Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Mimi Iryn akipotea kwenye hii story itakuwa ndio mwisho wangu wa kuisoma. Kiufupi bila Iryn haivutii wala nini..Iryn apatikane tu mana asipopatikana na story ndio iishe tu

Ila umeniacha na stress kama nikusindikize police vile... Dah mrembo wetu kimempata nini???

Next episode usiicheleweshe sana bro and thanks a lot for today
 
EPISODE 35

ENDELEA…

Jumanne nilimpeleka Mchepuko wa Mzee kuanza mafunzo ya Udereva pale Posta na alianza kuendesha kwa kutumia mashine za kisasa (SEDIRO). Nilimwacha pale na nikaenda kuonana na Maggy maana nilikuwa nataka kuongea naye suala la kutafuta apartment kwaajili ya Iryn.

Nilimkuta Maggy ofisini kwake na tukaanza maongezi ya kunitafutia apartment nzuri ya kisasa maeno ya msasani mpaka Mbezi beach na iwe full furnished.

MAGGY: “Insider hilo halina shida, hii apartment kwaajili ya nani?”

MIMI: “Kuna dada mteja wangu anahitaji.”

MAGGY: “Kama ya wifi unasema bhana usifiche maana maisha yako ya mahusiano siyajui”

MIMI: “Maggy au unafikiri nampangia mtu? Hizo dolali mimi natoa wapi?”

MAGGY: “Anaweza kuwa demu wako, maana yule dada (Mbotswana) na wasiwasi.”

MIMI: “Hahahaa afu atakuja soon alinambia utamtafutia apartment pia.”

MAGGY: “Haina shida, Insider kuna jambo nataka kukushirikisha rafiki yangu.”

MIMI: “Nambie Mummy ni jambo gani hilo?”

MAGGY: “Insider nimepata kazi Taasisi “X” na nina kwenda kuwa Mkuu wa Idara.”

MIMI: “Hongera Mummy nimefurahi sana kusikia hivyo jamani.”

MAGGY: “Nitakwenda Dodoma makao makuu ya Taasisi.”

MIMI: “Lini unaondoka?”

MAGGY: “Bado sijajua ila utaratibu ukikamilika nitakujulisha. But nitakumiss sana Insider ujue.”

MIMI: “Haya mambo tutaongea ukiwa unaondoka, mimi naumia mteja wangu unaondoka but sina jinsi. Kila jambo ni mipango ya Mungu.”

MAGGY: “Kweli Insider, sasa ishu ya apartment nitaanza ifanyia kazi then nitakujulisha.”

MIMI: “Sawa jitahidi kabla ya mwisho huu wa mwezi mambo yawe yamekaa sawa.”

MAGGY: “Na bajeti yake ikoje?”

MIMI: “Budget sidhani kama tatizo sana ila nitaongea naye afu nitakupa majibu.”

Baada ya kumalizana na Maggy nilimpigia simu Iryn nimpe taarifa kwamba nimeanza mchakato wa kutafuta apartment na pia nimuulize kuhusu bajeti aliyopanga. Lakini simu yake ilikuwa haipatikani nikapiga kwa mara nyingine tena ikawa haipatikani. Na muda huu mchepuko wa Mzee alinipigia simu kwamba yuko tayari nikamchukue nimrudishe Mbweni.

Baada ya kumchukua nilimwambia tunapitia Masaki ili miwachukue madogo na yeye hakuwa na pingamizi. Ndani ya masaa 2 tulikuwa tuko pale Mbweni tayari na baada ya kumshusha, Jane alisema niingize gari ndani.

“Insider usindoke bila kula tafadhali.”

Na mimi nilingia ndani kupata lunch na baada ya kushiba nilikaa seblen na nilikuwa naongea na mama yake Jane. Muda huu nilipata ujumbe kwa Whatsapp na ulionekana umetoka kwa Maggy na niliufungua palepale. Maggy alikuwa kanitumia picha za apartment nzuri sana na ilikuwa furnished, nikampigia simu chap

MIMI: “Maggy hiyo Apartment ni nzuri sana ipo wapi?”

MAGGY: “Ipo Msasani hiyo ni nzuri kama inawezekana aseme niishikilie maana kuna watu wanaitaka pia.”

MIMI: “Ngoja nimpigie simu afu nitakurudia, gharama zikoje?”

MAGGY: “$1,200 tu.”

Nilimpigia tena simu Iryn lakini ilikuwa haipatikani ikabidi nimcheki kwa whatsapp lakini alikuwa hayuko online pia, nikaplan kwenda kwake badae.

Jioni nilitoka pale Mbweni na lengo langu lilikuwa kwenda kwa Iryn, lakini wakati natoka pale Mbweni Mzee alinipigia simu akanambia badae niende kwake. Sababu nilikuwa karibu na Mzee nikamwambia niko around na sio muda mrefu nitakuwa pale nyumbani.

Niliwasili Ununio kwa Mzee Pama na nikapiga honi pale getini na alitoka kaka kufungua geti ambaye ni mfanyakazi wa pale.

Nilipark gari na nikaingia ndani seblen na nilimkuta Mzee akiwa amekaa seblen yuko na bint wanaongea.

MZEE PAMA: “Kijana huyu ni Bint yangu wa mwisho na amemaliza form 6 mwaka huu.”

Bint yake alinisalimia na akaondoka eneo hili,

MIMI: “Mzee hongera sana kama huyu ni Bint wa mwisho bila shaka wengine watakuwa ni wakubwa sana.”

MZEE PAMA: “Bint yangu wa kwanza yuko Canada na anafanya kazi huko, anayefuatia yuko chuo Australia, kabla ya huyu wa mwisho kulikuwa na mwingine ambaye alitangulia mbele za haki.”

MIMI: “Aisee pole sana.”

MZEE PAMA: “Nimebarikiwa kuwa na Mabint tu, ila Jane atanizalia dume la kuendeleza ukoo.”

MIMI: “Hongera sana bila shaka kwasasa unafuraha.”

MZEE PAMA: “Nafuraha sana, kijana mwanaume unatakiwa usikose mtoto kwa Kiume, huwa nawashangaa sana watu hasa mwanaume anakwambia nataka mtoto wangu wa kwanza awe wa kike, nawaonaga wamekosa akili kichwani.”

MIMI: “Kwanini Mzee?”

MZEE PAMA: “Mtoto wa kiume ndo aneyekuza na kueneza ukoo, mtoto wa kike akishakuwa na kuolewa sio wako tena, maana hata watoto wanakuwa ukoo wa baba.”

MIMI: “Mzee upo sahihi hata mimi mara yakwanza nilitamani sana kupata mtoto wa kike ila kwasasa najivunia kupata dume.”

MZEE PAMA: “Una mtoto?”

MIMI: “Ndiyo mzee pamoja na mke sema hatukawahi kukaa na kuongea mambo ya kifamilia ndomana, ila nilipanga kukwambia.”

MZEE PAMA: “Hongera sana Kijana ndomana upo serious kumbe una familia.”

MIMI: “Na mtoto mmoja na mwezi ujao atakuwa anatimiza mwaka.”

MZEE PAMA: “Mama yake ndo yule ambaye tulikuwa naye siku ile?”

MIMI: “Hahahaaa hapana Mzee yule ni mchepuko tu.”

MZEE PAMA: “Hahahahahaahha Kijana una mambo sana, kwasisi wanaume ni kawaida ila nikwambie jambo, kuwa makini sana na hawa michepuko wanaweza kukuharibia furaha yako. Unavyokuwa na mchepuko hakikisha anajua una mke ili asikusumbue pia ijali familia yako kwanza, yeye awe wa mwisho. Kumbuka wewe umemfata kimasilahi akutimizie haja zako hata yeye kwako atakuwa kimaslahi, uwe makini sana.”

MIMI: “Ahsante sana Mzee kwa ushauri, namchepuko sababu nakosa mambo fulani tu kwa kipindi hiki, maana wife yuko busy na kulea na anasoma pia.”

MZEE PAMA: “Naelewa sana na tunafanya hivi ili kuepusha ugomvi.”

MIMI: “Mzee ulinambia kuna jambo muhimu la kuongea.”

MZEE PAMA: “Hali yangu kiafya kwa sasa haiko vizuri nataka kwenda India kufanya vipimo na nitakuwa kule kwa week 2, nimekuita ili unisaidie kuhakikisha Jane anakuwa dereva mzuri na good news leo amenipa report kuwa ameanza mafunzo.”

MIMI: “Mzee kwa hili ondoa shaka nakuhakikishia utafurahi.”

MZEE PAMA: “Sina shaka na wewe nakuamini sana. Nitakupa pesa kwaajili ya mafuta ya ile gari na pesa zako za usafiri wa kumpeleka Posta. Nauli ya kwenda na kurudi ni tsh ngapi?”

MIMI: “Ni kama 30,000 kwenda na kurudi itakuwa 60,000/=.”

MZEE PAMA: “Haina shida vipi kuhusu gari performance ikoje barabarani? Kama kuna shida sema tuirudishe mapema.”

MIMI: “Mzee gari ipo vizuri sana na ile rangi imependeza kwelikweli.”

MZEE PAMA: “Endelea kuiendesha usiipark ndani, nataka uendeshe kama kuna tatizo turudishe hili ndo lengo la kukuachia, usiogope sawa?”

MIMI: “Haina shida Mzee.”

Mzee aliingia ndani na alitoka akiwa ameshika bahasha ya kaki mkononi ikiwa imekunjwa.

MZEE PAMA: “Hizi ni 2,500,000/= utakata pesa yako ya nauli kwa mwezi 1 inayobaki ni kwaajili ya mafuta na mambo mengine yatakayojitokeza kule mwenye mafunzo ya Jane. Nataka hiyo gari uende nayo hata Morogoro na kurudi ili ujue ulaji wa mafuta na hapa sasa utaisoma na kuielewa gari vizuri.”

MIMI: “Mzee haina shida nitakwenda nayo Dodoma mwisho wa mwezi huu.”

MZEE PAMA: “Hapo safi, sasa acha mimi nikapumzike maana kesho ninasafari naomba utanipeleka Airport maana jioni ndo naondoka.”

MIMI: “Haina shida mzee ahsante sana.”

Muda huu ilikuwa usiku tayari umeingia hivyo nikaamua kurudi zangu home mapema. Usiku huu Prisca alinipigia simu, tena alikuwa anapiga kwa fujo nikaamua kuizima simu na mimi nikalala.
*********

Kesho yake asubuhi wakati niko Posta na Maggy alinisisitiza sana kabla ya mchana niwe nimempa majibu kuhusu ile apartment maana nikichelewa kuna mtu atailipia. Na mimi nilimwambia kama mpaka mchana ikiwa kimya ampe mtu mwingine sababu anayetaka hapatikani.

Na muda huu nilipiga simu kwa Iryn tena mbele yake na ilikuwa haipatikani.

MIMI: “Maggy sijui atakuwa na shida gani maana hapatikan toka jana ujue.”

MAGGY: “Kwani mara ya mwisho mmewasiliana lini?”

MIMI: “Jumapili tulikuwa wote nikamdrop kwake baada ya hapo hatukuwasiliana jana ndio nilimpigia simu nimwambie kuhusu apartment na simu yake ikawa haipatikani.”

MAGGY: “Huenda kaibiwa simu au kapatwa na matatizo, umejaribu kwenda kwake kuangalia?”

MIMI: “Hapana sijaenda bado ila leo nakwenda.”

MAGGY: “Fanya hivyo mimi nahisi atakuwa kaibiwa simu.”

Tuliagana na Maggy na mimi nilikwenda Mbweni kwaajili ya kwenda kumchukua Jane na mapema nilikuwa nimefika pale kwake.

Baada ya kuwasili pale kwa Jane nilikaribishwa ndani ili nimsubiri maana alikuwa anajiandaa. Na muda huu nilikaribishwa Dining kupata breakfast.

Jane alitumia dakika 30 kujiandaa na baada ya kutoka tuliondoka kuelekea Posta. Na wakati tukiwa njiani alikuwa akiniangalia sana nikiwa naendesha gari.

“Naona unatizama kwa makini sana.”

“Yaani! najifunza hapa taratibu niko makini sana.”

“Soon tu utamasta cha muhimu wewe concentrate tu.”

Nilimshusha pale Posta kituo anachojifunzia na mimi nikaenda zangu kwa Maggy. Kipindi hiki nilikuwa navyorudi na Jane Mbweni naunganisha na watoto wa kule Masaki hivyo nilikuwa napiga ndege wawili kwa jiwe moja.

Baada ya kumrudisha Jane kwake, Mapema kabisa nilikuwa pale Ununio kumchukua Mzee nikiwa na Dualis na nilimkuta yuko tayari ni kama alikuwa ananisubiri mimi tuondoke. Nilichukua bag lake la nguo nikaweka kwenye buti na tukaanza safari ya kwenda JNIA.

MZEE PAMA: “Familia haijambo?”

MIMI: “Nashukuru Mungu iko salama kabisa.”

MZEE PAMA: “Maendeleo ya Jane unayaonaje?”

MIMI: “Kwasasa kutoa neno inakuwa ngumu tumpe muda kwanza.”

MZEE PAMA: “Nikishuka Airport nitaikagua gari vizuri ila kwa ndani nimeridhika.”

Tulitumia kama Lisaa na nusu kuwasili pale JNIA Terminal 3 na baada ya kushuka Mzee alitumia muda huu kuikagua gari na akaridhika.

Niliagana na Mzee kwa miadi ya kuonana akirudi na aliniomba sana nihakikishe ulinzi kwa mke wake.

Baada ya kuachana na Mzee niliondoka JNIA na plan zangu kichwani ni kwenda Kijitonyama kwa Iryn. Niliwasili kwa Iryn saa 12 jioni na nilipark gari nje na nikaingia ndani na nilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye apartment yake.

Nilijaribu kufungua geti na mlango lakini alikua kafunga, nilijaribu kugonga lakini hakukuwa na majibu yoyote. Mazingira yalionesha hakuna mtu pale, kwa upande wa jirani naye alikuwa hayupo maana hata gari yake haikuwepo eneo hili, hivyo nilijua bado hajarudi kutoka kazini.

Nilikaa pale nje kibarazani kama lisaa hivi na hapakuwa na dalili za Iryn kurudi wala majirani zake. Na muda huu nilipata wazo la kumpigia simu Lucy kama atakuwa na mawasiliano na Iryn lakini hakupokea simu yangu, na mimi nikawasha gari kuondoka eneo hili.

Wakati niko mataa ya Mwenge niliwasiliana na Mama wa2 nikampa taarifa napitia kwake na yeye akasema yupo.

Ndani ya dakika 20 nilikuwa pale kwake mitaa ya Rainbow na nilikaribishwa ndani.

MAMA WA2: “Mkwe unaendeleaje.”

MIMI: “Salama kabisa pole na kazi.”

MAMA WA2: “Aaaah Ahsante sana na wewe pia.”

MIMI: “Mama mkwe mimi sina mambo mengi ila nimekuja kupunguza mkopo wa lile deni letu.”

Na muda huu nilitoa bahasha mfukoni ambayo ilikuwa na zile pesa, na nikamkabidhi.”

“Mama mkwe hizo ni million 5 nimeziotea sehemu hivyo nimeona bora nipunguze deni.”

MAMA WA2: “Insider usinambie umepata lishangazi mara hii umeipata million 5 na ulikuwa unalalamika biashara ni ngumu.”

MIMI: “Mama mkwe wewe unaona mimi wa kulelewa? na hustle kila kona kupata hela.”

MAMA WA2: “Nakutania Mkwe, Insider itabidi nikufahamu na kwako hata kama unakaa geto.”

MIMI: “Hili ondoa shaka utapafahamu tu usiwe na wasiwasi.”

Nilimuaga Mama wa2 na wakati niko kwa gari mawazo ya kifisi yalinijia kichwani ya kuonana na Prisca. Nilichukua simu na kumpigia simu na ndani ya sekunde kadhaa alipokea na akanambia yuko Shoppers anafanya shopping, nikamwambia anisubiri nakuja.

Nilifika Shoppers na nikapark gari vizuri na nikaingia ndani supermarket, sikutaka kumpigia simu na nilivyoingia ndani nilianza kumsaka kwenye mashelfs na nilimwona mdogo wake Ivy na nikampa ishara ya “shhh” [emoji2958]. Nikazunguka upande wa pili ndo nikamwona Prisca nikamziba macho, na muda huu Ivy alikuwa anacheka sana.

Prisca na mdogo wao wa mwisho Ivy walikuwa wanapatana sana.

PRISCA: “You must be Insider.”

MIMI: “Hahahaa umemaliza shopping?”

PRISCA: “Ndo namalizia hapa.”

MIMI: “Fanya chap niwapeleke.”

Tulitoka pale Shoppers na tulielekea kwao na mimi nilipark gari nje kabisa getini. Prisca alishuka na Ivy akanambia anakuja, na haikuchukua muda Prisca alirudi na akaingia ndani ya gari.

PRISCA: “Insider umenunua gari mpya?”

MIMI: “Hapana hii sio yangu.”

Na muda huu nikawasha gari

PRISCA: “Vipi tunakwenda wapi? Mbona sikuelewi Insider.”

Muda huu mimi akili ilikuwa inawaza ngono tu.

Sikumjibu kitu na mimi nikakanyaga mafuta mpaka lodge tuliyokwenda mara ya kwanza kule whitesand.

PRISCA: “Insider muda huu unanileta huku na mama yuko home.”

MIMI: “It won’t be long, just an hour.”

Tulitumia kama lisaa na nusu kupeana utamu na baada ya hapo tukaondoka na nilianza kumrudisha Prisca kwao, na wakati tuko pale kwao nje getini alionekana Mary naye alikuwa ndo anarudi. Sikutaka kumsalimia, kwanza nilikuwa na gari mpya hivyo ingekuwa ngumu kunijua kwa muda ule na niliwaacha na Prisca wakiongea pale nje getini.

Ukweli ni kwamba nilianza kuwa addicted na Prisca kwenye suala la ngono hata yeye alikuwa vivyohivyo. Maana kila nikimkumbuka Prisca nawaza sex tu, nilikuwa kama nimerogwa.

Prisca ni aina ya mwanamke ambaye kama unamla unatamani hata ukeshe naye maana alikuwa ananyumbulika vizuri sana kitandani, hata ukitoa wafilipino unajikuta mnara unasimama tena kwa kasi ya 5G.

Baada ya kurudi home niliingia bafuni kuoga na baad ya kuoga simu yangu ilianza kuita kucheki alikuwa ni Lucy na nikaipokea.

MIMI: “Ndo unaamua kunipigia muda huu.”

LUCY: “Insider sorry nilikuwa na mteja ndo tumemalizana naye hapa na simu ilikuwa chaji.”

MIMI: “Ok haina shida hata kama umeamua kunidanganya.”

LUCY: “Kweli jamani.”

MIMI: “Bossy wako mnawasiliana?”

LUCY: “Mmhh hapana mara ya mwisho tumewasiliana Jumapili mkiwa Zanzibar.”

MIMI: “Iryn hapatikani kwenye simu toka jana, nimekwenda kwake pamefungwa.”

LUCY: “Mmh sasa atakuwa amekwenda wapi? na bila taarifa? Mbona huwa anatoaga taarifa hata kama amepata emergence.”

MIMI: “Mimi toka tuachane Jumapili ndo jana nilimpigia simu ikawa haipatikaniki nahisi kuna shida.”

LUCY: “Insider endelea ku-buy time kwanza huwezi kujua yule ni mwanamke pia.”

MIMI: “Yeah uko sahihi, usiku mwema.”

LUCY: “Goodnight.”

Niliwaza pale huenda labda kaondoka na Muajemi kimyakimya hajataka kutoa taarifa, na mimi nilikwenda kupata Dinna na nikarudi zangu kulala.
********

Alhamisi na Ijumaa nilizitumia vizuri kwa kumsimamia Jane kwenye mafunzo yake ya udereva. Kwenye upande wa kuendesha gari kwa kutumia mashine ya SEDIRO mwalimu alisema yuko vizuri hivyo jumatatu ataanza kuingia barabarani.

Nilikuwa nampeleka Posta na kumrudisha Mbweni kwa Dualis yake na hata alikuwa hajui kama ile gari ni yake, japo alikuwa akiisifia sana. Mzee alisema nisimwambie mchepuko wake chochote kuhusu ile gari, na mimi sikutaka kuongea jambo lolote kwa Jane.

Jumamosi nilifanya kuingia naye barabarani na nilikuwa na Ist, nilimfundisha kuendesha kwenye barabara za mitaani na alikuwa kidogo anajitahidi alionesha kujua kuendesha gari mapema.

Tulitumia masaa 3 kuendesha mitaani na tulirudi nyumbani. Jane alishaanza kuwa karibu sana na mimi maana tulikuwa tumezoeana vizuri na tulikuwa tunapiga story sana.

Pale Mbweni nilikuwa nishapazoea tayari na baada ya kuingia ndani nilipata lunch na nikaenda kupumzika kwenye sofa pembeni nikiwa na glass ya juice ya Pineapple.

Na muda huu Muajemi alinipigia simu kupitia whatsapp call na niliipokea simu yake kwa haraka sana.

MIMI: “Bro habari yako.”

MUAJEMI: “Salama sana za huko Dar es salaam.”

MIMI: “Bro! salama sijui wewe huko Iran.”

MUAJEMI: “Salama pia, Iryn hapatikani kabisa kwa whatsapp toka jumatatu anashida gani?”

MIMI: “Bro! sio wewe tu hata mimi, na kwake hayupo.”

MUAJEMI: “Unasema? sasa atakuwa wapi?”

MIMI: “Bro! I don’t know nimejaribu kila njia lakini sijafanikiwa kumpata bado.”

MUAJEMI: “Wasije wakawa wamemteka fanya kureport Police.”

MIMI: “Bro! Police sidhani kama ni jambo jema, soon nakwenda kwake pia nitaongea na majirani zake, ikishindikana ndo nitatafuta Plan B.”

MUAJEMI: “Bro! I’ll call you later.”

Muajemi alionekana kuchanganyikiwa sana na mimi nilianza kuingiwa na wasiwasi muda huu maana niliwaza sana pale.

“Kwasasa mimi na Iryn tuko close sana kama anasafari au jambo lolote lazima angenijulisha tu. Nilihisi huenda kuna jambo baya limemtokea na sio kawaida yake kutopokea simu au kutokupatikana, something fishy is going on.”

Niliaga pale Mbweni na nikaondoka kuelekea Kijitonyama kwa Iryn. Niliwasili pale Kijitonyama saa 11 jioni na baada ya kupark gari niliingia ndani na kwenda kwenye apartment yake. Niligonga tena mlango lakini hakukuwa na majibu hivyo ikabidi nifanye ujasusi wa kuikagua nyumba vizuri.

Nilizunguka kote na nilikuwa najaribu kufungua madirisha lakini yalikuwa yamefungwa na nikarudi kugonga mlango kwa Jirani maana gari yake ilikuwepo nje.

JIRANI: “Wow karibu jirani, karibu ndani.”

MIMI: “Acha leo niingie nitie baraka, lakini namazungumzo na wewe.”

JIRANI: “Jirani unataka kunambia nini?”

Na muda huu nilikuwa niko seblen tayari

MIMI: “Mara ya mwisho umemwona lini Iryn?”

JIRANI: “Last week ile siku uliyokuja tukaongea ndo tulionana, I remember kitu kama Alhamis.”

MIMI: “Toka ile siku hamjaonana tena?”

JIRANI: “Yes! kwani kuna nini?”

MIMI: “Jiran Iryn toka jumatatu hapatikani kwa simu wala whatsapp na hakuna taarifa yoyote aliyoacha, ndomana nikasema nije kwako labda kuna ujumbe amekuachia.”

JIRANI: “Hapana kwakweli na haiwezekani mtu asipatikane kwa simu from nowhere, Jiran something wrong. Iryn ni mwanamke mrembo na mzuri kupotea kwake kimazingara hivi lazima kuna shida, wasije kuwa wamemteka wahuni.”

MIMI: “Jiran tunafanyaje?”

JIRANI: “Twende Police kureport toka jumatatu ni parefu sana.”

Na muda huu Jirani (Rose) aliingia ndani na mimi nilibaki pale nje nikiwa na mawazo sana.

Muda huu nilianza kujilaumu kwa kutotilia maanani hili suala, niliwaza pale hata Police wangeniona mimi ni mzembe sana. Nilivuta pumzi ndefu sana na nilijikuta macho yangu yakiwa yamejaa machozi na mapigo ya Moyo yalianza kuongezeka spidi.

“TO BE CONTINUED.”
Leo umeupiga mwingi
 
Iryn unapoteaje kwenye Scenes na hujaliwa?

Naomba urudi popote Ulipo wanazengo tuna jambo letu .!!!
Najaribu kufikiria itakuwaje kama lryn atakiwa ametekwa na kufikwa jambo baya insider man atakuwa kwenye hali gani maana kitumbua kitakuwa kimeota mchanga,atakuwa amekoswa pia kwa muajemi hataree!
 
Back
Top Bottom