Kwanza binafsi nikupongeze kwa moyo mkunjufu kabisa, pamoja na hayo umejitahidi sana hata kufikia hapa ulipo amua kuishia (niliona hili mapema sana na nikaanza kuhisi kama hii simulizi haitokua na mwisho mzuri kutokana na ujuaji wa wengi hapa jf).
Nakupongeza sana na ingekua mimi ndio wewe kwa maneno ya wapuuzi humu ningesha acha kuandika muda mrefu sana.
Lakini pamoja na kuburudika, nimejifunza mambo mengi kupitia simulizi hii ingawa nilitamani iendelee but sina namna nyingine ya kubadilisha maamuzi yako.
Jf ilikua nzuri sana miaka ya nyuma kidogo kabla vijana wengi maJobless hawajaanza kumiliki simu, ambazo wamekua wakizitumia vibaya kutokana na stress za ukosefu wa ajira, basi wanahamishia makasiriko na chuki zao kwa watu wengine ambao wamefanikiwa.
Vijana wa skuizi wamekua na maneno mengi, uvumilivu hawana na ujuaji mwingi usio maana ambao hupelekea makasiriko na wivu wa kijinga kwa watu wengine.
Ukitaka kujua jf imebadilika, chunguza utakuja kugundua memba wengi wameacha kuandika nyuzi na hakuna tena nondo za maana kama zamani wakati watu waliheshimiana sana hapa ndani.
Wengi tumebakia kua wasomaji tu, tumeacha tena kuweka mawazo ya maana na fikra pevu zaidi ya kua wasomaji na wachangiaji tu.
Nakuona kabisa moyo wako ulivyo vunjika, na kutokana na maneno ya wengi mabaya na matusi juu yako bila kusita naamini unaenda kutoweka ama kubadili ID ama kuanzisha ID nyingine, then unabadilika na kua mpenzi mtazamaji hapa jf.