Kuna dada mmoja, jina lake linaanzia na G, chotara wa Ethiopia na South Africa. Aliwahi kunitafuta Instagram akiwa na uhitaji mkubwa wa cheti cha kuzaliwa ili apate NIDA. Nikamuunganisha na madalali wa RITA. Cha kushangaza, kuna code nyingi sana zinazofanana na hii story. Alikuwa na jamaa aliyekuwa anasoma Masters UDSM, ambaye pia alikuwa mchepuko wake, na mambo yakafanikiwa.
Lakini ilipofika hatua ya kufuatilia masuala ya NIDA, kulikuwa na kiasi kilitakiwa aingize jamaa yuleyule. Tangu Januari, jamaa akawa hapatikani kabisa. Juzi Jumamosi nikiwa Sinza, nikaambiwa yeye na mchepuko wake walipata ajali mbaya na kufariki wote maeneo ya Kimara.
Sisemi ni INSIDER, lakini kuna vitu vingi sana kwenye hadithi hii vinafanana kwa kiwango kinachotia hofu. MODS tafadhali fuatilieni, nina wasiwasi wa kama asilimia 60 huenda ni yeye.