Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Huyo Jamaa Ni mpinzani lakini it's good kama hujatembea, huna exposure utaona hivi vitu kama haviwezekani hapa hapa bongo kuna kampuni zinawalipa watu mpaka 20 M kwa mwezi sembuse international organization

hizo za kutoa hela bila kupata kitu wanaume watanzania tu wapo wanaofanya, once nilimshuhudia jamaa ana mwachia mwanamke business card yake halafu anampa 1 M anamwambia aweke vocha amcheki
Kuna mzee aliachana na mkewe restaurants.

Lilikuwa tukio eti X wake aliomba waongee robo saa pale hotel kwaa million 3. Mume alifikiria kidogo, aliinamisha kichwa chini. Alivyoangalia mkewe na akamuuliza wewe unasemaje, mke akasema anaenda kuongea nae hizo dkk 15. Mume akanuongezea iwe nusu saa. Lkn jamaa aache kibunda kabisa. X bf wa mmama akaingia kwenye gari akatoa vibunda vitano badala ya vitatu. Inamaana naye akaongeza dau la kuongea na mke wa mzee yule.

Kwa kuwa kuilikiwa na upande was bar yeye akahamia bar akaongea na meneja jambo.
 
INSIDER MAN mimi ninacho shangaa ni maisha yangu ya kimaskini sana naona mtu anatoa necklace na watch ya milioni 30 huku akitoa simu ya iphone 13 pro bila shida yoyote......basi wengine tunasindikiza tu maisha mkuu ila wewe ulikula vizuri sana hongera......ujue pia ulivokuwa pale kwa uncle uliteseka sana, vipi yule mke wa uncle anaendeleaje???...

Mkuu nakupa Task, fatilia international Organization mishahara yao ikoje ndo utaelewa kuna watu wanalipwa mishahara mikubwa sana. Mkuu hapa bongo kuna watu wa hela chafu sana, kuna watu wanazitumia hela na kupitia Uber nililithibitisha hili.

Sitaki kufungua CODE hapa subiri huko mbele utaelewa.

Kuhusu Aunt mbona nilileta story kama additional ya kilichoendelea mambo mengine nitaandika story ikiisha.
 
Wewe umejuaje mimi ni 1998-2003 kiufupi pengine mimi nipo aged kwako....
Namna unavyo argue vitu umu ndani mtu anaweza determine umri ulio nao maana kwa mtu ambae amesha kua exposed na maisha hivi vitu hata hawezi shangaa ila nyie vijana wa kisasa ndo mnaona ni vitu vya ajabu wakati bongo hii kuna watu wana spend mpaka mishahara ya mabosi wenu ofisini kwa usiku mmoja
refer attachment
 

Attachments

  • JamiiForums-190484886.jpeg
    JamiiForums-190484886.jpeg
    36.5 KB · Views: 69
Mkuu nakupa Task, fatilia international Organization mishahara yao ikoje ndo utaelewa kuna watu wanalipwa mishahara mikubwa sana. Mkuu hapa bongo kuna watu wa hela chafu sana, kuna watu wanazitumia hela na kupitia Uber nililithibitisha hili.

Sitaki kufungua CODE hapa subiri huko mbele utaelewa.

Kuhusu Aunt mbona nilileta story kama additional ya kilichoendelea mambo mengine nitaandika story ikiisha.
aanze tu na ubalozi wa Us wanapo tangaza nafasi za kazi hua wana onesha na annual salary ya kazi ambayo hata mkuu wa idara kibongo bongo hafikishi kwa mwaka ...
apo mtu ana lamba 49M / annual ukifika managerial position uko si ndo kijana utaanza temea watu mate barabarani 😂😂
 

Attachments

  • Screenshot_20230729-091218_Chrome.jpg
    Screenshot_20230729-091218_Chrome.jpg
    169 KB · Views: 70
Nimesoma story nyingi Sana.

Kiukweli mwanzo ilikuwa ni stori ya ukweli Ila baada ya kuona Ina mashabiki wengi akaanza kuongeza chumvi.

Yaani haina uhalisia wa maisha ya kawaida .

Kupewa million kwake ni kitu cha kawaida.

Wateja wake wote wazuri hajawahi kupakia demu mbovu.

Yaani yeye kupewa iPhone 13 kawaida ,Mara kapewa kwenye bahasha laki 3 Mara .


Tips kwenye Hii stori zimekuwa nyingi Sana kuliko hata kazi.


Kiukweli hii fiction acha tuone mwisho unakuaje.
Uber unakuwa bilionea Chap
 
Kuna mzee aliachana na mkewe restaurants.

Lilikuwa tukio eti X wake aliomba waongee robo saa pale hotel kwaa million 3. Mume alifikiria kidogo, aliinamisha kichwa chini. Alivyoangalia mkewe na akamuuliza wewe unasemaje, mke akasema anaenda kuongea nae hizo dkk 15. Mume akanuongezea iwe nusu saa. Lkn jamaa aache kibunda kabisa. X bf wa mmama akaingia kwenye gari akatoa vibunda vitano badala ya vitatu. Inamaana naye akaongeza dau la kuongea na mke wa mzee yule.

Kwa kuwa kuilikiwa na upande was bar yeye akahamia bar akaongea na meneja jambo.
Enhee
 
Yaani watu kama hawa hatukatai kusimulia story.

Ila mazingira ya madereva wa bolt au.uber hayako kama yeye anavyotaka kutuaminisha.

Uber yake amepanda waziri halfu akaanza kupiga nae story Sana na alisema sio mpenzi wakuongea na wateja.

Uber yake haijawahi kupata hasara siku zote mafanikio tu.

Madereva maisha yanavyowapiga na hela ya mafuta Ila yeye anaweza kwenda kiwanja akatumbua hata laki moja ikawa kawaida.

Stori now imefika kiasi kwamba hapati hata muda wa kazi Anaweza kushinda kwa iryn au prisca akasahau kupiga kazi...sasa sijui hela ya mafuta alikuwa Anapata wapi ?
Anapewa na uwoya
 
Halafu pia sidhan kama anasimulia Kila tukio, nafikiri kachagua wahusika wachache.

Sijataka kusema kila tukio maana ningeandika zaidi ya Episode 500, kama hawa wazungu nimefanya nao sana kazi na kilichokuwa kinanibeba ni kujua Ngeli, na wazungu walikua wanashngaa kuona najua ngeli, walikua wanasema Uber wa Tanzania hawajui English, walikua wanafurahi sana ndomana nilikua nafanya nao sana kazi.

Hii story nimeamua kudonoa noa tu na ni 20% tu ya matukio nilokutana nayo nitayaandika hapa napo kwa uchache sana. TANZANIA tungekua tunajali kazi za uandishi bhasi ningeandika kitabu kabisa.

Siwezi kupoteza muda wangu kuandika kitu ambacho hakipo never, mimi ni Economist ninajali muda sana na ukitegemea nina majukum kibao ya kufanya.

Nikimaliza hii story kuna CODE nyingi nitazifungua na zitaweza kukuwasaidia jinsi ya kukutana na hawa matajiri ila pia vitu vingine ni bahati na kila mtu Mungu kampa sehemu ya kupata riziki yake.

Na kama mtu umeuliza swali ukaona sijakujibu, jua majibu utayapata mbele kupitia Episodes, kuna mtu aliuliza nilijuaje kama gari ya mama Janeth ni 0-km?. Wakati tumeingia kwenye gari tuondoke Iryn alimwambia mama Janeth gari yake nzuri san ndo mama Janeth alimwambia ina mwezi toka aagize na amenunua Brand new kabisa. Ndo hapo nilijua ile gari ni mpya, kwanza hata ungeiona kwa macho jinsi ilivyokuaa usingeuliza.

Pia hii Organization hawalipi kodi hata akiagiza gari atalipia zile gharama za bandarini bhasi ila kodi halipi kabisa, na mama Janeth gari yake ilikua na namba za usajili za Organization.

Nashangaa pia kwanini hamjauliza kama Mama Iryn alimilikia gari au laah, hili nitaleta kama ADDITIONAL,

Leo tutaendelea na story yetu.
 
Namna unavyo argue vitu umu ndani mtu anaweza determine umri ulio nao maana kwa mtu ambae amesha kua exposed na maisha hivi vitu hata hawezi shangaa ila nyie vijana wa kisasa ndo mnaona ni vitu vya ajabu wakati bongo hii kuna watu wana spend mpaka mishahara ya mabosi wenu ofisini kwa usiku mmoja
refer attachment

Sallam SK akiingia element anamaliza zaidi ya 20million kwa usiku mmoja, kuna jamaa alitrend sana pale Kidimbwi alitumia kama 54million kwa usiku mmoja, kuna watu wanahela hapa bongo ni vile hatuna connection nao tu.
 
Mkuu unajua kuna watu wanalipwa zaidi ya $300,000/= kwa mwaka na hizi international Organization?? Kwa mtu ambaye ubongo wake uko vizuri bila shaka alishajua Mama yake na Iryn alikua anafanyia kazi Organization gani.

Unashangaa Muajemi kuhonga hizo necklace za almost 30m wakati kuna wabongo wanahonga hadi nyumba? na magari ya kifahari. Unajua wewe unaona ni kama haiwezekani sababu huna hela ila kwa wenye pesa ni vitu vya kawaida sana. Muajemi account zake zilikua zinasoma dollar $2Billions na mapoint kazaa huko, ashindwe kuhonga 30m?, wakati Harmonize anahonga hadi Range 2 [emoji23][emoji23]

Kwa mara ya kwanza nakutana na Muajemi alinipa 1million hio 3m umeitoa wapi mkuu?

Nilijifunza kitu kimoja kwenye hii Dunia, hakuna Mwanaume asiyehonga ila tumetofautina level za kuhonga tu. Kama unaweza kumuhonga demu savanna 5 kuna mtu anahonga gari au nyumba. Ukiwa huna hela unaweza ona haya mambo hayawezekani ila ukipata hela utaona ya kawaida sana.

Iryn alikua mwanamke mzuri sana aisee, tuseme Alibarikiwa tu. Endelea kufuatilia story kuna mambo mengi sana yaliendelea huko mbele.
Usiwe unajibu kila comment mkuu, wengi wa wanaojitia ujuaji NI wageni humu jf na wengi wao wanaishi huko Namtumbo na wengine ni walimu wa shule za Msingi huko Tandahimba

Mtu anayelipwa Mshahara Laki 3 si rahisi kuamin kuwa hapa Tanzania kuna binadam wanaolipwa zaidi ya Mil 50 Kwa mwezi.
 
Hao ndio wabongo. Kila kitu wanaona chai.

Kuna siku nimekaa sehemu naangalia mpira kuna jamaa alibet kwa 2M. Nikawa nashangaa kwa nini mtu urisk 2M kwenye kamali? Daktari mmoja mtu mzima arround 50 yrs of age alikuwa na familia yake pembeni anapata chakula aliniambia huna pesa ndio maana unasema hivyo. Akasema yeye huwa anaweka 10M na kuna wakati inapotea. Mwisho wa siku nilikubaliana na maneno.


Haya mambo yanaendana na levels . Na ukitaka kujipima uwezo wako wa kuhonga angalia aset unazomiliki. Kuna watu wana gari za milioni 100-800 hawaoni shida kuhonga 20m-50m. Mtu ana flat screen ya 25M ndani kuhonga 20M mtu haoni shida. Na kama unamiliki IST huwezi honga 2M mwisho wako utakuwa 100K. Mtu unamiliki flat screen TV singsung au Star X ya 350,000 automatically huwezi honga 500K utakuwa mwehu.

Hivi ile gari Diamond alimhonga Tanasha inaghalimu kiasi gani? Mbona mambo ya kawaida yapo tu.

Pia kuna mzee namfahamu ana magali ila yeye hapendi kuwa na gali ya kutembelea na hajui kuendesha mpaka leo amestaafu. Kuna dogo anaingiza pesa ndefu kwa kupitia professional yake huwezi amini kama hizo pesa anazipata hapa Tz.

Haya ni mambo ya kawaida kwenye maisha hatufanani songa mbele na story yako
Kwenye hao wahuni wa kubet nimetoa macho balaa
 
aanze tu na ubalozi wa Us wanapo tangaza nafasi za kazi hua wana onesha na annual salary ya kazi ambayo hata mkuu wa idara kibongo bongo hafikishi kwa mwaka ...
apo mtu ana lamba 49M / annual ukifika managerial position uko si ndo kijana utaanza temea watu mate barabarani [emoji23][emoji23]

Na huyu ni mtu wa kawaida sana mostly wanakuaaga wabongo, kuna watu hapo wanakunja zaodi ya 50m kwa mwezi hasa hawa wakubwa kama macoordinator, nknk
 
Back
Top Bottom