Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 3
CHAPTER 18

A TRUE STORY BY INSIDER MAN

PREVIOUS:
Baada ya kuona msongamano wa watu ukiongezeka, nilimwambia Samantha tuondoke na Aria turudi nyumbani kupumzika, tukiwa na Dullah. Hata pale nyumbani, pia kulikuwa na wageni wachache ambao wengi wao walikuwa ndugu na marafiki wa karibu.

Ilipofika saa kumi na mbili jioni, simu ya Jimmy iliingia. Alinijulisha kuwa yuko airport na wamefika salama. Habari iliyonifurahisha zaidi ni kwamba alikuwa ameongozana na Bibi. Alisema bibi amegoma kabisa kwenda kupumzika, anataka kwanza kumuona Iryn hospitalini.

Habari ile ilinipa faraja kubwa sana moyoni na bila kupoteza muda, nilimwambia Dullah tuondoke mara moja kuelekea hospitalini.

CONTINUE:

Ukweli ni kwamba, mara tu Bibi alipowasili South Africa, nilihisi kama mzigo mzito umeondoka mabegani mwangu. Ndani ya nafsi yangu niliamini kabisa kwamba, kama kuna jambo lolote baya lilikuwa linaendelea kuhusu Iryn, basi Bibi angegundua ukweli mapema au baadaye, hivyo uwepo wake ulinipa matumaini mapya.

Samantha alituomba tumsubiri kidogo ajitayarishe ili tuondoke wote kwa pamoja. Hatukuwa na namna nyingine zaidi ya kumsubiria. Baada ya kumaliza kujiandaa, alitokea seblen akiwa tayari kuondoka, lakini kabla hata ya kuchukua mkoba wake, alisimama ghafla kama amekumbuka jambo muhimu.

Kwa sauti ya wasiwasi aliuliza,


“Shem, vipi kuhusu Aria? Tumuache au tuondoke naye?”

Kwa wakati huo Aria alikuwa amelala fofofo. Nilifikiria haraka na kuona ni busara kumuacha aendelee kupumzika, hasa ukizingatia kwamba hakuwa amelala muda mrefu, haikuwa sawa kumsumbua bure.

Uber yetu ilikuwa tayari imeshawasili nje, hivyo tukatoka kwa haraka na kuanza safari ya kuelekea hospital. Njiani, Samantha hakuacha kuniuliza maswali kuhusu Bibi. Alitaka kujua ni nini hasa kilichokuwa kinaendelea hadi ikafikia hatua ya Bibi kupewa taarifa za kuumwa kwa Iryn?. Niliona hakuna maana ya kuendelea kuficha, hivyo nikamwambia ukweli wote kwamba huu ulikuwa mpango wangu na Jimmy, hadi Bibi alipofika South Africa.

Tulipofika hospitalini, nilimwona Jimmy amekaa eneo la kusubiria wagonjwa. Tukasalimiana kwa kukumbatiana, alionekana kufurahi sana kuniona. Alinipa pole kwa yote yaliyokuwa yakiendelea, kisha mazungumzo yetu yakahamia moja kwa moja kwa Bibi.

Jimmy aliniambia kuwa jana, Jumamosi, baada ya kurudi nyumbani Ethiopia, alikutana na Bibi na kumweleza ukweli kuhusu Iryn kuugua na kulazwa hospitalini. Baada ya kusikia habari hizo, Bibi alipanic sana maana hakupendezwa na maamuzi yao.

Alilalamika kwa uchungu, akihoji ni kwa nini walimficha ukweli wakati mjukuu wake alikuwa wodini kwa siku kadhaa bila yeye kujua chochote. Ilimchukua Jimmy muda kumtuliza Bibi, ndipo wakapanga safari ya haraka ya kuja South Africa. Mara tu walipowasili, jambo la kwanza Bibi alilolifanya hospitalini lilikuwa kuomba kumuona mjukuu wake.

Nikamuuliza,


MIMI: “Kwahiyo tangu aingie ndani hajatoka?”


JIMMY: “Yes! Ni almost masaa mawili sasa.”

Nikamuuliza tena kama yeye alikuwa amefanikiwa kumuona Iryn, lakini akanambia bado, kwa sababu hali yake haikuruhusu kuonana na wanaume kwa wakati huo. Baada ya kumaliza maongezi kuhusu bibi, nikamuuliza hali ya familia kwa ujumla, Jimmy alicheka sana kabla ya kusema,


JIMMY: “Bro, nina expect mtoto mwingine.”

Nilishtuka kidogo nikamuuliza,


MIMI: “Mama mwingine?”


JIMMY: “Hapana, ni Amara bro-ananizalia mtoto wa Pili.”

MIMI: “Hongera sana bro! Ufanye mpango uoe huyo mwanamke.”

Jimmy aliishia kucheka, sababu yeye alishanitamkia hawezi kuoa na hajawahi kuwa na huo mpango.

Baada ya mazungumzo ya awali, nilimtambulisha Dullah kwa Jimmy kama rafiki yangu wa karibu sana. Walipokuwa wakisalimiana, ghafla sauti ya Samantha ilisika kwa nguvu akimuita kaka yake huku akija mbio. Muda ambao tunaingia hospital Samantha alipitia dukani mara moja kuchukua mahitaji ya Iryn.

“My brother Jimmy!”

Waliishia kukumbatiana kwa nguvu, na ilikuwa wazi kwamba Samantha alikuwa kam-miss sana kaka yake. Kutokana na hali ile, mimi na Dullah tuliamua kuwaacha na kwenda kukaa pembeni.

Baada ya kukaa, Dullah aliniuliza kwa sauti ya chini,


“Senior, huyu jamaa ni nani hasa?”

Nikaanza kumweleza kwa utulivu kwamba ni cousin wa Iryn, kama kaka yake-mtoto wa mama yake mkubwa kutoka Ethiopia. Dullah alicheka na kuniambia kwa mzaha kwamba nimejenga connection kubwa sana ya watu. Nilicheka kwa sauti na kubadili mada haraka.

Muda mfupi baadaye, Brenda alikuja upande wetu, akatusalimia kisha akanijulisha kuwa Iryn anahitaji kuniona na aliagiza nipewe taarifa hii, pindi tu nitakapofika hospital. Bila kupoteza muda, niliinuka na kuelekea wodini. Nilipofika, nilikuta Bibi amekaa kitandani na Iryn, wakiongea kwa utulivu.

Nilimsalimia Bibi kwa heshima na kumbusu shavuni. Kwa upande wake alifurahi sana kuniona, nami pia nilijaa furaha sana kumuona. Baada ya mazungumzo mafupi, Bibi alituaga akisema anaenda kupumzika na pia kumuona kitukuu wake Aria. Akaondoka pamoja na Vivian, na muda mfupi baadaye wauguzi wote walitoka wodini pia. Ghafla tukabaki mimi na Iryn peke yetu mle ndani.

Tulianza kutazamana kwa sekunde kadhaa kabla Iryn hajavunja ukimya.

IRYN: “Baby, funga mlango.”

Bila kuuliza sababu, nilitii. Niliporudi nikasogea karibu yake, nikakaa kando ya kitanda. Iryn naye alinyanyuka kidogo, akasogea zaidi na kulaza kichwa chake mapajani mwangu.

MIMI: “How are you feeling?”

IRYN: “Leo niko sawa Darling. Hata kizunguzungu sisikii.”

MIMI: “Usijali baby, doctor nipo karibu na leo lazima turudi home pamoja.”

Akatabasamu kwa upole, kisha sauti yake ikabadilika;

IRYN: “I miss my daughter, Aria.”

MIMI: “She’s doing fine, and I’m taking good care of her. Halafu kwanini uliniambia nifunge mlango?”

IRYN: “I need some privacy with you. You know how much I miss you?”

MIMI: “I know baby, hata mimi nimekumiss sana. Bibi amesema nini?”

Huku akicheka kwa taratibu;

IRYN: “Amenifanyia miracles zake hapa. Utamweza Bibi?, kasema anaenda home kuendelea kunifanyia.”

Tulibaki tukicheka wote pale;

MIMI: “Wanakuachia lini urudi home?”

IRYN: “Kama nitaendelea kuimarika hivi, hata kesho wanaweza kuniruhusu.”

MIMI: “Basi mimi nipo na wewe hadi upone kabisa, na leo nakesha hapa mpaka asubuhi.”

Maneno yangu yalimfanya atabasamu zaidi, akajisogeza karibu yangu kama mtoto anayehitaji faraja. Niliendelea kumdekeza taratibu huku nikimnong’oneza maneno matamu ya kumtia moyo. Baada ya kama dakika ishirini, Jimmy aliingia wodini kumwona dada yake. Niliona ni vyema kuwapa nafasi, hivyo nikanyanyuka kimya kimya na kutoka nje.

Nilikwenda kumuona Vivian hasa ili nipate kujua maendeleo ya Iryn na msimamo wa madaktari kuhusu lini anaweza kuruhusiwa kurudi nyumbani. Kwa utulivu, Vivian aliniambia kuwa kama hali ya Iryn itaendelea kuwa nzuri, basi kufikia Jumanne angeweza kuruhusiwa. Kwa upande wangu nilishangaa kutomuona Bibi maeneo yale, ndipo Vivian akaniambia kuwa tayari alikuwa ameondoka pamoja na Samantha kwenda kumuona Aria.

Hapo ndipo nilipochukua nafasi ya kuendelea na mazungumzo ya kina na Vivian. Maswali yangu hayakuwa ya juu juu tu!, bali nilikuwa nachimba ukweli, hasa kuhusu mimi na Iryn. Nilifahamu wazi kuwa mama yake (mama mkubwa wa Iryn) hakuwa na furaha na ukweli kwamba mimi ndiye baba wa mtoto wa binti yake. Ndani ya nafsi yangu niliamini kuwa Vivian angeweza kunipa majibu ya kweli zaidi kuliko hata Iryn mwenyewe.

Vivian hakuzunguka na aliniambia wazi kuwa ni kweli mama yake hakufurahishwa na Iryn kupata ujauzito na mwanaume ambaye, kwa mtazamo wake, hana mustakabali kwa maisha yake. Aliongeza kuwa kabla ya mama yake Iryn kufariki, mama mkubwa ndiye aliachiwa jukumu la kumsimamia Iryn.

Vivian aliendekea kunambia kwamba asilimia kubwa ya familia na ndugu ipo upande wa Iryn. Na point yao muhimu ni kwamba Iryn ni mtu mzima na ana haki ya kufanya maamuzi yake mwenyewe. Ila kiuhalisia hakuna mzazi ambaye angefurahi kuona binti yake akizalishwa na mume wa mtu.

Nilimuuliza kwa nini mama mkubwa hajamtembelea Iryn hospitalini hadi sasa, nikihisi huenda kuna mgongano fulani kati yao. Vivian alinituliza kwa kuniambia kuwa mama yake yuko bize sana na kazi, lakini atakuja kumuona Iryn muda wowote.

Tulipokuwa katikati ya mazungumzo, Jimmy alitokea na kuungana nasi, akimtania dada yake kama kawaida yake. Vivian aliondoka kwenda kuendelea na majukumu yake ya kumhudumia mgonjwa, nami nikabaki na Jimmy. Aliniomba nimpe kampani ya kwenda Clifton Beach akakutane na rafiki yake. Nikaona isiwe tabu kwenda kutembea kidogo ili hata Dullah ayafahamu mazingira ya South Africa.

Haukuwa mwendo mrefu sana mpaka tunawasili pale, Jimmy alionana na rafiki yake. Waliongea kwa muda mfupi, kisha tukapanda gari yake na kuondoka. Njiani Jimmy akasema tunaelekea Saint Lounge kupoteza muda, mtaa wa Harrington-sehemu ambayo wenyeji wa huku bila shaka wanaifahamu. Kwa mwanzo sikukubaliana na wazo la kwenda kufurahia bata wakati Iryn bado anaumwa. Niliona ni jambo lisilo na busara kabisa, halafu ni kumfanyia ukatili Iryn, pia ningeonekana sijali kuhusu afya yake.

Nilimwomba Jimmy aende na Dullah, kisha mimi aniache nirudi hospital kukaa na Iryn ukizingatia nilikuwa nimemuahidi. Jimmy hakukubaliana na ombi langu na akanieleza kuwa anataka tupige story za mwisho maana kesho anarudi Ethiopia, na akaongeza kuwa Iryn tayari anaendelea vizuri, hivyo sina sababu ya kuwa na wasiwasi mwingi. Nilikaa kimya kwa muda, kisha nikakubali kimyakimya. Ukweli ni kwamba nilitamani pia Dullah akitembea mitaa tofauti ya South Africa, apate kumbukumbu za kusimulia nyumbani.

Tulipowasili pale ilikuwa kama saa tatu usiku. Eneo lilikuwa na pilika nyingi kama magari yakipishana, watu wakishuka na kupanda, wengine wakiwa wamesimama vikundini. Sisi tuliingia ndani na tulikaa kwenye meza iliyokuwa imejificha pembeni kabisa. Vinywaji viliagizwa, na tukaanza kunywa taratibu huku tukipiga story za kawaida, mimi nilikuwa nikiongea zaidi na rafiki wa Jimmy ambaye niligundua walisoma chuo kimoja.

Mimi na Jimmy maongezi yakaendelea;

JIMMY: “Bro, December unakuja Ethiopia?”


MIMI: “Nitakuja na familia yangu, Iryn pamoja na Aria”


JIMMY: “Umefanana sana na Aria, yule ni damu yako ni copy and paste.”

Nilicheka, naye akaongeza:


JIMMY: “Do you like the area?”


MIMI: “Very nice, na vibe iko juu sana.”


JIMMY: “Hata warembo wapo wa kutosha ni maamuzi yako.”

Nikacheka tena, kisha nikamgeukia Dullah:

MIMI: “Senior! Kuna mrembo umemuelewa?”

Dullah alinyamaza kwa sekunde chache, akitabasamu huku akiniangalia tu,

DULLAH: “Kaka, Masaki tumezunguka sana, ila hapa funga kazi. Kila manzi namuona mzuri dadeki.”

MIMI: “Kuna uliyemuelewa uondoke naye? Niko standby.”

DULLAH: “Hahaha, subiri kwanza.”

Ilipofika karibu saa tano usiku, Samantha alininitumia ujumbe WhatsApp kuniuliza nilipo, akaniambia Iryn ananiulizia alijua niko home na anataka kuongea nami. Nikamwambia niko na Jimmy na nitarudi muda si mrefu.

Nikiwa naendelea kuandika ujumbe mwingine nimtumie Samantha, mara Jimmy akanigeukia na kunambia;


JIMMY: “Bro, my sister wants to speak with you.”


MIMI: “Samantha already told me, so what are we gonna do?”

JIMMY: “Lets go out in the car.”

Tukaenda nje hadi parking kwenye gari. Wakati tunaingia ndani ya gari-simu ya Jimmy ikaita tena, palepale akaipokea na kuweka loudspeaker. Sauti ya Iryn, tulivu lakini yenye uzito, ikasikika:

IRYN: “Jimmy, where are you?”

JIMMY: “At Harrington, taking care of some business.”

IRYN: “What business is this at this time of night with Insider?”

JIMMY: “So you’re fully recovered and now you start causing trouble?”

IRYN: “Put him on the phone, please!”

Jimmy akanipa simu:


MIMI: “Baby, are you okay?”


IRYN: “Upo wapi na kaka Jimmy?”


MIMI: “Hata sijui, unajua mimi huku ni mgeni.”


IRYN: “Bibi anakuulizia home, alitaka muongee kabla hajalala.”

Jimmy haraka akaingilia maongezi yetu;


JIMMY: “Momo has been asleep for a very long time, leave Insider alone.”

IRYN: “Jimmy! Please!”

JIMMY: “Put my sister Vivian on the phone.”

Baada ya maongezi mafupi na Vivian, Jimmy akakata simu na tukarudi ndani. Baada ya nusu saa hivi, rafiki yake Jimmy alituaga anaondoka. Sisi tuliendelea kufurahia siku yetu na baadae warembo wawili waliopewa mwaliko na Jimmy, wakaungana nasi. Ilipofika saa saba, nasi tukaondoka, lakini Jimmy aliondoka na wale warembo wawili kwenda hotelini, lakini kwa upande wa Dullah ilikuwa tofauti, yeye aligoma kabisa kuondoka na mrembo.
******

Asubuhi kulipokucha nilifanya mazungumzo marefu sana na Bibi, hasa kuhusu mustakabali wa Aria. Bibi alianza kwa kuuliza kama suala la mtoto tayari linafahamika nyumbani. Nilimwambia bado, lakini nipo kwenye mchakato wa kuhakikisha wazazi wangu wanapata taarifa kwa wakati na kwa utaratibu mzuri.

Bibi alipendekeza kuwa kabla ya kwenda Ethiopia Desemba, ingekuwa vyema Aria akaanza kwenda kwa wazazi wangu kwani ndiko ukoo na asili yake ilipo. Baada ya kumaliza suala hili, aliniuliza pia mipango yangu kwa Iryn. Kuhusu suala la Iryn, tuliacha kiporo na alisema mengi yatazungumzwa Iryn atakaporudi nyumbani, kwani bado ana mengi moyoni na hawezi kutamka mbele ya Samantha.(Samantha alikuwa mkalimani wetu).

Saa 4 asubuhi Jimmy alifika nyumbani kuzungumza kidogo na Bibi kisha akamuaga anaondoka kwenda Ethiopia. Mimi nikaingia bafuni kuoga, nikijiandaa kwenda hospital kumuona Iryn. Baada ya kumaliza kujiweka sawa, nikaondoka na Jimmy moja kwa moja kuelekea hospital, safari hii bila kumpitia Dullah kwa kuwa nilijua wazi alikuwa amechoka sana kutokana na hekaheka za jana usiku.

Njiani tulikuwa tukizungumza mambo mengi, hadi Jimmy akaanza kwa kumuulizia Dullah.

JIMMY: “Jamaa yetu yuko wapi?”

MIMI: “Mwache apumzike kwanza, atakuwa hoi sana.”

JIMMY: “Nilipenda sana jinsi urafiki wenu ulivyoanza.”

MIMI: “Bila Dullah huenda nisingekutana kabisa na Iryn.”

JIMMY: “Kama ilikuwa imeandikwa mkutane, mngekutana tu bro.”

MIMI: “God’s plan, hivi wale dada wa jana ulienda nao hotelini wote?”

JIMMY: “Yeah bro… threesome ilikuwa kali! Sana”

Nilicheka kwa nguvu hadi nikakosa cha kusema.

Tulipofika hospitalini, nilimuona Iryn amekaa nje akizungumza na wageni wake. Mwonekano wake ulinipa matumaini makubwa na alionesha hali yake kuimarika sana. Jumla ya wageni walikuwa watano ambapo wanawake wanne na mwanaume mmoja. Baada ya kufika pale walipokuwa wamekaa tuliwasalimia, kisha nikamsogelea Iryn. Nikamshika shavu lake kwa upole, naye akanishika mkono wangu na kuuchezea huku akitabasamu.

MIMI: “Baby, how are you feeling?”

IRYN: “I’m good honey. Nilidhani mnakuja na Aria.”

MIMI: “Aria yuko na Bibi, natumaini baadaye utamuona.”

Kisha Iryn akaanza utambulisho pale. Kwanza akamtambulisha kaka yake Jimmy, halafu akanitambulisha mimi kama baba wa mtoto wake. Baada ya utambulisho huu, akaniegemea maana mimi nilikuwa nimesimama nyuma yake. Baada ya utambulisho ule, wote walinitazama kwa furaha na kusema wamefurahi sana kunifahamu.

Kwa upande wa Jimmy, alikuwa kimya kidogo akiwa anamtazama mmoja wa wanawake aliyekuwepo pale. Ni dada mzuri sana mwenye asili ya uchotara na macho meupe mazuri yaliyovutia sana. Hata yule dada baada ya kuona Jimmy akimtizama kwa macho ya kifisi, alipoteza confidence kabisa.

Iryn aliona kinachoendelea pale, na anamjua vizuri kaka yake ni mtu wa aina gani. Haraka akamuita na wakaanza kuzungumza kwa lugha yao ya asili. Nilihisi wazi kwamba Iryn hakupendezwa na namna Jimmy alivyokuwa akimtazama yule dada. Muda huu, simu ya Dullah iliingia, hivyo nikaenda pembeni kupokea simu.

Baada ya kupokea simu ile, Dullah alianza kwa kuniuliza nilipokuwa. Nikamjibu pale kuwa niko hospitalini, Dullah alinieleza kuwa ameamka muda mfupi uliopita, kutokana na pilika za siku iliyotangulia. Kwa sauti ya lawama ya mzaha, alinilaumu kwa mimi kushindwa kumpitia hotelini ili twende wote hospitalini. Nilimtuliza kwa kumwambia asiwe na wasiwasi, kwani nilijua wazi alikuwa amechoka sana. Zaidi ya yote, nilimhakikishia kuwa maendeleo ya Iryn ni mazuri kwasasa.

Kisha Dullah akanifahamisha kuwa mke wake, Latifah, alikuwa akimsumbua sana kwa simu, akitaka kujua ni lini angerudi nyumbani. Ilikuwa tayari karibu wiki nzima tangu tuondoke, na uvumilivu wake ulionekana kufikia kikomo. Nilimpa moyo kwa kumwambia kuwa tutakapokutana, tutakaa chini, tuzungumze na kupanga kwa busara safari ya kurejea Dar es Salaam.

Mazungumzo yetu yaliendelea kwa muda mrefu, na ghafla, akasema kuwa kabla ya kuondoka, lazima aonje utamu wa mademu wa South. Nilicheka kwa nguvu bila kujizuia, kwani sikutarajia Dullah kuzungumza maneno ya aina ile. Nilimjibu kwa mzaha na kumwambia aniachie hili jambo nitalifanyia kazi.

Dullah alionekana kuwa serious sana kwenye mazungumzo yake, jambo lililonifanya nione kabisa kuna haja ya kumsaidia angalau atimize ile ndoto yake. Ndipo nikamkumbuka mrembo Nala, yule dada niliyemfahamu pale hotelini kwa mara ya kwanza nilipokuwa South Africa na dada yangu, kipindi tulipokuwa tumekwenda kumtafuta Iryn (S2:Chapter 26, 40).

Nala ni mwanamke mwenye asili ya Lesotho, lakini uzuri wake wa sura ulikuwa wa kawaida, lakini kabarikiwa shape nzuri na umbo zuri, hivyo niliona kabisa Dullah angeweza kupona pale. Kwa kuwa nilikuwa bado na namba yake ya simu, nikajisemea moyoni, wacha nimtafute mapema, labda hata tukutane. Nilikuwa nimempa ahadi ya kuonana naye nje ya mazingira ya hotel, lakini kwa muda wote huo sikuwahi kuitimiza.

Nilipofungua WhatsApp yangu kumtafuta Nala, ghafla ujumbe kutoka kwa Hilda ukaingia. Bila kupoteza muda nikafungua ujumbe wake na ulisomeka hivi:

“Insider, so after we slept together, you’re just ignoring me? What’s your plan? You don’t even check on me or reply to my texts.”

Niliona pia jumbe nyingine kadhaa alizokuwa amenitumia bila mimi kuzijibu. Ukweli ni kwamba kipindi niko South Africa sikuwa mtu wa kushika sana simu, pia hali ya Iryn iliniumiza kichwa na ilichukua nafasi kubwa ya mawazo yangu. Kutokana na malamiko yale, niliamua kumpigia Hilda simu papo hapo. Bila kusita, alipokea na tukaanza mazungumzo.

Nilimweleza kwa ufupi kuhusu kuugua kwa Iryn hadi kulazwa hospitalini. Hilda hakuwa na taarifa hizi, hivyo ghafla sauti yake ikabadilika, akawa mpole na kunipa pole, bila kusahau kuulizia maendeleo yake. Nilimwambia wazi kuwa nitakaporudi Dar es Salaam tutazungumza kwa undani zaidi kuhusu mustakabali wetu.

Baada ya maongezi yale, nilijikuta nikitafakari sana. Nilijua wazi hili sakata la Hilda halitakuwa rahisi kulikwepa, lakini moyoni nilijiambia nitapata namna ya kulideali nalo. Kwa upande mwingine, Erica naye alikuwa akinitafuta sana kwa message, akilalamika kuwa hanipati kwa simu wala simjali kwa kumtafuta. Nilizisoma jumbe zake lakini sikujibu, nilipanga kuongea naye nitakapofika Dodoma.

Mchana, Jimmy aliondoka South Africa. Kabla hajaondoka, tulikaa chini tukazungumza mambo mengi, lakini uzito mkubwa ulikuwa juu ya Iryn. Jimmy naye alitaka sana kujua mimi na dada yake tuna mpango gani wa maisha, hasa ikizingatiwa tayari tumepata mtoto. Nilimwambia kuhusu msimamo wangu kuwa Iryn atabaki kuwa mke wangu, na huo ndio mpango wangu kwa sasa. Kwa upande wake, alinishauri nisifanye maamuzi kwa mihemuko wala shinikizo kutoka pande nyingine, alinisisitiza nifanye kama moyo unavyotaka na niwe makini sana.

Baada ya mazungumzo yale mazito, nilibaki nikijifikiria kwa muda na kisha nilimsindikiza nje huku tukipiga stori za hapa na pale. Kabla hajapanda uber na kuondoka, nilimwambia tutaonana Ethiopia mwezi December.

Jioni ile ile, Iryn aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali yake kuimarika. Wakati anaruhusiwa, mama yake mdogo alikuwa hospitalini pamoja na watoto wake, hivyo wakaondoka wote kwenda nyumbani kwa Iryn. Mimi sikuondoka nao bali nilichukua Uber na kuelekea hotelini kuonana na Dullah.

Nilipofika reception, nilikutana na dada wa mapokezi ambaye ananifahamu vizuri, kwani mimi ni mteja wao wa mara kwa mara pale hotelini. Baada ya kusalimiana, nilimuuliza kuhusu mgeni wangu Dullah, naye akanijibu yupo, hajatoka.

Nilielekea moja kwa moja kwenye room ya Dullah. Nikagonga mlango, lakini kulikuwa kimya, hakukuwa na dalili yoyote ya mlango kufunguliwa. Nikahisi labda ametoka, nikarudi tena reception kuuliza, lakini nikaambiwa bado yupo hotelini. Nikaomba wapige simu ya mezani, pia haikupokelewa.

Nikawaza pale, huenda yuko bafuni, hivyo nikarudi tena kugonga, lakini bado ukawa kimya. Ndipo wazo likanijia, wacha niangalie swimming pool. Na kweli, nilipofika pale nikamkuta Dullah aki-enjoy maisha.

Nikamsogelea huku nikicheka.

MIMI: “Senior, nakuona unakula maisha ya dunia.”


DULLAH: “Brother! Ukweli nina-enjoy asee.”


MIMI: “Nilitegemea ungekuwa na mrembo pembeni.”


DULLAH: “Kaka mimi siwezi kumu-engage mwanamke. Pisi za hapa hotelini ni kali sana, na hela sina hio nguvu natolea wapi?.”

Nikacheka.

MIMI: “uwepo wako hapa hotelini tu inaonesha una hela. Acha woga, chukua namba.”

Dullah alicheka na kubadilisha mada.

DULLAH: “Shemeji anaendeleaje kwanza?”


MIMI: “Ameruhusiwa kurudi nyumbani. Mimi ndio nikaja huku kukutimizia haja yako.”


DULLAH: “Kaka, kuchepuka mara moja sio dhambi.”


MIMI: “Twende ndani kwanza tukapange mipango yetu.”

Tulipanga kuondoka Jumatano, ili Jumanne niitumie kukaa na mama mtoto. Baada ya hapo, nilimpigia simu Nala, lakini hakupokea, papohapo akanitumia meseji akaomba tuchat. Nilimwambia niko South Africa, naye akaniambia alishaniona siku niliyofika. Nilimuomba tukutane, lakini akasema leo haiwezekani, labda tupange kesho jioni, mbali na mazingira ya hotel.

Baada ya Nala kusema vile, nilimuelekeza Dullah naye akasema haina shida tumvumilie hadi kesho.

Nikiendelea kuwa na Dullah pale hotelini, Iryn alinipigia simu kuniuliza nilipo na kuniomba nirudi home mapema kwani amenimiss sana. Baada ya kusikia hivyo, niliondoka haraka sana, akili yangu ikiwaza ngono, maana nilikuwa nime-mmiss sana.

Nilipofika nyumbani, nikakuta wageni pale sebuleni. Baada ya salamu, nilienda moja kwa moja chumbani na nikamkuta Iryn yuko na Samantha na Vivian.

MIMI: “Baby, how are you feeling now?”

IRYN: “Much better, but I hate these pills.”


MIMI: “Pole sana, Aria alikuwa kakumiss sana.”


IRYN: “Hata mimi nilika-miss sanaa, I’m happy alikuwa na baba yake.”

Baada ya dakika chache wote walitoka na kutuacha wawili chumbani.

Kipindi chote tunaongea Iryn alikuwa anakamua maziwa yake kwenye bakuli kubwa la glass. Yalikuwa ni maziwa mengi sana, na baada ya kumuuliza kwanini anafanya vile, alisema-ni ya kumwaga sababu Aria hawezi kunyonya hadi siku tatu zikapotimia.

MIMI: “Baby, jumatano mimi naondoka kurudi Dar es Salam, unajua week inakata bado niko huku.”

IRYN: “Si upo kwa mke wako? Kuna shida?”

MIMI: “No baby! Mama J anasumbua sana.”

IRYN: “Unakuwa na mama J kila siku, kitu ambacho kwangu hufanyi Baba Aria. Ni lini mimi na Aria utatupa muda wako kama hivi sasa?”.

MIMI: “Baby, December tutakuwa wote will enjoy okay?. I love you ndomana unaona nimekuja hadi South Africa kwaajili yako.”

Iryn aliniangalia kwa jicho la mahaba, kisha akaongea;

IRYN: “Always una maneno matamu sana ya kumanipulate hisia zangu, but okay. Ila kumbuka December tunaanzia kwenda kwenu, kisha tunamazia Ethiopia.”

MIMI: “Sawa mama watoto wangu usijali.”

IRYN: “Na kwanini hujamwambia wifi yangu kama ninaumwa?”

MIMI: “Baby nilivurugwa sana kwakweli, sorry.”

IRYN: “Okay, nimekumiss Insider.”

MIMI: “Ndomana nimerudi haraka baada ya simu yako hata mimi nimekumiss sana.”

Niliinuka na kwenda kufunga mlango, kisha nikamrudia, lakini akaishia kusema;

IRYN: “Sorry baby, we can’t f*ck at the moment.”

Niliishiwa pozi baada ya kusikia kauli hii kutoka kwake,
******
 
SEASON 03
CHAPTER 19

CONTINUE


Kesho yake jioni, mimi na Dullah tulielekea kukutana na mrembo Nala, ambaye alikuwa amependekeza tukutane Barristers. Tulichukua Uber kutoka hotelini, na ndani ya muda mfupi tukawa tayari tumefika, eneo la tukio halikuwa mbali sana, jambo lililofanya safari iwe fupi.

Tukiwa njiani, mimi na Dullah tulikuwa na mazungumzo mengi kuhusu yule mwanamke tuliyekuwa tunakwenda kukutana naye. Dullah alikuwa na maswali mengi kuhusu namna nilivyokutana na Nala, na alikuwa na hamu kubwa kujua kama niliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye. Wakati huohuo, alishindwa kuficha mshangao wake juu ya mazingira mazuri ya South Africa aliyoyaona kupitia kioo cha gari, na aliendelea kuyasifia kwa furaha.

Tulipofika Barristers, nilimuomba dereva ampigie simu Nala ili ajue tumefika. Haikuchukua muda, Nala alitokea kwa haraka akija kutupokea eneo la parking. Tulisalimiana kwa kukumbatiana kwa bashasha, kisha tukafuatana naye hadi ndani, sehemu aliyokuwa amekaa tayari.

Tulikaa, tukaagiza chakula, na mazungumzo yakaanza kuendelea taratibu. Nala alikuwa akinitazama kwa makini isivyo kawaida, kuna namna macho yake yalivyokuwa yakinitafuta kuonesha alikuwa na jambo moyoni, lakini bado akihangaika kulisema. Baada ya muda wa kumsoma, niliamua kuvunja ukimya.

MIMI: “Tell me miss, it’s been a while.”

NALA: “Yeah! it’s been a while, since you promised to find me.”

Nilicheka kidogo, nikijaribu kupunguza uzito wa maneno yake.

MIMI: “Sorry, I was planning to check on you, but today feels like the right time.”

Akanitazama kwa makini zaidi, kisha akasema kwa sauti ya chini,

NALA: “Mhh! tell me, what’s the matter?”

Nikachukua nafasi hiyo kuwatambulisha.

MIMI: “This is my friend Dullah, the guy I work with and do business together with.”

Nala alimtizama Dullah kwa umakini, kabla ya kuzungumza;

NALA: “Nice to meet you, Dullah. Welcome to South Africa!”

DULLAH: “Thank you, miss.”

Nikaendelea na utambulisho;

MIMI: “Dullah, meet Nala, the beautiful girl I have been mentioning to you every single day.

Dullah aliishia kucheka, huku Nala akitabasamu kwa aibu ya kupendeza.
Baada ya mazungumzo ya awali, Nala akauliza,

NALA: “So guys, when are you leaving?”

MIMI: “On Saturday, I think.”

Dullah alinitazama kwa macho ya mshangao kidogo. Nikampa ishara ya kumkonyeza, kumaanisha atulie. Bila shaka, alishtuka pale nilipomwambia Nala kwamba tunaondoka Jumamosi, huku tulipanga kuondoka jumatano.

Mazungumzo yaliendelea pale na stori za hapa na pale, vicheko, na hali ikazidi kuwa shwari. Baada ya kumaliza chakula, tuliagiza wine na kadri tulivyokuwa tukinywa, niliendelea kumchunguza Nala, nikitafuta gia nzuri ya kumwingia.

Nilitamani sana kuzungumza na Nala kwa utulivu, Dullah asiwepo ili tuwe na uhuru wa mazungumzo. Hivyo nikaona ni busara nikamuomba Dullah akaondoke kwa muda. Palepale nikamwandikia ujumbe kwenye simu yangu, kwa herufi kubwa:

“BRO, GIVE ME 10 MINUTES ZA KUONGEA NA HUYU MREMBO.”

Nikampa simu kwa ustadi, kuhakikisha Nala hatambui kinachoendelea. Baada ya dakika chache kupita, Dullah akasimama na kusema anaelekea washroom, kisha akaondoka taratibu.

Mara tu Dullah alipoondoka, sikutaka kupoteza muda. Nilijipanga haraka, nikaanza kumwangalia Nala kwa umakini namna alivyokaa, alivyozungumza, na vile alivyonitazama. Nilijua kabisa nilihitaji sababu yenye mashiko, maneno yaliyopangwa vizuri, ili nimuingie taratibu na kufanikisha lengo langu bila kumchanganya.

Nikavuta pumzi ndefu kabla ya kuanza kuongea;

MIMI: “Unajua Nala, mimi niko hapa South kwa ajili ya dada yangu. Alikuwa amelazwa Mediclinic hospital, lakini jana tu ndiyo ameruhusiwa.”

Alinitazama kwa macho yenye huruma.

NALA: “I’m really sorry.”

MIMI: “Thank you! Huyu Dullah ni mshikaji wangu sana ndiyo akanipa kampani ya kuja wote.”

Akatabasamu kidogo, kisha akasema kwa sauti ya utani.

NALA: “Niliwaona mkifika hotelini lakini hukutaka hata kunijulisha.”

MIMI: “Sorry! Yalikuwa mambo ya ghafla sana, dear. Nala mimi nimekutafuta kuna jambo nahitaji msaada kutoka kwako, please.”

NALA: “Ni jambo gani unataka kunambia.”

MIMI: “Ukweli ni huu, jamaa yangu yuko alone sana kule hotelini. Nilitamani apate mtu wa kumpa kampani hasa kuwa naye usiku kwa hizi siku chache zilizobaki hadi tunaondoka. Mimi naona wewe ndiyo mtu sahihi wa kunisaidia kuhusu hili, sababu nina kuamini, pia nitakupa offa nzuri tu.”

Nilikuwa wazi, straight maana najua wanawake wa South hawapendi maneno mengi yasiyo na maana-wana uzungu mwingi tofauti na wanawake wa bongo. Baada ya kusikia hayo, Nala alininyanyulia macho, akacheka kidogo kisha akatikisa kichwa.

NALA: “Hilo siwezi kulifanya. Mimi sio mwanamke wa aina hiyo.”

MIMI: “Kwahiyo unanisaidiaje kwa hili?.”

Akatabasamu tena,

NALA: “Ninaweza kuwatafutia mtu ambaye anaweza kuwapa mnachotaka.”

MIMI: “Unajua jamaa yangu hajui kuhusu huu mpango wangu. Ndio maana nimeanza kuongea na wewe baada ya yeye kutoka, nataka iwe saprize tu.”

Alikaa kimya kwa sekunde chache, kabla hajatia neno;

NALA: “Okay! Nitawapa connection ya mtu ninayemuamini sana. Ni mrembo, na ataenjoy kuwa naye. Lakini, kwanza itabidi nimshawishi juu ya hili

Nala alipiga simu kwa rafiki yake, wakaanza kuzungumza pale. Sikuwa naelewa anachozungumza sababu alitumia lugha yao ya asili (Zulu). Waliongea kwa takribani dakika tano, ndipo wakamaliza mazungumzo yao. Hatimaye walipomaliza, Nala alinigeukia kwa utulivu na kusema kuwa rafiki yake amekubali kuja, lakini kwa makubaliano USD 200. Nikamwambia haina shida tutampa hiko kiasi, hivyo amuimize aje mapema.

Ilipita kama saa moja hivi ndipo yule dada aliwasili pale Barristers. Aisee, alikuwa mrembo wa kuvutia sana macho, amevalia kimini na viatu virefu vya kisigino (heels) vilivyomfanya aonekane mwenye mvuto wa kipekee. Alikuwa mweupe kwa rangi, mwenye umbo lililojipanga vizuri kama ramani ya Masaki kwa kifupi, alikuwa mfano halisi wa wasichana wa South Africa wenye vishundu vilivyokaa sawasawa.

Kabla hata hajaketi, alitusalimia wote kwa tabasamu zuri lililopambwa na sauti laini, kisha akaketi karibu nasi. Bila kupoteza muda, Nala akaanza kufanya utambulisho. Alimtambulisha yake anaitwa Celine, kisha akanitambulisha mimi na Dullah kama rafiki zake wa muda mrefu.

Ukweli sikufikiria kama angeleta “project” nzuri kiasi kile. Nilishangaa sana, na hata Dullah naye alibaki ameduwaa akimtizama Celine kwa macho ya kifisi. Nikamnong’oneza Dullah kwa utani na kumwambia;

“Uber uliyo-request tangu jana ndiyo hii imefika.”

Dullah alicheka kwa sauti ya chini, na mara moja akaanza mazungumzo na Celine kwa bashasha kubwa, huku mimi nikibaki nikizungumza na Nala.

Ilipofika saa nne usiku, tulikubaliana kuondoka. Dullah aliondoka na mrembo wake Celine, lakini kabla hawajaondoka nilimwambia kwa utani, “Hakikisha unaiperusha vizuri bendera ya nchi!” Alinitazama akicheka, kisha wakaondoka zao.

Baada ya wao kuondoka, mimi na Nala tuliendelea kusimama pale nje kwenye parking tukizungumza. Nilimshukuru sana kwa msaada wake na nikamwambia wazi kwamba yule dada alikuwa mzuri sana. Nala alikubaliana nami huku tukicheka kwa furaha na baada ya dakika kama kumi hivi, tuliagana. Nilimpa nauli ya kurudi nyumbani, nami nikachukua Uber yangu ya kurudi home.

Nilipofika nyumbani, niliikuta familia yote imekaa sebleni wakipiga stori, na kinara wa maongezi hakuwa mwingine bali ni Momo. Nikajiunga nao na kukaa pembeni ya Brenda. Nilipomtazama Iryn, alinipiga jicho la tahadhari la kunionya nijihadhari na ninachofanya.

Bibi alikuwa anaongea kwa lugha yao ya asili huku wengine wakicheka sana, isipokuwa mimi na Brenda ambao tulionekana kama tumevamia kwenye mtumbwi wa vibwengo, hatuelewi chochote. Samantha ndipo akaanza kututafsiria baadhi ya walichokuwa wakizungumza. Moja ya stori za Bibi ilikuwa ni kumwambia Vivian kwamba umri unaenda lakini bado hajambariki mjukuu, na bado anakaa nyumbani bila kuolewa.

Baada ya muda, niliondoka sebleni na kwenda chumbani kuongea na Lucy, ambaye alikuwa amenitumia ujumbe akisema kuna jambo muhimu sana la kuzungumza. Alinieleza kuhusu malipo ya ofisini ambayo yalipaswa kufanyika tangu wiki iliyopita kwa ajili ya service za mashine za ofisini. Nikamwambia afanye malipo kwa kutumia salio la cash na atunze slip ya malipo.

Baada ya kumaliza mazungumzo nikampigia simu mama J na kumtaarifu kwamba kesho nitarudi Dar es Salaam pamoja na zawadi yake. Kwa upande mwingine tangu nimlipie gari lake, alikuwa na furaha sana, yaani hakuwa tena na maswali mengi kama zamani. Wife aliniomba sana nirudi home mapema kwani amenimiss sana.

Niliingia bafuni kuoga, nilipotoka, nikamkuta mama Aria amekaa juu ya kitanda akinitazama kwa macho yaliyojaa mashaka. Uso wake haukuwa wa kawaida, ulionesha kuwa na wasiwasi uliochanganyika na hasira ya chini kwa chini. Alivunja ukimya kwa sauti tulivu lakini nzito.

IRYN: “Where have you been?”

Nikajifuta maji usoni kwa taulo.

MIMI: “Hotelini kwa jamaa yangu.”

IRYN: “Why hupatikani?”

MIMI: “Baby, si unajua mpaka ni-connect WiFi ndiyo niweze kuwa online?”

IRYN: “Ulikuwa hotelini, ulishindwa vipi kutumia WiFi?”

MIMI: “Baby! Haya yote yanatoka wapi?”

Alinyamaza kwa sekunde chache akinitazama bila kupepesa macho, kisha akasema kwa sauti ya kuomba lakini yenye amri ndani yake:

IRYN: “Naomba simu yako.”

MIMI: “Unataka ya nini?”

IRYN: “Please!”

MIMI: “I can’t.”

Baada ya kugoma kutoa simu ndipo hali ilibadilika kabisa. Akaanza kulalamika kwa sauti iliyojaa hasira na maumivu, akinituhumu waziwazi kuwa nimetoka kwa mwanamke mwingine. Sikutaka kuongea wala kujibu chochote, hivyo nikapanda kitandani kimya kimya, nikajifunika shuka na kuamua kulala, nikimuacha akiwa bado amesimama pale, akiongea.
*******
Jumatano ilikuwa siku ya kurejea Dar es Salaam. Niliamka mapema, saa 12 asubuhi, wakati huo Iryn alikuwa bado amelala fofofo pamoja na mtoto. Hivyo bila kupoteza muda niliamua kuelekea gym kufanya mazoezi ya viungo na kujiweka fiti.

Nilipofika gym, nilikutana na watu wawili wapya ambao sikuwa nimewahi kuwaona hapo awali. Lengo langu kuu lilikuwa kukimbia, lakini nilikuta mashine ya kukimbia inatumiwa na mtu mwingine. Bila kukata tamaa, niliamua kuendelea na mazoezi mengine taratibu huku nasubiri mashine. Takribani dakika 40 baadaye, Iryn aliingia gym, akaja moja kwa moja hadi nilipokuwa, akasimama karibu nami na kuanza kuniangalia kimya kimya, wakati huo nikiwa nafanya push-ups.

Ghafla akajaribu kukaa juu ya mgongo wangu huku akicheka, kisha akaanza kuongea.

IRYN: “Baba Aria, ujue nilikuwa nakutafuta sana, kumbe umekuja huku.”

Nikasimama na kumtazama usoni.

MIMI: “Nimekuja kufanya mazoezi, sitaki kitambi.”

Alicheka, akasogea karibu zaidi.

IRYN: “Sorry for yesterday, baba Aria. Nakuwa na wivu sana juu yako I don’t know, nashindwa kujizuia.”

MIMI: “Naelewa mpenzi wangu, huna haja ya kujilaumu. Mimi nilishasahau yote ya jana.”

Alikuwa amevaa tight ya michezo iliyombana vizuri. Kwa mzaha, nilishika pindo lake na kulivuta kwa nguvu kidogo, likamgonga tumboni. Akatoa sauti ya juu, mchanganyiko wa maumivu na mahaba, “Aaaah!” Hata wale jamaa waliokuwa wanafanya mazoezi karibu nasi waligeuka kututazama.

IRYN: “Umeniumiza.”

MIMI: “Unatoa sauti za mahaba mpaka watu wanageuka kukuangalia.”

Akatabasamu kwa aibu kidogo.

IRYN: “I don’t know these guys, it’s my first time to see them here.”

MIMI: “Kwa hiyo huwajui hata wapangaji wako?”

IRYN: “Tunatumia kampuni kuwapangisha, kwa hiyo kuwajua si rahisi.”

Tulikaa pembeni tukaanza kupiga story. Iryn aliniambia kuwa alikuwa anaandaa lunch ya pamoja mchana huo kabla hatujaondoka, na akasisitiza nihakikishe Dullah anakuwepo. Kabla hatujaondoka gym, nilimuomba aniangalizie laptop nzuri kwa ajili ya zawadi ya Mama J. Akaniambia ana laptop nne mpya kabisa ndani, hivyo nitachagua ile itakayomfaa.

Tulikuwa kwenye mahaba mazito sana, kila mmoja alionyesha wazi kuwa alikuwa amemmiss mwenzake. Tulianza kupeana romance taratibu tena bila wasiwasi wowote, kama vile hakuna anayetuona. Baada ya wale jamaa waliokuwa anafanya mazoezi kuondoka, mahaba yakaongezeka spidi zaidi na tukazidi kubadilishana lita za ujazo.

Tuliporudi kwenye apartment, kwa mbali tulimuona bibi amekaa kibarazani akitutazama. Kadri tulivyokaribia, tabasamu lake lilizidi kuonekana wazi. Nilimsalimia kwa heshima, na Iryn akamsalimia kwa kumbusu shavuni, kisha wakaendelea kuzungumza kwa lugha yao ya asili.

Mimi niliingia ndani kuoga. Baada ya kutoka, niliwasiliana na Dullah ili kujua maendeleo yake. Aliniambia alikuwa “kaenjoy sana” akiwa na Celine na alisema mrembo bado amelala fofofo, hivyo anasubiri aamke ili amuweke tena cha mwisho. Nilicheka sana, nikamwambia kuwa shemeji yake anaandaa lunch, hivyo ahakikishe anakuja mapema nyumbani.

Baada ya kupata kifungua kinywa, tulikuwa na kikao kifupi na bibi. Ni kikao ambacho kilihusu watu watatu tu (Bibi, mimi, Iryn). Tulikaa nje garden na Bibi alianza kuzungumza, huku Iryn alikuwa akitafsiri kila alichosema.

Bibi (Momo) alianza kwa kueleza lengo la kikao. Alisema anafurahi sana kutuona pamoja na anatamani kujua mustakabali wa maisha yetu, hasa kwa upande wa mtoto, Aria. Kwa upande wetu, tulimweleza malengo yetu ya kuishi pamoja, nami nikamwambia wazi kuwa Iryn angekuwa kama mke wangu wa pili. Bibi alisema anajua mengi kunihusu, na kwa kuwa jambo tayari limeshatokea, basi yote ni mipango ya Mungu. Hakukuwa na sababu ya kulaumiana, kilicho muhimu sasa ni kuangalia future ya mtoto.

Hata hivyo, alisisitiza sana nihakikishe suala hili linafikishwa kwa wazazi wangu mapema iwezekanavyo ili wajue kinachoendelea na wamjue mjukuu wao. Kikao kilikuwa kifupi ambacho tulitumia takribani nusu saa na baada ya kumalizika, Iryn alienda sebleni kuwakaribisha wageni waliokuja kumuona nyumbani.

Saa 6 mchana, Dullah aliwasili nyumbani akitokea hotelini, na tulikaa kibarazani tukipiga story. Nilikuwa na hamu kubwa ya kujua yaliyojiri kati yake na mrembo Celine baada ya kuachana. Dullah alikuwa mwenye furaha sana, aliishia kumsifia Celine na hata akasema tayari amemwomba aje Tanzania, naye amekubali. Tulicheka sana na baadaye nilimwambia kabla hatujaondoka, tutaenda shopping kununua zawadi kwa ajili ya mke wake, Latifah.

Saa 7 mchana, lunch iliwasili pale home ambayo ilikuwa catered kutoka kwa mmoja wa wapishi maarufu wa Cape Town. Iryn alikuja pale kibarazani na kutukaribisha ndani kwaajili ya lunch na tulikaa pamoja. Tulikuwa jumla ya watu 15 pale kwake ambao walikuwa ni ndugu na baadhi ni marafiki zake wa chuo na sehemu mbalimbali.

Ilikuwa ni lunch ya kibabe sana ambayo kila mmoja wetu pale alionekana kuifurahia. Wakati tunakula nilimwambia Iryn kwamba mimi na Dullah tungeondoka kwenda kufanya shopping. Alisema anatamani kwenda na sisi, lakini nilimzuia na kumwambia abaki nyumbani na wageni, pia aendelee kuangalia afya yake.

Baada ya lunch, tulipumzika kwa muda mfupi nje kibarazani tukimsubiri Samantha, ambaye alikuwa ndani akijiandaa. Wakati huo, Dullah alikuwa bize akimshika Aria, akicheza naye kwa furaha. Iryn alikuja na kukaa juu ya mapaja yangu, kisha kwa siri akanikabidhi kadi ya bank bila Dullah kujua.

Kwa kuninong’oneza sikioni alinambia tufanye shopping tutakavyotaka na kisha akanitajia password. Muda si muda, Samantha alitoka nje akiwa amependeza sana, ndipo tukaondoka kuelekea kufanya shopping.

Tulielekea Canal Walk ambapo tungepata maduka yote kwa pamoja. Ukweli hii shopping ilikuwa kama maalumu kwa Dullah, maana alinunua mazaga mengi sana kwa ajili yake na mke wake. Samantha naye hakubaki nyuma bali alitumia fursa hii vizuri ya kununua nguo na viatu. Mimi kwa upande wangu sikuwa na habari na shopping, zaidi nilinunua raba moja tu ya Adidas. Tulitumia takribani masaa mawili tukifanya shopping na kupiga picha sehemu mbalimbali, kisha tukarudi nyumbani.

Jioni, tulikaa kibarazani mimi, Iryn na Dullah tukizungumza mambo mbalimbali kabla ya safari. Iryn alitumia nafasi hiyo kumfahamu Dullah vizuri na kumshukuru kwa kuja kumuona South Africa. Katika mazungumzo, Iryn alisema atakuja Dar es Salaam mapema sana mwanzoni mwa Desemba ili tuende nyumbani kwetu, kisha tuende Ethiopia.

Tuliongea mambo mengi sana mpaka muda wa kuondoka ulipokaribia, niliingia chumbani kwenda kujiandaa. Niliingia bafuni kuoga wakati Iryn akinisaidia kupanga nguo zangu kwenye bag.

Baada ya kumaliza kujiandaa, Iryn alimuagiza Samantha aje na laptop ili niweze kuchagua moja itakayonifaa. Haikuchukua muda Samantha akaja na laptop tatu, kisha kuziweka kitandani. Nilichagua MacBook Air ya 2022, ambayo bado ilikuwa latest, nikaiweka kwenye begi langu na kumshukuru.

Iryn alinisaidia kuburuza begi, kisha nikaelekea sebleni kumuaga Bibi na mwanangu Aria, pamoja na wageni wengine akiwemo Brenda. Wakati huo Uber ilikuwa tayari imewasili kutupeleka airport, hivyo tukaongozana kuelekea nje, Iryn akiwa bado anaburuza begi bila kutaka kusaidiwa.

Baada ya kupakia mabegi yetu kwenye buti la gari, tulibadilishana maneno machache kisha tukakumbatiana. Nikambusu Iryn shavuni, halafu nikawageukia kina Vivian na Samantha kuwaaga. Hata hivyo, nilibaki kuzungumza na Samantha kwa muda mfupi, maana nilikuwa na maneno mengi ya kubadilishana naye. Ukweli alikuwa kampani yangu kubwa kipindi Iryn alipokuwa anaumwa, na ndiye aliyekuwa akimhudumia na kumuangalia mtoto kwa umakini mkubwa.

Baada ya kuagana tukaondoka kuelekea Airport kwaajili ya kuanza safari ya kurudi Tanzania. Tulikuwa tunasafiri na Airlink saa 2 usiku, tukielekea Johannesburg, kisha kupanda ndege nyingine ya moja kwa moja hadi Dar es Salaam. Tulipofika Johannesburg, tulisubiri kwa muda mfupi kisha tukaondoka tena saa 5 usiku kurudi Dar es Salaam.

Tulifika Dar es Salaam saa 10 usiku kasoro, hapo bado nilikuwa ninaunganisha safari nyingine ya kwenda Dodoma saa 12 asubuhi. Wakati wote wa safari hadi tunafika, mimi na Dullah tulikaa viti tofauti. Hivyo, tulipowasili JNIA, tulizungumza kidogo wakati yeye akisubiri Uber ya kumchukua.

Dullah aligusia suala la Iryn, alikuwa makini kipindi nikizungumza naye kuhusu mpango wa kwenda kwetu, alikuwa akisikiliza kwa makini sana. Alionekana kuwa na hamu kubwa ya kujua ni hatua gani tayari nilikuwa nimefikia kuhusu hilo jambo. Nilimwambia kwa uwazi kuwa hata mimi mwenyewe sikujua nianzie wapi, kwani hadi wakati huo sikuwa bado nimechukua hatua yoyote, ilhali mwezi wa Desemba haukuwa mbali. Nilihisi wazi kuwa Iryn asingelewa kabisa hali hiyo.

Hata hivyo, hatukuweza kuendelea zaidi na mazungumzo yetu, kwa sababu Uber ilikuwa tayari imewasili Terminal 3 kumchukua. Akaniaga kwa haraka na kuniambia kwamba nikirudi kutoka Dodoma nimjulishe, ili tuketi tuzungumze kwa kina zaidi kuhusu suala hilo, kwani alikuwa na wazo ambalo angependa kunishirikisha.

Baada ya Dullah kuondoka, niliendelea kubaki pale airport nikisubiri ndege ya kwenda Dodoma. Kipindi chote cha kusubiri, nilijikuta nikiwa ndani ya dimbwi kubwa la mawazo kuhusu sakata la Iryn. Sikujua kabisa hatima yake itakuwa nini, hasa ikizingatiwa kuwa hadi wakati huo sikuwa nimechukua hatua yoyote ya maana.

Aria tayari alikuwa ametimiza miezi mitatu tangu azaliwe, na kufikia Desemba angekuwa na miezi sita. Hata hivyo, mpaka kufikia hatua hiyo bado hakujulikana kwa wazazi wangu. Hili lilikuwa jambo lililoninyima amani na kunikosesha raha kabisa. Dada yangu ndiye aliyekuwa na dhamana ya kulishughulikia suala hili, naye aliendelea kunisisitiza niwe na subira.

Mawazo yakaanza kunizonga zaidi:

“Desemba itafika na Iryn atakuta sijachukua hatua yoyote. Nilimuhakikishia kuwa nitalifanikisha jambo hili je, atanielewaje akigundua kuwa hakuna chochote nilichofanya? Huu utakuwa ugomvi mkubwa, na ninaweza kabisa kuharibu mood yake yote.”

Nilifikiri sana pale airport, lakini mwisho wa siku sikupata jibu lolote. Jambo hili lilionekana kuwa gumu sana, hasa kwangu. Nilihitaji msaada wa watu wenye uzoefu na uwezo, watu ambao wangenisaidia kuliona hili sakata kwa macho mapana zaidi na kuniongoza njia sahihi.
 
SEASON 03
CHAPTER 20

CONTINUE:

Baada ya kutua Dodoma, nilimpigia simu wife wangu na kumpa taarifa kuwa nimetua salama Dar es Salaam, lakini kwa wakati huo nilikuwa Dodoma mara moja kushughulikia masuala ya kampuni. Nilimueleza kuwa nilikuja kwa ajili ya mambo ya Biashara, ikiwemo kufanya mabadiliko ya taarifa za kampuni na kumuingiza rasmi kama mmoja wa Directors.

Mama J alifurahi sana baada ya kupokea taarifa hizi. Nilihisi furaha yake hata kupitia simu, jambo lililonipa amani ya moyo. Nilimwambia kuwa endapo nitafanikiwa kukamilisha mambo mapema, bhasi nitarejea nyumbani haraka.

Baada ya hapo, nilimpigia simu Sanchi kumjulisha kuwa nimefika Dodoma na pia kumkumbusha kuhusu appointment yetu ya jioni ya kukutana na Mr. Ando, ambapo tungeenda wote. Kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana kutokana na uchovu wa safari, niliamua nipumzike kwanza kabla ya kuendelea na shughuli nyingine.

Saa tisa alasiri, niliondoka kuelekea kwa Sanchi kwa ajili ya mazungumzo mafupi kabla ya kwenda kukutana na Mr. Ando. Sanchi alifurahi sana kuniona na kunikaribisha ndani kwa bashasha kubwa. Baada ya kusalimiana, alinipa pole nyingi kwa niaba ya Aria na mama yake, na akaendelea kuniuliza maendeleo yao ya kiafya kwa ujumla tangu nilipoondoka South Africa.

Baada ya salamu, tulianza kuzungumzia masuala ya kampuni. Nilimuweka wazi Sanchi na kumueleza mpango wangu wa kumwajiri rasmi kama Secretary wa kampuni na kuanza kumlipa mshahara. Nilifanya uamuzi huu kwa sababu alikuwa tayari mtu muhimu sana katika ukuaji wa kampuni. Kwa muda mrefu, alikuwa akinisaidia kuwasiliana na wadau kwa niaba yangu, na zaidi ya hapo, alikuwa mzuri sana katika communication na marketing.

Baada ya kumpa taarifa hizi, Sanchi alifurahi sana, japokuwa mara ya kwanza alionekana kusita na kutaka kukataa. Nilimueleza kwa kina mpango wangu wa dhati pamoja na maono makubwa niliyonayo juu ya kampuni hii. Hatimaye, alielewa na kukubali.

Baada ya hapo, tuligeukia mjadala wa kwenda kukutana na Mr. Ando. Sanchi alitaka kujua ni maamuzi gani nilikuwa nimeyachukua kuhusu pendekezo la Ando. Nilimueleza wazi kuwa kumpa hisa za kampuni ni jambo lisilowezekana kwa sasa, kutokana na risk kubwa iliyopo. Badala yake, niliona ni busara tumlipe kwa mfumo wa commission kwa kila kazi atakayoleta.

Sanchi aliunga mkono wazo langu mara moja, akisema hata yeye tangu mwanzo alikuwa na mtazamo huo huo, na akaona ni njia ya kitaalamu zaidi (a more professional approach). Hata hivyo, nilibaki na maswali moyoni kwa sababu Mr. Ando alikuwa anaonyesha interest kubwa sana kwenye kampuni. Nikaanza kuwaza kwa kina, nikaona huenda kuna kitu kikubwa ameona ndani ya kampuni yangu, ndiyo maana alikuwa ananifuatilia karibu na kutaka majibu kila siku.

Ilipofika saa kumi na moja jioni, mimi na Sanchi tuliondoka kuelekea Morena hotel kukutana na Mr. Ando. Tulikutana kwenye restaurant kwa ajili ya kikao chetu kifupi. Safari hii, Mr. Ando alifika kwa wakati, na bila kuchelewa, tulianza mazungumzo ya kibiashara.

Kwa makusudi kabisa, sikuwa na haraka ya kuzungumza. Nilimpa Sanchi nafasi ya kuongoza mazungumzo. Cha kushangaza, Sanchi alianza kuzungumza mambo ambayo hayakuwa exactly kama tulivyopanga, lakini aliyaeleza kwa ustadi mkubwa, kwa mtiririko na kwa hoja zenye mantiki.

SANCHI:

“Mr. Ando, kwanza tunafurahi sana kukutana na wewe kwa mara nyingine tena. Leo tumekuja kuzungumzia lile wazo ulilolitaja kwenye kikao chetu kilichopita. Management ya INSIDER INVESTMENT LTD inatambua na kuthamini nia yako njema ya kuisaidia kampuni hii kukua na kufikia malengo yake ya muda mrefu.

Kampuni hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na sera zake, na kwa muda mfupi tangu ianzishwe, tayari imeanza kutoa mchango chanya kwa jamii na Serikali kwa ujumla. Hadi sasa, tumeajiri vijana wanne ambao wanajipatia kipato na kuchangia katika kutatua changamoto ya ajira nchini.

Aidha, kampuni inalipa kodi zote stahiki za Serikali, ikiwemo PAYE, Withholding Tax, Stamp Duty, Corporate Income Tax, na kwa muda si mrefu tutaanza kufanya kazi kama Government VAT Agent.

Tunaamini mpaka sasa umeona jinsi kampuni yetu ilivyojipanga kitaendaji na kisheria. Baada ya management kukaa na kujadili kwa kina pendekezo lako, tuliona njia sahihi kwa sasa ni kushirikiana kwa mfumo wa commission kwa kila kazi utakayoleta.

Hata hivyo, tukiona unaendelea kuwa mdau wetu wa karibu na wa kudumu, kampuni iko tayari kuja kufikiria suala la kukupa hisa zake hapo baadaye. Kwa sasa, tunaomba tuendelee na utaratibu huu wa commission.

Tunakushukuru sana kwa nia yako njema na tunaamini kampuni ikikua, itasaidia vijana wengi zaidi kupata ajira na kuchangia mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali. Tunaomba ukubali pendekezo hili kutoka kwa management.”


Sanchi alizungumza kwa ufasaha mkubwa, bila kigugumizi, akipanga maneno yake kama hadithi inayovutia. Wakati wote alikuwa anaongea, nilibaki nikimtazama tu. Sikutarajia kabisa kumuona akiongea kwa confidence ile.

Mr. Ando, baada ya Sanchi kumaliza, alikaa kimya kwa muda mfupi, akanywa maji kwenye glass, kisha akaanza kuzungumza.

ANDO: “Nilikuwa napitia MEMART yenu, na nimeona share capital ni TZS 500 million. Nataka kufahamu, je, kiasi hiki chote kimeshaingizwa kwenye kampuni?”

MIMI: “Hiyo ni Authorised Share Capital. Thamani ya hisa moja ni TZS 10,000. Kati ya hisa 50,000, hisa 10,000 zimetolewa zenye thamani ya TZS 100 million, lakini ni hisa 5,000 tu ndizo zimelipwa hadi sasa. Hisa 5,000 zilizobaki zitalipwa muda wowote kuanzia sasa.”

ANDO: “Na zile hisa 40,000 zilizobaki mna mpango gani nazo?”

MIMI: “Zitabaki kwenye reserve account hadi pale kampuni itakapokuwa kubwa na kuwa na uhitaji wa kuongeza mtaji. Kwa sasa, kampuni itaendelea kutumia Equity, yaani mtaji pamoja na retained earnings kama source ya finance, tukichanganya kidogo na mikopo pale inapobidi.”

ANDO: “Director mwingine yuko wapi?”

MIMI: “Ni mama yangu.”

Mazungumzo yalikuwa marefu na ya kina, yakichukua takribani saa nzima, huku Sanchi akiwa kinara mkubwa wa majadiliano. Mwisho wa kikao, Mr. Ando alituaga na kuahidi kuwasiliana nasi baada ya kutafakari na kufanya maamuzi.

Baada ya Ando kuondoka, mimi na Sanchi tulianza kucheka na kuzungumza kwa furaha. Nilichukua nafasi hiyo kumpongeza kwa jinsi alivyo-handle mazungumzo kwa ustadi mkubwa. Alifurahi sana, na tukachukua nafasi hiyo kuagiza chakula na kula, maana muda ulikuwa umesogea.

Baada ya kumaliza kula, tuliamua kuondoka. Tuliendelea kupiga story nje kidogo huku tukisubiri usafiri wake. Usafiri wake ulipofika, tuliagana kwa kukumbatiana. Katika wakati huo, bila hata kutarajia, nilijikuta nikimshika makalio yake na kuyapapasa kwa utulivu. Sikuwa nimewahi kufanya hivyo kabla, lakini safari hii ilikuwa tofauti, nadhani ni furaha iliyonizidi siku ile;

SANCHI: “Insider, thank you.”

MIMI: “Ukifika home, nitumie account number yako.”

SANCHI: “Sawa, wewe unaondoka na usafiri gani?”

MIMI: “Nachukua pikipiki pale nje.”

SANCHI: “Bye Insider.”

Baada ya kurejea nyumbani, nilifanya mawasiliano na Iryn. Tangu nitue Dar es Salaam, sikuwa nimemtafuta, japokuwa yeye alikuwa akipiga simu mara kadhaa na kunitumia meseji. Alipopokea simu yangu, tulianza mazungumzo ya kawaida, kisha nikamjulisha kuwa nilikuwa Dodoma.

IRYN: “Hivi baby, huko Dodoma huna mwanamke kweli? Haiwezekani kila ukitoka South Africa lazima upitie Dodoma.”

MIMI: “Hamna baby, ni mambo ya kampuni tu ndiyo yamenileta huku. Pia niko kwenye process za kusajili VAT.”

IRYN: “Vipi, ulifanikiwa kuzungumza na Mr. Commission?”

Nilicheka kidogo niliposikia jina hilo.

MIMI: “Ndio, nimetoka kukutana naye si muda mrefu.”

IRYN: “Mmefikia wapi?”

MIMI: “Tumempa pendekezo letu la commission. Ametuomba tumpe muda wa kulifikiria, halafu atanijulisha akishafanya maamuzi.”

IRYN: “Mungu akutangulie baby. Napenda hustles zako sana tangu enzi ukiwa Uber. Natamani mwanao Aria arithi spirit hiyo.”

MIMI: “Nikifanikiwa kupata hizi deal, nakupeleka Santorini ukale bata.”

Maneno hayo yalimburudisha sana.

IRYN: “Awww… nikija Dar nitakusaidia kwenye marketing. Unanionaje nikianza kutupia vitu vyangu?”

MIMI: “Deal zote tutazipata, ila ujue watakutongoza sana, halafu mimi nina wivu.”

Tulicheka kwa pamoja.

IRYN: “Momo anakusalimia, ananionea wivu eti.”

MIMI: “Msalimie mke wangu mkubwa, mwambie nimemmiss.”

Mazungumzo yaliendelea kwa muda mrefu, tukizungumza mambo mengi sana. Na kubwa Iryn alikuwa kapona tayari na alinambia ameanza kumnyonyesha mtoto. Taarifa ile, ilinifurahisha sana na baada ya kumaliza maongezi yetu hatimaye, tuliagana, nami nikaelekea bafuni kuoga.

Nikiwa bafuni, hali ya ghafla ikanijia na nikaanza kumkumbuka Mary. Hasa kipindi kile kaja Dodoma na kuishi pamoja, nilianza kukumbuka jinsi tulivyokuwa tunadinyana mle bafuni. Nilimkumbuka jinsi nilivyokuwa nikimvuta karibu, nikimuinamisha, na kupeleka moto huku akitoa miguno ya sauti.

Kumbukumbu hizo zilinizidia nguvu, zikaanza kunipa maswali mazito moyoni. Nilishindwa kuamini kama kweli Mary alikuwa ameamua ku-move on kabisa. Kwa jinsi alivyokuwa akinipenda, sikutarajia kumuona akinichunia kwa muda mrefu namna ile. Hofu ilianza kunijia polepole, nikahisi labda kweli ameamua kufanya maisha yake bila mimi. Zaidi ya yote, tukio lile la kumkuta na mwanaume pale kwake liliendelea kunisumbua sana kichwani. Lilikuwa ni jeraha ambalo halikuwa limepona kabisa.

Moyo wangu haukuwa tayari kumpoteza Mary. Kadri nilivyofikiria, ndivyo nilivyozidi kuona kuwa bado kulikuwa na nafasi, au angalau nifanye jaribio la mwisho. Ndipo nikaamua kuwa ni lazima nimtafute Jane. Nilihitaji kuzungumza naye kwa kina kuhusu hili, kwa sababu nilimwona yeye kama mtu pekee ambaye angeweza kutuunganisha tena.

Nilijisemea moyoni, kama bado kuna uwezekano wowote wa kunirudisha kwa Mary, basi Jane ndiye funguo kwasasa.

Kesho yake saa tatu kamili asubuhi, nilienda ofisini kuonana na Erica pamoja na kukamilisha masuala ya kampuni. Nilipofika ofisini kwake, sikumkuta, hivyo nikakaa kwenye benchi nikimsubiri. Baada ya takribani dakika kumi, nilimuona akiingia na kukaa kwenye meza yake. Alipoinua macho na kuniona, alisimama ghafla na kuondoka tena bila kusema neno.

Nilishangaa kumuona anaondoka na nilijiuliza kimoyomoyo, huyu mama anaenda wapi tena? Nilihisi kama napoteza muda, hasa ukizingatia nilikuwa na ratiba nzito siku hiyo.

Haikupita hata dakika, simu yangu ikapokea ujumbe mfupi:

“Insider mpenzi, njoo mpaka parking.”

Nilisimama mara moja na kufuata maelekezo. Nilipofika parking, nilimkuta Erica amesimama pembeni, akinionyesha ishara ya kunisubiri. Tulitazamana kwa sekunde chache kabla sijaamua kuanza mazungumzo.

MIMI: “Hey baby.”

ERICA: “Insider, kwanini unanipa pressure?”

MIMI: “Samahani! Kulitokea emergency nikahitajika kwenda South Africa, nimerudi jana.”

ERICA: “Hata kunijulisha hukuweza? Hata message za WhatsApp hujibu. Ubusy gani huo hata kujibu ujumbe ni shida?”

MIMI: “Baby, naomba uniamini, naelewa unaweza kuona kama nakudharau au nakudanganya, lakini nimekuja Dodoma kwa ajili yako pia. Nimekumiss sana.”

Alikaa kimya kwa sekunde chache, kisha akabadili mada.

ERICA: “It’s okay! Hizo ndiyo documents nilizo-request?”

MIMI: “Yeah.”

Nilimkabidhi mafaili na aliyachukua na kuanza kuyapitia haraka, moja baada ya jingine.

ERICA: “Ziko sawa, sahivi unaenda wapi?”

MIMI: “Naenda kupitia biashara zangu kidogo, halafu nitarudi nyumbani. Ila ningependa baadaye uje home, upajue.”

Aliniangalia kwa aibu kidogo. Erica alikuwa mwanamke ambaye kujiamini kwake kulipungua kila mara nikimtazama moja kwa moja machoni.

ERICA: “Sawa, nitakupigia simu.”

Tuliagana, kisha nikachukua bajaji kuelekea ofisini kwangu. Dakika chache baadaye nilikuwa tayari nimefika, nikamsalimia Sanchi, nikazunguka ofisini kukagua shughuli na kuwasalimia vijana wangu.

Baadaye nilirudi tena kwa Sanchi. Safari hii, alianzisha mazungumzo kuhusu Erica. Unajua kipindi ambacho Erica anakuja ofisini kwangu kufanya ukaguzi, alikutana na Sanchi, ambaye nilimtambulisha kama Secretary wa kampuni. Sasa kipindi ambacho niko South, Erica ananitafuta halafu sipatikani na message zake sijibu, yeye alikuwa anamtafuta Sanchi na kumuulizia taarifa zangu.

Kutokana na experience ya Sanchi kama dada mkubwa, alinusa kuna something fishy kinaendelea kati yetu. Sasa muda ambao tunapiga story alinibana kwa maswali mengi, akitaka kujua kama kuna uhusiano wa kimapenzi kati yangu na Erica . Hatahivyo sikupenda kuingia ndani sana, nikajibu kwa mkato kwamba ni ushirikiano wa kikazi tu, na hakuna chochote.

Sanchi alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anafurahi sana akiwa karibu na mimi. Tulikuwa ni watu wakupiga story nyingi sana na kupanga mipango mbalimbali ya biashara. Nilikaa pale kwa takribani masaa mawili, kisha nikaondoka kwenda kupumzika nyumbani, nikimuaga Sanchi.

Saa kumi jioni, Erica alinipigia simu kunijulisha kuwa alikuwa anatoka ofisini, akaniomba nimuelekeze mahali napoishi. Nilimpa maelekezo, akasema asingechukua muda mrefu kufika.

Baada ya simu ile, nilijikuta nikitabasamu peke yangu. Nilijua tu, jioni ile ingekuwa tofauti, kimoyomoyo nilijisema huyu leo lazima nimle siwezi kumwacha salama “Mbuzi kafia kwa muuza Soup.”

Baada ya dakika ishirini, Erica alifika nyumbani. Nilitoka nje, nikamfungulia geti na kumkaribisha kwa heshima. Alikuwa bado amevaa nguo zilezile za asubuhi kazini wakati tunakutaba. Nilimpokea mkoba wake na kumkaribisha ndani kwa tabasamu nene, hao tukaingia ndani na kukaa sebleni.

MIMI: “Chakula au kinywaji?”

ERICA: “Maji tu yanatosha.”

MIMI: “Nikuagizie chips bhana.”

ERICA: “No thank you, niko full.”

MIMI: “Unywe wine bhasi.”

Akaniangalia na kutabasamu,

ERICA: “You know situmii alcohol.”

MIMI: “I know.”

ERICA: “So! Hapa ndiyo unaishi ndugu Director.”

Nikacheka sana baada ya kusikia akiniita vile,

MIMI: “Ndio mummy, nimefurahi umekuja kutia baraka kwenye nyumba yako.”

Mazungumzo yetu yalianza kuhusu mambo ya kampuni ambapo alinihakikishia kuwa kila kitu kinafanyika kwa kufuata sheria na taratibu, na kwamba suala la kampuni lingekamilika muda si mrefu. Baada ya hapo, mazungumzo yakageukia maisha yake binafsi. Alinihadithia kuhusu familia yake, malezi yake, na mambo mengine mengi. Kwakweli nilimjua kwa undani zaidi kuliko nilivyowahi kumjua hapo awali.

Wakati huo, akili yangu ilikuwa ikitangatanga mbali. Nilikuwa nawaza ngono tu kichwani muda huu, nilikuwa namtamani sana. Erica ni mwanamke aliyebarikiwa sura, na hips ila ana makalio ya kawaida, sasa akikaa hips zake zinajiachia “bwelelee!” -Ahh! I hate this life.

Hesabu zangu zilikuwa ni kumtoa pale seblen na kwenda naye chumbani, nikamuweke wala sikuwa nawaza vingine. Alikuwa akinipigisha story nyingi, lakini mimi hata sikuwa pale, nikaamua kuanza kushambulia;

MIMI: “Baby, twende chumbani tukapumzike.”

ERICA: “Hapana, hapa hapa panatosha.”

MIMI: “Nilifikiri umechoka na kazi.”

ERICA: “Bado nipo sana na wewe, leo ungependa kula nini, nikupikie?”

Tulikwenda jikoni, na tulipofungua fridge, hakukuwa na kitu, akanicheka sana, kisha tukaamua kwenda supermarket kununua mahitaji. Tulirudi baada ya muda mfupi na kuanza kupika pamoja, tukicheka, nikimpa utani na kupiga story mbalimbali. Kwenye suala la kuongea na mwanamke na kumfanya afurahi hapa nina A+ kabisa, ni mtihani mwepesi sana kwangu.

Baada ya kumaliza kupika tulirudi tena kukaa seblen. Erica suala la kwenda chumbani hakutaka hata kulisikia, ni kama alihisi kwamba hawezi kutoka salama. Kwangu mimi haikuwa kikwazo, maana ninaelewa fika kwamba, kwa mara ya kwanza ili uichape lazima msumbuane sana. Taratibu nilimsogelea na kuanza kumuonesha mahaba waziwazi, nikianza kwa kumshikashika baadhi ya maeneo chokozi, huku namwambia maneno matamu ya kumfurahisha.

Mwanzoni, hakuwa ananipa ushirikiano sababu alionesha kutojiamini na alishikwa na aibu. Baadae alianza kunipa ushirikiano hadi kupelekea mahaba kukolea. Ilifika stage akawa anatetemeka sana na kuweweseka sana kadri navyoongeza spidi ya kucheza na maeneo yake muhimu.

Nilimbeba juu juu na kuanza kwenda naye chumbani na hapa akaanza kuongea kwa kutoa sauti ndogo, lakini iliyosikika;

“Please, let’s not go to the bedroom

Lakini, mimi hata sikujali maana nilikuwa tayari nina mizuka yangu imepanda. Changamoto ilikuwa ni kwenye kutoa pichu maana kote nilifanikiwa, ila hapa ilikuwa ni kimbembe maana ni kama akili zake zilirudi kwa kasi ya 5G. Imagine unaona kila kitu live, lakini kuitoa pichu ni mtihani maana alikuwa hataki kabisa. Hadi nafikia hii stage, tayari tulikuwa tumesumbuana vya kutosha, ilikuwa ni kurupushani.

Baada ya kuona tunasumbuana sana, hata mimi munkari ulinikata kabisa, hivyo nilihisi wazi kuwa sikuwa tayari kuendelea na zoezi. Nilifanya maamuzi ya kuacha, nilisimama na kwenda bafuni kuoga. Muda huu nilijikuta nikitafakari kwa kina misingi niliyoiweka kwenye maisha yangu, principles ambazo nimeishi nazo kwa muda mrefu bila kuzivunja hata siku moja.

Kwanza kabisa, sijawahi na sitawahi ku-force sex. Kwangu, mapenzi hayalazimishwi, yanatakiwa yatokane na ridhaa ya dhati ya pande zote mbili. Pili, sijawahi kufanya sex na mwanamke aliyekunywa au ambaye hajitambui. Hilo huwa naliona kama kuvuka mipaka ya utu na heshima, jambo ambalo dhamira yangu hailikubali. Na mwisho, sijawahi kununua malaya wala kumhonga mwanamke ili nipate sex. Sioni fahari yoyote kwenye tendo linalonunuliwa au kulazimishwa na mazingira ya kiuchumi.

Ndani ya moyo wangu, nilijua kuwa maamuzi niliyoyachukua yalikuwa sahihi, hata kama hayakuwa mepesi. Nilimaliza kuoga, nikajifuta taratibu, na nilirudi kwenye hali yangu ya kawaida na kuwa mtulivu.

Baada ya kutoka bafuni, nilirudi sebuleni nikiwa na laptop yangu. Erica alikuwa amelala kitandani. Niliendelea na kazi zangu, nikichambua ripoti mbalimbali, hasa zile za ofisini Masaki. Lakini akili yangu ilikuwa ikivuta taswira ya tukio ya kilichotokea awali.

Ilipita kama nusu saa hivi. Kulikuwa na ukimya mzito ndani ya nyumba. Nikaamua kuchungulia chumbani. Nilimkuta amelala fofofo, usingizi mzito wa mtu aliyechoka kimwili na kiakili. Nilimtazama kwa sekunde chache, kisha nikatoka kimya kimya.

Nikatoka nje kwenda kumuulizia kaka Bony, nikidhani ningempata ili kumsalimia. Kesho yake nilitegemea kuondoka kurudi Dar es Salaam, na kuondoka bila kumuona kaka Bony niliamini isingekuwa jambo la busara. Nilipofika mlangoni kwa apartment yake na kugonga, mke wake ndiye aliyenifungulia. Aliniambia kuwa Bony alikuwa bado hajarejea kutoka kazini.

Nikamuaga kwa heshima, kisha nikarudi ndani kwangu, sebuleni, nikaendelea na kazi zangu. Muda ulikuwa umesogea sana tayari ilikuwa saa mbili usiku.

Baada ya takribani dakika ishirini, nilimsikia Erica akitoka chumbani. Alikuja sebuleni taratibu na kukaa pembeni yangu. Alikuwa bado amevaa pichu, lakini juu alikuwa amevaa bra. Hakuwa anaongea, alikaa tu kimya, karibu nami. Ukweli sikuwa na hamu naye tena na nilizungumza mkono nikamshika kiuno chake laini.

MIMI: “Uko sawa?”

Alinitazama kwa macho yaliyojaa hisia, kisha akatikisa kichwa taratibu kuashiria ndiyo. Alikaa kimya kwa sekunde chache, kama alikuwa anapanga maneno moyoni, kisha akaanza kuzungumza kwa sauti ya chini.

ERICA: “Insider, I’m so sorry. Mimi ni bikra sijawahi kabisa kuingiliwa na mwanaume yeyote. I swear.”

Maneno yale yaligonga masikio yangu kwa uzito mkubwa. Bila kusema neno, nilifunga laptop yangu polepole na kuiweka mezani. Kisha nikamgeukia kabisa, nikamkazia macho, nikimtazama kwa umakini na utulivu.

Kwa mara ya kwanza nilihisi kama ananidanganya, sikuyakubali maneno yake moja kwa moja. Kwa umri wa mwanamke kama yeye, aliyeajiriwa na aliyekuwa kazini, niliona ni jambo gumu sana kuwa bado ni bikra. Nilikuwa mkubwa kwake kwa miaka mitatu, na mawazo yakaanza kunijia, yaani amalize Form 4 salama, amalize Form 6 salama, apite chuo bila matatizo hapa nilihisi kama akili zangu zinachezewa.

Kulipita kama dakika kadhaa tukiwa hatuongei. Mimi nilikuwa nikitafakari kwa kina kauli yake. Baada ya muda, nikamwambia asogee karibu nami, nikamkumbatia taratibu.

MIMI: “Are you sure wewe ni virgin?”

ERICA: “Kweli, sikutanii mpenzi. I swear, lakini ninaigopa mwenzio.

MIMI: “I will do it gently, na uta-enjoy. Huna haja ya kuogopa.”

Aliniangalia, akatabasamu kwa aibu ya kuvutia, na hapo nikajua amekubaliana na kauli yangu. Bila kupoteza muda, nikamnyanyua kwa haraka na kuingia naye chumbani kwa mara nyingine, nikiwa na dhamira ya kumleta Erica katika ulimwengu mpya wa mapenzi.

TO BE CONTINUED
 
IMG_5143.jpeg
 
Back
Top Bottom