Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 18

Baada ya kusoma ile text ya Iryn na ilikua imetumwa muda mrefu nilisema kuna kitu kibaya kimeshampata Iryn. Na muda ule nilijikuta nikijilaumu sana kwa kulala kwangu kwenye gari na muda uleule nilitoka kwenye gari haraka na kuelekea Reception.

Na hapo nilikua nikimpigia simu Iryn lakini ilikua haipokelewi kabisa. Nilifika pale reception nikamkuta dada na nikamsalimia.

MIMI: “Dada mambo, Bossy wangu amenitumia message yuko in danger na amenitumia Room No.222, ni muda mrefu toka ametuma hii text, naomba twende tukaangalie anashida gani maana kwa sasa hata simu hapokei.”

RECEPTION: “Yule dada alikuja hapa nakumbuka si mweupe? na alisema anakwenda Room hio na alijiandikisha hapa ni iryn eeh.” (Baada ya kuangalia kwenye visitors register)

MIMI: “Ndio dada ndo huyo naona unachelewa twende haraka.”

Na muda huo dada alimwita mlinzi na tukaelekea usawa wa hiyo room ilipo, na muda huo alitumia kuwasiliana na manager. Room ilikua floor ya 2 na tulivyofika pale mlangoni tulisikia kama purukushani ni kama kuna ugomvi ulikua unaendelea pale.

Upande mwingine kuna dada oppositie na chumba hicho alikua katoka kama mtu mwenye mishe zake, lakini alivyomwona mlinzi na tuko pale mlangoni alisogea karibu ili ajue kinachoendelea pale.

Na tukiwa pale mlangoni tulikua tukisikia sauti ya Iryn,

“Leave me alone, I said leave me alone”

“You want to rape me?”

Na muda uleule Mlinzi aligonga mlango, lakini ulikuwa haufunguliwi, ilibidi mlinzi atumie vitisho ndo jamaa kufungua mlango.

Baada ya kufungua ilibidi tuingie wote ndani na wakati huo alionekana Iryn akiwa anahema sana, alionekana ni mtu aliyekuwa amechoka sana kama alikua jogging.

Kwa upande mwingine ni kama alikua haamini macho yake kama sisi tuko pale, na pant yake ya jeans ilionekana imefunguliwa nzipu na chupi yake ya pink ilionekana kwa mbali, pia upande wa juu alikua na brass kama ungeendelea kumwangalia ungeishia kudindisha tu kwa ule uzuri wake na alivyokuwa vile.

Iryn alikuja haraka kwangu na akanikumbatia na alianza kulia palepale, na dada Manager alikua kafika eneo la tukio tayari, na akaanza kuhoji ni nini kinaendelea pale.

MANAGER: “Ni nini kinaendelea hapa, maana matukio yanayoonekana hapa ni kama ubakaji, kaka shida ni nini?”

Jamaa alikua kimya na ikabidi dada ahamie Upande wa Iryn.

IRYN: “Dada mimi najishughulisha na masuala ya body therapy hii ndo kazi yangu, na ninafanya kwa wateja wengi sana. Huyu mteja tuliwasiliana toka juzi hata chats zetu hizi hapa (muda huu Iryn alikuwa ameshika simu yake Iphone 13 Pro Max ambayo ilionekana kuweka crack kubwa kwenye kioo na akamwonesha zile chats manager).

MANAGER: “Haya ndo makubalino yenu, endelea nakusikiliza”

IRYN: “Tulikubaliana ninafanya massage na sio zaidi na alikubali, nimemaliza kazi yangu naomba malipo akasema hawezi…..”

Dada Manager alimkatisha Iryn na alimwuliza swali,

MANAGER: “Malipo mlikubaliana kiasi gani?”

IRYN: “Tulikubaliana $1500”

MANAGER: “Okay Endelea”

IRYN: “Nilivyomaliza kazi yangu niliomba malipo yangu lakini alianza kuomba sex, nilimwambia I can’t do sex ni nje na makubaliano yetu na nilimkumbusha we had a deal, akanambia ataniongezea $1000, lakini nilimkatalia na nilimwambia hata apandishe dau kiasi gani siwez fanya sex. Na yeye akasema bila sex hanilipi na mimi sikutaka kubishana naye nilivyotaka kuondoka nilishindwa fungua mlango sababu ya card, na yeye akagoma kufungua mlango, nikaomba card ili nifungue mlango lakini hakutaka kunipa wala kunifungulia.”

SHAHIDI: “Pole sana dada huu ni ubakaji.”

IRYN: “Muda huo akanivuta kwa nguvu na akanisukumia kitandani akanambia siwezi kutoka mpaka tusex. Muda huu nilikua sijui cha kufanya maana nilipiga kelele lakini hakuna msaada wowote niliopata. Ilibidi nimwambie atafute condom bila hivyo sitoweza na alikwenda kuchukua kwenye bag. Mimi muda huo ndo nikapata nafasi ya kutuma text kwa dereva wangu huyu hapa. Alivyorudi akanambia nivue nguo zangu lakini nilimgomea sababu nilikua najua dereva wangu atakuja haraka kunisaidia. Alinishika kwa nguvu akanivua brauz yangu na tukaanz purukushani kwa zaidi ya dk 20 sasa, inamaana msingekuja leo ningekua raped.”

Maneno ya Iryn yalifanya tusijikie vibaya wote muda ule na kila mtu alikua anashangaa kwa lile tukio. Jamaa alikua anaforce kula mzigo tena kwa kutaka kubaka.

Kiukweli hata mimi ningeforce muda ule yaani uwe na mrembo kama yule umwache aende ni inataka moyo sana. Jamaa kimuonekano alikua ni lightskin na alikua ni mtu wa Uingereza.

Muda ule jamaa alianza kuomba msamaha kwa kile kilichotokea na alikiri alikosea sana, upwiru ndo ulimplekea kufanya vile.

SHAHIDI: “Kaka nadhani mpaka sasa ushahidi upo na wewe umekiri nafikiri sheria zinaweza kuchukuliwa.”

Jamaa alimfata Iryn na alimwomba sana msamaha maana nadhani alikua anajua kwa UK raping na harassment ni kesi kubwa sana.

Kwa upande mwingine Manager naye hakutaka mambo yafike mbali na alikua akijaribu kutafuta solution na Mlinzi, maana wao ile ni biashara isingeleta picha nzuri kama kesi ingefika mbali.

MANAGER: “Dada naomba haya mambo yaishe hapahapa please nakuomba sana.”

IRYN: “Dada hivi unavyoomba haya mambo yaishe kirahisi hivi ningebakwa je? Ungesema hivi?”

SHAHIDI: “Dada mimi nimerecord maongezi yake akiwa ameconfess alichofanya nafikiri nenda kashitaki huu ni unyanyasaji.”

Kwa upande mwingine jamaa alikuwa haamini macho yake na alionekana kuwa na wasiwasi sana. Na pia alikua akijutia kwa alichofanya muda ule na aliendelea kuomba yale mambo yaishe kwa namna yoyote. Kilichoniuma sana kuona jamaa kapiga magoti akiomba msamaha, kama mwanaume nilijiskia vibaya sana kuona baharia anapiga magoti.

Mimi niliteta na Iryn pembeni nikamwambia amsamehe Jamaa, sababu hajamfanya kitu chochote zaidi ya kumharras afanye kusamehe tuendelee na mambo mengine maana kwa Tanzania kesi kama hizi ni kupoteza muda. Iryn alinambia anaweza mpigia simu Mama Janeth na akaisimamia kesi na sheria ikachukua mkondo wake. Mimi nikamwambia cha muhimu jamaa amlipe simu yake, pesa ya simu mpya na usumbufu, mengine amwachie Mungu tu, na Iryn alikubali kufanya hivo.

“Insider nasamehe kwa sababu yako, ila alichonifanya siwezi kusahau ni udhalilishaji na unyanyasaji.”

IRYN: “Manager kutokana na masuala yenu ya kibiashara nitajali hili maana kuna siku nitarudi tena hapa ila ninauwezo wa kuiendesha hii kesi vizuri kabisa. Naomba nilipwe pesa ya simu mpya, hii imecrack sababu yake, anilipe pesa yangu $1500 na ninataka $4000 za usumbufu, simu ni kama $1800 kama yuko tayari kutoa $7500 mimi nitasamehe.

SHAHIDI: “Dada kwanini unamsamehe kirahisi hivyo wakati ushahidi upo na atakulipa pesa kibao, usiwe na haraka naweza kukusaidia Mwanasheria.”

IRYN: “Dada ni kweli unachosema ila sisi sote ni Binadamu kuna kesho, nina Mama yangu yuko Organization X ningempa taarifa hii kesi ingeisha haraka, ila nimeamua kusamehe tu.”

Jamaa ni kama hakuamini Iryn ameamua kumsamehe na jamaa aliomba alipe $6500 maana yuko Tanzania kikazi. Iryn aliamua kukubali na jamaa akafanya kutransfer hiko kiasi kwenda kwenye account ya Iryn

RAPIST: “You have an account in french bank?”

IRYN: “Yeah, transfer that amount to my account number.”

Pale wote tulibaki tunashangaa hata jamaa kama hakuamini kuona Iryn anamiliki Account kwenye moja ya bank za kifaransa, hata mimi nilishangaa maana Iryn hakuwai nambia hili, lakini pia sikuwaza sana maana nilikuambuka Iryn kasoma kule Ufaransa asingekosa kuwa na bank account kule.

Baada ya kutransfer Iryn alipata ujumbe kwenye email kuonesha pesa imeingizwa na akaaga tuondoke maana hakutaka tuendelee kukaa pale.

Na muda ule Manager alifurahi sana kuona jambo limeisha na alitusindikiza mpaka parking na muda huu walikua wakiongea na Iryn, mimi niliingia kwenye gari na nikatoa 50,000 nikampa mlinzi na alishukuru sana.

“Kaka Ahsante sana ila Bossy wako ni pini asee ni ngumu sana kuwa na mrembo kama huyu Getto afu umwache, ni balaa sana hii Dunia ina warembo wengine tunaishia kula kwa macho.”

Niliishia kucheka pale na tukaagana na jamaa pale. Manager aliendelea kuongea na Iryn na baada ya dakika 5 Iryn aliingia kwenye gari.

IRYN: “Insider lets go, twende home tu nikalale sina mood now.”

Tulianza kuondoka na muda ule kutoka eneo lile.

MIMI: “Iryn am so sorry for being late, nilikua nimelala yaani kitendo cha kupiga simu ndo nilishtuka”

IRYN: “I thought umelala that time hata hivyo thank you so much Insider ungechelewa kidogo ningebakwa. Kitendo cha kupiga simu ndo kilipelekea simu kuvunjika nilipambana sana.”

MIMI: “Nisingejisamehe maisha yangu yote kama jambo baya lingetokea, It was my fault”

IRYN: “It wasn’t your fault Insider, don’t be”

MIMI: “Yule ni nani na mlikutana wapi?”

IRYN: “Isabella ndo kani connect na huyu mtu, na mimi namuamini sana Isabella hata wateja anaonipaga sinaga shida nao.”

MIMI: “Pole sana Mummy unaonekana kupoteza so much energy”

IRYN: “Insider nimepambana sana usiione hivi kumbuka yule mwanaume ananguvu kuliko mimi.”

MIMI: “Ilishawai kukutokea kama hii before?”

IRYN: “Hii ya leo ni too much, ilishawai nitokea ila sio kama ya leo, wengi nilokutana nao walikua hawanilipi.”

MIMI: “Pole sana najiskia vibaya ujue.”

IRYN: “Ni moja ya changamoto za kazi.”

MIMI: “Pole sana Mummy.”

IRYN: “Hii weekend sitotoka usiku maybe next week.”

Sikutaka kabisa kuleta utani hii siku maana Iryn alikua kabadilika sana na hakuwa mtu wakuongea. Na muda huu yule jamaa alikua anampigia simu Iryn, lakini Iryn hakutaka kupokea simu yake.

Tulipitia pale Mikocheni kwa Osama na nikamnunulia Iryn chips yai “zege” nilijua lazima ana njaa, tukaendelea na safari yetu ya kwenda kijitonyama.

Tulifika pale kwake na muda huo saa 6 usiku ilikua tayari, na nikampeleka mpaka ndani na nikamwaga naondoka nitamcheki .

IRYN: “Insider…”

MIMI: “Naam Mummy”

IRYN: “Thank you for today bila wewe ningeweza pata jambo baya sana.”

MIMI: “Usijali Iryn sisi ni Familia tayari.”

IRYN: “Naomba nipe account yako ni transfer Pesa, sina cash ya kukupa.”

MIMI: “No usifanye hivo.”

IRYN: “Why? you saved me today.” Iryn alikua mkali kidogo.

MIMI: “Have you forgotten our agreement?”

IRYN: “I remember”

MIMI: “So don’t, byee”

Muda huo Iryn hakujua aseme nini aliishia kuniangalia nikipotea machoni pake, na mimi nilitoka hapo nikarudi home kulala.

###########

Jumamosi ndo siku ambayo nilikua na miadi na Mama wa2 kama tulivyokuwa tumekubaliana mwanzoni mwa week. Nilifika kwake saa4 kasoro asubuhi na baada ya kufika pale, nilimpigia simu niko nje akasema sawa.

Hapa alipokuwa anakaa Mama wa2 ni apartment ambayo ina nyumba 2 tu, tena za kujitegemea kwenye compound moja.

Baada ya dakika chache alikuja dada wa kazi na akanifungulia geti akanambia amesema dada uingie ndani. Niliingiza gari nje kwake parking na nikaingia ndani seblen, sikuwa na wasiwasi sababu nilikua najua hana mme.

Upande mwingine alionekana dada akiandaa chai dining, na muda mfupi mama wa2 alikua katoka na amependeza sana.

MAMA WA2: “Insider mambo!”

MIMI: “Salama Mama mkwe , umependeza sana.”

(Alikua amevaa kipensi cha jeans na tishirt nyeupe zile za kubana)

MAMA WA2: “Eti eeh, karibu chai bhasi”

Na muda huu alikua akielekea dining na mimi nikamfuata kwa nyuma,

Mama wawili akaniandalia chai pale na tukaanza kunywa. Ilikua ni chai ya maziwa, chapati za maji, na maini ya roast.

MIMI: “Rachel yuko wapi? Simwoni”. (Rachel ni yule mtoto wake wa pili ambaye nampelekaga shule)

MAMA 2: “Rachel kalala bado.”

MIMI: “Muamshe mke wangu bhana.”

MAMA 2: “Yule akilalaga anamka mwenyewe.”

Baada ya ya kupata breakfast nilimshukuru Mama wa2 kwa chai na yeye alikwenda chumbani akatoka na mkoba, akasema yuko tayari kwa safari tuondoke.

Tukitoka pale kwake ilikua saa 4 na tukaanza safari ya kwenda Bagamoyo “The horizon”.

MAMA 2: “Insider itabidi tuingie ATM ya CRDB nitoe pesa sawa?”

MIMI: “Sawa bossy wangu, kuna ATM nitakupeleka.”

MAMA 2: “Nilishakwambia mimi sio Bossy wako.”

MIMI: “Sawa mama mkwe.”

MAMA 2: “Unakujua tunakokwenda?”

MIMI: “Ondoa hofu mimi ndo Insider.”

Tulitumia barabara ya Mwaikibaki ya Mbezi beach chini na tukaingia na ile barabara ya Mwamunyage, tukaja tokea kunduchi road hao tukaunga na Bahari beach.

Kabla hujafika Budget mbele kidogo ya Jambo supermarket kuna ATM za “NMB & CRDB upande wa kushoto wa barabara kama unakwenda Budget. Niliingia pale ili Mama wa2 aweze kutoa hela kama alivyokuwa ameomba.

MIMI: “Toa pesa nyingi bhasi tupate na hela ya mafuta.”

MAMA 2: “Leo nitakupa offa ya mafuta full tank”

MIMI: “Mvua itanyesha, unafanya kazi bank ila ni mbahili balaa.”

Muda huo alikua ameshuka kwenye gari ili aingie kutoa hela, lakini kulikua na foleni hivyo ilibidi asubiri mpaka ile foleni iishe na yeye ndo aingie. Si unajua mambo ya weekend tena, foleni ya kutoa pesa ilikua kubwa kubwa.

Mama wa2 alitumia kama dakika 5 mpaka anatoa hela na hao tukaondoka kuendelea na safari yetu.

MAMA 2: “Insider ukiona sheli ingia tuweke mafuta.”

MIMI: “Mama mkwe kumbe ulikua serious?”

MAMA 2: “Ulifikiri utani?, sasa subiri uone”

MIMI: “Leo unaonekana una vibe sana.”

MAMA 2: “Insider sijatoka muda mrefu sana, sijui ndo kuzeeka?”

MIMI: “Bado mbichi kabisa wewe, na unawazidi watoto wa 2000 mbali sana.”

MAMA 2: “Hahahaaa! Insider ningekua nimeolewa kama unayosema ni kweli, ona nimeishiwa kuzalishwa tu.”

Na muda huu tulikua tumeingia sheli ya ORYX pale Bahari Beach.

Na muda huu nilikua namsikiliza mama2 aseme tuweke mafuta ya shilling ngapi, na dada pale sheli alikua kaja upande wa dirishani kutusikiliza.

MAMA 2: “Dada weka full-tank”

Gari yangu ilikua na bar 2 tu za mafuta, sasa nilivyosikia full tank, nilifurahi sana.

Baada ya kujaza gari full tank, mama wa2 alilipia na nikaomba risiti kwa dada, nilikua siachi risiti baada ya kujaza mafuta.

MAMA 2: “Umeona eeh, leo nimekupa offa maana sjawai kukupa offa, japo wewe unanipaga offa sana.”

MIMI: “So unalipiza?”

MAMA 2: “Hamna narudisha fadhila tu.”

Ukweli ni kwamba licha ya kuingia mkataba na Mama wa2 ila bado nilikuaga nampa offa mfano, sometimes kama niko Posta nataka rudi home nilikuaga nina mpigia simu afu nampick nampeleka kwake for free, sababu tulikua tunakwenda njia moja.

Tulikwenda moja kwa moja na Bagamoyo road tulivyofika kijiji kinaitwa Zinga kuna sehemu tuliingia kulia, ilikua ndo njia ya kwenda “The Horizon”.

Muda tuliotumia kutoka Mbezi Beach mpaka tunafika Horizon ilikua ni kama saa 1 na nusu, na tulikwenda kuna sehemu moja ilikua imetulia na imejitenga.

Alikuja kaka ambaye ni mhudumu wa pale kutusikiliza na mama wa2 aliomba apewe mocktail na mimi niliagiza mocktail pia. Mocktail niliyoagiza mimi inatengenezewa ndani ya nanasi. (Nanasi linatobolewa afu mixers zinawekwa humo, ni nzuri sana)

Mama wa2 alinonekana kulipenda eneo hili jinsi ya utulivu wake na pia kulikuwa na watu wastaarabu sana maeneo haya.

Tulitoka hapo tukaenda sehemu ya Range (kupiga shabaha), mama wa2 akawa anapiga shabaha zake pale na mimi nilimwacha mimi nikarudi kukaa.

Muda huu Mary alinipigia simu na nikapokea simu yake haraka;

MIMI: “Hi Mary”

MARY: “Salama uko poa?”

MIMI: “Niko poa Mary, siku yako inakwendaje?”

MARY: “Leo ni weekend uliahidi tunatoka out.”

MIMI: “Yes nakumbuka ila niko Bagamoyo kuna mteja nimemleta huku namsubiri kama nitawai rudi nitakucheki sawa?”

MARY: “Sounds like today’s impossible.”

MIMI: “No I can’t break my promise.”

MARY: “Insider sema hutaki tu, hauko Bagamoyo wala nini.”

MIMI: “Mpaka nikutumie Location ndo uniamini?”

MARY: “I don’t trust you.”

Baada ya kumaliza kuongea naye nilimtumia palepale Location na Mary alionekana kukasirika sana. Sasa baada ya kumtumia Location kwa whatsapp na palepale alinipigia simu tena;

MARY: “Insider Horizon uko na nani?”

Hapo ndo nikakumbuka kumbe location niliyomtumia imeniumbua.

MIMI: “Nimemleta mteja Mary, si nimekwambia lakini?”

MARY: “Insider acha kuniona mimi mtoto, yaani umepeleke mteja Horizon na umsubirie tu, from nowhere?”

MIMI: “So you don’t trust me?”

MARY: “Insider mimi sio mtoto, huko upo na demu mnakula bata not more, anyway mimi sio mtu muhimu Kwako na nilishaliona hili.”

MIMI: “Mary huko unafika mbali sasa, nyie ni washikaji zangu sana.”

MARY: “Prisca akiomba date muda wowote unamkubalia ila mimi naomba kwa mara ya kwanza unani avoid.”

MIMI: “Mary si nimekwambia nikirudi nakucheki? Usinilaumu wakati siku haijaisha, kumbuka hii ni kazi yangu.”

MARY: “Insider bye have a good time there”
Na mary akakata simu.

Mary alionekana kuwa na hasira sana alikua kama mtu aliyepaniki na mimi nikampotezea sikutaka kujihangaisha naye kabisa.

Na baada ya saa mama wa2 alirudi kutoka range na alikuwa anahema sana;

MIMI: “Vipi kulikoni?

MAMA WA2: “Insider nimepatia shabaha 2, hahahaah” alikua akicheka

MIMI: “Muda wote huo ulotumia ndo umepata shabaha 2 tu?”

MAMA WA2: “Eeh Insider.”

MIMI: “Unachezea hela tu.”

MAMA WA2: “Afu kwanini umenikimbia?”

MIMI: “Niliona michezo ya kitoto ile.”

MAMA WA2: “Eeeh mimi nimeupenda mzuri kweli.”

MIMI: “Sawa bhana”

Na muda huo alikuja jamaa mmoja akasema kama tunataka kwenda kisiwani kuna boti inatoka beach sa10 na gharama zake ni 10,000 kwenda na kurudi kwa kichwa. Na mama wa2 alifurahi hizo taarifa na akalipa 20,000, alinilipia na mimi.

Na muda huo tuliagiza chakula maana ilikua ni mchana saa7 tayari imefika na njaa zilikua zikiuma sana. Tuliendelea kupiga story pale na tulikua tukizungumza sana mambo ya maisha, Mama wa2 alikua ni mtu ambaye alikuwa na mipango mingi sana.

Kupitia mazungumzo yetu niliweza kujua kwamba Mama wa2 anajenga nyumba Madale, pia anabiashara ya kutoa huduma za kifedha kwa simu na Bank. Hivyo akanambia anampango wa kufungua biashara ya mapazia na urembo wa nyumba.

Aliniuliza mipango yangu pia na sikusita kumwambia baadhi ya mipango yangu, nilimwambia kesho ambayo jumapili ninakwenda Dodoma kwaajili ya mambo ya ujenzi. Na alinipongeza sana akanambia kama nitahitaji mkopo kutoka bank nimwambie atanisaidia kupata kwa haraka na bila masharti mengi.

Tulizungumza mambo mengi sana na alikua pia akiniuliza sana kuhusu origin yangu na kuhusu familia yangu na maisha yangu kwa Ujumla.

MAMA WA2: “Hivi Insider unakaa wapi?”

MIMI: “Mbezi Massana kule juu.”

MAMA WA2: “Kumbe hutokei mbali.”

MIMI: “Sio sana ila kuna kaumbali.”

MAMA WA2: “Kidogo kule kumechangamka sana.”

MIMI: “Sababu ya Hospital naona pia ni kama kacentre flani hivi.”

MAMA WA2: “Chuo umesoma wapi?”

MIMI: “Chuo X “

MAMA WA2: “Mtoto wa mjini wewe, ndomana baada ya kumaliza chuo hukutaka kurudi home.”

MIMI: “Niliamua kuhustle hapahapa mjini. Hivi kwanini huna mpango wa kumiliki gari.?

MAMA WA2: “Nilikua na gari mbona, mwakajana nilipata ajali mbaya sana Insider na gari ilikua haifai. Nashukuru Mungu nilitoka salama kabisa, niliitengeneza ila gari na nikauza, sitak kusikia tena habari za gari, ila nikimaliza ujenzi nitanunua.”

MIMI: “Pole sana na ilikua gari gani?”

MAMA WA2: “Harrier, na nilichukuaga mkopo kisa gari.”

MIMI: “Pole sana Mama mkwe.”

MAMA WA2: “Ahsante, gari hata mwaka haikufikisha ikala mueleka.”

Na baada ya kumaliza kula tuliagiza wine na tukaendelea kunywa taratibu pale huku story zikiendelea.

Mida ya saa 10 jioni tulitoka na kwenda Beach kwaajili ya kwenda kisiwani, sasa kama unakwenda kupanda boti beach kuna kidaraja cha mbao kizuri sana na watu wanapendaga sana kupiga picha pale. Na pale Mama wawili alinipa simu yake nimpige picha na mimi sikuwa na hiyana nikampiga picha za kutosha.
(Kwa mtu anayekwenda Horizon lazima apige picha pale)

Tulipanda kwenye boat na kwenda kisiwani, Boat lilikua kubwa na tulikua kama watu 30 mle ndani. Kilikua ni kisafari cha kama dakika 20 mpaka kufika kisiwani. Muda huo kila mtu alikua na simu yake akichukua self wengine wakichukua video na wengine wakipigana picha, ilikua ni burudani kwakweli.

Tulifika kisiwani na tuliwakuta watu wengine kule, yaani kulikua na watu kibao pale kisiwani. Ni kisiwa kadogo sana wala sio kikubwa kihivyo. Na mle kisiwani kulikuwa na michezo kibao kama mpira wa miguu, na wanawake walikua wakicheza netball, ilikua ni burudani sana asee.

Tulikua watu wazima mle kisiwani na full vibe wanawake walionekana na vichupi, wengine taiti nknk, wanaume wapo waliokuwa na boxer na wengine bukta. Mimi nilikua nimevaa track nikavua nikabaki na boxer, kwa upande mwingine nilimwona mama wa2 kwa mbali akiwa na taiti alivua kile kipensi chake.

Tulitengeneza timu za watu sita (6) na zilikuwepo team 3 sasa ilikua ni mtoano. Tulilisakata kabumbu pale na kila mtu alikua na vibe sana mle kisiwani. Hakuna sehemu ngumu kusakata kabumbu kama Beach asee unatumia sana energy watu walikua wanaflop balaa.

Kuna muda tulipumzika na Mama wa2 akaomba twende upande wa2 wabahari na akaomba nimpige picha.

Tulikaa pale mpaka saa 12 ndio tukaanza kutoka pale kisiwani, wakati tumepanda kwenye Boat, Nahodha aliuliza kama wote tumefika kabla hatujaondoka na seat zote zilikuwa zimeenea.

Tulitumia kama nusu saa hivi kuwasili pale Beach na tulirudi tukakaa na tuka order vinywaji, muda huu palionekana kupendeza sana maana kulikuwa na watu wengi wakinywa, wakienjoy maisha.

Mama wa2 aliagiza Savannah na mimi niliagiza Heineken kinywaji changu pendwa. Muda ule hata mimi nilikua nahamu ya kuvibe, maana sikuwa na miadi na Iryn. Nilichungulia simu yangu na nikakuta, Prisca, Mary na Mama J wamenipigia simu.

Nilishangaa sana kuona Mama J kanipigia simu na alikua kanitumia text ambayo ilisomeka

“Naona nimekupa chance ya kuwa na Malaya wako ndomana hunitafuti.”

Palepale nilitabasamu nikasema Mama J tayari hasira zimeisha. (Mama J ni mtu ambaye hapendagi kufosiwa huwa anataka maamuzi afanye mwenyewe ndomana mimi na yeye tukigombana, huwa namuacha atulie kwanza au anitafute mwenyewe hapo ndo tunayajenga).

Nilimuaga Mama wa2 naenda kwenye gari maramoja ili nimpigie simu, na nilitumia muda huo kumpigia Mama Junior lakini hakupokea simu, nilipiga mara3 lakini hakupokea simu zangu.

Muda huo nikampigia simu Prisca na alipokea muda uleule ni kama mtu ambaye alikua akisubiri simu yangu kwa hamu sana.

PRISCA: “Hi Insider”

MIMI: “Safi tu, now uko sawa?”

PRISCA: “Yeah, ulisema tuonane tuongee”

MIMI: “Ndio nafikiri tufanye J3 Prisca maana kwa leo itakua ngumu si unajua leo ni weeknd kazi ni nyingi?”

PRISCA: “Jumatatu ni mbali sana why not tomorrow?”

MIMI: “Kesho nasafari ya Dodoma ndomana nikasema nitakuona Jumatatu.”

PRISCA: “Insider unaondoka hata hunambii are you serious?”

MIMI: “Sorry hata hivyo safari imetokea haraka tu, haikuwa kwenye mipango yangu.”

PRISCA: “Unakwenda kufanya nini Dodoma?”

MIMI: “kuna kazi mzee amenituma nikaifanye.”

PRISCA: “Kazi gani.?”

MIMI: “Prisca sijajua bado ila nikienda ndo nitajua maana kuna mtu nitaonana naye nikifika.”

PRISCA: “Na unarudi lini?”

MIMI: “Prisca si nilikwambia narudi jumatatu na tutaonana? Nitatumia ndege ili niwai.”

PRISCA: “Okay nilisahau na unaondoka muda gani?”

MIMI: “Natakiwa kuchek-in saa 2 asubuhi naondoka saa4”

PRISCA: “See you later, byee.”

Kuhusu Mary sikutaka kuhangaika naye hata kumpigia maana nilikua sina cha kumwambia muda ule, zaidi ningemdanganya tu.

Muda ule nilirudi kwa Mama wawili na tukaendelea kunywa pale, Mama wa2 akaanzisha maongezi,

MAMA WA2: “Vipi ulienda kuomba ruhusua nini?”

MIMI: “Hahaahaa nilikwenda chukua chaji ya simu na muda huu nilikua nimeishika mkononi.”

MAMA WA2: “Kama wamekupigia simu sema bhana tuondoke.”

MIMI: “Wewe ukisema tuondoke ni sawa mimi sina shida kabisa. Nikalale mapema kesho nasafari asubuhi.”

Nilikaa pale tukaendelea na story na muda ule Mama wawili alinonekana na furaha sana,

MIMI: “Mama mkwe naona leo unafuraha sana kuliko siku zote.”

MAMA WA2: “Leo nimeinjoy sana kule Beach honestly huku nitakuja tena, nilikuona unasakata kabumbu upo vizuri sana.”

MIMI: “Mpira ni kipaji changu sana, nimechezea team ya shule wakati niko form4 na 6.”

MAMA WA2: “Nilikuona asee unakimbiza balaa.”

MIMI: “Si unajua life is too short, If you get a chance celebrate.”

MAMA WA2: “You only live once”

MIMI: “Vipi lakini kuhusu mwanao Pili anaendeleaje na masomo?

(yule mtoto wake wa kwanza ambaye yuko Advance).

MAMA WA2: “Yuko salama kabisa na jana nimeongea na Matron wao yuko vizuri.”

MIMI: “Anasoma wapi?

MAMA WA2: “Yuko hapo Kerege Marian Girls.”

MIMI: “Sasa mbona hukusema tupitie kumsalimia?”

MAMA WA2: “Insider kuna tarehe special za visiting, pia watapewa likizo kwaajili ya Easter.”

MIMI: “Hongera sana kwa kuwa na bint mkubwa, soon utaanza kula matunda yake.”

MAMA WA2: “Insider sipendi bint zangu waje kuwa kama mimi mama yao.”

Na muda huu tuliongeza vinywaji vingine na mama wa2 alikua akitawala mchezo katika maongezi.

MIMI: “Kwanini? Maana mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.”

MAMA WA2: “Insider you know sometimes sisi wanawake tunapitia vipindi vigumu sana, kuna mwanaume kukuoa na mtoto ni ngumu sana. Mimi siwezi kuwa na mume tena mpaka kufa kwangu.”

MIMI: “You never know, sometimes Mungu anakua na mipango yake huwezi jua kakupangia nini na amekuepusha na nini.”

MAMA WA2: “Unajua sometimes tunamwonea Mungu, kwamba alipanga mimi kuwa single mother?. Unajua Mwanamke bila mume hajakamilika, hakuna mwanamke asiyependa kuolewa Insider. Mwanaume ni kama kiongozi kwenye mahusiano au familia, unafikir najiskiaje kuona wanangu hawawaoni baba zao? Mwanaume mpaka ajiskie ndo anakuja kumwona mtoto atlist rachel anamwona Baba yake mara kwa mara ila Pili anaenda mwaka hajamwona Baba yake.”

MIMI: “Aisee pole sana, unakidonda kikubwa sana Mama mkwe.”

MAMA WA2: “Usione tunavaa tunapendeza tunacheka lakini nakidonda kikubwa sana moyoni. Nashukuru Mungu na kazi ambayo inanipa kipato napata pesa ya kuishi na Familia yangu.”

MIMI: “Kwani Baba yake na Pili yuko wapi?”

MAMA WA2: “Yuko Mwanza ni moja ya wanaume ambao wamesababisha mimi leo kuwa hivi.”

MIMI: “Kwanini unasema hivyo?”

Kwa kifupi kutokana na maelezo ya Mama wa2 alisema alikutana na Baba Pili mwaka 2003 mwanza wakati anafanyia kazi kampuni moja huko. Baada ya hapo wakaanza mahusiano na Baba yake Pili ni mfanyabiashara, hatimaye akapata mimba ya Pili ila baadae alikuja kujua jamaa ana mke na watoto wa2. Na kipindi hicho alianza kupata vitisho kutoka kwa mke wa jamaa, na pia kutokana na kuwa na mimba kampuni ikamwachisha kazi ikabidi afanye mchakato wa kurudi kwao Moshi kwa Mama yake.

Baada ya kuzaa alikaa kama miaka 2 kwao akimlea mtoto na hicho kipindi chote Baba mtoto hakuwai mtafuta wala kujua hali yake. Baada ya hapo alianza kutafuta kazi na akapata moja ya shirika pale Moshi na alifanya kazi mpaka 2012 ndo akapata connection na moja ya wateja wake. Anasema kwenye lile shirika alikuwa akilipwa mshahara kidogo sana na kipindi hicho alikua anakaa kwao. Huyo mtu alimuunganisha Mama wa2 na huyu mtu ambaye ndo Baba yake Rachel kwa sasa.

Baada ya kupewa namba za Baba Rachel aliwasiliana naye na akamtumia CV yake, Baada ya Mwezi alimpigia simu aende Dar es salaam kwaajili ya training. Mama wa2 anasema alishangaa sana maana hata hakufanya Interview yoyote, jamaa alifanya kumsaidia tu. Alifika Dsm na alikutana na Jamaa ambaye alimpokea na baada ya kumaliza training alipangiwa kazi hapahapa Dar es Salaam. (Baba yake Rachel ni moja ya watu wakubwa sana kwenye hiyo Bank hapa nchini na ni moja ya Directors anaonekana sana kwenye TV).

Baada ya hapo Jamaa alimtongoza kutokana na jamaa kumsaidia hakusita kumkatalia sababu ndo aliyemsaidia kupata kazi. Lakini Jamaa alimwambia kuwa ana mke tayari na wakakubaliana akipata mtu sahihi awe huru kuolewa naye. Waliendelea kuwa na mahusiano ya siri mwisho wa siku akapata mimba ya Rachel, hakutaka kutoa mimba ikabidi azae tu ndo kupata mtoto wa pili.

MIMI: “Aisee yule ndo Baba yake Rachel?”

MAMA WA2: “Ndio yule ni Baba yake Rachel, Nashukuru anampenda sana mwanaye huwa anatafuta muda sana wa kukaa ba Bint yake japo ndo siri mke wake hajui lolote.”

MIMI: “Kama anajali mtoto sio mbaya, vipi kuhusu Baba Pili ndo alitelekeza mtoto.?”

MAMA WA2: “Baba Pili alikuja kunitafuta wakati Pili ana miaka 2 ndo kidogo akaanza kutuma Pesa za matumizi na kumwona.”

MIMI: “Mama mkwe ulipitia kipindi kigumu sana, pole sana.”

MAMA WA2: “Ahsante kipindi niko pale Moshi na lile shirika nilipata mwanaume ambaye alinipenda sana na alikua tayri kunioa ila nilivyomwambia nina mtoto alikimbia nduki na hakuwai nitafuta tena, kwa ujumla nilipata wanaume 3 lakini wakisikia habari ya mtoto ndo inakua tiketi ya kuondoka.”

MIMI: “Muda bado Mama Mkwe utapata tu wa kukuoa usiwe na wasi wasi umri bado unaruhusu.”

MAMA WA2: “Insider Mwanaume kamili aliyekamilika ambaye hatumii hisia kwenye maamuzi hawezi kukubali kuoa mwanamke aliyezalishwa na Mwanaume mwingine. Insider wewe uko tayari kuoa mwanamke ambaye amezalishwa na mwanaume mwingine?”

MIMI: “Hapana kwakweli siwezi.”

MAMA WA2: “Sasa unaona! Mimi huwa nawashangaa sana vijana wanaoa single mothers hata kama ni kupenda ila ni Risk sana.”

MIMI: “Aisee kwamba hutaki Single mothers waolewe?

MAMA WA2: “Hapana ila kwa Mwanaume hakikisha Baba mtoto amekufa na akuonyeshe kaburi otherwise hesabu maumivu. Ila wapo wanawake single mothers wanajitambua ila ni wachache sana.”

MIMI: “Unachosema ni kweli na upande wa Single fathers?”

MAMA WA2: “Tofauti wanaume anaweza kuzaa na mwanamke yoyote yule, wanaume wana tamaa tofauti na mwanamke anazaa na mwanaume anayempenda regardless kama anapendwa au laah!”

MIMI: “Naona leo umenipa lecture ya Mapenzi.”

Na muda huu tulikua tunaendlea kunywa bia kwa wingi sana kama ratiba za kurudi home zilipotea hivi,

TUTAENDELEA!
Mkuu, uzi wa hadithi yako nilikuwa nnaupuuzia sana kila nilipokuwa nnafungua jf. Lakini siku nilipoamua kufungua na kusoma episode ya kwanza nimevitiwa sana kuendelea kufuatilia.

Nnakupa pongezi sana kwa hadithi hii, kama ni ya kweli umepitia mengi mazuri na mabaya na ndio yanafanya mtu awe na hekima. Lakini kama ni ya kutunga basi una kipaji kikubwa sana.

Mchango wangu.

1.Usiifanye hadithi iwe ndefu sana, watu wanatamani kujua mwisho utakuwaje jaribu kupunguza vitu ambavyo sio vya lazima.

Hata kama hadithi ni nzuri ila kama ni ndefu sana inafikia sehemu watu wanapoteza hamasa kuifuatilia.

2. Episode ya mwisho haijaisha vizuri na wewe unajua hilo bila shaka.

Nina tumaini episode inayofuata itakuwa vizuri zaidi.
 
Story inaanza ndani.ya miaka miwili kazini ametengeneza million 24 .

Halfu alikuwa intern wale wataesa wanaolipwa laki 4 .halfu muda huohuo akafungua biashara ya hardware kama sijakosea.

Hata kama ni upigaji Ila kwa million 24 alitupiga
Kuna Madogo wanafanya kazi za kukusanya Ushuru huko Mipakani na Vile vimashine ukiwaona utawadharau, wanapiga sana hela. Kuna mmoja kwa mwezi alifikisha Zaidi ya milioni 10 kama malipo yake. Kipindi kile mahindi yanavuka sana border kwenda Kenya.

Kwahiyo upigaji wa pesa unategemea na namna gani unajituma katika maisha yako na kazi unayofanya.
 
Alika na ndugu zako kuwa umepata mradi wa kutukana. Mana hizi ishu zinarithishana kizazi na kizazi. Kuna baadhi ya vinasaba vya Koo fulani zinafanya biashara,michezo,matusi,nk ivyo Ni ngumu mie kubadilisha beliefs,na vinasaba vya kwenu. Naomba alika wote mje hapa Mana inaonekana hapo kwako Ni sawa na mbape ama mesi yupo uwanjani kwake,mie Ni Nani niizuie sumaku isivute chuma wakati ndio kazi iliyoumbiwa
Mkuu keisangora hi uli maliza kabisa 🤒💪.
 
Stori imepoteza mvuto mwandishi hana jipya .

Anatumia Episode nzima kueleza jinsi anavyokula bata na mama wa2.

Kiukweli insider maliza story huko mbele hakuna cha maana.

Ulijitahidi Sana mwanzo Ila kwa sasa Ahsante kwa mchango.

Kujisifia kumekuwa kwingi kuliko hata uhalisia wa jambo.

FICTION STORY
 
Mkuu, uzi wa hadithi yako nilikuwa nnaupuuzia sana kila nilipokuwa nnafungua jf. Lakini siku nilipoamua kufungua na kusoma episode ya kwanza nimevitiwa sana kuendelea kufuatilia.

Nnakupa pongezi sana kwa hadithi hii, kama ni ya kweli umepitia mengi mazuri na mabaya na ndio yanafanya mtu awe na hekima. Lakini kama ni ya kutunga basi una kipaji kikubwa sana.

Mchango wangu.

1.Usiifanye hadithi iwe ndefu sana, watu wanatamani kujua mwisho utakuwaje jaribu kupunguza vitu ambavyo sio vya lazima.

Hata kama hadithi ni nzuri ila kama ni ndefu sana inafikia sehemu watu wanapoteza hamasa kuifuatilia.

2. Episode ya mwisho haijaisha vizuri na wewe unajua hilo bila shaka.

Nina tumaini episode inayofuata itakuwa vizuri zaidi.
Anatunga na amekosa concentration ndo maana amepunguza matukio amebaki na ushenzi wake wa kujimwambafai.


ACHA KUSIMULIA TU.

INACHOSHA NOW
 
Ni story nzuri liyojaa uongo nashangaa mtunzi anaiita true story. Kuna gap nyingi haswa yeye kukutana sana na abiria wa kike na wote wakamshobokea...zile trip za kupeleka abiria private posta...pesa zinavyotiririka upande wake nk

Otherwise ni mtunzi mzuri
Wanaobisha ni wakolomije wanaokaa misituni.
Ila kwa mtu mwenye akili timamu na unayeishi dar utaona sukari imeongezwa.

Mistake wateja wake wote wako single kuanzia mama wawili,maggy,iryn.

Wote wanamkubali na kumuamjni na wote wanampa hela.

Wote wanamshobokea na marafiki zake.

Jamaa anajua kuwapanga washenzi shenzi wanaofuatilia story za kifala kama hii.

Angesema ya kutunga tungemwamini.

Uko sahihi dada
 
Watu wanaamini hii ni true story ya kweli yaani,

hakuna kitu kama icho....sema jamaa anajua kutunga hadithi....leta hadithi mkuu unajua kutunga sana.

Hivi true story nyie mnazijua kweli yaani muajemi akanipa milioni 5 alafu akaniongeza na milioni 2 😅😅😆😅😅 you guys na nyie mnaamini kabisa.....

hivi mnakumbuka jamaa alipewa milioni 3 mwanzo kabisa na muajemi.😁🤣😂 afu muajemi ampe demu vitu vya thamani ya 40milions hapo bado mashine za kisasa zilizopo dubai zinakuja...... demu naye hataki iphone 13 kamuachia msela, na msela naye hataki iphone 13 pro 😆😅😅😅😅😁😁muajemi mwenyewe hata papuchi hataki kweli....

mama alianza kazi mwaka 91 na alikuja kulipwa milioni 45 kwa mwezi na organization X nchi hii hii ya walala hoi.....too much salt....too much sugar..... too much alcohol.....stori za kutunga hizi.....

Hakuna true stori ya hivi ila unajua kutunga sana....mbotswana pia alilala appartment za milioni 3 per month mswana mwenyewe ni black melanin afu jamaa kamezea hakula 😁😁😁

Wewe hunaga gundu kabisa yaani.
Unaishi wapi mkuu??
Huenda crew unayokuaga nayo hamjawahi kutana na mijitu yenye pesa za mchezo mchezo.

Kuna watu wanapesa jama, huyu jamaa hata kama story katunga au niaje ila watu wa hivo wapo kabisa.

Unadhani hizo 5 star hotel zinakaliwa na kina nani?? Ndo hao mabwenyenye mkuu.
Hawa matajiri wa kwenye wilaya wilaya wanakufuru kwelikweli ndo wawe hao wanaomiliki visima na sheli kama siafu.
 
Mkuu unajua kuna watu wanalipwa zaidi ya $300,000/= kwa mwaka na hizi international Organization?? Kwa mtu ambaye ubongo wake uko vizuri bila shaka alishajua Mama yake na Iryn alikua anafanyia kazi Organization gani.

Unashangaa Muajemi kuhonga hizo necklace za almost 30m wakati kuna wabongo wanahonga hadi nyumba? na magari ya kifahari. Unajua wewe unaona ni kama haiwezekani sababu huna hela ila kwa wenye pesa ni vitu vya kawaida sana. Muajemi account zake zilikua zinasoma dollar $2Billions na mapoint kazaa huko, ashindwe kuhonga 30m?, wakati Harmonize anahonga hadi Range 2 [emoji23][emoji23]

Kwa mara ya kwanza nakutana na Muajemi alinipa 1million hio 3m umeitoa wapi mkuu?

Nilijifunza kitu kimoja kwenye hii Dunia, hakuna Mwanaume asiyehonga ila tumetofautina level za kuhonga tu. Kama unaweza kumuhonga demu savanna 5 kuna mtu anahonga gari au nyumba. Ukiwa huna hela unaweza ona haya mambo hayawezekani ila ukipata hela utaona ya kawaida sana.

Iryn alikua mwanamke mzuri sana aisee, tuseme Alibarikiwa tu. Endelea kufuatilia story kuna mambo mengi sana yaliendelea huko mbele.
2 billion dollar kwenye account ni uongo. Unaijua 2bilion dollar
 
EPISODE 19
“A TRUE STORY BY INSIDER”

Saa 4 usiku ndo muda ambao nilimrudisha mama wa2 kwake na alikua kalewa haswa, baada ya hapo na mimi nikirudi kwangu kulala ili asubuhi niwai kuamka na niwai safari yangu.

Jumapili nilikua na safari ya kwenda Dodoma na niliamka asubuhi mapema sana na nikajiandaa kuondoka kuelekea JNIA. Hii siku nilifanya kurequest Uber kwenda Airport na ndo ilikua mara yangu ya kwanza kupanda ndege.

Na muda huo asubuhi dada Tyna alikua amenipigia simu na kunikumbusha niwe on-time kufika pale.

Saa 07:30 nilikua nimeshawasili pale na muda huo Tyna alikua akinisubiri. Sababu alisema anataka tuongee kidogo na mimi. Nilifika pale Terminal 2 na tukaonana na Tyna,

MIMI: “Dada yangu nakuona”

TYNA: “Nambie mdogo wangu za toka ile siku.”

MIMI: “Salama, vipi umekesha leo Airport?”

TYNA: “Niliingia shift ya usiku ndo nimemaliza asubuhi hii.”

MIMI: “Aisee siwezi kuoa mwanamke anayelala nje usiku.”

TYNA: “Na mke wako akiajiliwa huku?”

MIMI: “Si namkataza tu, atachagua moja kati ya mimi au kazi.”

TYNA: “Kwanza hongera kwa kuoa, nilipata taarifa kutoka kwa dada yako Violet (Hili ni Jina halisi la Dada yangu)

MIMI: “Ndo hivyo nilimtia mimba mtoto wa watu ikabidi nijilipue tu.”

TYNA: “Ulifanya jambo jema sana, mwezi huu ujao nitakuja kuwasalimia pamoja na mtoto.”

MIMI: “Uje kweli, vipi kuhusu wewe lini tutakula pilau?”

TYNA: “Insider mimi bado niko sokoni, bidhaa haijapata mteja bado.”

Na muda huu TYNA alikua akicheka…

MIMI: “Usije ukawa unachagua wateja.”

TYNA: “Mdogo wangu sikuhizi wanaume mmekua washenzi sana, ukishampa ndo imetoka hiyo. Waoaji ni wachache sana kwasasa.”

MIMI: “Dada ana watoto wa2 tayari, unatambua hilo.”

TYNA: “Violet anabahati yeye ndo alikua wa kwanza kuolewa kwa wanawake tuliokua pamoja pale mtaani.”

MIMI: “So unaishi wapi kwa sasa?”

TYNA: “Nimepanga tabata segerea.”

MIMI: “Nitakuja kukusalimia siku ila itabidi uanze wewe kuja kwetu.”

TYNA: “Insider nimefurahi tumeonana na tumeongea ni muda sana, muda umefika now unaweza kucheck-in uondoke, uwe na safari njema mdogo wangu.”

Saa 6 mchana nilikua Dodoma tayari na nilifikia lodge moja ipo karibu na CBE. Nilimpa taarifa mzee Mollel kuwa nimefika tayari na kasema atakuja ndani ya nusu saa.

Wakati nimetulia mle lodge simu yangu ilianza kuita kucheki alikua ni Iryn. Nikaipokea simu yake,

IRYN: “Hi Insider”

MIMI: “Za wewe, now Unaendeleaje?”

IRYN: “Niko sawa now, vipi uko wapi? Nataka unipeleke kwa Mama Janeth.”

MIMI: “Sorry niko Dodoma nilipata emergence”

IRYN: “Toka lini?”

MIMI: “Sina hata saa toka niingie hapa.”

IRYN: “Mbona hukunambia kama unaondoka na umepatwa na matatizo?”

MIMI: “Nilipata taarifa jana na mzee wangu nije Dodoma kuna jambo la ku takecare hakuna matatizo.”

IRYN: “Sasa why hukunambia? Insider unaona mambo yako hunishirikishi inamaana bila kupiga simu usingenitafuta kabisa.

MIMI: “Jana nilikua busy na kazi nikasema nitakupigia lakini nilisahau naomba nisamehe Bossy wangu, nitakuletea zabibu kama zawadi.”

IRYN: “Ok no problem na unarudi lini?”

MIMI: “Kesho mchana nitakua huko, siwezi kukaa huku.”

IRYN: “Are you sure au upo kwenye mishe zako.?”

MIMI: “Trust me.”

IRYN: “Okay takecare, see you later.” Na akakata simu chap.

Mzee Mollel alinipigia simu na tukakutana pale CBE ambako alinipick na tukaelekea Makulu, tulisalimiana na pale ndo nikamkumbuka nilishwai kumwona kitambo sana akiwa na mzee. Pia kwenye gari alikua na vijana wa2 na akanitambulisha kama vijana wake.

Mzee Mollel alikua ni Engineer wa serikali kwenye moja ya Wizara hapa nchini.

Tulifika eneo la tukio na nikamwonesha kile kiwanja, na mzee Mollel alishangaa sana kuona namiliki kiwanya mitaa ile ya Oysterbay maana ni ngumu sana alisema.

Walipima na vijana wake na tulitumia kama 1hr kukagua eneo lile na kufanya vipimo vyao na tukaondoka pale. Mzee Mollel alinambia tunakwenda kwake nikapajue nile na lunch kabisa.

Tulifika kwake mapema tu na yeye anakaaa karibu na chuo cha Mipango ndo kajenga kule. Baada ya kufika pale nimsalimia mke wake na alinitambulisha kwa baadhi ya watoto wake ambao walikuwepo.

Tulipata lunch pale ya kibabe na tukakaa palepale dining kuendelea na maongezi ya ujenzi. Walipiga hesabu zao na tukapata gharama za kuanza ujenzi pamoja na ufundi, maana nilitaka wanipe kwanza gharama za kuanza msingi mpaka kupaua na kuweka grill na mageti.

Baada ya kumaliza na kupata figure halisi nilimwambia kesho ambayo jumatatu waanze ujenzi na mimi nikasema nitaacha kiasi cha pesa ili ujenzi uanze.

Sikuwa na wasiwasi kabisa na Mzee Mollel maana mzee wangu alinambia hana shida na anamuamini sana, wametoka mbali. Mzee mollel naye alinambia wale vijana wake watakua wanakwenda kusimamia kama yeye anakua busy hivyo kila kitu kitakwenda sawa kabisa.

Upande mwingine mzee Mollel alikataa kabisa malipo sababu alisema ananichukulia kama kijana wake na Mzee wangu wanasaidiana sana mambo yao. Ila mzee Mollel aliomba niwafikirie wale vijana wake ambao watakua wanakwenda kukagua na kuwasimamia mafundi.

Nilimkabidhi kiasi cha pesa ambacho kingesaidia katika kuanza ujenzi, maana nilibeba kiasi kikubwa cha pesa navyotoka home. Hata yeye hakuamini kama nimejipanga kuanza ujenzi kwa haraka vile na alinipongeza sana.

Muda huo ilikua kama saa 10 jioni tayari na niliaga pale naondoka akasema kesho vifaa vitaanza kushushwa pale, mambo ya vibali nimuachie yeye atatakecare. Nilimshukuru sana na yeye akanipa lift mpaka pale CBE.

Nilirudi Lodge na nilikua nimetulia na laptop yangu nikiset mipango kuhusu ujenzi pia nilikua nawaza namna ya kupata hela ili ujenzi uende haraka.

Baada ya kumaliza mambo yangu nikampigia simu best yangu mmoja ambaye tulisoma naye chuo na tulisoma faculty moja. Maana yeye akija Dar huwa ananitafuta hivyo sikuona sababu ya kutomtafuta.

Nilimpiga simu Aggy ambaye ndo best yangu na nikamwambia niko Dodoma na akanambia soon atakua around. Aggy ni mshikaji wangu sana toka chuo na mpaka sasa, na alibahatika kupata kazi kwenye taasisi ya serikali ambayo makao makuu yake yapo pale Dodoma, pale ni kama Mchumi.

Ndani ya muda mfupi alikuwa around na tukaenda kwake alikopanga na tulipiga story sana baada ya hapo tulikwenda “chako ni chako” kupata dinna.

Lengo langu kubwa ilikua ni kuomba awe ananisaidia kufanya ukaguzi kule site, nilitaka na mimi niwe na mtu wangu. Hivyo nilimwambia kilichonileta Dodoma na yeye hakuwa na shida alikubali na akanipongeza kwa hatua niliyoamua kuchukua.

Nilimwomba Aggy kesho kama anaweza tuweze kwenda pamoja site na akasema hiyo haina shida atatoka ofisini na tutakwenda.

Tuliagana pale na yeye akanidrop pale CBE na muda huo ulikua usiku tayari, wakati naelekea lodge niliyofikia simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikua ni dada yangu Violet.

MIMI: “Nambie dada yangu kipenzi.”

VIOLET: “Safi tu za wewe.”

MIMI: “Safi kabisa, nipe habari.”

VIOLET: “Ulikua na Tyna na leo?”

MIMI: “Yeah, anasemaje?”

VIOLET: “Kanambia ulikuwa unakwenda Dodoma, vipi unamishe gani huko?”

Dada nilikua sijamshirikisha mipango yangu hivyo ilibidi nimwambie maana sikuwa na sababu ya kumficha na yeye kwa upande wake alizifurahia zile habari.

Suala lingine dada yangu aliongea ni kuhusu mimi na Mama Junior hivyo alinishauri na aliniomba niyamalize mapema, mtoto kukaa ukweni bila sababu za maana sio vizuri. Nilimuahidi Dada nikirudi Dar nakwenda kulimaliza hili jambo nayeye alifurahi kusikia hivo.

++++++++++

Jumatatu nilikua nasafari ya kurudi Dar na ndege ya saa7 mchana na siku hiyo asubuhi saa 3 tulionana na Aggy.

Aggy alikuja kunichukua pale lodge na tulikwenda pale site na tulikuta vifaa vishaanza kununuliwa na mafundi walikua wakifanya setting. Niliweza kuwakuta wale vijana wa Mzee wakisimamia muda ule na mimi niliwasalimia tukaendelea na mazungumzo.

Saa 4 mzee alifika na tulisalimina naye na nikamtambulisha Aggy kwake na nikamwambia atakua anapita pita pale site, Mzee hakuwa na shida, bhasi tuliaga pale na mimi nikarudi lodge kujiandaa ile niondoke kurudi Dar.

Nilijiandaa haraka sana na na saa 6 kasoro nilitoka pale na kwenda Airport, Aggy alinipa kampani mpaka Airport. Tuliagana pale na yeye akasema anarudi ofisini kuendelea na majukumu yake ya kiofisi.

Saa 9 mchana nilikua tayari JNIA na ilibidi nifanye kurequest Uber tena kurudi kwangu na tulitumia saa1 kufika home.

Nilifika Home na muda ule plan zangu zilikua nikwenda moja kwa moja kwa Mama Junior. Na muda huu nilikua nikijuuliza kama naweza mkuta au laah, sikutaka mpigia simu nilitaka iwe saprise.

Nikawasiliana na mdogo wake akanambia Mama Junior yupo home, bhasi nikajiandaa vizuri nikatoka kwenda kwao.

Nilifika pale kwao na nikafungua geti, pale kwao palikuwaga kama home tu, baada ya kushuka nilimwona dada akiwa na Junior na nikampokea, wanasema damu ni nzito kuliko maji, Junior baada ya kuniona alinifurahia sana.

“Mama J yuko wapi?”

“Yuko ndani anasoma”

“Kwanini mliondoka bila kutoa taarifa?”

“Dada ndo alisema tuondoke mimi sikuwa na jinsi.”

Ukweli niliona dada hahusiki na haya hivyo ikabidi niingie ndani, nilimkuta seblen mamdogo wao tukasalimiana. Hii siku nyumba yao ilikua na utulivu sana na sio kama nilivyozoea.

Mamdogo alinambia niende tu chumbani maana kile ni chumba chake anakaa na dada wa kazi hivyo hakuna shida. Nikagonga hodi kwa kugonga na akasema “come in”, ofcourse hakujua ni mimi ambaye nagonga mlango.

Nilifungua na aligeuka kuangalia ni nani baada ya kuniona ndo mimi alijifanya hana habari na mimi. Na muda huo nilikua nimemshika Junior na ile simu mkononi ilikua kwenye mfuko.

MIMI: “Nambie mke wangu, nimekumiss san.”

MAMA J: “Umekuja kufanya nini hapa?”

MIMI: “Si nimekuja kukuchukua mke wangu pamoja na mtoto.”

MAMA J: “Alokwambia mimi nataka kurudi ni nani?”

Na muda huu alikua anajifanya yuko busy sana na kusoma.

MIMI: “Niliona umenipigia nikajua umenimiss.”

MAMA J: “Mpaka nikupigie ila wewe huwezi kupiga ukanijulia hali na mwanao?”

MIMI: “I did lakini hukuwa unapokea simu zangu.”

MAMA J: “Baba J mimi naomba uondoke tu, kwanza unanipotezea muda mimi na kazi hapa.”

MIMI: “Mimi nimekuja kukuomba msamaha na tuyajenge, yule mwanamke sio malaya wangu kama unavyodai. Naomba uwe mwelewa wewe si ulikuwa unasoma chats uliona kuna sehemu yoyote nimemtongoza?, yeye ndo ananitaka ila nothing happened.”

Mama Junior alikua kama anajifanya hanielewi na hana habari na mimi bhasi nikaenda kulock
Mlango. Nikamsogelea nikasimama nyuma yake na yeye alikua amekaa kwenye kiti, sababu najua maeneo ambayo ni dhaifu kwake na yakumyegeza bhasi nikamshika maeneo yaleyale.

Mama J alikua anajifanya kama hataki ila nilikua naona ni mtu anayependa ila anafanya kunikazia tu na alikua amevaa kibukta cha adidas kinachoishia mapajani kwa juu, kilinifanya nipate mzuka sana.

Kutokana na yale maneo kuendelea kumpa khashikhashi aliendelea kulegea na mwisho wa siku nikampa mdomo kwa nyuma hata hakugoma akanipa ulimi.

Na muda huu Junior alikua busy sana na kuchezea droo za makabati alikua na miezi 9 ndo anajifunza kusimama na alikuwa akisamia vitu.

Na kadri muda ulivyozidi kwenda nilijua Mama J anataka zaidi nikamtoa kwenye kiti na tukakaa kitandani tukaendelea kubadilishana lita za maji ya baraka. Sikutaka kufanya makosa kabisa maana nilikua hii ndo tiketi yangu ya kumu-win na kuyajenga.

Kilikua ni kitendo kilichotokea haraka sana hata dakika 15 hazikuzidi ila tulikua tushafika sayari ya Jupita na kurudi duniani. Na baada ya kumwaga asali ya moto ndo nilipata akili kwamba niko ukweni.

Muda huo Junior alikua hana habari kabisa na sisi yeye alikua busy na mambo yake.

Na muda huo mimi na mama J ilikua tumemaliza tofauti zetu kwa njia hiyo na nikamkabidhi simu yake ile zawadi niliyopewa na Iryn. Mama J alifurahi sana kumpa ile zawadi na mimi nikachukua simu yake Iphone Xs Max.

Tuliongea pale na nikamwomba arudi home na alikubali akasema weekend atarudi home. Nilimwuliza kuhusu masomo yake na akasema anaendelea vizuri, nikampa na story za Dodoma akafurahi sana kusikia nimeanza ujenzi.

Nilikaa pale mpaka jioni saa 1 na mama mkwe alirudi akanikuta, tukasalimiana na nikaaga.

Baada ya kutoka pale kwa Mama J nilimpigia simu Prisca ili tuonane na akasema yupo kwao niende tu kwao, Mama yake hayupo ameenda kwa sherehe.

Nilifika pale kwao na nilikaribishwa nikaingia ndani, nilimkuta Mary seblen nimamsalimia lakini alikua ni mtu ambaye kama ana chuki na mimi hata Prisca alitambua hilo.

Nikamwambia Prisca mimi sikai sana hivyo twende kibarazani tuongee, lengo langu kwenda kwa Prisca ilikua ni kumchana ukweli kuhusu suala la mahusiano kati yangu na yeye. Baada ya kufika pale kibarazani tulianza mazungumzo;

PRISCA: “Insider nini kinaendelea kati yako na Mary?”

MIMI: “Jana kanipigia sana simu afu sikumpokelea, atakua kachukia hicho.”

PRISCA: “Nilishakuambiaga dada Mary ana tu feelings na wewe anyway, nitaongea naye nijue kama kuna lingine.”

MIMI: “Ooh sawa, but naomba nikwambie jambo moja before its too late.”

PRISCA: “Nini unataka kunambia Insider?.”

MIMI: “Prisca mimi nina Mke na mtoto ujue?, ndomana unaona mara nyingi nakuignore sababu hio hivyo sitaki kuendeleaa kukuficha.”

PRISCA: “Insider what are you talking about?”

MIMI: “Hata hivyo kuna option mbili you can choose, kama tuendelee kuwa na mahusino ila ufate sheria nitakazokupa au tuendelee kuwa washikaji wa kawaida.”

Muda huu Prisca alibalika sana na alikuwa kama mtu ambaye haamini maneno ambayo alikuwa akiyasikia kutoka kwangu.

PRISCA: “And if kama sina choice hapo?”

MIMI: “Ni maamuzi yako mimi sitakuwa na shida, think about that mimi naondoka inabidi nirudi home mapema.”

Nilimwacha Prisca katika situation ambayo hajui ajibu nini na mimi nikapotea eneo lile.

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 
Your mental block beliefs inventory unazo za kutosha. Yaani kumbadilisha mtu anachoamini utamuua. Ni sawa kumbadilisha paroko aka bishop awe shekhe,unadhani Ni kazi rahisi.
Yaani unaposema nchi ya walalahoi hakuna anayelipwa iyo hela ,hivi una akili kweli.hujasikia kuwa Kuna manager sijui CEO wa bank fulani alikuwa akalipwa 52M,
Manager wa voda aliyekataliwa na jpm unajua alikuwa analipwaje,

Sema wewe ndiye mlalahoi usidhani wote wako ivyo. Kiufupi Kuna wenzako hapa hapa bongo iyo milioni yako wanaiona Kama buku unavyoiona kwa taarifa yako.


Yaani unadhani kuwa you're the universal standard unit to set the reference or benchmark kwa wengine
keisangora huwa ni Jamaa flani Nima, kiroho safi
 
Back
Top Bottom