Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Mkuu, uzi wa hadithi yako nilikuwa nnaupuuzia sana kila nilipokuwa nnafungua jf. Lakini siku nilipoamua kufungua na kusoma episode ya kwanza nimevitiwa sana kuendelea kufuatilia.

Nnakupa pongezi sana kwa hadithi hii, kama ni ya kweli umepitia mengi mazuri na mabaya na ndio yanafanya mtu awe na hekima. Lakini kama ni ya kutunga basi una kipaji kikubwa sana.

Mchango wangu.

1.Usiifanye hadithi iwe ndefu sana, watu wanatamani kujua mwisho utakuwaje jaribu kupunguza vitu ambavyo sio vya lazima.

Hata kama hadithi ni nzuri ila kama ni ndefu sana inafikia sehemu watu wanapoteza hamasa kuifuatilia.

2. Episode ya mwisho haijaisha vizuri na wewe unajua hilo bila shaka.

Nina tumaini episode inayofuata itakuwa vizuri zaidi.
 
Story inaanza ndani.ya miaka miwili kazini ametengeneza million 24 .

Halfu alikuwa intern wale wataesa wanaolipwa laki 4 .halfu muda huohuo akafungua biashara ya hardware kama sijakosea.

Hata kama ni upigaji Ila kwa million 24 alitupiga
Kuna Madogo wanafanya kazi za kukusanya Ushuru huko Mipakani na Vile vimashine ukiwaona utawadharau, wanapiga sana hela. Kuna mmoja kwa mwezi alifikisha Zaidi ya milioni 10 kama malipo yake. Kipindi kile mahindi yanavuka sana border kwenda Kenya.

Kwahiyo upigaji wa pesa unategemea na namna gani unajituma katika maisha yako na kazi unayofanya.
 
Mkuu keisangora hi uli maliza kabisa 🤒💪.
 
Stori imepoteza mvuto mwandishi hana jipya .

Anatumia Episode nzima kueleza jinsi anavyokula bata na mama wa2.

Kiukweli insider maliza story huko mbele hakuna cha maana.

Ulijitahidi Sana mwanzo Ila kwa sasa Ahsante kwa mchango.

Kujisifia kumekuwa kwingi kuliko hata uhalisia wa jambo.

FICTION STORY
 
Anatunga na amekosa concentration ndo maana amepunguza matukio amebaki na ushenzi wake wa kujimwambafai.


ACHA KUSIMULIA TU.

INACHOSHA NOW
 
Wanaobisha ni wakolomije wanaokaa misituni.
Ila kwa mtu mwenye akili timamu na unayeishi dar utaona sukari imeongezwa.

Mistake wateja wake wote wako single kuanzia mama wawili,maggy,iryn.

Wote wanamkubali na kumuamjni na wote wanampa hela.

Wote wanamshobokea na marafiki zake.

Jamaa anajua kuwapanga washenzi shenzi wanaofuatilia story za kifala kama hii.

Angesema ya kutunga tungemwamini.

Uko sahihi dada
 
Unaishi wapi mkuu??
Huenda crew unayokuaga nayo hamjawahi kutana na mijitu yenye pesa za mchezo mchezo.

Kuna watu wanapesa jama, huyu jamaa hata kama story katunga au niaje ila watu wa hivo wapo kabisa.

Unadhani hizo 5 star hotel zinakaliwa na kina nani?? Ndo hao mabwenyenye mkuu.
Hawa matajiri wa kwenye wilaya wilaya wanakufuru kwelikweli ndo wawe hao wanaomiliki visima na sheli kama siafu.
 
2 billion dollar kwenye account ni uongo. Unaijua 2bilion dollar
 
EPISODE 19
“A TRUE STORY BY INSIDER”

Saa 4 usiku ndo muda ambao nilimrudisha mama wa2 kwake na alikua kalewa haswa, baada ya hapo na mimi nikirudi kwangu kulala ili asubuhi niwai kuamka na niwai safari yangu.

Jumapili nilikua na safari ya kwenda Dodoma na niliamka asubuhi mapema sana na nikajiandaa kuondoka kuelekea JNIA. Hii siku nilifanya kurequest Uber kwenda Airport na ndo ilikua mara yangu ya kwanza kupanda ndege.

Na muda huo asubuhi dada Tyna alikua amenipigia simu na kunikumbusha niwe on-time kufika pale.

Saa 07:30 nilikua nimeshawasili pale na muda huo Tyna alikua akinisubiri. Sababu alisema anataka tuongee kidogo na mimi. Nilifika pale Terminal 2 na tukaonana na Tyna,

MIMI: “Dada yangu nakuona”

TYNA: “Nambie mdogo wangu za toka ile siku.”

MIMI: “Salama, vipi umekesha leo Airport?”

TYNA: “Niliingia shift ya usiku ndo nimemaliza asubuhi hii.”

MIMI: “Aisee siwezi kuoa mwanamke anayelala nje usiku.”

TYNA: “Na mke wako akiajiliwa huku?”

MIMI: “Si namkataza tu, atachagua moja kati ya mimi au kazi.”

TYNA: “Kwanza hongera kwa kuoa, nilipata taarifa kutoka kwa dada yako Violet (Hili ni Jina halisi la Dada yangu)

MIMI: “Ndo hivyo nilimtia mimba mtoto wa watu ikabidi nijilipue tu.”

TYNA: “Ulifanya jambo jema sana, mwezi huu ujao nitakuja kuwasalimia pamoja na mtoto.”

MIMI: “Uje kweli, vipi kuhusu wewe lini tutakula pilau?”

TYNA: “Insider mimi bado niko sokoni, bidhaa haijapata mteja bado.”

Na muda huu TYNA alikua akicheka…

MIMI: “Usije ukawa unachagua wateja.”

TYNA: “Mdogo wangu sikuhizi wanaume mmekua washenzi sana, ukishampa ndo imetoka hiyo. Waoaji ni wachache sana kwasasa.”

MIMI: “Dada ana watoto wa2 tayari, unatambua hilo.”

TYNA: “Violet anabahati yeye ndo alikua wa kwanza kuolewa kwa wanawake tuliokua pamoja pale mtaani.”

MIMI: “So unaishi wapi kwa sasa?”

TYNA: “Nimepanga tabata segerea.”

MIMI: “Nitakuja kukusalimia siku ila itabidi uanze wewe kuja kwetu.”

TYNA: “Insider nimefurahi tumeonana na tumeongea ni muda sana, muda umefika now unaweza kucheck-in uondoke, uwe na safari njema mdogo wangu.”

Saa 6 mchana nilikua Dodoma tayari na nilifikia lodge moja ipo karibu na CBE. Nilimpa taarifa mzee Mollel kuwa nimefika tayari na kasema atakuja ndani ya nusu saa.

Wakati nimetulia mle lodge simu yangu ilianza kuita kucheki alikua ni Iryn. Nikaipokea simu yake,

IRYN: “Hi Insider”

MIMI: “Za wewe, now Unaendeleaje?”

IRYN: “Niko sawa now, vipi uko wapi? Nataka unipeleke kwa Mama Janeth.”

MIMI: “Sorry niko Dodoma nilipata emergence”

IRYN: “Toka lini?”

MIMI: “Sina hata saa toka niingie hapa.”

IRYN: “Mbona hukunambia kama unaondoka na umepatwa na matatizo?”

MIMI: “Nilipata taarifa jana na mzee wangu nije Dodoma kuna jambo la ku takecare hakuna matatizo.”

IRYN: “Sasa why hukunambia? Insider unaona mambo yako hunishirikishi inamaana bila kupiga simu usingenitafuta kabisa.

MIMI: “Jana nilikua busy na kazi nikasema nitakupigia lakini nilisahau naomba nisamehe Bossy wangu, nitakuletea zabibu kama zawadi.”

IRYN: “Ok no problem na unarudi lini?”

MIMI: “Kesho mchana nitakua huko, siwezi kukaa huku.”

IRYN: “Are you sure au upo kwenye mishe zako.?”

MIMI: “Trust me.”

IRYN: “Okay takecare, see you later.” Na akakata simu chap.

Mzee Mollel alinipigia simu na tukakutana pale CBE ambako alinipick na tukaelekea Makulu, tulisalimiana na pale ndo nikamkumbuka nilishwai kumwona kitambo sana akiwa na mzee. Pia kwenye gari alikua na vijana wa2 na akanitambulisha kama vijana wake.

Mzee Mollel alikua ni Engineer wa serikali kwenye moja ya Wizara hapa nchini.

Tulifika eneo la tukio na nikamwonesha kile kiwanja, na mzee Mollel alishangaa sana kuona namiliki kiwanya mitaa ile ya Oysterbay maana ni ngumu sana alisema.

Walipima na vijana wake na tulitumia kama 1hr kukagua eneo lile na kufanya vipimo vyao na tukaondoka pale. Mzee Mollel alinambia tunakwenda kwake nikapajue nile na lunch kabisa.

Tulifika kwake mapema tu na yeye anakaaa karibu na chuo cha Mipango ndo kajenga kule. Baada ya kufika pale nimsalimia mke wake na alinitambulisha kwa baadhi ya watoto wake ambao walikuwepo.

Tulipata lunch pale ya kibabe na tukakaa palepale dining kuendelea na maongezi ya ujenzi. Walipiga hesabu zao na tukapata gharama za kuanza ujenzi pamoja na ufundi, maana nilitaka wanipe kwanza gharama za kuanza msingi mpaka kupaua na kuweka grill na mageti.

Baada ya kumaliza na kupata figure halisi nilimwambia kesho ambayo jumatatu waanze ujenzi na mimi nikasema nitaacha kiasi cha pesa ili ujenzi uanze.

Sikuwa na wasiwasi kabisa na Mzee Mollel maana mzee wangu alinambia hana shida na anamuamini sana, wametoka mbali. Mzee mollel naye alinambia wale vijana wake watakua wanakwenda kusimamia kama yeye anakua busy hivyo kila kitu kitakwenda sawa kabisa.

Upande mwingine mzee Mollel alikataa kabisa malipo sababu alisema ananichukulia kama kijana wake na Mzee wangu wanasaidiana sana mambo yao. Ila mzee Mollel aliomba niwafikirie wale vijana wake ambao watakua wanakwenda kukagua na kuwasimamia mafundi.

Nilimkabidhi kiasi cha pesa ambacho kingesaidia katika kuanza ujenzi, maana nilibeba kiasi kikubwa cha pesa navyotoka home. Hata yeye hakuamini kama nimejipanga kuanza ujenzi kwa haraka vile na alinipongeza sana.

Muda huo ilikua kama saa 10 jioni tayari na niliaga pale naondoka akasema kesho vifaa vitaanza kushushwa pale, mambo ya vibali nimuachie yeye atatakecare. Nilimshukuru sana na yeye akanipa lift mpaka pale CBE.

Nilirudi Lodge na nilikua nimetulia na laptop yangu nikiset mipango kuhusu ujenzi pia nilikua nawaza namna ya kupata hela ili ujenzi uende haraka.

Baada ya kumaliza mambo yangu nikampigia simu best yangu mmoja ambaye tulisoma naye chuo na tulisoma faculty moja. Maana yeye akija Dar huwa ananitafuta hivyo sikuona sababu ya kutomtafuta.

Nilimpiga simu Aggy ambaye ndo best yangu na nikamwambia niko Dodoma na akanambia soon atakua around. Aggy ni mshikaji wangu sana toka chuo na mpaka sasa, na alibahatika kupata kazi kwenye taasisi ya serikali ambayo makao makuu yake yapo pale Dodoma, pale ni kama Mchumi.

Ndani ya muda mfupi alikuwa around na tukaenda kwake alikopanga na tulipiga story sana baada ya hapo tulikwenda “chako ni chako” kupata dinna.

Lengo langu kubwa ilikua ni kuomba awe ananisaidia kufanya ukaguzi kule site, nilitaka na mimi niwe na mtu wangu. Hivyo nilimwambia kilichonileta Dodoma na yeye hakuwa na shida alikubali na akanipongeza kwa hatua niliyoamua kuchukua.

Nilimwomba Aggy kesho kama anaweza tuweze kwenda pamoja site na akasema hiyo haina shida atatoka ofisini na tutakwenda.

Tuliagana pale na yeye akanidrop pale CBE na muda huo ulikua usiku tayari, wakati naelekea lodge niliyofikia simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikua ni dada yangu Violet.

MIMI: “Nambie dada yangu kipenzi.”

VIOLET: “Safi tu za wewe.”

MIMI: “Safi kabisa, nipe habari.”

VIOLET: “Ulikua na Tyna na leo?”

MIMI: “Yeah, anasemaje?”

VIOLET: “Kanambia ulikuwa unakwenda Dodoma, vipi unamishe gani huko?”

Dada nilikua sijamshirikisha mipango yangu hivyo ilibidi nimwambie maana sikuwa na sababu ya kumficha na yeye kwa upande wake alizifurahia zile habari.

Suala lingine dada yangu aliongea ni kuhusu mimi na Mama Junior hivyo alinishauri na aliniomba niyamalize mapema, mtoto kukaa ukweni bila sababu za maana sio vizuri. Nilimuahidi Dada nikirudi Dar nakwenda kulimaliza hili jambo nayeye alifurahi kusikia hivo.

++++++++++

Jumatatu nilikua nasafari ya kurudi Dar na ndege ya saa7 mchana na siku hiyo asubuhi saa 3 tulionana na Aggy.

Aggy alikuja kunichukua pale lodge na tulikwenda pale site na tulikuta vifaa vishaanza kununuliwa na mafundi walikua wakifanya setting. Niliweza kuwakuta wale vijana wa Mzee wakisimamia muda ule na mimi niliwasalimia tukaendelea na mazungumzo.

Saa 4 mzee alifika na tulisalimina naye na nikamtambulisha Aggy kwake na nikamwambia atakua anapita pita pale site, Mzee hakuwa na shida, bhasi tuliaga pale na mimi nikarudi lodge kujiandaa ile niondoke kurudi Dar.

Nilijiandaa haraka sana na na saa 6 kasoro nilitoka pale na kwenda Airport, Aggy alinipa kampani mpaka Airport. Tuliagana pale na yeye akasema anarudi ofisini kuendelea na majukumu yake ya kiofisi.

Saa 9 mchana nilikua tayari JNIA na ilibidi nifanye kurequest Uber tena kurudi kwangu na tulitumia saa1 kufika home.

Nilifika Home na muda ule plan zangu zilikua nikwenda moja kwa moja kwa Mama Junior. Na muda huu nilikua nikijuuliza kama naweza mkuta au laah, sikutaka mpigia simu nilitaka iwe saprise.

Nikawasiliana na mdogo wake akanambia Mama Junior yupo home, bhasi nikajiandaa vizuri nikatoka kwenda kwao.

Nilifika pale kwao na nikafungua geti, pale kwao palikuwaga kama home tu, baada ya kushuka nilimwona dada akiwa na Junior na nikampokea, wanasema damu ni nzito kuliko maji, Junior baada ya kuniona alinifurahia sana.

“Mama J yuko wapi?”

“Yuko ndani anasoma”

“Kwanini mliondoka bila kutoa taarifa?”

“Dada ndo alisema tuondoke mimi sikuwa na jinsi.”

Ukweli niliona dada hahusiki na haya hivyo ikabidi niingie ndani, nilimkuta seblen mamdogo wao tukasalimiana. Hii siku nyumba yao ilikua na utulivu sana na sio kama nilivyozoea.

Mamdogo alinambia niende tu chumbani maana kile ni chumba chake anakaa na dada wa kazi hivyo hakuna shida. Nikagonga hodi kwa kugonga na akasema “come in”, ofcourse hakujua ni mimi ambaye nagonga mlango.

Nilifungua na aligeuka kuangalia ni nani baada ya kuniona ndo mimi alijifanya hana habari na mimi. Na muda huo nilikua nimemshika Junior na ile simu mkononi ilikua kwenye mfuko.

MIMI: “Nambie mke wangu, nimekumiss san.”

MAMA J: “Umekuja kufanya nini hapa?”

MIMI: “Si nimekuja kukuchukua mke wangu pamoja na mtoto.”

MAMA J: “Alokwambia mimi nataka kurudi ni nani?”

Na muda huu alikua anajifanya yuko busy sana na kusoma.

MIMI: “Niliona umenipigia nikajua umenimiss.”

MAMA J: “Mpaka nikupigie ila wewe huwezi kupiga ukanijulia hali na mwanao?”

MIMI: “I did lakini hukuwa unapokea simu zangu.”

MAMA J: “Baba J mimi naomba uondoke tu, kwanza unanipotezea muda mimi na kazi hapa.”

MIMI: “Mimi nimekuja kukuomba msamaha na tuyajenge, yule mwanamke sio malaya wangu kama unavyodai. Naomba uwe mwelewa wewe si ulikuwa unasoma chats uliona kuna sehemu yoyote nimemtongoza?, yeye ndo ananitaka ila nothing happened.”

Mama Junior alikua kama anajifanya hanielewi na hana habari na mimi bhasi nikaenda kulock
Mlango. Nikamsogelea nikasimama nyuma yake na yeye alikua amekaa kwenye kiti, sababu najua maeneo ambayo ni dhaifu kwake na yakumyegeza bhasi nikamshika maeneo yaleyale.

Mama J alikua anajifanya kama hataki ila nilikua naona ni mtu anayependa ila anafanya kunikazia tu na alikua amevaa kibukta cha adidas kinachoishia mapajani kwa juu, kilinifanya nipate mzuka sana.

Kutokana na yale maneo kuendelea kumpa khashikhashi aliendelea kulegea na mwisho wa siku nikampa mdomo kwa nyuma hata hakugoma akanipa ulimi.

Na muda huu Junior alikua busy sana na kuchezea droo za makabati alikua na miezi 9 ndo anajifunza kusimama na alikuwa akisamia vitu.

Na kadri muda ulivyozidi kwenda nilijua Mama J anataka zaidi nikamtoa kwenye kiti na tukakaa kitandani tukaendelea kubadilishana lita za maji ya baraka. Sikutaka kufanya makosa kabisa maana nilikua hii ndo tiketi yangu ya kumu-win na kuyajenga.

Kilikua ni kitendo kilichotokea haraka sana hata dakika 15 hazikuzidi ila tulikua tushafika sayari ya Jupita na kurudi duniani. Na baada ya kumwaga asali ya moto ndo nilipata akili kwamba niko ukweni.

Muda huo Junior alikua hana habari kabisa na sisi yeye alikua busy na mambo yake.

Na muda huo mimi na mama J ilikua tumemaliza tofauti zetu kwa njia hiyo na nikamkabidhi simu yake ile zawadi niliyopewa na Iryn. Mama J alifurahi sana kumpa ile zawadi na mimi nikachukua simu yake Iphone Xs Max.

Tuliongea pale na nikamwomba arudi home na alikubali akasema weekend atarudi home. Nilimwuliza kuhusu masomo yake na akasema anaendelea vizuri, nikampa na story za Dodoma akafurahi sana kusikia nimeanza ujenzi.

Nilikaa pale mpaka jioni saa 1 na mama mkwe alirudi akanikuta, tukasalimiana na nikaaga.

Baada ya kutoka pale kwa Mama J nilimpigia simu Prisca ili tuonane na akasema yupo kwao niende tu kwao, Mama yake hayupo ameenda kwa sherehe.

Nilifika pale kwao na nilikaribishwa nikaingia ndani, nilimkuta Mary seblen nimamsalimia lakini alikua ni mtu ambaye kama ana chuki na mimi hata Prisca alitambua hilo.

Nikamwambia Prisca mimi sikai sana hivyo twende kibarazani tuongee, lengo langu kwenda kwa Prisca ilikua ni kumchana ukweli kuhusu suala la mahusiano kati yangu na yeye. Baada ya kufika pale kibarazani tulianza mazungumzo;

PRISCA: “Insider nini kinaendelea kati yako na Mary?”

MIMI: “Jana kanipigia sana simu afu sikumpokelea, atakua kachukia hicho.”

PRISCA: “Nilishakuambiaga dada Mary ana tu feelings na wewe anyway, nitaongea naye nijue kama kuna lingine.”

MIMI: “Ooh sawa, but naomba nikwambie jambo moja before its too late.”

PRISCA: “Nini unataka kunambia Insider?.”

MIMI: “Prisca mimi nina Mke na mtoto ujue?, ndomana unaona mara nyingi nakuignore sababu hio hivyo sitaki kuendeleaa kukuficha.”

PRISCA: “Insider what are you talking about?”

MIMI: “Hata hivyo kuna option mbili you can choose, kama tuendelee kuwa na mahusino ila ufate sheria nitakazokupa au tuendelee kuwa washikaji wa kawaida.”

Muda huu Prisca alibalika sana na alikuwa kama mtu ambaye haamini maneno ambayo alikuwa akiyasikia kutoka kwangu.

PRISCA: “And if kama sina choice hapo?”

MIMI: “Ni maamuzi yako mimi sitakuwa na shida, think about that mimi naondoka inabidi nirudi home mapema.”

Nilimwacha Prisca katika situation ambayo hajui ajibu nini na mimi nikapotea eneo lile.

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 
keisangora huwa ni Jamaa flani Nima, kiroho safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…