Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Toka ijumaa niko na mteja wangu from US na tulikutana kupitia Uber. Tumetembea sana toka ijumaa na sasa navyoandika tuko Barra Beach Kunduchi, tunamaliza siku huku.

Leo tunamalizia thread yetu saa1 kma kawaida. Nobody can stop Insider, na mkiendelea nikera nitatuma picha ya Iryn.

Lakini wew jamaa si unakumbuka ulituambia ulishaacha kazi ya uber sahivi unafanya mbishe zingine kabisa, iweje tena bado unabeba abiria wa uber..?
 
Uzi umejaa comment za watu wenye mawazo hasi tu.
Mungu hatunusuru yani ety lijianaume linakomaa kumuonea wivu mwanaume mwenzie kisa tu ni msafi, anaosha gari yake vzuri, anapata pesa nzuri.
Baraka zinaanzia kwa wazazi zinafuata kwa watoto wetu na watu tunaowapenda.
Sa ww ndugu yangu ulishawatolesha mimba kina Mwajuma, umkumbuki mama ako hata kwenye maombi unategemea Mungu akubariki kwa kipi.
Wanaume kueni na tabia za kiume sio aaaeeeiiiioouuuu, Alafu ukiitwa wew ni upinde uchukie kitimoto wewe[emoji2955][emoji2955][emoji2955][emoji2955]
[emoji23][emoji23][emoji23] team negatives (hate) wakiendelea baada ya hii comment basi watakuwa beyond repair

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EPISODE 21

“Insider……. Nimekubali option ya kwanza kwa zile mbili ulizonipa.”

ENDELEA……..


Na muda huu nilitumia kusogea pale kitandani na kumsogelea karibu maana alikua amekaa kitandani.

“Prisca kwahiyo umekubali kuwa mchepuko?”

Prisca alijibu kwa kutingisha kichwa kuonesha yuko tayari kufanywa kuwa mchepuko wa Insider.

“Kwanini unataka nikufanye mchepuko? Nafikiri option 2 ingekua nzuri zaidi, tuwe washikaji tu.”

“Ulinipa choice sasa nimechagua option ya 1. Nimeridhika hivyo kwa maamuzi yangu.”

“Okay haina shida kama umeamua hivyo ila…..” Prisca alinikatisha wakati nikiendelea kuongea.

“Insider, nioneshe picha za mke mkubwa bhasi nimjue hata kwa picha na mtoto wangu.”

Nilichukua simu ambayo ilikua mezani na nikaanza kumwonesha picha za Mama Junior, pamoja na zile za Junior.

“Insider umefanana sana na mwanao copyright.”

“Risasi zangu mimi ni genuine grade A”

“Hivi na mimi nikipata mimba si tutapata mtoto mzuri sana, tena atakuwa wa kike.”

Yaani tuseme Prisca alikua tayari karidhika kuwa mchepuko kiukweli nilishangaa sana, na bado akaanza kuleta story za kushika mimba, nilimwona mwanamke wa ajabu sana.

“Upate ujauzito na mme wa mtu, are you serious?”

“Insider najikuta natamani kupata mtoto, Junior ni mzuri sana. Najikuta natamani na mimi nipate mtoto.”

“Embu nenda kaoge tuondoke maana ulisema unataka kurudi mapema home au tulale hapahapa?”

“Natamani ila Mzee Mapembe yupo leo, acha nikaoge tuondoke.”

Ile anashuka kitandani nika muwasha kibao cha kalioo “Paaah”

Nilijiona Alpha kwakweli nikasema sasa huyu nitampa sheria zangu ili asije kuleta sintofahamu huko mbeleni, lazima nimcontol kama remote, maana nikifanya makosa tu itakula kwangu.

Na muda huu niliwaza asajili namba mpya ila kwa jina lingine, na pia nitampa ratiba za kuwasiliana naye pamoja na kuchat na mimi.

Na wakati huo alikuwa katoka kuoga kajifunga taulo kuanzia usawa wa matiti kushuka chini, na mimi nilivyomwona tena akiwa vile nikaanza kusisimuka. Na palepale nikamsogolea nikampiga kingine cha kuondokea nyumbani.

Nilimrudisha kwao saa 6 usiku na mimi nikaondoka kurudi kulala.

**********

Asubuhi Muajemi alinipigia simu na akaniomba niende kwake saa4 asubuhi kuna sehemu twende wote, na mimi niliikubali ile offa sikutaka kumkatalia Tajiri.

Saa4 ilipowadia nilikwenda kwa Muajemi na yeye alikua anakaa msasani unaingilia kushoto kabla hujafika Tanesco Mikocheni. Na alikuwa hakai mbali sana na maeneo yale.

Nilifanikiwa kufika pale anapoishi maana alikuwa kanitumia location kupitia Telegram, Muajemi alikua anatumia sana huu mtandao sijui kwanini.

Ilikua ni nyumba ya ghorofa 2 na ilikua nzuri sana na alikua anakaa na mke wake (Mke mdogo) na alikuwa amezaa naye watoto wawili (2).

Mlinzi alinifungulia geti na nikapark gari langu, alitoka dada wa kazi kunikaribisha, na ndani ya dakika chache Muajemi alikua ametoka na tulikaa garden.

MUAJEMI: “Bro! Hapa ndo naishi, jiskie upo nyumbani.”

MIMI: “Ahsante sana”

MUAJEMI: “Dada tuletee chai tunywee hapahapa na Insider.” Nilishangaa kuona dada anajua kuongea kiingereza.

MIMI: “Bro! shemeji yuko wapi?”

MUAJEMI: “Yuko mishemishe anachacharika”

MIMI: “Na watoto?”

MUAJEMI: “Watoto wako shule”

Tulikaa pale na Muajemi tukipiga story mbalimbali na moja kubwa alilisema ana mpango wa kufungua Filling stations hapa Tanzania, ila bado anakutana na upinzani mkubwa sana hasa kutoka kwa wenye mamlaka.

Saa 5 ndo muda tuliotoka pale na tulitumia gari yake Range sport nyeusi. Mimi nilikua sijui tunakwenda wapi lakini tulikwenda mpaka Kigamboni “South Beach hotel”.

Aliniacha na alikwenda kuonana na watu wake na alitumia masaa 3 wakatoka. Baada ya hapo tulikwenda Kurasini kwenye ofisi za Puma, na tukaondoka pale tukarudi Posta.

Tulikwenda kwenye duka moja kubwa la simu ambalo ni la mke wake alinambia hivyo, tukaenda mtaa wa India kwenye maduka ya Jewerly na tukaingia moja ya duka kubwa pale, alinambia nalo ni la mke wake.

“Insider ukitaka pete ya uchumba, pete za harusi, necklaces kila kitu kipo hapa”

“Bro! hizi bei mimi siwezi kwakweli.”

“Wewe utapewa discount usijali.”

Hapo ndo nikajua kumbe zile zawadi alizompa kwa Iryn alizichukua madukani.

Tulitoka hapo tukaenda pale Holliday inn tukapata chakula japo ilikua jion tayari. Na wakati tuko pale tulikuwa tukizungumza mambo mengi sana.

MIMI: “Tanzania una muda gani toka umeanza kuja?”

MUAJEMI: “Bro! Tanzania nimeanza kuja since 2008, kampuni yetu inafanya kazi karibu nchi zote za Africa, tunauza hizo pumps za mashine za sheli, tunauza lubricants za aina zote. Kwa upande wa mafuta kampuni yetu ina deal kama middle man, kwa ufupi tunaingia mikataba na serikali na makampuni mbalimbali hasa kwa Africa.”

MIMI: “Na kuhusu lubricants?”

MUAJEMI: “Bro! sisi ni exporter ila kila nchi tuna Madalali wetu tunaofanya nao kazi, ndo biashara zinavyokwenda hapa duniani, middle man huwezi wakimbia. Mfano tuna export contena 20 za lubricants kuja Tanzania kwa Agent yetu (middle-man) yeye anasupply kwa agents zake.”

Muajemi aliniambia siri nyingi sana hasa kwenye mafuta alisema watu wanapiga sana hela hasa hawa viongozi wa serikali, sitaki kufungua code kabisa. Muajemi alisema viongozi wa Africa wengi ni ma middle man wanakula sana hela huko, invoice zinachezewa balaa, ila mnaoumia ni nyinyi watumiaji wa mwisho.

MIMI: “Vipi mnawasiliana na Iryn?”

MUAJEMI: “Bro hata jana nimempigia simu, nikamwambia mzigo wake umefika tayari, aliniambia nimtumie account yangu anitumie pesa. Nimeshangaa sana na nimeona dharau sana kwangu.”

MIMI: “Hahahaha wewe ulifanyaje?”

MUAJEMI: “Nilimwambia nimempa offa tu, alinambia pia hakuna cha bure hapa duniani”

MIMI: “Unajua nini, we fanya kumwomba mtoke out, uendelee kumsogeza karibu.”

MUAJEMI: “Badae nitaongea naye, ukisha mpelekea mzigo wake.”

Tulitumia kama nusu saa pale na tulielekea Upanga na kuna mtu tulikutana naye ambaye ni Muajemi alikuwa, akatutolea ile mizigo kwenye Box, na zilikua box 7.

Kijana alipanga kwenye buti vizuri na tukaondoka kurudi Msasani, na muda huo ilikua giza limeanza kuingia.

Tuliwasili pale kwake na akanambia jumapili anakwenda Saudi Arabia hivyo lazima aonane na Iryn haraka iwezekanavyo. Mlinzi alikuja akatoa ile mizigo kwenye gari na akaipanga kwnye gari yangu.

Nilimuaga Muajemi pale na alitoa hela mfukoni akanikabidhi mkononi, alizitoa bila kuhesabu. Nilimshukuru pale na nilivyofika kwenye gari na kuhesabu zilikua ni 420,000/=.

Niliwasiliana na Iryn muda ule akasema nitamkuta kwake, nilifika pale nikafungua geti nikaingiza gari ndani. Na muda huo jirani alikua pale nje amekaa kibarazani.

MIMI: “Jirani nakuona umepumzika huna baya.”

JIRAN: “Jirani nimechoka tu.”

MIMI: “Huonekani siku hizi, ulikuwa umesafiri nini?”

JIRANI: “Mimi au wewe? Maana mimi nipo wewe ndo umetutenga bhana.”

MIMI: “Ngoja nikasalimie ndani, badae bhasi.”

JIRANI: “Wahi baba, atakua amekumiss.”

Niliishia kucheka tu nikasema lait Jirani angelijua hata asingesema hivi.

Niliingia ndani nikamkuta Iryn kalala kizembe pale seblen, maana alikua kavaa vile vibukta vifupi sasa mimi nikawa namwangalia pale kwa macho ya kifisi.

IRYN: “Insider vipi mbona sikuelewi?”

MIMI: “Unalalaje kizembe hivo.”

IRYN: “Sasa ulitaka nilalaje?”

MIMI: “Na mizigo yako kutoka kwa Muajemi ipo kwenye gari.”

IRYN: “Wow jana alinambia imefika, ila hataki nimtumie hela yake.”

MIMI: “Muajemi amekupa offa wewe unaleta habari za malipo”

IRYN: “There is no free meal in this world”

MIMI: “What do you mean?”

IRYN: “Twende tukatoe kwenye gari.”

Tulitoka nje na yeye alikuwa na kibukta chake vilevile tukasaidiana kutoa ile mizigo na tukaweka pale nje kibarazani. Na muda huo Jiran alikuwa akituangalia sana.

MIMI: “Hivi hapa kibarazani hawawezi kuiba?”

IRYN: “I don’t think so.”

Bhasi baada ya kumaliza kuweka zile box pale ambazo zilikua no vifaa vya saloon, kutokana na Iryn alisema zile mashine ni advanced kwenye upande wa saloon pia ni ghali. Na alisema zile mashine zimecost $24,000 mpaka kodi pale bandarini na zitakwenda Masaki.

Na wakati huo muda ulikuwa umekwenda sana, ilikua usiku tayari.

“Insider kesho uje mapema twende Posta nikanunue nguo maana nina hitajika kwenda kwenye ofisi ya mama.”

“Unakwenda muda gani?”

“Saa 7 mchana.”

Bhasi na mimi sikukaa pale kabisa nikaaga nikaondoka kurudi home maana nilitaka kurudi mapema nikaongee na Mzee Mollel nijue hata Ujenzi unakwendaje kule Dodoma.

*********

Ratiba zangu za asubuhi zilikuwa vilevile lazima nikawachukue wateja zangu lakini hii week ilikua tofauti kidogo toka nitoke Dodoma. Mtoto wa Mama wa2 naye alikuwa kaanza likizo ya Easter, hivyo nilikua namchukua Maggy tu.

Baada ya kumpeleka Maggy Posta ilibidi niende Kijitonyama mapema kwa Iryn kama tulivyokubaliana. Nilifika pale kwake na alikuwa bado kalala, nilimpigia simu na akatoka kunifungulia mlango.

Tulisalimiana pale na yeye akasema anakwenda kuoga ili tuwai kwenda mapema Posta.

Baada ya kuwasili Posta kuna duka tuliingia la nguo “special”. Iryn alinunua nguo nyingi tu pale za kiofisi ikiwemo suti ya suruali na alikua anajaribisha palepale.

Tulirudi haraka Kijitonyama na alijiandaa pale kwa haraka na alitoka akiwa amependeza sana. Alikuwa kavaa suti ya dark blue na ilionekana kumpendeza sana mrembo Iryn.

Tukaondoka kuelekea Masaki kwenye hio Organization. Muda huo ilikua saa 7 mchana na nilimshusha nje ya geti la Organization.

“Insider nitakupigia nikiwa tayari sawa?” na yeye akaingia ndani.

Mimi nilitoka hapo na nikatafuta chimbo kwa mbele nikapark gari langu.

Lengo kubwa la kwenda kwenye hii Organization ni kufanyiwa interview na kusaini forms, Iryn alisema wanamfanyia interview ili wajue zile pesa atazifanyia nini maana ni nyingi sana kwa umri wake.

Wakati niko kwenye gari nilikua nikiperuzi peruzi kwenye social medias nikiangalia mambo yanayoendelea na kutrend. Na muda huo Mary alinipigia simu, nilishangaa sana kuona akipiga simu.

MIMI: “Mary mambo.”

MARY: “Salama za kunisusa?”

MIMI: “Mimi au wewe ndo umenisusa?”

MARY: “Mimi sijakususa ila uliniboa, na unajua sababu.”

MIMI: “Ok am sorry, sindo unataka kusikia hivi?

MARY: “Insider juzi ulikuwa na Prisca?”

MIMI: “Why?”

MARY: “Insider ulikuwa na Prisca, don’t lie”

MIMI: “Afu Mary mimi sikuelewagi ujue, you keep asking me everyday. Mdogo wako akichelewa kurudi unaniuliza mimi badala umbane Prisca, this behavior has to stop”

MARY: “It’s okay, upo wapi?.”

MIMI: “Niko masaki now, unahitaji usafiri?”

MARY: “Kama utakuwepo Posta, jioni utanambia.”

MIMI: “Sawa Bossy wangu”

Na muda huo alikata simu
emoji3513.png


Ukweli ni kwamba nikizurura hivi na Iryn nilikuwa naingiza pesa nyingi tu, sikosi laki, laki2 itadepend na yeye hio siku ana mood gani, japo kuna baadhi ya trip nilikua nakataa pesa zake.

Nilisubiri pale kwa almost saa zima nikimsubiri atoke na muda huo ndo alinipigia nisogee ili tuondoke.

Wakati nimesogea pale karibu nilimwona akiwa na Mama Janeth na wakapanda kwenye gari.

“Insider twende Levant tukale nafikiri ni sehem nzuri ambayo imetulia.”

Kutoka kwnye ile Organization hata sio mbali na ndani ya muda mfupi tulikuw pale Levant.

Na kila mmoja aliagiza msosi anaojua yeye na Mama Janeth na Iryn waliendelea kuongea, maana toka tukiwa kwenye gari walikuwa wakiongea sana, ni kama walikuwa wanaendeleza mazungumzo yao.

IRYN: “Mama ndo hivyo kama nilivyokwambia zile mashine zimefika tayari, utaziona ni nzuri sana na zitatusaidia.”

MAMA JANETH: “Na suala la massaji tutapata wataalamu na wakuaminika?”

IRYN: “Mama hata mimi nitawafundisha niko vizuri sana.”

MAMA JANETH: “Sawa mwanangu uwepo wako umekuwa baraka sana.”

IRYN: “Director muda ule alikuwa anasema Organization itanipa sponsorship ya Postgraduate, ni muda gani ita expiry?”

MAMA JANETH: “Hio ni wewe tu sidhani kama ina kikomo, vipi kwanini hutaki kufanyia kazi Organization?”

IRYN: “Mama si nitabanwa sana, na biashara zikayumba?”

MAMA JANETH: “Mbona mama yako alikuwa busy na mambo yalikuwa yanakwenda vizuri tu.”

IRYN: “Mama labda baadae kwa sasa hapana.”

MAMA JANETH: “Pale home unaishije? Maana sijaja na muda.”

IRYN: “Salama ila nafikiri mwezi ujao niondoke, ili uweke mtu ile ni biashara yako. Kipindi kile nilikuwa mgeni ila sasa nishayazoea mazingira, Insider ananisaidia sana.”

MAMA JANETH: “Hata mimi nakuona kuna utofauti mkubwa sana ulikuwa unajifungia tu ndani. Ila pale ni nyumbani unaweza kuendelea kukaa tu mwanangu hata usiwe na wasiwasi.”

IRYN: “Nataka nibadilishe mazingira pia.”

MAMA JANETH: “I understand.”

Tulitumia kama dakika 45 pale Levant na tukaondoka pale, tulimrudisha Mama Janeth kazini na sisi tukaondoka kurudi Kijitonyama.

Na wakati tunarudi tulitumia Kimweri Ave Road, hii barabara inakuja kutokea pale Mikocheni, Mwaikibaki road.

MIMI: “Iryn muda ule nilisikia mkiongea na Mama Janeth kuhusu kuhama pale Kijitonyama.”

IRYN: “Ndio Insider nataka kuhama pale, sikukwambia kama zile Apartments ni za mama Janeth?.”

MIMI: “Hapana hujawai kunambia.”

IRYN: “Ni Apartment zake, wakati nimerudi Tanzania kutoka Ufaransa nilifikia kwa Mama Janeth. Niliona nakosa uhuru wa kutoka usiku na kufanya kazi zangu, ndo nikamwambia nataka kupanga ndo akanionesha apartments mbili ya Mikocheni na hii ya Kijitonyama. Mimi niliipenda ya Kijitonyama ndo akaninulia vitu vyote unavyoviona mle ndani.”

MIMI: “Aisee kumbe”

IRYN: “Insider kukutana na wewe ni kama Baraka kwangu maana nilikuwa mtu wa kujifungia ndani tu.”

MIMI: “Nilikuahidi kukupeleka kula kitimoto na pia nitakupeleka ukale Biriani la selebonge.”

IRYN: “Week tayari hujatimiza ahadi.”

MIMI: “Better late than never.”

IRYN: “Don’t make Promises you can’t keep.”

MIMI: “Sema tumekula tayari, tena leo Ijumaa ningekupeleka pale kwa Selebonge tukale biriani.”

Tulitumia muda mchache kufika pale kwake baada ya kupark gari yeye aliingia ndani na mimi nikaenda kufunga geti.

Niliingia seblen na nikakaa kwenye coach na kwenye meza kulikuwa na kitabu kama magazine tuseme, kilikuwa ni cha mambo ya fashion, nilikuwa nakipitia nakiangalia yaliyomo ndani.

Wakati nikiendelea kuangalia picha za mle ndani nilisikia Iryn akiniita kutoka chumbani kwake,

IRYN: “Insider………”

MIMI: “Nambie mummy”

IRYN: “Come in please.”

MIMI: “In your room?”

IRYN: “Yes are you afraid? Njoo bhasi haraka.”

MIMI: “Okay am coming.”


TO BE CONTINUED

Sunday: 19:00

EPISODE 22

“A TRUE STORY BY INSIDER”

Na mimi muda huo niliinuka kuelekea chumbani kwake sikutaka kubisha, niligonga mlango na akasema niingie.

Nilifungua mlango na yeye alikuwa kajilaza kitandani, na muda huo macho yangu yote yalikuwa yakimwangalia Mwanamke mrembo aliyejilaza pale kitandani. Maana alikuwa na kibukta kifupi kinachoishia mapajani katikati, na upande wa juu alikuwa kavaa sport bras.

Sasa ule uzuri wake na vile alivyokuwa nikiona maungo yake vizuri tena live kwa macho nilijikuta nataka kupagawa na mimi sikutaka kuendelea kumtizama maana mnara ulishaanza kusimama wima.

MIMI: “Umeniita nakusikiliza”

IRYN: “Insider nataka unisaidie kutoa vitu humo kwenye makabati, nataka tuvipange vizuri.”

MIMI: “Sawa haina shida.”

IRYN: “Afu Grizmann anakuja mwezi huu, anakusalimia.”

MIMI: “Msalimie pia, mwambie aje na mazaga bhasi.”

Room yake ilikuwa na zile kabati za kutengeneza moja kwa moja. Nilifungua kabati na droo zote moja kwa nyingine.

Sasa kila nikifungua droo nilikuwa nakuta simu na vitu vingine kama chaji, earpods, apple watches na saa. Baada ya kumaliza kukagua drow zote nilihesabu jumla ya idadi za simu na zilikuwa simu 14 ambazo ni Samsung na iphone. Samsung Galaxy S22 ultra (2), Iphone 12 Pro Max (3), Iphone 13 Pro (3) na Iphone 13 Pro Max (6).

Nilishangaa sana asee yaani mtu anakaa na simu nyingi vile ndani na zote zilikuwa ni brand new hakuna hata moja ilofunguliwa. Muda ule nilitamani niibe hata simu moja nifiche lakini ilikuwa ngumu kwa upande wangu. Kuomba simu pia nilikuwa siwezi maana nilipewa simu na Iryn na hakuwai niuliza kuhusu ile simu, nilimpa Mama J na nikachukua simu yake, tulifanya kuexchange na Mama J.

IRYN: “Insider hizo simu zipo ngapi?”

MIMI: “Jumla ziko 14, unakaaje na duka la simu ndani?”

IRYN: “Insidier hizo simu nilipewa kama zawadi tu na watu tofauti, kama hizo iphone 12 Pro Max nilipewa muda mrefu sana toka zinatoka.”

MIMI: “Aisee unabahati sana, unajua uzuri wako unawapagawisha sana wanaume.”

IRYN: “Insider umeanza tena, hizo iphone 12 kuna dada nitawapa saloon, wanani-furahisha sana.”

MIMI: “Na hizo zingine? Si bora hata uuze upate hela maana thamani zinazidi kushuka, na mwaka huu iphone 14 inatoka.”

IRYN: “Sasa naziuzia wapi?”

Nilitamani kumwambia aongee na Muajemi maana anaduka la simu lakini nikaona haitakuwa good idea, Muajemi angejisikia vibaya sana yaani kapeleka zawadi ya simu afu mtu anasimu kibao ndani.”

MIMI: “Niachie hili mimi, nitatafuta mtu wa kumuuzia.”

IRYN: “Okay sawa, nataka now nitumie na Samsung Ultra maana wanaisifia sana.”

Samsung S22 ultra ilikuwa released February lakini Iryn alikuwa nayo tayari tena mbili (2).

MIMI: “Sawa Bossy.”

Alinipiga jicho kali sana maana alikuwaga hapendi kusikia nikimuita hili jina.

MIMI: “Una nipiga jicho na hayo macho yako ya kirembo.”

IRYN: “Insider njoo angalia.”

Na muda huu alikuwa akinionesha picha zake na video mbalimbali alizokuwa Ufaransa.

MIMI: “Ulikuwa unashiriki fashion?”

IRYN: “Niligombea Miss college.”

MIMI: “Ikawaje?”

Na muda huu Iryn alikuwa akitafuta picha ya kunionesha,

IRYN: “Ona nilikuwa wa2, sikushinda. Huyu dada alishinda.”

Huyu dada aliyekuwa akinionesha ambaye ndo alishinda, alikuwa ni mhindi.

MIMI: “Ni kisu hatari.”

IRYN: “Kumbe hata wewe umeona, alishinda huyu alikuwa anasoma Finance.”

MIMI: “Hata hvyo ulijitahidi kuwa wa2 sio kitoto.”

IRYN: “Kupitia haya mashindano ndo nili-miti na Grizmann, kipindi hicho yeye alikua Masters.”

MIMI: “Everything happen for a reason.”

IRYN: “Yeah sure”

MIMI: “Hivi huko Ufaransa Grizz hakucheat kweli?”

Muda huu Iryn aliniangalia akaanza kucheka, ni kama hakutegemea lile swali.

IRYN: “Ana mke na watoto 2.”

MIMI: “Aisee na wewe umeridhika kuwa mchepuko?”

IRYN: “Insider Grizz kuna mambo ananisaidia mengi sana, sometimes we don’t have a choice.”

MIMI: “Ni kweli unachosema ila naona anakupenda sana.”

IRYN: “Yeah he loves me but ni mme wa mtu.”

Sikutaka kuendelea kumwuliza sana kuhusu Grizz na muda huo yeye alitoka kwenda Seblen akiniacha pale chumbani nikiendelea kumpangia vitu vyake.

Wakati amekwenda seblen Mary alikuwa akinipigia simu na Iryn alisikia simu ikiita.

IRYN: “Insider somebody Mary is calling.”

MIMI: “Njoo na simu bhasi.”

Muda huo nilitumia kuongea na Mary, alikuwa akiniuliza kama nipo around ili nikampick ila nikamwambia niko Kijitonyama. Mary pia aliomba kama tutaweza onana muda ule na nikamwambia maybe jumapili nitamcheki.

Na muda huo wakati nikiongea na Mary, kwa upande mwingine Iryn alionekana kuwa makini sana kusikiliza maongezi yetu.

IRYN: “Insider nani huyo?”

MIMI: “Kila nikiongea na mwanamke lazima uulize ni nani.”

Na Iryn kama hakufurahishwa na hili jibu nilimwona kamind flani hivi. Pia kama alijiona ananikosea sana kufuatilia calls zangu.

IRYN: “Ok Insider am sorry”

MIMI: “Usijali najua huna nia mbaya, huyu ni mshikaji wangu.”

IRYN: “Ngoja nikapike chap”

Na mimi nilitoka nikakaa pale seblen na muda huo nilikuwa nikiangalia Tv utafikiri ni Baba mwenye nyumba. Na mimi niliamua kwenda Jikoni kumsaidia kupika muda ule.

“Unanipikia nini Mummy?”

“Nilitaka kupika ndizi na nyama ila nimeona uvivu kumenya ndizi.”

“Si ungesema nikusaidie? Mimi niko kwaajili yako”

“Kesho nitapika usijali.”

“Sasa unapika nini?”

“Tambi za maini.”

Na muda huu mimi niliamua kutengeneza juice ya nanasi na story zikiendelea.

IRYN: “Insider Muajemi anataka twende Zanzibar kutembea”

MIMI: “Aaah mnakwenda lini?”

IRYN: “Ndo najifikiria hapa”

MIMI: “Wewe unapenda?”

IRYN: “Kwenda napenda, ila yule mtu simwamini bado.”

MIMI: “Kwamba unaogopa atakuteka?”

IRYN: “Hamna sio rahisi, anyway nitaangalia.”

MIMI: “Si unakwenda na mimi hapa Bodyguard wako.”

IRYN: “Hahahaah Insider huishiwi vituko”

MIMI: “Nimekwenda jeshini wewe cheka, sikutaka kuwa mjeshi tu.”

Na muda huo nikamwonesha cheti changu cha JKT kile cha Mujibu wa sheria, Iryn haya mambo hajui hivyo alishangaa sana, maana alikuwa haamini kama nilikwenda jeshini.

IRYN: “Insider kumbe umekwenda Jeshi, upo vizuri ndomana mambo yako ni chap sana, na unajali sana muda.”

MIMI: “Nitakulinda kila unakokwenda na hakuna wa kukuzingua.”

Iryn alishiia kufurahi tu muda huu hakuwa na chakusema, pia alisema kesho ambayo ni jumamosi angeenda kuonana na Muajemi. Na mimi niliunga mkono hili jambo kwa asilimia mia kabisa, maana Iryn angekua karibu na Muajemi mimi ningeendelea kufaidi matunda.

MIMI: “Vipi kuhusu kutoka usiku kwenye kazi zako.”

IRYN: “Tutaendelea next week nataka kudeal na wateja wa web tu kwasasa tena ambao wana offa nzuri tu.”

MIMI: “Sawa Bossy Lady.”

Baada ya kumaliza mapishi tulikula chakula na nikamshukuru kwa Dinna, nikamuaga nasepa muda ule, lengo langu ilikuwa kwenda barabarani kuendelea na majukumu ya kusaka pesa.

Wakati nataka kuondoka Iryn aliniita

IRYN: “Insider…. Leo tumeanza mwezi mpya, nikiwa nakulipa naomba upokee hela sijisikii vizuri kuona unakataa hela hata kama tulikuwa kwenye makubaliano.”

MIMI: “Sawa haina shida mummy”

IRYN: “Byee Insider takecare”

Nilitoka pale ilikuwa saa2 usiku tayari na mimi nikaendelea kupiga kazi non-stop, kama mnavyojua kwa Dar weekend ndo watu wanatoka out kutumia hela.

Nilipiga kazi mpaka saa 7 usiku na niliamua kurudi baada ya kupata mteja aliyekuwa anaelekea Mbezi Beach.

*********

Jumamosi niliamka asubuhi sana kama kawaida yangu na nilipiga sana kazi hii siku. Ile Asubuhi kwenye saa5 Msomali alinipigia simu na aliuliza niko wapi nikamwambia niko tabata Baracuda.

Msomali akasema kama nitakwenda mjini nimpigie simu anataka twende Mbweni na alisisitiza sana.

Saa 12 jioni ndo muda ambao nilionana na Msomali na alikuwa pale CBD hotel Gerezani.

Tulitoka hapo kwanza tulianza kupitia Mlimani city kuna mtu alikwenda meet naye na nilisubiri kama 1 hour. Baada ya hapo sasa tukaanza safari ya kwenda Mbweni na tulipitia Barabara ya Mwaikibaki ili kukimbia foleni ya Bagamoyo Road.

MSOMALI: “Insider gari yako ni safi sana na inanukia vizuri.”

MIMI: “Si unajua ofisi lazima iwe safi muda wote, hata hapa umekuta Gari ni chafu.”

MSOMALI: “Kwa hili unajitahid sana hongera.”

MIMI: “Ahsante sana Bossy wangu I really appreciate.”

Saa 3 tulikuwa tumefika Mbweni na tulifika sehemu anayokwenda tukaingia ndani na mimi nilikwenda msubiri kwenye garden

Msomali alitumia kama masaa 2 pale na akatoka akanambia tunakwenda Sea cliff hotel Masaki, ndo nitamwacha pale.

Wakati tuko njiani tulikuwa tunapiga story mbalimbali hasa za Maisha na mademu.

MSOMALI: “Insider kwa kipindi kifupi tulichokutana nimetokea kukubali sana, kuna deal nitakushirikisha by next week, au umeridhika na maisha ya Uber?”

MIMI: “Hapana Bossy sijaridhika maana hii kazi sometimes ni mateso ila ndo hivyo tunapambana kibishi. Kama deal zuri mimi napiga kwasasa nachoangalia pesa tu.”

MSOMALI: “Sawa haina shida Bro!, nitakupigia simu.”

MIMI: “Sawa Bossy nasubiri na nitashukuru sana.”

Tulifika pale Sea cliff na nikamshusha Msomali pale.

MSOMALI: “Bro nikupe kiasi gani? Maana hatukuelewana kabisa.”

MIMI: “Bossy wewe nipe utakayoona haitoniumiza mimi, si unaona wese limepanda bei? Vita ya Ukraine na Russia ndo imeleta majanga.”

MSOMALI: “Ni kweli Bro! vita ya wakubwa hizo sisi wengine ni watizamaji tu, wewe ongea kuwa huru.”

MIMI: “Ok kutoka Posta mpaka Mlimani city 15,000, kutoka Mliman mpaka Mbweni 25,000 na kutoka Mbweni mpaka hapa utanipa 30,000 unipa 70,000 sio mbaya.”

MSOMALI: “Haina shida Bro ngoja nikupe na offa ya bia maana leo weekend”

Msomali alinipa 100,000 na akaondoka pale huku akiahidi kunitafuta kwa ajili ya hilo deal. Na muda huo niliwaza Msomali atakuwa na deal gani?

Na muda huu nilipata request ya mteja alikuwa anakwenda Airpot na alikuwa palepale Sea cliff.
Na huyu mteja alikuwa kauzu sana nakumbuka, maana tulitoka pale Sea cliff mpaka Terminal 3 bila kuongea njiani.

Nilipiga kazi mpaka saa 9 usiku ndo nikarudi kulala, maana nilikuwa na usingizi hatari.

*******

Jumapili saa 4 asubuhi Mama Liam alirudi home na aliletwa na Mamdogo wake home. Niliwapokea na tulishinda na mamdogo pale home mpaka tukala chakula cha mchana na yeye akaaga.

Hii siku nilicheza sana na Junior maana nilim-miss sana, na Junior alikuwa mtundu sana kipindi kile mpaka sasa ni mtundu balaa huyu mtoto.

Mchana Iryn alinipigia simu akasema kama nitapata muda niende kwake ili nipeleke ile mizigo (mashine za saloon) kule Masaki kwa Mama Janeth.

Jioni saa10 nilitoka home na nikamwaga Mama J natoka ila nitawai kurudi tutoke out. Mama J alifurahi sana kusikia hizi taarifa maana ni kama alikuwa amemiss kutoka out na mimi mme wake.

Nilifika kwa Iryn ila sikuingia ndani na niliitoa ile mizigo kibarazani na kuiweka kwa gari. Muda huo nilihisi Iryn atakuwa amelala hivyo sikutaka kumsumbua kabisa. Kwasababu nilikuwa najua ile mizigo inakwenda kwa Mama Janeth nikasema acha niipeleke tu, nikirudi ndo nitamcheki.

Nilipeleka ile mizigo kwa Mama Janeth Masaki, baada ya kufika Mlinzi alinifungulia geti na nilimkuta yuko nje akipanda maua . Nilimsalimia nikamwambia nimeleta mizigo na nikaitoa nikaingiza ndani.

“Mwanangu Ahsante sana.”

Nilimwaga Mama Janeth na mimi nikaondoka kurudi kwa Iryn, na wakati niko njiani Iryn alipiga simu.

“Insider kumbe umepeleka mizigo kwa Mama Janeth.”

“Yeah, wakati nafika hapo ulikuwa umelala, sikutaka kukusumbua.”

“Nilitaka twende wote bhasi lakini.”

“Niko njiani soon nitakuwa hapo.”

Wakati narudi nilitumia njia ya Heilasie Road ambayo inakuja kutokea Bagamoyo Road, kwangu naonaga hii barabara ni rahisi, maana hainaga mambo mengi.

Nilitumia kama dakika 15 kufika Kijitonyama kwa Iryn na nilipark gari nje ya fensi getini, sikutaka kukaa sana pale. Lengo langu lilikuwa nirudi home mapema ili nitoke out na wife.

Niliingia ndani na nilimkuta seblen akichezea laptop yake ya Macbook, nilimsalimia na nikaenda kukaa kwenye kiti.

“Insider…….”

Iryn aliniita na mimi nikamtizama kumsikiliza anataka kusema nini;

“Naam mummy”

“Huyu ni mwanao?

Iryn alikuwa akionesha picha ambayo nilikuwa nimeipost whatsapp status nikiwa na Junior.

TO BE CONTINUED
Antonia njoo
 
Unalinga sana story yako. Si uweke hata episod zote imekuwa kama matamthilia ya kwenye tv
 
Duh, kama na wewe ume scroll kuja ku reply hapa chini like twende sawa. Mtu anaandika thread title halafu anaanza na stori tofauti kabisa dah.
 
Back
Top Bottom