kwa kukubali kunipa kampani.”
DULLAH: “Mimi ndiye natakiwa nikushukuru kwa kunipeleka kwa Madiba. Ila kwanza, shemu anasumbuliwa na nini hasa?”
MIMI: “Kaka, hata mimi sijui kwa uhakika. Nilipigiwa simu tu na shem wangu akanipa taarifa hizi. Juzi tu hapa Aria kaumwa hadi kulazwa, akapona. Ila nahisi kuna kitu hakipo sawa bro… kuna something fishy kinaendelea.”
DULLAH: “Ameshindwa kujua kabisa anasumbuliwa na nini?”
MIMI: “Ni mdogo bado, huenda wameamua kumficha ukweli. Ila vipi wewe, umeongea nini na shem wangu Latifah hadi akakubali kutoa ruhusa?”
DULLAH: “Latifah hana shida akisikia Insider. Ila aliuliza tu kuna mishe gani South.”
MIMI: “Eeh! Ukamjibu nini?”
DULLAH: “Nikamwambia una mishe zako unaenda kufuatilia, halafu ukanikumbuka mwanao Dullah.”
MIMI: “Na kipindi hiki cha ujauzito atakusumbua sana.”
DULLAH: “Nishazoea tayari, tunaondokaje Senior?”
MIMI: “Namsikilizia Agent. Alisema kuna uwezekano tukaondoka na ndege tofauti, halafu tukasubiriana Cape Town.”
Wazo la kuondoka na ndege tofauti halikumkaa vizuri Dullah. Hakuwa na uzoefu kabisa wa safari za anga, na alitamani sana tuwe pamoja tangu mwanzo hadi mwisho wa safari.
Baada ya nusu saa kupita bila kupigiwa simu na Agent, niliamua kumpigia mwenyewe. Alinijibu kuwa amepata ndege ya Ethiopian Airlines, lakini ingetulazimu kwanza kupitia Ethiopia, ndipo tuendelee na safari ya kuelekea South Africa.
Ndege ilikuwa imepangwa kuondoka saa sita usiku kuelekea Ethiopia. Niliona hakuna sababu ya kuendelea kupoteza muda pale Airport, hivyo tukakubaliana tuondoke na hiyo ndege. Ilipofika saa sita na nusu, safari yetu ikaanza rasmi. Kwa bahati mbaya mimi na Dullah hatukuweza kukaa pamoja, yeye alikaa seat ya mbele, nami nikakaa upande wa kati.
Tulipowasili Addis Ababa, Ethiopia, tulipata mapumziko ya takribani saa moja kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea South Africa. Kipindi cha kusubiri, mimi na Dullah tulienda kukaa kwenye moja ya migahawa pale Airport, tukajipatia chakula cha haraka. Wakati huo huo, nilikuwa nachat sana na Samantha. Alishangaa mno kusikia niko Addis Ababa, hakutarajia kabisa ningeonekana upande huo kwa wakati huo.
Baada ya hapo, tulianza safari kutoka Addis saa kumi na moja alfajiri kuelekea Cape Town. Safari hii tulikaa pamoja na Dullah, na hapo ndipo mazungumzo marefu yakaanza. Tulizungumza mambo mengi hasa kuhusu maisha, hasa mambo magumu nayoyapitia kipindi hiki.
Nilimwambia Dullah asinione kama nimewin maisha, lakini msoto naopitia ni mkubwa sana hata mara nyingine huwa najutia sana. Nilimwambia jinsi ambavyo ninaumiza kichwa kuhusu suala la Iryn, namna ya kulifikisha kwa wazazi maana ni gumu sana. Kwa upande wake alinitia moyo kwa kuniambia kwamba, nisijilaumu sana sababu haya maisha nayoishi sasa, ndio niliyopangiwa.
Kwa upande wake alinipa habari kubwa zaidi kwamba mke wake Latifah ana mimba ya mapacha wawili, jambo lililothibitishwa baada ya vipimo vya ultrasound. Nilimpongeza kwa dhati kwa habari hiyo njema. Kwa upande wake, Dullah alijaa furaha, na aliendelea kunivimbia pale.
Saa sita mchana ndipo ndege ilipotua Cape Town. Baada ya kumaliza taratibu zote za Airport, nilichukua Uber iliyotupeleka hadi Southern Sun Newlands Hotel, moja ya hotel ambayo nimezoea kufikia kila ninapokuwa mjini hapo. Tayari nilikuwa nimefanya booking kwaajili ya Dullah, hivyo baada ya kufika hotelini, nilimwambia apumzike kidogo, nitamcheki baadaye ili tuende hospitalini.
Niliendelea kuwasiliana na Samantha, naye alinijulisha kuwa yeye yuko hospital, ila nyumbani yuko dada wa kazi, hivyo nisiwe na wasiwasi-niende tu. Baada ya kumuacha Dullah hotelini, mimi nikaendelea na safari ya kuelekea nyumbani kwa Iryn.
Nilipofika, pale getini nilikutana na mlinzi ambaye alinitambua baada ya kuniona, kisha alinisaidia bag langu hadi ndani kwa heshima kabisa. Dada wa kazi alikuja kunifungulia mlango, tayari akiwa na taarifa za ujio wangu kutoka kwa Samantha.
Dada wa kazi alikuwa binti mrembo kutoka Ethiopia, pia nilishangaa sana kuona anaongea Kiingereza, japokuwa kwa shida kidogo, lakini alikuwa anajitahidi kwa nguvu zake zote. Tulipiga story chache za kawaida, kisha akaanza kuniandalia chakula. Kwa kweli sikuwa hata na hamu ya kula, nikamwambia aache. Muda huu mawazo yangu yote yalikuwa hospitalini kwa Iryn. Nikaingia ndani kuoga haraka, nikajiandaa ili niwahi kwenda kumuona mama Aria.
Nilikaa nyumbani pale takribani dakika 30 tu, kisha nikatoka na kurudi hotelini kumpitia Dullah. Baada ya hapo, tukaelekea Mediclinic Hospital. Umbali kutoka hotelini hadi Mediclinic ni kama kilomita 15 hivi ni sawa na safari ya Mwenge hadi Kivukoni. Hii ni hospital ambayo Iryn anaipenda sana, hata Aria alizaliwa hapo.
Njiani, tulipitia kwenye moja ya maduka ya maua, nikanunua ua kubwa zuri kwa ajili ya Iryn. Kwa upande mwingine Samantha alikuwa ameniambia nimjulishe pindi nitakapofika, naye angenisubiri kwenye lobby ya hospitali.
Tulipofika hospitalini, niliingia moja kwa moja ndani maana mazingira hayakuwa mageni kwangu. Mimi na Dullah tulikaa pale reception tukimsubiri Samantha, pis nikamtumia ujumbe wa WhatsApp kumjulisha kuwa tayari nimefika.
Dullah, kwa upande wake, alikuwa haishi kushangaa, akigeuza shingo kila upande, macho yakitembea kila kona ya eneo lile. Ukweli ni kwamba wanawake waliokuwa wakipita na waliokaa pale walikuwa wazuri sana. Nilimsoma kimya kimya, nikamuacha aendelee kusafisha macho yake, sikuhitaji kumkatisha raha wala kumharibia focus yake.
Baada ya muda mfupi, Samantha alifika pale mapokezi. Tulikumbatiana kwa nguvu, kama watu waliokuwa wamekosa kuonana kwa muda mrefu. Baada ya salamu chache, nilimtambulisha Dullah kama mshikaji wangu, kisha tukaanza kuelekea upande wa wodi aliyolazwa Iryn.
Kwa bahati mbaya sikuweza kuingia mara moja kumuona Iryn. Alikuwa yuko na madaktari anahudumiwa, hivyo ilibidi nisubiri kwa muda. Wakati tukisubiri, hamu yangu kubwa pia ilikuwa ni kumuona binti yangu Aria. Nilimuuliza Samantha kama Aria yuko pale hospitalini, akasema yuko na dada yake Iryn.
Nikauliza,
MIMI: “Vivian?”
SAMANTHA: “No, dada yake Brenda.”
MIMI: “Yuko wapi sasa?”
SAMANTHA: “Yuko around, atakuja hapa muda si mrefu. Ngoja nimpigie simu.”
Brenda ni dada yake Iryn ni ndugu kwa upande wa baba. Iryn aliwahi kuniambia habari zake awali, ndiyo maana jina lake halikuwa geni kwangu. Nilikuwa namfahamu hata kwa sura, maana Iryn aliwahi kunitumia picha zao wakiwa pamoja, Brenda ni mzungu kabisa kama baba yake Iryn.
Baada ya kama dakika kumi kupita, Brenda alitokea akiwa amembeba Aria mikononi mwake. Nilipomuona tu, moyo wangu uliniruka Kwa furaha. Nilimsogelea haraka, nikamchukua kutoka mikononi mwa Brenda na kuanza kumbusu bila kujizuia.
“Waow! my girl, you’re so cute.”
Aria alikuwa akinitazama huku akitabasamu, macho yake yaking’aa kwa furaha ya ajabu, kama ananitambua mimi ni baba yake. Tukio lote lilikuwa likishuhudiwa live na Samantha, Brenda pamoja na Dullah.
SAMANTHA: “Kakumiss! Anajua kabisa wewe ni baba yake, huoni alivyo furahi?”
BRENDA: “Are you Insider?” Aliuliza.
MIMI: “Yeah… it’s me.”
BRENDA: “You resemble your daughter.”
Nilitabasamu tu! Ilikuwa ni kauli niliyoipenda sana kuisikia, kauli iliyogusa moyo wangu moja kwa moja. Tulianza kusalimiana vizuri, na Brenda alisema sura yangu haikuwa ngeni kwake kabisa, maana alikuwa ameshaziona picha zangu kupitia Iryn. Mazungumzo yakahamia kwenye hali ya Iryn, na hapo ndipo uzito wa mambo ulipoanza kujionesha.
Samantha alianza kuelezea kilichotokea na alisema Iryn alianza kujikia kichefu chefu na kutapika na baadae Alipatwa na homa kali ghafla, akahisi kizunguzungu kikali na kuanguka. Mwili wake ulikuwa moto sana kiasi cha kutoweza hata kuzungumza vizuri. Hali yake ililazimu akimbizwe hospitalini kwa uangalizi wa karibu.
Nilisikia kifua kinabana, nilitamani sana kujua hali yake kwa sasa. Waliniambia bado hali haijaridhishi hata kuongea hawezi na hana nguvu kabisa. Nikiwa na wasiwasi mwingi, nilianza kumuuliza Samantha maswali ya kijasusi, hasa kuhusu kipindi walichokuwa kwa mzee wake Somerset West. Nilihitaji kujua kila kitu.
MIMI: “Kule kwa mzee, mlikiwa mnashare chakula au mambo mengine na wenyeji?”
SAMANTHA: “Hapana! Kule tulikuwa tunakaa sehemu yetu, kila kitu tulikuwa tunajitegemea.”
MIMI: “Na vipi kuhusu mama mdogo na Iryn, walikuwa wanaishije?”
SAMANTHA: “Shem, unajua dada hampendi yule mama kwa sasa. Walikuwa wakikutana, wanasalimiana tu, ila sio kama zamani walivyokuwa karibu.”
Wakati huo, Dullah aliomba amshike Aria. Alimchukua kwa umakini mkubwa, akamwangalia kwa makini sana usoni. Alishindwa kujizuia, akaongea kwa sauti iliyojaa hisia.
DULLAH: “Senior, umefanana sana na dogo, hongera sana. Hii ni damu yetu asee! Mimi kama Senior hapa sina pingamizi kabisa.”
Nilicheka kwa kivivu, lakini ukweli ni kwamba mawazo yangu hayakuwa pale. Maneno ya Dullah yalikuwa yanapita juu juu tu. Akili yangu yote ilikuwa kwa Iryn. Nilikuwa natamani sana kumuona kwa wakati huo. Kichwani maswali yakaanza kunijia bila mpangilio.
Nilikuwa nawaza pale, Aria anaishije bila mama yake? Anakula nini? Ananyonya maziwa gani?. Nikamuangalia Aria, nikamwangalia tena Samantha, nikahitaji majibu ya haraka kwa maswali yaliyokuwa yakinisumbua moyoni.
MIMI: “Kwasasa Aria anakunywa maziwa gani?”
SAMANTHA: “Anakunywa ya mama yake. Dada alikuwa anayamkamua na kuyahifadhi kwenye fridge.”
MIMI: “Hayajakaa muda mrefu?”
SAMANTHA: “Yakikaa siku tatu huwa tunayamwaga. Mtoto wako hapendi kunyonya kabisa, na dada ana maziwa mengi sana. Ndiyo maana alikuwa anayakamua na kuyahifadhi kwenye fridge.”
Baada ya takribani saa moja kupita, Vivian dada yake Iryn alifika pale tulipokuwa tumekaa. Aliponiona, tulisalimiana kwa furaha na kukumbatiana na bila kupoteza muda, tuliongozana kwenda kumuona Iryn wodini.
Tulipoingia ndani ya wodi, macho yangu yalimuona Iryn kwa mbali. Alikuwa amelazwa, mwili wake umeunganishwa na madrip kadhaa, macho yakiwa yamefumba. Taswira ile ilinifanya nipate mshituko wa ghafla. Hapo ndipo nilipotambua kwa macho yangu mwenyewe kwamba hali yake haikuwa nzuri kabisa.
Nilisogea taratibu hadi pembeni ya kitanda chake, nikamshika mkono kwenye kiganja. Sikuishia hapo, nikamshika mashavuni, na nikahisi alikuwa na joto kali sana.
Kwa muda nilikaa kimya, nikimtazama bila kusema neno, nikihisi uzito mkubwa moyoni. Baadaye nikamgeukia Vivian na kuanza kumuuliza maswali kwa sauti ya chini. Vivian alinieleza kuwa vipimo vilionesha ana Pyrexia, lakini akanituliza kwa kusema hali yake ilikuwa mbaya zaidi jana, na leo kulikuwa na dalili za nafuu, japo bado alikuwa chini ya uangalizi mkali.
Sikukaa sana na nilitoka nje ya wodi ili kuwapa nafasi madaktari na wauguzi kuendelea na majukumu yao, kwani walikuwa wakiingia na kutoka mara kwa mara. Nilibaki nje nikiendelea kuzungumza na Vivian, nikiwa na hamu kubwa ya kujua kama Iryn alikuwa anakula chochote kutokana na hali niliyomuona nayo. Vivian aliniambia anakula japo kwa shida, na wanampa vyakula vyepesi kama supu na uji, pamoja na dripu inayomsaidia kupata virutubisho muhimu mwilini.
Baada ya kuachana na Vivian, nilirudi kukaa pembeni, lakini mawazo yalinizidi nguvu. Kile nilichokiona wodini kilinikaa vibaya sana. Nilianza kuwaza mambo mengi, hadi mawazo yangu yalinipeleka mbali na nikahisi huenda kuna jambo baya limemkuta Iryn, pengine hata kafanyiwa kitu na mama mdogo wake.
Nilijitenga kidogo nikiwa nimezama kwenye mawazo, nikijiuliza nifanye nini. Niliwaza kumwambia mama yangu afanye maombi, lakini kwa wakati huo sikupata nguvu wala namna ya kufanya hivyo. Wakati huo Samantha alikuja pale nilipokuwa nimekaa, akanita kwa sauti ya chini. Aliniaga, akiniambia anaondoka kwenda nyumbani pamoja na Aria ili akamuogeshe, na tukakubaliana kuonana baadaye.
Ilipofika majira ya saa mbili usiku, baba yake Iryn aliwasili hospitalini. Tuliposalimiana, tulianza mazungumzo mara moja. Aliniuliza nimefika lini South Africa, nikamweleza, pamoja na muda tuliowasili hospitalini. Kisha nikamtambulisha Dullah kwake.
Mazungumzo yetu yakajikita zaidi kwenye hali ya Iryn, maana ndiyo iliyokuwa inatisha zaidi. Mzee naye alisema yote yametokea ghafla sana, lakini alikuwa na matumaini makubwa kwamba binti yake atakuwa sawa. Aliniongeza kuwa alikuwa na safari ya kwenda India siku hiyo, lakini kutokana na hali ya Iryn ilibidi aghairi safari hadi pale binti yake atakapopata nafuu.
Ilipofika saa tatu usiku, tulienda kwenye restaurant kupata chakula cha usiku tukiwa watu watano: mimi, Dullah, Vivian, Brenda na rafiki wa Brenda ambaye naye alikuwa amekuja kumjulia hali Iryn kwani walifahamiana. Tulipokuwa tunakula, Vivian alinambia naweza kuondoka kwenda kupumzika kwa sababu ya uchovu wa safari ndefu. Lakini nilimwambia ukweli kwamba moyo wangu ulikuwa bado hospitalini, sikuwa na nguvu ya kwenda kulala, na hata usingizi usingeweza kunipata.
Nilimgeukia Dullah nikamwambia anaweza kwenda hotelini kupumzika, lakini alikataa kabisa. Aliniambia hawezi kwenda kulala wakati mimi niko kwenye wakati mgumu namna ile. Aliahidi atanipa kampani na kubaki nami hadi pale Iryn atakapokuwa sawa.
Ilipofika majira ya saa sita usiku, mzee alituaga mimi na Dullah kisha akaondoka. Baada ya muda, Brenda na Vivian waliungana nasi, na tukaendelea kupiga stori za hapa na pale ili kupunguza mawazo. Katikati ya mazungumzo yetu, nilipata nafasi ya kumuuliza Vivian kuhusu maendeleo ya bibi yao, Momo, na kama anafahamu chochote kinachoendelea kuhusiana na hali ya Iryn.
Vivian aliniambia kuwa Momo hajui kinachoendelea, na wameamua kwa makusudi kumficha ukweli huo kwa sababu wanaogopa anaweza kupata presha akijua mjukuu wake yuko hospitalini katika hali mbaya. Nilimsikiliza kwa makini, kisha nikamwambia wazi kuwa wanakosea sana kumficha bibi yao. Nilimweleza kuwa endapo Iryn atapata shida zaidi, au Momo akija kugundua baadaye kwamba mjukuu wake aliugua na wao wakanyamaza, huenda hatawaelewa kabisa.
Vivian aliendelea kusisitiza kuwa msiba uliotokea Ethiopia ulimuathiri sana Momo, na ndiyo sababu hawakutaka kumpa mzigo mwingine wa mawazo. Nilihisi hoja zake zinaingia kwenye siasa za kifamilia za “kumlinda mtu kwa kumficha ukweli”, jambo ambalo sikuliona kuwa sahihi. Ndipo nikatambua wazi kuwa hapa kuna haja ya kumtafuta Jimmy ili tuzungumze kwa kina kuhusu suala hili.
*****
Asubuhi iliyofuata, nilionana tena na Vivian ili kupata taarifa za maendeleo ya Iryn. Aliniambia kuwa hali yake ilikuwa nafuu kidogo ukilinganisha na jana, japokuwa bado alikuwa chini ya uangalizi mkali. Vivian alituomba sana mimi na Dullah tuende tukapumzike na turudi hospitalini mchana, kwani aliona wazi tumechoka sana. Ingawa nilitamani mno kumuona Iryn asubuhi hiyo, haikuwezekana kwa sababu alikuwa anafanyiwa matibabu na madaktari.
Mimi na Dullah tuliondoka hospitalini kwa kutumia Uber. Nilianza kwa kumwacha Dullah hotelini, kisha nikaendelea hadi nyumbani. Nilipofika, nilimkuta Samantha akiwa na Aria sebleni, wakicheza. Aria alionekana mwenye furaha, uso wake ukiwa umejaa tabasamu. Nilimuuliza Samantha kama mtoto anamsumbua, akaniambia Aria ni mtulivu sana.
Nilimnyanyua Aria juu, nikakaa naye kwenye sofa kwa muda, tukacheza kidogo. Baada ya mazungumzo mafupi na Samantha, nilihisi uchovu mzito ukinizidi nguvu, hivyo nikaenda kulala.
Niliamka saa saba mchana, nikakuta simu yangu imejaa missed calls nyingi, hasa WhatsApp. Ghafla nikakumbuka kuna jambo muhimu sana la ofisini ambalo nilitakiwa kulisimamia, lakini niliondoka bila kumpa Lucy taarifa. Bila kupoteza muda, niliamua kumpigia simu Lucy.
Baada ya kuita kwa sekunde kadhaa, Lucy alipokea, sauti yake ikiwa na wasiwasi:
LUCY: “Insider, mbona simu zako hazipatikani? Tangu jana usiku nakutafuta.”
MIMI: “Lucy, niko South Africa. Iryn anaumwa sana, amelazwa hospitalini.”
LUCY: “What? Tangu lini? Anaumwa nini?”
MIMI: “Acha tu rafiki yangu, alipata homa kali sana na kizunguzungu cha ghafla, ndiyo maana akalazwa.”
LUCY: “Pole sana. Sasa anaendeleaje?”
MIMI: “Lucy hali ni mbaya rafiki yangu, bado hali hairidhishi.”
Baada ya maelezo hayo, Lucy alipaniki sana. Aliniomba niwe nampa taarifa kwa kila kinachoendelea kuhusu Iryn. Hakuwa na tena hamu ya kujadili masuala ya ofisi, akaniambia tuzungumze baadaye.
Kwa upande mwingine, Erica alikuwa amenipigia sana, lakini sikuona umuhimu wa kumpigia kwa wakati huo. Badala yake nilimpigia simu Dullah kujua hali yake, lakini hakupokea. Nikahisi huenda bado alikuwa amelala kutokana na uchovu wa safari na tukio la usiku kucha, hivyo nikamtumia ujumbe kwamba akiamka ani-check.
Nilishuka kitandani na kuelekea sebleni niliposikia Aria akilia. Nilipofika, nilimkuta Samantha anamvalisha nguo. Nilisita kidogo nikimuangalia, kisha nikasema kwa utani:
MIMI: “Nakuona umeshazoea kulea, kilichobaki na wewe upate mtoto wako kabisa.”
Samantha aliniangalia na kutabasamu kwa upole.
SAMANTHA: “Mwanao anapenda sana kuoga. Nimemtoa kwenye dishi akaanza kulia.”
MIMI: “Muda wote nakuona wewe na mtoto. Dada wa kazi anajua kucheza naye?”
SAMANTHA: “Yeah, anajitahidi sana. Na Aria si mtoto wa kulialia, si naona mama yake hayupo, lakini katulia tu.”
Nilisogea karibu yao na kukaa kwenye sofa, kisha nikamwuliza swali lililokuwa likinisumbua sana:
MIMI: “Kwanini hamjamwambia bibi kuhusu Iryn kuumwa?”
SAMANTHA: “Hata mimi sijui kwanini hawataki kumwambia. Akija kujua mjukuu wake aliugua na tukanyamaza, atatuchukia sana.”
MIMI: “Mwambie bibi kuhusu hali ya Iryn. Wewe unaishi naye hapa, na wewe ndiyo wa kwanza kukutana na athari za jambo hili.”
SAMANTHA: “Nitaongea na dada Vivian. Ila ukweli ni kwamba tangu ule msiba wa nyumbani, hali ya bibi haiko sawa kabisa, ndiyo maana wanaogopa.”
Nilikaa kimya kwa muda nikifikiria, kisha nikaona wazi kuna haja ya kuwasiliana na Jimmy. Sikupoteza muda, nikatoka nje kibarazani kumpigia simu, lakini hakuwa online. Nilirudi ndani nikamuuliza Samantha kama Jimmy ana namba nyingine. Bila kusita, akanipa. Nilipiga ile namba nyingine, simu ilikuwa online lakini haikupokelewa. Nikamuandikia ujumbe mfupi, nikimwambia akija online anicheki haraka, maana suala ni urgent.
Niliendelea kucheza na Aria pale sebleni, nikijaribu kumpa muda na mapenzi ya baba, ingawa mawazo yangu mengi yalikuwa bado hospitalini. Ilipofika saa kumi na moja jioni, nilianza kujiandaa kwenda hospitali. Kwa upande mwingine, Dullah alikuwa tayari kanicheki, nikamwambia achukue Uber aelekee hospitalini na tutakutana pale.
Mimi na Samantha tuliondoka pamoja kuelekea hospitalini, tukawahi kufika kabla ya Dullah. Tulipoingia, tulienda moja kwa moja hadi kwenye waiting area. Hapo ndipo nilipokutana na kaka yake mkubwa wa Iryn upande wa baba, kaka yake wa kwanza kabisa.
Baada ya kusalimiana, tulianza mazungumzo ya hapa na pale. Nilimuuliza kama tayari amefanikiwa kumuona Iryn, akaniambia bado hajapata nafasi, maana naye hakuwa amekaa muda mrefu hospitalini. Kwa ujumla, kulikuwa na ndugu na marafiki wengi wa Iryn kutoka chuo na sehemu mbalimbali, hali iliyodhihirisha wazi namna alivyopendwa.
Nilimtafuta Vivian ili nipate taarifa za maendeleo ya Iryn. Baada ya kuonana naye aliniambia kuwa kwa sasa hali yake imeanza kuimarika, japokuwa bado hakuwa sawa kabisa. Nilimuuliza kama kuna chochote kinahitajika, nikamwambia asisite kuniambia. Akanihakikishia kuwa hakuna shida yoyote kwa sasa, labda mahitaji madogo ya kwenda kununua supermarket.
Kwa kuwa Vivian alikuwa bize sana na majukumu mengi, sikutaka kumpotezea muda. Nilirudi kukaa, na nikamkuta Dullah tayari ameshawasili. Nilisogea karibu naye, tukaanza mazungumzo, na swali lake la kwanza lilikuwa ni maendeleo ya Iryn.
Ghafla simu yangu ikaanza kuita. Nilipoangalia nikagundua ni Jimmy, bila kusita niliipokea. Jimmy alianza kwa kuniomba radhi kwa kuchelewa kupokea simu zangu, kisha akanipa pole kwa yaliyoikumba familia. Aliniambia yuko UK kwa shughuli fulani lakini ana mpango wa kuungana nasi muda si mrefu.
Baada ya mazungumzo marefu, nilimfungulia mada ya kumficha bibi, Momo, kuhusu hali ya Iryn. Nilimweleza kuwa kuna haja kubwa ya bibi kujua ukweli. Jimmy alikiri kuwa walimficha kwa nia ya kulinda afya yake kutokana na msiba wa hivi karibuni, lakini baada ya kujadili kwa kina, alikubaliana nami kuwa Momo anatakiwa kupewa taarifa. Hatimaye tukafunga mazungumzo kwa Jimmy kuahidi kuwa atazungumza na bibi kuhusu hali ya Iryn.
Baada ya takribani nusu saa kupita, mama mdogo wa Iryn aliwasili hospitalini akiwa ameongozana na watoto wake wawili wa mwisho. Nilipomuona, nilisogea na kumsalimia. Hatukuwa na mazungumzo marefu, maana kwa muda mrefu sikuwa namkubali sana, hivyo niliamua kurudi kukaa karibu na Dullah.
Baada ya dakika chache, Samantha alinijia na kuniomba nimpe kampani ya kwenda supermarket kununua matunda na mahitaji mengine kwa ajili ya mgonjwa. Nikampa taarifa Dullah ya kuondoka, nikambeba binti yangu Aria na kuondoka.
Tulikaa zaidi ya saa moja supermarket tukinunua mahitaji mbalimbali ya Iryn. Baada ya hapo tulirudi hospitalini. Tulipofika, tulikuta mama mdogo alikuwa tayari ameondoka, lakini kaka yake Iryn bado alikuwepo. Nilimuuliza kama alikuwa amefanikiwa kumuona Iryn, akaniambia amemuona, ila bado anaona hali yake haijaridhisha.
Ilipofika saa nne usiku, nilipata nafasi ya kuingia wodini kumuona Iryn. Mara hii niliona tofauti kidogo ukilinganisha na jana. Alikuwa anaweza kuongea, japokuwa kwa shida sana. Nilimshika mkono, na niliona wazi furaha usoni mwake aliponiona, hata tabasamu lake lilikuwa dhahiri. Sikupenda kumchosha, hivyo nilimuacha apumzike, nami nikaendelea kukaa wodini kwa muda nikizungumza na Vivian.
Baada ya takribani saa mbili, nilitoka nje kwenda kumpa kampani Dullah. Nilishangaa kumkuta bado yuko pale pamoja na kaka yake Iryn. Nikajiunga nao, tukaanza kupiga story mbalimbali ili kupunguza muda. Nilikumbuka nilikuwa nimenunua last cards pale supermarket, hivyo tukaanza kucheza karata.
Kadri tulivyoendelea kucheza, niligundua kuwa kaka yake Iryn ni mtu poa sana na yuko real, mcheshi na mzungumzaji mzuri. Alikuwa anatupatia story nyingi kuhusu South Africa na maisha ya huku, hasa masuala ya wanawake. Dullah alikuwa anafurahia sana kusikiliza story hizi maana jamaa alikuwa anatoa mbinu mbalimbali za kuwavuta wanawake wa huku, story zilizotufanya kucheka mara kwa mara.
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, huyu kaka yake Iryn-tuseme jina lake ni ‘Scott’ ni mtoto wa kwanza wa mzee Virgil, aliyezaliwa na mwanamke mwingine wa South Africa. Ana mchanganyiko wa kizungu na kiafrika, kwa mbali ni kama chotara.
Baada ya story nyingi, Scott alianza kuniuliza maswali kuhusu Iryn, hasa akitaka kujua jinsi tulivyofahamiana:
SCOTT: “So bro, how did you meet my sister?”
MIMI: “It’s a long story! I thought she told you.”
SCOTT: “We are not talking much yet. You know, I’m still getting to know her slowly, but I like my sister. She’s a very serious person.”
MIMI: “And what about you?”
SCOTT: “She always says I’m not a serious person.”
MIMI: “If she’s telling you that, then you need to change.”
SCOTT: “Hahaha! But still, you haven’t told me how you met my sister.”
MIMI: “Ask her, She’ll tell you everything.”
Baada ya mazungumzo mengi na vicheko, Scott alituaga akisema anaondoka kwenda kulala. Alituacha mimi na Dullah pale hospitalini, tukibaki na mawazo yetu, tukisubiri kesho ije na matumaini mapya kwa afya ya Iryn.
*********
Kufikia Jumapili, hali ya Iryn ilianza kuonyesha dalili za kuimarika kwa kasi. Aliweza kuongea vizuri zaidi, japo bado kwa taratibu. Sasa asubuhi ile niliingia wodini nikiwa na Dullah, nikamtambulisha rasmi kwa Iryn. Ukweli alifurahi sana uwepo wetu pale.
Nilimsogelea, nikamshika mkono wake na kuanza kuzungumza naye kwa upole. Alikuwa akinitazama kwa macho yenye furaha, ishara wazi kwamba uwepo wangu ulimpa nguvu.
MIMI: “How are you feeling?”
IRYN: “At least najisikia nafuu kidogo. Unaona naweza kuongea sasa, japo kizunguzungu bado kinanisumbua.”
MIMI: “Pole sana mke wangu, utakuwa sawa kabisa. Aria amekumiss sana mama yake.”
IRYN: “Amem-miss pia baba yake. Sasa hivi atakuwa na furaha kuwa na baba yake karibu”
Tuliishia kucheka wote pale na akaendelea kuongeza;
IRYN: “Thank you so much for the beautiful flowers”
MIMI: “You’re welcome. Umeipenda?”
IRYN: “Yes, sana tu! Si unaona ipo pembeni yangu.”
MIMI: “I really miss everything about you.”
Iryn alinitazama, akatabasamu kwa aibu ya furaha.
IRYN: “I know umemiss sex.”
Nikatingisha kichwa kukubali ndio na nikaanza kumchezea nywele zake,
MIMI: “It’s been such a long time since I last saw it. The coochie was always in my mind, so clear that I could draw it just by closing my eyes. But now that image is slowly disappearing, and it hurts, I really miss it.”
Alibaki akicheka kwa furaha, kisha akasema kwa sauti ya mapenzi:
IRYN: “You always know how to make me smile.”
Niliendelea kumsemesha maneno ya faraja na mapenzi. Baadaye Samantha aliingia wodini akiwa na Aria ili amuone mama yake. Zlikuwa ni dakika chache zenye hisia nzito sana. Baada ya muda mfupi, baba yake Iryn aliingia wodini akiwa ameongozana na mama mdogo wake. Niliwasalimia wote, kisha mimi na Dullah tukatoka nje kuwapa nafasi ya kifamilia.
Tulielekea kwenye restaurant ya hospitali kunywa chai. Tukiwa pale, simu yangu ilianza kuita kupitia WhatsApp. Nilipoangalia nikaona jina la Sanchi, niliipokea mara moja.
Sanch alilalamika kwamba amekuwa akinipigia simu bila mafanikio. Nilimweleza kuwa niko South Africa. Akaendelea kuniambia kuwa Erica amekuwa akimpigia simu, akilalamika kwamba hanipati, na kuna nyaraka muhimu nilitakiwa kuzisaini ili kazi ikamilike. Nilimwahidi Sanchi nitawasiliana na Erica na kupanga utaratibu.
Baada ya hapo, Sanch alibadilisha mada:
SANCH: “Huyu dada ni nani hadi anakuulizia hivyo? Mbona ana wasiwasi sana juu yako?”
MIMI: “Unaniuliza wakati unajua yuko ofisi gani.”
SANCH: “Hapana, sisi wanawake tunajuana. Kama sio mpenzi, basi anakutaka, hivi unajua ananipigia sana kukuulizia.”
MIMI: “Ni masuala ya ofisi tu, yeye ndo ananisaidia kuhakikisha lile jambo letu linakamilika.”
SANCH: “Na unarudi lini Bongo?”
MIMI: “Probably next week, nitaanzia Dodoma.”
Baada ya mazungumzo hayo, nilimpigia Erica lakini hakupokea. Nikamtumia ujumbe wa kumsalimia. Nilijaribu kumpigia pia mama J, hakupokea, nikahisi yuko kanisani-nikamtumia ujumbe wa kumsalimia. Niliendelea kuipitia simu yangu nikijibu watu wachache muhimu tu. Pia nilikuta jumbe mbili kutoka kwa Hilda, lakini sikuona umuhimu wa kujibu kwa wakati huo.
Wakati huo Dullah alianza kuzungumza:
DULLAH: “Shemeji yako Latifah anauliza nitarudi lini Dar, ana wasiwasi sana.”
MIMI: “Hali ya mama mtoto inaendelea kuimarika, by next week tunarudi Dar.”
DULLAH: “Tangu mimba ya kwanza ya Latifah iharibike, mapenzi yake kwangu yameongezeka sana.”
MIMI: “Hujawahi kuniambia sababu ya ile mimba kuharibika.”
DULLAH: “Uzembe wake ulisababisha.”
MIMI: “Kila jambo na wakati wake. Angalia sasa mna mapacha.”
DULLAH: “Naogopa hata hii mimba inaweza kuharibika tena.”
MIMI: “Haiwezi! Cha muhimu azingatie lishe na ajitunze vizuri.”
Dullah akanitazama, akasema kwa uzito:
DULLAH: “Insider, unaishi maisha ya ndoto yako sasa.”
Nilicheka kidogo.
MIMI: “Kwanini unasema hivyo bro?”
DULLAH: “Unasafiri kwa ndege kumwona mtoto wako na mama yake. Una mwanamke mzuri, mwenye hadhi, na familia inayokupenda na kukuheshimu. Haya maisha wachache sana wanaume wanayaishi. You’re lucky, bro.”
Nilitabasamu, lakini moyoni niliona kama ni jambo la kawaida tu. Kadri siku zilivyozidi kwenda, nilikuwa namuona Iryn kama mwanamke wa kawaida tu kwenye maisha yangu.
Hospitalini, ndugu na marafiki wa Iryn walikuwa wakimiminika kwa wingi. Baadhi yao walitamani sana kunifahamu. Kwa kuwa Iryn ni mwanamke mwenye hadhi na heshima, maswali kuhusu baba wa mtoto yalikuwa mengi. Wengi walinishangaa, hasa kwa jinsi nilivyofanana sana na Aria, jambo lililonifanya kuwa gumzo.
Siku hiyo ya Jumapili wageni walikuwa wengi sana kutoka sehemu mbalimbali, kadri walivyopata taarifa ndivyo walivyozidi kumiminika. Wengi wao walimuulizia au walitaka kumuona na kumbeba Aria, jambo ambalo halikunipendeza. Kwa hofu ya usalama wake, mara nyingi tulijitenga na kukaa naye sehemu nyingine kabisa ili kumlinda. Hatukuruhusu kila mtu kumbeba; ni watu wa karibu sana pekee ndio tuliowaamini na kuwapa mtoto.
Baada ya kuona msongamano wa watu ukiongezeka, nilimwambia Samantha tuondoke na Aria turudi nyumbani kupumzika, tukiwa na Dullah. Hata pale nyumbani, pia kulikuwa na wageni wachache ambao wengi wao walikuwa ndugu na marafiki wa karibu.
Ilipofika saa kumi na mbili jioni, simu ya Jimmy iliingia. Alinijulisha kuwa yuko airport na wamefika salama. Habari iliyonifurahisha zaidi ni kwamba alikuwa ameongozana na Bibi. Alisema bibi amegoma kabisa kwenda kupumzika, anataka kwanza kumuona Iryn hospitalini.
Habari ile ilinipa faraja kubwa sana moyoni na bila kupoteza muda, nilimwambia Dullah tuondoke mara moja kuelekea hospitalini.